MADAM PRESIDENT 22
Tulifika kwenye kile chumba Kisha tukawasiliana na Janet ambaye bila shaka alikua akisubiri Simu yetu kwa hamu,
"Madam, mpaka kesho saa 8 mchana tupate hapa million 800 keshi, hiyo Ni Kama faini kwa kutuma watu wajaribu kuja kutuvamia huku,
Jambo la pili,
Niifutie kesi inayonikabili nikirudi Tanzania nisiwe na kesi ya kujibu,
Jambo la mwisho tangaza hadharani kuwa serikali inahusika na vifo na kupotea kwa watu nane tuliosoma wote mombo sekondari,
Nadhani Ni hayo tu,
Kesho pesa zikifika tutaachia Hawa wawili, then ukitangaza Mambo hayo mengine Jack nae atafuata"
Nilisema,
Janet alishusha pumzi ndefu,
"Come on Allan unajua siwezi kufanya huo upuuzi wote! Unajua siwezi, yaani Mimi nitangaze hadharani kuwa serikali inaua watu!? Am I crazy?"
Janet alihoji,
"Sikiliza Janet, kwanza umenitengenezea kesi, lakini Kama haitoshi umelazimisha watu waongee uongo, mwisho wa siku umeua wengine, Kama bado hujaridhika umenitumia watu waniue, lakini kuonyesha wewe Ni katili Janet unamtuma mpaka ndugu yako wa Damu! Hivi wewe mwanamke Ni mtu gani wewe?"
Niliendelea kuongea huku Shemeji akirekodi Yale mazungumzo kupitia vifaa vyake pale mezani,
"Kesho utaletewa pesa waachie wote tafadhali,"
Janet alisema,
Sikumsikiliza nilikata Simu,
***************
Mambo yalikwenda Kama yalivyopangwa kesho yake tulikua baharini kwenye boti ndogo ambapo Janet alituma watu wake,
Tulikaa umbali wa mita kadhaa tulituma mtu wetu ambaye alienda kuchukua zile pesa tukazihesabu zilikua kamili,
Tuliziweka kwenye mfuko mwingine Kisha lile begi tukalitupa baharini,
Baadae tukawaachia wale jamaa wawili tukarudi zetu!
Tulibakia na mateka mmoja tu, Jack,
Usiku ule Janet hakuongea chochote, hivyo tulisubiri siku ya kesho endapo atahutubia taifa
Ni kweli kesho yake Janet alikuwa mubashara asubuhi saa 3 akihutubia taifa katika mkutano wa dharula,
Tulifuatilia tukiwa kwenye chumba maalum pale ofisini,
"Kwahiyo ndugu zangu Watanzania, nimewaita kuwapa taarifa muhimu,
Katika nafasi hii zipo changamoto nyingi nimekumbana nazo, nilijitahidi kutatua kwa kadri ya uwezo wangu,
Hata hivyo kutokana na Raisi Ni Kiongozi anayetakiwa kutawala na kuongoza kwa Haki yapo maeneo ambayo Kama Raisi, lakini Kama Binadamu sijatenda Haki, hivyo naomba Sana kukiri kuwa yapo mapungufu,
Nitataja maeneo machache,
Kwanza eneo la kukusanya mapato,
Nikiri wazi Kama serikali tunakiri kuzembea,.
Lakini eneo la pili Ni katika usimamizi wa miradi hapa napo Kama serikali tumekosea Sana,
Eneo la mwisho Ni eneo la utoaji Haki,
Eneo Hili naomba kukiri kuwa kumekuwa na lawama nyingi, na nyingine zikielekezwa kwangu moja kwa moja..
Mfano ipo kesi ya ndugu Allan,.
Nikiri wazi Kama serikali hatukupata muda wa kutosha kuchunguza kesi hii na kupelekea matatizo ambayo wengi mnayafahamu na sitaki kurudia,
Baada ya kutuma wapelelezi wangu kuchunguza vizuri tuliona ukiukwaji mkubwa wa Haki na Ndugu Allan alionewa,
Pamoja na kuwa ametoroka ama alitoroshwa lakini Raisi ninayo mamlaka kikatiba kumsamehe yoyote, na hivyo nimemfutia mashtaka yake,
Lakini tupo kwenye maongezi na serikali kule alikokimbilia Kama uhamishoni, Kama akiridhia Basi arudi nchini kwake na atimize majukumu yake ikiwemo kuitumikia nchi yake,
Nina amini wizara ya kazi watajaribu kuwasiliana hata na mkewe ambaye Ni daktari arudi kutumikia nchi yake,
Niwashukuru Sana wanahabari kwa kuitikia wito"
Alihitimisha Janet,
Tuliangaliana pale chumbani huku tukigonga mikono kwa Furaha,
Jioni muda ule ule tulienda kumtoa Jack na kumsindikiza Hadi bandarini ambapo alirudi Tanzania,
***************
Hata hivyo niliona niendelee kukaa Comoro kwa mwaka mmoja zaidi maana bado sikuwa na Imani na Janet,
Tuliona Ni vyema kusubiri wakati wa uchaguzi kwani miezi kadhaa ijayo ungefanyika uchaguzi Mkuu na Janet kuhitimisha miaka yake mitano,
Tulipanga kabisa Janet asigombee Tena Uraisi,
Tuliendelea kupanga Mipango kuhakikisha Mambo yanaiva,
***************
Zile pesa tuliamua kununua vifaa vya kampuni ikiwemo kuongeza magari na kuwalipa malipo mengine wote walioshiriki katika Lile zoezi la kuniokoa,
Maisha Comoro yalizidi kunoga na taratibu nikaanza kusahau mikiki mikiki yote ya Tanzania,
Siku moja nikiwa ofisini Shemeji alifika akiwa na gazeti la Tanzania mkononi alinirushia lile gazeti nilitupia macho haraka kidogo na kukuta habari ya kuhusu Bwana Shija,
Mkurugenzi mtendaji ambaye amehukumiwa kifungo Cha miaka 10 jela kwa sababu ya kupotosha ukweli kuhusu kesi Yangu,
"Ah Sasa inakuwaje Tena?"
Nilimuuliza Bwana Shem,
"Imegundulika Bwana Shija ndie alikua anatupa Siri lakini pia alikutorosha huku kwahiyo Sasa amegeuziwa kesi na hivi Sasa yupo Gerezani ameanza siku yake ya tatu, we must do something"
Bwana Isack alisema