MPANGAJI 10
By CK Allan 0746 266 267
Nje ya mlango alikuta wale jamaa wakiwa chini ya ulinzi mkali wa “POLISI” Sele nae alikua amesimama alipomuona Esta alimkimbilia kwa furaha na kumkumbatia huku machozi yakimtoka hakuamini kuwa Esta angeweza kumpenda na kumlinda kiasi hicho
“vipi umeumia?” Sele aliluliza
“Hapana mpenzi wewe je wamekuumiza?” alisema Esta akimkagua kagua Sele
“hapana niko fresh tuwahi nyumbani” alisema Sele akimvuta Esta nje na kukuta polisi mmoja akiwasubiri
“gari lako liko salama nitawasindikiza mpaka mnapoishi na kesho mtakuja kuandika maelezo poleni sana na wote waliohusika tumewakamata” alisema Yule polisi sasa akiwasha gari kuwapeleka akina Sele nyumbani
Sele alitamani kucheka kwani hakujua kama wenzake wangecheza mchezo wa hatari kiasi hiki,
“yaani hawa wajinga mpaka Sare za Polisi!” aliwaza sasa akimkumbatia Esta kurudi kwao Mbweni
Walifika majira ya saa 8 na nusu usiku baada ya kuoga walienda kulala kutokana na uchovu mwingi hakuna aliyemsemesha mwenzake mpaka kesho yake asubuhi walipokuwa wakipata kifungua kinywa kwa namna Fulani Sele aliona aibu kumuangalia usoni Esta
“Pole kwa masaibu ya jana” alianza Sele
“mh pole na wewe!” alisema Esta
“lakini Sele kuna kitu labda umenificha? Hiyo kadi ni kadi gani hivi mpaka watu watake kunitoa roho mie?” aliuliza Esta
“hakuna kadi yoyote ni mchezo tu esta ulikua unachezewa” alijisemea kimoyo moyo Sele
“kwakweli hata mimi sijui, hakuna kadi yoyote ambayo ninayo, na niliwaambia sina kadi yoyote!”
“Sele kumbuka nilishakuahidi kuwa nitakuwa na wewe bega kwa bega , na siwezi kukusaliti sele tafadhali niambie kama kuna jambo lolote unanificha jamani!’ alisema Esta
“hakuna Esta nilishakuambia kila kitu” alisema huku akimvuta Esta na kuelekea nae chumbani
Alifika na kufungua kabati lake na kutoa sanduku dogo
Alifungua na kutoa baadhi ya picha na vitu vingine
“huyu ndie mama yangu, na huyu hapa kwenye picha ni mimi na Baba, na huyu pembeni hapa ni dada Doreen” alisema huku akimuonyeshea picha mbali mbali Esta sasa alikijuta machozi yakimtoka
“hakuna mtu alishawahi kuona hizi picha Esta, ndio maana kipindi chote nilichoishi pale hakuna mtu aliwahi kuingia chumbani kwangu, sikutaka mtu yoyote kwa bahati mbaya au nzuri aone hizi picha Esta, lakini kwakuwa nakuamini wewe sina mashaka na wewe Esta” alisema Sele huku akirudisha vitu vyake vizuri’
“Hivi laptop yako unayo eeh” alisema Sele
“yeah siwezi kuiacha D , yaani kila nilipokuwa nikiitumia nakukumbuka wewe tu!”
Alisema akimtolea kwenye begi
“Password ngapi ngapi vile” aliuliza Sele
“andika ‘esgift16’ herufi ndogo
“mh haya bhana” alisema Sele akimalizia kufungua ile laptop aliunga mtandao kisha akaweka program kadhaa hivi kisha akasubiri muda ufike,
Majira ya saa 12 jioni sasa alirudi chumbani na kuwasha taa na kuweka mazingira mazuri na kuweka ile laptop mezani kisha akarudi sebuleni kumuita Esta
“leo kuna mtu nataka uongee nae leo!” alisema Sele akimvuta mkono kueleka chumbani
Alibonyeza bonyeza ile laptop kisha wakawa wanajitazama kwenye kioo chake na baada ya muda mfupi ikaunganishwa na Sele akamuweka pembeni kidogo Esta
“dada, kwema huko?”
“huku kwema naona mazingira , usiniambie uko lodge tena !”
“haapana dada kwasasa niko mbweni”
“waooh hongera sana mbona kama una furaha sana leo?”
“ndio nina Saprise yak oleo angalia’ alisema sasa akimvuta esta karibu na ile laptop
“weeee! Wifi yake na mtu huyo jamani, walahi nakuja Tanzania mdogo wangu!”
