Hadithi: Mpangaji

MPANGAJI 09
by CK Allan+255746 266 267

β€˜ kwa haraka anaweza kuwa anafaa ngoja tuendelee kumchunguza” alisema Mr K
β€˜Kwani mpango uko tayari?” aliuliza Sele
β€œndio , leo usiku” alisema Mr K akiondoka
β€œokay ila tafadhali asiumizwe” alisema Sele akirudi ndani
Ilipofika usiku majira ya saa Mbili Sele alimtoa esta kuwa wakatembee Mjini
β€œleo kuna Movie nzuri wanazindua kwenye Cinema hall, twende kuichek”
Alisema Sele
β€˜ooh Kwani hatuwezi kuisubiri tukaagiza hapa tukaangalia hapa nyumbani Dear” alisema Esta,
β€˜Ah tukatembee bhana hatuwezi kukaa hivi hivi tutaishia kufanya tu hapa kila dakika” alisema Sele akitangulia nje
Alienda na kutoa gari kwenye parking na kumsubiri Esta
β€œnonono ! hahaha! Umependeza sana mke wangu ila bhana kavae Suruali!” alisema Sele akimtaka akavue gauni lake
β€œhaha Sijui kama nitazoea Sele unajua tena mwalimu mimi” alisema Esta akifunga mkanda
β€œvipi mlango umefunga,”
β€œloh hata nimesahau mlango wenyewe sijajua unafungwaje!” alisema Esta
β€œunaufunga kawaida halafu ingiza 0316 iyo password
Alisema sele sasa akiwasha gari
Baada ya muda esta alirejea akitabasamu
β€œkwahiyo unaamini kabisa pale mtu hawezi kufungua!” alisema Esta
β€œhawezi dear, na mtu akikosea mara tatu, nitapata ujumbe mfupi kuwa kuna mtu anajaribu kufungua mlango β€œ alisema sele akicheka kisha akatoa gari nje wakatoka
Walienda kuangalia Cinema ambayo Esta alisema hata hakuipenda sana na kujikuta usingizi ukimnyemelea

β€œbaby hii muvi sijailewa twende zetu tukalale” alisema Esta akimlalia Sele kwenye bega
β€œokay nisubiri niende kupunguza maji kidogo” alisema Sele akinyanyuka kwenda msalani halafu baada ya muda mfupi akarudi na kumshika mkono Esta na kuondoka wakati muvi hiyo ikimalizika,
β€œmovie tamu sana ngoja nitaimalizia mtandaoni kesho” alisema Sele wakitoka,
Waliingia kwenye gari na kuondoka na wakati huo gari jingine dogo jeusi liliondoka kuwafuatilia
Wakati Sele anakatisha kuelekea barabara kuu ya mwenge lile gari lililiwapita kwa kasi na kwenda kusimama mbele yao
Sele alisimamisha gari na kufunga vioo
β€œEsta jitulize tafadhali ngoja nitoke”
β€œhapana usitoke!”
Wakatii wanabishana walishuka watu wawili wakiwa wameziba nyuso zao na kuwaonyesha ishara washuke ndani gari
Sele hakuwa na jinsi alimtoa Esta na kisha wakawekwa chini ya ulinzi na kuingizwa kwenye lile gari jeusi hakuna aliongea chochote na sasa Esta alikua analia
β€œjamani msituue sisi hatujafanya chochote” alipiga kelele
β€œmnatupeleka wapi?” aliuliza Sele
Hakuna yoyote aliyemjibu na mwishowe waliamua kuwafunga vitambaa usoni na kuwapeleka mpaka kwenye jumba moja ni kuwafungia kwenye chumba kimoja
β€œSele mpenzi upo”
β€œNipo mama! Usijali kila kitu kitakaa sawa tu” alisema Sele kwa kujiamini
Baada ya muda walikuja kutolewa na kufungwa kamba miguuni na mikononi sasa Esta alizidi kupiga kelele
β€œwe mwanamke sisi tungetaka kukuaa tungekuua toka kule hebu tuachie kelele!” mmoja wa wale jamaa alisema na sasa waliwafungua vile vitambaa usoni na kujikuta wanatazamana na mitutu ya bunduki

