Hadithi: Madam President

Hadithi: Madam President

MADAM PRESIDENT 18

Wa kwanza kuvua barakoa yake sikumfahamu , alivua Kisha akanipa mkono au tano Kisha akapanda na kuelekea kwenye boti,

Mwingine alivua barakoa yake nilitaka kupiga kelele, alikua Ni Shemeji yangu aliyemuoa dada Yangu Tatu,


Kila siku nilijua Shemeji yangu huyu alikua mfanyabiashara wa spea za magari na alisafiri Sana nje ya nchi, na ilikua Ni aghalabu kumpata, alikuja akanikumbatia huku akinipiga piga mgongoni nae akaingia kwenye boti,

Mwingine huyu nilimtambua hata kabla hajavua barakoa vizuri...


"Josee!"

"Woza wozaaa" alijibu nae akinikumbatia huku akirusha Ile barakoa baharini,


Sasa alibakia mtu mmoja ambaye alisogea pole pole na huyu Ni Yule ambaye alikua karibu na Mimi Tangu kule juu,...

Pole pole aliivua barakoa yake

Naam hakuwa amebadilika Sana isipokuwa mwili wake ulikua umejaa zaidi labda kutokana na mazoezi..


Nilipigwa na butwaa...


"Jacob...Brooo!?"

Nilijikuta nikitamka huku tukikumbatiana kwa dakika nyingi...


Nilishindwa kuongea chochote tukaingia kwenye boti na kutokea kwenye vyumba vingi..


"Haya jamani tukutane baada ya dakika ishirini!"

Jacob alisema huku kila mmoja akichukua ufunguo wa chumba chake,

Ilikua Ni boti nzuri ya kisasa,

Nilichukua ufunguo wangu na kutafuta jina lililokua limeandikwa kwenye ufunguo Kisha nikafungua ndani,


"Waoooh"

Nilijikuta nafurahia kuona chumba kizuri kitanda kikubwa pamoja na nguo kadhaa za kubadili,

Niliingia bafuni na kufanya usafi wa mwili Kisha nikavaa nguo nilizokuta pale Kisha nikatoka kurudi sebuleni,
Tayari nilikuta meza imechafuka kwa vinywaji na vyakula vya kila Aina,

"Cheers for Allan!!!!"

Shemeji Isack alisema Kisha watu wakaanza kuburudika huku boti ikiendelea kukata mawimbi,

Baada ya chakula Sasa utambulisho ukaanza,


Alianza kutambulisha Ni Shemeji Isack , akamtambulisha Yule kijana mwingine kuwa anaitwa Steve,


"Wengine watajitambulisha wenyewe" alisema Shemeji akicheka


"Mimi Naitwa Bwana Jose"

Jose alisema,...


"Mimi Ni Bwana Jacob, "

Walisema Kisha wakacheka

Sikuelewa nianze mazungumzo na Nani lakini Ni Kama wote walikua wanasoma hisia zangu...


Jacob akaanza kufunguka..

"Kama ujuavyo nilitoka Arusha kiuhalisia nilikua kwenye kazi maalum Jeshini,


Sasa siku moja nikiwa Dar nilikuona umekuja kwa Madam, wakati unarudi Kuna mtu alitumwa kukuua nadhani ulimuona ulipanda nae mpaka mlandizi,

Mimi nikabadili misheni kuwa usiuwawe utekwe,

Na siku Ile umetekwa kwenye Ile nyumba kule porini ilitakiwa wakuue usiku ule ule Sasa Tena nikabadili misheni, kuwa uuliwe kesho jioni,

Sasa nikiwa kule porini kuna boya mmoja alifanikiwa kufungua ofisini kwangu na kuiba picha ambayo tulikua tumepiga Mimi na wewe akampelekea madam,


Madam akaagiza niuliwe haraka Sana,


Sasa alishachelewa maana wakati wanatumwa kuja kunimaliza nikawamaliza wao halafu nikapotea...
Ah mengine tutaongea bhana siwezi kusimulia Hadithi mimi "

Jacob alisema,.
Ndio ilikuwa kawaida yake Mambo magumu yeye aliongea kawaida tu ...

