Hadithi: My Soulmate

Hadithi: My Soulmate

..funguo ya gari hadi chooni...🙂 [emoji14]

Hongera boss imetulia,nyingine lini tena?
 
..funguo ya gari hadi chooni...🙂 [emoji14]

Hongera boss imetulia,nyingine lini tena?
Hhahahaahhaah Stela maskini akipata????. Leo nitpost ya 25 usicheze mbali ngoja nimalize majukumu kadhaa!
 
My soulmate .Mwenzi wa roho yangu
Sehemu ya 25.

Ni asubuhi nyingine ndani ya mji wa Arusha . Alarm ya simu ili ita na Braiton ambaye ni mfanyakazi mpya wa Kampuni ya Sambeke.
Mdada : “We mkaka amka….”. Ilisikika sauti ya binti aliekuwa amelala kitanda cha vyumba vya wageni pamoja na Braiton.
Braiton : “Unasema nini?”. Braighton alishtuka usingizini na akauliza . “Kwani leo lini!? Saivi saa ngapi?” . Huku akiendelea ku soma majira kwenye simu yake. Ndipo alipostuka kuwa amechelewa kwenda kazini.
Mdada : “Umeamkaje Mume wangu?.”. Mdada aliuliza kwa mahaba . Braiton aligeuka na kumuangalia huyo mdada kwa mshangao na madharau.
Braiton alikimbia mpaka bafuni ili kuoga. Lakin kwa sababu ya muda alifanya kujifuta na maji tu kwa sababu hakutaka kuchelewa kazini .
Mdada : “Jamani Braiton mtundu wewe yani una imba vizuri kwaya na pia unajua mambo ya kitandani . Nilidhani na wewe ni mvivu kama yule Mume wangu Muinjilisti yeye anajuaga tu kazi mjinga kabisa Yule.“
Braiton hakumtilia maaanani alicho kisema mdada Yule aliendelea ku kimbia huku na kule akikusanya vitu vyake ili aondoke.
Mdada : “Brai njoo bhana unipe ya mwisho. Jamani!” Alijaribu kumshika Braiton kwa shati lake lakini Braiton ali jitoa mikononi kwa Yule mdada na akaondoka na kufunga mlango mbio mbio mpaka kituoni atafute usafiri wa kwenda kazini.
Wakati huohuo Linah ambaye ni mmoja wapo wa wafanyakazi wapya wa kampuni ya Sambeke Inc alikua kwenye harakati za kwenda kazini.
Linah : “We mwanaume una lala mpaka saivi na huna hela!.”
Jimmy : “Sasa naamka mapema naenda wapi nadhani baadae ntaenda kanisani Bishop aliniambia leo nitahuhudumia.”
Linah : “Embu nipe elfu kumi hapo nipate ya kula leo!.”
Jimmy : “Unasema elfu kumi unakula mwenyewe au na ofisi . We jana si nlikuambia ile elfu kumi ndio nlio kuwa nayo uka ng`ang`ania ukunywe pombe!?”.
Linah : “Eeeh eeeh wewe sijakuomba mawaidha nimekuomba hela sio vingine mxxxxxheeeewww.”
Jimmy : “We una msunya nani?”. Wakati Jimmy anauliza hivyo mke wake alikuwa akiondoka kwa hasira.
Linah : “Kwaheri bhana sijui hata kwa nini najisumbua kwa ajili gani kwanza…”
Watu walianza kufika katika ofisi ya Sambeke mmoja baada ya mwingine lakini alie chelewa hiyo siku kuliko wote ni Braiton wakati anaingia ofisini . Stela alimwona aka amua kumuita pembeni.
Stela : “Habari za asubuhi?”.
Braiton : “Salama tu!. Mzima wewe?”
Stela : “Mimi mzima swali ni kwako!?”. Stela aliuliza huku akimnyooshea mkono akionesha nguo na muonekano wa Braiton.
Braiton : “Swali gani Dada?”.
Stela : “Huoni ulivyo ulivyo rafu rafu? Upo kama hukulala nyumbani kwako!.”
Braiton : “Nini kwani nipo uchi!?. Afu usinishobokeeee we secretary tu sijui umeishia la sita.”.Braiton alisema hivyo akiondoka.
Alipo ondoka akamwacha Stela akimshangaa kwa hasira yamkini hakujua kuwa Stela ni kama Boss wake maaana ndo mke wa Boss wa kampuni hiyo . Ali geuka ki unyonge akaenda kukaaa mezani kwake.
**************
Upande mwingine ndani ya nchi ya Somalia katika kambi ya M16 chini ya kiongozi wao Jenerali Bashiru .