β€œhaya hatutaki kupotezeana muda hapa jibuni maswali yetu chap!’ alisema Yule jamaa ambaye alikua amejifunga usoni kabla zoezi halijaanza mmoja alimnon’goneza kitu mwenzake na Kisha aliwakonyeza wenzake wengine wakamkokota sele na kumpelea chumba kingine
β€œhaya mkikaa pamoja mtatuchelewesha na sio vyema kuona damu ya mpenzi wako!” alisema Yule jamaa sasa akimsogelea Esta aliyekuwa anatetemeka
β€œhaya tuambie kadi yetu iko wapi?” aliuliza Yule jamaa
β€œkadi, kadi gani mbona jamani siwaelei mmemchukua mpenzi wangu, sijui mmpeleka wapi? Na sasa mnaniuliza kadi kadi !” alisema Esta sasa akizidi kuchanganyikiwa
β€œkwahiyo jana mumeo hajaja na kadi yoyote nyumbani?”
β€œjamani jana hatujatoka kwenda popote, hajatoka kabisa na hakuna kadi yoyote anayo!” alisema Esta akizidi kutetemeka
β€œsikiliza kama unataka kumuona tena mumeo Sele basi toa ushirikiano vinginevyo hutamuona tena”
Alisema Yule jamaa
β€œhaya taja namba ya siri ya mlango”
β€œmlango upi tena jamani!”
β€œwewe usitusumbue, si umesema hujui kadi ilipo? Taja password ya mlango tukachukue wenyewe!” alisema Yule jamaa huku akimkaba shingo Esta
β€œsijui hiyo password kabisa” alisema esta akilia
β€œsasa sikiliza utaitaja hiyo password!” alisema Yule jamaa huku akimkonyeza jamaa mwingine ambaye alitoka na kisha wakarejea na Sele ambaye alionekana ameloa maji huku akihema kwa nguvu
β€œtaja password ya mlango au tumuue mumeo!” alisema huku akiwa amemuelekezea bastola Sele
Esta alimtazama Sele ambaye alikua amefumba macho kama anayesikilizia maumivu
β€œSIIJUI HIYO PASSWORD” alisema Esta kwa sauti kubwa
β€œmuondoeni hapa” alisema Yule mtu na Esta akachukuliwa mpaka kwenye chumba kingine ambacho kilikua na meza na viti viwili kisha baada ya muda akaingia mtu mmoja mzee hivi akiwa amevaa suti moja nzuri sana,
β€œsikiliza binti yangu mimi ni Afisa upelelezi, alisema akitoa β€œkitambulisho” chake kumuonyesha Esta,
β€œlakini hapa sio polisi, ninyi ni watekaji kabisa, watekaji wazoefu!’ alisema Esta kwa ukali
β€œmpenzi wako akishirikiana na wenzake wameiba kadi muhimu ambayo inaweza kuhatarisha usalama wa nchi yetu, najua wewe ni mwalimu Mwanangu unatakiwa kuwa mzalendo, tuambie yote unayofahamu kuhusu huyu mtu anaitwa Sele, majina yake kamili na chochote kingine unachokijua,
Sikiliza vijana wangu walitaka kutumia nguvu lakini mimi nataka kukuhakikishia kuwa ukishirikiana na sisi vizuri ipo hapa pesa nzuri unaondoka nayo na sisi tutakupa ulinzi wote ikiwemo kukubadilishia mazingira ya kazi yako na kukupa kazi nzuri zaidi” alisema Yule mzee akimkonyeza mtu mmoja wa pembeni ambaye aliinua briefcase moja na kuiweka mezani kisha akaifungua
β€œhizi ni million 20 cash, na tutakuhamishia wizarani baada ya muda mfupi endapo tu utatupa ushirikiano wako”
Esta alitazama zile Pesa kisha akasema
β€œmzee haijalishi wewe ni polisi, kachero au ni nani lakini mimi sijui chochote, na kuhusu password ya mlango mimi sijawahi hata kufika huko nyumbani kwa Sele huwa tunakutana lodge tu!” Esta aliongea kwa ujasari mpaka Yule mzee alitamani kucheka na kupiga makofi
Upande wa pili Sele alikua akishudia na kusikia kila kitu
β€œAsante Mungu”
alijipiga kifuani akifurahi kuona Esta amefaulu mtihani ule vizuri kabisa
baada ya zoezi kukwama Yule Mzee alitoka na watu wake na kumuacha Esta akiwa analia Pale sakafuni, bila kupoteza Muda Alisikia purukushani huko nje na milio ya Risasi na mlango ukapigwa teke na kufunguka
Esta alijua sasa maisha yake yalifika ukingoni lakini alipigwa na mshangao kuona polisi wawili ambao walimsaidia kusimama huku wakimtuliza na kutoka nae nje
 
