Hadithi: My Soulmate

Hadithi: My Soulmate

My Soulmate Episode 22.

Produced by EquatorStory.

******Ilipoishia **********************

Nickson na Bertha walivamiwa na watu walio kuwa wamefunika nyuso zao. Na walizibwa midomo n pua mpaka walipozimia.

####### Endelea #####################

Pale Nickson alipo kuwa aki ishi mama Grace ambaye ndiye mwenye nyumba alifika na kukuta hamna mtu alichukulia kuwa waliondoka mapema cha kushangaza mlango haukufungwa kwa funguo ulirudishwa tu kiasi flani mama Grace kwa muda alichukia lakini akaona hakuna jambo lilo haribika kwa sababu waliacha mkeka wao tu. Mama grace alifanya usafi wa hapa na pale ili kuweka mazingira sawa na sawia. Alipo toka alikutana na Dulla.

Dulla : "Shkamo mama."

Mama Grace : "Marahaba hujambo? Umewaona hawa wakiondoka?".

Dulla : "Hapana itakua wametoka mapema sana na leo nimelala lala kidogo."

Mama Grace : "Haya sawa!."

Dulla : "Sawa mama!".

Maisha yaliendelea maeneo hayo bila kujua wameondoka mda gani na hawana namna ya kudhibitisha wamekwenda wapi maana Nickson na Bertha waliuza mpaka simu zao ili kupata hela ya kwenda kuanza maisha mapya walipokwenda.

Dulla alikumbuka ahadi kuwa Nickson akipata kununua simu lazima ata mpigia ampe salamu japo amjulie hali.

_____________________________________________________________________

Upande mwingine Nickson ana amka kutoka usingizini. Ana gundua yupo ndani ya gari la mizigo aina ya fuso kwenye sehemu ya mizigo alikuwa yupo na bertha pamoja na watu wengine wawili Monica na Yustar.

Nickson : "Tuko wapi? tuachieni tufungulieni tuacheni!!........"Alianza kupiga kelele akiwa anafanya hivyo aligundua amefungwa minyororo mikononi na miguuni kwa namna hiyo alishindwa kukimbia kama angekuwa na sehemu iliowazi .

Yustar : "Nyamaza wewe....". Yustar aliongea huku anatumbua macho na kidole kimoja kikionyesha ishara kuwa Nickson anyamaze.

Yustar na Monica walionekana kupauka karibu kila mahali inaonekana haja pata nafasi ya kuoga takribani wiki sasa . Mdomo ulikuwa umepauka kama alilalmba majivu siku 2 mfululizo . Uso ulikuwa umepauka kweli kweli alikua ana onekana kama mdomo umepasuka pasuka na nywele zake zilikuwa ni fupi lakini zilivurugika na kukaa kwa mtindo wa ajabu ajabu.

Nickson : "Nifungulieni niachieni mimi sijakosea kitu.."

Monica na yeye alijaribu kumnyamazisha Nickson . "Kaka kaaa kimya watakuja kutupiga tena".

Nickson alianza kulia akimuegema Bertha alionekana alikuwa amelia mpaka kukata tamaa.

Betha , Monica , Yustar : "Ssssssshshhhhhhhhh!.".

Yustar: "We mwanaume naye ukilia sisi wanawake tufanyaje?".

Monica : "Kaka jikaze. Japo ule usipokula watakuadhibu kaka yangu."

Nickson baada ya kuona chakula alikikimbilia akafungua aka anza kula kwa fujo kama mbuzi alieona chakula asubuhi.Alipo maliza kula akili zake zika anza kumrejea na aka anza kuwa angalia waliokuwa nae vizuri.

Nickson : "Jamani kwa nini tupo hapa?".Aliuliza akimtazama kila mtu usoni japo kama kuna anae jua sababu ya kuepo hapa.

Monica : "Kaka yangu hakuna anayejua kusema kweli."

Nickson : "Sasa we umefikaje?".

