Hadithi: Nitakupata Tu

Hadithi: Nitakupata Tu

NITAKUPA TU
SEHEMU YA 018
Yalikuwa mateke mazito kwake,
mateke ambayo yalipigwa katika aina
ya kushtukiza. Alianguka kama furushi
la mahindi. Hakuweza kuinuka. Alikuwa
ametulia akionyesha kupotewa na
fahamu. Masimba hakusubiri, alimfuata
pale chini kisha kumpekua. Vitendo
vyote hivyo vilitendeka katika muda
mfupi tu. Alichukua bastola ambayo
aliikuta kwenye mavazi ya binti yule,
akaondoka akimuacha amelala
sambamba na bunduki yake. Kwa kuwa
alikuwa analitambua jengo lile, na kwa
vile alishawahi kupita katika majengo
yanamna ile. Haikuwa kazi ngumu
kuzikwepq camera za usalama ndani
ya jengo lile. Safari hii aliubadilisha
mwelekeo, aliubadilisha mwelekeo
sababu hakutaka kuua ama kukutana
na wanausalama wasiolijua tatizo.
Alitaka kuondoka bila kumwaga damu
ya mtu isipokuwa pale itakapobidi
kufanya hivyo. Akachepuka hapa na
kutokea pale, mpaka alipofika karibu
na lango la kutokea baharini ndipo
aliposikia king'ora cha hatari. Hapo
akahisi kwamba alikuwa hatarini.
Akaondoka akiongeza kasi kuwahi
kutoka ndani ya jengo. Hakutaka
kukamatwa tena, hakutaka kurudi tena
mikononi mwa watu wa usalama wa
taifa. Alitaka kwenda kuwafikishia
ujumbe wale waliomsingizia. Wale
waliomuwekea mtego na kusababisha
yeye kukamatwa..
******
Muda ulikuwa unakwenda lakini bado
hakumuona Masimba, alikuwa
amezoea kutokumuona masimba
akiwa nje ya nyumba, lakini hili la leo
lilimshangaza na kumtia wasiwasi.
Matukio ya muda mfupi uliopita, kisha
kutokufika kwa masimba mpaka muda
ule, ni kitu ambacho kilimpa wasiwasi.
Akaendelea kuivuta subira huku muda
wote macho yake yakiitizama saa
iliokuwa ukutani. Muda uliendelea
kusogea, hakumuona Masimba,
hakuiona ishara kwamba masimba
atarudi. Hilo likaufanya usingizi wake
upae, hakuiona sababu ya kulala. Kwa
mara ya kwanza alikuwa akimuhitaji
Masimba kuliko siku yoyote nyingine.
Angelalaje wakati masimba hakurudi.
Angelalaje wakati amegeukwa na watu
aliowaamini? Akainuka kutoka
kitandani kwa mara nyingine.
Hakuuona usalama wa kuendelea
kuwepo pale. Akayapitia mavazi yake
sambamba na bastola zake mbili.
Akazivuta hatua kuliacha jumba lao.
Wakati anamaliza kufunga mlango wa
nje akausikia mngurumo wa magari,
magari zaidi ya moja, michuno ya
matairi ndio kitu pekee kilichomfanya
Teddy ahisi uhatari. Uhatari ambao
alianza kuuona pale watu waliovalia
suti nyeusi wakipaa angani na kutua
ndani katika namna inayovutia, namna
ambayo ingekuwa burudani kama
ungekuwa ukiitizama. Teddy hakuwa
mgeni na kikundi hiki, kikundi maalum
cha kulinda viongozi wa taifa hili.
Kuwaona wakitua pale katika aina ile,
lilikuwa jibu kuwa Masimba
ameshageukwa, masimba
ameshaharibu. Kutua kwa watu wale
kukafuatiwa na kitendo ambacho
kilimuacha Teddy akiwaangalia.
Walipotua kwa ndani kila mmoja
alikuwa akichupa katika namna yake
na kwa upande wake, hata
walipomkaribia Teddy hawakuonyesha
kutaka utani. Midomo ya bastola
ilielekezwa kwake, macho ya watu
yakimtizama katika aina ya kumuuliza
maswali. Ni katika maswali hayo
kupitia macho yao Teddy alipohisi kitu.
Kitu ambacho hakikuwa cha kawaida.
Masimba hakufika, watu kuivamia
nyumba yao, gari yao kulipuliwa na
sasa kuvamiwa na kikosi maalum cha
kumlinda Rais ni suala zito sana. Aliiona
siku ile haikuwa nzuri kwako, haikuwa
nzuri kwa kilichotokea. Macho
yalikuwa yakimuangalia yeye kwa aina
ya maswali. Naye akajibu kwa aina ya
sijui kwa kutumia macho. Hawakutaka
kumsikiliza, wawili wakapita huku
wangine wakiendelea kumuweka kati.
Hazi kupita sekunde hata ishirini
walikwisha toka wakiwa na baadhi vitu
mikononi mwao. Hawakuongea tena
na mwanamke yule zaidi ya kumpita
na kuondoka wakimuacha
amesumama. Muda huo huo akayasikia
magari yakiondolewa kwa kasi. Bado
Teddy alikuwa ameduwaa, bado teddy
alikuwa akisafiri mbali kimawazo.
Kupotea kwa madawa ya kulevya,
kushikiwa bastola na washirika
wenzake haikuwa picha nzuri kwake.
Alijua kutakuwa na msukumo kutoka
sehemu moja kwenda sehemu
nyingine. Lakini bado hakulipata
jawabu, nani amelazimisha hili?
Masimba atakuwa wapi muda huu?
Kwa nini Kikosi maalum cha kumlinda
Rais kiwe kwenye hili suala la
kumtafuta masimba? Hayo na maswali
mengine mengi ndio yaliomchanganya
teddy.
Hakuona sababu ya kuendelea kubaki
pale. Aliondoka usiku ule ule akiamua
kwenda nyumbani kwa Jimmy
Lambert. Aliamua kwenda huko kwa
kuwa alitaka kuujua ukweli kuhusu hiki
kinachoendelea kutokea. Pia alitaka
kujua ni nani ambao walikuja
nyumbani kwake. Ilikuwa safari
ambayo alihisi ingekuwa ya Hatari.
Wakati akiwa juu ya usafiri akielekea
nyumbani kwa Jimmy, akamuona mtu,
hakumtilia manani pale alipomuona
mara ya kwanza, lakini akajikuta
akimuangalia yule mtu ambaye sasa
alikuwa akitembea kama mlevi. Macho
yake yakavutika kumuangalia mtu yule
tena na tena. "Masimba!? Yalikuwa
maneno pekee kutoka kinywani
kwake. Kilichofuata ni kuufungua
mlango ili kushuka,lakini ya kufanya
hivyo akaliona gari, gari ambalo hapo
mwanzo aliliona karibu na nyumbani
kwake. Hapo akagundua alikuwa
akifuatiliwa. Mawazo yakumfuatilia
yule mtu mlevi yakaisha. Alimtambua
kuwa mtu yule ni Masimba.
Alimtambua kwa urahisi kwa kuwa
alimjua masimba.
******
Aliendesha gari mpaka maeneo ya
Ambience club, akaipaki gari na
kushuka kisha kuongoza moja kwa
moja mpaka ndani ya ukumbi.
Akatafuta sehemu nzuri ya kukaa.
Katika kuangaza kwake akaiona meza
moja ikiwa tupu. Akasogea hapo,
akavuta kiti nakukaa. Baada ya kukaa
hapo, mhudumu akasogea na
kumuuliza kinywaji gani ambacho
angetaka kutumia. Teddy akamjibu na
baada ya hapo akaendelea kutulia
akiwaza na kuwazua kile alichokiona
kule njiani. Masimba akiyumba njiani,
masimba akitembea katika aina hii ya
ulevi? Kuna nini kimemtokea Masimba?
Kuna nini kimetokea nyuma ya hiki
anachokifanya masimba? Ina maana
kuna hili tu ama kuna kingine nyuma?
Mawazo yake hayo yakakatizwa na
mtu aliyemuona akiingia. Huyu alihisi
kumuona mahala, wakati akiendelea
kuangalia hilo akamuona mtu
mwingine akiingia. Huyu alikuwa
amejibadilisha sana. Licha kujibadilisha
huko lakini alimjua licha ya
kujibadilisha kwake. HUYU ALIKUWA
MASIMBA
No photo description available.

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 019
Licha ya kujibadilisha sana, licha ya
kuonekana kama mtu mwingine, lakini
kwa teddy haikuwa hivyo. Alimjua
Masimba, alimjua kama alivyokuwa
akiujua mwili wake. Akayahamisha
macho yake sasa akimtizama mtu yule
aliyeingia. Mtu ambaye aliwahi
kumuona sehemu, mtu ambaye
uingiaji wake ulikuwa wa kinamna
fulani. Bado mtu yule alikuwa
amesimama akiangaza kama mtu
mwenye kutafuta kitu. Hilo lilimpa
uhakika kuwa kijana yule alikuwa
akimtafuta yeye, lakini hili la kufika
pale kwa masimba nalo hilo kiasi fulani
likakipa kichwa wakati mgumu wa
kufikiria. Muda mfupi alikuwa
akitembea kama mlevi akiyumba,
lakini muda huu hakuwa yule wa
kuyumba. Na alifika pale akiwa
mwingine. Jibu lake lilikuwa moja tu,
jibu lake lilikuwa ni kwamba, masimba
alimuona wakati anaondoka na ile gari,
masimba alikuwa karibu na nyumbani
na inawezekana masimba alishuhudia
kila kitu kilichotokea. Hilo likausisimua
mwili wake, alijikuta tabasamu matata
likichanua usoni mwake. Lakini licha ya
tabasamu hilo, macho yake
hayakuganduka kumuangalia kijana
yule. Alikuwa akimtizama kwa uhuru
kutokana na uwepo wa kiza sehemu
alipokaa. Kijana yule baada ya
kuangaza huku na huko bila kuona
kitu, akatoka ndani ya ukumbi
akionyesha kuelekea sehemu za nje.
Bado Teddy alijipa subira. Alitaka
kuhakikisha kama kuna watu wengine
ama. Licha ya kuvuta subira kwa dakika
mbili, hakumuona mtu yeyote akitoka
kumfuata kijana aliyetoka. Hilo
likamfanya atake kusimama kuelekea
huko, lakini kabla ya kufanya hivyo
alitaka kumuangalia masimba kama
alikuwepo ama lah! Akafanya hivyo,
lakini hakumuona masimba, akaangaza
tena na tena lakini bado hakumuona
Masimba Akainuka naye akielekea nje
ya ukumbi wa club. Alitembea
akidance kufuata midundo ya muziki
uliokuwa ukiporomoshwa. Alipotokea
nje, macho yake yakapokewa na
makelele ya watu wakionekana
kupagawa. Hilo likamvutia, akaamua
kuelekea kule zinapotokea kelele.
Muda wote mikono yake ilikuwa tayari
kwa chochote ambacho kingetokea.
Akafanikiwa kujipenyeza katikati ya
umati na kusogea mpaka mbele kabisa.
Mwili wake ukamsisimka baada ya
kuuona mwili wa mtu ukiwa umelala
kifudifudi huku sehemu ya mgongoni
kukiwa na mpini wa kisu kuonyesha
mtu yule alikuwa amechomwa.
Akasogea zaidi na zaidi mpaka karibu
kabisa. Alikuwa yule yule kijana
aliyetoka ndani muda sio mrefu akiwa
amelala katikati ya dimbwi la damu.
Hilo likamshangaza, katika yote
aliyoyategemea hakuwaza kama mtu
yule angeuawa kwa aina ile. Swali
likabaki kwake ni nani aliyemuua
kijana huyu? Swali hilo likamfanya
arudi tena ndani ya Club, kurudi
kumuangalia masimba kama yupo ama
lah. Alitaka kwenda kumuangalia
masimba. Kitendo cha masimba
kuingia na kijana yule, kisha muda
mchache mtu huyu auawe katika
namna hii! Hapo akajua kuna kitu.
Teddy akahisi akili yake ikishindwa
kufanyqkazi. Mambo yaliomtokea siku
hii ya leo yalikivuruga kichwa chake,
alitakiwa kutulia kwanza, alitakiwa
kuituliza akili yake kwanza. Alitambua
anapitia katika wakati mgumu na
wahatari sana. Akaingia tena ukumbini
safari hii akiwa makini tofauti na
mwanzo. Macho yake yalimtizama kila
mtu, yakamdadisi na kumchunguza.
Muziki bado ulikuwa ukiporomoshwa,
watu walikuwa wakiserebuka
pasipokujua chochote kilichotokea nje.
Akajimwaga katikati akinengua kwa
staili hatari sana. Alikuwa akisakata
katika staili ambayo ilisababisha macho
kadhaa ya watu wamtizame na
wamuangalie. Wanaume wa kwale
walianza kukitamani kiuno cha teddy.
Kule kukata kiuno na kwenda mpaka
chini kiliwafanya watu wa wehuke.
Sasa vitu havikalika.
Hilo halikuwastaabisha hao tu, hata
masimba aliyekuwa amebana pembeni
alikuwa akimtizama mama watoto
wake akikizunguusha kiuno. Hata pale
alipokuwa akienda mpaka chini bado
macho yake hayakuamini. Ni kweli ni
mume mtarajiwa wa teddy, nikweli
anaishi na Teddy lakini hakuwahi
kufikiria kama ni mtamu kiasi hiki
katika kudance, hakufikiria kama ule
utamu wa kitandani una utamu
mwingine. Hakumwangalia teddy tu,
macho yake yaliangaza kila upande
akiutizama usalama wa mwanamke
huyu. Alitizama kama ataona hila
zozote lakini hakuziona.
*********
"Haiwezekani, nasema tena
haiwezekani!!!" Ilikuwa sauti ya jimmy
lambert ikinguruma katika chumba
kimoja chenye watu wasiopungua
watano. Alikuwa amechukia kupita
kiasi. Mishipa ilikuwa imemtoka usoni
huku mikono yake ikiwa imekunjwa.
Alikuwa akitoka upande huu wa
chumba kwenda upande ule. Alikuwa
amechanganyikiwa vya kutosha.
Taarifa kuwa Masimba ametoroka
akiwa chini ya ulinzi wa Idara ya
Usalama wa Taifa ilimchanganya sana.
Hakuitegemea hiyo taarifa,
alichokitegemea kilikuwa ni
kupatikana kwa mzigo wao ambao
uliibiwa na Masimba. Lakini hazikuwa
taarifa hizo, hazikuwa taarifa nzuri
kwake.
"Mtu anatoroka chini ya usalama wa
taifa? Mtu anatoroka pasipokuua? Mtu
ambaye anaishi na mamilioni ya pesa
yetu. Kwa nini asingeuawa tu?
Aliendelea kufoka huku akiendelea
kuzunguka mle chumbani. Wajumbe
wengine walikuwa kimya
wakumuangalia. Hakuna ambaye
aliinua kinywa chake kumjibu kitu
chochote. Kila mmoja alikaa kimya
akifikiria jinsi ya kujinasua katika hili.