MPANGAJI 10

By CK Allan 0746 266 267


Nje ya mlango alikuta wale jamaa wakiwa chini ya ulinzi mkali wa β€œPOLISI” Sele nae alikua amesimama alipomuona Esta alimkimbilia kwa furaha na kumkumbatia huku machozi yakimtoka hakuamini kuwa Esta angeweza kumpenda na kumlinda kiasi hicho
β€œvipi umeumia?” Sele aliluliza
β€œHapana mpenzi wewe je wamekuumiza?” alisema Esta akimkagua kagua Sele
β€œhapana niko fresh tuwahi nyumbani” alisema Sele akimvuta Esta nje na kukuta polisi mmoja akiwasubiri
β€œgari lako liko salama nitawasindikiza mpaka mnapoishi na kesho mtakuja kuandika maelezo poleni sana na wote waliohusika tumewakamata” alisema Yule polisi sasa akiwasha gari kuwapeleka akina Sele nyumbani
Sele alitamani kucheka kwani hakujua kama wenzake wangecheza mchezo wa hatari kiasi hiki,
β€œyaani hawa wajinga mpaka Sare za Polisi!” aliwaza sasa akimkumbatia Esta kurudi kwao Mbweni
Walifika majira ya saa 8 na nusu usiku baada ya kuoga walienda kulala kutokana na uchovu mwingi hakuna aliyemsemesha mwenzake mpaka kesho yake asubuhi walipokuwa wakipata kifungua kinywa kwa namna Fulani Sele aliona aibu kumuangalia usoni Esta
β€œPole kwa masaibu ya jana” alianza Sele
β€œmh pole na wewe!” alisema Esta
β€œlakini Sele kuna kitu labda umenificha? Hiyo kadi ni kadi gani hivi mpaka watu watake kunitoa roho mie?” aliuliza Esta
β€œhakuna kadi yoyote ni mchezo tu esta ulikua unachezewa” alijisemea kimoyo moyo Sele
β€œkwakweli hata mimi sijui, hakuna kadi yoyote ambayo ninayo, na niliwaambia sina kadi yoyote!”
β€œSele kumbuka nilishakuahidi kuwa nitakuwa na wewe bega kwa bega , na siwezi kukusaliti sele tafadhali niambie kama kuna jambo lolote unanificha jamani!’ alisema Esta
β€œhakuna Esta nilishakuambia kila kitu” alisema huku akimvuta Esta na kuelekea nae chumbani
Alifika na kufungua kabati lake na kutoa sanduku dogo
Alifungua na kutoa baadhi ya picha na vitu vingine
β€œhuyu ndie mama yangu, na huyu hapa kwenye picha ni mimi na Baba, na huyu pembeni hapa ni dada Doreen” alisema huku akimuonyeshea picha mbali mbali Esta sasa alikijuta machozi yakimtoka
β€œhakuna mtu alishawahi kuona hizi picha Esta, ndio maana kipindi chote nilichoishi pale hakuna mtu aliwahi kuingia chumbani kwangu, sikutaka mtu yoyote kwa bahati mbaya au nzuri aone hizi picha Esta, lakini kwakuwa nakuamini wewe sina mashaka na wewe Esta” alisema Sele huku akirudisha vitu vyake vizuri’
β€œHivi laptop yako unayo eeh” alisema Sele
β€œyeah siwezi kuiacha D , yaani kila nilipokuwa nikiitumia nakukumbuka wewe tu!”
Alisema akimtolea kwenye begi
β€œPassword ngapi ngapi vile” aliuliza Sele
β€œandika β€˜esgift16’ herufi ndogo
β€œmh haya bhana” alisema Sele akimalizia kufungua ile laptop aliunga mtandao kisha akaweka program kadhaa hivi kisha akasubiri muda ufike,
Majira ya saa 12 jioni sasa alirudi chumbani na kuwasha taa na kuweka mazingira mazuri na kuweka ile laptop mezani kisha akarudi sebuleni kumuita Esta
β€œleo kuna mtu nataka uongee nae leo!” alisema Sele akimvuta mkono kueleka chumbani
Alibonyeza bonyeza ile laptop kisha wakawa wanajitazama kwenye kioo chake na baada ya muda mfupi ikaunganishwa na Sele akamuweka pembeni kidogo Esta
β€œdada, kwema huko?”
β€œhuku kwema naona mazingira , usiniambie uko lodge tena !”
β€œhaapana dada kwasasa niko mbweni”
β€œwaooh hongera sana mbona kama una furaha sana leo?”
β€œndio nina Saprise yak oleo angalia’ alisema sasa akimvuta esta karibu na ile laptop
β€œweeee! Wifi yake na mtu huyo jamani, walahi nakuja Tanzania mdogo wangu!”
β€œwifi unaitwa nani?”
β€˜Esta”
β€œwifi asante sana Mungu wa mbinguni akubariki kwa kuwa na mdogo wangu, najua ulikomtoa ni mbali, nafahamu unajua changamoto yake, usichoke endelea kumpenda, mimi naandaa ratiba yangu kazini, nitaomba likizo fupi nakuja wifi yangu usiondoke hapo!” alisema Doreen Esta alikua anaitikia tu sasa huku nae akiwa amejawa na furaha
β€œhaya nitachukua namba yako ya whatsapp’ tuatachati kwa uhuru zaidi
β€˜dada huyu ndio Esta, ni mwalimu”
Alisema Sele sasa akiwa amemkumbatia Esta.