Monica :"Mimi nilikuwa nafua nguo zangu karibu na kwenye bomba nikashangaa nimefunikwa uso. Nakuja kuzinduka nipo ndani ya gari hili na nimemkuta huyu dada Yustar."

Nickson : "Jamani hawa ni kina nani wanataka nini jamani?".

Monica : "Mi sijui jamani."

Nickson : "Na wewe Yustar umefikaje hapa?".

Yustar :"Kaka yangu mimi ni mwimba muziki mdogo mdogo nili rekord nyimbo fupi nikiwa naimba bila muziki.Watu wakanisifia sana."

Nickson : " Ukaja ukashtukia upo humu ndani pia?. "

Yustar : "Si utulie sasa."

Bertha : "Ndio alivyo kila mda ni utani mxxxxxxxhew.".Nickson alimgeukia Bertha akashangaa anasonywa leo alijua labda ni hali ndo inamfanya hivyo.

Monika : "Jamani si anatuchangamsha. Hahahahahaah"Alisema hivyo huku akimkonyeza Nickson kiutani.

Yustar: "Sasa bhana katika walio kuwa wana toa maoni kuna mmoja ana jiita pastor Chris. Alisema ana sema ata ni dhamini ili nitoe ule wimbo atalipia kila gharama .Huyu mchungaji nlikua nina wasiwasi nae kwa sababu anapost neno la Mungu lakini haoneshi yupo kanisa gani wala hatajagi kanisa lake. Mi sikuliwaza hilo sana nikasema labda sio mwenyeji sana wa haya maswali."

Nickson : "Enhee...". Alisema huku akiwa mtulivu aliogopa kufanya utani tena.

Yustar aliendelea. "Mimi nili anza kuzungumza nae kuhusu maswala yangu ya muziki na alionesha kubarikiwa na kazi yangu. Tukaendelea kuwasiliana mpaka ilipofika siku moja. "Yustar aliacha kusimulia aka anza kushusha machozi.

Monika : "Pole usilie jikaze.".Monika alimpa faraja Yustar kwa kumkumbatia akimbembeleza.

Yustar aliendelea huku akiangusha machozi. "Siku hiyo alisema yupo maeneo ya Arusha kwa hiyo angependa tuonane. Mimi nikaenda nafika ofisini kwake sijaona mtu nampigia hapatikani nikasema niondoke wakati nageuka nlishutshwa na mtu aliokuwa na bunduki akisema aaaha yustar karibu. Nikajaribu kumpita niondoke wakati nimempa mgongo nilisikia kishindo cha nguvu akinipiga shingoni mwangu . Nikajikuta hapa sijui wananipeleka wapi."

Nickson : "Pole dada Yustar".

Yustar : "Sijui mume wangu Johnson akinitafuta atanipata wapi wakati sikumuaga hata."

Monica : "Na nyie mmefikaje hapa?".

Nickson : "Sisi tulikuwa tunataka kuhama turudi kijijini usiku wa kuamkia safari yetu ndo wakatuteka ."

Basi walianza soga za hapa na pale na walianza kujenga urafiki ilipofika mchana gari lilisimamishwa kipande cha juu cha mlango ulifunguliwa . Waka amrishwa wageukia ukuta wa gari ili wasiwaone waliokuwa wanakuja . Wakafungwa machoni kwa vitambaa wakashushwa kwenye gari. Nickson alijaribu kufurukuta akapigwa rungu la miguuni akatulia.

Nickson : "Mnatupeleka wapi?".

Bertha : "Nickson wataniua ama?".

Mteka nyara : "Nyamaza!."Alisema kwa kuamrisha wote wakakaa kimya.

Wakapewa nafasi ya kujisaidia na wakapandishwa kwenye gari wakafunguliwa macho waka amrishwa wasifungue macho wala kugeuka kama wanapenda maisha yao . Walipofunga mlango ndipo walipata nafasi ya kugeuka na wakakaa waka anza kula chakula walicholetewa.