Nilibaki kupigwa na butwaa ,

"Haya Sasa mlikutana vipi na Jose?"

Nilimuuliza Jacob,

"Ah Jose Hebu mueleweshe jamaa ako"

Jacob alisema akimtupia mpira Jose,

"Dah kiukweli huyu jamaa Ni jini,

Maana wakati napanga kumtafuta ili tukachukue lile box yeye ndio alinitafuta Mimi, nilikua natoka Kigamboni siku Ile, ili niende Mlandizi wakati Niko nashuka kwenye Pantoni nikasikia mtu ananiita Joseee,

Basi kugeuka nikamuona huyu jamaa Mimi nilikua simjui kwahyo nikadhani Ni mojawapo ya watu ambao nilikua napakia mizigo yao labda Mara kwa Mara maana si unajua sisi madereva tunajulikana, Basi nikamsogelea akaniambia Kuna dili tukaongee,.


Tuliingia kwenye Gari ndio nikawakuta jamaa wengine Hawa tukaenda mpaka kwenye Jengo moja hivi na sasa jamaa akasema Yeye anaitwa Jacob, rafiki yake Allan!"

Nilishangaa Sana na akaniambia alikuwepo mahakamani na Mambo mengine mengi,

Cha kwanza jamaa walitaka kuhakikisha Kama naweza kweli kuendesha Gari, ama naweza kusogeza Gari!

Nilipewa ufunguo na nikatakiwa kuzunguusha Gari pale ndani kwenye ule uzio wa Ile nyumba kwa dakika mbili!

Niliingia kwenye Gari na nikafanya vitu vyangu ndani ya dakika mbili nikatoka Jacob akasema bado kidogo ingawa kutokana na kazi yenyewe ningeweza kufaa kwenye mzunguuko wa pili ndipo Sasa nikapewa ile nafasi ya kuendesha kutoka Banana mpaka pale tulipoingia,

Tulifanya mazoezi kwa siku mbili mfulululizo na Mimi kazi yangu nilitakiwa kuendesha Gari!


Jacob alikua na watu wake tayari ambao walishampa taarifa kuhusu hukumu ya kesi itakayokuwa na hivyo ndio wakaandaliwa watu kuvamia msafara"

Inatosha Sasa"

Jose nae alimalizia,


Kidogo nilianza kupata picha na nilijikuta nakosa maneno ya kusema kwa watu kujitolea nafsi zao kwa ajili yangu,


Sasa nilimgeukia Shem

"Sasa Shem imekuwaje haya yote na Sasa tunaelekea wapi?"

Nilisema,.

Shemeji yangu huyu ilikua Ni zaidi ya mwaka Sasa hatukuonana kila nilipokuwa nikifika kwa dada sikumkuta..

Hata hivyo alikuwa mtu mpole ambaye sikutegemea hata angeweza kushika bunduki,


Hivyo nilitegemea hadithi ya kustaajabisha kabisa kutoka kwake
 
MADAM PRESIDENT 19

Shemeji Sasa Kama haya Mambo yanakushangaza je hayo utakayoyakuta huko tuendako?"

Alianza Shemeji Kisha akaanza story Yake,

"Kipindi kile mama anaumwa ujue alinikabidhi wewe niwe na kuangalia,

Kiuhalisia Shemeji mimi Ni mfanyabiashara wa spea za magari lakini pia Mimi Ni mwanachama mkubwa wa chama Cha Uzalendo, na kimsingi hatukubaliani kabisa na nchi kuongozwa na mwanamke mpumbavu Kama Janet, kwahyo tunaelekea kufanya Jambo fulani hivi Sasa dada yako juzi ananipigia Simu analia Lia tu ananiambia eti Raisi anataka kukuua ndio nikafanya nililichofanya utaona mengi tukifika huko tuendako aisee Shemeji"

Alisema huku akiachia kicheko kikali,

Niliamua kukaa kimya tu na kusubiri huko tuendako...