"Tumemkosa Masimba, na mpaka sasa
hajulikani aliko, pia nina mashaka
teddy amegundua kitu kutoka kwetu.
Ameonekana Ambience club akicheza
na akionekana ni mwenye furaha sana.
Yaani sisi tunaumiza vichwa huku,
mwenzetu anafurahi huk.... alikatizwa
na mlio wa simu yake ikiitakuonyesha
kwamba alikuwa akipigiwa. Aliichomoa
mfukoni kabla ya kupokea akaangalia
jina la mpigaji. SILENT KILLER
lilisomeka Jina juu ya kioo cha simu
yake. Jimmy akasita kuipokea simu.
Hakujua kwa nini lakini alihisi haikuwa
simu ya usalama. Macho yake yaliwaka
mithili ya paka, pia alikuwa
akiwatizama wajumbe wenzake
mmoja baada ya mwingine. Hata wao
walimtizama sura zao zikiacha
maswali, sura zao zikiachwa na
mshangao. Hata simu ilipokatwa na
mpigaji kurudia tena ndipo Jimmy
akakurupuka na kuipokea. Hakuongea
kitu kingine zaidi ya kuitoa simu sikioni
na kuwageukia washirika wenzake.
Huku midomo ikimtetemeka kwa
hasira akajiondoa pale na kusogea
kisha kujibweteka Juu ya kitu.
"Saidi Mbega ameuawa muda huu
katika mazingira ya kutatanisha, nje ya
Ambience Club. Vijana wetu waliweka
mtego wa kumnasa Teddy lakini kabla
hawalifanya hilo, wakapewa taarifa za
kifo cha mwenzao. Aliongea Jimmy
akionyesha kuchoka kimwili, kiakili
mpaka kimawazo.
Ilikuwa taarifa iliyopokelewa kwa
mshtuko na wajumbe wale.
Walitambua kuwa wanatakiwa kufanya
kazi usiku na mchana kufanikisha kujua
pale alipo masimba.
********
Sauti za mbwa zilikuwa pekee
zikiosikika usiku ule, hapakuwa na
sauti ya binadamu katika eneo lote.
Ukimya ulikuwa umechukua sehemu
kubwa ya sehemu yote ya mikocheni.
Hilo halikumsumbua sana Teddy,
alikuwa hapo kwa kazi moja, kazi ya
kuonana na Jimmy. Kuongea na Jimmy
sambamba na kujibiwa maswali yake.
Ukimya wa eneo na giza la usiku
vilimsaidia teddy kuifikia nyumba ya
Jimmy pasipo kizuizi chochote. Hata
alipozunguka kwa kupita kwenye vivuli
vya miti bado hapakuwa na kizuizi.
Bado hakupata ugumu wowote. Hilo
likamfanya apate mashaka. Mashaka
ambayo yalimfanya ajiulize swali.
Wako wapi walinzi wa Jimmy? Kabla
hajapata majibu Akahisi kitu cha baridi
kikimgusa kisogoni. TULIA HIVYO
HIVYO...
May be an image of 1 person

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 020
Kitu cha Baridi kikagusa kichwani, kisha
sauti nzito ikafuatia.. TULIA HIVYO
HIVYO. Teddy akatulia kama
alivyoamliwa. Akili yake ilitakiwa
kufanyakazi zaidi ya uwezo wake.
Alitakiwa kufanyakitu ambacho
kingemtoa sehemu ile. Akatii na
kutulia zaidi na zaidi. Hakutaka kuwa
kondoo kufuata kila anachoambiwa.
Mikono ilikuwa juu kuonyesha kutii
amri. Sauti ikaamrisha tena, safari hii
sauti ikimwambia atembee kuelekea
kule ilipo nyumba ya Jimmy Lambert
bila kugeuka nyuma. Ni kweli teddy
hakugeuka, ni kweli teddy aliongoza
kuelekea alipoambiwa. Muda wote
alitembea akicheza na kivuli cha mtu
wa nyuma yake, mtu ambaye
alimshikia bastola. Hatua ya kwanza
mpaka ya tano zilipotea pasipokufanya
kitu, sio kama hakupenda, sio kwanba
hakutaka kufanya, alitaka na alitanani
sana, lakini bado umbali ulikuwa tatizo,
wakati wakiianza hatua ya sita, teddy
akakisikia kishindo na ukelele kutoka
nyuma yake. Akakumbuka kutakiwa
kutokugeuka, hakugeuka.. lakini hatua
moja nyingine akagundua kutokukiona
kivuli cha mtu ambaye alikuwa nyuma
yake. Hilo likamfanya ageuke sasa..
akageuka.. Cha kwanza kukiona ni
mwili wa mtu uliolala kuonyesha kuwa
haukuwa na uhai. Hilo
halikumshangaza sana, alijua Masimba
alikuwa nyuma akimlinda. Hilo likampa
uhueni na moyo wa kusonga mbele.
Alikuwa ameamua Kumuona Jimmy
Lambart. Hakuwa na hofu lakini
hakutaka kujiamini tena. Muda wote
alitembea akiwa makini kwa kila
hatua. Alitaka kuzijua mbivu na mbichi.
Hakuhofia na wala hakuogopa. Muda
mfupi alikuwa nyuma ya uzio wa
Jumba la Jimmy. Kwa kuwa alilijua lile
jengo kwa undani zaidi, akaamua
kuingia kwa kuruka uzio. Muda mfupi
alikuwa akitua ndani bila kutoa
kishindo. Kutoka hapo akachapuka
mpaka pembeni mwa mlango wa
kuingilia ndani kabisa. Hapo akatulia
kwa muda kusikiliza kama kuna mtu
yoyote, lakini bado ukimya ulimpa
majibu kuwa hapakuwa na mtu.
Akaunyoosha mkono wake mpaka
sehemu ya chini ya mlango. Akagusa
sehemu na bila kuchelewa mlango
ukajifungua. Baada ya mlango
kufunguka, akaichomoa bastola yake
na kuingia ndani kwa tahadhali kubwa.
Mdomo wa bastola ulikuwa
umetangulia mbele tayari kwa kufanya
kazi. Bado hapakuwa na sauti za kitu
chochote ambacho kingemtambulisha
uwepo wa watu ndani ya jumba lile.
Kimya kilichukua nafasi yake, kimya
kilichofanya Teddy aendelee kusogea
na kusogea. Akavipita vyumba viwili
pasipokusikia chochote kile. Hilo
likamfanya aamini kuwa Jimmy
hakuwepo hapo ndani. Alimtambua
jimmy awapo nyumbani huwa mtu wa
kupendelea muziki. Ukimya huo
ulimaanisha kwamba hapakuwa na
mtu ndani ya jengo hilo. Akaendelea
kusonga mbelembele. Mdomo wa
bastola ukiendelea kutangulia mbele.
Akaukuta ukumbi ambao mara nyingi
waliutumia kwa mikutano. Hapo bado
macho yake hayakukiona kitu. Bado
hakufanikiwa kumuona yoyote. Bado
ukimya uliichukua sehemu kubwa.
Bado akaivuta subira, bado aliitaka
subira tayari kumsubiri, lakini hilo
likapotea baada ya kuusikia mngurumo
wa gari kutoka nje, kisha kuishia hapo
hapo pasipokuendelea. Akaamini kuwa
Huyo alikuwa Jimmy, hata sauti ya geti
kufunguliwa ilipopenya masikioni
mwake, alitambua kuna mtu alikuwa
akiingia. Mawazo kuwa Jimmy ndiye
yalikuwa asilimia themanini. Akajivuta
mpaka karibu na mlango wa kungilia
ndani kwa upande wa mbele ya
nyumba. Hapo akatulia akiisubiri hatma
ya mtu huyo.
Haukupita muda akakiona kitasa
kikitingishwa kisha mlango
kufunguliwa. Watu watatu wakaingia
bila wasiwasi. Lakini Jimmy hakuwa
mmoja mmoja wao. Hawa walikuwa
wengine, hawa walikuwa wageni
kwake. Kwa kuwaangalia walikuwa
wageni kabisa. Akaendelea
kuwatizama vijana wale. Aliwaangalia
katika utulivu mkubwa. Kutokuwepo
kwa Jimmy kulimshangaza sana.
Haikuwahi kutokea Jimmy
kuwatanguliza watu nyumbani kwake
bila yeye mwenyewe kuwepo.
Aliwatizama watu wale
walivyojibweteka pale sebuleni,
moyoni akacheka. Alitabasamu na hata
kufurahi. Alikuwa na uwezo wa
kuwamaliza kwa risasi, alikuwa na
uwezo wa kufanya chochote, lakini
hakutaka kufanya hivyo. Alihitaji subira,
ni subira ambayo ingemkutanisha na
Jimmy. Ni kweli, katika muda ule ule
akamuona Jimmy akiingia sambamba
na mwanamke. Aliwatizama
walivyokuwa wakitembea. Alikuwa na
uwezo wa kuwapiga risasi kwa urahisi,
lakini hakupenda kufanyq hivyo.
Wakati Jimmy na mwanamke yule
wakitembea kuelekea sebuleni. Jambo
jingine la kuustajabisha kama sio
kushangaza likatokea. Nyuma ya
Jimmy na mwanamke yule, akamuona
masimba naye akitokea. Akitokea
akitembea kikawaida kana kwamba
alikuwa akiingia nyumbani kwake. Hili
nalo likimfurahisha, hili nalo likamfanya
sasa asitishe kufanya chochote
aendelee kumshangaa Masimba.
Ilikuwa pichq nzuri iliovutia kuitazama.
Hata pale jimmy alipokuwa
akijibweteka ndipo nadhani alimuona
masimba. Mshtuko alioupata Jimmy
baada ya kumuona masimba ndani ya
nyumba yake, iliwafanya vijana wake
waipeleke mikono yao mifukoni mwao
tayari kwa kutoa bastola.
Hakuna aliyeujua wepesi wa masimba,
hakuna aliyejua ni muda gani masimba
alitumia, lakini wote wakajikuta
wakimtizama mwenzao ambaye
alikuwa akigalagala chini baada ya
kulimwa shaba ya kifua. Hakuna
aliyeamini, Jimmy ndio hakuamini
kabisa. Macho yake yalimtoka mishipa
ya usoni ikaonekana. Midomo miwili ya
bastola ilikuwa ikimtizama. Masimba
hakuonyesha utani, macho yake
yalikuwa yakiwaka na kuwaka. Jimmy
akatamani kuongea lakini sauti
haikutoka. Mate yalimkauka na
maneno hayakutoka kabisa. Alikuwa
akimsikia masimba lakini hakuwahi
kuonana naye. Leo alikuwa
akimuangalia, huku pia midomo miwili
ikimtizama.
"Jimmy nadhani kiburi chako cha kuwa
karibu na viongozi imekupa mamlaka
ya kujipa utawala katika nchi hii.
Unaonekana una nguvu kuliko Rais,
Makamu wake na Waziri mkuu.
Imekupa mamlaka ya kuua watu wasio
na hatia kwa sababu ya kufanikisha
biashara yako haramu. Asteria anakosa
gani hadi kumuua? Uchungu wa taifa
lake ndio kisa cha kumuua. Dada wa
Asteria na mumewe Godfrey Maboba
sambamba na mtoto wao, ni kosa lipi
wamefanya? Sasa leo nimekuja na
mimi. Nimechoka kutumiwa watu wa
Idara ya Usalama wa taifa. Nimechoka
kupambana na watu wengine kwa ajili
yako. Sasa nataka uniambie ukweli
kabla sijaruhus......... kabla hajamalizia
maneno yake mlango ukasukumwa
kwa nguvu, wakaingia watu watatu na
kuanza kuvurumisha risasi pale
alipokaa Masimba.. Lakini hazikumkuta,
bali zilipita na kutua kwa kichana
mwingine, yowe la Uchungu
likamtoka. Watu wale wakaendelea
kushambulia bila tahadhali. Hawakujua
Teddy alikuwepo pale, hawakujua
kwamba alikuwa nyuma yao tena na
Bastola mbili katika mikono yake, huku
vidole vikiwa kwenye trigger tayari
kwa Kuruhusu Risasi
No photo description available.

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 021
Hawakujua kwamba nyuma yao
alikuwepo teddy, tena akiwa na
bastola mbili mikononi, vidole viwili
vikiwa tayari kwenye trigger kuruhusu
risasi. Alikuwa akizihesabu sekunde,
hakutaka kufanya kwa haraka sana
kukifanya kile alichotaka kukifanya.
Sekunde ya kwanza ilipita wakati
kidole bado kikiwa kwenye kitufe cha
kuruhusu risasi. Hata sekunde ya pili
ikapita patupu pasipo kitendo
chochote. Lakini sekunde ya tatu
haikupita na kwenda bure, bastola
ikakohoa mara tatu mfululizo, risasi
zikatua na kupenya pale zilipoagizwa,
watu watatu walikuwa chini wakivuja
damu katika kuonyesha hawakuwa hai.
Kilikuwa kitendo mujarabu machoni
kwa Teddy, kitendi kilicho mfanya
atabasamu. Aliipenda damu, alipenda
kuiona ikitoka mwilini kwa mtu na
aliihusudu zaidi pale yeye awapo
chanzo cha kutoka kwa hiyo damu.
Hakutoka pale kwa haraka, bado
aliendelea kutizama pale alipoangukia
Jimmy. Bado alitaka kuitumbukiza
Risasi katika kichwa cha mtu huyu.
Licha ya kuangalia sana lakini
hakuonekana, hakumuona Jimmy na
kibaya zaidi hakumuona Masimba na
hatq mmoja kati ya wale watatu
walioingia. Sebule ilikuwa kimya,
ukimya wa kuonyesha hapakuwa na
mtu. Hilo likamfanya auvute muda, hilo
likayafanya macho yake yawe makini
kwa kila kitu. Bastola mbili bado
zilitangulia mbele. Lakini ukimya nao
bado uliendelea kutamalaki. Sasa
alikuwa ameamua kujitokeza,
kujitokeza kuangalia zaidi na zaidi,
ikiwezekana aondoke kabisa. Lakini
wazo hilo likapingwa na hisia zake,
bado hapakuwa na usalama wa yeye
kujitokeza. Akaangaza macho yake
pembeni kama ataona chochote cha
kumsaidia, akakiona kisadolini kidogo
ambacho kilionekana kama kimejaa
maji. Akainama na kukichukua, baada
ya hapo akajaribu kukitupa upande
mwingine kama angeweza kugundua
chochote, lakini haikuwa hivyo... Bado
ukimya uliendelea kuwepo. Hilo
likampa uhakika kwamba hapakuwa na
watu eneo lile. Akaipiga hatua ya
kwanza na ya pili, alipotaka kupiga
hatua ya tatu akasikia yowe likitokea
nyuma yake. Yowee lililofuatana na
mgugumio wa maumivu kutoka kwa
mtu. Hakutaka kugeuka kuangalia,
kugeuka kwake nyuma kungesaidia
kupigwa Risasi iwapo angekuwepo
mtu wa kufanya hivyo. Alichokifany
yeye ni kuchupa na kuangukia
pembeni. Akatulia akiangaza huku na
huko. Bado ukimya ulichukua nafasi
yake. Hapakuonekana kama kuna tukio
kutokana na ukimya. Hapakuonyesha
kuwepo kwa mtu. Nani amelifanya
tukio lililopita muda mfupi? Masimba!
