Hadithi: Madam President

Hadithi: Madam President

MADAM PRESIDENT 22

Tulifika kwenye kile chumba Kisha tukawasiliana na Janet ambaye bila shaka alikua akisubiri Simu yetu kwa hamu,

"Madam, mpaka kesho saa 8 mchana tupate hapa million 800 keshi, hiyo Ni Kama faini kwa kutuma watu wajaribu kuja kutuvamia huku,

Jambo la pili,
Niifutie kesi inayonikabili nikirudi Tanzania nisiwe na kesi ya kujibu,

Jambo la mwisho tangaza hadharani kuwa serikali inahusika na vifo na kupotea kwa watu nane tuliosoma wote mombo sekondari,

Nadhani Ni hayo tu,

Kesho pesa zikifika tutaachia Hawa wawili, then ukitangaza Mambo hayo mengine Jack nae atafuata"


Nilisema,

Janet alishusha pumzi ndefu,


"Come on Allan unajua siwezi kufanya huo upuuzi wote! Unajua siwezi, yaani Mimi nitangaze hadharani kuwa serikali inaua watu!? Am I crazy?"


Janet alihoji,

"Sikiliza Janet, kwanza umenitengenezea kesi, lakini Kama haitoshi umelazimisha watu waongee uongo, mwisho wa siku umeua wengine, Kama bado hujaridhika umenitumia watu waniue, lakini kuonyesha wewe Ni katili Janet unamtuma mpaka ndugu yako wa Damu! Hivi wewe mwanamke Ni mtu gani wewe?"

Niliendelea kuongea huku Shemeji akirekodi Yale mazungumzo kupitia vifaa vyake pale mezani,


"Kesho utaletewa pesa waachie wote tafadhali,"


Janet alisema,

Sikumsikiliza nilikata Simu,


***************
Mambo yalikwenda Kama yalivyopangwa kesho yake tulikua baharini kwenye boti ndogo ambapo Janet alituma watu wake,


Tulikaa umbali wa mita kadhaa tulituma mtu wetu ambaye alienda kuchukua zile pesa tukazihesabu zilikua kamili,


Tuliziweka kwenye mfuko mwingine Kisha lile begi tukalitupa baharini,

Baadae tukawaachia wale jamaa wawili tukarudi zetu!

Tulibakia na mateka mmoja tu, Jack,


Usiku ule Janet hakuongea chochote, hivyo tulisubiri siku ya kesho endapo atahutubia taifa

Ni kweli kesho yake Janet alikuwa mubashara asubuhi saa 3 akihutubia taifa katika mkutano wa dharula,


Tulifuatilia tukiwa kwenye chumba maalum pale ofisini,


"Kwahiyo ndugu zangu Watanzania, nimewaita kuwapa taarifa muhimu,


Katika nafasi hii zipo changamoto nyingi nimekumbana nazo, nilijitahidi kutatua kwa kadri ya uwezo wangu,


Hata hivyo kutokana na Raisi Ni Kiongozi anayetakiwa kutawala na kuongoza kwa Haki yapo maeneo ambayo Kama Raisi, lakini Kama Binadamu sijatenda Haki, hivyo naomba Sana kukiri kuwa yapo mapungufu,

Nitataja maeneo machache,


Kwanza eneo la kukusanya mapato,

Nikiri wazi Kama serikali tunakiri kuzembea,.

Lakini eneo la pili Ni katika usimamizi wa miradi hapa napo Kama serikali tumekosea Sana,

Eneo la mwisho Ni eneo la utoaji Haki,

Eneo Hili naomba kukiri kuwa kumekuwa na lawama nyingi, na nyingine zikielekezwa kwangu moja kwa moja..

Mfano ipo kesi ya ndugu Allan,.
Nikiri wazi Kama serikali hatukupata muda wa kutosha kuchunguza kesi hii na kupelekea matatizo ambayo wengi mnayafahamu na sitaki kurudia,


Baada ya kutuma wapelelezi wangu kuchunguza vizuri tuliona ukiukwaji mkubwa wa Haki na Ndugu Allan alionewa,

Pamoja na kuwa ametoroka ama alitoroshwa lakini Raisi ninayo mamlaka kikatiba kumsamehe yoyote, na hivyo nimemfutia mashtaka yake,


Lakini tupo kwenye maongezi na serikali kule alikokimbilia Kama uhamishoni, Kama akiridhia Basi arudi nchini kwake na atimize majukumu yake ikiwemo kuitumikia nchi yake,


Nina amini wizara ya kazi watajaribu kuwasiliana hata na mkewe ambaye Ni daktari arudi kutumikia nchi yake,


Niwashukuru Sana wanahabari kwa kuitikia wito"

Alihitimisha Janet,


Tuliangaliana pale chumbani huku tukigonga mikono kwa Furaha,


Jioni muda ule ule tulienda kumtoa Jack na kumsindikiza Hadi bandarini ambapo alirudi Tanzania,


***************

Hata hivyo niliona niendelee kukaa Comoro kwa mwaka mmoja zaidi maana bado sikuwa na Imani na Janet,


Tuliona Ni vyema kusubiri wakati wa uchaguzi kwani miezi kadhaa ijayo ungefanyika uchaguzi Mkuu na Janet kuhitimisha miaka yake mitano,


Tulipanga kabisa Janet asigombee Tena Uraisi,


Tuliendelea kupanga Mipango kuhakikisha Mambo yanaiva,


***************


Zile pesa tuliamua kununua vifaa vya kampuni ikiwemo kuongeza magari na kuwalipa malipo mengine wote walioshiriki katika Lile zoezi la kuniokoa,


Maisha Comoro yalizidi kunoga na taratibu nikaanza kusahau mikiki mikiki yote ya Tanzania,

Siku moja nikiwa ofisini Shemeji alifika akiwa na gazeti la Tanzania mkononi alinirushia lile gazeti nilitupia macho haraka kidogo na kukuta habari ya kuhusu Bwana Shija,

Mkurugenzi mtendaji ambaye amehukumiwa kifungo Cha miaka 10 jela kwa sababu ya kupotosha ukweli kuhusu kesi Yangu,

"Ah Sasa inakuwaje Tena?"

