My soulmate .Mwenzi wa roho yangu
Sehemu ya 25.
Ni asubuhi nyingine ndani ya mji wa Arusha . Alarm ya simu ili ita na Braiton ambaye ni mfanyakazi mpya wa Kampuni ya Sambeke.
Mdada : βWe mkaka amkaβ¦.β. Ilisikika sauti ya binti aliekuwa amelala kitanda cha vyumba vya wageni pamoja na Braiton.
Braiton : βUnasema nini?β. Braighton alishtuka usingizini na akauliza . βKwani leo lini!? Saivi saa ngapi?β . Huku akiendelea ku soma majira kwenye simu yake. Ndipo alipostuka kuwa amechelewa kwenda kazini.
Mdada : βUmeamkaje Mume wangu?.β. Mdada aliuliza kwa mahaba . Braiton aligeuka na kumuangalia huyo mdada kwa mshangao na madharau.
Braiton alikimbia mpaka bafuni ili kuoga. Lakin kwa sababu ya muda alifanya kujifuta na maji tu kwa sababu hakutaka kuchelewa kazini .
Mdada : βJamani Braiton mtundu wewe yani una imba vizuri kwaya na pia unajua mambo ya kitandani . Nilidhani na wewe ni mvivu kama yule Mume wangu Muinjilisti yeye anajuaga tu kazi mjinga kabisa Yule.β
Braiton hakumtilia maaanani alicho kisema mdada Yule aliendelea ku kimbia huku na kule akikusanya vitu vyake ili aondoke.
Mdada : βBrai njoo bhana unipe ya mwisho. Jamani!β Alijaribu kumshika Braiton kwa shati lake lakini Braiton ali jitoa mikononi kwa Yule mdada na akaondoka na kufunga mlango mbio mbio mpaka kituoni atafute usafiri wa kwenda kazini.
Wakati huohuo Linah ambaye ni mmoja wapo wa wafanyakazi wapya wa kampuni ya Sambeke Inc alikua kwenye harakati za kwenda kazini.
Linah : βWe mwanaume una lala mpaka saivi na huna hela!.β
Jimmy : βSasa naamka mapema naenda wapi nadhani baadae ntaenda kanisani Bishop aliniambia leo nitahuhudumia.β
Linah : βEmbu nipe elfu kumi hapo nipate ya kula leo!.β
Jimmy : βUnasema elfu kumi unakula mwenyewe au na ofisi . We jana si nlikuambia ile elfu kumi ndio nlio kuwa nayo uka ng`ang`ania ukunywe pombe!?β.
Linah : βEeeh eeeh wewe sijakuomba mawaidha nimekuomba hela sio vingine mxxxxxheeeewww.β
Jimmy : βWe una msunya nani?β. Wakati Jimmy anauliza hivyo mke wake alikuwa akiondoka kwa hasira.
Linah : βKwaheri bhana sijui hata kwa nini najisumbua kwa ajili gani kwanzaβ¦β
Watu walianza kufika katika ofisi ya Sambeke mmoja baada ya mwingine lakini alie chelewa hiyo siku kuliko wote ni Braiton wakati anaingia ofisini . Stela alimwona aka amua kumuita pembeni.
Stela : βHabari za asubuhi?β.
Braiton : βSalama tu!. Mzima wewe?β
Stela : βMimi mzima swali ni kwako!?β. Stela aliuliza huku akimnyooshea mkono akionesha nguo na muonekano wa Braiton.
Braiton : βSwali gani Dada?β.
Stela : βHuoni ulivyo ulivyo rafu rafu? Upo kama hukulala nyumbani kwako!.β
Braiton : βNini kwani nipo uchi!?. Afu usinishobokeeee we secretary tu sijui umeishia la sita.β.Braiton alisema hivyo akiondoka.
Alipo ondoka akamwacha Stela akimshangaa kwa hasira yamkini hakujua kuwa Stela ni kama Boss wake maaana ndo mke wa Boss wa kampuni hiyo . Ali geuka ki unyonge akaenda kukaaa mezani kwake.
**************
Upande mwingine ndani ya nchi ya Somalia katika kambi ya M16 chini ya kiongozi wao Jenerali Bashiru .