Ndiye mtu pekee wa kulifanya hili,
lakini amekalia wapi? Mbona Jimmy
haonekani, nani amepigwa risasi
nyuma yangu? Amepigwa na Masimba
au na mtu gani? Kabla hajalipata jibu
bastola ikagota tena kwa mara ya pili
kisogoni. Tofauti ya huyu na yule wa
mwanzo, huyu hakuongea kitu.
Aliendelea kuikandamiza bastola
kisogoni. Kabla hajakaa sawa,
akashikwa na kugeuzwa kwa nyuma.
Hapo akajikuta akitizamana uso kwa
uso na Masimba, Bastola yake ilikuwa
bado kichwani kwa teddy. Macho yake
yalikuwa yamebadilika kupindukia.
Sura yake haikuonyesha utani, sura
yake haikuwa na masihara. Teddy
akatulia akimuangalia masimba, alitulia
akihofu na kuwa na mashaka na
mabadiliko yale. Macho ya Masimba
hayakuonyesha ule utani. Macho ya
masimba yalimaanisha kitu kingine.
Akakiona kidole cha Masimba kikishuka
kwenye kitufe cha kuruhusu risasi.
Akauona uso wa Masimba ukiendelea
kubadilika. Hakuonyesha masihara,
hakuonyeshq utani, macho yake
yalisomeka kifo na sura yake
aliongelea mauti. Teddy bado alitulia,
bado alikuwa akiiomba toba. Alitulia
kuruhusu chochote, haikuwa hivyo
wala vile, bali ilikuwa hivi. Bastola
ilishushwa kisha bila kuambiwa
chochote akamuona masimba
akiondoka. Akiondoka huku akiachwa
yeye akiwa amesimama. Hakubaki
hapo, alikuwa nyuma akimfuata
Masimba. Alikuwa nyuma akimfuata
mpenzi wake. Hakuwa na wazo tena la
kukumbuka uwepo wa Jimmy.
*********
Chumba kilikuwa kimya, kila mmoja
alikuwa kimya akimtizama mwenzake
kwa utofauti. Wakati teddy akimtizama
masimba kwa staili ya nisamehe,
masimba alikuwa akimtizama kwa
staili ya nautaka ukweli. Uso wake
haukuwa na tabasamu, mishipa ya
hasira bado ilichukua sehemu kubwa
usoni. Sura ya Asteria, Godfrey Maboba
sambamba na familia yake, bado
zilikuwa usoni mwake. Kumuangalia
teddy kulifuatana na kumbukumbu ya
mtoto aliyelala mbele ya macho yake
akiwa na matundu mawili ya Risasi.
Mtoto ambaye hakuwa na hatia, mtoto
ambaye hakujua chochote kile aliuawa
kwa risasi. Chanzo kikiwa teddy. Ni
teddy huyu huyu aliyetaka kumuua
kule kigamboni. Kufikia hapo akaanza
kutembea kusogea pale aliposimama
teddy. Teddy bado hakusogea wala
hakurudi nyuma. Alisimama pale pale
akimuangalia masimba usoni.
"Kwa nini Umemuua Asteria na familia
yake?" Lilikuwa swali, swali ambalo
halikutarajiwa na teddy. Sio kutarajiwa
kwa kuwa alidhani masimba anajua.
Lilikuwa swali ambalo lilimshtua na
kumgutusha kupita kiasi. Ni kweli
alipewa amri ya kumuua Asteria, lakini
hakumuua yeye kwa kuwa alimfahamu
Asteria tokea wapo wote Ifakara.
Alimfahamu asteria kwa undani zaidi,
na hata familia yake aliijua. Ingawa
alipokea kweli amri lakini asingeweza
kumuua asteria na hata dada yake.
"Sikumuua Asteria wala familia ya dada
yake. Ni kweli amri ya kuua nilipewa,
lakini kabla sijatekeleza hilo
wakatumwa watu wengine wakaua ili
nionekane mimi ndio nimefanya.
Kuhusu familia ya dada yake sikuhusika
na chochote kwa kuwa tukio lililotokea
mjimwema Kigamboni lilinichanganya
baada ya kugundua kuwa gari yetu
ndio imelipuliwa na wewe ukiwemo
ndani yake. Hilo likanifanya nirudi tena
kigamboni kuangalia uwezekano wa
kuuona mwili wako lakini sikuuona.
Hapo nikatambua kuwa hukuwepo
ndipo niliporudi nyumbani kukusubiri.
Teddy alimueleza Masimba kila kitu
kilichotokea, hata kuvamiwa na walinzi
binafsi wa taasisi nyeti. Hakuacha
kuongelea usaliti na kukubali kuwa
alikuwa tayari kusaliti.
"Nani Yupo nyuma ya mpango wenu
wa kutorosha madawa kutoka kwenye
mikono ya usalama? Aliuliza Masimva.
"Jimmy Lambert!" Akajibu Teddy
"Ukimtoa Jimmy?
"Yupo mtu mwingine mkubwa sana,
lakini mtu huyo anajulikana na watu
wawili tu." Akajibu teddy.
"Nani na nani wanamjua?
"Jimmy na suresh. Akajibu teddy
Lilikuwa jibu ambalo halikutegemewa
na masimba. Akamuangalia teddy zaidi
na zaidi, akihitaji ahakikishiwe kama
jibu hilo lina ukweli. Bado teddy
alimjibu pasipo na wasiwasi.
Alimhakikishia kwamba Suresh alikuwa
mmoja kati ya watu wanaomfahamu
mmoja ya vigogo waliokuwa nyuma ya
mpango huo. Akamuangalia Tena,
kisha kwa sauti tofauti akamuuliza.
"Unajua kuwa nilikamatwa na
kupelekwa makao makuu kabla
sijahamishiwa katika nyumba moja ya
siri inayomilikiwa na usalama wa
TAIFA?
"Mwanzo sikujua, lakini nilipowaona
walinzi wale nikajua hili suala
limepelekwa mamlaka nyingine. Nilijua
utakuwa umeharibu ama njama za
kukushurutisha uonyesha ulipo mzigo
wa madawa zinaendelea." Akajibu
Teddy.
"Upo tayari kuwa na mimi au bado
unaitaka pesa?
AKAULIZA MASIMBA HUKU
AKIMUANGALIA TEDDY USONI.
May be an image of 1 person

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 021
Hawakujua kwamba nyuma yao
alikuwepo teddy, tena akiwa na
bastola mbili mikononi, vidole viwili
vikiwa tayari kwenye trigger kuruhusu
risasi. Alikuwa akizihesabu sekunde,
hakutaka kufanya kwa haraka sana
kukifanya kile alichotaka kukifanya.
Sekunde ya kwanza ilipita wakati
kidole bado kikiwa kwenye kitufe cha
kuruhusu risasi. Hata sekunde ya pili
ikapita patupu pasipo kitendo
chochote. Lakini sekunde ya tatu
haikupita na kwenda bure, bastola
ikakohoa mara tatu mfululizo, risasi
zikatua na kupenya pale zilipoagizwa,
watu watatu walikuwa chini wakivuja
damu katika kuonyesha hawakuwa hai.
Kilikuwa kitendo mujarabu machoni
kwa Teddy, kitendi kilicho mfanya
atabasamu. Aliipenda damu, alipenda
kuiona ikitoka mwilini kwa mtu na
aliihusudu zaidi pale yeye awapo
chanzo cha kutoka kwa hiyo damu.
Hakutoka pale kwa haraka, bado
aliendelea kutizama pale alipoangukia
Jimmy. Bado alitaka kuitumbukiza
Risasi katika kichwa cha mtu huyu.
Licha ya kuangalia sana lakini
hakuonekana, hakumuona Jimmy na
kibaya zaidi hakumuona Masimba na
hatq mmoja kati ya wale watatu
walioingia. Sebule ilikuwa kimya,
ukimya wa kuonyesha hapakuwa na
mtu. Hilo likamfanya auvute muda, hilo
likayafanya macho yake yawe makini
kwa kila kitu. Bastola mbili bado
zilitangulia mbele. Lakini ukimya nao
bado uliendelea kutamalaki. Sasa
alikuwa ameamua kujitokeza,
kujitokeza kuangalia zaidi na zaidi,
ikiwezekana aondoke kabisa. Lakini
wazo hilo likapingwa na hisia zake,
bado hapakuwa na usalama wa yeye
kujitokeza. Akaangaza macho yake
pembeni kama ataona chochote cha
kumsaidia, akakiona kisadolini kidogo
ambacho kilionekana kama kimejaa
maji. Akainama na kukichukua, baada
ya hapo akajaribu kukitupa upande
mwingine kama angeweza kugundua
chochote, lakini haikuwa hivyo... Bado
ukimya uliendelea kuwepo. Hilo
likampa uhakika kwamba hapakuwa na
watu eneo lile. Akaipiga hatua ya
kwanza na ya pili, alipotaka kupiga
hatua ya tatu akasikia yowe likitokea
nyuma yake. Yowee lililofuatana na
mgugumio wa maumivu kutoka kwa
mtu. Hakutaka kugeuka kuangalia,
kugeuka kwake nyuma kungesaidia
kupigwa Risasi iwapo angekuwepo
mtu wa kufanya hivyo. Alichokifany
yeye ni kuchupa na kuangukia
pembeni. Akatulia akiangaza huku na
huko. Bado ukimya ulichukua nafasi
yake. Hapakuonekana kama kuna tukio
kutokana na ukimya. Hapakuonyesha
kuwepo kwa mtu. Nani amelifanya
tukio lililopita muda mfupi? Masimba!
Ndiye mtu pekee wa kulifanya hili,
lakini amekalia wapi? Mbona Jimmy
haonekani, nani amepigwa risasi
nyuma yangu? Amepigwa na Masimba
au na mtu gani? Kabla hajalipata jibu
bastola ikagota tena kwa mara ya pili
kisogoni. Tofauti ya huyu na yule wa
mwanzo, huyu hakuongea kitu.
Aliendelea kuikandamiza bastola
kisogoni. Kabla hajakaa sawa,
akashikwa na kugeuzwa kwa nyuma.
Hapo akajikuta akitizamana uso kwa
uso na Masimba, Bastola yake ilikuwa
bado kichwani kwa teddy. Macho yake
yalikuwa yamebadilika kupindukia.
Sura yake haikuonyesha utani, sura
yake haikuwa na masihara. Teddy
akatulia akimuangalia masimba, alitulia
akihofu na kuwa na mashaka na
mabadiliko yale. Macho ya Masimba
hayakuonyesha ule utani. Macho ya
masimba yalimaanisha kitu kingine.
Akakiona kidole cha Masimba kikishuka
kwenye kitufe cha kuruhusu risasi.
Akauona uso wa Masimba ukiendelea
kubadilika. Hakuonyesha masihara,
hakuonyeshq utani, macho yake
yalisomeka kifo na sura yake
aliongelea mauti. Teddy bado alitulia,
bado alikuwa akiiomba toba. Alitulia
kuruhusu chochote, haikuwa hivyo
wala vile, bali ilikuwa hivi. Bastola
ilishushwa kisha bila kuambiwa
chochote akamuona masimba
akiondoka. Akiondoka huku akiachwa
yeye akiwa amesimama. Hakubaki
hapo, alikuwa nyuma akimfuata
Masimba. Alikuwa nyuma akimfuata
mpenzi wake. Hakuwa na wazo tena la
kukumbuka uwepo wa Jimmy.
*********
Chumba kilikuwa kimya, kila mmoja
alikuwa kimya akimtizama mwenzake
kwa utofauti. Wakati teddy akimtizama
masimba kwa staili ya nisamehe,
masimba alikuwa akimtizama kwa
staili ya nautaka ukweli. Uso wake
haukuwa na tabasamu, mishipa ya
hasira bado ilichukua sehemu kubwa
usoni. Sura ya Asteria, Godfrey Maboba
sambamba na familia yake, bado
zilikuwa usoni mwake. Kumuangalia
teddy kulifuatana na kumbukumbu ya
mtoto aliyelala mbele ya macho yake
akiwa na matundu mawili ya Risasi.
Mtoto ambaye hakuwa na hatia, mtoto
ambaye hakujua chochote kile aliuawa
kwa risasi. Chanzo kikiwa teddy. Ni
teddy huyu huyu aliyetaka kumuua
kule kigamboni. Kufikia hapo akaanza
kutembea kusogea pale aliposimama
teddy. Teddy bado hakusogea wala
hakurudi nyuma. Alisimama pale pale
akimuangalia masimba usoni.
"Kwa nini Umemuua Asteria na familia
yake?" Lilikuwa swali, swali ambalo
halikutarajiwa na teddy. Sio kutarajiwa
kwa kuwa alidhani masimba anajua.
Lilikuwa swali ambalo lilimshtua na
kumgutusha kupita kiasi. Ni kweli
alipewa amri ya kumuua Asteria, lakini
hakumuua yeye kwa kuwa alimfahamu
Asteria tokea wapo wote Ifakara.
Alimfahamu asteria kwa undani zaidi,
na hata familia yake aliijua. Ingawa
alipokea kweli amri lakini asingeweza
kumuua asteria na hata dada yake.
"Sikumuua Asteria wala familia ya dada
yake. Ni kweli amri ya kuua nilipewa,
lakini kabla sijatekeleza hilo
wakatumwa watu wengine wakaua ili
nionekane mimi ndio nimefanya.
Kuhusu familia ya dada yake sikuhusika
na chochote kwa kuwa tukio lililotokea
mjimwema Kigamboni lilinichanganya
baada ya kugundua kuwa gari yetu
ndio imelipuliwa na wewe ukiwemo
ndani yake. Hilo likanifanya nirudi tena
kigamboni kuangalia uwezekano wa
kuuona mwili wako lakini sikuuona.
Hapo nikatambua kuwa hukuwepo
ndipo niliporudi nyumbani kukusubiri.
Teddy alimueleza Masimba kila kitu
kilichotokea, hata kuvamiwa na walinzi
binafsi wa taasisi nyeti. Hakuacha
kuongelea usaliti na kukubali kuwa
alikuwa tayari kusaliti.
"Nani Yupo nyuma ya mpango wenu
wa kutorosha madawa kutoka kwenye
mikono ya usalama? Aliuliza Masimva.
"Jimmy Lambert!" Akajibu Teddy
"Ukimtoa Jimmy?
"Yupo mtu mwingine mkubwa sana,
lakini mtu huyo anajulikana na watu
wawili tu." Akajibu teddy.
"Nani na nani wanamjua?
"Jimmy na suresh. Akajibu teddy
Lilikuwa jibu ambalo halikutegemewa
na masimba. Akamuangalia teddy zaidi
na zaidi, akihitaji ahakikishiwe kama
jibu hilo lina ukweli. Bado teddy
alimjibu pasipo na wasiwasi.