*************


Baada ya Kama masaa sita hivi tuliwasili katika kisiwa sikuwahi kufika pale,

Tulishuka na kutoka nje kabisa na kukuta Gari moja likiwa tayari linasubiri tuliingia na baada na baada ya dakika kadhaa tulitokea kwenye Jengo moja kubwa ambalo lilikua na

Maandishi makubwa

"I3 security Company"


Pembeni yake kulikua na nyumba kubwa nzuri tuliongozana na kuingia...

Nilipigwa na butwaa kumuona mke wangu Mary na mtoto wangu Fred, wakiwa pale ..

Walinikimbilia kwa Furaha,.

Ni kweli haya yalikua Mambo ya kustaajabisha Sana kwangu,

Nilikua nimeshakaa wakati Shemeji aliposema bado Kuna mtu mwingine wa kumuona...

"Bila shaka atakuwa Shem Aida"

Niliwaza ,

Hata hivyo baada ya mtu huyo kusogea mbele yangu nilipigwa na butwaa ,...

"Haiwezekani huyu jamaa ndio alisema Mimi nimeiba!"

Nilisema Sasa nikitoa macho kwa Bwana Shija, mkurugenzi mtendaji ambaye alikua Ni Bosi wangu,


"Relax Bwana Shemeji!"


Alisema Shemeji Isack,.

"Broo Mambo hayapo unavyodhani,

Mimi na Isack Ni marafiki Sana,

Alisema Bwana Shija


"Sikiliza Shem, Mambo yote namna kesi ilivyokuwa unaenda huu ndio alikua ananipa ripoti lakini huyu ndio amesaidia Familia yako kufika hapa!"


"Lakini Bwana Shija kwanini ukasema Mimi nimeiba pesa?"


"Sikiliza bhana Lile Ni agizo la Raisi , tunafanya kwanza agizo Ila Sasa dawa iko jikoni"

Alisema Bwana Shija akirudi zake,

"We kaa hapa kwanza na mke wako kwa siku hizi tatu Kisha nitakufuata hapa kesho kutwa tuanze kazi Rasmi "


Usiwaze kuhusu kule Tanzania kila kitu kitakuwa sawa ..



Aida yupo kule,"

Alimalizia Shemeji Kisha nikabaki na mke wangu Mary...


Sikujua pa kuanzia niliona aibu Sana,


Nilishindwa kuongea...


"Najua unachowaza, unafikiria kuniambia kuhusu kutembea na Raisi?"

Alianza Mary,


"Mke wangu....."

Alinikatisha kwa kuniwekea kidole mdomoni,


"No uliyopitia yanatosha Darling usiongee kitu"


Alisema huku akinikumbatia

Tulijisahau kuwa Fred alikuwa anatuangalia...

Ikabidi tuhamie chumbani...


******************************************


Tulikaa katika mji wa Comoro kwa wiki mbili, huku taarifa nchini Tanzania zikizidi kupamba Moto,

Tayari vikundi mbali mbali vya watu na vyama pamoja na wanaharakati walikua wakishinikiza Raisi Janet ajiuzulu,


Shemeji yangu alikua akimiliki kampuni kubwa ya ulinzi ambayo ndani yake kulikua na watu wengi wenye uzoefu katika medani za mapigano na Vita,


Mke wangu alipata kazi katika hospitali ya Shirika moja la Dini pale Comoro,


Jose alikuwa dereva Binafsi wa Mkurugenzi mtendani wa I3 security Company,

Nilianza kufurahia Maisha ya Comoro,

Shem alinipatia kazi ya duty roster manager ambapo kazi yangu ilikua Ni kupanga ratiba na kugawa walinzi kwenye vituo kutokana na Oda mbali mbali tulizokuwa tukipata,

