Hadithi: Mpangaji

Nash Nash mkuu kama kawaida yangu nakimbiza mwizi kimya kimya ,najua story zako huwa zinaisha hivyo usiache kunitag jmn
 
MPANGAJI 05

Sasa Esta alitafuta namna ya kuanza mazungumzo yake yale aliyoyaita rasmi,
Aliweka komputa pembeni na kisha akamsogelea Sele pale kwenye sofa na kumshika bega,
“Sele, naomba kwanza nisamehe sana ila sina namna nyingine isipokuwa hii” alisema akianza
Alimsimulia Sele kuhusu historia yake ya maisha, elimu yake na mapenzi na kisha akamsimulia kuhusu mama Mwajuma na hadithi nyingine ambazo hakuona umuhimu wa kuzificha
“ mama Alikuja kutafuta maisha Dar miaka wakati huo aliniacha na bibi, kwa uhalisi mama alipata ujauzito akiwa darasa la saba, na mara baada ya kujifungua na mimi kuacha kunyonya ndio akaja huku Dar, alikuwa kila mwaka anakuja na kuniletea nguo na pesa za matumizi na hatimaye nikamaliza darasa la saba na kuchaguliwa kidato cha kwanza, wakati nikiwa likizo mwezi wa sita nakumbuka mama alikuja kijijini kwetu Moro goro akiwa na mtoto mwingine mdogo akasema anaitwa Mwajuma na ndio mama akatutambulisha rasmi kuwa ameolewa na mwanaume muislamu na kuamua kubadili na yeye” alisema Esta,
“kuna kitu nakiona kwako Sele, nilivyokuja nilisikia habari nyingi sana kuhusu wewe ndio maana hata siku ile nikasubiri kuonana na wewe , nimeona unahitaji msaada Sele ,na mimi ndio wa kukupa huo msaada Sele, tafadhali kama ulikua huna imani na mimi naomba sana uniamini, naomba sana Sele, naahidi kukutunzia siri yako yote kabisa utakayoniambia kuna kitu naona kabisa hakiko sawa Sele na mbaya zaidi hata wewe mwenyewe huna furaha na maisha haya unayoishi!” alisema Esta sasa na machozi yakaanza kumtoka
“tafadhali niambie sele, wewe ni nani hasa, umetokea wapi na familia yako iko wapi, sele, tafadhali nimeangalia mpaka usajili laini yako umeandika “sele sele sele” yaani majina yote matatu ni sele tu,” esta alizidi kumbananisha Sele
Sasa Sele machozi yalikua yanamelenga lenga tayari kabisa kutoka
Lakini alijikaza kiume na kuuondoa mkono wa Esta,
“kwanini nikueleze hayo yote Esta kwanini?” aling’aka sele
“ah kwasababu, ah kwasababu.. nimekupenda Sele” alimalizia Esta huku akisimama na kuweka mikono mdomoni kama mtu aliyesema jamboa ambalo hakutakiwa kusema,
Sele alipigwa na mshangao sasa , ndio hata yeye alishikwa na bumbuwazi na kujikuta sasa anatamani kuona kama yuko ndotoni ili aamke kutoka usingizini
“Esta wewe ni mwanamke pekee ambaye umeyabadili maisha yangu na nakupenda pia, lakini kuhusu historia Yangu, mimi ni nani nisingependa kukueleza Esta, kwakuwa inaniumiza mimi mwenyewe na itakuumiza wewe pia lakini kukueleza wewe ni hatari zaidi ya unavyofikiri wewe” alisema Sele,
“kumbukuka nimekuambia kila kitu Sele, na naapa kabisa Sele, nitatunza siri yako yoyote ile kuanzia leo hii na hata kama itakuwa ngumu kiasi gani basi siwezi kuachana na wewe Sele”
“Esta unajua wewe ni mzuri, una macho mazuri sana, lakini baada ya kusikia hayo yote hutakuwa hivi ulivyo Esta, tafadhali usitake kujua haya!’ alisema Sele kwa kumsihi sana Esta
“nakuahidi Sele usiponiambia basi hata Lindi siwezi kwenda Tena” alisema Esta
“Esta sikiliza kwa umakini, na naomba sana unisikilize nitakuambia kila kitu ila kwa masharti” alisema Sele
‘masharti yoyote Sele niko tayari” alisema Esta akikaa vizuri sasa kusikiliza hadithi ya Sele