Nilimuuliza Bwana Shem,

"Imegundulika Bwana Shija ndie alikua anatupa Siri lakini pia alikutorosha huku kwahiyo Sasa amegeuziwa kesi na hivi Sasa yupo Gerezani ameanza siku yake ya tatu, we must do something"

Bwana Isack alisema
 
MADAM PRESIDENT 23

Aisee Shija lazima tumuokee kwanza anajua Siri nyingi sana za kwetu, lakini ndio alileta familia yangu hapa"

Nilisema Sasa nikizunguusha zunguusha kalamu,

"Hivi hakuna namna ya kulipa faini hivi ili tumtoe Shija?"

Niliuliza

"Hakuna, tayari Ni kifungo Ila Nina wazo, njoo ofisini"


Alisema Shemeji huku akitoka nilimfuata kuelekea ofisini kwake,

Tulifika na Shemeji akabonyeza bonyeza kwenye komputa yake Kisha akanitaka kusikiliza ,


Nilijikuta natabasamu baada ya kusikia Yale maongezi yetu na Janet kipindi kile akiwa anataka kuwakomboa Akina Jack,

"Yeah naamini hili Ni wazo zuri tumpigie Janet"



Nilisema tulifanya namna kuwasiliana nae na hatimaye Janet akawa hewani,.

"Tahadhali Janet mwachie Shija, ujue Ana familia inanitegemea!"

Nilianza maongezi,


"Hapana yule mshenzi isingekuwa msaada wake wewe usingetoroka kabisa mikononi mwangu, ngoja ajutie"


Janet alisema kwa madaha,

"Kwakweli waliokupa Uraisi wamekosea Sana Yaani"

Nilisema,


"Sikiliza wewe mwanaharamu huwezi kunivua nguo na kunifanya halafu ukimbie, na kunitangaza, kwa taarifa yako huu ni mwanzo tu, yule Malaya wako mwingine utasikia habari zake muda si mrefu!"

Sikuelewa anamlenga Nani,

"Sikiliza mpenzi wangu Janet,

Kuna kitu hapa nitapenda usikie,


Nilisema Kisha nikasogeza Simu kwenye Ile computer na kumsikilizisha Yale maongezi


"Sikujua kuwa wewe Ni mshenzi kiasi hiki Allan, pamoja na kukupa mwili, wangu, kukupa pesa bado umenifanyia ujinga huo....sema Tena safari unataka Nini ?"


"Punguza Jazba Janet unajua Mimi sio mkorofi , mwachie tu Shija aendelee na maisha yake na maongezi haya yatabaki kuwa Siri na tutakupa original tape"


Nilisema

"Nikikataa?"

"Tutajua Cha kufanya Ila sidhani Kama utapenda haya maongezi wayasikie watu wako wa kamati kuu, vinginevyo unataka uwe Raisi wa kipindi kimoja"


Nilisema huku nikikata Simu,

Tulijaribu kuona Kama Janet atapiga Simu lakini hakupiga,




"Imefeli hii"

Nilisema,


"Basi hakuna namna ngoja tufanye plani B,

Tunaenda Tanzania kumtoa, "


Alisema Bwana Shemeji huku akipiga simu ya Jacob,

Alifika na tukajadili namna ya kwenda kumuokoa Shija kutoka Gerezani,

Tayari nilishakuwa na kibali Cha kurudi Tanzania kwahiyo tusingepitia njia za panya Tena Bali tulipanga safari ya kawaida kabisa,


Hata hivyo Jacob pamoja na watu wengine kadhaa walitakiwa kutufuata wakiwa na silaha nchini Tanzania kupitia njia za panya...


Mipango ilikamilika kwa msaada wa Jacob,


Na safari ikawadia Mimi na Shemeji tukatua Dar es Salaam

Tulifika na kukodisha Gari moja zuri ambalo lingefaa kwa kazi yetu ,

Shija alikua Gereza la Ukonga
Tulifanya ukaguzi pale na kuona njia nzuri Ni Ile ya kupitia Nyuma ya Gereza kutokea Stendi ya Gereza kuu la Ukonga kupitia KM halafu tunatokea Kivule,


Kesho yake tulipita Ile njia ya vumbi huku tukikagua maeneo yote ambayo tulihisi tunaweza kupata upinzani wa polisi

Tuliandaa Mambo yote Kisha tukaelekea matembele ya Pili kwenye Jengo tulilokua tumeandaa,

Usiku ule tuliwapokea Jacob na kundi lake Kisha tukampa Jacob Ile ramani ya Gereza pamoja na njia ya kutokea,

Jacob alisema lazima apitie Ile njia peke kesho asubuhi,

*************"

Saa mbili tulitoka tukiwa kamili ndani ya magari matatu ambayo tuliachiana dakika tano tano,


Tulifika na kushusha piki piki zetu na kupanda wawili,


Tulipofika karibu na Gereza tulivaa mavazi yetu Kisha tukasogea getini,


Jacob aliongea na yule Askari kidogo tu Kisha tukaruhusiwa kupita,

Tulifika mpaka ndani ya Gereza huku vitambulisho vyetu vikionekana wazi, wazi

Mimi nilivaa suti pamoja na Jacob wakati Shemeji alivaa gwanda la Jeshi na vitambulisho vyetu vilionyesha tumetoka idara ya usalama wa taifa,


Na Kuna habari nyeti ambazo tulitakiwa kuzichukua kwa wafungwa kadhaa,

Tulifika na majina ya wafungwa kadhaa ambao tuliwahoji Kisha badaae ikafika zamu ya Shija, tulimhoji kiasi Kisha tukaampa kikaratasi fulani hivi kwa Siri tukatoka nje ya Gereza na kuvua Yale mavazi Kisha tukasubiri...