Milango ilisikika ikigongwa na filimbi zikipigwa na milio ya risasi . Nickson alitoka kwa mshtuko akitaka kujua ni nini kinaendelea .
Nickson : “Nini nini jamani msituueee!!!!!!!!!.”.Alisema kwa sauti kali. Watu wote waligeuka waka kaa kimya na kucheka.
Bertha : “Wewe ni muda wa mazoezi usikae kishamba wewe!.”
Mchakamchaka ulianza taratibu yakifuatiwa na mazoezi mengine lakini aliekuwa legelege ni Nickson hata Bertha alikuwa sio mlegevu hivyo. Yamkini ndo mwanzo watu walisema!.
Baada ya mazoezi kuisha Nickson alionekana kuchoka kuliko wote .
Bertha : “Pole mwaya . Hahahahaahahaha”.
Nickson : “Daaah haya mazoezi hatari. ”. Nickson aliongea huku akihema juu juu.
Bertha : “Hahahaha haya mazoezi kidogo tu mbona. Haya ya kawaida sana nlikua na fanya na mume wangu Mandoto!.”
Nickson : “Kwel mazoezi ya umuhimu.”
Bertha : “Haya baaadaae!. Afu Jenerali alisema badae baada ya chai tukamwone. ”
Nickson : “Haya badae.”
Nickson alienda kuoga na alipotoka alivaaa na kuelekea kwenye sehemu ya kula ya kambi hilo. Aka chukua kifungua kinywa chake akamwona Bertha amekaa na waenyeji wa hapo . Bertha alionekana aki kaaa kwa amani na akicheka na kuwapa mikono.
Baaada ya kumaliza kula kifungua kinywa Nickson alienda na Bertha kwenye ofisi ya Jenerali wa kambi hiyo.
Jenerali : “Za asubuhi?. Je mumeamkaje?”.
Bertha na Nickson : “Salama”. Walijibu huku wakichukua viti na kukaaa.
Jenerali : “Nickson na Bertha Nimewaita leo asubuhi kuwaaambia kuhusu mpango wetu sisi. Sisi M16 hatuezi kushindwa kamwe!. Wengi wamejaribu kutupindua wameshindwa sisi ndio tulio na Somalia ndani ya mikono yetu sio umoja wa Marekani , sio umoja wa mataifa yani UN hawatuwezi kamwe.”
Nickson : “Kweli nime angalia historia yenu miaka mia na hamsini tokea mumeanza hakuna alio waweza.”
Jenerali : “Safi sana kijana una tujua vyema.”.Jenerali aliacha kuzungumza na kuwasha sigara .
Jenerali : “Tuna hitaji watu kama nyie ambao mna akili tuka wavamie tuilipue hio Banki sisi hamna alieweza tushinda tukiamua kuvamia meli tumezivamia bila kusumbuliwa sisi indo mabingwa.”
Nickson : “Mimi nitakaa chini na kupanga ramani ni ijue tuna vamia aje lakini nikishindwa kuja na mpango. Basi hatuta waunga mkono nyie ni mpaka pale nitakapo ona ipo sawa na kuridhika!”.
Bertha : “Na mimi vipi?”.
Nickson : “Wewe kuhusu nini?”.
Bertha : “Kwani nitakuwa nafanyaje?”
Nickson : “Kuhusu!?”.
Bertha : “Kuhusu kuhusu nini?”.
Nickson : “Sikuelewi!.”
Bertha : “Nataka kushirikishwa!.”
Nickson : “Ah we tulia usije kuharibu.”
Bertha : “Kwahyo kisa mwanamke ndo sifai?”
Nickson : “Hapana unafaaa karibu!.”
Jenerali : “Safi sana nilizani utamtenga Bertha lakini umefanya la maaana. ”
Bertha : “Eeeeh bhana haki sawa hamnaga wa kike wa kiume wote tuna pambana!.”
Jenerali : “Sawa unahitaji vifaa gani?”.
Nickson : ”Kwa sasa nahitaji komputa mpakato moja na moja kwa ajili ya Bertha.”
Mipango ya kuchora ramani ya kuvamia Bank hiyo iliopo baharini ilianza kwa ushirikiano wa watu wote!.
Itaenddeeeeleaaa………
 
Nimekuja[emoji136].
Alafu avatar yako inaendana na kinachoendelea kune hii story. Le professory.. hahha

#money Heist. aka La casa de papel.
🙂 A criminal mastermind "The Professor".
Yeah am interested with money,power and status but through involving in legal activities i.e business ventures & technology>ethical hacking,DevOps engineering etc..
 
Back
Top Bottom