Hadithi: Lulu

Hadithi: Lulu

Ndugu wawili hawa wakaendelea kutembea huku wamebana macho kidogo, kama tu mababu zao walivyofanya kwa miaka mia nne iliyopita. Toka kipindi wageni walipofika mafundisho mapya na utawala mpya, na bunduki za kulinda vitu hivyo. Na katika miaka hiyo mia nne ulinzi pekee wa watu wa jamii ya Kino umekuwa ni kufumba kidogo macho na kukaza midomo na kuacha mambo yalivyo. Huo ndiyo ulikuwa ulinzi wao thabiti.

Umati uliozidi kukusanyika ulikuwa tulivu na makini, walikuwa wamehisi umuhimu wa wa siku hii. Mtoto yoyote aliyeleta vuruga, aliyelia kwa kele au kutaka kuchukua kofia na kuvuruga nywele za watu alinyamazishwa mara moja. Siku hii ilikuwa muhimu sana kiasi kwamba mzee mmoja alifika kushuhudia akiwa kabebwa mabegani mwa mpwa wake. Sasa umati ukawa umetoka kwenye nyumba zao za miti na majani na kuingia mjini kwenye nyumba za mawe, zilizopakwa chokaa. Barabara za mji zilikuwa ni pana kiasi. Na kwa mara nyingine tena, walipopita mbele ya kanisa na ombaomba wakajiunga nao; wauza maduka waliwaangalia wakipita; watu waliokunywa pombe wakaacha kunywa na kuungana na msafara, wauzaji nao baada ya kupoteza wateja, wakafunga na kuungana na umati. Na jua nalo likazidi ukali.

Taarifa za ujio wa umati zilitangulia kufika mbele kuliko umati wenyewe. Katika ofisi zao, wanunuzi wa lulu wakazidi kujiweka tayari. Walitoa makabrasha na kuweka mezani ili Kino atakapofika waonekane kuwa walikuwa wametingwa na kazi. Na waliweka lulu zao kwenye kabati, walionelea haitakuwa sawa kwa lulu mbovu kuonekana mbele ya lulu nzuri inayokuja. Habari za uzuri wa lulu ya Kino zilikuwa zimewafikia.

Ofisi za wanunua lulu zilikuwa zimerundikana pamoja kwenye mtaa mmoja mwembamba, madirishani kulikuwa kumewekwa nondo.

Mtu mmoja mkakamavu alikuwa amekaa katika ofisi moja. Uso wake ulikuwa wa baba mtu mzima na mpole, macho yake yaling’aa kirafiki. Alikuwa ni mtu wa matani mengi, mwenye kusalimu watu wote, mtu mwenye shangwe. Lakini bado alionekana kama ana huzuni ndani yake. Angeweza kukumbuka kifo cha shangazi yako katikati ya kicheko na machozi yake yakalengalenga kwa huzuni. Asubuhi hii alikuwa ameweka ua kwenye chupa mezani pake. Alikuwa kanyoa ndevu vizuri kabisa, mikono yake ilikuwa safi na kucha zake zilisuguliwa vyema. Mlango wa ofisi yake ulikuwa wazi na alikuwa akiimba kwa sauti ya chini isiyosikika vizuri. Mkononi alikuwa akichezea sarafu vidoleni mwake kama mwanamazingaombwe stadi. Kisa ghafla akasikia sauti ya vishindo vya umati ukija. Vidole vyake vikazidi kuongeza kasi ya kuchezea sarafu, na mara Kino alipotokea akahamishia mkono ule chini ya meza.

“Habari za asubuhi rafiki yangu,” alisalimia mtu yule. “Nikusaidie nini?”

Kino alishangaa-shangaa ndani mule mwenye mwanga hafifu, maana alikuwa ametoka nje kwenye mwanga mkali. Lakini macho ya mnunuzi yule yalikuwa yameshazoea, yalionekana makali na ya ukatili kama ya mwewe, lakini hapohapo sura yake ilionyesha tabasamu. Na chini ya meza, bado aliendelea kuchezea ile sarafu kwa vidole vyake.

“Nina lulu,” alisema Kino. Juan Tomas aliyekuwa amesimama pembeni yake, akaguna kwa maana aliona kama Kino hajaitendea haki lulu yake kwa kusema vile. Majirani wengine walikuwa wakichungulia kupitia mlangoni, watoto wadogo walijivuta dirishani kuchungulia, wengine walichuchumaa na kupiga magoti ili wachungulie kwa chini.

“Una lulu, moja tu? Wakati mwingine watu huleta dazani nzima. Hebu tuione lulu yako, tutaikadiria thamani yake na kukupa bei nzuri.” Vidole vyake vilizungusha sarafu kwa kasi hata zaidi.

Hapo Kino alitoa pochi ya ngozi, akafungua polepole na kutoa kipande kichafu cha ngozi ya swala, na kisha kutoa lulu ile na kuiweka kwenye sinia jeusi lililokuwa mezani na kisha kukaza macho yake kumuangalia mnunuzi usoni. Mnunuzi hakuonyesha ishara zozote, uso wake haukubadilika lakini mkono uliokuwa chini ya meza ukizungusha sarafu haukuweza kufanya kazi yake barabara. Sarafu ilimteleza na kumuangukia pajani. Aliishika lulu ile na kuizungusha ndani ya sahani; aliinua kwa vidole viwili na kuisogeza karibu na macho yake huku akiigeuzageuza.

Pumzi ikambana Kino kwa shauku, majirani zake nao vilevile. Minong’ono ilisikika kati yao, “Yupo kuikagua-bado hajataja bei-bado hawajakubaliana bei.”

Mlanguzi yule akairudisha lulu kwenye sinia, na akaigusagusa kwa kidole kama vile kuinyanyapaa, kisha akaonyesha tabasamu la huzuni na dharau.

“Samahani rafiki,” akasema huku akibinua mabega.

“Ni lulu ya thamani sana,” alisema Kino.

Dalali yule akaizungushazungusha tena lulu ile, kisha akasema. “Umewahi kusikia juu ya dhahabu ya mpumbavu? Lulu hii ni kama dhahabu ya mpumbavu. Ni kubwa mno. Nani atainunua? Hakuna soko kwa lulu kama hii. Ni ya kustaajabia tu. Samahani sana. Ulifikiri ni kitu cha thamani, lakini ni kitu cha kustaajabia tu.”