Baada ya dakika 20 tulisikia king'ora sauti ya ambulance kwa mbali tulijiandaa na dakika kadhaa Ile ambulance ikaingia pale Gerezani tulibaki pale nje wakati Ile ambulance inatoka Jacobo alitoa ishara na Gari yetu mmojawapo ikaenda kuzuia njia


Wakati ambulance inapunguza Mwendo tayari vijana walishafika na kushambulia kwa risasi Kisha wakaondoka na Shija mgongoni wakakimbilia tulipokuwepo Kisha tukawasha piki piki na kuondoka kuelekea Ile njia ya vichochoroni ambapo tulitokea Kivule na kuingia kwenye gari Sasa safari ya matembele ya Pili ikaanza
 
MADAM PRESIDENT 24

Tulifika Matembele Ya pili na kubadili nguo zetu Kisha tukaingia kwenye Ile nyumba,

Bwana Shija alipewa dawa nyingine ambayo ilimfanya kujisikia Vizuri,

Usiku ule ule Shemeji na Jacob waliondoka pamoja na Shija kurudi Comoro Mimi niliamua kubaki kidogo Tanzania kuangalia Hali inavyokwenda,..


Nilitamani kuwaona Tena ndugu na jamaa hususani Shemeji Aida,


Lakini nilimua kwanza kujiwekea ulinzi,

Na hivyo kesho yake nilienda kwenye kituo Cha Runinga Cha Dar TV na kufanya mahojiano machache,


"Nashukuru Sana mheshimiwa Raisi kwa kunifutia makosa yangu hata hivyo suala la kurudi na kufanya kazi Tanzania tutaendelea kulitafakari kwa kuwa tayari Mimi nimeajiriwa kule pamoja na mke wangu"


Nilimalizia mahojiano Kisha nikatoka zangu na kuelekea mlandizi,


Nikiwa kwenye Gari Sasa habari zilianza kusambaa kuwa Mfungwa mmoja ametoroshwa Gerezani Ukonga na anatafutwa na Polisi,


Nilitabasamu ,


****************"


Saa 7 mchana nilifika kwa Shemeji Aida na alifurahi Sana kuniona,


Tulipiga stori nyingi za hapa na pale Kisha nikaenda Halmashauri kusalimia,



Kila mmoja alinikimbilia na kunisalimia,



Wengine walishindwa kujizuia machozi baada ya kuwaelezea purukushani zote nilizopitia..

"Aisee tuliskia eti ulikua na dawa ya kujigeuza kuwa kipepeo, Mara Ndege, eti polisi walikua wanashindwa kukutambua kabisa"



Jenifa alichombeza

Nilitoka na kuingia kwenye ofisi yangu ambayo zaidi ya mwaka Sasa sikufanikiwa kuingia,

Tayari kulikua na mtu anakaimu ofisi yangu lakini baadhi ya picha zangu na mafaili yangu bado yalikuwepo,


Vile vile Kama nilivyokua nimeyaacha,


Baada ya kutoka ofisini nilienda kwenye nyumba yangu mabatini na kuchukua vifaa vyangu muhimu Kisha kesho yake nikarudi zangu Comoro

Baada ya kurudi Comoro nilikaa siku Chache tu ndipo nilipopokea Simu ambayo ilibadili kabisa maisha yangu,


Ilikua Ni Kama mzaha hivi lakini ndivyo ilivyokua,

"Hello naitwa Bwana Brian Ni kampeni meneja wa Mama Devota wa chama Cha ATC,"

Alijitambulisha

"Ndio Bwana Brian Karibu!"

Nilimjibu huku nikaa vizur,


"Naomba Sana tuweze kuonana uje Tanzania ndani ya siku Chache zijazo tutakutumia tiketi ya ndege na Mambo mengine tunashida na wewe Sana"


Alisema Bwana Brian,


Nilikubali , maana haikua Jambo Jema kukataa wito,



Hivyo niliandaa Tena safari baada ya siku Chache Nikawa tayari kuonana na Bwana Brian,


Alinipokea Vizuri kabisa uwanja wa Ndege na Safari Yetu ikaishia kwenye ofisi kuu za chama Cha ATC,


Tuliingia ndani moja kwa moja na kufika kwenye chumba ambacho tayari mama Devota alikua anatusubiri akiwa na wajumbe wengine wa chama,


Jambo la Msingi walinitaka kuungana nao katika kampeni zinazoanza mwezi ujao kwa ajili ya uchaguzi na lengo likiwa kumtoa Janet madarakani,


"Tuna amini utakuwa msaada Sana kwetu katika na tunaomba Sana usitukatalie"


Alisema mama Devota,..

Nilipenda Sana kujifunza mambo mapya hivyo nilikubali wazo Hilo na nilipewa nafasi ya kurudi Comoro kujiandaa kwa ajili ya zoezi hilo,

Shemeji aliunga mkono ikiwemo kutoa msaada wa ulinzi na vifaa pamoja na magari kadhaa,

**************

August 2005,


Tulizindua kampeni zetu viwanja vya Saba Saba Jijini Dar,..hakika watu walikua wengi Sana,


Watu wengine maarufu walitoa hotuba zao,


Kisha ikafika zamu yangu kupanda jukwaani..


"Shemeji!!
Shemejii!!
Shemejj!!

Shemeji!!"


Zilikua Ni kelele za wananchi wengi wakiwa vijana wakiniita shemeji...

Nilisimama jukwaani nikiwa nimeshikilia kipaza sauti na kuwasihi watu watulie,

"Lazima tufanye mabadiliko,

Imetosha Sasa, chama hiki hakijafanya mema zaidi ya uonevu na Mambo mengine mabaya,

Chagueni ATC kwa faida ya nchi yetu...

Nawasihi Sasa Kama Shemeji yenuu,.

Dada yenu hafai!!


