MADAM PRESIDENT 04
Nilipita kwenye bustani ndogo ya maua Kisha nikaendelea mbele ambapo alitokea mlinzi mmoja akanikaribisha Kisha akachukua begi langu dogo akaniongoza njia, tulienda sehemu Nyingine ambapo tulipita kwenye ofisi Nyingine Kisha nikaambiwa nisubiri hapo,
Kwa kila namna Sasa nilianza kujisikia vibaya kukaguliwa Mara kupitishwa kwenye vidude gani nilitamani kugeuza kurudi....
Ni Kama Yale yote yalikuwa madogo..
Ni wakati nimekaa hapo nikikunja kunja vidole na kuangaza macho huko na huko akatokea mzee mmoja hivi ambaye alinisalimia kwa tabasamu Kisha akafungua mlango uliokuwa mbele yake akaniita ,
Hakuwa na maneno mengi akaniashiria nikae kwenye kiti ambacho Kiko mbele yake Kisha akafungua kabati na kutoa vifaa Kama vya kidaktari hivi....
"Aah mzee achana na Mimi aisee"
Nilijikuta Sasa uvumilivu unanishinda,
"Hahaha Tulia bhana Kijana mbona saa ulivaa? Tunamalizia tu zoezi dogo" alisema huku akichukua kidole changu na kukitoboa kidogo kwa sindano Kisha akachukua damu na kuipachika kwenye kidude Kama saa,
Alinipigisha Hadithi ambazo hazikuwa na kichwa Wala miguu nilishaelewa kuwa anasubiri vipimo vyake hivyo sikumjibu kitu na hatimaye akaacha kuongea baada ya kuona nimekasirika ...
Baada ya dakika Kama nane hivi alikichukua kile kidude na kukiingiza Tena kwenye kitu mfano wa saa ambapo alibinya binya namba fulani Kisha akatabasamu...
"Haya twende"
Alisema Kisha tukatoka Tena na kupanda ngazi ambapo aliniacha kwenye chumba kingine akaondoka zake...
Ni baada ya dakika tatu alitokea madam Janet akiwa na walinzi wawili nilisimama na tukasalimiana wale walinzi hawakunisalimia walinikodolea macho mpaka nikaishiwa pozi..
Tuliongozana na madam tukipiga stori mbili tatu mpaka kwenye chumba kingine kikubwa ambacho walinzi walibaki nje ..
"Aisee siwezi kurudi Tena hapa"
Nilisema wakati nikikaa vizuri kwenye sofa
"Haha pole hata hapo bado Kuna step tumekanyaga kanuni zinasema uje hapa wiki moja kabla, "
Alisema Janet kana kwamba haikuwa Shida kubwa...
Aliniuliza habari za kazi na Mipango mingine ya maisha
Sikuwa na maneno mengi kwanza sikuwa najisikia vizuri...
"Nimekumisi Sana wewe mwanaume yaani hapa ofisini hapakaliki mpaka navurugana na mawaziri yaani sijui Hilo dudu lako likoje yaani"
Alisema Janet huku akicheka,
"Ah mzee si yupo nilimuona siku Ile ya kuapishwa"
Nilisema
"Wee bado mgeni kwenye hii nchi ndugu? Mimi Janet niwe na mzee Kama Yule na watoto hao niwapate lini?"
Hahahaa hata hivyo wapo hapa kama utataka kuwaona! "
Janet aliongea Kish akanishika mkono...
"Sikia tunaingia kwenye chumba ambacho hatuonekani kuwa na amani mpenzi wangu"
Alisema Janet akinivuta nami nikaingia chumbani na kazi ikaanza....
Ni Kama alikua amenipania hata hivyo shughuli aliipata na mwishowe akapitiwa na usingizi nilienda bafuni kuoga Kisha nikachukua begi langu ambalo lililetwa nikavaa suti nyingine niliangalia saa yangu ilikua saa 12 jioni, njaa iliniuma Sana, nilimwamsha Janet ambaye alistuka kuniona nimevaa nguo nyingine.
"Vipi? "
Alisema akijifinyanga macho
"Madam siwez kulala hapa, halafu hapa Ni nyumbani kwako"
Nilisema huku nikionyesha dalili za kukasirika..
