MADAM PRESIDENT 10
Tulifika mpaka kwenye Ile gesti nikachukua ufunguo na Kuingia ndani,
Yule dada Alikua anapepesa macho huko na huko,
"First Money, brother,!"
Alisema kingereza chake Cha kuunga unga,
"Asubuhi utapata pesa yako"
Nilimwambia huku nikienda bafuni kuoga,
Niliacha kila kitu mezani na nilijaribu kumchungulia Kama atafanya chochote lakini niliona tu amekaa kwenye kiti vile vile akichezesha miguu yake,
Nilimaliza kuoga na kuvaa bukta kule kule bafuni, Kisha nikatoka,
"Kaoge na wewe"
Nilisema huku nikiweka sawa wigi langu kana kwamba Ni nywele zangu
alienda bafuni kuoga Kisha akarudi amejifunga Taulo tu..
"Ila Kaka yangu utaongeza pesa hatukupatana kulala"
Alisema Sasa akipanda kitandani...
Sikumjibu nilikaa kitandani nikatoa laptop yangu nikaendelea na kazi yangu ndogo Kisha nikamgeukia...
"Sijui unaitwa Nana Dada"
Nilisema kwa upole
"Jesca"
"Okay Jesca kwanza samahani lakini naomba uvae nguo zako hatutafanya chochote nataka Kuna Jambo tuongee"
Nilisema bila kumuangalia
"We mkaka vipi yaani unilete Hadi hapa ujue mi nipo kazini ,au unaionaje kwanza? Nakujazia watu hapa Sasa hivi!"
Aling'aka,
"Hahaha sikiliza Jesca tumepata elfu 20, Ila ukasema tukilala niongeze pesa nikasema elfu 30,
Sasa Mimi nitakupa elf 50 Ila kwanza unisikilize"
Nilisema Sasa nikimgeukia,
"Sitaki kujua kwanini unafanya hii biashara, Ila macho yako yanaonekana kabisa hutaki kuifanya hii biashara"
Nilianza hotuba yangu,
"Nimekuchagua wewe nikiamini utanisaidia kazi yangu ndogo"
"Hivi karibuni umesikiliza vyombo vya habari unaweza kumjua huyu jamaa?"
Nilisema nikimgeuzia picha yangu pale kwenye laptop
"Mmmh ndio Nani sijui mkurugenzi wa huko mlandizi aliyeiba milioni Mia sijui?"
Alisema Jesca,
"Yap, "
nilitabasamu Kisha nikatoa lile wigi na kutoa miwani
"Aah kumbe ndio wewe"
Alisema Jesca huku akionyesha kutokujali Sana..
"Okay Sasa iko hivi Mambo Ni tofauti na wanavyosema huko nje, sijaiba hizo pesa ingawa najua zilipo, Sasa Cha kwanza kabisa nataka ukubali kunisaidia au la nikupe pesa yako elfu 20 usepe na naamini hutamwambia yeyote, Kama ukikubali nitakuambia Jambo lenyewe"
Nilisema
"Okay niambia nione namna ya kukusaidia"
. alisema
"Kwanza nataka utafute nyumba uswazi Kama manzese, tandale, temeke au buguruni ya vyumba viwili au vitatu na sebule ukishapata nitakupa pesa ulipie miezi mitatu, Ila ionekane ni wewe unapanga, lakini rafiki zako au mtu yoyote asifahamu, ukishapata hiyo nyumba utanipigia kwenye namba hii 0688 990 975
Uniambie hivi
"Kuku wako tayari "
Nitakuambia tukutane wapi..
"Mmh Ila Kaka Yangu Mimi naogopa haya Mambo jamani Nina familia inanitegemea"
Alisema
"Jesca kwa mtazamo Wangu kazi hii unayofanya Ni ngumu zaidi ya hii"
Nilimwambia
Nilitoa elf 50 na kumpa Kisha nikamruhusu aondoke zake,
****************
Ilikua majira ya saa 10 baada ya siku tatu,
Jesca alinipigia kuwa kuku Yuko tayari manzese,.
Tulikutana manzese darajani nikiwa nimevaa vile vile Lile wigi kubwa kichwani tulitembea na kushuka vichochoro vya mitaa mpaka tukafika kwenye nyumba yenyewe
Ilikua nyumba ya vyumba vitatu na sebule niliangalia na kuikubali wakati nataka kutoa kiasi Cha pesa nimpe nilijjikuta nikitazamana na mitutu ya bunduki,
Askari walikua chumba Cha pili,
"Jesca umeshindwa kuniamini mama?"