“wifi unaitwa nani?”
‘Esta”
“wifi asante sana Mungu wa mbinguni akubariki kwa kuwa na mdogo wangu, najua ulikomtoa ni mbali, nafahamu unajua changamoto yake, usichoke endelea kumpenda, mimi naandaa ratiba yangu kazini, nitaomba likizo fupi nakuja wifi yangu usiondoke hapo!” alisema Doreen Esta alikua anaitikia tu sasa huku nae akiwa amejawa na furaha
“haya nitachukua namba yako ya whatsapp’ tuatachati kwa uhuru zaidi
‘dada huyu ndio Esta, ni mwalimu”
Alisema Sele sasa akiwa amemkumbatia Esta.
Baada ya siku kadhaa sasa Esta alienda kwa mama Mwajuma na Sele hakuonekana tena pale aliwajulisha wapangaji wenzake kuwa amesafiri kikazi lakini hata hivyo Esta aliufahamu ukweli wote, wakati mwingine walikua wakimsema Vibaya Sele basi Esta alicheka tu huku akiwaambia Sele anaweza kutokea muda wowote na kuwashtaki
Siku hiyo jioni mama Mwajuma alipokea ugeni wa mzee mhina, Ephraim na mzee mwingine ambaye hakumtambua, baada ya kujitambulisha walisema kwamba wameleta barua ya Posa
“mnanichanganya mjue, sasa huyu mwanangu hapa ana wiki moja tu, nyie mmejuaje kuwa anahitaji mchumba, kwanza mmemuona wapi!” aliuliza mama Mwajuma
“kijana wetu na binti yako wanajuana mama Mwajuma na ni yeye aliyetutuma” alisema Yule mzee mwingine akitoa barua ya posa, Mzee mhina na Epharaim walitabasamu tuu wakati mama Mwajuma akipokea ile barua na kupigwa na butwaa kuwa ilitoka kwa Sele!
“kweli haya ni maajabu, yaani Sele huyu huyu, Sele huyu nimjuae mimi amuoe Binti yangu?” mama mwajuma alianza kumaindi
‘mama nilishasema Vijana hawa tayari wanajuana wanapendana wewe wape Baraka zako tu!” alisema Yule mzee
“kwanza wewe ni nani?’
“mimi naitwa Mr kibwana, ni baba yake mdogo na Sele”
Alisema Yule mzee akiweka miwani yake vizuri, mama mwajuma alimuita Esta na kumuleza kuhusu ujio wa wale wageni
“mama kiukweli mimi nampenda sana Sele” alisema Esta
“unampenda unamjua?”
‘nakuuliza wewe unamjua mpaka umpende?” alisema mama mwajuma
“mama waruhusu wageni waondoke mama” alisema Esta akiondoka
Mama mwajuma aliiwataka warudi baada ya wiki moja kuchukua majibu ya barua yao
“huyu Binti bibi yake ambaye ndie mlezi wake yuko huko Morogoro kwahiyo nitaongea nae njooni baada ya wiki moja!” alisema mama Mwajuma
Baada ya wageni kuondoka sasa mama mwajuma aliwaita mashoga zake na kuanza kumsimanga Sele, mpaka Esta ilibidi kuingilia kati na kumuita mama yake pembeni
“mama sio vizuri kumuita Sele sijui Zimwi, Jini, sijui jambazi, humjui Sele wewe na ipo siku utaona aibu mama, na kumbuka maneno yako hayo hayawezi kubadili chochote yaani” alisema Esta
Mama mwajuma aliona aibu na kurudi ndani kukaa
“sasa mwanangu utaishije, utakula nini, Sele Yule ana kazi ya maana kweli ya kukutunza wewe? Huko shule umekosa hata mwalimu mwenzako kweli? Na usomi wako mwanangu unaenda kwa sele kweli?’ aliuliza mama Mwajuma
“mama maisha yananzia chini kikubwa ni amani ya moyo” alisema Esta sasa akiendelea na kazi zake
Hata hivyo Sele alifuata hatua zote alienda Rasmi kujitambulisha kwa mama Mwajuma kisha yeye na Esta wakaenda Morogoro kwa bibi yake ambaye alifurahi kuona mjukuu wake anapata mume
Baada ya wiki chache sasa Esta alihamia moja kwa moja kwa Sele na baada ya kushauriana aliamua kuacha kazi ya ualimu na kuhamia rasmi Dar ili kufanikisha lengo lao