"Okay nashukuru hata hivyo nitajua namna ya kufanya najua una njaa Ila Sasa chakula Cha hapa Ni hakiivi Sasa hivi na ningependa ule chakula Cha Raisi leo"
Alisema janet Kisha akasimama vile vile na kunibusu..
Nitafanya mpango wiki mbili zijazo tuinjoy zaidi
Alivaa nguo zake Kisha akanitoa nje ambapo mlinzi mmoja alinifikisha kwenye chumba kingine ambacho nilimkuta dada mmoja ambaye alininipa begi langu Pamoja na bahasha nyingine nilitoka nje ya geti nikapiga ishara ya msalaba kutoka salama mle ndani....
"Siwezi kurudi Tena hapa kwakweli" nilijikuta nasema moyoni huku nikichanganya miguu .....
Niliangalia Ile bahasha na kukuta kiasi Cha pesa na zilikua Ni Dola za kimarekani..
Nilitafuta mgahawa mzuri nikapata chakula Kisha nikarudi zangu mlandizi,
Nikiwa kwenye Basi nilifikiri mengi Sana niliwaza mwisho wa Jambo hili utakuwaje,
Vipi Raisi akijua kuhusu familia yangu? Vipi ikijulikana natembea na Raisi?
Ni wakati natoa Simu yangu niliangusha kitambaa changu kwa bahati mbaya nikainama kukiokota wakati nanyanyua uso macho yangu yakagongana na huyu abiria mmoja aliyekaa upande wa nyuma,
Nilijaribu kumuangalia lakini kwa haraka Sana akaendelea kubonyeza Simu yake kana kwamba hakuniona,
Sikutilia maanani ingawa nilijikuta tu namuwaza na Sasa akili yangu ikakumbuka, wakati naingia pale rock mall kupata chakula alikuwa nyuma yangu na wakati nakula yeye alikua anakunywa maji
Ni wakati gani alipanda kwenye Basi sikutilia maanani...
"Au labda namfananisha" nilijisemea
Tulifika mlandizi majira ya saa tatu na robo usiku, moyoni nilikua najisikia huzuni kubwa na nilikua nikijihisi aibu kurudi nyumbani kwa mke wangu usiku ule,
Nilishuka na kuvaa begi langu Kisha nikasogea mpaka kwenye kijiwe Cha boda boda, ndipo yule jamaa nae kwa mbali niliona akiwa anashuka kwenye Basi wakati naongea na boda nilipogeuka sikumuona tena!
"Twende misongeni kwa mzee kivu"
Nilisema nikichukua boda boda,
"Wapi Ile ya juu au kule madukani"
Boda aliuliza
"Ya juu"
Nilisema nikikaa kwenye piki piki.
Nilifika nyumbani kwangu na mke wangu alikua ananisubiri Kama ilivyokuwa kawaida yake,
Nilitoa uongo tu kuhusu kazi na bla bla ikaisha...
Hata hivyo nilijiambia Mara hii siwezi kutoka Tena na Madam President potelea pote,
"Aniue tu, Kama mbwai na iwe mbwai"
Nilijisemea huku nikipanda kitandani.
*****************
Katikati ya usiku wa manane nilihisi Kama Kuna mtu anapita sebuleni,
Halafu Tena nikahisi Kama amekuja chumbani kwetu na kusimama baadae sikukumbuka Tena kilichotokea tulikuja kuamshwa na dada wa kazi Stella saa 4 asubuhi kwa ajili ya chai!
"Mimi nilijua leo hamuendi kazini"
Alisema Stella akiwa mlangoni, nilijaribu kunyanyuka lakini mwili ulikua mzito, mke wangu pia nae alijihisi uchovu...
Ndipo fahamu zangu zilirejea
"Mama tumevamiwa, wezi bila shaka wametupulizia dawa ya usingizi"
Nilisema Sasa nikisimama kutoka kitandani
Nilipitia mpaka sebuleni ambapo Kila kitu kilikua sawa , nilirudi Tena chumbani ambako niliangalia kabati lilikua sawa Ni Kama Kila kitu kilikua sawa...
