Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naona jamaa bado ana compose next episode
Now you wont!Mhh!.. "Now you see me"
Eti eeh Swa mkuuu sante kwa ushauri!Asee uwe unatupia episode 3 kama ulivyokua unafanya season 1
sante MkuuShukrani mkuu equator
Nice,,,,nextMy soulmate .Mwenzi wa roho yangu
Sehemu ya 23.
Ni mida ya saa mbili asubuhi . Nickson na Bertha wapo kwenye msafara wa magari ma tatu ya hao watu wasio wafahamu. Walikuwa kwenye gari la katikati kaati ya magari hayo waliwekwa sehemu ya nyuma ya gari hilo na walikuwa kwenye ulinzi mkali kana kwamba ni wahalifu wanapelekwa kituoni au kama vile wafungwa wametolewa kusikiliza kesi zao na wanarudi rumande.
Kwenye gari waliokuwa wamekaa walizingirwa na watu wenye sura kama za kiarabu sio kiarabu wasomali sio wasomali . Ni watu ambao ni weusi na hawana afya sana wenye mwili angalau ni wachache sana. Lakini kilichokuwa kinawapa ujasiri ni silaha nzito walizokuwa wamebeba.
Safari iliendelea porini mpaka kufikia maeneo yaliyo changamka kidogo . Wenyeji wa maeneo hayo walionekana kama wasomali .Na nywele zao zilikuwa za singasinga .
Nickson : "Jamani tuko wapi?".
Watu hao hawakudiriki kuwajibu chochote.
Bertha : "Mnatupeleka wapi tupo wapi?".
Nickson :"Jamani nasikia njaa!."
Bertha : "Wala hata hawajibu .Ngoja niwaoneshe.".Bertha akamtemea moja wapo mate usoni.
Omar : "Wewe ntakuua!.".Omar aliongea kwa hasira na kwa lugha ambayo Bertha na Nickson hawakuelewa.
Omar aliamua kuchukua vitambaa vyeusi na kuwa funika macho.
Safari iliendelea wakatoka sehemu ambayo ilikuwa na watu wakaingia tena porini na wakaendelea na safari bila ya kuwaongelesha wageni wao ambao walikuwa wamependeza kama wanaenda kwenye harusi ama shughuli flani ya muhimu sana.
Baada ya muda kwenda waka simamisha magari yao na kuwashusha Bertha na Nickson wakiwa bado na vitambaa usoni.
Bertha na Nickson wakafunuliwa uso kutazama ni wapo kwenye kambi ambayo ni kama ya kijeshi. Magari ya kijeshi yalikuwa yakionekana na watu walikuwa na bunduki mikononi mwao. Waka pelekwa kwenye ofisi na kuwekwa kwenye viti. Mara baada ya muda wali letewa kifungua kinywa na alieleta hakuzungumza kitu.
Nickson alianza kuki fakamia chakula hicho.
Bertha : "We una kulaje wakati hujui kama kina sumu."
Nickson : "Unasema?".Aliendelea kukazana kutafuna chakula hicho na kujilamba vidole.
Bertha : "Acha bhana kitakua na sumu."
Nickson : "Yani watutoe huko kooooote waje kutupia hapa sumu?".
Bertha : "We unawajua kwani?".
Nickson : "Kuwajua na chakula wapi na wapi kwani hotelini ukienda kula unajua nani kapika?."Nickson aliendelea kula bila hata ya kumuangalia Bertha.
Bertha : "Mi sili bhana mi si wa amini hawa watu."
Nickson : "Hii wiki nzima kwanzia watuteke umekula leo una ringa?".Nickson ali unyoosha mkono wake aki taka kupunguza chakula kidogo cha Bertha.
Bertha : "Acha bhana"Aliongea akimpiga Nickson kijibao cha mkononi.
Nickson : "We si umesema huli?".
Bertha : "Kwani nani kakuambia uchukue?".Bertha alianza kujikaza kula.
Walipo maliza kula walianza kuongea wakiwa wame egemea ukutani.
Bertha : "Nickson."
Nickson : "Naaam."