Milango ilisikika ikigongwa na filimbi zikipigwa na milio ya risasi . Nickson alitoka kwa mshtuko akitaka kujua ni nini kinaendelea .
Nickson : βNini nini jamani msituueee!!!!!!!!!.β.Alisema kwa sauti kali. Watu wote waligeuka waka kaa kimya na kucheka.
Bertha : βWewe ni muda wa mazoezi usikae kishamba wewe!.β
Mchakamchaka ulianza taratibu yakifuatiwa na mazoezi mengine lakini aliekuwa legelege ni Nickson hata Bertha alikuwa sio mlegevu hivyo. Yamkini ndo mwanzo watu walisema!.
Baada ya mazoezi kuisha Nickson alionekana kuchoka kuliko wote .
Bertha : βPole mwaya . Hahahahaahahahaβ.
Nickson : βDaaah haya mazoezi hatari. β. Nickson aliongea huku akihema juu juu.
Bertha : βHahahaha haya mazoezi kidogo tu mbona. Haya ya kawaida sana nlikua na fanya na mume wangu Mandoto!.β
Nickson : βKwel mazoezi ya umuhimu.β
Bertha : βHaya baaadaae!. Afu Jenerali alisema badae baada ya chai tukamwone. β
Nickson : βHaya badae.β
Nickson alienda kuoga na alipotoka alivaaa na kuelekea kwenye sehemu ya kula ya kambi hilo. Aka chukua kifungua kinywa chake akamwona Bertha amekaa na waenyeji wa hapo . Bertha alionekana aki kaaa kwa amani na akicheka na kuwapa mikono.
Baaada ya kumaliza kula kifungua kinywa Nickson alienda na Bertha kwenye ofisi ya Jenerali wa kambi hiyo.
Jenerali : βZa asubuhi?. Je mumeamkaje?β.
Bertha na Nickson : βSalamaβ. Walijibu huku wakichukua viti na kukaaa.
Jenerali : βNickson na Bertha Nimewaita leo asubuhi kuwaaambia kuhusu mpango wetu sisi. Sisi M16 hatuezi kushindwa kamwe!. Wengi wamejaribu kutupindua wameshindwa sisi ndio tulio na Somalia ndani ya mikono yetu sio umoja wa Marekani , sio umoja wa mataifa yani UN hawatuwezi kamwe.β
Nickson : βKweli nime angalia historia yenu miaka mia na hamsini tokea mumeanza hakuna alio waweza.β
Jenerali : βSafi sana kijana una tujua vyema.β.Jenerali aliacha kuzungumza na kuwasha sigara .
Jenerali : βTuna hitaji watu kama nyie ambao mna akili tuka wavamie tuilipue hio Banki sisi hamna alieweza tushinda tukiamua kuvamia meli tumezivamia bila kusumbuliwa sisi indo mabingwa.β
Nickson : βMimi nitakaa chini na kupanga ramani ni ijue tuna vamia aje lakini nikishindwa kuja na mpango. Basi hatuta waunga mkono nyie ni mpaka pale nitakapo ona ipo sawa na kuridhika!β.
Bertha : βNa mimi vipi?β.
Nickson : βWewe kuhusu nini?β.
Bertha : βKwani nitakuwa nafanyaje?β
Nickson : βKuhusu!?β.
Bertha : βKuhusu kuhusu nini?β.
Nickson : βSikuelewi!.β
Bertha : βNataka kushirikishwa!.β
Nickson : βAh we tulia usije kuharibu.β
Bertha : βKwahyo kisa mwanamke ndo sifai?β
Nickson : βHapana unafaaa karibu!.β
Jenerali : βSafi sana nilizani utamtenga Bertha lakini umefanya la maaana. β
Bertha : βEeeeh bhana haki sawa hamnaga wa kike wa kiume wote tuna pambana!.β
Jenerali : βSawa unahitaji vifaa gani?β.
Nickson : βKwa sasa nahitaji komputa mpakato moja na moja kwa ajili ya Bertha.β
Mipango ya kuchora ramani ya kuvamia Bank hiyo iliopo baharini ilianza kwa ushirikiano wa watu wote!.
Itaenddeeeeleaaaβ¦β¦β¦