“okay, kwanza hutamwambia mtu yoyote kwa namna yoyote ile, kwasababu yoyote ile utaendelea kuniita Sele , na hutanipigia simu popote mpaka mimi nianze kunitafuta, na hivyo hivyo kwenye meseji” alisema Sele
“hakuna shida Sele” nitaweza yote hayo
“okay sasa Esta mimi jina langu halisi ni GiFT Lukas Tupa”
Alisema akiweka kituo huku akimtazama vizuri Esta, ambaye hakuonyesha kustuka”
“narudia naitwa Gift Lukas Tupa esta” alisema tena akimwangalia Esta machoni na sasa Esta akili zake zilielewa haraka
“whaaat! Unasemaje Sele? Unataka kusema baba yako ni Mheshimiwa Lukas Tupa, the President?” aliuliza esta huku akiweka mikono mdomoni Sele alitingisha kichwa tu kukubali
“bado hadithi haijaanza Esta nilikuambia mapema !” alisema Sele sasa akimhurumia Esta
“Sele noo ,”
“okay sasa kwa mzee tuko wawili mimi na dada Yangu Doreen ambaye yeye yuko Italy ameolewa huko na alibadili kabisa na uraia, kwa ufupi iko hivi mzee Tupa alikua Mhadhiri mwandamizi pale udsm kabla hajateuliwa kuwa mbunge na Raisi aliyepita kama unakumbuka

Sasa mama yangu alikua ndio kwanza assistant lecturer pale kitengo cha sheria huko na huko akawa na mahusiano na mzee Tupa na ndio akazaliwa dada Doreen, na mimi ndio nikafuatia, mzee tupa alipoteuliwa kuwa Mbunge na hatimaye kuwa waziri wa Fedha akatupangia nyumba maeneo ya mikocheni, na mama alituambia wazi wazi kuwa mzee alikua na mke wake mkubwa na yeye alikua mke wake mdogo! Dada Doreen yeye alienda Kenya kusoma na mama akakataa mimi kwenda nje ya nchi kusoma na badala yake akasema nisome hapa hapa Tz ili niwe nae karibu” Sele aliendelea na story yake kisha akanywa maji kidogo na kuendelea
“mzee akikua anakuja kwa mwezi mara mbili, na kila siku aliyokuwa anakuja basi angeniletea zawadi mbali mbali, kiuhalisia tulikua na maisha mazuri sana”
“hata hivyo hatuweza kukutana na ndugu zetu wengine wa mama mkubwa na hatukupewa habari zao kabisa, nakumbuka kuna siku mama alisema kuwa mahusiano yao bado hajawa rasmi na endapo tungetambulishwa basi mzee angeweza kukosa kazi, na uteuzi wake ukaishia hapo kwakua ni kashfa ambayo ingeweza kumkosesha kibarua chake, unajua tena waziri haipendezi kuwa na mchepuko!” alisema Sele,
Maisha yaliendelea vizuri tu na dada Doreen akamaliza shule kule na mimi nikamaliza sekondari na nikaendelea na kidato cha tano na kumaliza vizuri kabisa kidato cha sita na kufaulu vizuri kwenye vyeti vyangu Jina langu ni Gift Jonathan Charles ambalo ndilo jina la babu yake mama, na hii ilifanyika makusudi ili k uficha ubini wangu, kumlinda mzee,
Hakukua na tatizo lolote kwani wakati ambao nilitaka kuongea na baba niliongea nae na hakuna kitu ambacho ningekosa
Nakumbuka siku hiyo nilikua najiandaa kwenda chuo kikuu majira ya saa moja usiku nilishangaa kuona gari la baba nje, nilistuka kidogo kwakuwa ilikua ni siku chache tu zimepita alikua pale,
“labda amekuja kuniaga” nilisema huku nikishuka ngazi haraka kutoka nje kumpokea baba,
Uso wake haukuwa na furaha kama siku zote lakini alionyesha bashasha,
“mama yako yupo?” alisema haraka akiingia ndani
“ndio yupo chumbani kwake” nilisema nikirudi zangu “juu” kupanga mizigo yangu kwani nilikuwa miongoni mwa wanafunzi watano tuliopata ufadhili wa masomo kusoma nje ya nchi
“mzee alipitiliza ndani huku walinzi wake wakibaki nje, namkumbuka mmoja aliitwa Joshua “
Baada ya masaa mawili hivi niliona baba akiondoka zake na mimi niliamua kushuka chini kumfuata mama na kumkuta Sebuleni analia