Sasa jasho likamtoka Kino usoni kwa wasiwasi. “Hakuna lulu kama hii duniani,” alisema kwa sauti. “Hakuna aliyewahi kuona lulu kama hii.”

“Sivyo hata kidogo,” alisema dalali. “Lulu hii ni kubwa na si bora. Kwaajili ya kustaajabia au maonyesho inafaa; pengine baadhi ya majumba ya makumbusho wanaweza kuichukua na kuitunza sehemu ya makombe ya baharini. Labda naweza kukupa peso elfu moja tu.”

Uso wa Kino ukawa mwekundu kwa hasira. “Ina thamani ya peso elfu hamsini, najua bei yake, unataka kunitapeli.”

Dalali akasikia sauti ya umati ukiguna waliposikia bei aliyotaja. Na akaingiwa na uoga kidogo.

“Usinilaumu mimi,” alisema haraka. Mimi ni dalali ni mkadiria bei tu. Waulize wengine. Nenda kawaonyeshe lulu yako ofisini mwao-au tuwaite waje hapa ili ujionee mwenyewe kwamba hakuna njama yoyote. Kijana,” alimwita kijakazi wake. “Nenda kamwite fulani na fulani. Waambie wafike hapa, lakini usiwaambie kwanini. Waambie tu ninataka kuwaona.” Hapo alitoa sarafu nyingine kutoka kabatini na kuanza kuizungusha vidoleni mwake.

Majirani wa Kino walinong’ona kati yao. Walikuwa na wasiwasi kuwa kitu kama hiki kitatokea. Lulu ilikuwa ni kubwa lakini ilikuwa na rangi ya tofauti na zingine. Walikuwa na mashaka nayo toka walipoiona kwa mara ya kwanza. Hata hivyo walionelea kuwa peso elfu moja si haba. Kwa mtu maskini zilikuwa ni pesa nyingi. Jana yake tu Kino alikuwa hana chochote, peso elfu moja ni nyingi.

Lakini Kino akibaki imara. Aliona hatima yake; hatima mbaya ikimnyemelea, mbwa mwitu wakimzunguka, ndege wala mizoga wakimzengea. Alihisi uovu ukimzunguka na kumtanda, na hakua na jinsi ya kujisaidia. Alisikia muziki wa uovu masikioni mwake.

Umati pale mlangoni ulisogea pembeni na kuwaruhusu wanunuzi watatu wa lulu kuingia. Na kisha kukawa kimya kabisa, watu waliogopa wasije wakashindwa kusikia yaliyoongelewa au kuona ishara. Kino alikuwa kimya na makini kabisa. Alihisi kuguswa mgongoni, alipogeuka akakutana na macho ya Juana. Akipogeuka kutazama mbele nguvu mpya ilikuwa imemuingia.

Walanguzi wale walisimama wima, hawakuangaliana wala kuiangalia lulu ile. Yule aliyewaita akaanza kwa kusema, “Nimethaminisha thamani ya lulu hii, lakini mmiliki wake anaona kama nataka kumpunja. Naomba nanyi muichunguze na kutoa bei yenu.” Hapo akamgeukia Kino na kumwambia, “Umeona mwenyewe, sijataja kiasi cha bei nilichoithaminisha.”

Mnunuzi wa kwanza akajidai kuwa ndiyo anaiona lulu kwa mara ya kwanza. Aliichukua na kuizungusha-zungusha vidoleni mwake, na kisha kwa dharau akairudisha kwenye sinia.

“Mimi nitoe kwenye hili suala,” alisema kikauzu. “Siwezi kununua. Siihitaji. Hii siyo lulu-ni dubwasha tu.” Alimaliza kusema na kukunja midomo.

Mlanguzi wa pili, mtu mmoja mfupi mwenye aibu-aibu; akaichukua lulu na kuichunguza kwa makini. Alitoa lensi mfukoni mwake na kuichunguza lulu ile kwa kutumia lensi. Hapo akacheka kicheko cha dharau na kusema.

“Kuna lulu zilizotengenezwa kwa saruji na ni bora kuliko hii. Nafahmu lulu za namna hii. Si lulu bora, itapoteza rangi yake na kumegukameguka baada ya miezi michache tu. Angalia mwenyewe-.” Alisema huku akimpatia Kino lensi na kumuelekeza jinsi ya kutumia. Kino; ambaye hajawahi kuiona lulu kupitia lensi ya kukuza, alishangaa kuona sura ya ajabu ya lulu.

Mlanguzi wa tatu aliichukua lulu kutoka kwa Kino. “Nina mteja ambaye anapendelea vitu kama hivi,” alisema. “Nitakupatia peso mia tano, pengine labda nitaweza kumuuzia mteja wangu kwa peso kama mia sita hivi.”

Kino akainyakua lulu yake haraka kutoka mikononi mwa mlanguzi yule. Alifunga kwenye kipande kile cha ngozi ya swala na kukiweka mfukoni.

Yule mlanguzi mwenye ofisi akasema, “Nafahamu kuwa nitaonekana mpumbavu, lakini bei yangu bado ipo mezani. Peso elfu moja-unafanya nini?” alimuuliza Kino alipoona anaweka lulu yake mfukoni.

“Mnataka kunitapeli,” alisema Kino kwa kufoka. “Sitauza lulu yangu hapa. Ikibidi kwenda makao makuu nitakwenda.”

Hapo walanguzi wale waliangaliana kwa wasiawasi. Walijua kuwa hila zao zimepita kiasi; walijua kuwa wataadhibiwa iwapo watashindwa kuipata lulu ile, yule mlanguzi mwenye ofisi akasema haraka, “Naweza kukuongezea mpaka kufikia peso elfu moja na mia tano.”

Lakini Kino hata hakusikia, akaanza kupenya katika ya umati kuondoka, hasira imemjaa, hata mwendo wake ulikuwa wa hasira. Juana alimfuata nyuma, akilazimika kukimbia polepole kuendana naye.