Safari iliendelea bila wao kujua wapo wapi na wanaelekea wapi na wanaenda wapi?.Jinsi muda ulivyo kuwa unaenda waliendelea kulishwa . Walikaa humo siku mbili.

Siku iliyo fuata waliposhuka kujisaidia wali shangaa kuona Monica hakurudishwa kwenye lile gari . Monica alipandishwa kwenye gari dogo aina ya pickup aka pelekwa sehemu nyingine iliowafanya waliobaki kuanza kumlilia kwa uchungu wasijue kaenda wapi na wao wanapelekwa wapi.

Baada ya siku moja walishangaa kuona kuna gesi ikipuliziwa ndani ya gari hilo walijitahidi kupambana wasi ipumue hewa hiyo lakini baada ya dakika 20 walianza kusinzia . Nickson ali ishiwa nguvu akaona Yustar akipandishwa gari lingine na akaondoka. Waliwa chukuwa Nickson na Bertha na kuwaweka kwenye gari lingine dogo. Yustar ni dhahiri alipelekwa sehemu nyingine. Nickson alijaribu kuangalia uso zao lakini alishindwa kwa sababu ya barakoa zao.

Baada ya muda Nickson aliamka ndani ya chumba kidogo kilichokuwa na vitanda pamoja na samani kama meza na vingine. Alijaribu kupiga kelele kuomba msaada ili aachiwe lakini juhudi zake ziligonga mwamba.Alipojaribu kuchungulia dirishani akaona samaki baaada ya kutafakari alijua yupo chini ya maji . Kwenye bahari au ziwa alijua hakika yupo kwenye manowari. Alianza kulia asijue atafanyaje na alipoteza matumaini. Bertha muda wote alikuwa mkimya sana .

Walianza kuzoea maisha ya humo ndani kwa ma juma kadhaa walipokuwa isitoshe mara zingine manowari ili simama kwa siku kadhaa kana kwamba ina nyata vile au inajificha isionekane . Ni wakati wa chakula walikuwa wana pewa chakula na kila mara chakula kinapokuja walikuja watu wawili wenye silaha nzito.

Nickson alijaribu kumshawishi Bertha wafanye kutoroka watakapo kuja kuleta chakula. Bertha alimwambia tutatoroka twende wapi . Tupo kwenye manowari katikati ya bahari tutulie tu tusije uwawa tuone wanataka nini na sisi.

Walikaaa huko wa kitazama televisheni . Filamu kadhaa zilizokuwa humo ndani.

Waliendelea kusafiri mpaka muda ukafika waliokuwa wana leta chakula mara hii hawakuleta chakula bali waliwaletea nguo mpya na kuwa ambia . Vaeni sasa mkaonane na mkuu wetu anawangojea.

Nickson na Bertha bila ubishi walienda kubadilisha nguo zao na kuvaa nguo walizoletewa. Nickson aliletewa suti yenye rangi ya damu ya mzee na shati jeupe kabisa.Na Berha aliletewa gauni la masawi (Bluu). lenye mpasuo mguu wa kushoto . Nickson na Bertha walipendeza . Wakatolewa kwenye chumba hicho waka pelekwa nje ya manowari hiyo. Ilikuwa ni mida ya usiku kuna giza nene . wakafika ufukweni kwa kutumia mtumbwi mdogo. Waka panda gari dogo aina ya cruser (TDI). Walikaa nyuma ya gari hilo wakiwa na watu wanne wenye silaha za moto . Safari ilianza kuelekea kwa huyo mkuu mwenyewe.

Itaendeleaa...................
 
My soulmate .Mwenzi wa roho yangu

Sehemu ya 23.

Ni mida ya saa mbili asubuhi . Nickson na Bertha wapo kwenye msafara wa magari ma tatu ya hao watu wasio wafahamu. Walikuwa kwenye gari la katikati kaati ya magari hayo waliwekwa sehemu ya nyuma ya gari hilo na walikuwa kwenye ulinzi mkali kana kwamba ni wahalifu wanapelekwa kituoni au kama vile wafungwa wametolewa kusikiliza kesi zao na wanarudi rumande.

