MADAM PRESIDENT 20
Nilijaribu kuwasiliana na marafiki zangu Tanzania Ni kweli karibia wenzangu wote tuliomaliza wote Mombo, walikua wakipotea katika mazingira ya kutatanisha,
"I must stop this shit"
Nilisema huku nikipekua pekua pale mtandaoni na kuchukua namba za simu za kile Kituo Cha Runinga,
"Hallo naitwa Allan"
Nilisema baada ya simu kupokelewa,
"Ndio Allan, unapiga Simu kutoka wapi na una Shida gani "
Aliuliza mtu wa upande wa pili,
"Naomba kuongea na Mwandishi au mtangazaji wa kipindi Cha Dira"
Nilisema,
"Unaweza kusema Shida yako tafadhali kabla sijakuunganisha nae?"
"Mimi Ni Allan, ambaye Raisi Janet anamtafuta!"
Nilisema Sasa kwa utulivu..
"Ooh, ooh, unaongea ukiwa wapi?,
Tafadhali?"
Aliuliza,
"Wewe mpe mhusika Simu"
Nilisema
"Tafadhali subiri kidogo, baada ya dakika kadhaa"
Nilisubiri baada ya dakika tatu hivi nilisikia Sauti nyingine ya mwanamke
"Hallo Allan Naitwa Jemima mwandishi na mwandaaji wa kipindi Cha Dira"
"Okay Naitwa Allan Nataka tufanye mahojiano kuhusu kile alichoongea Rais Janet"
"Tafadhali uko wapi tukufuate?"
Aliuliza.
"Chukua email yangu
allankv@yahoo.com
Tuwasiliane Binafsi sehemu ya kukutana tafadhali iwe Siri"
Nilisema .
Alikubali Kisha nikakata Simu ..
Baada ya Nusu saa alinitumia email, na tukaanza kuchati,
Bado sikuwa najua namna ya kuweza kufanya mahojiano hayo,
Lakini niliamua kuwasiliana na Shemeji ambae alishauri tufanye mahojiano pale pale nchini Comoro,
Hivyo tulimwambia Jemima aje vifaa atakutana navyo,
***************
Jemima aliwasili nchini Comoro baada ya wiki moja,
Tayari tulishaandaa chumba Cha mahojiano kikiwa na vifaa vyote na mahojiano hayo yalikadiriwa kutazamwa na maelfu ya watu nchini Tanzania,
"Hello karibuni katika kipindi chetu Cha kila wiki Cha Dira, Kama tulivyokwisha kusema Tangu awali Leo hii tupo na Bwana Allan, ambaye miezi kadhaa nyuma kulikua na Hali ya tafrani akihusishwa na Mambo ya uhalifu, lakini kubwa Ni kutoa utata wa kile ambacho kinaendelea Kati yake na Mheshimiwa Raisi Janet,"
Sasa karibu katika kipindi chetu
Kipindi kilianza ambapo nilianza kuelezea historia yote huku nikitoa vielelezo vyote muhimu ikiwemo barua na picha kadhaa kuhusu uhusiano wetu na Janet , mwisho kabisa nilizungumza kuhusu kesi na namna ilivyotengenezwa ,
Kisha nikamalizia na watu tuliosoma nao kupotezwa, ili kuficha ukweli
Nilimalizia maelezo yote hayo na kujibu maswali yote ya Jemima.
****************
Sasa nchini Tanzania hisia ziliibuka kwa upya na maandamano ya wanaharakati kutaka sakata Lile lichunguzwe ikiwemo la watu kupotea...
Ni kutokana na vurumai hizo
Shemeji alihamisha familia yake kabisa Nchini Comoro,
Hata hivyo nilitamani kabisa kurudi Tena nchini Tanzania kuendelea na kazi yangu ya ualimu niliyoipenda sana.
****************
Ilikua majira ya saa 12 jioni nilikua nimetoka kwenye supamaketi moja hivi kumnunulia mwanangu Fred zawadi fulani aliyoniagiza,
Wakati nataka kufungua mlango wa Gari nilihisi Kama haujafungwa vizuri...
"Hivi sikufunga mlango wa Gari vizuri au?"
Niliwaza huku nikitoa ufunguo na kufungua mlango na kuingia ndani
Nilivaa mkanda Kisha nikaweka ufunguo na kuwasha Gari....
