Hadithi: Mpangaji

Mzee Kidude aumbuka😀
Umalaya umemponza😂
 
Majibu ya bwana Sele mi hoi ...
....anamjua hadi Esther ambae hajawasili
 
Kumbe mambo ni moto Hivi lol ubarikiwe mkuu ngoja niendelee nilipoishia!
 
MPANGAJI ----- MWISHO WA MWISHO

BY CK ALLAN
“ kwahiyo ninaomba sana mheshimiwa Hakimu mahakama inisamehe tu maana nilitishiwa maisha yangu, kuwa nisipofanya hivi maisha yangu yatakuwa hatarini”
Alimaliza kujieleza mzee Kidude huku wakili wake akipigwa na butwaa na kujaribu kuingilia kati
“Mheshimiwa Hakimu mteja wangu hayuko sawa kisaikolojia hivyo naiomba mahakama yako tukufu isitoe uamuzi leo hii” alisema wakili
“napinga mheshimiwa Hakimu” aliingia Kati Rapha
“ mahakama yako tukufu ikubali maelezo ya mshtakiwa kwakuwa hakuna vielelezo vya daktari kuwa ana tatizo la kisaikolojia” alisema Rapha akikaa
“nakubaliana na wewe, maelezo yake yamechukuliwa na mahakama” alisema Hakimu na kisha akajiweka sawa ili kutoa hukumu ya kesi,
Mwendesha mashtaka alisoma maelezo ya kesi na ushahidi wa maelezo ya pande zote mbili na kisha akatoa ushauri wake kuhusu mwenendo wa kesi kisha akamkaribisha hakimu ambaye alisoma tena maelezo na kurejea vifungu kadhaa vya sheria kisha akatoa hukumu yake
“kwahiyo basi, Mahakama imeona kwamba ndugu Sele Selemani Sele hana kesi ya kujibu na mahakama imemuachia huru, hata hivyo kuhusu kesi yake ya madai kuhusu kuwa na undugu na ndugu Lukas Tuppa, mahakama inaruhusu mdai kuleta vielelezo ikiwemo kupima vipimo vya nasaba na mdaiwa, hata hivyo mahakama imemuona kuwa na hatia mshtakiwa Janet Lukas Tuppa , na kutoa adhabu ya miaka 25 gerezani kwa kupanga na kutekeleza mauaji , na vile vile mahakama inamhukumu kifungo cha miaka 15 gerezani kwa kupanga na kutekeleza utakatishaji wa fedha na uhujumu uchumi, na vifungo hivi vinaenda kwa pamoja, vile vile Mahakama inamhukumu Kidude James Tito miaka 8 gerezani kwa kupanga na kutekeleza njama za uhalifu wa kifedha pamoja na kuidanganya mahakama..”
Sele alipiga magoti chini huku akimshukuru Mungu na kisha akatazama huko na huko na kukumbatiana na wakili wake kisha akakumbatiana na watu wengine huku akisogea sasa kumuelekea mama Joan
Wakati huo mama Joan alikuwa akilia huku askari wakiwa wamemzunguuka katika harakati za kumtia pingu, ni wakati akiwa amenyoosha mikono ili wamfunge pingu kwa haraka alichomoa bastola ya askari mmoja na kujiwekea kichwani, taharuki ilizuka kwa ghafla huku sasa polisi wakimsihi asifanye alichokuwa akitaka
Hata hivyo bila kusita alifyatua risasi na kumpasua kichwa na kuanguka chini..
BAADA YA WIKI MOJA
Doreen alirudi zake Italy huku akiwa amemaliza kabisa kuweka mambo yote sawa,
Siku hiyo Sele alikuwa nyumbani na mke wake wakicheza mchezo wa mpira wa miguu kwenye komputa huku wakitaniana wakati kengele ya mlangoni ilipolia kuashiria kuna ugeni Haraka Sele alifungua simu yake na kufungua program maalum na kuangalia kamera ya nje
“mmhhh mbona kazi ipo!”alisema Sele akimuonyesha mkewe hao wageni wenyewe
“loh, Lukas, waziri Joan, Na Jesca’ mh
Alisema huku akimuangalia mumuwe, wakati huo tayari mzee Lukas alikua akijiandaa kubonyeza kengele kwa mara ya pili, ndipo Sele alimshika mkono mke wake na kutoka nje kwenda kuwapokea,
Alifungua geti kisha akamsogelea mzee Lukas na kumkumbatia kisha akawasalimia Joan na Jesca na kuwakaribisha ndani,
Walitulia zaidi ya dakika tano huku kila moja akishindwa namna ya kuanza mpaka pale mzee Tupa lipovunja ukimya
“usishangae Gift, damu ni nzito kuliko maji, yaliyotokea yametokea, hawa ni dada zako!” alisema mzee Lukas akiwaangalia akina Joan ambao walisimama tena kukumbatiana huku machozi yakiwatoka kisha wakamkumbatia na Esta pia
Baada ya maongezi kiasi sasa waliaga na kusimama
“sasa nataka kuja tena kucheza na wajukuu hapa Gift, wajukuu!” alisema mzee Lukas kwa utani huku akipanda gari na kuondoka
Hakika ilikua siku ya furaha sana kwa Gift na Esta siku hiyo alirudi ndani haraka na kumshika mkono mke wake na kumvuta
“nini tena Gift!’ alisema Esta
“hujamsikia Mzee anasema anataka wajukuu!’’
Alisema Gift huku wote wakiangua kicheko.
MWISHO_____
Asanteni sana kwa uvumilivu wenu na kusoma hadithi hii!
Siwez kuwataja wote lakini niseme mmenitia moyo sana, ni hadithi yangu ya 3 kuleta humu baada ya Kesi ya Mzee Mnyoka na Madam president,
Kwasasa nitaweka pozi kidogo kwakuwa kifaa nilichokua natumia (laptop) nimekisukuma! Kutokana na sababu za hapa na pale!
Basi niseme Tena nawashukuru sana na in shall Allah tutaonana Tena kwenye MZAHA WA DAMU, Huko mbeleni , panapo majaaliwa
Wabilah towfiq
CK Allan
0746 266 267
 
Daaaaah THANKS A LOT BRO I LIKE IT
 
Hongera sana chief, wewe ni mwandishi mzuri sana . Jaribu kuweka hizi kazi kwenye vitabu

Asante

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
shukran sana allan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…