Alimhakikishia kwamba Suresh alikuwa
mmoja kati ya watu wanaomfahamu
mmoja ya vigogo waliokuwa nyuma ya
mpango huo. Akamuangalia Tena,
kisha kwa sauti tofauti akamuuliza.
"Unajua kuwa nilikamatwa na
kupelekwa makao makuu kabla
sijahamishiwa katika nyumba moja ya
siri inayomilikiwa na usalama wa
TAIFA?
"Mwanzo sikujua, lakini nilipowaona
walinzi wale nikajua hili suala
limepelekwa mamlaka nyingine. Nilijua
utakuwa umeharibu ama njama za
kukushurutisha uonyesha ulipo mzigo
wa madawa zinaendelea." Akajibu
Teddy.
"Upo tayari kuwa na mimi au bado
unaitaka pesa?
AKAULIZA MASIMBA HUKU
AKIMUANGALIA TEDDY USONI.
May be an image of 1 person

Story imetulia san.
 
Hivi kutupia sehemu nyingi za story mara moja ni sawa?
 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 022
"Tokea niliposhikiwa bastola na walinzi
wa Jimmy, nilishaamua kuachana nao.
Nilishaamua kuondoka katika kile
tulichokuwa tunakifanya. Nipo upande
wako tokea pale ulipokoswakoswa
kulipuliwa. Nilifadhaika sana kwa
kushindwa kugundua kile
kilichotendwa. Ulikuwa mpango wao
na hawakupenda kunishirikisha. Kule
kuuona ule mlipuko nikauona moyo
wangu ukiingia simanzi. Nipo na wewe
na nitakuwa na wewe mpaka mwisho
wa hili. Lakini nina hofu, wanaweza
kuniua Masimba." Aliongea Teddy
akimuangalia Masimba. "Lakini nina
hofu" lilikuwa neno lililojirudia
kichwani mwake. Teddy alikuwa ana
hofu, teddy alikuwa akiogopa,
akiogopa kitu gani? Lilikuwa swali
pekee kichwani kwa masimba.
Hakuwahi kumsikia popote teddy
akiwa na hofu ya kitu chochote.
Aliipenda damu na kuyapenda
mapigano. Hakuogopa kifo bali alikuwa
akipenda sana kuua. Lakini kwa nini leo
ana hofu? Hofi ya nini? Hofu ya kuuawa
ama? Hilo likamfanya masimba
amgeukie Teddy na kumuangalia.
Macho yake peker yalijenga maswali
lukuki kwenda kwa teddy. "Umeanza
lini kuogopa teddy, umeanza lini kuwa
muoga? Hukuogopa Tulipokuwa Syria,
uje uogope hapa, tena kwa watu wasio
na chochote kile. Unaweza kunieleza
kile unachoogopa?. Teddy alimuangalia
masimba kwa muda, alimuangalia kana
kwamba ndio alikuwa akimuona leo.
Kweli aliyapenda mapambano,
hakuiogopa damu na hakukiogopa kifo.
Lakini leo alikuwa akikiogopa kifo na
kuiogopa damu. Alijishangaa na
kutokujiamini. Teddy leo alikuwa
akikiogopa kifo? Lilikuwa jambo pekee
lililokisumbua kichwa chake. "Masimba
ingawa unawaona watu hawa si lolote
lakini ni hatari hasa kwa watu ambao
wapo nyuma ya mzigo uliouchukua.
Mtu huyo alie nyuma, ndiye mtu pekee
ninaye muogopa. Anaweza kuamua
chochote kwetu na tukapotea.
Unadhani ni mtu gani mwenye uwezo
wa kuruhusu mzigo kama ule
uchukuliwe kirahisi? Unadhani na afisa
gani mwenye uwezo huo? Aliye nyuma
ya tukio hili mi mtu mkubwa.
Tunaweza kupotea endapo
hatutakuwa makini. aliongea teddy
akiendelea kumuangalia masimba.
Hata masimba alinyamaza kwanza
akimuangalia Teddy. Alizidi
kushangazwa na uoga wa mwanamke
huyu. Uoga ambao hakuwahi
kuuonyesha huko mwanzo. "Teddy
tulipokuwa Syria tulikuwa
tukipambana na watu gani? Tulipitia
mangapi Teddy? Ni mara ngapi
tumenusurika kifo? Mbona huwa
muoga kama leo hii? Hiki
unachonionyesha leo ni tofauti?
Tuachane na uoga nataka kumjua huyu
mtu. Nataka kumfahamu usiku wa leo
ama kesho. Nataka nimfahamu kwa
njia yoyote. Suresh ndio atakaye
niambia. Lakini hata wewe naamini
unamjua mtu huyo. Inaonyesha kuna
kiapo umekula cha kutokutoa siri nio
maana unaogopa. Lakini kama wewe
unashindwa kuniambia mimi kwa
kuhofia kuuawa, basi mimi nitauawa
kwa kumtafuta na kumjua huyu mtu."
Aliongea masimba huku akionyesha
kutokuwa na masihara. Teddy akachwa
katika tafakuli zito, ni kweli aliogopa
na kuhofia. Ni kweli alimuogopa mtu
huyu, lakini atakuwa tayari kumuona
masimba akiuawa kwa sababu ya woga
wake? Yupo tayari kukisaliti kiapo kwa
ajili ya uoga wake? Hapana! Hapana!
Alijikuta akitamka maneno hayo kwa
sauti kubwa, sauti iliomtoa kwenye
uoga na kumpa ujasiri. Muda mfupi
alikuwa akibembea kwenye kifua cha
Masimba. Alikuwa tayari kupambana
bila kuhofia. Na moyo wake ulimtuma
kufanya hivyo pasipokuogopa.
*******
Moshi mzito ulikuwa angani ukipita na
kupenya kwenye matundu ya watu
mbalimbali kabla ya kutoka ndani ya
chumba kile. Chupa tatu za Jack Daniels
zilikuwa mezani zikitekezwa kama sio
kuteketea. Watu wanne walikuwa
wameizunguka meza hiyo
wakiendelea kuburudika tani yao.
Mwanaume alikuwa mmoja lakini
wanawake walikuwa watatu. Kila
mmoja alikuwa ana uhuru wa kuushika
mwili wa mwanaume yule pasipo na
masharti yoyote. Mwanaume naye
alikuwa akifurahishwa na vitendo
vyote. Akicheka na kuongea hili, punde
akamuona mtu mmoja akingia
chumbani hapo pasipo na taarifa. Mtu
huyu alikuwa akionekana akivuja jasho
sambamba na mavazi yake kuchafuka
kwa damu. Hilo likamfanya kinywaji
kilichopo mdomoni kumpalia.
Akaruhusu mshangao machoni mwake,
mshangao ambao haukudumu hasa
pale mtu yulr alipoanza kuvuta hatua
kusogea pale alipo. Bado macho
hayakuweza kuupoteza kabisa
mshangao ule. Hata pale mtu yule
alipoifikia meza yake ndipo
alipogundua kama kuna watu ambao
hawakupaswa kuwepo pale. Akawapa
ishara wanawake wale watoke. Hata
wao hawakuchelewa. Baada ya kutoka
kwa wanawake wale, sasa alikuwa
akimtizama mtu huyu. Hakuwa
mwingine bali alikuwa Jimmy
Alikuwa Jimmy akionyesha kulowa
damu.
Jimmy alikuwa na hofu kubwa Moyoni,
machoni na hata uso wake uliongea
hofu. Alikuwa akitetemeka
kanakwamba ametoka kunyeshewa
mvua, alitetemeka kanakwamba ndani
ya chumba kulikuwa na baridi kama ya
Arusha na Hata mbeya. Hilo lilikuwa
geni kwa Suresh, hilo lilikuwa geni
machoni mwa kijana huyu mwenye
asili ya India. Jimmy amelowa damu na
tena alikuwa akitetemeka!! Jimmy leo
alikuwa na hofu? Jimmy leo alikuwa
akiogopa? Hilo likawa gumu kwa
mhindi yule kulikubali. Bado mhindi
yule alimuangalia Jimmy Kwa
wasiwasi. Akainua glass na kupiga
mafunda matatu kisha kuirudisha pale
pale. Alimjua Jimmy kindani, alimjua
jimmy kimipango na hata kimapigano,
jimmy hakuwahi kumuogopa mtu,
hakuwa kutetemeshwa na mtu, leo hii
Jimmy alikuja akitetemeka tena huku
amelowa Damu. Nani amelifanya hili?
Teddy? Hapana! Teddy hawezi kufanya
kitu kama hiki. Bado hakutaka kuamini
kile alichokuwa akikiwaza. Maswali
yake mengi sana yalikosa majibu kwa
kuwa mtu mwenyewe wa kumjibu
alikuwa kimya. Alikuwa kimya kama
bubu ama zuzu. Hilo likamfanya Mhindi
yule kusimama. Akapiga hatua huku
akiyumba huku na huko kumfuata
Jimmy. Sasa alimkaribia kwa karibu
sana. Akamuangalia kwa umakini wa
hali ya juu. Akashangaa kumuona
Jimmy akiwa hana hata kovu, akiwa
hana hata jeraha la kucha. Hilo
likaendelea kumshangaza. Hilo
likaendelea kumuweka njia panda.
Akataka kuinua mdomo kuongea kitu,
lakini hakufanikiwa kufanya hivyo
kwani muda ule ule Teddy alikuwa
akiingia pale katika mwendo wa twiga
nyikani. Alikuwa akitembea na kunesa
huku na kule, macho yake yakiangalia
hapa na kucheki kule. Ulikuwa
mshangao wa mhindi yule uliomshtua
Jimmy na kumfanya naye ageuke
kuangalia kule mlangoni.
Ndio aligeuka, na akakiona kilichopo
nyuma yake midomo ikamkauka
jimmy. Hofu ikaongezeka maradufu.
Akataka kurudi nyuma lakini akajikuta
miguu ikiwa mizito. Miguu haikuweza
kusogea popote. Yule mhindi mkono
ulishashuka tayari kwa kuichomoa
bastola yake. Lakini jicho alilotazamwa
na Teddy,. Likaufanya mkono wake
uondoke hapo haraka. Teddy
akaendelea kutembea zaidi na zaidi,
alikuwa makini kwa kila hatua
aipigayo. Masikio yalikuwa yakinasa
kila mchakato hata kama ulikuwa wa
sisiminzi. Akasimama hatua mbili
kutoka waliposimama Jimmy na
Suresh. Macho yake yalikuwa
yakimtizama mmoja mmoja pasipo
kuongea chochote kitu. Bado Mhindi
yule akashangazwa na hali ile, bado
Mhindi yule hakuamini kama Teddy
anaweza kufanya kile anachokifanya
pale.
"Nimekuja kuuliza mgao wangu kutoka
kwenye ule mzigo." Aliongea teddy
akizidi kuwatizama. Licha ya hilo swali
lakini hapakuwa na aliemjibu. Wote
walikuwa kimya.
"Naondoka siku nitakayokuja tena
naomba niukute mgao wangu,
kinyume na hapo nitaondoka na Roho
zenu." Baada ya kuongea maneno hayo
teddy akageuka akiondoka kwa
mwendo ule ule. Mpaka unapotelea
mlangoni, si Jimmy wala Suresh
aliyeongea kitu. Wote walikuwa kimya.
Jeuri ya Teddy ilipitiliza. Uso wa Jimmy
sasa Ulibadilika kabisa. Mishipa ya
Hasira ilionekana waziwazi.
"TEDDY LAZIMA UFE, LAZIMA
TUKUONDOE HAPA DUNIANI."
akanong'ona Jimmy Kwa Sauti ya Chini.
"Yeah, lazima afe lazima tumuue.
Kinyago tulichokitengeneza wenyewe
hakiwezi kututisha. Sasa ameitangaza
vita na hatafika popote tutamzima.
Maelezo ya picha hayapo.

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 023
******
Muziki ulikuwa ukisikika kwa mbali
ukitokea ndani ya nyumba moja kubwa
maeneo ya mbezi beach. Taa
nyekundu zilikuwa zikiwaka kuonyesha
kuwa ulikuwa usiku thabiti, usiku wa
mahaba na usiku wa mapenzi.
Mwanamke alikuwa katika vazi jepesi
la kulalia ambalo hili lilimuonyesha
mpaka nguo yake ya ndani aliovaa.
Mkononi alikuwa na glass ya mvinyo
mwekundu huku pembeni yake
kukiwa na bastola. Muda wote alikuwa
akiitizama saa ya ukutani kanakwamba
ndio kwanza alikuwa akiitizama. Kila
baada ya sekunde alikuwa akiitizama
saa yake ya ukutani. Akaonyesha
kukerwa na kitu, muda mfupi
alinyanyuka na kuliendea pazia la
dirishani. Alipolifikia akalifunua kisha
akaanza kutupa macho yake nje
akiangalia uzuri wa jiji la dar es salaam.
Alisimama hapo kwa muda wa dakika
kama mbili akitizama nje. Alionekana
akimsubiri mtu, mtu ambaye alikuwa
mpenzi wake ama hawara. Lakini bado
muda ulizidi kwenda bila kumuona
huyo mtu. Akiwa ameanza kukata
tamaa akaliona gari nyeusi ikisogea
taratibu ikielekea uelekeo wa kwake.
Moyo wake ukachanua kwa tabasamu
safi. Bado aliuvuta muda akiitizama
gari ile ikiendelea kusogea. Punde
mkono wake wa kulia ukapanda
mpaka juu ya titi lake lake la kushoto.
Akaishika chuchu na kuanza kuichezea
polepole. Mara akaisikia honi ikitokea
kwa nje. Akashuka taratibu kwa
mwendo wake wa mapozi. Mtoto wa
kipare alitembea kama analazimishwa.
Alikuwa mwamvita Rajabu. Alikuwa
hapo kwa minajili ya kuuburudisha
mwili wake. Akaufungua mlango
akaelekea huko kulifungua geti. Ni
wakati akilifungua geti akashangazwa
na kitu ambacho alikiona. "DAMU" Ndio
neno pekee kumtoka mdomoni kwake.
Kwenye mlango wa gari la mtu wake
ilionekana damu ikichuruzika. Damu
ikitoka ndani ya gari na kudondokea
sakafuni. Hakulitegemea wala
kulitarajia. Hilo likamfanya aduwae
kwa sekunde kadhaaa akishindwa
kufanya maamuzi. Hakuliwaza hilo,
mwili wake uliwaza mapenzi, moyo
wake ulihitaji kuburudishwa, lakini
mbona damu tena? Hilo likamuondoa
katika mawazo. Punde bastola yake
ilikuwa mkononi akijivuta kuelekea
garini. Macho yakizunguka mfano wa
bundi alizidi kusogea. Akaufikia mlango
kisha kuushika. Kwa kasi ya umeme
akaufungua mlango...