Siku hiyo nilikua nimekaa ofisini baada ya kumaliza kupanga ratiba yangu nilijaribu kuingia kwenye mtandao nilikuta mahojiano ya Raisi wa Tanzania na Kituo kimoja Cha Television,

Katika mazungumzo hayo Raisi Janet alikua akijibu tuhuma za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mimi wakati nikiwa nasoma,


"Unajua uongo ukisemwa Sana bila kukanushwa unakua ukweli, huyo Allan ambaye tunamtafuta kila Kona alikua Ni rafiki ya Mume wangu huyu wa Sasa aliyenioa, kwahyo Kama ujuavyo ukiwa unasoma lazima kuficha baadhi ya Mambo kwahiyo sasa alitumia mgongo huo kupata Kiki,
Tena alikua akitaka hata asichukuliwe hatua za kisheria pindi alipoiba pesa!".

Janet alikuwa akisema ,..
Baadae alikuwa anahojiwa huyo mumewe Janet

"Yeah Allan alikuwa Rafiki yangu , nilimpokea wakati anakuja pale mombo sekondari Mimi nilikua kidato Cha sita , kwahiyo wakati Janet alipokua anakuja kunitembelea nilikua namtuma Allan kwenda kumpokea ili watu wasijue, hizi Ni baadhi ya picha nikiwa na Allan"

Alisema huku akitoa picha ambazo zilikua zinaonyesha tukiwa nae tumekaa maeneo mbali mbali, na nyingine alikua amekaa na Janet Kitandan ws Mimi nikiwa nimesimama

"Hahaha huyu mjinga anajiona ana akili Sana"

Nilisema nikivuta picha jinsi alivyokuwa anadanganya watu,


Nilijaribu kuwasiliana na jamaa zangu ambao tulikua tumesoma wote mombo,


Nilifanikiwa kumpata Dani,..


"Hali Ni mbaya Kaka, ikijulikana tu umesoma mombo unapotea, na wengine wameokotwa wamefariki!

Hali inatisha Kaka, wote wale tuliomaliza mwaka ule Hali Yetu Ni mbaya!

Aliongea Dani kwa uchungu

"Ina maana Janet ndio anafanya hivyo?"

Niliuliza

"Yaani wengine wanalazimishwa kusema eti wanamjua baba Janet jamaa ujinga mtupu"

Alimalizia Dani huku akikata Simu..

Kumbe Janet anataka kuaminisha watanzania kuwa Mimi Ni muongo?

Niliwaza
 
MADAM PRESIDENT 20

Nilijaribu kuwasiliana na marafiki zangu Tanzania Ni kweli karibia wenzangu wote tuliomaliza wote Mombo, walikua wakipotea katika mazingira ya kutatanisha,

"I must stop this shit"

Nilisema huku nikipekua pekua pale mtandaoni na kuchukua namba za simu za kile Kituo Cha Runinga,


"Hallo naitwa Allan"

Nilisema baada ya simu kupokelewa,

"Ndio Allan, unapiga Simu kutoka wapi na una Shida gani "

Aliuliza mtu wa upande wa pili,

"Naomba kuongea na Mwandishi au mtangazaji wa kipindi Cha Dira"

Nilisema,

"Unaweza kusema Shida yako tafadhali kabla sijakuunganisha nae?"


"Mimi Ni Allan, ambaye Raisi Janet anamtafuta!"
Nilisema Sasa kwa utulivu..

"Ooh, ooh, unaongea ukiwa wapi?,
Tafadhali?"