Mimi ndio nasemaaa"


Nilimaliza hotuba yangu huku vifijo na kelele za shangwe zikisikika kila kona

Tuliendelea na kampeni tukizunguuka kila mkoa na karibia sehemu nyingi watu walionyesha kukubali Sera za chama chetu,

Shemeji aliendelea kuunga mkono huku akituma misaada mbali mbali,


Janet nae na kundi lake waliendelea kufanya kampeni huku wakigawa nguo, chakula , pesa , n.k

Kampeni zilikwenda Kama zilivyopangwa na kulikua na kila dalili tunashinda uchaguzi,


Tayari tulishaweka mtandao Mpana,


Nakumbuka ilikua tumetoka Mtwara kesho yake ilitakiwa tufanye kikao Cha tathmini halafu tuhitimishe mkutano wetu wa kampeni,


Tulikuwa kwenye Gari moja Mimi na Brian wakati huo Deo, pamoja na mama Devota walikua Gari nyingine ya mbele, tulikua tunapita maeneo ya sinza kupitia barabara ya shekilango,


Tulisimama kidogo kwenye mataa pale ghafla ikatokea Gari Aina ya Fuso ikiwa na kifusi Cha mchanga wakati Gari ya mama Devota ikiwa inatoka kunyoosha Ile fuso ikatokea kwa Kasi kana kwamba inaenda mwenge kufumba na Kufumbua macho yangu yakashuhudia ajali kubwa kabisa kuwahi kutokea

Ile Gari ilirushwa na kwenda kugonga Nguzo ya umeme Kisha ikadumbukia mtaroni,

Tulitoka haraka kwenda kwenye eneo la tukio lakini haikua inahitajika utaalamu kujua hakuna mtu aliyeweza kupona,.



Tayari wananchi walishafika na polisi wa barabarani walisogea na kuendelea na majukumu Yao,


Yule dereva wa fuso alikua akikata Roho pale kwenye Gari iliyopondeka,

Tulibaki pembeni Mimi Ni Brian tukitazamana,


Kwa Mara ya kwanza nilijikuta machozi yakinidondoka,....

Kazi yote ya usiku na mchana Leo hii imevurugwa , zaidi Sana imeondoka na uhai wa watu watatu...

"Bila shaka Ni Yule mwanamke"

Niliwaza

Janet ,


Polisi walikua wanasukuma watu huku wakizunguusha utepe eneo la tukio...


"Brian Twende, Nilisema nikimvuta mkono"
 
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]duuuh hatari sana
 
MADAM PRESIDENT 25

Tulirudi kwenye Gari na kuwasiliana na katibu wetu wa chama ambaye alifika muda mfupi baadae na tukaongozana na polisi kwenda hospitali Hali Sasa ilikua tete wiki ijayo tu ilitegemewa kufanyika kwa uchaguzi Mkuu,

Hakukuwa na namna tulioomba tume isogeze mwezi mmoja mbele tupate mgombea wa kukaa kwenye nafasi ya mama Devota,


Tayari tulishaweka Mafanikio makubwa kwenye kundi la wanawake hivyo Sasa kuweka mgombea wa Jinsia nyingine kungeharibu Tena kile tulichokua tukikiamini,

Kulikua na chama kingine Cha upinzani CDM ambacho ndicho kilikua chama kikuu Cha upinzani huku tukifuatia sisi,

Na kwa bahati nao walikua wameweka mgombea mwanamke ,
Bi ZainaB Ali,


Tulifanya nao mazungumzo na kuuangana nao kutokana na ufinyu wa muda tusingeweza kuunda chama kimoja tukawaunga mkono,

*****************


Tuliaandaa kituo chetu maalum Cha kukusanyia matokeo yetu maana tuliamini bila shaka tungeshinda uchaguzi ule mapema Sana!

Siku ya kupiga kura tuliwahi kufungua chumba chetu na kuweka computer zetu ipasavyo,

Kila Mara nilikua nikitabasamu kwani Nilijua mwisho wa Janet ulikua umefika,

Tulikuwa watu nane kwenye kile chumba Mimi na Brian, pamoja na jamaa Joackim na Belinda, kutoka chama Cha CDM,


Halafu kulikua na wataalamu wa komputa wawili wajapan, pamoja watu wawili kutoka Comoro ...

Mpaka saa 5 na dakika ishirini asubuhi tulikua tunaongoza kwa matokeo ya kura kwa ujumla,

Nje ya chumba kulikua na ulinzi wa kutosha kuhakikisha tunafanya Ile kazi kwa ufasaha,

Jacob tulimpa Jukumu la kutulinda dhidi ya jaribio lolote la serikali,.

Na ilibidi anipigie Simu moja kwa moja

Nilikua na kawaida ya kuweka Simu "kimya"

Kwa ajili ya kuepusha usumbufu,

Wakati natoa Simu mfukoni ili nimpigie Brian aliyekuwa ametoka kidogo nilistuka kuona "missed calls 10"

Kutoka kwa Jacob,.

Wakati natafakari niliona ujumbe wake pia aliokua ametuma

"Fungeni vifaa mkimbie hapo niwakute nje ya geti la mbio"


Moyo wangu ulipiga Kasi sikuwa na utani na Jacob Ila niliona anatania,


Mbaya zaidi hiyo sehemu tulioipa jina geti la mbio ilikua Ni mbali Sana kutoka pale,

Wakati nawaza nikasikia sauti za risasi huko nje

Tulifunga vile vifaa haraka na kuondoka na vile vinavyowezekana Kisha nikawapa ishara wanifuate tayari tulishajiandaa kwa hili,


Nilifungua mlango wa dharula na kutokomea,


Tulitokea kwenye Gari tulilokuwa tumelitegesha Kisha tukaondoka Sasa tulikua Saba bila Brian


Tuliwahi kwenye geti la mbio na kwa bahati Jacob alikuwepo Safari ikaanza kwenda kwenye kwenye sehemu ya maficho,

Tayari tuliwasiliana na bi ZainaB Ali,


Ambaye aliwasiliana na Taasisi nyingine za kisheria na Haki za Binadamu kuhusu kuvamiwa kwa kituo chetu,

Msemaji wa Serikali alijitokeza hadharani kuwa chama Cha CDM walikuwa wameajiri wataalamu wa Komputa ili kuingilia na kudukua mfumo wa utendaji kazi wa tume ili ipike matokeo,


Hata hivyo wamefanikiwa kusambaratisha kundi Hilo na kuonyesha baadhi ya komputa walizochukua pale ofisini,

"Niwatoe wasi wasi serikali itahakikisha matokeo sahihi yanatangazwa na maamuzi ya wananchi yanaheshimiwa"

Alimalizia.