Sikujua hata pa kuanzia lakini mama aliniita na kuniambia yaliyojiri
“baba yako anateuliwa kuwa Raisi kwenye chama chake mwaka ujao, kutokana na ushindani uliopo kwenye Chama ni yeye na Waziri mkuu wa sasa ndio wanapewa nafasi kubwa sana hata hivyo mheshimiwa Raisi anataka kumuachia yeye kijiti”
Alisema mama
“sasa mbona unalia?” nilimuuliza mama
“iko hivi, mimi ni mchepuko tu mwanangu, mimi ni mchepukooo!” alisema kwa hasira akitupa glass ya maji sakafuni
“ah sijaelewa mama”
“iko hivi mwanangu Gift kuanzia sasa hivi baba yakao hatakuja tena hapa! Kwa ufupi hutakutana nae popote sio wewe tu lakini hata mimi pia” alisema akilia
“mama kwanini Lakini?” nilisema nikiwa sielewi
“mwanangu wewe ni msomi sasa unajua, Raisi hatakiwi kuwa na makando kando, kuanzia keshoa anaanza kufuatiliwa hata akienda chooni, anayetakiwa kuwa nae bega kwa bega ni mke wake wa ndoa” alisema mama
“naelewa mama, sasa bado nashindwa kuona kwanini unalia!’ nilisema
“leo amekuja kutupa tahadhari kuwa mkewe amejua tunapoishi hivyo tuwe makini na ikibidi tuhame kabisa hata nje ya nchi mapaka uchaguzi upite” alisema mama kwa uchungu
Sasa nilielewa uzito wa lile jambo, na sikuona namna ya kufanya, mama yangu hakuwa na ndugu tuliyeweza kumfahamu zaidi alituambia tu kuhusu baba yake ambaye alifariki alipokuwa mdogo na mama yake alifariki wakati akijifungua, na akaenda kulelewa katika kituo cha watoto Yatima cha Samaritan Morogoro ambapo alisomeshwa na wamisionari mpaka alipofika UDSM na kukutana na baba yangu,
Hata hivyo kwa macho na kwa vitendo baba yangu alinipenda sana na alimpenda mama yangu pia alishamfungulia miradi mikubwa sana na kumuachia pesa nyingi kabla ya uchaguzi na alimuahidi kuwa nae bega kwa bega
Wakati naondoka pale sebuleni mama alinipa barua ambayo ilikua imetoka kwa mzee
 
MPANGAJI 6
Niliichukua haraka na kuisoma aliniambia tu ananipenda sana na hana jinsi kwani majukumu ya nchi yalikua muhimu zaidi na kwamba itachukua miaka 10 tu kisha atarudiana na sisi tena alinihakikishia kuwa hataniacha mimi pamoja na mama yangu na dada , akasema mambo mengine atanieleza mama yangu
Kwa mara ya kwanza tulikaa mezani kwa chakula mimi na mama bila kuongea chochote, kila nilivyokuwa najaribu kuwaza niliona mama yangu akiwa kwenye huzuni sana na hatimaye niliamua kurudi zangu chumbani,
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
Kesho yake asubuh mama aliongea na dada Doreen na kumtaka bakie Italy na mimi nikaamua kutokwenda tena kusoma ili nibaki na mama yangu, kwani hali ya hatari tayri ilishagonga kwenye ufahamu wangu, na hivyo nikajiunga na masomo kwa njia ya mtandao kwenye chuo cha Yale uingereza na nikaanza masomo kwa njia ya mtandao, na nikawa nashinda ndani bila kutoka nje,
Mama yangu aliendelea na kazi na baadae akahamishiwa wizara ya fedha sikujua alifanya kwenye kitengo gani ila baadae tulihama pale na kwenda kuishi Mbezi beach,
“ni kweli baada ya…” sele alikatishwa na sauti ya mhudumu aliyekuja kuchukua vyombo na kisha akachukua oda ya chakula cha mchana
“aisee mimi nitakula ugali wa dona na samaki” alisema Sele
“mimi wali kuku” alisema Esta
‘ehh tuendelee sele, ujue kama naangalia Tamthilia Fulani hivi ya kituruki” alisema Esta