Aliuliza,

"Wewe mpe mhusika Simu"
Nilisema

"Tafadhali subiri kidogo, baada ya dakika kadhaa"


Nilisubiri baada ya dakika tatu hivi nilisikia Sauti nyingine ya mwanamke

"Hallo Allan Naitwa Jemima mwandishi na mwandaaji wa kipindi Cha Dira"

"Okay Naitwa Allan Nataka tufanye mahojiano kuhusu kile alichoongea Rais Janet"

"Tafadhali uko wapi tukufuate?"

Aliuliza.

"Chukua email yangu allankv@yahoo.com
Tuwasiliane Binafsi sehemu ya kukutana tafadhali iwe Siri"

Nilisema .
Alikubali Kisha nikakata Simu ..

Baada ya Nusu saa alinitumia email, na tukaanza kuchati,

Bado sikuwa najua namna ya kuweza kufanya mahojiano hayo,


Lakini niliamua kuwasiliana na Shemeji ambae alishauri tufanye mahojiano pale pale nchini Comoro,



Hivyo tulimwambia Jemima aje vifaa atakutana navyo,


***************

Jemima aliwasili nchini Comoro baada ya wiki moja,

Tayari tulishaandaa chumba Cha mahojiano kikiwa na vifaa vyote na mahojiano hayo yalikadiriwa kutazamwa na maelfu ya watu nchini Tanzania,

"Hello karibuni katika kipindi chetu Cha kila wiki Cha Dira, Kama tulivyokwisha kusema Tangu awali Leo hii tupo na Bwana Allan, ambaye miezi kadhaa nyuma kulikua na Hali ya tafrani akihusishwa na Mambo ya uhalifu, lakini kubwa Ni kutoa utata wa kile ambacho kinaendelea Kati yake na Mheshimiwa Raisi Janet,"

Sasa karibu katika kipindi chetu


Kipindi kilianza ambapo nilianza kuelezea historia yote huku nikitoa vielelezo vyote muhimu ikiwemo barua na picha kadhaa kuhusu uhusiano wetu na Janet , mwisho kabisa nilizungumza kuhusu kesi na namna ilivyotengenezwa ,

Kisha nikamalizia na watu tuliosoma nao kupotezwa, ili kuficha ukweli


Nilimalizia maelezo yote hayo na kujibu maswali yote ya Jemima.


****************

Sasa nchini Tanzania hisia ziliibuka kwa upya na maandamano ya wanaharakati kutaka sakata Lile lichunguzwe ikiwemo la watu kupotea...


Ni kutokana na vurumai hizo

Shemeji alihamisha familia yake kabisa Nchini Comoro,


Hata hivyo nilitamani kabisa kurudi Tena nchini Tanzania kuendelea na kazi yangu ya ualimu niliyoipenda sana.

****************

Ilikua majira ya saa 12 jioni nilikua nimetoka kwenye supamaketi moja hivi kumnunulia mwanangu Fred zawadi fulani aliyoniagiza,


Wakati nataka kufungua mlango wa Gari nilihisi Kama haujafungwa vizuri...


"Hivi sikufunga mlango wa Gari vizuri au?"

Niliwaza huku nikitoa ufunguo na kufungua mlango na kuingia ndani

Nilivaa mkanda Kisha nikaweka ufunguo na kuwasha Gari....


Nilishtuka kuona watu wawili wakiibuka kutoka kwenye siti ya nyuma ya Gari na kunionyeshea bastola .


Kwa kawaida Comoro hakukua na kesi nyingi za ujambazi wa kutumia silaha ingawa Mara chache Sana kulikua na wizi wa Magari na utekaji wa watu kwa ajili ya pesa...

"Nyie Ni wakina Nani?"

Niliuliza Sasa nikisita sita.


"Sikiliza bastola hii Ina kiwambo Cha kuzuia sauti kwahiyo usijaribu kufanya ujanja wowote "

Mmoja wapo alisema huku akihamia siti ya mbele ..


Endesha Gari kuelekea kushoto mpaka hapo karibu na Midlands tower

Haya twende"


Aliamuru,

Sasa moja kwa moja nilijua hawa watu walitoka Tanzania maana waliongea Kiswahili fasaha kabisa..