Nilisema niking'ata meno kwa hasira
Jesca Sasa alianza kunionea huruma huku akijaribu kuniomba radhi kwa macho ..
Polisi waliniweka Kati Kati huku mmoja akiwasiliana na makao makuu kuwa wapo na Mimi,
Niligeuka Tena kumuangalia Jesca huku nikimtingishia kichwa...
Tulitoka kwenye Ile nyumba huku Polisi mmoja akiwa amebeba begi langu tayari walishanivalisha pingu mkononi,
Kwa mbali nilisikia Sauti za ving'ora na wakati tunatokea barabarani tayari magari ya polisi yalikua Kama utitiri, wananchi walikua wameshaanza kujitokeza barabarani na waandishi wa habari kibao,
Niliingizwa kwenye Gari ya polisi huku msafara ukianza kuelekea kituo Cha polisi magomeni,
Polisi walifanya kazi ya ziada kuzuia umati wa watu ambapo kila mmoja alikua anataka kuniona
Tuliingia kituo Cha polisi nikapelekwa moja kwa moja kwenye chumba Cha mahojiano,
Polisi walinitoa Lile wigi na miwani na mahojiano yakaanza Polisi walitaka kujua zilipo pesa nilizoiba
Milioni hamsini,
Niliwajua vizuri Polisi wetu wa Tanzania endapo ningekataa Basi wangenipiga Sana wakiamini Ni kweli najua pesa zilipo
"Nitawaeleza kila kitu lakini kabla ya yote Kuna ujumbe nataka ufike kwa Raisi moja kwa moja"
Nilisema
"Hahaha wewe mpuuzi huo muda hatuna, sema pesa iko wapi"
Alisema Yule Afande.
"Afande nilishakuahidi kukupa ushirikiano ,na wewe nipe ushirikiano!"
Nilisema kwa upole Yule Askari alitoka na Kama dakika kumi hivi alirejea..
"Haya lete huo ujumbe wako tuupeleke"
"Kwani wewe ndio Raisi?"
Hakunijibu kitu aliachia bonge la kibao mpaka nikaona Giza hivi,..
"Basi Afande utaniua bure tu, lakini pasipo ujumbe wangu kumfikia Raisi moja kwa moja sitaongea chochote"
Nilisema huku nikifumba macho ili kusubiria Kama kutakuwa na kipigo
Yule Askari alitoka na Kama dakika ishirini alikuja kunitoa na kunipeleka chumba kingine kulikua na Simu ya ofisini,
Baada ya muda Simu iliita na ikasadikika mheshimiwa Raisi yupo hewani,
Nilikua naijua Sauti ya Janet hivyo wasingenifanyia mchezo wowote wale Askari...
"Halo Una dakika mbili za kueleza Shida yako baada ya sekunde kumi kutoka Sasa Raisi ataongea na wewe,
Nilisubiri sekunde kumi na kweli Janet alienda Hewani.
"Hello bila shaka una Jambo la Msingi Allan"
Alisema Janet sauti yake ilijaa hofu
"Ni kweli tafadhali Sana kabla sijahukumiwa nilikuwa na kitu fulani ningependa kukupa haswa ikizingatia wewe Ni Raisi wa watu wote Kuna Jambo lipo nyuma ya hii kesi Kama Raisi nataka ulijue" nilianza.
"Allan kumbuka upo chini ya watu wa usalama hapo Ni vyema ukajikita Sasa kueleza hoja yako ya Msingi una dakika moja"
Alisema
"Tuma watu wako Sasa hivi waende pale Kimara darajani Kuna mtu anauza vitabu anaitwa bwana nditi, Kuna mzigo niliacha kwa ajili yako"
Nilisema Kisha Mimi ndio nikakata Simu!
Polisi waliangaliana tu, Kisha nikarudishwa kwenye chumba Cha mawasiliano..
Nakumbuka kila jioni nilifika kwa Bwana nditi pale Kimara na kuchukua kitabu kimoja nikatafuta gesti nikalala,
Kwa muda wa wiki nzima pale tayari nilishasoma vitabu vitano,
Nilijua lazima ipo siku nitakamatwa hivyo niliweka tahadhari
Nikachukua picha moja na barua moja ambayo alikua ameniandikia Janet nikaitoa nakala mbili Kisha nikaweka kwenye bahasha,
Nilifika siku hiyo baada ya kuchukua kitabu nilimwambia Bwana Nditi aweke hiyo bahasha siku yoyote Kuna watu watakuja kuichukua ,
"Kwahiyo pesa umeweka wapi?"
Nilishtuka kwenye dimbwi la mawazo na swali Hilo la polisi,
"Ni kweli nilichukua pesa Ila sio million hamsini"
Nilisema tu huku nilitabasamu
"Umechukua tsh ngap?"