"Mamaaaa" kwa mara ya kwanza
Mwamvita akapiga yowe huku mwili
wake ukimtetemeka. Mbele ya macho
yake alikuwa akiiutizama mwili wa
mpenzi wake ukiwa ukiwa umelalia
usukani wa gari huku kichwa kikiwa
hakitamaniki kutokana na kufumiliwa
kwa Risasi. Akashikwa na woga,
akaogopa na kutaka kurudi nyuma.
Lakini akajipa utulivu, kukimbia
haikuwa suluhu ya hiki kinachotokea.
Alitakiwa kulijua tatizo, alitakiwa kujua
nani ambaye amefanya mauaji haya.
Akaendelea kuuangalia mwili wa
mpenzi wake, damu ilikuwa ikiendelea
kuvuja. Akaizunguka gari akiutafuta
kila upande. Hakumuona mtu, ingawa
hakumuona lakini akakiona kitu
ambacho kilimpa hisia tofauti. Hii
ilikuwa magazine ya risasi. Kwa nini
magazine? Na kwa nini iko hapa? Ina
maana hakuuawa hapa? Kama
hakuuawa hapa, nani alikuja na hii gari
hapa? Haya yalikuwa maswali, maswali
ambayo bado hakupata jibu. Wakati
akiendelea kujiuliza, mara akaiona gari
nyingine ikija na uelekeo ule. Uelekeo
wa nyumbani kwake. Akarudi na
kujitupa uvunguni mwa gari. Ujaji wa
gari ili ulimshtua sana. Akatulia pale
uvunguni akiangaza macho kuelekea
kule mbele. Bastola ilikuwa mkononi
mdomo ukiitizama gari ile. Kidole
kilikuwa tayari kwa kuiruhusu risasi
akaamua kuivuta subira. Gari ile
ikaendelea kusogea na kusogea.
Hakuendelea tena baada ya kufika
hatua sita, gari ikasimama kisha taa
kuzimwa. Ukimya wa ajabu ukatokea.
Hakushuka MTU kutoka kwenye gari na
hapakuwa na dalili yoyote ya kushuka
kwa MTU. Hata yeye akatulia akitaka
kukiona kile kitakachotokea. Baada ya
ukimya wa dakika mbili akauona
mlango wa gari ukifunguliwa. Punde
akashuka MTU ambaye alimtambua.
MTU ambaye alimjua. Licha ya
kumtambua lakini hakujitokeza. Bado
hakuamini MTU na bado hakutaka
kumuamini. MTU aliyeshuka alikuwa
Jimmy . Hata pale alipoanza kusogea
pale kwenye gari bado Mwamvita
hakujitokeza. Bado alivumilia kuuona
mwisho. Jimmy alikuwa amesogea na
sasa alikuwa ameikaribia gari, macho
yake yakakiona kitu mfano wa maji
yakichuruzika kutoka ndani ya gari.
Hakuwa mgeni wa maji Yale, na
hakuwa mwepesi wakuamini kwamba
yalikuwa maji. "Damu" ndio neno
lililogonga kichwani. Wakati huo huo
mkono wake ukashuka kiunoni na
kuchomoa bastola yake. Akaendelea
kusogea kwa hatua za mashaka.
Akaufikia mlango ambao ulikuwa wazi.
Macho yake yakatua juu ya mwili wa
binadamu uliofumuliwa kichwa kwa
risasi, akahisi baridi ikimuingia, baridi
ya woga na fadhaa. Aliogopa na
kuogopa. Hakuwahi kukiona kifo cha
aina ile. Ni hapo alipokumbuka kuwa
Mwamvita alikuwa ndani ama naye
atakuwa ameshauawa. Akaliendea geti
na kujaribu kulisukuma. Geti likamtii.
Akaingia ndani sasa akiwa ameuvaa
ujasiri. Hakuwa muoga tena. Akaanza
kuzikwea ngazi kuingia ndani kabisa ya
jengo. "Jimmy nipo huku." Ilikuwa sauti
iliomfanya Jimmy ageuke kwa kasi ya
umeme huku bastola mkononi. Hata
alipomuona Aliyemuita hakuishusha
bastola. Alikuwa akimuangalia
Mwamvita kwa mashaka. Mashaka
yakutokumuamini kwa kile alichokiona
nje. Hakuwahi kuona Unyama wa aina
ile. Kwa Mara ya kwanza akauona
Umuhimu wa kuongeza watu.
Hakuwahi kufikiria hilo.
*********
Alikuwa akiishi kama mwizi kama sio
kibaka. Muda wote alikuwa akibadilika
kama kinyonga. Mtaani alikuwa
akitafutwa na wana usalama wa kila
aina. Kila hoteli ilipandikizwa watu
maalum wa kuchunguza kila aingiaye
na atokae. Anayekuja kula na hata
wale waliokuwa na mambo yao binafsi.
Kila mmoja alikuwa akiangaliwa kwa
umakini sana. Wana usalama walikuwa
wakimtafuta masimba kila kona ya
mtaa na hata mji. Wakati huku Dar
yakiendelea hivi, Masimba alikuwa nje
kidogo ya jiji LA dar es salaam. Hakuwa
huko kwa sababu ya kuogopa
purukushani za maafisa usalama wanao
msaka. Bali alikuwa nyumbani kwa
Mama wa Marehemu Asteria kupata
kile ambacho alitaka kupewa kabla ya
kifo cha mwanawe na hata mwanawe
wa pili. Alitelemka kwenye daladala
kama abiria wa kawaida. Kichwani
alijifunika kwa kofia aina ya cowboy.
Chini alivaa suruali sambamba na raba
ambazo zilisababisha aonekane kama
kijana mtanashati pale kijijini. Baada ya
kushuka hapo akaingia sehemu yenye
huduma ya vyakula. Akatafuta sehemu
nzuri na kutulia kisha kuagiza chakula.
Baada ya chakula kuletwa, akaanza
kula taratibu huku macho yake
yakiangaza huku na huko kuona kama
alikuwa akifuatiliwa ama lah!
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 024
Macho yake yalikuwa yakimtizama kila
atokae na hata aingiae. Muda wote
alikuwa akimshuku kila mtu ambaye
angeingia na kusimama pasipo kufanya
kitu. Alijua kinachoendelea Jijini ni
kutafutwa kwake katika namna ya
kipekee. Alitambua kujiokoa kutoka
kuzimu ni kitu ambacho mkurugenzi na
majasusi wote wasingekubali. Hakuna
mtu alieingizwa ndani ya chumba kile
na kutoka akiwa hai. Lakini kwake
yeye aliweza na kuthubutu. Hilo ndio
lingekuwa chanzo cha kutafutwa
kwake. Na sio kutafutwa tu bali
kupotezwa kabisa katika uso wa dunia
hii. Maelezo kutoka kwa Teddy juu ya
kinachoendelea kilimsisimua sana
mwili wake. Watu wenye suti
sambamba na waliovalia mavazi ya
kawaida walikuwa wakipishana
kumtafuta katikati ya jiji. Hata wale wa
kike waliokuwa wakitembeza mboga
za majano walikuwa wakimtafuta
yeye. Nyumba yao haikukosa
kuangaliwa kila wakati, wasichana
wachafu wenye mabeseni yenye
mboga za majani walipita kila wakati.
Yote hiyo ilikuwa ni kutafutwa kwake.
Hakuihofu taarifa hiyo kutoka kwa
teddy, hakuiogopa kwa kuwa alikuwa
ameizoea purukushani, alishazoea
mapigano na hata kusumbuana na
wana usalama. Aliutazama ujumbe ule
kutoka kwa teddy kwa makini,
aliporidhika akairudisha simu mahala
pake. Akaendelea kula huku sasa
akiiwaza kazi iliyo mbele yake. Kazi
ambayo mwanzo haikuwa ngumu, kazi
ambayo aliichukulia kama kazi ya
kawaida. Lakini sasa ilikuwa ngumu
baada ya kuingilia na Idara ya usalama
wa taifa. Kitendo cha mkurugenzi
kumkalipia kilionyesha ni kiasi gani
mkurugenzi amekubali kudanganywa.
Hakuamini na hakutaka kuamini kama
Jasusi mwandamizi kama yeye
anaweza kudanganywa kwa hila kisha
kukubali. Hata alipowaza nani alipanga
kile kilivhotokea hakuweza kugundua.
Kuuawa kwa Godfrey Maboba na
familia yake, kisha kukutwa na kikosi
maalum cha kupambana na ujangili wa
kutisha, ni mpango ambap ulipangwa
na kutengenezwa na watu
wanaomfahamu. Nani alimuona wakati
anakwenda nyumbani kwa dada wa
Marehemu Asteria. Hilo likampa picha
kuwa mtu anayeogopewa na Teddy
inawezekana ndio mpangaji wa haya
matukio. Ndio huyu aliyemshawishi
hata DG wa TISS akubali kukitenda kile
ambacho hakuwaza kama kitatendwa
na Mtu mwenye mafunzo yote kama
yeye. Ni nani huyu anayeogopewa? Ni
nani huyu mwenye nguvu kuliko Idara
ya Usalama wa taifa? Ina maana hata
kile kitengo chenye watu watano
kimeshindwa kumgundua huyu mtu?
Nina huyu? Yalikuwa maswali
yaliyomtia hamu, hamu ya kumuona na
kumjua huyo mtu. Alitaka kuonana
naye uso kwa uso ama kumtafuta na
kuhojiana naye kupitia mawasiliano.
Hakuwahi kumuogopa mtu na
hakuwahi kuogopa kabisa. Aliyawaza
hayo akiendelea kula taratibu. Mara
moja moja hakuacha kuangalia nje.
Baada ya kumaliza kula sasa alikuwa
tayari kwenda kwa mama wa
marehemu Asteria. Akainuka kama
kawaida huku macho yake
yakimuongoza kwa kila hatua.
Akakiacha kimgahawa kile na
kuchepuka mpaka upande wa pili wa
barabara. Ingawa alikuwa mgeni katika
maeneo yale ya mkuranga, lakini
alikuwa na maelezo yote ya kumfikisha
nyumbani kwa mama Asteria.
Alitembea kama mtu wa kawaida,
wakati akiikaribia nyumba ile
akamuona mtu akitoka ndani. Mtu
ambaye alimshangaza na kumsisimua,
mtu ambaye hakuamini kama
angemuona pale. Alikuwa Teddy
akitoka ndani ya Nyumba ya Mama wa
Marehemu Asteria. Hilo
likamstaajabisha, likamshangaza na
kumduwaza. Teddy amefikaje huku,
teddy amekuja kufanya nini huku?
Yupo na nani? Wakati akijiuliza hilo,
akamuona mtu mwingine ambaye
alizifanya kengele za hatari kulia
kichwani mwake. Huyu alikuwa
Mwamvita, huyu alikuwa yule
mwanamke aliyehusika na mlipuko
kule kigamboni. Kwa Mara ya pili teddy
alikuwa ameasi. Teddy alikuwa
ameamua kurufi kundini kwake.
Alikuwa ameikubali pesa na sio taifa
lake. Kumbe wakati anatoa taarifa
kuhusu wanausalama kuiweka chini ya
uangalizi alikuwa akiipumbaza akili
yake. Kumbe alikuwa yupo katika
mipango ya kufika huku. Akauona
usalama wa Mama Asteria kuwa
mdogo.
Hakuweza kukurupuka, bado
aliwatizama hasa akimuangalia Teddy.
Alimuangalia kwa muda wote huku
mishipa ya hasira ikajitokeza.
Akawaona wakishuka ma kujipakia
ndani ya gari kisha kuondolewa kwa
kasi. Bado masimba aliduwaa, akili
yake ilimtuma kuwahi pale, lakini bado
kuna kitu alikihofu. Wakati bado
anashindwa kitu cha kuamua,
akamuona mama wa Asteria akitoka
akiwa sambamba na kitoto kingine
kidogo cha kike. Masimba akajitokeza
sasa akielekea pale. Hatua ya kwanza
kupiga akahisi kitu, kitu ambacho
hakukijua. Hatua ya pili akahisi kitu
kingine ambacho hata hiki hakukijua.
Hatua ya tatu akagundua kuwa alikuwa
akitizamwa na mtu kutoka sehemu
fulani. Akaendelea kutembea
akiziamini hisia zake, hisia ambazo
hazikuwahi kumdanganya. Sasa
akaikaribia nyumba ile, zilikuwa ni
hatua tano kutoka ilipo nyumba.
Kengele za hatari zikagonga tena.
Safari zikiambana na uhatari wenyewe.
Mama alikuwa akitabasamu, alikuwa
akimuangalia masimba. Mkono alikuwa
ameshikilia simu kubwa, simu ambayo
kwa macho ya Masimba haikuwa simu,
haikuwa simu ya aina yoyote bali
ilikuwa rimoti, akili za masimba
zikafanya kazi kwa haraka sana..
akaanza kukimbia huku akimuomba
mama yule aitupe ile rimoti. Kabla
hajamfikia akashuhudia mama yule
akibonyeza kitu. Kilikuwa kitendo cha
sekunde tatu Masimba kuruka hewani
na kutua pembeni kabisa ya barabara.
Mlipuko mkubwa ukasikika. Moto
mkubwa ulikuwa angani huku jumba la
mama wa Asteria likiwaka moto.
Kilikuwa kishindo kilichotingisha mji
wote wa mkuranga. Masimba alikuwa
akikimbia kwenye moto kwenda
kumuokoa yule mama. Hakuujali moto,
hakujali kelele za watu ambao
walikuwa wakipiga kelele. Alikimbia na
kuingia katikati ya moto. Baada ya
kuingia akaanza kutafuta. Alitafuta kwa
shida kutokana na hewa nzito. Wakati
anataka kukata tamaa akasikia sauti ya
mtu akilia. Akaangalia hapo kwa tabu,
akamuona Mama wa Asteria akiungua
huku akimngika mjuu wake asiungue.
Haikuwa picha nzuri kuitizama.
Alisogea haraka na kumshika yule bibi.
Akataka kumuinua lakini yule mama
akamzui. Hata macho yake yalikuwa
yakionyesha kukata tamaa.
"Naku....faaa mwa mwa.. nangu..
nao..mba muokoe huyu ni..nia.che
mimi nife." Aliongea mama kwa
uchungu huku machozi yakimtoka.
Masimba hakuchelewa akamuangalia
mama kwa sekunde. Akamuachia
mkono huku akilia kwa uchungu.
Akamchukua mtoto na kuanza kutoka
naye. Hakutoka kupitia alipoingilia bali
alitokea kwa upande wa nyuma. Mtoto
alikuwa begani. Akafanikiwa kuuvunja
mlango wa nyuma. Akatoka sambamba
na mtoto yule. Akakimbia naye mpaka
sehemu ambayo kulikuwa na watu
wengi akasimama kisha kuomba maji.
Hayakuwa maji ya kunywa, mwili wa
mtoto ulikuwa na moto. Akamuweka
mtoto chini ili apewe huduma ya
kwanza. Lakini kumuweka tu chini
akagundua mtoto alikuwa ameshakufa.
Ameshakufa sambamba na bibi yake.
Masimba hakuamini, hakuamini kama
yule mtoto amefariki. Akaendelea
kumtingisha kwa nguvu huku akilia.