Jioni ilipofika, majirani wa Kino walikuwa wamekaa ndani ya nyumba zao wakila mikate ya mahindi na maharage huku wakijadiliana yaliyotokea asubuhi. Hawakujua wasimamie lipi. Waliona kuwa ilikuwa ni lulu nzuri, lakini hata wao hawajawahi kuona lulu kama ile, na bila shaka walanguzi wale wanajua vema maswala ya lulu na thamani yake kuliko wao. “Na kumbuka kwamba wale walanguzi hawakuzungumza hili suala kati yao, lakini kila mmoja alifahamu kuwa lulu ile haina thamani yoyote.”

“Lakini labda walipangana mapema”

“Kama ni hivyo basi sote tumekuwa tukitapeliwa maisha yetu yote.”

Wengine wakasema kuwa pengine ilikuwa ni jambo jema kwa Kino kuchukua zile peso elfu moja na miatano. Hiyo ni pesa nyingi, nyingi kuliko alizowahi kuona. Pengine Kino anakuwa mjinga na kichwa ngumu. Fikiria akienda makao makuu na kukuta hakuna mnunuzi aliyetayari kununua lulu yake?

Mtu mmoja muoga-muoga, “Na sasa kwa sababu amewakatalia walanguzi, hawatataka tena kufanya naye biashara. Pengine Kino amejikata kichwa na kujiharibia.”

Wengine wakasema, Kino ni mtu jasiri na shupavu; yupo sahihi kufanya alivyofanya. Na sisi tunaweza kufaidika na ujasiri wake. Watu hawa ni wale waliokuwa wakisifa kitendo cha Kino.

Ndani ya nyumba yake Kino alichuchumaa kwenye mkeka wake wa kulalia akitafakari. Alikuwa tayari ameifukia lulu yake kwenye figa moja. Alikuwa ametulia akishangaa jinsi mkeka wake ulivyosukwa. Ndani yake alikuwa amejawa na uoga. Katika maisha yake hajawahi kuwa mbali na nyumbani. Aliogopa dubwana linaloitwa makao makuu. Lilikuwa liko mbali kuvuka maji na milima, umbali wa maili zaidi ya elfu moja na kila maili ikiwa na kila namna ya hatari. Lakini ulimwengu wa zamani wa Kino ulikuwa umepotea, hakuwa na budi kuukabili ulimwengu mpya. Mipango yake ilikuwa ni halisi, na hakuna cha kuiharibu, alijisemea “Nitakwenda,” na hapo jambo hilo likawa halisi. Kuwa na nia ya safari na kuisema ilikuwa ni kwenda nusu ya safari.

Juana alimuangalia alipokuwa akifukia lulu yake. Baada ya muda akatengeneza keki za mahindi kwaajili ya chakula cha usiku.

Juan Tomas alifika nyumbani kwa Kino na kuchuchumaa pembeni yake, walitulia kimya bila kusemezana kwa kitambo kirefu, mwishowe Kino akasema.

“Unafikiri ningefanya nini? Wale ni matapeli.”

Juana Tomas alitikisa kichwa chake tu. Yeye ndiye alikuwa mkubwa na kino alikuwa akimtegemea kwa ushauri. “Si rahisi kujua,” alisema Juan Tomas. “Tunachojua ni kuwa tumekuwa tukidanganywa toka tunazaliwa, gadi tunapouziwa majeneza yetu kwa bei ya kitapeli. Lakini pamoja na yote, bado tunaishi. Hujasimama dhidi ya walanguzi tu, bali mfumo mzima. Juu ya utamaduni wote. Nina wasiwasi juu yako.”

“Kitu gani cha kunitisha zaidi ya njaa?” alisema Kino.

Lakini Juan Tomas alitikisa kichwa polepole. “Wote tunaogopa hilo. Lakini fikiria labda upo sahihi. Kwamba lulu yako ni kweli ina thamani kubwa, unafikiri huo ndiyo utakuwa mwisho wa haya?”

“Unamaanisha nini?”

“Sifahamu.” Juana Tomasa alisema, “Lakini nina wasiwasi juu yako. Ni nchi mpya unayotembea, nawe hufahamu njia.”

“Nitakwenda. Nitakwenda haraka iwezekanavyo,” alisema Kino.

“Sina pingamizi na hilo, “ alisema Juan Tomas. “Wasiwasi wangu ni iwapo utakuta hali ya makao makuu ni tofauti na hapa. Hapa walau una rafiki zako na mimi kaka yako, huko hautakuwa na mtu yeyote.”

“Sasa nifanyaje?” alisema Kino….mwanangu anatakiwa kupata fursa. Na hicho ndicho wanachotaka kunipora. Rafiki zangu watanilinda.”

“Watakulinda iwapo kufanya hivyo hakuhatarishi maisha yao au hali zao.” alisema Juan Tomas. Hapo alisimama na kusema, “Mungu awe nawe katika safari yako.”

Kino naye akajibu, “Mungu awe nawe pia,” lakini hakuinua uso kumuangalia kaka yake.

Baada ya kaka yake kuondoka Kino alibaki amekaa kichovu kwenye mkeka wake kwa muda mrefu akitafakari. Ilionekana kama njia zote mbele yake zimezibwa. Kichwani mwake ni muziki wa adui tu ndiyo ulisikika. Hisia zake zilikuwa chonjo lakini akili yake ilikuwa mbali kwa mawazo.

Juana alikuwa na wasiwasi juu ya hali ya Kino, lakini alimfahamu vizuri. Alijua kuwa njia pekee ya kumsaidia ni kukaa kimya na kuwa karibu naye. Alimbeba Koyotito mikononi na kumuimbia ili kufukuza mkosi, sauti yake ilikuwa ya kishupavu, ikikabiliana na muziki wa uovu.

