MPANGAJI 05
Sasa Esta alitafuta namna ya kuanza mazungumzo yake yale aliyoyaita rasmi,
Aliweka komputa pembeni na kisha akamsogelea Sele pale kwenye sofa na kumshika bega,
“Sele, naomba kwanza nisamehe sana ila sina namna nyingine isipokuwa hii” alisema akianza
Alimsimulia Sele kuhusu historia yake ya maisha, elimu yake na mapenzi na kisha akamsimulia kuhusu mama Mwajuma na hadithi nyingine ambazo hakuona umuhimu wa kuzificha
“ mama Alikuja kutafuta maisha Dar miaka wakati huo aliniacha na bibi, kwa uhalisi mama alipata ujauzito akiwa darasa la saba, na mara baada ya kujifungua na mimi kuacha kunyonya ndio akaja huku Dar, alikuwa kila mwaka anakuja na kuniletea nguo na pesa za matumizi na hatimaye nikamaliza darasa la saba na kuchaguliwa kidato cha kwanza, wakati nikiwa likizo mwezi wa sita nakumbuka mama alikuja kijijini kwetu Moro goro akiwa na mtoto mwingine mdogo akasema anaitwa Mwajuma na ndio mama akatutambulisha rasmi kuwa ameolewa na mwanaume muislamu na kuamua kubadili na yeye” alisema Esta,
“kuna kitu nakiona kwako Sele, nilivyokuja nilisikia habari nyingi sana kuhusu wewe ndio maana hata siku ile nikasubiri kuonana na wewe , nimeona unahitaji msaada Sele ,na mimi ndio wa kukupa huo msaada Sele, tafadhali kama ulikua huna imani na mimi naomba sana uniamini, naomba sana Sele, naahidi kukutunzia siri yako yote kabisa utakayoniambia kuna kitu naona kabisa hakiko sawa Sele na mbaya zaidi hata wewe mwenyewe huna furaha na maisha haya unayoishi!” alisema Esta sasa na machozi yakaanza kumtoka
“tafadhali niambie sele, wewe ni nani hasa, umetokea wapi na familia yako iko wapi, sele, tafadhali nimeangalia mpaka usajili laini yako umeandika “sele sele sele” yaani majina yote matatu ni sele tu,” esta alizidi kumbananisha Sele
Sasa Sele machozi yalikua yanamelenga lenga tayari kabisa kutoka
Lakini alijikaza kiume na kuuondoa mkono wa Esta,
“kwanini nikueleze hayo yote Esta kwanini?” aling’aka sele
“ah kwasababu, ah kwasababu.. nimekupenda Sele” alimalizia Esta huku akisimama na kuweka mikono mdomoni kama mtu aliyesema jamboa ambalo hakutakiwa kusema,
Sele alipigwa na mshangao sasa , ndio hata yeye alishikwa na bumbuwazi na kujikuta sasa anatamani kuona kama yuko ndotoni ili aamke kutoka usingizini
“Esta wewe ni mwanamke pekee ambaye umeyabadili maisha yangu na nakupenda pia, lakini kuhusu historia Yangu, mimi ni nani nisingependa kukueleza Esta, kwakuwa inaniumiza mimi mwenyewe na itakuumiza wewe pia lakini kukueleza wewe ni hatari zaidi ya unavyofikiri wewe” alisema Sele,
“kumbukuka nimekuambia kila kitu Sele, na naapa kabisa Sele, nitatunza siri yako yoyote ile kuanzia leo hii na hata kama itakuwa ngumu kiasi gani basi siwezi kuachana na wewe Sele”
“Esta unajua wewe ni mzuri, una macho mazuri sana, lakini baada ya kusikia hayo yote hutakuwa hivi ulivyo Esta, tafadhali usitake kujua haya!’ alisema Sele kwa kumsihi sana Esta
“nakuahidi Sele usiponiambia basi hata Lindi siwezi kwenda Tena” alisema Esta
“Esta sikiliza kwa umakini, na naomba sana unisikilize nitakuambia kila kitu ila kwa masharti” alisema Sele
‘masharti yoyote Sele niko tayari” alisema Esta akikaa vizuri sasa kusikiliza hadithi ya Sele
“okay, kwanza hutamwambia mtu yoyote kwa namna yoyote ile, kwasababu yoyote ile utaendelea kuniita Sele , na hutanipigia simu popote mpaka mimi nianze kunitafuta, na hivyo hivyo kwenye meseji” alisema Sele
“hakuna shida Sele” nitaweza yote hayo
“okay sasa Esta mimi jina langu halisi ni GiFT Lukas Tupa”
Alisema akiweka kituo huku akimtazama vizuri Esta, ambaye hakuonyesha kustuka”
“narudia naitwa Gift Lukas Tupa esta” alisema tena akimwangalia Esta machoni na sasa Esta akili zake zilielewa haraka
“whaaat! Unasemaje Sele? Unataka kusema baba yako ni Mheshimiwa Lukas Tupa, the President?” aliuliza esta huku akiweka mikono mdomoni Sele alitingisha kichwa tu kukubali
“bado hadithi haijaanza Esta nilikuambia mapema !” alisema Sele sasa akimhurumia Esta
“Sele noo ,”
“okay sasa kwa mzee tuko wawili mimi na dada Yangu Doreen ambaye yeye yuko Italy ameolewa huko na alibadili kabisa na uraia, kwa ufupi iko hivi mzee Tupa alikua Mhadhiri mwandamizi pale udsm kabla hajateuliwa kuwa mbunge na Raisi aliyepita kama unakumbuka