Kwenye gari waliokuwa wamekaa walizingirwa na watu wenye sura kama za kiarabu sio kiarabu wasomali sio wasomali . Ni watu ambao ni weusi na hawana afya sana wenye mwili angalau ni wachache sana. Lakini kilichokuwa kinawapa ujasiri ni silaha nzito walizokuwa wamebeba.

Safari iliendelea porini mpaka kufikia maeneo yaliyo changamka kidogo . Wenyeji wa maeneo hayo walionekana kama wasomali .Na nywele zao zilikuwa za singasinga .

Nickson : "Jamani tuko wapi?".

Watu hao hawakudiriki kuwajibu chochote.

Bertha : "Mnatupeleka wapi tupo wapi?".

Nickson :"Jamani nasikia njaa!."

Bertha : "Wala hata hawajibu .Ngoja niwaoneshe.".Bertha akamtemea moja wapo mate usoni.

Omar : "Wewe ntakuua!.".Omar aliongea kwa hasira na kwa lugha ambayo Bertha na Nickson hawakuelewa.

Omar aliamua kuchukua vitambaa vyeusi na kuwa funika macho.

Safari iliendelea wakatoka sehemu ambayo ilikuwa na watu wakaingia tena porini na wakaendelea na safari bila ya kuwaongelesha wageni wao ambao walikuwa wamependeza kama wanaenda kwenye harusi ama shughuli flani ya muhimu sana.

Baada ya muda kwenda waka simamisha magari yao na kuwashusha Bertha na Nickson wakiwa bado na vitambaa usoni.

Bertha na Nickson wakafunuliwa uso kutazama ni wapo kwenye kambi ambayo ni kama ya kijeshi. Magari ya kijeshi yalikuwa yakionekana na watu walikuwa na bunduki mikononi mwao. Waka pelekwa kwenye ofisi na kuwekwa kwenye viti. Mara baada ya muda wali letewa kifungua kinywa na alieleta hakuzungumza kitu.

Nickson alianza kuki fakamia chakula hicho.

Bertha : "We una kulaje wakati hujui kama kina sumu."

Nickson : "Unasema?".Aliendelea kukazana kutafuna chakula hicho na kujilamba vidole.

Bertha : "Acha bhana kitakua na sumu."

Nickson : "Yani watutoe huko kooooote waje kutupia hapa sumu?".

Bertha : "We unawajua kwani?".

Nickson : "Kuwajua na chakula wapi na wapi kwani hotelini ukienda kula unajua nani kapika?."Nickson aliendelea kula bila hata ya kumuangalia Bertha.

Bertha : "Mi sili bhana mi si wa amini hawa watu."

Nickson : "Hii wiki nzima kwanzia watuteke umekula leo una ringa?".Nickson ali unyoosha mkono wake aki taka kupunguza chakula kidogo cha Bertha.

Bertha : "Acha bhana"Aliongea akimpiga Nickson kijibao cha mkononi.

Nickson : "We si umesema huli?".

Bertha : "Kwani nani kakuambia uchukue?".Bertha alianza kujikaza kula.

Walipo maliza kula walianza kuongea wakiwa wame egemea ukutani.

Bertha : "Nickson."

Nickson : "Naaam."

Bertha : "Eti hawa watakua kina nani?".

Nickson : "Mi sijui nimeshakuambia mara ngapi?"

Bertha : "Au ulipitia jeshini ndo wamekuja kuku lipizia kisasi?".

Nickson : "Mh hapana sijawahi hata kufikiria kuwa hata askari."

Bertha : "Hahahaah kwanza wewe ungekuwa askari watu wangekupiga vibaya kwa ulivyo mpole mpole!."

Nickson : "Ukishiba ndo una anza kuongea shobo syeti?."

Bertha : "Hahahahahahhhaahahahaaa.". Bertha aliendelea ku angua kicheko.