Lakini halikuubadilisha ukweli. Mtoto
yule alikuwa ameshakufa. Masimba
akamuangalia kanakwamba haamini
kama yule mtoto amekufa. Teddy
alikuwa amemrudisha tena kwenye
maumivu. Akasimama huku watu
wakimshangaa. Akarudi kwenye
utimama wake. Ilikuwa ni lazima arudi
kwenye utimamu wake. Kila kitu
kilikuwa kigumu kwake. Alikuwa teddy
pekee aliyeijua safari yake ya kwenda
mkuranga. Ni yeye aliyejua kwamba
anakwenda kuonana na mama wa
Asteria. Kwahiyo hapa alijua teddy
ndiye amehusika na kitendo kile cha
kinyama
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 025
Teddy pekee ndiye aliyekuwa
akiifahamu safari yake. Safari ya
kwenda kuongea na Mama wa Asteria.
Lakini ni Teddy huyu huyu ambaye
alimuona akiwa sambamba na
mwamvita. Teddy ambaye alimueleza
kuwa hakuwa tena kule. Teddy
ambaye alimuamini na kuamini
maneno yake. Lakini leo hii teddy
alikuwa ameamua kuimaliza familia ya
Asteria. Mama yake alikuwa akiendelea
kuteketea na moto, huku mtoto
mdogo wa kike akiwa amelala mbele
yake akiwa hana uhai tena. Hilo
likamuuma sana? Licha ya kuumia
lakini hakutakiwa kuwa pale. Ulikuwa
muda wa kuondoka na kupotea kabisa.
Hakujali macho yaliokuwa
yakimtizama, hakujali vilio na ving'ora
vya polisi.. aliondoka akiwa
amechanganyikiwa, aliondoka akiwa
na Hasira na teddy, alitamani kupiga
Risasi katika kichwa chake. Alianza na
Asteria akafuatia Mwamvua, kisha dada
yake na familia yake akiwemo
Mumewe, Mr Godfrey Maboba. Sasa
ameamua kuwamaliza wote. Kuna siri
gani hapa nyuma? Ina maana ni mzigo
tu wa madawa ndio sababu ya vifo
vyote vile? Hapo akahisi kitu kingine,
alihisu kuna kitu kingine nyuma ya
mauaji haya. Alihisi hivyo na aliamini
hivyo. Akaamua sasa kumfungia kazi
Teddy, alitaka kwenda kumuonyesha
kuwa yeye ni mtu mwingine katika
medani ile. Kama mzigo wa madawa
ameshauchukua kipi kinampa hofu
teddy? Kwa nini aendelee kuua?
Hakuweza kujibu hilo swali bali
akasonya na kutukana tusi zito. Baada
ya kutembea sana akajikuta akitokea
sehemu yenye kituo cha daladala, bila
kujali macho ya watu, akajipakia ndani
ya costa moja na safari ya kurudu dar
ikaanza. Muda wote wa safari alikuwa
amekiinamisha kichwa chake kwenye
siti akiliwaza tukio lililotokea punde.
Sauti ya mama wa Asteria ilikuwa
ikijirudia kila wakati. Tukio zima
liliendelea kumtesa. Akatamani afike
Dar akamuone Teddy. Alikuwa tayari
ameapa kwenda kuitumbukiza Risasi
Kichwani kwa Teddy. Ni wakati
akiliwaza hilo akausikia Ujumbe
ukiingia kwenye simu yake. Akataka
kupuuza, alitaka kutoitazama simu,
lakini akaisikia sauti ikimwambia
"wewe ni mpelelezi unayetafutwa
usipuuze kitu."!!! Akaitii sauti ile. Muda
mfupi vidole vyake vilikuwa na kazi ya
kuifungua Meseji.
"Uko salama, nasikia kuna nyumba
imelipuliwa huko!!!? Ulisomeka
Ujumbe ulionekana kutumwa na
Teddy. Hilo pia hakuliacha lipite hivi
hivi. Teddy alikuwa akimchezea akili
yake, teddy alikuwa akimuona mjinga.
Lakini kingine kilichomfurahisha ni kule
kugundua kuwa teddy hakuwa
amemuona wakati akitoka ndani. Hilo
likampa uhuweni wa kumfikia pasipo
rabsha yoyote. Teddy alikuwa
ameingiwa na tamaa, ni yeye na
mwamvita waliotoka ndani ya nyumba
ya mama wa Asteria. Lakini muda huu
anamtumia Ujumbe kuhusu
kilichotokea, alikuwa akiipima akili ya
masimba. Hakuona sababu ya kumjibu,
akaitizama simu kwa muda kisha
kuirudisha mfukoni. Alimchukia teddy
na bado alitamani kufika Dar es salaam
akutane nae.
*******
Alishuka maeneo ya mbagala saa moja
na nusu usiku. Baada ya kushuka hapo
akaona ilikuwa muhimu kumpigia
teddy kutaka kujua wapi alipo.
Akatafuta sehemu yenye utulivu
akaipiga simu ya teddy, lakini cha
ajabu haikuwa hewani. Akajaribu tena
na Tena lakini bado hali ikawa ni hivyo.
Simu ya teddy haikuwa ikipatikana.
Akakiona kitu ambacho alikihisi hapo
mwanzo. Teddy alikuwa amemchezea
akili yake, inawezekana alimuona kule
ndio maana akamtumia ule ujumbe.
Sasa kutokupatikana kwa teddy
kilikuwa ni kitu kingine cha
kushangaza. Akaona haukuwa muda
wa kuendelea kubaki mbagala. Ilikuwa
ni lazima arudi kinondoni kwa usiku
ule. Lakini kabla hajaamua kurudi
lazima awasiliane na rafiki zake ambao
wapo katika nafasi nyeti nchini. Wa
kwanza kumpigia alikuwa Dee Plus,
huyu alikuwa mmoja kati ya vijana
wake. Aliongea naye mawili matatu.
Baada ya hapo akarudi tena kituo cha
daladala. Hapo akachukua usafiri wa
kuelekea huko.
********
"Masimba anaelekea mkuranga kwa
mama wa Asteria. Hakikisheni anazuia
au mama anafutwa katika uso huu wa
Dunia." Ilikuwa sauti ya teddy akiongea
na mwamvita. Simu hiyo alipiga baada
ya kikao kizito kati yake na washirika
wenzake kufanyika na kufanikiwa
kumrudisha teddy kundini. Ni simu
hiyo ambayo iliwalazimu teddy na
mwamvita kuelekea mkuranga. Ni
simu hiyo iliyotumika kumtumia
ujumbe masimba kwamba alikuwa
akisakwa na wanausalama. Ujumbe ule
kwenda kwa masimba ulitumwa na
teddy wakati huo wakiwa mkuranga.
Aliutuma mahususi ili kumfanya
masimba achelewe kurudi Jijini, ili
watu wao waendelee na utafutaji wa
mzigo wao ambao uliibiwa. Licha ya
watu waliotumwa kuipekua nyumba
ya masimba nje ndani na ndani nje.
Hawakuweza kupata chochote.
Hawakuweza kuupata mzigo wao,
mzigo ambao ndio chanzo cha mauaji
na uasi uliofanywa na Teddy. Lakini
kingine ambacho kiliwashangaza
Jimmy na washirika wake, nikule
kuambiwa hata masimba
hawakumuona kule mkuranga. Ni
taarifa hiyo ambayo bado ili
wachanganya na kuwafanya kila
mmoja awaze lake.. ndipo hapo amri
ilipotoka kwamba wategeshe bomu
ndani ya nyumba ya mama wa Asteria
na kabla ya hapo walipewa amri ya
kumsubiri masimba hapo. Muda
ulivyokuwa ukisonga na
kutokuonekana kwa masimba ndipo
maamuzi ya kilichotokea mkuranga
yakafanyika. Hawamuona masimba
wakati akisogea pale, hawakumuona
kwa kuwa walikuwa katika uharaka wa
kuondoka. Na hicho ndicho
walichokosea.
**********
Simu ya teddy bado haikupatikana
licha ya kuipiga mara kwa mara. Bado
hakikuwa kitu cha kawaida kwake,
teddy amtumie meseji lakini ndani ya
muda huu alikuwa hapatikani. Haikuwa
kawaida kwake, haikuwa kawaida kwa
kuwa alimfahamu teddy. Wakati
akiwaza hilo akausikia mlio wa simu
yake kuonyesha kwamba alikuwa
akipigiwa. Ikaichomoa simu, akatupa
macho Juu ya kioo, akakutana na
namba mpya. Akaitizama ile simu kwa
muda bila kuipokea mpaka ilipokatika.
Hakuwa na utaratibu wa kupokea
namba ngeni katika kazi yake hii ya
hatari. Baada ya ile simu kuita na
kukata bila kuipokea, akapata hisia za
kuingalia namba ile vizuri, alitaka
kumjua mmiliki na alitaka kujua
inapigwa kutoka wapi. Muda mfupi
alikuwa akiongea na simu Nyingine
hewani. Baada ya kukata akatulia
akisubiri kupata maelekezo kutoka
kwa mtu wake. Haikupita muda muda
mrefu simu yake ikaita tena. Alikuwa ni
yule mtu wake. Akaipokea na kuongea
kwa dakika kama moja hivi kabla ya
kuikata simu. Mwili wake ulisisimkwa
na kushikwa na ubaridi. Namba mpya
iliompigia ilipigwa kutokea katikati ya
jiji la dar es salaam maeneo ya posta.
Ilikuwa taarifa aliyoitegemea kqbisa.
Alijua simu hiyo ilitoka kwenye moja ya
majengo yanayomilikiwa na Idara ya
Usalama Wa Nchi. Hilo likamfanya
aamue kuelekea huko, alitaka kwenda
kumjua mwenye namba ile. Hakuwa na
sababu ya kuogopa wakati alikuwa
akisakwa. Baada ya daladala aliopanda
kufika maeneo ya uhasibu alishuka,
kisha akachukua usafiri wa pikipiki
mpaka maeneo ya posta. Alishuka na
kulipa ujira kisha kuongoza kuelekea
pale ambapo alipakusudia. Alitembea
kwa uangalifu mpaka maeneo ya
bandarini nje ya kituo cha mabasi
yaendayo kasi. Kulikuwa na umbali
mfupi sana kutoka kwenye jengo
binafsi linalotumiwa na usalama wa
taifa. Jengo ambao lilikuwa
likitizamana na Makao makuu ya
Mamlaka ya mapato Tanzania. Vilevile
ulikuwa umbali mfupi na kilipo kituo
kikuu cha polisi Dar es salaam (Central
police) baada ya kusimama hapo kwa
muda akiangalia hili na lile,
akaichomoa simu yake, kisha
akaitafuta ile namba harafu akaipiga
akiwa mkononi pasipo kuipeleka
sikioni. Baada ya kuita tu, akaikata
kisha akaondoka pale kwa haraka
mpaka pale kituo cha posta ya Zamani.
Akatulia pale huku macho yake
yakitizama kule alipotoka. Haikupita
hata sekunde thelathini, akawaona
watu wanne ambao hawakuonyesha
kama wako pamoja wakipishana huku
na huko. Hakuwa mgeni na majasusi,
aliwajua na kuwatambua hata kama
wamejibadilisha kwa kiasi gani.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 026
Aliwajua wanausalama na
kuwatambua. Hata wangekuwa umbali
gani haikuwa shida kwake
kuwafahamu. Akaendelea kuwaangalia
huku akiondoka pole pole kutoka eneo
lile. Utimamu wa akili bado ulimpa
uhuru na uwezo wa kutenda kile
ambacho alipaswa kufanya kwa wakati
ule. Alijua uwezo wa wanausalama wa
Tanzania. Aliutambua weledi wao.
Kwahiyo alitakiwa kuwa makini kwa
kila hatua. Bado alikuwa akiwaona
watu wakiongezeka katika eneo husika
kutokana na kumulikwa na taa za
magari. Kuna ambao walikuwa
wakiyumba kama walevi, wengine
walikuwa wamevaa mavazi chakavu
wakionekana kuokota vitu chini. Hicho
ndio kitu ambacho alikitaka masimba.
Alitaka kuhakikisha ni kweli alikuwa
akitafutwa? Kuipiga simu akiwa pale
alitambua angegundua chochote kama
ni kweli namba ile ilitumiwa na watu
wa usalama. Hilo likafanikiwa, hata
wale walevi na omba omba waliokuwa
pale ilikuwa ni mbinu ya wanausalama.
Akaendelea kutizama kila kilichokuwa
kikiendelea. Purukushani ilikuwa
kubwa sana, purukushani ya watu na
hata magari yaliokuwa yakipita huku
na kule. Wana usalama wengi
walikuwa wakipanda kwenye mabasi
ya mwendokasi, wengine walikuwa
madirishani wakichungulia kwa ndani.
Ni hapo alipoiona gari aina nissan
patrol ikitembezwa taratibu. Haikuwa
gari ngeni machoni mwake, ilikuwa
gari anayoifahamu vizuri tu. Ilikuwa
gari ambayo ilitumiwa mara nyingi na
watu tofauti wa idara. Hii ilikuwa gari
iliyotumiwa mara nyingi na kitengo
kimoja ambacho kipo ndani ya Idara.
Kitengo ambacho hujulikana kama
black mambaz. Macho yake yakazidi
kuitizama gari ile. Wakati ikielekea
katikati ya jiji, masimba naye
alisimamisha pikipiki, akamuomba
aifiatilie gari iliyombele yao kwa siri.
Dereva yule hakubisha, taratibu
akaanza kuifuatilia gari ile ambayo sasa
ilikuwa ikielekea maeneo ya posta
mpya. Muda wote masimba alikuwa
akiitizama ile gari. Alitaka kujua ni wapi
inapoelekea. Akamwambia dereva
aache magari manne yatangulie mbele
yao ili kutokuwagutusha watu
waliokwenye gari. Dereva wa pikipiki
akatiii. Akaendesha huku akiwa makini
na kila kitu. Punde wakaiona gari
ikiingia barabata ya Allhasan Mwinyi.
Magari ya mbele yao nayo yakaelekea
huko. Wakaendelea kuifuatilia ile gari.
Baadaa ya kupita daraja la salenda ile
gari ikaacha barabara Ally Hassan
Mwinyi ikaingia barabara ya kinondoni.
Hapo dereva akageuka kumuangalia
masimba. Masimba akampa ishara ya
kuendelea kuifuatilia kwa nyuma.
Baada ya kuifuatilia kwa muda
wakaiona gari ile ikisimama maeneo ya
kinondoni Manyanyq. Masimba
akamwambia dereva yule aipite ile
gari pasipo kuonyesha wasiwasi
wowote. Baada ya kuipita ile gari na
kutembea mbele kidogo. Masimba
akamwambia asimame hapa,
akachomoa noti tatu za Elfu kumi na
kumkabidhi yule dereva. Baada ya
kumkabidhi aliondoka taratibu kurudi
nyuma pale ilipoegesha gari
waliokuwa wakiifiatilia. Alitembea kwa
umakini mkubwa mpaka jirani kabisa
na iliposimama ile gari. Akaangaza
macho yake kwa umakini kule gizani.