Polisi aliuliza.
"Ni laki 2 na elfu kumi pesa ya posho ya safari"
Nilisema Tena
Yule polisi alicheka tu Kisha akaanza kunishushia kipigo mpaka damu zikaanza kunitoka,
Nilikua nawazuga nikijua muda wowote Janet atapata ujumbe wake niliomuandikia pamoja na Ile picha,
Yule Polisi baada ya kuridhika na kipigo alitoka nilikua najisikia maumivu kila sehemu na sikutegemea Kama ningeweza Tena kuvumilia ilikua Ni wakati namalizia kidato Cha sita Wakati Janet anaenda chuo kikuu tulikutana Korogwe Mara ya mwisho na tukapiga picha nyingi Sana za ukumbusho ,
Tofauti na picha nyingine hii tulipiga kitandani! Tena tukiwa na nguo chache tu mwilini...
Pamoja na barua yake ya upendo ambayo alinitumia alipokua chuo kikuu katika barua hiyo pia alikua amekumbushia mapenzi niliyompa siku Ile Korogwe kuwa hawezi kuyasahau....
"Janet tucheze hii game tuone"
Nilijisemea nikiwa pale kwenye kiti
Niliendelea waliniacha pale pale huku nikisikia majadiliano huko nje, ilikua wazi kulikua na kundi kubwa la waandishi na watu wengine waliotaka walau kuchukua picha,
Nilipiga mahesabu ya muda na kuona Sasa Janet atakua ameshika barua mkononi,
"Hizo Ni copies, hakuna barua yako Hata moja niliwahi kuichana, hakuna chochote ambacho umenifanyia kiwe kibaya au kizuri ambacho sijaweka ushahidi,
Nifutie kesi hii vinginevyo jambo lolote baya likinitokea hutakua salama, utachafuka Sana Janet,
Think about that"
Nilihitimisha katika barua hiyo fupi,
Na hicho ndicho ambacho kilikuwepo katika Lile boksi ambalo nililiweka kule kwenye nyumba yangu,
Katika maelezo hayo kulikuwa na sehemu maalumu ya kupeleka vitu hivyo, pamoja na hayo kulikua na email na nywila yangu , ili kupata taarifa nyingine muhimu juu ya mahusiano yetu...
"Sidhani Kama Janet atakubali Siri ifichuke"
Niliwaza.
***************
Sasa Ni zamu ya Jose kusimulia..
Niliamua kuzima Simu kabisa ili nisipatikane nilikua sina Majibu hususani baada ya Ile taarifa ya habari,
Nisingekua na Jambo la kumueleza Shemeji ..
Kwanza angenilaumu ,
Niliwaza kwenda kuchukua Hilo sanduku, lakini kwanza niliona nifanye mpango wa kuwasiliana nae,
Nilikwenda benki na kutoa zile pesa mpaka zikaisha zote ,
Nilichukua ndoo Kisha nikaweka Michele, halafu nikaziweka zile pesa Kisha nikaweka mchele mwingine juu yake na kupanga ndio nyingine ya mchele juu yake,
Baada ya siku chache ndio nikapata taarifa kuwa Allan amekamatwa manzese ,
Niliumia Sana, muda ule ule nikatafuta usafiri kwenda Dar,
Niliwaza haraka endapo kutakuwa na taratibu zozote za kisheria n.k,
Nilifika dar saa 11 na nusu jioni,
Haraka niliuliza mpaka nikafika magomeni hata hivyo kulikua na watu wengi nikashindwa kabisa kumuona...
Nilikaa pale nje na watu wengine tukiendelea kupiga stori,
Na kila Mara Polisi aliyetoka tulijaribu kusogea lakini hakukua na uwezekano wa kumuona,
Ilipofika saa mbili nikaona nifanye namna, nilimfuata Polisi mmoja na kumvuta pembeni ...
"Afande huyo jamaa Ni Broo wangu naomba Sana kujua kinachoendelea"
"Utaratibu utatorewa wewe kaenderee kusubiri"
Yule Afande alisema akinisukuma hivi..
Niliamua kurudi pale na kuendelea kukaa Mara ghafla tukasikia ambulance na tukatawanywa na polisi,
Ambulance ilipaki baada ya dakika kadhaa nilimuona Allan akiwa chini ya ulinzi mkali akaingia kwenye Ile ambulance na Gari za polisi zikaongoza
Nilitoka mbio na kujaribu kutafuta piki piki Ila sikupata kwa haraka
Wazo la haraka likanijia nikarudi kule ndani..