Kino hakuinuka pale wala kudai chakula cha usiku. Juana alijua kuwa ataulizia iwapo atahitaji. Macho ya Kino yalionyesha mashaka makubwa aliyokuwa nayo. Alihisi kama kuna kitu kiovu nje ya nyumba yake kikimnyemeloea. Kikimwita kupambana naye. Alishika kisu chake kuhakikisha kama kipo na kisha akaelekea mlangoni. Juana alitaka kumzuia lakini sauti haikumtoka, aliishia tu kuinua mkono. Kino alisimama kidogo mlangoni na kisha akatoka nje gizani. Ghafla Juana akasikia purukushani kutoka nje, alishikwa na uoga mkubwa lakini ujasiri ukamuingia haraka. Akamuweka Koyotito chini na akachukua jiwe moja la mafiga na kukimbia nje. Lakini purukushani zilikuwa zimeshatulia, Kino alikuwa amelala chini akijaribu kuinuka, hakukuwa na mtu mwingine. Juana aliachia jiwe lake na kuzungusha mikono yake kwa Kino kumsaidia kuinuka. Alimshikilia kwenda ndani. Damu ilimvuja Kino kutoka kichwani na alikuwa na jeraha kubwa la kukatwa kutoka kwenye sikio hadi kidevuni. Ilionekana kuwa Kino hajitambui vizuri, alitingisha kichwa chake huku na huku, nguo ake zilikuwa zimechanika-chanika. Juana alimlaza mkekani na kumfuta damu iliyoanza kuganda usoni mwake kwa sketi. Baada ya hayo akamletea kikombe cha Pulque na kumuuliza:

“Ni nani?”

“Sijui,sijamuona.” Alijibu Kino.

Juana akaleta mtungi wa maji na kumuosha jeraha lililokuwa usoni pake huku akimkazia macho usoni.

“Kino mume wangu,” alisema Juana huku machozi yakimlengalenga. “Kino unanisikia?”

“Nakusikia,”

“Kino hii lulu ni mkosi. Tuiharibu kabla haijatudhuru. Tuiponde kwenye mawe. Au tuitupe baharini ilikotoka. Kino hii ni mkosi, mkosi kabisa!”

Alipokuwa akiongea hayo udhaifu ukamuisha Kino. Macho yake yaliwaka na misuli ikamkaza.

“Hapana,” alisema Kino. “Nitapambana hadi mwisho. Na nitashinda. Hii ndiyo fursa yetu, tutaitumia.” Alisema hayo huku akipiga ngumi mkeka wa kulalia. “Hakuna atakayetupora bahati yetu,”. Hapo macho yake yakaonyesha upole, akamshika Juana begani . “Niamini, mimi ni mwanaume.”

Juana akasema, “Kino, nina wasiwasi kuwa hata wanaume wanaweza kuuwawa. Tuitupe baharini.”

“Nyamaza,” alifoka Kino. “Mimi ni mwanaume, nyamaza.” Hapo Juana akakaa kimya, maana Kino aliongea kwa amri. “Mwanga wa kwanza ukitoka tu tutaanza safari. Unaogopa kwenda na mimi?”

“Hapana mume wangu.”

Hapo macho ya Kino yakaonyesha upole, alimshika mke wake mashavuni na kusema, “Basi na tulale kidogo.”
 
Nilisoma km kitabu cha kujibia mtihani hyo form two!
 
SURA YA 5

Mwezi ulitoka kwa kuchelewa, lakini ulitoka kabla ya jogoo kuwika. Kino alifungua macho lakini alitulia tuli, maana alihisi kama kuna kitu kinatembea karibu yake. Alijaribu kutizama huku na huko gizani, kwa msaada wa mwanga wa mwezi ulioingia aliweza kumuona Juana akiamka polepole. Alimuona akienda kwenye mafiga, kwa utulivu sana kiasi kwamba kino alisikia sauti ndogo tu Juana alipokuwa anainua figa moja kisha akatoka nje. Kabla ya kutokomea, alisimama kidogo kumuangalia Koyotito kwenye kitanda chake cha bembea.

Hasira zilimpanda Kino. Akainuka na kuanza kumfuata kimyakimya. Alizidi kumnyemelea huku hasira ikizidi kumuwaka. Juana akawa ametoka kwenye eneo la nyumba akielekea baharini, akajikwaa kwenye jiwe na kupepesuka kidogo, hapo pia akamsikia Kino akimfuata nyuma, akaanza kukimbia. Alikuawa anajiandaa kurusha kitu lakini Kino akamrukia na kumnyanganya lulu aliyoishika. Akampiga ngumi ya uso, ngumi iliyomfanya Juana kuangukia kwenye mawe, Kino akampiga teke la mbavu. Kwa wanga wa mwezi aliweza kumuona Juana amelala ufukweni akipigwa na mawimbi yaliyokuwa yakiinua sketi yake na kuirudisha.

Kino alimwangalia Juana kwa hasira, meno yamemtoka huku akifoka kelele kama nyoka. Juana alimtazama Kino, lakini macho yake hayakuonyesha uoga wowote, alikuwa kama kondoo mbele ya mchinjaji; alikubaliana na hali yake, hakubisha wala kupinga. Hasira zilipompoa Kino, akaondoka akimuacha Juana ufukweni pale. Akapita vichakani kuelekea nyumbani. Kwa hisia alizokuwa nazo, akili yake haikuwa inafanya kazi vizuri.

Alipokuwa akipita vichakani akasikia sauti na kama kuna kitu mbele yake, akatoa kisu chake na kuchoma kitu kilichokuwa hakionekani vizuri gizani, akahisi kisu chake kikizama, akapigwa mueleka mpaka chini. Mikono yenye nguvu ikawa ikimsachi kwenye nguo zake kwa fujo, lulu ikamtoka mkononi na kuanguka mchangani, iling’aa kwa kupigwa na mwanga wa mwezi.

Huku nyuma Juana alijikokota kutoka ufukweni. Alikuwa akihisi maumivu makali usoni na mbavuni lakini hakuwa na hasira juu ya Kino. Alikuwa amesema, “Mimi ni mwanaume,” na hilo lilikuwa na maana fulani kwa Juana. Lilimaanisha alikuwa nusu mwendawazimu, na nusu mungu. Ilimaanisha kuwa Kino alikuwa tayari kushindana nguvu na milima na bahari. Juana, kwa uanamke wake alitambua kuwa mlima utasimama wakati mwanaume akivunjika vipande vipande; alifahamu kuwa bahari itadumu wakati mwanaume akizama ndani yake. Lakini alitambua kitu hicho ndicho kinamfanya mwanaume kuwa mwanaume, nusu mwendawazimu, nusu mungu, na Juana alihitaji mwanaume; asingeweza kuishi bila mwanaume. Japo tofauti hii kati ya mwanaume na mwanamke ilimstaajabisha, lakini alikubaliana nayo na aliihitaji. Hakukua na shaka kuwa atamfuata popote. Pengine sifa za mwanamke za Juana; tahadhari, kufikiri kwa makini, na kuweka usalama mbele zitapunguza uanaume wa Kino na kuwaokoa wote. Alisimama huku akiugumia maumivu, alichota maji ya bahari kwa mikono miwili na kunawa usoni, chumvi ilimuumiza kwenye mikwaruzo aliyopata. Kwa kujikokota akaanza kwenda kumfuata Kino.