Nickson : "We nichukulie wa mzaha mzaha tu!."

Bertha : "Hamna nakutania mwaya.Lakini naogopa nickson hawa ni kina nani?."Bertha alianza kuangusha machozi.

Nickson : "Ndio nlikuwa nafikiria labda itakuwa mama mwenye nyumba katuleta huku."

Bertha: "Hahhaahahahahah wewe kaka jamani kweli unajua kunifurahisha. Hahahahhaaha". Bertha alicheka huku bado ana machozi usoni .

Mara ghafla yule dada alieleta kifungua kinywa akarudi tena.

Bertha : "Dada tusaidie.".Bertha aliongea kwa huruma ili angalau yule mdada amuonee huruma.Yamkini atamsaidia.

Mdada : "Shhhh".

Huyo mdada Aliendelea na shughuli za kukusanya vyombo.

Bertha : "Jamani dada tusaidie.Kwa nini tupo hapa."

Mdada : "Msubirieni Jenerali."

Bertha : "Nani?". Kabla ya kujibiwa mmoja wa walinzi waliokuwa mlangoni akafungua kumuharaikisha yule mdada atoke nje.

Mlinzi : "Wewe unataka nini?".Bertha na Nickson wali shangaana kusikia anaongela kiswahili.

Bertha "Nataka kwenda uwani".Bertha alitumia akili ya haraka haraka.

Mlinzi : "Ndo wapi uwani?".Mlinzi huyo aliekuwa akitafuna mirungi alionekana alishindwa kuelewa msamiati huwo.

Bertha : "Chooni."Alisema akiruka ruka kama kabwana na mkojo!.

Mlinzi : "Oooooohoo chooni haya kuja!."

Nickson : "Na mimi nataka kwenda.".

Mlinzi : "Kuja kujeni tuta wapeleka chooni sasa kuja."

Nickson : "Haya asante".

Walipotoka waliongozona na mlinzi kila moja. Nickson alipelekwa choo cha wanaume na Bertha cha wanawake.Walipofika Nickson akafunga mlango na kaunza kupa angalia maeneo hayo vizuri. Alipoangalia dirishani aliona hakuna namna ya kupita pale . Na hivyo hivyo bertha alikosa namna ya kutoroka kwa sababu ya ulinzi na dirisha la choo halikutoa ushirikiano.

Walipo maliza haja zao wote wakarudishwa kwenye ofisi ile ile waliokuwamo mwanzo.

Nickson : "Sasa tuna msubiri nani?".

Mlinzi : "Usiogope kabisa Jenerali ana kuja!..". Aliendelea kuweka mirungi mdomoni na akaendelea akisema ."Jenerali anakuja kuwaona yeye ana roho nzuri kabisa hato wa dhuru."

Bertha : "Sasa Jenerali ndo nanI?'.

Mlinzi :"Hamumjui jenerali?".

Bertha : "Ndio kaka yangu ata tuua jamani sisi hatuja fanya kitu!."

Mlinzi : "Mtamuona usiogope jenerali amenilea mimi mpaka nimekuwa mtu mzima."

Bertha : "Sasa ametuleta hapa ili iwaje!?"

Mlinzi :"We ngoja.". Alisema akielekea mlangoni na kuufunga.

Bertha : "Jenerali nani?".

Nickson : "Hivi unakumbuka ile siku tuliandika ujumbe kwenye account ya kikundi cha mgambo somali?."

Bertha: "Enhee ile tulikuwa tuna wa tania wakaibe hela kwenye ile benki ya baharini?".

Nickson : "Ndio! Yamkini ndo hawa wametuleta watu uwe?."

Bertha : "Ah wapi wewe!. Wale hawawezi kututafuta bhana acha ndoto zako kwanza usikute ile account ni ya uongo."

Nickson : "Sasa una dhani hawa ni kina nani?."Nickson aliuliza kwa msisitizo.