“so mzee kweli akapitishwa kwenye chama chake kuwa mgombea Uraisi na kama ujuavyo nchi yetu mtu akishapita kwenye chama tawala ndio anakuwa Raisi huyo Basi mzee akaanza kuzunguuka na kupiga kampeni nchi nzima kampeni zilinoga sana na nilikua nafuatilia sana nikiwa nyumbani na kwa mara ya kwanza ndio nikamuona mke mkubwa wa Mzee pamoja na watoto wake wawili wa kike wote Jesca Na Joan, na ni huyo Jesca alikuwa anafanana na dada Doreen,
Niliendelea kuwasiliana na dada Doreen na yeye alikua akifuatilia sana kampeni na sisi sote pamoja na mama tulikua tunamuombea sana baba achaguliwe, nakumbuka kuna siku tulifunga siku mbili tukimuombea baba ashinde uchaguzi ule

Nakumbuka siku moja usiku dada Doreen alinipigia huku akisema ni jambo la muhimu ilibidi lifanyike usiku huo huo
“niliamka na kuwasha taa ilikua ni saa 8 usiku, na kabla sijamaliza kuongea nae mama nae alikuja na kunigongea, nilivaa tisheti na kutoka nje,
“futa picha zako zote mtandaoni hata kama kuna mtu ulimtag , sijui ulimtumia delete haraka iwezekanvyo na kuna mtu wa IT anakuja sasa hivi kukusaidia anza kufuta”
Alisema mama huku akishuka chini
“ndio mdogo wangu jitoe pia kwenye magroup, nakuambia jitoe” alikua anasisitiza dada Doreen sikuwa na jinsi nilingia kwenye akaunti zangu na kufuta picha zangu za mama na kila mtu,
Ni kweli baada ya muda alikuja kijana akiwa na laptop ndogo kila baada ya dakika moja mzee alikua akimpigia kuwa afanye kazi haraka
“mzee nipe muda ukinipigia kila dakika nashindwa mkuu, niamini nipe nusu saa” alisema Yule kijana hukua akiwa tayari ameshaingia hofu
“dogo kuwa Raisi wa nchi sio mchezo, mimi tangu juzi sijalala” alisema Yule jamaa huku akibonyeza lap top yake kama umeme
“lete simu yako” alisema kisha akatoa usb na kuichomeka,
“mama nipe ya kwako pia” alisema mama nae akampa
Akaendelea kubonyeza bonyeza kisha akaniagiza maji ya kunywa
Baada ya dakika ishirini alituruhusu kuchukua simu zetu,
“sasa mama kwasasa msitumie mtandao wowote , yaani mnaweza kuingia, lakini huruhusiwi kufungua akaunti, kukoment, wala kulike chochote, hata kwa kutumia akaunti fake” alisema huku akifunga begi lake na kuondoka
“hata whatsap?” niliuliza
“aisee dogo tena kama upo kwenye group hata la kwaya ya kanisani kwenu jitoe na ikibidi usitumie kabisa,” alisema akiondoka
“sasa sisi tumekosa nini?’ mama aliuliza hakukua na majibu
Sikuwa na majibu kwa usiku ule lakini kulikua na jambo kubwa ambalo sikulifahamu kwa wakati ule, kesho yake asubuhi mama aliniita na kuniambia mambo mengi sana ambayo sikuyafahamu,

Mama alisema kuwa Yule mama Joan alimlazimisha mlinzi mmojawapo wa baba kwa kutishia kumharibia kazi kwa mzee hivyo akamueleza mama mkubwa kuhusu mahali tunapopatikana ikiwemo na sura zetu, na yule mama alimueleza mumewe kuwa ameshafahamu mchepuko wake na hivyo atadili nayo ili kuhakikisha hakuna wa kumzuia yeye kuwa first lady mama alisema
Kwa jinsi alivyobadili maneno Yule mwanamke baba yako hataki kuniona tena! Mama alisema huku machozi yakimtoka
“baba yako amenipigia simu asubuhi kwa uhalisia hakunipigia mimi ila alituma mtu asubuhi asubuhi nikatumia simu yake, anasema kwamba mimi nataka kumharibia safari yake ya ikulu kwasababu nimemfuata mke wake mama Joan na kumwambia mimi nimezaa na Mzee Tuppa kitu ambacho sio kweli nimejaribu kujiteteta lakini baba yako hanielewi kabisa hata hivyo
Kuna kitu kibaya kabisa naona kinataka kutokea yaani mama,
Sikiliza kuanzia sasa hivi uwe makini sana na sitapenda kukuona hata nje ya hapo sijui kucheza basket sijui nini, hapa nataka ninunue mahitaji ya mwezi mzima nenda huko juu ujisomee mpaka uchaguzi huu upite.