Mwezi ukawa umetoka kwenye mawingu yaliyokuwa yameuziba, na sasa Juana akawa anatembea kwenye mwanga. Mwezi ulikuwa ukitoka na kuingia mawinguni mara kwa mara, hivyo Juana alijikuta yumo gizani au kwenye mwanga mara kwa mara. Alitembea mgongo ameuinamisha sababu ya maumivu, kichwa pia kimemuinama. Mara baada ya kupita vichaka akaona lulu iking’aa pembeni ya njia, nyuma ya jiwe. Alipiga magoti na kuikota, mwezi ukaingia mawinguni tena. Juana akabaki amepiga magoti akiwaza iwapo arudi baharini kumaliza kazi yake, alipokuwa akiwaza hilo mwezi ukatoka na akaona maumbo mawili meusi yamelala njiani mbele yake. Alikimbia haraka, alipofika akaona kuwa mmoja ni Kino, na mwingine ni mtu asiyefahamika ambaye kimiminika cheusi chenye kung’aa kilikuwa kinamiminika toka shingoni mwake.

Kino alijigeuza kichovu, miguu na mikono ikimcheza kama mdudu aliyekandamizwa. Mara moja Juana alitambua kwamba maisha yao hayatakuwa kama zamani tena. Mtu amekufa njiani, na kisu cha Kino kikiwa pembeni vilimhakikishia hilo. Muda wote Juana alikuwa akijaribu kurudisha amani ya zamani, zamani kabla ya lulu. Lakini sasa amani hiyo imeshatoweka kabisa na hakuna njia tena ya kuirudisha. Kwa kufahamu haya, mara moja akaachana na ndoto za maisha ya zamani. Hakukua na cha kufanya zaidi ya kujiokoa wao wenyewe. Maumivu yalikuwa yamemuisha, na akawa chonjo. Haraka, akauburuza mwili wa mtu yule hadi vichakani. Akarudi kwa Kino na kumkanda usoni kwa sketi yake mbichi. Fahamu zilianza kumrudia Kino, na akaanza kugumia.

“Wamechukua lulu. Nimeipoteza. Ndiyo basi tena. Lulu imeondoka,” alisema Kino.

Juana alimnyamazisha kama vile anamnyamazisha mtoto anayeumwa. “Hush, lulu yako hii hapa. Nimeikota njiani. Unanisikia? Lulu yako hii hapa, unaelewa? Umeua mtu. Inatupasa kuondoka. Watakuja kutukamata, unaelewa? Tunatakiwa kuondoka kabla hakujakucha.”

“Nilivamiwa,” alisema Kino kwa kujitetea. “Nilishambulia ili kujilinda tu.”

“Unakumbuka yaliyotokea jana?” aliuliza Juana. “Unafikiri watajali hilo? Unawakumbuka watu wa mjini? Unafikiri utetezi wako utasaidia?”

Kino alivuta pumzi ndefu na kujikaza, akajibu,”Hapana, upo sahihi.” Na ujasiri ukamrudia, akawa mwanaume tena.

“Nenda nyumbani kamchukue Koyotito. Pia beba mahindi yote tuliyanayo. Nitaweka mashua kwenye maji kisha tuondoke.”

Kino akachuku akisu chake na kuelekea ufukweni kwenye mashua yake. Alipofika; kwa msaada wa mwanga aliweza kuona kuwa kuna tundu kubwa limetobolewa chini ya mtumbwi. Hasira kali zilimpanda, lakini pia zilimpa nguvu. Sasa giza lilikuwa linainyemela familia yake; muziki wa uovu ulijaza usiku ule, ulisikika juu ya mikoko, ukiimba kufuata mapigo ya mawimbi. Mtumbwi wa babu yake, mtumbwi uliotunzwa miaka na miaka leo hii una tundu chini yake. Huu ni uovu usiofikirika. Uovu wa kuua mtu hauwezi kuzidi uovu wa kuua mtumbwi. Sababu mtumbwi hauna watoto, wala hauwezi kujilinda, na mtumbwi uliojeruhiwa hauwezi kupona. Hasira ya Kino ilichanganyikana na huzuni, jambo hili lilimbadilisha kabisa, sasa akawa kama mnyama, yupo tayari kushambulia, kitu pekee alichojali ni kujilinda yeye na familia yake. Ni kama hakuhisi maumivu kichwani mwake. Aliondoka ufukweni kuelekea nyumbani kwake, wazo la kuchukua moja ya mitumbwi ya jirani yake halikumjia kabisa. Jambo kama hilo kwake ilikuwa sawa tu na kuharibu mtumbwi.

Jogoo wakaanza kuwika, ishara ya kukaribia kukucha. Moshi ulianza kutoka kwenye baadhi ya nyumba na harufu ya mikate ya mahindi ilisikika. Ndege wa asubuhi walikuwa wakiruka vichakani, na mwezi nao ukaanza kufifia polepole na mawingu yakaanza kujikusanya upande wa kusini. Na upepo mkali ulivuma kuelekea kwenye ghuba.

Kino alikuwa akitembea haraka haraka kurudi nyumbani kwake. Sasa akili yake ilikuwa ikifanya kazi zaidi. Alifahamu kuwa kuna jambo moja tu analotakiwa kufanya. Akaishika lulu yake, na kisha kushika kisu chake kuhakikisha kama vipo.