Sasa mama yangu alikua ndio kwanza assistant lecturer pale kitengo cha sheria huko na huko akawa na mahusiano na mzee Tupa na ndio akazaliwa dada Doreen, na mimi ndio nikafuatia, mzee tupa alipoteuliwa kuwa Mbunge na hatimaye kuwa waziri wa Fedha akatupangia nyumba maeneo ya mikocheni, na mama alituambia wazi wazi kuwa mzee alikua na mke wake mkubwa na yeye alikua mke wake mdogo! Dada Doreen yeye alienda Kenya kusoma na mama akakataa mimi kwenda nje ya nchi kusoma na badala yake akasema nisome hapa hapa Tz ili niwe nae karibu” Sele aliendelea na story yake kisha akanywa maji kidogo na kuendelea
“mzee akikua anakuja kwa mwezi mara mbili, na kila siku aliyokuwa anakuja basi angeniletea zawadi mbali mbali, kiuhalisia tulikua na maisha mazuri sana”
“hata hivyo hatuweza kukutana na ndugu zetu wengine wa mama mkubwa na hatukupewa habari zao kabisa, nakumbuka kuna siku mama alisema kuwa mahusiano yao bado hajawa rasmi na endapo tungetambulishwa basi mzee angeweza kukosa kazi, na uteuzi wake ukaishia hapo kwakua ni kashfa ambayo ingeweza kumkosesha kibarua chake, unajua tena waziri haipendezi kuwa na mchepuko!” alisema Sele,
Maisha yaliendelea vizuri tu na dada Doreen akamaliza shule kule na mimi nikamaliza sekondari na nikaendelea na kidato cha tano na kumaliza vizuri kabisa kidato cha sita na kufaulu vizuri kwenye vyeti vyangu Jina langu ni Gift Jonathan Charles ambalo ndilo jina la babu yake mama, na hii ilifanyika makusudi ili k uficha ubini wangu, kumlinda mzee,
Hakukua na tatizo lolote kwani wakati ambao nilitaka kuongea na baba niliongea nae na hakuna kitu ambacho ningekosa
Nakumbuka siku hiyo nilikua najiandaa kwenda chuo kikuu majira ya saa moja usiku nilishangaa kuona gari la baba nje, nilistuka kidogo kwakuwa ilikua ni siku chache tu zimepita alikua pale,
“labda amekuja kuniaga” nilisema huku nikishuka ngazi haraka kutoka nje kumpokea baba,
Uso wake haukuwa na furaha kama siku zote lakini alionyesha bashasha,
“mama yako yupo?” alisema haraka akiingia ndani
“ndio yupo chumbani kwake” nilisema nikirudi zangu “juu” kupanga mizigo yangu kwani nilikuwa miongoni mwa wanafunzi watano tuliopata ufadhili wa masomo kusoma nje ya nchi
“mzee alipitiliza ndani huku walinzi wake wakibaki nje, namkumbuka mmoja aliitwa Joshua “
Baada ya masaa mawili hivi niliona baba akiondoka zake na mimi niliamua kushuka chini kumfuata mama na kumkuta Sebuleni analia
Sikujua hata pa kuanzia lakini mama aliniita na kuniambia yaliyojiri
“baba yako anateuliwa kuwa Raisi kwenye chama chake mwaka ujao, kutokana na ushindani uliopo kwenye Chama ni yeye na Waziri mkuu wa sasa ndio wanapewa nafasi kubwa sana hata hivyo mheshimiwa Raisi anataka kumuachia yeye kijiti”
Alisema mama
“sasa mbona unalia?” nilimuuliza mama
“iko hivi, mimi ni mchepuko tu mwanangu, mimi ni mchepukooo!” alisema kwa hasira akitupa glass ya maji sakafuni
“ah sijaelewa mama”
“iko hivi mwanangu Gift kuanzia sasa hivi baba yakao hatakuja tena hapa! Kwa ufupi hutakutana nae popote sio wewe tu lakini hata mimi pia” alisema akilia
“mama kwanini Lakini?” nilisema nikiwa sielewi
“mwanangu wewe ni msomi sasa unajua, Raisi hatakiwi kuwa na makando kando, kuanzia keshoa anaanza kufuatiliwa hata akienda chooni, anayetakiwa kuwa nae bega kwa bega ni mke wake wa ndoa” alisema mama
“naelewa mama, sasa bado nashindwa kuona kwanini unalia!’ nilisema
“leo amekuja kutupa tahadhari kuwa mkewe amejua tunapoishi hivyo tuwe makini na ikibidi tuhame kabisa hata nje ya nchi mapaka uchaguzi upite” alisema mama kwa uchungu
Sasa nilielewa uzito wa lile jambo, na sikuona namna ya kufanya, mama yangu hakuwa na ndugu tuliyeweza kumfahamu zaidi alituambia tu kuhusu baba yake ambaye alifariki alipokuwa mdogo na mama yake alifariki wakati akijifungua, na akaenda kulelewa katika kituo cha watoto Yatima cha Samaritan Morogoro ambapo alisomeshwa na wamisionari mpaka alipofika UDSM na kukutana na baba yangu,
Hata hivyo kwa macho na kwa vitendo baba yangu alinipenda sana na alimpenda mama yangu pia alishamfungulia miradi mikubwa sana na kumuachia pesa nyingi kabla ya uchaguzi na alimuahidi kuwa nae bega kwa bega
Wakati naondoka pale sebuleni mama alinipa barua ambayo ilikua imetoka kwa mzee