Nilishtuka kuona watu wawili wakiibuka kutoka kwenye siti ya nyuma ya Gari na kunionyeshea bastola .
Kwa kawaida Comoro hakukua na kesi nyingi za ujambazi wa kutumia silaha ingawa Mara chache Sana kulikua na wizi wa Magari na utekaji wa watu kwa ajili ya pesa...
"Nyie Ni wakina Nani?"
Niliuliza Sasa nikisita sita.
"Sikiliza bastola hii Ina kiwambo Cha kuzuia sauti kwahiyo usijaribu kufanya ujanja wowote "
Mmoja wapo alisema huku akihamia siti ya mbele ..
Endesha Gari kuelekea kushoto mpaka hapo karibu na Midlands tower
Haya twende"
Aliamuru,
Sasa moja kwa moja nilijua hawa watu walitoka Tanzania maana waliongea Kiswahili fasaha kabisa..
Niliondoa Gari na kufanya Kama walivyosema huku nikitafuta namna ya kujiokoa
Niliendesha Gari huku nikiwaza namna ya kujiokoa kwani tayari kengele ya hatari ilishalia kichwani mwangu,
Yule jamaa pale mbele alikuwa akiniangalia kila Tendo nalofanya huku bastola yake ikiwa wazi mkononi,
Nilifika karibu na Midlands tower,
Wakaniamuru kusimamisha Gari,
Nilitafuta sehemu nzuri ya kupaki huku nikiendelea kusubiri maelezo yao,
"Kuna Gari itakuja hapo mbele baada ya dakika kadhaa piga honi Mara mbili, "
Alisema Yule jamaa pale mbele,
Ni kweli baada ya dakika kadhaa ilikuja Gari ndogo iliyokua na vioo vyeusi nilipiga honi Mara mbili Kisha nikatulia,
Lile Gari lilisogea kabisa mpaka pale tulipo Kisha mlango ukafunguliwa
"Shuka twende na kuingia kwenye hiyo Gari hapo weka vitu vyako vyote kwenye Gari lako"
Walisema ,
Nilitoa saa na waleti, na simu Kisha nikaweka kwenye Gari langu na kutoka nje,
Nilitembea pole pole huku nikitazama Gari langu,
Sasa wale jamaa tulitembea huku wakiwa wameficha bastola zao na ilikua Ni Kama watu walio katika safari zao tu,
Tuliingia kwenye Gari ambalo nilikuta watu wengine wawili nao wakiwa na bastola zao huku wameziba nyuso zao,
Haraka safari iliianza pole pole tukitoka nje ya mji,
Tulitembea dakika chache na Sasa tukawa tunaelekea ilipo bandari,
Hadi hapo nilijua ninarudishwa Tanzania,
Maana njia pekee ya haraka ilikua Ni kupitia Majini kuliko usafiri wa ndege ambao ungekuwa na mlolongo mrefu,
Ni wakati tunakaribia kabisa kufika bandarini kwa ghafla yalitokea magari mawili ambayo niliyatambua wazi wazi kutokana na nembo yao I3 security Company,
Nilijawa na furaha na kupata nguvu,
Gari moja lilikua nyuma Yetu na lingine lilienda kupaki mbele Yetu na kutuweka katikati,
"Ooh shit"
Dereva alitoa matusi Sasa akijaribu kufunga breki ,
Wenzake walijiweka sawa kwa kushika bunduki zao hata hivyo kufumba na kufumbua tayari Gari ilikua imezunguukwa na watu wenye silaha zaidi ya 10,
Wale jamaa walikubali kujisalimisha na Mimi nikatoka huku nikienda kumsalimia Jacob ambaye alikua ameongozana na Ile Timu,
"Aisee mmejuaje?"
Nilipigwa na butwaa
"Anajua Boss , turudini chap kabla wanoko hawajajaa hapa"
Jacob alisema huku wale jamaa wakifungwa pingu na tukarudi nao ofisini,.
Nilifika moja kwa moja ofisini kwa Mkurugenzi ambaye hakuonyesha kushtuka kuniona alinipa pole huku aliwahi haraka kwenda kuwaona hao wahuni walioniteka,
"Shem hebu kidogo niambie umejuaje nimetekwa?"