Mbele yake aliona kuna mwanga kidogo, kisha ghafla akaona moto mkubwa ukiruka angani huku ukifoka, njia yote ikawa nyeupe kwa mwanga wa moto. Kino akaanza kukimbia; alijua itakuwa ni nyumba yake inaungua, alifahamu jinsi nyumba za miti zinavyoweza kuteketea ndani ya muda mfupi. Mbele yake akaona mtu anakuja kwa kasi upande wake. Alikuwa ni Juana akiwa amembeba Koyotito mkononi na huku amebebelea blanketi la Kino. Mtoto alikuwa akigumia kwa uoga na macho ya Juana yalionyesha uoga mkubwa. Kino akaona kuwa hawezi tena kuokoa nyumba yake. Hakumuuliza chochote mke wake. Alijua kilichotokea. “Ilikuwa imevurugwa kwa kupekuliwa na sakafu ilichimbuliwa, hata mahali pa mtoto palikuwa pamepekuliwa. Nilipokuwa nachunguza wakawasha moto kwa nje.”

Mwanga wa moto ulimmulika Kino usoni. “Ni nani?” aliuliza.

“Sifahamu hata, “ alijibu Juana.

Kufikia sasa majirani wakaanza kutoka majumbani mwao. Waliona cheche zikiruka na kutua, walikazana kuzikanyaga na kuzizima ili kuokoa nyumba zao. Ghafla Kino akaingiwa na uoga, mwanga ulimfanya apatwe na uoga akakumbuka yule mtu aliyekufa kule kichakani kando ya njia. Alimshika mkono Juana na kwenda naye nyuma ya nyumba moja mbali na mwanga, mwanga ulikuwa ni kitu hatari kwake. Alifikiri kwa muda kidogo, kisha akaanza kutembea kuelekea nyumbani kwa kaka yake; Juan Tomas. aliingia ndani moja kwa moja huku akiwa bado kamshika mke wake. Nje aliweza kusikia sauti za vilio vya watoto na kelele za jirani zake, jirani zake walifikiri pengine alikuwa ndani ya nyumba inayoungua.
 
Nyumba ya Juan Tomas ilikuwa kama tu ya Kino; karibu nyumba zote eneo lile zilikuwa zinafanana, na zote ziliikuwa zinaruhusi mwanga na hewa kuingia ndani. Kwa hiyo Juana na Kino walikaa kwenye pembe moja ya nyumba ya kaka yake na kuweza kuona miale ya moto ikiruka. Miale mirefu sana yenye hasira, waliona paa likiporomoka na moto ukififia polepole. Walisikia kelele za rafiki zao, na Apolonia akilia. Yeye ndiyo alikuwa ndugu wa karibu wa kike, hivyo ni kama lilikuwa jukumu lake kuanzisha kilio.

Katika kulia kwake, Apolonia akatambua kuwa amevaa mtandio ambao siyo bora, akakimbia haraka ndani ya nyumba kuchukua ule mpya na mzuri zaidi. Alipokuwa akipekua kwenye sanduku, Kino akasema kwa sauti ndogo, “Apolonia usipige kelele, hatujadhurika.”

Apolonia alishtuka sana, “Mmefikaje hapa?” alihoji.

“Acha maswali, nenda kamlete Juan Tomas, usimwambie mwingine yeyote. Hili ni muhimu sana.”

“Sawa shemeji,” alijibu Apolonia.

Baada ya muda mfupi Apolonia alirudi na Juan Tomas. Juan Tomas aliwasha mshumaa na kwenda kwenye pembe ambayo Juana na Kino wamejibanza. Akamwambia mke wake, “Apolonia, kaa hapo mlangoni. Usiruhusu mtu yeyeto kuingia. Nini kimetokea mdogo wangu?” alimuuliza Kino.

“Nilishambuliwa gizani, na katika huo ugomvi nimeua mtu.”

“Ni nani?’ aliuliza Juan Tomas haraka.

‘Sifahamu, ilikuwa giza tupu.”

“Ni lulu,” alisema Juan Tomas. “Kuna shetani kwenye hii lulu. Ulitakiwa kuiuza na kuondokana shetani. Pengine bado unaweza kuiuza na kuepukana na mikosi.”

Kino akasema, “Kaka yangu, jambo baya kabisa maishani mwangu limetokea. Mtumbwi wangu umeharibiwa, nyumba yangu imechomwa, na huko vichakani kuna maiti ya mtu. Hakuna kwa kukimbilia. Naomba utufiche kaka yangu.”

Kino akaona mashaka yaliyokuwepo usoni mwa kaka yake, hivyo akamuwahi . “Si kwa muda mrefu, “ alisema haraka. “Ni kwa mchana wa leo tu. Usiku ukiingia tutaondoka.”

“Nitakuficha,” akakubali Juan Tomas.

“Sitaki kukuletea hatari. Najua niko kama ukoma. Lakini usiku nitaondoka nawe utakuwa salama.” Alisema Kino.

“Usijali nitakulinda,” alisema Juan Tomas kisha akamwita mke wake. “Apolonia, funga mlango na usimwambie mtu yeyote kuwa Kino yupo humu ndani.”

Siku hiyo walishinda ndani mchana kutwa, walikuwa wakiwasikia majirani wakiwazungumzia. Kupitia nafasi ukutani waliweza kuwaona majirani wakichambuachambua mabaki ya nyumba yao kuona kama wanaweza kupata mifupa.

Wakiwa wamejibanza ndani ya nyumba ya Juan Tomas, walisikia jinsi ambavyo habari za kuharibiwa kwa mtumbwi zilivyowashtua majirani zao. Juan Tomas yeye alishinda nje ili kuwazubaisha majirani zao, akitoa dhana mbalimbali juu ya kilichotokea kwa Kino, Juana na Koyotito. Katika dhana moja alisema, “Nafikiri wameelekea kusini wakifuata ufukwe. Bila shaka wamekimbia mkosi.” Kwa dhana nyingine alisema, “Kino hawezi kwenda mbali na bahari, pengine amepata mtumbwi mwingine.” Kisha akaongezea, “Jambo hili limemuhuzunisha sana Apolonia.”

Siku hiyo upepo mkali sana ulivuma. Uling’oa vichaka na kuvuma kwa kelele juu ya nyumba, hakuna mtumbwi ulioingia majini siku hiyo. Juan Tomas akasema, “kama Kino alienda baharini, kufikia sasa atakuwa amezama.” Na kila mara Juan Tomas alipoenda kwa majirani aliazima kitu. Alirudi na mfuko wa maharage mekundu na kibuyu kilichojaa mchele. Aliazima kikombe cha pilipili, donge la chumvi na kisu kikubwa ambacho kinaweza kutumika kama silaha pia. Macho ya Kino yaling’aa kwa furaha alipokiona kisu hicho, akakikagua kuona makali yake.