Bertha : "Labda itakuwa ndio walio muuwa Mandoto bhana wanajua mimi ni mke wake kwa hiyo ndo maana wamenileta hapa."

Nickson : "Kwani Mandoto alipokufa hamkujuaga ni nani alimu ua?".

Betha : "Hakuna mtu ajuae na hawa waarabu arabu….. mhhh sio watu wema!."

Nickson : "Mhhhhh. tutajua tu ngoja tumsubirie huyo jenera....".Kabla ya Nickson kumaliza sentesi hiyo mlango ulifunguliwa na wakaingia watu kama sita hivi.

Mlinzi : "Simameni Jenerali ameingia.".

Nickson na Bertha walisimama bila kupenda . Mmoja wapo wa hao watu alikuwa amevalia nguo za kupendeza na angavu kuliko wengine lakini pia alikuwa ana nyota za kijeshi nyingi sana kwenye koti lake la kijeshi pamoja na kwamba wengine walio simama nao walikuja na nguo za ki raia.

Nickson : "Msi tuue jamani."

Wote walicheka kasoro Bertha na Nickson .

Jenerali "Kimyaaa!.". Wote waliokuwa wanchecka wakanyamaza baada ya jenerali huyo kutoa amri hiyo kwa wafuasi wake.

Jenerali : "Kaeni jamani.". Nickson na Bertha walipewa ishara ya kurejea kuketi.

Jenerali alitoa sigara kubwa ijulikanayo kama "cigar". Akaiwasha wakati anafanya hivyo wawili walienda kusimama nyuma ya Bertha na Nickson . Na wengine walirudi nje ya ofisi hiyo.

Jenerali : "Karibu Bertha na Nickson."

Bertha : "Wewe nani?."

Jenerali : "Hamnijui?".

Bertha : "Hapana! au Nickson unamjua?.".

Nickson : "Hapana.".

Bertha : "Wewe nani jamani tumekuja huku kufanya nini?.".Bertha alijaribu kunyanyua mikono japo bado anazo pingu mikononi.

Jenerali aliamuru zile pingu zifunguliwe na zilifunguliwa kwa wote.

Jenerali akaendelea kusema : "Mimi ni Jenerali wa wanamgambo wa kikundi cha M16."

Bertha na Nickson wali tazamana kwa mshangao na kwa uoga.

Jenerali : "Msiogope. Jisikieni nyumbani.". Jenerali aliendelea ku vuta pafu jingine la sigara hiyo.

Nickson : "Tujisikie nyumbani wakati hatuna uhakika wa maisha yetu?."

Jenerali : "Wewe ni mwanaume wasiwasi wa nini?."

Bertha : "Kwa nini tupo hapa?. Sisi hatuku fahamu".

Jenerali : "Kama nilivyo sema mimi ndiye jenerali .Jina kamili ni Jenerali Bashiru."

Bertha : "Kwa nini tupo hapa?."

Jenerali : "Kabla sijakuambia kwanza tuende uka ione kambi yetu angalua kichwa kitatulia.Jisikieni tu mpo nyumbani"

Itaendelea………..
 
Asee uwe unatupia episode 3 kama ulivyokua unafanya season 1
 
Nice,,,,next
 
sonnita boss embu niambie hadithi nyingine best niichek coz huyu jamaa ananiongeze arosto na depression hapa.
 
My soulmate .Mwenzi wa roho yangu

Sehemu ya 24.

***********Tuipoishia.******

Nickson na Bertha walitekwa na wasomali baada ya kutoa mawazo ya kuvamia banki moja iliopo baharini .

********** Tuendelee********

Ni asubuhi nyingine ofisini kwa bwana Sambeke hapa nchini Tanzania .Baada ya Bwana Sambeke kuweza kuliuza lile wazo la aplikeshen amepata hela ya kuweza kuongeza ofisi yake na muda huu ame ongeza wafanya kazi wengine 6. Na alikuwa akiwapa hotuba fupi ya kuwa karibisha .

Sambeke : “Habarini za ashubuhi?”.