Brian alipiga ngumi ukutani kwa hasira huku akikaa chini kwa hasira

Ni wakati naendelea kuwaza Sasa Shemeji Isack alinitumia ujumbe

"Nishawaambia hamuwezi kumtoa huyo kizee madarakani kupitia vikaratasi tu"

Niliamua kuzima Simu kwa muda huku nikiondoka pale sebuleni na kuingia kwenye chumba changu,

"Janet Janet why unataka kubaki madarakani unaogopa Nini"

Niliwaza,

******************
Matokeo ya uchaguzi yalitangazwa na Janet akatangazwa mshindi kwa 78% huku bi ZainaB akipata 20% ya kura na wengine wakagawana zilizobaki,


Ilikua Ni siku chungu sana na hakuna aliyekubali kula tuliangalia kazi yetu tuliyokua tumefanya na kuona Ni kazi bure,

"Weka Dar TV chap"

Nilipokea ujumbe kwenye simu yangu na kumtaka Brian aweke Dar TV ,

Macho yetu yaliganda kwenye TV

Wananchi walikua wameingia barabarani wakishinikiza hawakukubali matokeo ya uchaguzi polisi walikua wakipambana na Raia Sasa,

"Lets go guys,

Twendeni , twendeni wananchi wakituona watapata nguvu zaidi!"


Nilisema Sasa nikivaa koti langu la kijeshi pamoja na kofia

Tulitoka nje na kuingia kwenye Gari na kuondoka hatukujua tunaenda wapi,


Tuliwaachia wale wajapan kazi ya kufanya mawasiliano na Shemeji sisi na Jacob tukaingia barabarani,

Jacob alikuwa bize na simu yake pengine kuliko siku zote nilizowahi kumuona,


Hata hivyo Ni lugha aliyokuwa akitumia kuongea na simu hizo

Kwanza ilikua lugha ambayo Mimi na Brian hatukuelewa,

Lakini pia aliongea kwa ufupi mno,


Tulifika sehemu na kukuta barabara imefungwa na wananchi wamechukua hatamu na kuzuia magari yote ,


Tulitoka kwenye Gari na walipotuona walianza kushangilia huku wakipiga nilisimama juu ya Gari na sikujua ujasiri ulitoka wapi!

Nikapaza sauti kwa nguvu,

"Jamani Ni kweli tumedhulumiwa haki yetu,

Mama yetu aliuliwa,


Tumenyang'anywa Haki yetu ,


Lakini hatujanyang'anywa nguvu zetu,


Polisi Ni wachache sisi Ni wengi!!

Sasa suala tunachukua Haki yetu Sasa!!



Lakini kumbukeni hakuna raia Ni adui yetu na sio kila polisi Ni adui yetu!!


Naomba tusichome majengo Wala tusiuane sisi kwa sisi, na polisi akikubali kutulinda msimdhuru"

"Watuuuuuuuuu"

"Nguvuuuuuuuu"

Waliitikia kwa sauti
 
MADAM PRESIDENT 26

Tulitoka pale huku tukiendelea na maandamano Sasa tayari nilishapoteza Simu yangu ya mkononi nilijitahidi kwenda mbele zaidi huku nikihakikish Nakua karibu na Brian,

Nilishasahau kabisa kuhusu Jacob,

Wakati tunakaribia mwananyamala

Sasa Polisi walianza kusogea mahali tulipo,


Walikua na vipaza sauti kututaka tusogee mbali sisi tuliendelea kusogea

Na Sasa polisi wakaanza kurusha risasi hewani na maji ya kuwasha washa,


Tuliendelea kusogea na wale polisi walikua Kama kumi hivi,


Mara ghafla kundi lingine la watu likatokea na hivyo kuwaweka polisi Kati Kati,


Nilijaribu kuwasihi wananchi kutulia lakini ilikua Ni kazi bure tu,


Walianza kuvamia wale polisi na mapambano yakaanza,


Mapambano yalidumu kwa zaidi ya saa moja, Sasa sikua na namna zaidi ya kuondoka eneo Hilo kwani hata Brian sikujua alipokua,


Hali ilichafuka na Biashara zikaanza kufungwa,


Nilipenya Kati Kati ya watu na kutoka huku nikikimbia kuelekea kusikojulikana,


Tayari helkopta za kijeshi zilikua zinaranda Randa


Ni wakati sijui muelekeo wa niliona uchochoro mmoja nikapita na kutokea upande wa Pili wa bara bara,

****************

Tayari Dar es Salam ilishachafuka na Hali ilikua tete,


Milio ya risasi ilisikika kila sehemu,


Nilivua Lile koti la kijeshi na kofia na kubaki na Tisheti tu

Magari ya polisi yalikua yanapita huko na huko na kila aliyeonekana alibebwa ,

Wakati nawaza Mara ghafla nilimuona Mzee mmoja akikimbia kuelekea upande wangu nilijiweka tayari niliokota jiwe moja kubwa Kisha nikajibanza kuangalia yule anayemfukuza Mzee,


Alikuwa ni Askari nilitoka pale mafichoni kwa Kasi ya ajabu nikampiga jiwe yule Askari akaanguka chini ,

Nilimshika mkono yule Mzee na kumkokota kuelekea kwenye nyumba moja tukajibanza tukihema kwa nguvu,

"Naitwa mr Eric"
Alisema akinipa mkono,

"Allan"
Nilisema nikitazama huko na huko,

"Allan? Ha kijana nimefurahi kukuona Sasa nimeona sura yako ni wewe kweli"

Yule Mzee aliongea,


"Samahani naomba Simu "

Nilichukua Ile simu na kumpigia Jacob,


Simu iliita tu haikupokelewa,

Nilijaribu tena na ikapokelewa

"Allan"

"Nenda Melinda stationary manzese Sasa hivi gonga Mara moja tu kwa nguvu"

Jacob aliongea akakata Simu na haikupatikana Tena!