Upepo ulizidi kuvuma na kuchafua bahari, mikoko iliinamishwa na mchanga ulipeperushwa huku na kule. Ulikimbiza mawingu yote na kufanya anga kuwa jeupe.

Jioni ilipokaribia kufika, Juan Tomas alikaa kuongea na mdogo wake. “Utakwenda wapi?” alimuuliza.

“Nitaelekea kaskazini,” alijibu Kino. “Nasikia kuna majiji makubwa huko kaskazini.”

“Sawa, ila kuwa makini usiwe karibu na bahari. Nimesikia kuwa watu wa mjini wanajiandaa kukutafuta kandokando ya bahari. Bado unayo lulu?”

“Ninayo bado. Na nitaitunza. Pengine ingefaa ningeigawa kama zawadi lakini sasa imekuwa ni mkosi wangu na tegemeo la maisha yangu. Nitaitunza.” Aliongea Kino huku macho yake yakionyesha ukatili, ujasiri na uchungu mwingi.

Koyotito alisikika akilia na Juana alimuongelea maneno fulani kumnyamazisha.

“Upepo ni mkali, hamtaacha alama njiani.” Alisema Juan Tomas.

Giza lilipokolea waliondoka haraka kabla mwezi haujatoka. Juana alimbeba Koyotito mgongoni, akimfunga kwa mtandio wake na haikuchukua muda mtoto akawa amelala. Juan Tomas alimbusu mdogo wake kwenye mashavu yote, “Mungu awe nawe,” alisema kama vile hatamuona tena. “Hutaki kabisa kuachana na lulu?’

“Lulu hii imeshakuwa roho yangu,” alijibu Kino. “Nikiachana nayo, na roho yangu itapondeka. Mungu awe nawe pia.”
 
SURA YA 6



Upepo mkali ulikuwa ukivuma, uliwapiga Juana na Kino kwa vijiti, mchanga na mawe madogomadogo. Walijitanda nguo zao vizuri zaidi, wakafunika pua zao na kuanza safari ya kuelekea kwenye dunia pana. Anga lilikuwa jeupe kwa kusafishwa na upepo, nyota nyingi zilionekana angani. Walitembea kwa uangalifu mkubwa wakiepuka kupita katikati ya mji; wasijeonwa na wale wanaolala vibarazani. Kawaida mji huwa tulivu kabisa usiku hivyo yeyote anayetembea-tembea usiku ni rahisi kugundulika. Kino alipita pembeni-pembeni ya mji na kuelekea kaskazini akifuata nyota. Huko alishika barabara ya mchanga iliyopita katikati ya vichaka, ikielekea Loreto.

Kino alifurahi kutembea kwenye njia ya mchanga, alijua kuwa baada ya muda mfupi hakutakuwa na alama ya nyayo zao, nyota ndizo zilimuongoza. Nyuma yake alisikia hatua za Juana, ilimlazimu Juana kukimbia mara kwa mara ili kuendana na kasi ya Kino.

Upepo ulivuma kutoke nyuma yao, ulipiga kelele ulipopita vichakani lakini familia ya Kino ilikaza mwendo kimya kimya, saa baada ya saa. Njiani hawakupishana wala kuona mtu yeyote. Baada ya mwendo wa saa kadhaa mwezi ukatoka. Mwezi ulipotoka, upepo ukatulia na nchi ikawa kimya kabisa.

Sasa waliweza kuona njia wanayotembea. Ilikuwa tuta mabonde mawili yaliyotengenezwa na magurudumu. Kwa sababu sasa upepo ulikuwa umetulia, Kino alikuwa na wasiwasi kuwa wataacha alama za nyao, lakini labda wameshaenda mbali sana na mji na alama zao hazitagundulika; aliwaza Kino. Sasa Kino akaanza kutembea kwenye yale mabonde ya magurudumu, aliwaza kuwa kama ukitokea mkokoteni mkubwa unaenda mjini wakati wa asubuhi basi utafuta alama za nyayo zao.

Walitembea usiku mzima, bila kupumzika wala kupunguza mwendo. Kuna wakati Koyotito aliamka, Juana alimtoa mgongoni na kumbembeleza hadi alipolala tena. Vimbwanga vya usiku navyo havikuwaacha, mbwa mwitu walilia na kutoa sauti kama wanacheka vichakani. Bundi waliruka karibu yao wakipiga kelele. Mara nyingine vilisikika vishindo vya mnyama mkubwa akikimbilia vichakani. Kino akashika mpini wa kisu chake barabara, akiwa tayari kwa lolote. Muziki wa lulu ulijaa kichwani mwake, huku ala aya muziki wa familia ukisikika kwa mbali, nyimbo hizi zilichanganyikana sauti za ndala miguuni mwao. Walitembea usiku wote. Asubuhi ilipokaribia, Kino akatafuta maficho pembeni ya barabara ambamo wangejificha mchana, aliona sehemu moja kando ya barabara, pengine yalikuwa makazi ya paa. Lilikuwa ni eneo pana kidogo, lenye vichaka vingi vilivyoziba upande wa barabara. Juana alipokaa na kuanza kumyonyesha mtoto, Kino alirudi barabarani. Alikata kipande cha tawi na akafuta alama za nyayo zao kwa uangalifu. Mwanga ulipotoka kabisa akasikia sauti ya mkokoteni, alipochungulia aliona mkokoteni mkubwa unaokokotwa na ng’ombe ukipita. Ulipotokomea alirudi barabarani na kuona kuwa alama zote za nyayo zimefutika. Akafuta alama alizoweka na kurudi kwa Juana.

Juana alimpatia Kino keki ya mahindi ambazo Apolonia alikuwa amewafungia, kisha yeye akalala kidogo. Kino yeye hakulala, alikaa akitazama ardhi, akiangalia msafara wa siafu uliokuwa karibu na mguu wake. Aliweka mguu wake kuwaziba njia. Siafu wale walipanda juu ya mguu wake na kuendelea na safari yao, kino akaacha mguu wake pale akiendelea kuwatazama.