Bertha : "Eti hawa watakua kina nani?".
Nickson : "Mi sijui nimeshakuambia mara ngapi?"
Bertha : "Au ulipitia jeshini ndo wamekuja kuku lipizia kisasi?".
Nickson : "Mh hapana sijawahi hata kufikiria kuwa hata askari."
Bertha : "Hahahaah kwanza wewe ungekuwa askari watu wangekupiga vibaya kwa ulivyo mpole mpole!."
Nickson : "Ukishiba ndo una anza kuongea shobo syeti?."
Bertha : "Hahahahahahhhaahahahaaa.". Bertha aliendelea ku angua kicheko.
Nickson : "We nichukulie wa mzaha mzaha tu!."
Bertha : "Hamna nakutania mwaya.Lakini naogopa nickson hawa ni kina nani?."Bertha alianza kuangusha machozi.
Nickson : "Ndio nlikuwa nafikiria labda itakuwa mama mwenye nyumba katuleta huku."
Bertha: "Hahhaahahahahah wewe kaka jamani kweli unajua kunifurahisha. Hahahahhaaha". Bertha alicheka huku bado ana machozi usoni .
Mara ghafla yule dada alieleta kifungua kinywa akarudi tena.
Bertha : "Dada tusaidie.".Bertha aliongea kwa huruma ili angalau yule mdada amuonee huruma.Yamkini atamsaidia.
Mdada : "Shhhh".
Huyo mdada Aliendelea na shughuli za kukusanya vyombo.
Bertha : "Jamani dada tusaidie.Kwa nini tupo hapa."
Mdada : "Msubirieni Jenerali."
Bertha : "Nani?". Kabla ya kujibiwa mmoja wa walinzi waliokuwa mlangoni akafungua kumuharaikisha yule mdada atoke nje.
Mlinzi : "Wewe unataka nini?".Bertha na Nickson wali shangaana kusikia anaongela kiswahili.
Bertha "Nataka kwenda uwani".Bertha alitumia akili ya haraka haraka.
Mlinzi : "Ndo wapi uwani?".Mlinzi huyo aliekuwa akitafuna mirungi alionekana alishindwa kuelewa msamiati huwo.
Bertha : "Chooni."Alisema akiruka ruka kama kabwana na mkojo!.
Mlinzi : "Oooooohoo chooni haya kuja!."
Nickson : "Na mimi nataka kwenda.".
Mlinzi : "Kuja kujeni tuta wapeleka chooni sasa kuja."
Nickson : "Haya asante".
Walipotoka waliongozona na mlinzi kila moja. Nickson alipelekwa choo cha wanaume na Bertha cha wanawake.Walipofika Nickson akafunga mlango na kaunza kupa angalia maeneo hayo vizuri. Alipoangalia dirishani aliona hakuna namna ya kupita pale . Na hivyo hivyo bertha alikosa namna ya kutoroka kwa sababu ya ulinzi na dirisha la choo halikutoa ushirikiano.
Walipo maliza haja zao wote wakarudishwa kwenye ofisi ile ile waliokuwamo mwanzo.
Nickson : "Sasa tuna msubiri nani?".
Mlinzi : "Usiogope kabisa Jenerali ana kuja!..". Aliendelea kuweka mirungi mdomoni na akaendelea akisema ."Jenerali anakuja kuwaona yeye ana roho nzuri kabisa hato wa dhuru."
Bertha : "Sasa Jenerali ndo nanI?'.
Mlinzi :"Hamumjui jenerali?".
Bertha : "Ndio kaka yangu ata tuua jamani sisi hatuja fanya kitu!."
Mlinzi : "Mtamuona usiogope jenerali amenilea mimi mpaka nimekuwa mtu mzima."
Bertha : "Sasa ametuleta hapa ili iwaje!?"
Mlinzi :"We ngoja.". Alisema akielekea mlangoni na kuufunga.
Bertha : "Jenerali nani?".
Nickson : "Hivi unakumbuka ile siku tuliandika ujumbe kwenye account ya kikundi cha mgambo somali?."