Niliondoa Gari na kufanya Kama walivyosema huku nikitafuta namna ya kujiokoa

Niliendesha Gari huku nikiwaza namna ya kujiokoa kwani tayari kengele ya hatari ilishalia kichwani mwangu,

Yule jamaa pale mbele alikuwa akiniangalia kila Tendo nalofanya huku bastola yake ikiwa wazi mkononi,


Nilifika karibu na Midlands tower,

Wakaniamuru kusimamisha Gari,

Nilitafuta sehemu nzuri ya kupaki huku nikiendelea kusubiri maelezo yao,

"Kuna Gari itakuja hapo mbele baada ya dakika kadhaa piga honi Mara mbili, "

Alisema Yule jamaa pale mbele,

Ni kweli baada ya dakika kadhaa ilikuja Gari ndogo iliyokua na vioo vyeusi nilipiga honi Mara mbili Kisha nikatulia,


Lile Gari lilisogea kabisa mpaka pale tulipo Kisha mlango ukafunguliwa


"Shuka twende na kuingia kwenye hiyo Gari hapo weka vitu vyako vyote kwenye Gari lako"

Walisema ,

Nilitoa saa na waleti, na simu Kisha nikaweka kwenye Gari langu na kutoka nje,

Nilitembea pole pole huku nikitazama Gari langu,

Sasa wale jamaa tulitembea huku wakiwa wameficha bastola zao na ilikua Ni Kama watu walio katika safari zao tu,

Tuliingia kwenye Gari ambalo nilikuta watu wengine wawili nao wakiwa na bastola zao huku wameziba nyuso zao,

Haraka safari iliianza pole pole tukitoka nje ya mji,

Tulitembea dakika chache na Sasa tukawa tunaelekea ilipo bandari,


Hadi hapo nilijua ninarudishwa Tanzania,


Maana njia pekee ya haraka ilikua Ni kupitia Majini kuliko usafiri wa ndege ambao ungekuwa na mlolongo mrefu,

Ni wakati tunakaribia kabisa kufika bandarini kwa ghafla yalitokea magari mawili ambayo niliyatambua wazi wazi kutokana na nembo yao I3 security Company,

Nilijawa na furaha na kupata nguvu,


Gari moja lilikua nyuma Yetu na lingine lilienda kupaki mbele Yetu na kutuweka katikati,


"Ooh shit"

Dereva alitoa matusi Sasa akijaribu kufunga breki ,


Wenzake walijiweka sawa kwa kushika bunduki zao hata hivyo kufumba na kufumbua tayari Gari ilikua imezunguukwa na watu wenye silaha zaidi ya 10,


Wale jamaa walikubali kujisalimisha na Mimi nikatoka huku nikienda kumsalimia Jacob ambaye alikua ameongozana na Ile Timu,


"Aisee mmejuaje?"


Nilipigwa na butwaa

"Anajua Boss , turudini chap kabla wanoko hawajajaa hapa"

Jacob alisema huku wale jamaa wakifungwa pingu na tukarudi nao ofisini,.

Nilifika moja kwa moja ofisini kwa Mkurugenzi ambaye hakuonyesha kushtuka kuniona alinipa pole huku aliwahi haraka kwenda kuwaona hao wahuni walioniteka,

"Shem hebu kidogo niambie umejuaje nimetekwa?"
 
MADAM PRESIDENT 21

"Shemeji ungesoma mkataba wako wa ajira Wala usingeuliza Hilo swali la tumejuaje umetekwa hebu kwanza tuwashughulikie hawa wahuni wanaodhani hapa Tanzania"

Shemeji aliongea Sasa akishuka ngazi kwa Kasi kuelekea chini,.

Tulifika na kuwakuta wale jamaa wakiwa wanapewa kipondo kikali huku wakiwa wamefungwa minyororo ukutani...