Punde akawaona watu wawili ambao
wakikuwa wamesimama kwa kumpa
mgongo. Walikuwa wamevaa
mabaibui kuficha sura zao, lakini
maumbo yao hayakumfanya masimba
kupotea. Mbele yake alikuwa
akiwatizama Teddy Sambamba na
Mwamvita wakiwa wamempa Mgongo.
Hapo akaongeza umakini, sasa alikuwa
akiwaangalia kwa karibu zaidi. Bado
walionekana wakiongea kitu, bado
walionekana kulikuwa na
mazungumzo yakifanyika. Punde
akaiona gari ya kifahari ikisogea
taratibu katika eneo lile. Ilikuwa gari
ya bei mbaya, gari ambayo thamani
yake iliweza kuhudumu kwenye
wizara kama tatu za hapa nyumbani.
Wakati akiendelea kuiangalia ile gari
ikisogea, macho yake yakavutiwa na
watu wawili wengine waliongezeka
pale. Kitendo bila kuchelewa
akawaona watu wale wakimuongoza
teddy kuelekea kwenye ile gari
ambayo bado ilikuwa ikitembea.
Akaliangalia tena lile tukio la teddy
kupelekwa kwenye gari. Haukuwa
ukokotwaji wa kawaida,haukuwa
ukokotwaji wa hiari bali ulikuwa
ukokotwaji wa lazima. Kwani kuna
wakati teddy alikuwa akigoma lakini
alikuwa akilazimishwa kwa mtutu wa
bunduki. Kilikuwa kitendo
kilichofanyika kwa muda wa nusu
dakika na hata alipoifikia gari na
mlango kufunguliwa akashuhudia pigo
la kitako cha bastola likitua kisogoni
kwa Teddy. Hilo likaufanya mwili wake
kuingiwa na ganzi, damu kusimama
kwa muda huku mwili wake
ukitetemeka. "Naam mapenzi
yalichukua sehemu yake. Aliumia sana
katika kile ambacho kilitendwa kwa
Teddy. Licha ya yote aliotendewa na
teddy bado alimpenda. Bado
alimuhitaji katika kina cha moyo wake.
Akaendelea kushangaa na kuduwaa.
Teddy alikuwa akiadhibiwa, teddy
alikuwa akipelekwa sehemu ambayo si
salama kwake. Alitambua kama
angemuacha bila kufanya kitu basi
asingemuona teddy akiwa hai tena.
Hakulikubali hilo na hakuwa tayari.
Ilikuwa lazima afanye jambo, jambo la
kumuokoa teddy. Lakini hawa
waliomchukua ni nani? Na
wanampeleka wapi? Haukuwa muda
wa kutafuta majibu wala kujiuliza
maswali. Muda mfupi alikuwa kwenye
tax wakiwa nyuma ya gari iliyombeba
teddy, wakiifuatilia kwa nyuma. Muda
wote alimhimiza dereva kuongeza kasi
na kuhakikisha gari ya mbele
haiwapotei. Hilo likafanywa kwa
umakini, bado katikati yao waliyaacha
magari matatu kama kanuni nyingi za
kipelelezi zilivyo. Mpaka wanafika
magomeni usalama na gari kuonyesha
ishara ya kuingia barabara ya
morogoro hata wao wakafanya hivyo.
Kufika mbele kidogo eneo la
magomeni usalama, wakaiona gari
wanayoifuata Ikiingia maeneo ya
ukumbi maarufu kwa burudani ya
muziki wa mwambao uitwao
Travertine Hotel. Baada ya gari
ilikukatisha na kuingia kabisa masimba
alishuka kwa haraka ni baada ya kulipa
ujira wa Dereva, akaongoza kama mtu
wa kawaida kuelekea hotelini hapo.
Bastola zilikuwa kila upande ndani ya
mavazi yake. Hatua tano mbele
akakutana na madada poa wanaofanya
biashara ya kuuza mili yao katika eneo
hilo. Akamuita mmoja na kusimama
naye pembeni kama wafanyavyo
wanunuzi. Lakini yeye hakumuita hapo
kwa sababu ya kutaka huduma, bali
alitaka kuutumia kama moja ya kuzuga
ili ajue ni wapi twddy anapelekwa.
Akasimama na yule binti tena ni baada
ya kumpa yule chqngudoa elfu kumi.
Macho yake yalikuwa yakitizama kule
iliposimama ile gari. Akaushuhudia
mlango ukifunguliwa. Kwa kuwa
palikuwa karibu sana, alikuwa
akishudia kila kitu ambacho kilikuwa
kikitendeka.
Baada ya mlango wa gari kufunguliwa
wakashuka watu watatu tofauti na
wale wa mwanzo. Kati yao mmoja wao
alikuwa amebeba kitu kama furushi
begani. Baada ya watu wale kushuka
wakaongoza moja kwa moja kwenda
ndani upande wa hotel. Bado masimba
alitulia akichunguza kila kitu. Baada ya
watu wale kuingia ndani, huku nyuma
mlango wa kati ukafunguliwa tena.
Mara hii akashuka mtu mzima ambaye
sura yake ilifunikwa kwa kofia ya
pama. Baada yq mtu yule kushuka
akaonekana akiongozwa na walinzi
ambao kwa kuwaangalia tu.. walikuwa
ni walinzi wale wa kulinda viongozi wa
Kitaifa. Lakini hapa walionekana
wakimlinda huyu mtu aliyeshuka
kwenye gari. Haikuwa sawa kwa
presidential protect unit kuwa katika
eneo hili tena kwa mtu ambaye
hahusiki na serikali. Hilo likampa
wasiwasi wa kutaka kujua zaidi. Teddy
kupelekwa ndani, kisha mtu huyu
kushuka naye kuelekea huko kilikuwa
kitendo kilichomshtua. Hatua ya
kwanza aliipiga akimuacha yule
changudoa akishangaa. Hatua ya pili,
changudoa hakukubali naye akawa
anafuata kwa nyuma. Hatua ya tatu
alishamfikia masimba na sasa walikuwa
wakitembea sambamba wakizipanda
ngazi wakiwa kama wa penzi. Kwa
kuwa kulikuwa na giza hakuna
aliyeweza kumgundua. Baada ya
kumaliza ngazi na kutokea mapokezi
akashangazwa na watu waliotapakaa.
Watu ambao sura zao zilikuwa
zikiongea lugha moja. WOTE
WALIKUWA MAIFISA USALAMA WA
TAIFA
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 027
Watu waliokuwa wakiongea lugha
moja, watu ambao kwa kuwaangalia
wangekujulisha wao ni kina nani.
Masimba bado akilimshikilia changudoa
wake. Mwili na mikono vikiwa kwenye
utayari. Hata yeye macho yake
yalikuwa yakiwatizama. Sasa alikuwa
akienda mapokezi na changudoa wake.
Changudoa aliemuokota nje na
kumfanya kama chambo cha
kumuingiza hapo hotelini. Kufika
mapokezi hakuongea chochote zaidi ya
kuchomoa bulungutu la pesa na
kuliweka juu ya meza ya mapokezi.
Mhudumu alitmhamaki kutokana na
wingi wa pesa zilizowekwa mezani.
Hata changudoa naye alikuwa katika
hamaniko, hamaniko lililozaa sononeko
la moyoni. Alikuwa akiitafuta pesa kwa
kuuza utu wake, lakini leo hii
amakutana na mtu anayeitumia pesa
kwa fujo. Wote wakabaki wameduwaa
wakiisubiria kauli ya masimba. Kauli
kuhusu matumizi ya pesa ile. "Nataka
kujua watu waliobeba mzigo
wamekwenda chumba namba ngapi. "
ilikuwa sauti iliopenya masikioni mwa
watu hawa wawili, mhudumu na
changudoa. Hawakujibu wala kupata
jibu kwa wakati ule. Huyu ni nani? Na
kwa nini anataka kujua? Yalikuwa
maswali ambayo hayakupata majibu
kwa wakati ule. "Fanya hivyo uchukue
pesa kama hutaki hii hapa itakuwa
zawadi yak0." Alinong'ona safari hii
sura yake ikiwa haina masihara.
Wasichana wote waliduwaa.
Hawakuduwaa kwa kutokujua cha
kufanya, bali waliduwaa baada ya
kuuona mdomo wa bastola
ukichungulia. Binti akatii bila
kuonyesha wasiwasi. Akainuka na
kuwapa ishara wafuatane. Ishara
ambayo haikuonekana popote. Bado
changudoa alikuwa mkono wake wa
kushoto. Walitembea kwa hatua za
umakini huku macho yake
yakitambazwa kila sehemu kwa
utulivu. Wakawapita wanausalama na
kuanza kuipanda ngazi kuelekea juu.
Hatua tano baada ya kutokea kwenye
korido wakauona mlango wa mbele
ukifunguliwa. Watu wawili
aliowafahamu walikuwa wakitoka
hapo. Alikuwa Jimmy sambamba na
mtu mwingine mwenye asili ya kihindi.
Masimba akainama kisha kuonekana
akimbusu changudoa yule.alifanya
kitendo kile mpaka pale walipopishana
na watu wale ndio wakaacha. Hapa
akaukuta uhuru, hapakuwa na
wanausalama na hapakuwa na mtu
mwingine. Ishara ikafuata kutoka kwa
mhudumu yule. Ishara ya
kuwaonyesha kwamba hapa ndio
sehemu yenyewe. Akaimpa ishara ya
mwanamke yule kuugonga mlango.
Muda wote yeye alikuwa ameikamata
bastola akitizama nyuma. Mhudumu
akaugonga mlango kwa mara ya
kwanza, kukapita kimya, mara ya pili
bado hapakuwa na mtu wa kujibu.
Wakati mhudumu yule akigeuka
amuulize masimba cha kufanya,.
Mlango ukafunguliwa kisha mtu
kuchungilia. Kilikuwa kitendo cha nusu
dakika kufanywa na Masimba. Kwani
wakati dakika inatimia masimba
Alikuwa ndani huku mtu yule
aliyechungulia akivuja damu. Macho
yake yalishatambaa kila upande mle
chumbani na kukinasa kitu
kilichompandisha Hasira. Teddy
alikuwa juu ya kitanda akiwa na nguo
ya ndani tu, huku fahamu zikiwa bado
zimempotea. Hakushughulika sana na
teddy. Bastola yake ilikuwa
ikimuangalia mtu yule. Hata
alipomuangalia mtu yule na macho yao
kuonana hakuamini. Hakuamuni mtu
aliyekuwa akitizamana naye.
Hakuamini kumuona mtu huyu akiwa
chumbani na Teddy. Alikuwa kiongozi
mzito wa serikali. Kiongozi wa ngazi za
juu kabisa katika nchi husika. Mtu
mwenye jina kubwa katika jamii na
katika nyanja za kimataifa.
Alimuangalia kisha kumuangalia teddy
pale kitandani. Haukupita muda sauti
ya chafya ikasikika ndani ya chumba
kile. Damu ikaruka na kusambaa
chumba kizima. Yule changudoa
hakutegemea kuliona lile tukio
kufanywa na mtu huyu aliyemchukulia
kama mteja. Akataka kupiga kelele
lakini alipouona mdomo wa bastola
unamtizama, akanyamaza akibaki
anatetemeka. Macho yake yalikuwa
yakiutizama mwili wa kiongozi wa nchi
ukiwa umalala katikati ya dimbwi la
damu. Masimba akaufunga mlango
kwa ndani kisha kumvuta mwanamke
yule.
"Sikiliza naomba unisikilize kwa
makini. Ukileta ukaidi kilichompata
huyo mtu hapo hata wewe kitakupata.
Nataka tuondoke humu ndani tukiwa
na huyu dada kwa kupitia mlango wa
dharura wa hoteli hii. Sasa chukua hii
bastola, mimi nitambeba huyu
mwanamke, wewe utakuja nyuma
yangu ukinilinda. Yoyote ambaye
atajitokeza piga risasi. Umenielewa?
Changudoa yule akajibu kwa kutingisha
kichwa. Akachukua mavazi ya Teddy na
kumvisha. Muda mfupi walikuwa Nje
ya chumba kile wakielekea nyuma ya
hoteli kwenye mlango wa dharura.
Kilikuwa kitendo kilichotendeka kwa
muda mfupi sana. Kitendo ambacho
hakikuchukua hata dakika mbili.
Wakatembea kwa uhuru bila kukutana
na chochote. Mpaka wanatokea nje
hawakuonekana na mtu yoyote. Baada
ya kufika nje wakaivuka barabara kama
wanaelekea magomeni mapima. Hatua
kadhaa mbele wakaiona tax mbele
yao, wakaisimamisha, kisha kumuomba
jamaa awapeleke kimara mwisho.
Dereva akawasha gari na safari ya
kimara kuanza. Baada ya kutembea
mpaka magomeni mwembe chai,
masimba akachomoa burungutu la
pesa na kumpa yule changudoa.
"Shuka hapa nitakutafuta, lakini
nakuomba ufumbe mdomo wako."
Akanong'ona masimba huku akimpa
kile kitita. Binti akakipokea huku
akionyesha wasiwasi. Hiyo haikuwa
dalili nzuri kwa masimba. Baada ya
kushuka na kuondoka masimba
akamuomba dereva ashuke amfuatie
msichana yule kwani kuna kitu
ambacho alisahau kumwambia. Dereva
hakuwa na hiyana, akaipaki gari
pembeni mwa barabara. Masimba
akashuka na kuanza kumfuatilia
mwanamke yule bila mwenyewe kujua
kama anafuatiliwa. Ilimchukua
masimba dakika tano kuifahamu
nyumba ambayo anaishi msichana
yule. Baada ya kuigundua nyumba ile
akarudi kwenye gari.
*******
Siku zote kazi ya kijasusi huwaga
hazitakiwi kuacha ushahidi nyuma. Kifo
cha kiongozi yule wa nchi alijua
kitaibua mambo mengi sana. Alijua
msako utakuwa mkali na hoteli nzima
lazima ipekuliwe. Alitambua
wahudumu na hata baadhi ya
wapangaji watatiwa kashkash
kutokana na hilo. Ni katika kashkash
hizo nipo watakapo mpata mhudumu
ambaye alikuwa zamu katika siku hiyo.
Alitambua akipatikana mwanamke yule
basi na hata yule changudoa
angepatikana. Hapo kila kitu
kingewekwa wazi na angejulikana
kwamba ni yeye aliyetengeneza
mauaji hayo. Baada ya kuwaza sana
akaona hakuna njia nyingine zaidi ya
kuwafuta watu hawa wawili kwenye
ulimwengu. Ilikuwa ni lazima
mhudumu auawe na ilikuwa bora zaidi
kwa changudoa yule kuondolewa uhai
ili kuufuta ushahidi. Hilo hakutaka
kulifanya yeye, hili aliamua kumpa
rafiki yake. Akachomoa simu yake na
kubonyeza namba kadhaaa. Akaipeleka
simu sikioni. Baada ya muda simu
ikapokelewa.