Mama hakuishia hapo siku hiyo kwa siri sana aliwaleta watu kadhaa pale nyumbani wakanipiga picha na kuchuka alama za vidole na kisha wakaondoka, kesho yake asubuhi nikaletewa bahasha ambayo ilikua ina passport kadi ya kilinki, cheti cha kuzaliwa, kadi ya kupigia kura, kadi ya NIDA na vyote vilikua na majina ya SELE SELEMAN SELE,
Nilijaribu kukataa lakini mama akanielewesha
“this is for your own sake!” nakumbuka mama aliniambia , na siku zote mama alikua akitumia neno la kingereza katika mazungumzo basi alikua anamaanisha anachosema
Mama alinikabidhi rasmi miradi yake yote chini ya jina la Sele , na ndani ya muda mfupi tayari nilishajua ofisi zote za mama na tayari alishanifungulia akaunti binafsi ya jina langu jipya
Kwanza nilidhani mama anachukua tahadhari tu kumbe kulikua na jambo lililokuwa nyuma ya pazia
Kama bahati ilikua upande wetu dada yangu Doreen alipata mchumba huko huko Italy na wakafunga ndoa ,
Kwa usalama wetu Binafsi na bila hata kumuambia mama nilifunga camera kwa siri Sebuleni na nikatega na kinasa sauti pembeni ya camera iyo ambayo niliweka kwenye saa ya ukutani kisha nikaweka settings Fulani ili picha na videos ziende kwenye email yangu,
Zilikua zimebaki siku tatu zimebaki kabla ya uchaguzi mkuu na tayari mzee alikua anaongoza kwa kura za maoni katika mitandao ya kijamii na makundi mbali mbali,
Mwanasiasa wa chama cha upinzani bwana Rashidi Isihaka alikuwa akihojiwa na kituo kimojawapo cha televisheni alisema kuwa
“hatuwez kumchagua Raisi fuksa mwenye michepuko’ Esta alidakia
“ooh kumbe unakumbuka! Ndio pale aliulizwa ana ushahidi gani akasema Baba yaani mzee Tuppa aulizwe na akibisha yeye ataweka wazi watoto wawili wa kando wa Raisi huyo mtarajiwa”
Wakati tunaangalia habari hiyo mama yangu alishikwa na presha ghafla na sikuwa na namna nikampigia daktari wake kisha ambaye alisema atachukua nusu saa kufika, alinielekeza dawa za kumpa haraka , ni kweli baada ya dakika 26 hivi daktari alifika na wakati wakati anamhudumia akanielekeza niende duka la dawa kuna dawa Fulani nikaichukue,
Mbezi beach kama ujuavyo nyumba nyingi zina uzio na kuyapata maduka ya dawa ilibidi kuzunguuka sana , hivyo nilitoka haraka na kuingia kwenye gari la dokta na kuwasha kurudi mjini, nilizunguuka na kila duka waliniambia iyo dawa hawana, mwishowe nilifka kwenye duka moja huyo dada akaniambia kuna dokta mmoja anayo hiyo dawa akampigia,
Basi wakati anaongea nae kwani tayari nishatumia masaa mawili niliamua kumpigia dokta ili niulize habari ya mama lakini simu haikupokelewa, nikampigia mama simu yake nae ikawa inaita tu, na mwishowe nikaamua kumpigia dada wa kazi nae simu yake iliita tu, nikampigia mlinzi nae simu yake haikupokelewa, basi sikuchukua tena dawa nikarudi kwenye gari haraka kurudi nyumbani na wakati nakaribia nikaona moshi mwingi umetanda na polisi wamejaa kuzunguuka nyumba yetu nilisogea lakini akili yangu iliniambia sikutakiwa kuwepo eneo hilo kabisa hivyo nilisogea zaidi kisha nilipokuwa umbali wa kabisa nilishuhudia maiti zikitolewa kutoka ndani ya nyumba yetu na kupakiwa kwenye gari ya polisi
Nilichanganyikiwa na kuanza kuendesha gari hovyo bila kujua niendapo, ilikua ni saa sita kasoro usiku nilifika sehemu na kuegesha gari kisha nikaanza kutembea kwa miguu bila mara ghafla nikakumbuka simu yangu, haraka nirudi kwenye gari na kuichukua kisha nikaingia kwenye email yangu n akufungua kuangalia video za ile camera niliyotega
Sasa sele alikua ameshindwa kuvumilia machozi mengi yalikuwa yakimtoka
 
Duuuh. We jamaa ni moto, hongera sana kwa hadithi zako,zina mtiririko mzuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…