Baada ya siku kadhaa sasa Esta alienda kwa mama Mwajuma na Sele hakuonekana tena pale aliwajulisha wapangaji wenzake kuwa amesafiri kikazi lakini hata hivyo Esta aliufahamu ukweli wote, wakati mwingine walikua wakimsema Vibaya Sele basi Esta alicheka tu huku akiwaambia Sele anaweza kutokea muda wowote na kuwashtaki
Siku hiyo jioni mama Mwajuma alipokea ugeni wa mzee mhina, Ephraim na mzee mwingine ambaye hakumtambua, baada ya kujitambulisha walisema kwamba wameleta barua ya Posa
β€œmnanichanganya mjue, sasa huyu mwanangu hapa ana wiki moja tu, nyie mmejuaje kuwa anahitaji mchumba, kwanza mmemuona wapi!” aliuliza mama Mwajuma
β€œkijana wetu na binti yako wanajuana mama Mwajuma na ni yeye aliyetutuma” alisema Yule mzee mwingine akitoa barua ya posa, Mzee mhina na Epharaim walitabasamu tuu wakati mama Mwajuma akipokea ile barua na kupigwa na butwaa kuwa ilitoka kwa Sele!
β€œkweli haya ni maajabu, yaani Sele huyu huyu, Sele huyu nimjuae mimi amuoe Binti yangu?” mama mwajuma alianza kumaindi
β€˜mama nilishasema Vijana hawa tayari wanajuana wanapendana wewe wape Baraka zako tu!” alisema Yule mzee
β€œkwanza wewe ni nani?’
β€œmimi naitwa Mr kibwana, ni baba yake mdogo na Sele”
Alisema Yule mzee akiweka miwani yake vizuri, mama mwajuma alimuita Esta na kumuleza kuhusu ujio wa wale wageni
β€œmama kiukweli mimi nampenda sana Sele” alisema Esta
β€œunampenda unamjua?”
β€˜nakuuliza wewe unamjua mpaka umpende?” alisema mama mwajuma
β€œmama waruhusu wageni waondoke mama” alisema Esta akiondoka
Mama mwajuma aliiwataka warudi baada ya wiki moja kuchukua majibu ya barua yao
β€œhuyu Binti bibi yake ambaye ndie mlezi wake yuko huko Morogoro kwahiyo nitaongea nae njooni baada ya wiki moja!” alisema mama Mwajuma
Baada ya wageni kuondoka sasa mama mwajuma aliwaita mashoga zake na kuanza kumsimanga Sele, mpaka Esta ilibidi kuingilia kati na kumuita mama yake pembeni
β€œmama sio vizuri kumuita Sele sijui Zimwi, Jini, sijui jambazi, humjui Sele wewe na ipo siku utaona aibu mama, na kumbuka maneno yako hayo hayawezi kubadili chochote yaani” alisema Esta
Mama mwajuma aliona aibu na kurudi ndani kukaa
β€œsasa mwanangu utaishije, utakula nini, Sele Yule ana kazi ya maana kweli ya kukutunza wewe? Huko shule umekosa hata mwalimu mwenzako kweli? Na usomi wako mwanangu unaenda kwa sele kweli?’ aliuliza mama Mwajuma
β€œmama maisha yananzia chini kikubwa ni amani ya moyo” alisema Esta sasa akiendelea na kazi zake
Hata hivyo Sele alifuata hatua zote alienda Rasmi kujitambulisha kwa mama Mwajuma kisha yeye na Esta wakaenda Morogoro kwa bibi yake ambaye alifurahi kuona mjukuu wake anapata mume
Baada ya wiki chache sasa Esta alihamia moja kwa moja kwa Sele na baada ya kushauriana aliamua kuacha kazi ya ualimu na kuhamia rasmi Dar ili kufanikisha lengo lao
 