Nilijaribu kuongea na yule Mzee akanionyesha uchochoro mmoja wa kutokea barabarani,


Nilitokea barabarani ambapo kulikua kumetulia kabisa nilianza kukimbia ,


Kwa bahati niliona piki piki ikiwa imeegeshwa tu,


Nilichukua kipande Cha jiwe na kunyofoa waya wa Moto Kisha nikakata na kuunganisha,

Nikajaribu kuisukuma ikawaka!


Nilifika manzese stendi na nikaweka piki piki na kuanza kuitafuta Melinda Stationary,

Kwa saa nzima nilikuwa natafuta bila Mafanikio niliamua kuvuka barabara na kuingia mtaa wa Pili kulikua na Jengo la ghorofa likiwa na frem za maduka kwa chini ambayo yalikuwa yamefungwa,
Kwa mbali niliweza kuona maandishi ya Melinda Stationary
Nikaongeza mbio nikagonga Mara moja Kama nilivyoambiwa....

Mlango ulifunguliwa Kisha nikaingia haraka ndani mlango ukafungwa Tena,

Ndani kulikua na wasichana watatu na mvulana mmoja sura zao zilikua ngeni kabisa,


"Karibu hatuna muda mrefu umechelewa Sana"

Alisema Yule dada huku wakisimama na kufungua mlango uliokua Kama stoo,


Tulipita hapo na kutokea nje kulikua na gari moja ndogo tukaingia,

Hakuna aliyekuwa anaongea na mwenzake,


Tulipita njia za panya panya tukikwepa polisi,

Na hatimaye tukatokea njia ya lami Tena mbele yake kulikua na kizuizi Cha polisi,


"Sharon malizana nao,"

Msichana mmoja aliyekuwa Kama kiongozi alisema huku akipunguza Mwendo,


Na gari ikasimama,

Msichana mwingine alitoka nje na kumsogeza Askari mmoja pembeni na kuanza kuongea nae huku akionyoosha mikono kuelekea kwenye Gari,

Baada ya muda alikuja nae yule Askari akachungulia ndani Kisha akaenda kuongea na wenzake baada ya dakika kadhaa tukaruhusiwa na kunyoosha njia kuu ya kuelekea Mbezi,


Tuliacha barabara na kuingia kwenye barabara ya vumbi

Gari ilikua kwenye spidi Kali na hakukuwa na haja ya kuelekezwa kushikilia Vizuri,


Tulifika kwenye nyumba moja kubwa ilivyokuwa na Geti Jeusi na likafunguliwa Gari ikaingia baadae geti likafungwa Tena,

Tulishuka na kuingia ndani na kukaa kwenye sofa ,

Ilikua Ni nyumba nzuri ya kuvutia,


"Allan utabaki hapa

Huyu Ni Alex, na huyu Ni Dama, mtakaa nao hapa,


Huruhusiwi kutoka hata nje ya Hii nyumba achilia mbali kutoka nje ya geti!"

Alisema Yule dada

"Wewe Ni Nani? Yaani mniweke hapa Sasa mmeniteka au?"

Niliuliza huku nikisimama,


"No usiondoke!"

Alisema Sasa yule jamaa,


Yule msichana alitoka zake na wale wasichana wawili tukabaki watatu

"Ukiingia hapo kulia Kuna chumba Ni master Kuna kila kitu isipokuwa chakula Mtakuwa mnakuja hapa sebuleni Sasa Mimi naelekea jikoni kuandaa chakula Cha usiku"

Alisema kwa upole Yule msichana,


Alex alikuwa ananitazama tu hakuongea chochote,

Niliingia chumbani na kuwasha Tv Sasa ilikua Ni matukio ya maandamano nchi nzima,


Watu walikuwa wakiendelea kupambana na kwa Mara ya kwanza Sasa nilimuona Bi ZainaB akiongea na vyombo vya habari huku akiwa amezunguukwa na walinzi wenye mavazi ya kijeshi,


Kwa karibu kabisa alikuwepo Jacob


"Tunamsihi Bi Janet Sasa kuachia madaraka kwa hiari badala ya kusubiri damu nyingi kumwagika,

Kwasasa kama mnavyoona ndugu Wana habari tayari wakuu wa mikoa 10 wameshaungana na sisi hivyo tunamsihi Janet kuheshimu maamuzi ya Raia"

Bi ZainaB alimalizia hotuba yake huku Sasa akina Jacob wakimuongoza kuingia kwenye Gari

"This is ridiculous!"


Nilijisemea Sasa nikizunguuka zunguuka mle chumbani,

Nilienda bafuni kuoga na Kisha nikarudi na kufungua kabati,

Nilikuta nguo mpya za kiume nikachukua mojawapo na kuvaa Kisha nikafungua mlango,


Sikuamini kumkuta Alex pale mlangoni

"Aisee sikusomi kwahiyo muda wote uko hapa mlangoni wima namna hii?"


Nilimuuliza huku Sasa nikitabasamu,


Hakujibu kitu alinifuata tu nyuma nyuma nikaenda mpaka sebuleni ambapo kulikuwa na mabakuli ya chakula nikafunua na kuweka chakula,


Alex nae akaweka chakula chake..



"Wewe Ni Nani"
Nilimuuliza Sasa

"Alex"

"Okay hapa mmekuja lini?"