Baada ya sisi kuingia walinzi walisitisha kipigo na kusogoea pembeni

"Sihitaji kuongea vitu vingi Sana Nina kazi zinasubiri


Nataka kujua Nani aliyewatuma,"

Shemeji aliongea akiwaangalia mmoja mmoja lakini hakuna aliyethubutu kufungua mdomo,


"Nani Kiongozi wenu hapa? Nani Team leader?" Shemeji aliuliza Tena lakini hakuna aliyejibu,


"Okay Basi vizuri nashukuru kwa kuwa mnataka zoezi liende haraka,"

Alisema huku akifungua bastola yake na kuweka risasi kadhaa, alianza kwa mmoja kumuuliza maswali Yale Yale alivyokaa kimya akamtandika risasi ya kichwa huku nikishuhudia....


Ilikua Ni Mara yangu ya kwanza kuona mtu akiuwawa kikatili vile,


Aliendelea kwa mwingine ambaye alianza kutetemeka na kusema kiongozi wao Ni Jack"

"Okay Jack Yuko wapi?"

Aliuliza Shemeji na mmojawapo alitingisha kichwa,

"Bwana Jack sisi Ni watu wazuri tu, Jambo hili Ni rahisi Sana,

Nipe kode ya mawasiliano na bosi wenu ili tuongee nae namna ya kuwasamehe"


Shemeji aliongea kwa upole..


Jack hakuwa na namna ambapo alitaja namba za simu na maneno fulani hivi ya kutumia ..


Simu ililetwa na ikapigwa shemu akataja zile kode Kisha baada ya muda mfupi

Ikasikika sauti ya mwanamke Simu ikazoegwa karibu na Jack,.

"Madam Jack alisema kwa tabu kidogo"...


"Jack mko wapi ndege inawasubiri hakuna dalili za nyie kuonekana?"


Ilisikika wazi sauti ya Janet huku kukiwa na Kama upepo hivi bila shaka alikua sehemu ya wazi Sana,

Shemeji alichukua Ile simu,..

Na kuniambia niongee na Janet kumpa Mashart ya kuwapata watu wake,


"Sikiliza mpenzi wangu wa zamani Janet , Mimi Ni Allan,

Unajua nilidhani utatuma watu wenye uwezo kidogo Sasa sikiliza Janet, najua wazi huyu Ni Jack mtoto wa mama yako mkubwa Adela, huwezi kumuacha akafia huku...

Kila mmoja alishangaa pale kwenye chumba hata Bwana Shemeji macho yalimtoka,

Janet alianza kuhema kwa wasi wasi,

"Wewe mwanaharamu sema unataka Nini?"

Janet aliuliza kwa wasi wasi,..


"Okay Sasa kwa Sasa nilitaka kukuambia tu kuwa kwa Sasa akina Jack wapo sehemu salama, Sasa tunachotaka tutakuambia baada ya masaa mawili jipange mama,

Maana naweza kukutaka wewe uje Comoro nipige mzigo!".

Nilisema Kisha nikakata Simu,

Kila mmoja ndani ya chumba aliangua kicheko,

Bwana Shemeji aliagiza kutolewa Ile maiti Kisha akaamuuru wakina jack wafunguliwe..

Wawekwe sehemu nzuri Ila ulinzi mkali,

Kisha tukatoka kwenda kujadiliana

"Haya umemjuaje huyo Jack?"

Shemeji nae aliuliza,.


"Ah Shemeji ulitakiwa usome tu kwenye faili langu, ungejua Jack Ni Nani?"

Na Mimi niliamua kulipiza kisasi baada ya yeye kukataa kuniambia alijuaje kuwa nimetekwa,.