Wote : “Salama!”. Watu wote walijibu salamu hiyo na kuendelea kumuangalia bwana sambeke machoni kwa umakini.

Sambeke : “Leo ni mwanzo wa hii safari yetu mpya. Ya kufikia malengo makuu ambayo tuliyo nayo ndani ya vichwa vyetu natumai tutakuwa wote katika kazi hii kwa muda mrefu.”. Sambeke ali nyamaza kwa muda kidogo akapitisha macho yake kwenye umati mdogo aliokuwa anauhutubia.”Napenda mjisikie mko nyumbani. Nataka mfanye ofisi hii kama ni yako nataka kila mtu ajisikie uzito wa kutoa mchango wake wa maana na kuweza kuifanya ofisi hii iweze kufanikiwa hata nisipo kuwepo mambo yasiyumbe. Tunaelewana!?”

Wote : “Ndio.”

Sambeke : “Safi nataka kampuni hii iwe ni kazi tu! Tuweze kufika mbali sana kimaendeleo!.Mpaka hapo kuna mtu mwenye swali!?.”.Sambeke alikaa kimya akipitisha macho yake aki subiri mwenye swali anyooshe mkono wake!.

Wote : “Hapana!”

Sambeke : “Safi msisite kuuliza ama kusema kitu mkiwa na cha kusema. Basi naomba niwa ache na stela Secretary wetu awasomee sheria za humu.”

Stela alisimama na aka anza kusogea mbele lakini dhahiri ame badilika sana sio kama Yule stela wa zamani tokea aolewe na bwana sambeke amekuwa tofauti kabisa. Nguo alizo kuwa akivaa amebadili sio kuvaa tena ma gauni marefu bali ana vaa vimini na zinazobana sura yake imebadilika kiasi kwamba hazifanani ni mikono yake. Saivi kwa sababu analo gari funguo za gari amekuwa akiwa nazo kila mahala japo kuwa pochi anayo lakini funguo haziachi hata akienda chooni.

Stela : “Habari za asubuhi?”.

Wote : “Salama!.”

Stela alianza kuwa somea sheria za pale. Hii ilikuwa ni siku ambayo wali ajiri wafanya kazi wapya ndani ya chumba hicho alikwepo bwana sambeke ,Stela ,Angela na wafanya kazi hao. Baada ya stela kumaliza kuzisoma sheria hizo . Bwana Sambeke alikaribishwa mara nyingine.

Sambeke : “Asante Stella kwa kutusomea hizo sheria. Je mume elewa?”Alisema huku Stela akielekea kuketi.

Wote : “Ndio!”.

Sambeke : “Sawa basi naomba tujitambulishe. Tuanzie upande huu wa kulia kuelekea kushoto.”

Hellena : “Habari za asubuhi. Mimi naitwa Hellena nipo kitengo cha uhasibu.”

Sambeke : “Sawa karibu Hellena!.”

Miriam : “Habarini jamani!. Mimi naitwa Miriam nipo kitengo cha Tehama.”

Sambeke : “Karibu Miriam”.

Linah : “Habarini mimi naitwa Linah nipo kitengo cha matangazo!.”

Sambeke : “Karibu sana Linah”.

Rapha:”Habarini naitwa Rapha . Nipo kitengo cha IT ama Tehama.”

Sambeke : “Karibu sana Raphael.”

Kelvin : “Jamani wazima?.Mimi naitwa Kelvini nipo kwenye kitengo cha ITau Tehama pia.”

Sambeke : “Karibu Kelvin.”

Braiton : “Habarini jamani mimi naitwa Braiton na nipo kitengo cha Tehama na ufundi pia!.”

Sambeke : “Karibu Braiton . Basi kuna mmoja kati yetu hajajitambulisha ni mwenyeji sio mgeni basi tumpe wakati huu ajitambulishe!.”

Angela : “Jamani karibuni sana. ”

Wote : “Asante.”