Nilimuuliza
 
MADAM PRESIDENT 27

"Ndio Kama hivi Broo"

Alisema Alex,


"Kwahiyo wale wakina Dada wengine wanaenda wapi?"

Nilimuuliza


"Nani Sharon na Elice?"


Alex aliuliza,


"Ndio"

"Aisee sijui Ila nimesikia Kuna Broo mwingine wanaenda kumpa ulinzi "

Alisema,


"Kwahiyo nyie mpo chini ya Nani?"

Nilimuuliza,

"Kila mmoja na mkataba wake Broo"

Alisema Alex huku akiendelea kupiga msosi,

Tulimaliza chakula Kisha nikarudi zangu kulala


Nilijaribu kutafuta Simu Ile nyumba nilikosa,


Hakuna aliyekuwa na simu,

Niliwasha Tena Televisheni na habari zilikua zile zile,



Nafsi ilinisuta kukaa pale ndani huku wananchi wakiendelea kupambana na polisi,


Hata hivyo sikuwa na namna nikajikuta napanda kitandani na kupitiwa na usingizi,


Niliamka asubuhi kupitia saa ya pale mezani tayari ilikua saa 2 kasoro asubuhi niliwasha Televisheni Tena na Sasa kulikua na kipindi mubashara ambapo baadhi ya mitaa Jijini Dar ilikua inaendelea na shughuli Kama kawaida,


Wananchi walikua wakiimba na kwa furaha barabarani wakiwa na Bendera za chama Chetu,

Baadae mtangazaji akaonekana nje kidogo ya makao yetu makuu ya chama,


"Mpendwa mtazamaji Kama tulivyokujuza muda mfupi uliopita kuwa tupo hapa kwa ajili ya kumsikiliza bi ZainaB ambaye anatoa msimamo wa chama katika hatua hii ya mwisho ambapo Raisi aliyeko madarakani ametangaza kukubali maridhiano yafanyike huku akikubali kujiuzulu nafasi yake

Tupo hapa moja kwa moja na muda si mrefu basi Bi ZainaB atafika hapa Endelea kuwa nasi!"


Mtangazaji alisema


"Kwahyo Janet kakubali yaishe kweli kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho!"

Niliwaza huku nikienda bafuni kuoga.

***************



Janet aliongea na waandishi wa Habari,


Huku akisisitiza umoja wa kitaifa huku akikubali kuachia ngazi na kumpisha bi ZainaB,

***********

Nilikaa pale kwa siku tatu Kisha baada ya hapo alikuja Brian,

Tulikumbatiana kwa furaha na Safari ikaanza ,

Tulifika mpaka makao makuu ya chama ambapo bi ZainaB alifurahi sana kutuona,


Nilifurahi Sana kuonana na Jacob Tena,


"Haikuwa rahisi Broo but imekuwa!"


Jacob alisema huku Sasa tukiingia kwenye chumba Cha mikutano


Tuliweka Mipango sawa ikiwemo kuandaa Baraza la mawaziri kwa kushirikiana na baadhi ya vyama huku tukichukuwa wachache kutoka chama tawala ambao tuliona uwezo wao ,

Hatimaye kila kitu kikawa tayari na siku ya makabidhiano ya ikulu ikatangazwa!

*****************


Nikiwa nimevaa suti yangu Safi kabisa huku pembeni yangu akiwa amekaa mke wangu nilisubiri kwa hamu kuona maridhiano hayo ya amani yakifanyika

Janet alikabidhi ofisi huku Bi ZainaB akitawazwa kuwa Raisi mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Bi ZainaB hakuchelewa Mara TU baada ya kupewa kipaza sauti alitangaza Baraza lake la mawaziri,

Makamu wa Raisi alikua Bwana Kambona kutoka chama Cha orange,


Waziri Mkuu akawa Brian,

Na mawaziri wengine kutoka vyama mbali mbali

Kama nilivyoomba Tangu mwanzo Mimi sikuwa mwanasiasa hivyo nilikua na cheo Cha mwandishi wa Hotuba za Raisi!

Na hivyo Sasa nilikua na jukumu la kuandika hotuba zote za Bi ZainaB,

Janet aliondoka na kuelekea kwao Morogoro kwenda kuishi huko,

Maisha yakaendelea Kama kawaida.



**************


Baada ya miezi mitatu,

Tulipata habari Janet Ni mgonjwa amelazwa hospitali ya taifa niliongozana na bi ZainaB kwenda kumtembelea kweli Hali yake ilikua mbaya,


Janet alikuwa amekonda Sana ,

Wakati tunatoka aliomba nibaki niongee nae,

"Allan naomba unisamehe Sana kwakweli kila kitu ,naomba unisamehe nife kwa amani kabisa!"

Alisema kwa unyonge

Nilichukua mkono wake Kisha nikakaa pale kitandani

"Ah Janet Yale yamepita kumbuka haya Ni maisha tu na ndio maana sijalipiza kisasi kwa chochote kile"

Nilisema Huku nikisimama na kuondoka


Madaktari walisema Janet anasumbuliwa na ugonjwa wa Moyo pamoja na kisukari


Baada ya wiki moja Janet alifariki Dunia
Na bi ZainaB aliamua kutangaza maombolezo ya siku tatu,


Siku moja kabla ya mazishi Sasa nilijifungia ndani na kuandika hotuba nzuri ambayo nilifikiri bi ZainaB ataipenda Sana,


Kwa Mara ya kwanza nilijikuta naandika hotuba kwa hisia zaidi badala ya kutumia akili,

Nilimaliza kuisoma Kisha nikaihariri

Nikaongeza baadhi ya maneno Kisha nikaichapa.


Alikuja katibu muhtasi wa Raisi kuchukua Ile hotuba nikatoka pale chumbani nikiwaza mengi kuhusu Janet,



Nilienda kwenye kabati langu kubwa na kutoa lile sanduku,


Nikalifungua,..