"MPANGAJI 01
Hakuna mpangaji yoyote ambaye alikuwa anafahamu asili ya Yule mpangaji mwenzao, hata jina lake la β€˜sele’ wapo waliosema halikua jina lake halisi, lakini yote kwa yote Sele kama unavyoweza kusema alikua mpangaji wa kudumu wa mzee Mhina, miaka ilikatika na sio mzee Mhina wala wapangaji ama watoto wake walijua kazi halisi ya Sele,
Wapo waliosema sele alijihusisha na kazi ya kuzibua vyoo huko mjini mbali na hapo, wengine walisema sele Alikuwa mtu wa β€˜kitengo” na kama ilivyo kawaida ya wabongo basi wengine walizua kuwa sele ni jahili mzoefu,
Kwanza Sele asingetoka nje ya chumba chake bila kuitwa, na kwakuwa chumba chake kilikua ni selfu basi huwezi kujua kama sele yupo ndani au ametoka,"


Nimekumbuka Mwanzo wa story ya Bigi ya Steve.....


Naweka kambi rasmi hapaa!!

Wapii Tayukwa Lovelovie Bantu Lady Kalpana baby zu Kigi Makasi Tyrone Kaijage mmash Restless Hustler Unforgettable Mafian cartel mtzmweusi mshaisoma hii storee???
 
Narudia tena kumuita Bantu Lady Firdaus9 baby zu Johnnie Walker
Na wengine wengi
Wapi Half american DeepPond
 
"β€˜wewe ni mzee Lota, una watoto wanne , watatu wa kike na mdogo wa mwisho wa kiume, Yule ni Aisha na mumewe Mkude, Yule ni mama Mama Mwajuma na mume wake Ngoda, pale ni Isa , kule ni John na hapa ni kaka Ephraim na mke wake mama Joan’"


Sele nyookkoo

Pozi lazima ziliwaisha hapa

Aaliyyah kuna story ya Sele hukuu!!
 
"Sele alikua anakutana na wasichana wengi kila siku, na hata hapo walikuja wapangaji wengi tu wa kike na kuondoka lakini haijawahi kutokea msichana aliyeubamba moyo wake kama ilivyokuwa kwa Ester,"



Kumekuchaaaaaaaaaaa hapaaaa!!
Ngoja niendelee kusoma kwanza πŸ™‡
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…