Angela : “Mimi naitwa Angela .Nafurahi sana kuwaona hapa natumai tutafanya kazi ya nguvu kama Mkuu alivyotangulia kusema hapo awali.”

___________________________________________________

Upande mwingine kule kwenye kambi ya kijeshi ya M16 waliopo Nickson na Bertha ndani ya nchi ya Somalia.

Jenerali baada ya kuwaonesha mazingira ya kambi waliopo na wakarudi kwenye ofisi ya Jenerali huyo.

Jenerali : “Nickson na Bertha nafurahi sana kuwaona kwenye himaya yangu karibuni sana.”

Nickson : “Asante.”Nickson na Bertha wailikuwa wamekaa kwa makini wakisikiliza kisa na mkasa kuletwa huku nchi ya Somalia.

Jenerali: “Sisi tumepata ujumbe zenu mlizo zituma kwenye mtandao wa kijamii wa twiter. ”

Nickson na Bertha waligeukiana na wakatoleana macho kwa kushangazwa.

Jenerali: “Tume ishiwa na silaha na hela za kuendesha shughuli zetu ”.

Nickson : “Sisi hatuna hela Jenerali!”. Nickson alijaribu kujibu kwa ajili ya kujitetea.

Jenerali : “Ndio tuna taarifa zenu zote ndio maana tuka diriki kuwa teka na kuwa ficha huku.”

Nickson : “Ndio!. Endelea!”Nickson alijibu kwa upole.

Jenerali : “Sasa kama mlivyo tushauri kuhusu kuiba kwenye ile benki ya baharini ijulikanayo kama Dolphin Bank au banki D.”

Jenerali ali nyamaza kwa muda na kupiga pafu lingine la sigara yake.

Jenerali : “Sisi tunaona kama ni nafasi nzuri tu ya kupata kipato ikiwezekana kuachana na huu uharamia na kufanya shughuli zingine. Ya nini kukimbizana na wanajeshi kila siku tukae bila amani ya nini?”.

Bertha : “Jenerali sisi hatuku dhania kuwa wazo letu mtalichukulia kwa uzito wa kiasi hiki!.”

Nickson : “Kweli na ilikuwaje mkatupata kirahisi hivyo?.”

Jenerali : “Kuhusu kuwapata sisi tuna watu wetu ndani ya kila mahali ilo sio tatizo kubwa sana.”

Nickson : “Sasa Jenerali kwenye hii kazi sisi tunatakiwa kufanya nini?”.

Jenerali : “Nyie kama mlivyo anzisha hili wazo mtakua ndio wapangaji wakuu lakini pia mtakua watakao kutekeleza shughuli hiyo.”

Bertha : “Jenerali mimi sijui chochote nikienda ntapigwa hata vibao nife.”

Nickson : “Kweli Jenerali hatujui chochote hatuja wahi tenda tokeo lolote la kutupa uzoefu kwenye uwizi ama uvamizi.”

Jenerali : “Mtapewa mafunzo na wana mgambo wa hapa msijali kuhusu hilo.”

Nickson : “Jenerali sisi tuna chaguo tuna ruhusiwa kukataa? .”

Jenerali : “Ndio mnaweza. Lakini jiulizeni kwanza. Mnaogopa nini maisha haya ni mafupi hii ni nafasi yenu ya kuwa ma bilionea kwa muda mfupi sana. Kabla hamja kataa kumbukeni huku kukipunguwa ujangili kutakuwa na amani kama Tanzania.”

Nickson : “Jenerali unachotuambia ni kigumu ngoja tupe muda wa kufikiria.”

Jenerali : “Hapo umenena vyema! Yani Marhabaaa!.Nitawapa juma zima mfikirie najua mta amua vitu vya maaana.”

Nickson na bertha walipewa hema lao . Nickson akapendekeza wakae hema moja na Bertha lakini Bertha hakuridhia ikabidi kila mmoja akae kwenye hema lake . Kwenye kambi Ile ya M16.

Itaendelea……………………
 
Back
Top Bottom