Lilikua na vitu vingi alivyonipa Janet ikiwemo picha, kadi na barua nyingi Sana alizokuwa ananiandikia Janet,


Nilisoma baadhi huku machozi yakitiririka

Ni wazi Janet alikua ananipenda Sana,

Amefanya alivyoweza kulinda upendo wake,

************


"Tutamkumbuka Bi Janet kwa ucheshi wake, lakini pia kwa ujasiri wake,

Kama wanawake Janet Ni kielelezo kizuri sana kwetu katika namna ya kusimamia na kutekeleza ndoto zetu,


Janet alikuwa hodari katika Mambo mengi ya maisha ikiwemo uchumi, masomo na hata namna alivyolea familia yake,

Lakini Janet alikuwa mrembo pia ambaye alistahili kabisa kuwa mama wa taifa hili,
Apumzike kwa amani"


Alimaliza kusoma hotuba yake bi ZainaB huku akiniangalia na kutabasamu kwa namna nilivyopangilia Ile hotuba
 
MADAM PRESIDENT - FINAL EPISODE

Tulimzika Janet na kusahau kabisa,

Niliomba likizo ya mwezi mmoja na nikaenda kijijini Mlandizi nilienda maalum kwa ajili ya kusalimia ndugu na jamaa lakini kikubwa nilienda kuweka sawa utaratibu wa Mali zangu hususani nyumba,


Nilimkuta shemeji Aida akiwa pale kwake na kidogo alikuwa amefanya usafi nyumba yake imekaa Vizuri,


"Naona shemeji yake leo umetukumbuka, nikajua umekuwa mwanasiasa Hadi uchaguzi mwingine!"

Alisema shemeji Aida

"Hapana shemeji Aida, unajua Mimi siwezi kukusahau kabisa,


Sasa hebu fanya kwanza ugali samaki aisee"

Nilisema Huku nikikaa pale kwenye sofa,


Tulipiga stori mbali mbali baadae nilimwambia


"Shem nakumbuka Sana msaada wako, Nina zawadi yako kidogo naomba uikubali"
Nilisema Huku nikienda kwenye Gari na kutoa bahasha,


"Shemeji Ile nyumba ambayo mlikaa kule mabatini kuanzia Sasa hivi Ni yako,"
Nilisema Huku nikimpa Ile hati ya nyumba,

Shemeji Aida alifurahi Sana,

Niliona Ile ingeweza kumfaa kwa makazi na hii ya kwake kwakuwa ilikua mjini kabisa angeweza kuipatia wapangaji.


Nilitoka na kumtafuta Jose ambaye naye nilimpa Nyumba yangu nyingine pamoja na Gari dogo,

"Hivi bado Nini tena kwenye maisha kinahitajika?"


Nilijiuliza wakati narudi Dar,

Niliamua kumalizia likizo yangu kwa dada Tatu,

Mbezi

**************
Wakati namalizia likizo walikuja watangazaji Wa Dar TV kufanya mahojiano na Mimi ya kipindi Chao kipya Cha " Mapito"


"Labda wengi wanakufahamu Kama shemeji lakini Kuna mengi sana ambayo hawajui hususani mahusiano yako na marehem Madam President, hebu Leo tuambie ilikuwaje kuwaje yaani"


Alisema mtangazaji

Nilikunywa maji kidogo Kisha nikatabasamu na kuongea..


"Ni kweli Mimi mwenyewe nimetamani Sana kuiweka wazi hii story Sasa tuanze..


Madam President....02 (SOMA SEHEMU YA 1)


Juni 1998

Ilikua jioni nzuri kabisa ambapo sehemu mbali mbali za jiji la Tanga Kuna Hali ya baridi na mvua nyepesi zilikua zimeanza, nikiwa na Rafiki yangu Jacob tulikua mwisho kabisa ya mstari kuingia kwenye Basi la shule tayari kwenda Tanga mjini ambapo kesho yake mashindano ya mkoa umiseta yalikua yanaanza,

Mimi na Jacob Kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wengine tulikua na Furaha kabisa ya kutoka eneo la shule na kwenda kwenye mashindano hayo... Mimi nilikua nacheza mpira wa miguu na Jacob yeye alikua mchezaji mahiri wa mpira wa kikapu..

Tulipenda kumuita Joo tukikatisha jina la Jordan tukimfananisha na mchezaji mahiri Michael Jordan,

Hakika alifanya vizuri lakini pia umbo lake lilimbeba kwani alikua mrefu ...


Kwenye mpira wa miguu Mimi nilicheza Kama winga wa kulia namba 7, pamoja na Mambo mengine lakini nami nilipewa jina la Beckam kutokana na kuwa mahiri katika kucheza mipira iliyokufa,
Tulisogea kwenye basi huku tukishikilia mabegi yetu na Safari ikaanza ...


**************

Ni saa 3 tuliwasili Shule ya Tanga technical ambapo Kama ilivyo kawaida wanafunzi walipiga makelele na Furaha huku wakigombania kushuka,


Ilikua Ni Mara ya kwanza kufika eneo Hilo hivyo nilihakikisha kila kitu kimekaa vizuri kabisa Kisha nikashika begi langu na kusogea kuelekea kwenye mabweni ya wavulana ambayo tulikua tumeandaliwa...


"Dah mwanangu angalia watoto walivyo wazuri kweli hii ndio Tanga! Tutatoka kweli?"
Alisema Jacob akinisukuma bega kidogo,

"Hapana kaka Mimi siwezi kumsaliti Mary kabisa" nilisema huku nikionyesha dalili za kukasirika kidogo tulipanda ngazi na kuelekea vyumbani huku ratiba zingine zikifuata!

*************


MWISHO...‼
 
Natanguliza shukrani zangu kwa ninyi nyote mliosoma story hii na Sasa niwatakie Kila la kheri

Labda tutakutana kwenye MZAHA WA DAMU , MPANGAJI AU KESI YA MZEE MNYOKA
!!!!
Kura kwa Mpangaji.

Asante Mwandishi
 
Back
Top Bottom