Jua lilianza kupanda na kuwa kali. Walikuwa mbali na ghuba hivyo hewa ilikuwa kavu na na ya moto kiasi kwamba vijiti vya vichaka vilisikika vikipasuka kwa joto na harufu ya unga ulio ndani yake ilisambaa. Juana alipoamka, ilipokuwa karibu na mchana, Kino akaanza kumuambia vitu ambavyo tayari Juana alivifahamu.

“Kuwa makini na huo mti,” alisema Kino akionyeshea mti Fulani. “Usiushike, ukiushika kisha akashika macho unapofuka. Na kuwa makini na huo mti unaotoa utomvi, huo hapo. Ukiuvunja na ukatoa damu, unapata mkosi.” Juana alitikisa kichwa na kutabasamu, alikuwa anjua vitu hivi vyote.

“Watatufuatilia? Unafikiri watajaribu kututafuta?” aliuliza Juana.

“Bila shaka,” alijibu Kino. “Na yeyote atakayetupata ataanza kwa kutupora lulu.”

Juana akasema, “Pengine wale walanguzi walikuwa sahihi. Pengine ni kweli lulu hii haina thamani yoyote.”

Kino aliingiza mkono mfukoni na kutoa lulu. Aliiweka kwenye mwanga wa jua na ikang’aa hadi kumuumiza macho. “Kama ingekuwa haina thamani wasingejaribu kuiiba,” alijibu Kino

“Unamfahamu waliokushambulia? Walikuwa walanguzi?”

“Hata sifahamu, sikuweza kuwaona.” Alijibu Kino.

Kino aliingalia taswira yake iliyokuwa ndani ya lulu ile. “Nikiiuza nitanunua bunduki.” Alitazama ndani ya lulu kuangalia bunduki yake lakini badala yake aliona tu mwili wa mtu umelala chini gizani, huku kitu chenye kung’aa kikimtoka shingoni. “Tutafunga ndoa kanisani.” Alisema Kino, lakini ndani ya lulu alimuona Juana akiwa na majeraha usoni, akijikongoja kurudi nyumbani katikati ya usiku. “Mtoto wetu lazima ajifunze kusoma.” Alisema kwa shauku, lakini ndani ya lulu alimuona Koyotito akiwa amevimba kwa homa kutokana na dawa alizonyweshwa.

Kino akaiweka lulu yake mfukoni , muziki wa lulu umegeuka kuwa muziki wa hatari masikioni mwake, umechanganyikana na muziki wa uovu.

Jua lilizidi kuwa kali hivyo Kino na Juana wakajisogeza kwenye kichaka zaidi. Katikati ya mchana Kino akaamua kupata usingizi kidogo. Akafunika uso wake kwa kofia, akavuta blanketi lake na kulala.

Lakini safari hii Juana hakulala. Alitulia tuli kama jiwe. Mdomo wake ulikuwa umevimba sehemu aliyopigwa na kino, na nzi mmoja mkubwa alikuwa akimzonga kwenye jeraha kidevuni mwake. Koyotito alipoamka alimlaza mbele yake na kuanza kucheza naye, alikata tawi dogo na kuanza kumtekenya nalo, kisha akampatia maji aliyokuwa amebeba katika kibuyu.

Kino alikuwa akipiga kelele kwa usingizini na mikono yake ikaonyesha ishara ya kupigana. Haikuchukua muda akawa ameamka. Macho yalikuwa yamemtoka na pua yake ilikuwa nyekundu. Alijaribu kusikiliza kwa makini lakini aliweza tu kusikia kelele za vichaka vikipigwa na joto na mvumo kwa mbali.

“Ni nini?” aliuliza Juana.

“Shh,” alimnyamazisha Kino.

“Ulikuwa unaota.”

“Pengine.” alijibu Kino kwa mkato. Juana alipompatia mkate, alikula huku akiacha kutafuna na kusikiliza kwa makini. Alikuwa amejaa wasiwasi; aliangalia huku na huko; alishika kisu chake vizuri. Koyotito alitoa sauti ya kukoroma.

“Mnyamazishe.” Alisema Kino.

“Kuna nini?” alihoji Kino.

“Sijui.”

Kino alitulia na kusikiliza kwa makini. Kisha akasimama na polepole na kwa tahadhari akapenya vichakani kuelekea barabarani. Lakini hakufika barabarani, alijibanza kichakani na kuchungulia njia waliyojia.

Hapo ndipo alipowaona. Mwili wake ukamkakamaa akajificha na kuchungulia zaidi. Kwa mbali aliweza kuona watu watatu, wawili wakiwa kwa miguu na mmoja akiwa juu ya farasi. Alitambua ni watu wa aina gani. Baridi ya uoga ikamuingia mwilini. Japo alikuwa mbali lakini aliweza kuona kuwa wawili wale walikuwa akitembea polepole wakiwa wameinama. Mara kadhaa walikuwa wakisimamam na kuchunguza ardhini. Walikuwa ni wafuatilia alama, walikuwa ni wawindaji. Waliweza kuchunguza alama alimopita mbuzi-pori hata kama eneo hilo ni miamba mitupu. Walikuwa na hisia kama za mbwa. Hata kama alama ya nyayo zimepitiwa na magurudumu ya mkokoteni lakini wawindaji hawa wangeweza kuzifuata. Waliweza kusoma vijiti vilivyovunjika au lundo dogo la mchanga. Nyuma yao alikuwepo mpanda farasi, pua yake ilikuwa imefunikwa kwa blanketi na pembeni ya tandiko la farasi alikuwa ameweka bunduki iliyong’aa juani. Kino alitulia kimya kama tawi la mti. Hata pumzi haikumtoka, akapeleka macho pale alipokuwa amefuta alama za nyayo. Hata alama ile ya kufagia inaweza kuwagutusha wawindaji wale. Aliwajua vema watu hawa. Waliweza kuishi kwenye nchi kame yenye wanyama wachache sababu ya uwezo wao wa kuwinda, na leo walikuwa wakimuwinda yeye. Sasa walikuwa wamechuchumaa, ilionekana kuna kitu wamegundua. Mpanda farasi alikaa pembeni kuwasubiri.
 
Back
Top Bottom