Bertha: "Enhee ile tulikuwa tuna wa tania wakaibe hela kwenye ile benki ya baharini?".
Nickson : "Ndio! Yamkini ndo hawa wametuleta watu uwe?."
Bertha : "Ah wapi wewe!. Wale hawawezi kututafuta bhana acha ndoto zako kwanza usikute ile account ni ya uongo."
Nickson : "Sasa una dhani hawa ni kina nani?."Nickson aliuliza kwa msisitizo.
Bertha : "Labda itakuwa ndio walio muuwa Mandoto bhana wanajua mimi ni mke wake kwa hiyo ndo maana wamenileta hapa."
Nickson : "Kwani Mandoto alipokufa hamkujuaga ni nani alimu ua?".
Betha : "Hakuna mtu ajuae na hawa waarabu arabu….. mhhh sio watu wema!."
Nickson : "Mhhhhh. tutajua tu ngoja tumsubirie huyo jenera....".Kabla ya Nickson kumaliza sentesi hiyo mlango ulifunguliwa na wakaingia watu kama sita hivi.
Mlinzi : "Simameni Jenerali ameingia.".
Nickson na Bertha walisimama bila kupenda . Mmoja wapo wa hao watu alikuwa amevalia nguo za kupendeza na angavu kuliko wengine lakini pia alikuwa ana nyota za kijeshi nyingi sana kwenye koti lake la kijeshi pamoja na kwamba wengine walio simama nao walikuja na nguo za ki raia.
Nickson : "Msi tuue jamani."
Wote walicheka kasoro Bertha na Nickson .
Jenerali "Kimyaaa!.". Wote waliokuwa wanchecka wakanyamaza baada ya jenerali huyo kutoa amri hiyo kwa wafuasi wake.
Jenerali : "Kaeni jamani.". Nickson na Bertha walipewa ishara ya kurejea kuketi.
Jenerali alitoa sigara kubwa ijulikanayo kama "cigar". Akaiwasha wakati anafanya hivyo wawili walienda kusimama nyuma ya Bertha na Nickson . Na wengine walirudi nje ya ofisi hiyo.
Jenerali : "Karibu Bertha na Nickson."
Bertha : "Wewe nani?."
Jenerali : "Hamnijui?".
Bertha : "Hapana! au Nickson unamjua?.".
Nickson : "Hapana.".
Bertha : "Wewe nani jamani tumekuja huku kufanya nini?.".Bertha alijaribu kunyanyua mikono japo bado anazo pingu mikononi.
Jenerali aliamuru zile pingu zifunguliwe na zilifunguliwa kwa wote.
Jenerali akaendelea kusema : "Mimi ni Jenerali wa wanamgambo wa kikundi cha M16."
Bertha na Nickson wali tazamana kwa mshangao na kwa uoga.
Jenerali : "Msiogope. Jisikieni nyumbani.". Jenerali aliendelea ku vuta pafu jingine la sigara hiyo.
Nickson : "Tujisikie nyumbani wakati hatuna uhakika wa maisha yetu?."
Jenerali : "Wewe ni mwanaume wasiwasi wa nini?."
Bertha : "Kwa nini tupo hapa?. Sisi hatuku fahamu".
Jenerali : "Kama nilivyo sema mimi ndiye jenerali .Jina kamili ni Jenerali Bashiru."
Bertha : "Kwa nini tupo hapa?."
Jenerali : "Kabla sijakuambia kwanza tuende uka ione kambi yetu angalua kichwa kitatulia.Jisikieni tu mpo nyumbani"
Itaendelea………..
Jamani mni wie radhi majukumu ya Home na kazi yamenibana lakini msi kate tamaaa nitaendelea mni vumilie tasavali!
Bado una tunga!!?Jamani mni wie radhi majukumu ya Home na kazi yamenibana lakini msi kate tamaaa nitaendelea mni vumilie tasavali!
Sio kwamba nina tunga master lakini mud a wa kuandika ndo sina lakini usikate tamaa maybe ikizid saaaaana j3 napost 3 Episodes!Bado una tunga!!?