Sasa tuliingia kwenye chumba Mimi na Jacob na Bwana Shemeji ili kutengeneza masharti

Tulimaliza kujadiliana Kisha tukakubalina kuonana baada ya Saa moja,


Nilitoka haraka na kuangalia huko na huko Kisha nikapanda Gari Sasa kuelekea nyumbani,


Ulikua Ni Mwendo wa dakika 10 tu kwa Gari hivyo niliendesha taratibu huku nikifungulia redio kwa sauti,


Kwa mbali kulikua na Gari ambayo Ni Kama ilikua inanifuata,

Nilijifanya kuongeza Mwendo nayo ikaongeza,

Nilijaribu kupunguza nayo ikapunguza,

Sasa nilipata uhakika Ni kweli inanifuata niliendelea kwenda Mpaka getini kwangu nikapiga honi niliingiza Gari Kisha nikatoka haraka nje ya Gari na kutoka nje kuchungulia ,


Iile Gari lilikuwa limepaki kwa mbali kidogo Ni Kama watu waliokuwa Kama wanahakikisha nimefika au kuangalia mahali ninapoishi,


Nilirudi ndani na kupata chakula ,

Sikumwambia chochote mke wangu,

Nilimwambia kulikua na kikao Tena saa 2 na nusu usiku ,

Nilingiia kwenye Gari ili kurudi ofisini nilichukua bastola na kuichimbia kwenye koti,

Zaidi ya kuishia kufanya mazoezi kila siku ya kulenga shabaha sikuwahi kumpiga mtu risasi hata ya mguu..


Leo hii niliingiwa na wasi wasi,

Nilitoka na kuingia kwenye Gari Kisha nikatoa taarifa Kama ilivyokuwa kawaida,

Kwa wafanyakazi wote wa I3 security Company,

Ilikua Ni lazima kutoa taarifa yoyote endapo mtu angetoka baada ya Saa 1 usiku,

Niliendesha Gari na kuona Lile Gari likiwa pale pale,

Nililipita na baada ya muda mfupi nalo likaanza safari kunifuatilia...


"Eneugh is eneugh"

Nilijisemea nikiweka bastola yangu sawa Kisha nikaendesha Gari huku nikiangalia nyuma kupitia kioo,

Karibu na kufika ofisini nilifunga breki haraka huku nikitoka kwa haraka bastola ikiwa mkononi,


Ile Gari nayo ilifunga breki na tayari nilishafika,

Nilipiga piga kioo Cha mlango kumuamuru atoke nje,


Alitoka nje huku akiwa haonyeshi kustuka,

Sikuwa namfahamu ingawa sura yake pia haikua ngeni Sana,

"Why are you following me?"
Nilimuuliza huku nikimkwida shati lake,

"Sorry boss, sorry boss!"

Alisema ..


Nilimbananisha huku nikimuwekea bastola kichwani...


"Nakuua dogo, !"

Nilisema sasa nikimchimba mkwara,....


" I'm your body guard sir!"

Alisema

"What?"


Nilisema Sasa nikimuachia,

"Usije kumwambia CEO , samahani Sana nilianza kazi Leo tu, sikuwa nafahamu kwako!"


"Toka zako!"

Nilisema nikimsukuma huko,

Nilifika ofisini kwangu haraka nikatoa faili la mkataba wa kazi,

Nilisoma kipengele Cha ulinzi kwa mwajiriwa ambacho sikuwahi kukisoma...

"Meneja, meneja msaidizi, mkurugenzi na wakuu wengine wa idara watakuwa na walinzi Binafsi ambao hawatatakiwa kuwajua !"

Mkataba ulisomeka hivyo,


"Ooh shit kwahiyo kumbe nilikua na mlinzi ndio maana alitoa taarifa za Mimi kutekwa,

Sasa huyu mgeni Ni kwamba yule amefukuzwa kazi au?"

Dah shemu nae!


Niliwaza huku nilitabasamu na kutoka kwenda kwenye kile chumba Cha kutuma Yale masharti yetu Kwa Janet
 
Back
Top Bottom