Nilichukua Simu yangu na kumpigia Mkuu wa idara kumueleza Hali yote iliyotokea na Polisi walifika muda mfupi, walijaribu kuangalia sehemu kadhaa na kutuhoji ,
Daktari alifika pia na kutupima na alithibitisha kuwa dawa Kali ya usingizi ilikuwa imepulizwa
*****************
Ni wiki moja baada ya tukio sikuwa na mawasiliano yoyote na Janet kitu ambacho niliona kizuri sana,
Nikiwa ofisini baada ya kazi kupungua niliingia kwenye akaunti ya Yahoo ili nisome baadhi ya jumbe kutoka kwa marafiki,
Lakini kipekee tu nilidhani ningepata Hata meseji moja kutoka kwa Jacob,
Maana ilishapita miezi sita hatujawasiliana,
Ni wakati nafungua nilikuta meseji ambayo ilitumwa siku kadhaa zilizopita na mtu ambaye hakutaja jina lake Wala anuani yake haikuonekana,
"Unavuka barabara na ukiwa na mke wako na watoto angalia hiyo Gari inayokuja Kasi,
Jitahidi uvuke kwa spidi au urudi nyuma"
Ujumbe uliishia hapo, nilijaribu kuelewa lakini sikuambulia chochote hatimaye niliamua kumtumia Jacob Ile ujumbe huku nikiomba msaada wake,
Hata hivyo sikuelewa Jacob Anaweza kunijibu lini...
Ghafla wazo lilinijia,
Niliona Tena sio salama kukaa mazingira yale tayari mke wangu alikua mjamzito wa mtoto wetu wa pili, na tayari alishachukua likizo ya kwenda kujifungua,
Nilitoka ofisini haraka na kuchukua boda boda mpaka kwangu,
"Dear jiandae taratibu funga mizigo yako ya muhimu taratibu, Stella atakusaidia kwenye usiku tutaondoka hapa sitaki tukae mazingira haya kwa kipindi hiki"
Nilimuelewesha Kisha nikarudi kazini,
Nilitoa Simu Yangu na kumpigia jose,
"Kaka naomba unipeleke sehemu Leo usiku "
Nilisema baada ya simu kupokelewa
"Ha Kaka usiku Tena, vipi kwema"
Jose aliongea,
Huyu alikua Ni dereva pale stendi na Mara nyingi alikua ananibebea mizigo yangu wakati wa ujenzi wa nyumba zangu...
Tulikubaliana Kisha nikampigia gogo aliyekuwepo huko misufini ambako nilitegemea kumpeleka mke wangu,
Haikuwa mbali Sana na mjini lakini ilikua Ni sehemu nzuri sana kwa kutulia ama kujificha Kama nilivyowaza,
**************
Saa mbili usiku tulianza safari na ndani ya masaa matatu na nusu tulishafika na kushusha mizigo,
Nyumba ilikua kubwa na nzuri Sana,..
Tulishusha mizigo kwa kusaidiana na Yule kijana ambaye nilimuacha kama mlinzi, Mimi na Jose tulirudi Tena kumalizia mizigo iliyobaki...
"Kaka usiniambie ule mjengo Ni wako"
Nilitabasamu tu Kisha nikamwambia Jose kwa msisitizo..
"Jose wewe Ni Rafiki yangu, nimekuchagua kwenye hii kazi kwakuwa nakuamini,
Siku sio nyingi pengine Kuna Mambo mabaya yanaweza kunipata, naomba mtu yoyote asijue kuwa mke wangu anakaa katika Ile nyumba ndio maana tumehamia usiku,
Jose alisimamisha Gari ghafla na kutoka nje..
"We jamaa unaumwa? Mbona unongea ujinga hivi?" Eti Nini?
Jose alihamaki akitweta...
"Jose sikiliza bhana sijasema nitakufa! Nimesema naweza kupatwa na jambo baya kwa tahadhari tu sitaki mke wangu aguswe tutaongea zaidi hebu tumalize kazi kwanza tukachukue mizigo iliyobaki....
Ilikua Ni Kama saa Saba usiku na tulikuwa tunakaribia kufika kwangu ndipo kwa mbali nikaona piki piki imeegeshwa nje kwangu,
"Jose ona kule!"
Nilisema nikinyoosha kidole
"Aisee huyu fala anaweza kuegesha kabisa piki piki nje kwa mtu saa hizi?"
Jose alisema akiongeza Mwendo..
"Sikiliza usipaki pale home fanya Kama unapita hiyo nyumba tumsome kwanza huyo boya" nilisema