"Don." Ilisikika sauti kutoka upande wa
pili.
"Dee plus kuna watu wawili nahitaji
uwasafirishe kuzimu usiku huu kabla ya
jua la asubuhi." Alinong'ona Masimba.
"Nipe ramani, nina hamu sana ya
kupambana." Alijibu Dee plus.
Muda mfupi alikuwa akipewa maelezo
yote ya kufuata kufanikisha safari za
watu hao.
"Nimekuelewa Don, nimeshachukua
tiketi zao nawapelekea muda sio
mrefu." Akajibu De plus. Masimba
akakata simu kisha kugeuka na
kumtizama teddy pale kitandani.
Alikuwa akimpenda sana teddy.
Akajisogeza na kujilaza pembeni yake.
******
Ilikuwa yapata saa kumi na mbili za
asubuhi, wananchi wengi wakiwa bado
vitandani.. Kila mmoja alishtushwa na
wimbo wa Taifa kupigwa asubuhi ile.
Hakikuwa kitu kiliozoeleka kwa watu.
Punde ikasikika sauti ya kiongozi wa
nchi akitangaza kitu ambacho
kilimshtua kila mtu.
"Ndugu wanachi, nasikitika kutangaza
kifo cha Waziri wenu mkuu
kilichotokea usiku wa jana. Nawaomba
wote muwe kwenye utulivu katika
kipindi hiki kigumu. Mambo mengine
mtaendelea kupewa kadili muda
utakavyo kwenda."... ilikuwa taarifa
iliomsha watu, watu wakaanza kukaa
vikundi vikundi wakiongea hili na lile.
Kila mmoja akionyesha kuguswa na
kifo cha kiongozi huyu wa nchi. Wakati
watu wakiendelea kuhuzunika, upande
mwingine, wanausalama walikuwa
wakihaha kila sehemu kutafuta
chochote cha kuwasaidia lakini
haikuwa hivyo. Hawakupata chochote.
Ni wakati huo walipopqta taarifa kuwa
kuna changudoa mmoja alionekana
akiwa na mwanaume ambaye
anahisiwa kufanya mauaji hayo.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 028
******
Kunachangudoa mmoja ambaye
inasemekana alionekana akiwa na
mwanaume ambaye begani alimbeba
mtu, walichukua tax lakini walipofika
magomeni mwembechai mwanamke
yule alishuka na haukupita muda na
huyo mwanaume naye akatelemka
akimuaga mtoa taarifa kuwa kuna
maagizo amesahau kumpa yule
mwanamke. Alikwenda huko kwa
muda wa dakika tano, kisha kurejea na
kuomba apelekwe kimara. Yalikuwa
maelezo kutoka kwa dereva wa tax
aliyekodiwa usiku wa jana hotelini
pale. Kikundi cha wanausalama
kikatumwa huko na kingine
kimara,wengine wakabaki pale hotelini
wakihangaika na camera za usalama
sambamba na mhudumu ambaye
alikuwa zamu siku ya mauaji. Barabara
zikafungwa kwa muda huku magari
yakipekuliwa na madereva kutiwa
kashkash. Mhudum Hakuwepo hotelini
ama hakuonekana kabisa.
Wanausalama walipekua hata chini ya
mazuria. Kila kitu kilikuwa kikitiliwa
shaka. Wengine ambao walielekea
chumba cha kuongozea camera, nao
wakapigwa na butwaa. Hapakuwa na
chochote katika camera zile.
Hapakuonekana mtu wala kikundi cha
watu. Hapakuonekana mtu wa kutilia
mashaka katika hilo. Bado wataalam
wakahangaika huku na huko lakini
hapakuonekana chochote. Hata wakati
Waziri Mkuu akiingia haikuonekana
kwenye camera. Hilo likawafanya
wachoke. Kitu kwamba mpango huo
ulipangwa mapema kama ya ujio wa
mheshimiwa waziri likatawala akilini
mwa wanausalama. "Nani amelifanya
hili? Nani ameingia na kutekeleza
mauaji haya ya waziri mkuu? Je kuna
kisasi hapa? Kipi kilimtoa waziri
nyumbani kwake mpaka kuja hapa? Ni
mtu gani alimbeba mtu? Na ni nani
aliyebebwa? Yalikuwa maswali
yaliovisumbua vichwa vya
wanausalama. Maswali ambayo
hayakuwa rahisi kujibiwa kwa wakati
ule. Wakatamani hata kumhoji
marehemu mwenyewe awaambie.
Walitamani waziri ainuke na kukitegua
kitendawili kile. Lakini kilikuwa kitu
kigumu kama kulazimisha jua kuwaka
usiku na mbalamwezi kuangaza
mchana. Vichwa vyao vilichoka na
kuchokeana. Wakatafakari sana huku
wakitamani zingekuwa zama zile,
zama za kina Joram Kiango na Willy
Gamba. Wasingesubiri waambiwe
katika hili bali wangeamua wenyewe.
Wasingesubiri muuaji apotee bali
wangemtafuta na kumrudisha ama
kumsafirisha. Zilikuwa Nuru na Tunu
pekee katika nchi ya Tanzania. Nuru
iliyong'ara kama Madini ya TANZANITE.
Lakini hapakuwepo na Willy Gamba
wala Joram Kiango, alikuwepo mtu
mmoja aitwaye Masimba, alikuwepo
mtu huyu ambaye uwezo wake
ulijulikana katika mipaka na mataifa
yote. Lakini wana usalama wengine
hawakujua kilichopo nyuma. Ni hapo
walipokuwa wakiliwaza hilo,
wakapewa taarifa kuonekana kwa
matone ya damu katika chumba fulani.
Wote wakaelekea huko. Hata
walipofika hapo ni kweli waliyaona
matone ya damu. Damu ilikuwa
imeganda kuonyesha haikuwa ya
muda ule. Hatua kumi mbele ndani ya
pipa ndani ya chunba kile wakauona
mwili wa mwanamke ukiwa hauna
uhai. Kila mmoja kengele ya hatari
ikagonga kichwani. Hawakuamini kama
hata huyo changudoa alikuwa salama.
Kwa mara ya kwanza wakakili kuwa
walikutqna na mtu anayeijua kazi yake.
Mtu aliyewajua na kuwatambua.
*****
Baada ya Dee plus kupokea maelezo
kutoka kwa masimba, alichokifanya ni
kuondoka usiku ule akiamua kuanzia
pale hotelini. Alitambua kazi ya
kumpata changudoa yule ilikuwa rahisi
kuliko kwenda kuharibu camera za
usalama. Hakutaka kuchukua gari yake
kwa kuhofia kujulikana. Bali
alichofanya ni kuchukua usafiri wa
pikipiki ambao ulimpeleka mpaka
magomeni. Akashuka kama mtu wa
kawaida, kisha akaongoza mpaka
hotelini. Alipanda ngazi kama mteja,
lakini wakati anatokea mapokezi
akapokelewa na mhudumu
anayeonekana ni mwenye wasiwasi.
Uso wake ulikuwa ukiongea hofu tu.
Alionyesha woga wawaziwazi. Dee
plus akatabasamu ili kuitoa hofu kwa
mwanamke yule. Lakini hilo
halikufanikiwa, mwanadada yule
alikuwa na hofu. Kuna wakati alijaribu
kuongea vitu lakini hayakusika
masikioni kwa dee plus.
"Habari yako mrembo? Dee plus
aliamua kujizungumzisha ili kujaribu
kumvuta mwanamke yule. Lakini bado
salamu haikujibiwa.
"Kaka naomba nikwambie kitu lakini
sio hapa." Akaropoka mwanamke yule
akionyesha kupagawa. Dee plus
akatingisha kichwa, kwa mara ya
kwanza alikubaliana na masimba suala
la kutaka kuwasafirisha watu hawa.
Kwa muonekano wa huyu mhudumu
asingeweza kuufumba mdomo wake
kama angekutana na wanausalama.
Hakuchelewa kumvuta mpaka sehemu
aliyotakiwa. Binti naye bila kujua
ameletewa tiketi ya kifo, akaufumbua
mdomo na kutaka kuongea...
hakupewa hiyo nafasi, tayari basi
lilimfika tayari kwa kumchukua. Risasi
mbili kutoka kwenye bastola yenye
kuzuia mlio zilipenya upande wa
kushoto wa kifua chake. Hakuweza
kupiga ukelele wowote. Alitupwa
umbali wa hatua tatu akaanguka chini.
Alikuwa maiti tayari. Baada ya
kuhakikisha mwanamke yule
hatafumbua mdomo tena, akamuinua
na kumtupia ndani ya pipa. Sasa
alikuwa akihamia kwenye chumba cha
camera za usalama katika hoteli ile.
Aliwapita wana usalama akiwa amevaa
kitamburisho kama mfanyakazi wa
hoteli ile. Akaingia pasipokuonyesha
wasiwasi. Muda wa dakika kumi
akatoka ndani akiwa ameshaimaliza
kazi na sasa ilikuwa safari ya kuelekea
nyumbani kwa changudoa yule.
Akawapita wanq usalama kwa mara ya
pili bila kushtukiwa na yoyote yule.
*******
Ni nyumba yenye watu wengi, nyumba
ambayo asubuhi hii iliwakuta watu
wakiwa kwenye vikundi vidogo vidogo
wakijadili na kuongea kuhusu kifo cha
waziri mkuu wa nchi. Kila mmoja
alikuwa akiongea kile ambacho ana
uhakika nacho. Huku wengine
wakiongelee kuuawa kwa waziri
kunatokana na mwanamke, wengine
walikuwa wakilihusisha hili suala na
mtifuano wa kisiasa unaoendelea
nchini. Watu kutekwa na watu
wasiofahamika ni kitu ambacho
kiliufanya mjadala juu ya kifo cha
kiongozi mkuu wa nchi upambe moto.
Wakati wakijadiliana hilo,
wakashtushwa na gari jeusi likisimama
mbele ya uwanja wa nyuma ile. Kabla
hawajakaa vizuri, wakashtushwa na
kuwaona watu wanne wakishuka.
Ushukaji wa watu wale ulikuwa ukitia
fora na kuogopesha miongoni mwa
watu wachache waliokuwepo pale.
Kila mmoja akaliacha alilokuwa
anaongea, macho yao sasa yalikuwa
kwa watu ambao tayari walishaufikia
mlango wa nyumba ile. Hakuna
aliyeinua mdomo kuongea chochote.
Sura za watu hawa hazikuwa sura za
kawaida. Punde mmiliki wa nyumba ile
akafika naye akionekana ni mwenye
wasiwasi. Macho ya watu waliokuwa
wakimtizama yalimfanya atetemeke.
Hakuna aliyeongea chochote zaidi
kutoa kitu mfano wa picha na
kumuonyesha. Mama yule akaipokea
na kuitizama. Bila kuongea chochote
akawaongoza watu wale kuingia
ndani. Hatua mbili tatu akawaonyesha
kwa kidole chumba anachoishi
msichana yule. Sekunde moja
wanausalama walikuwa mlangoni mwa
chumba kile. Kila mmoja bastola
ilikuwa ikitizama ndani. Ukagongwa
kidogo, lakini cha kushangaza mlango
ukafunguka kuonyesha haukuwa
umefungwa.
Wanausalama wakaangaliana huku
kengele za tahadhari zikigonga
kichwani. Mmoja akaukamata mlango
na kuufungua taratibu. Wote macho
yao yakatizama ndani...
wakaushuhudia mwili wa mwanamke
ukiwa mtupu umelala kitandani
pembeni kidogo kukiwa na dimbwi
kubwa la damu. Wote wakaangaliana.
Simu za upepo zikatembea kona zote
za nchi. Sasa kila kitu kilikuwa kigumu.
Wanausalama wakaingia na kuuanza
kuuchunguza. Risasi mbili za kifua
upande wa kushoto zilitosha
kuuchukua uhai wa mwanamke huyu.
Licha kupekuwa kila sehemu, lakini
wanausalama wale hawakufanikiwa
kugundua ama kupata chochote.
Wakatoka nje na kumuita tena mama
mwenye nyumba, safari hii
wakamuomba awaitie wapangaji
waliokuwepo hapo usiku uliopita.
Mama yule akawaita wote, kisha
akawatambulisha kwa wana usalama.
Kila mmoja akanyamaza kimyq huku
wengine presha ikianza kupanda.
"Sisi ni wanausalama tumekuja hapa
kufuatilia kuhusu mauaji yaliyotokea
usiku wa jana." Alijitambulisha mmoja
huku akionyesha kitambulisho chake.
Wapangaji wote wakatizamana.
Wakatizamana huku sura zao
zikishindwa kuuficha mshangao.
Mshangao ambao hata wana usalama
wenyewe waliligundua hilo.
Haiwezekani kifo cha mtu mkubwa
nchini uchungizi uje ufanyike pale.
Kama kawaida ya wanawake wa
magomeni walivyo na midomo mirefu,
hawakuchelewa kuuliza hilo.
"Sasa kipi mmetuitia hapa? Ina maana
mauaji ya waziri yamefanywa na mtu
wa nyumba? Alihoji mama chausiku
huku akiwaangalia wana usalama kwa
zamu.
Hawakumuangalia yeye bali walitoa
ishara wapangaji wa sogee. Wakafanya
hivyo, mmoja ya wana usalama
akaufungua mlango na kuwataka wote
waangalie ndani. Kila mmoja akafanya
hivyo.
Maelezo ya picha hayapo.

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 029
Wapangaji na mwenye nyumba wote
wakatupa macho yao chumbani kwa
msichana yule. Hakuna aliyeshindwa
kunyamaza, kila mmoja akalitaja jina la
mungu kwa imani yake. Wapo
waliopiga mayowe na wapo
walionung'unika moyoni. Mama
mwenye nyumba akabaki ameduwaa
kana kwamba alikuwa haamini kile
alichokiona. Dimbwi la damu pembeni
ya mpangaji wake lilimfanya ahisi
presha kupanda. Wanausalama
wakaufunga mlango na kuwageukia
wapangaji tayari kwa kuwahoji.
"Nani ambaye alikuwepo jana wakati
marehemu akirudi? Lilikuwa swali la
kwanza kuulizwa. Wapangaji wote
wakaacha kulia, wakanyamaza na
kuanza kuwaangalia. Mara mmoja wa
kike akajitokeza mbele.
"Wewe ndiye ulimuona akirudi?
Akaulizwa tena.
"Hapana! Bali tulikuwa wote pale
travertine hotel, mpaka pale
alipotokea mkaka mmoja na
kumchukua." Akajibu yule msichana
huku akiendelea kulia. Jibu lake hilo
likawafanya wapelelezi wale
waangaliane.
"Yukoje huyo mtu? Na alikuja kama
nani? Swali jingine akarushiwa.
"Ni kijana mmoja hivi mwenye mwili
uliojengeka kimazoezi, ukimuangalia
kwa woga unaweza kudhani ni mcheza
sinema wa Hollywood. Na pale alikuja
kama mteja na kumchukua
mwenzetu." Akajibu yule dada. Jibu la
kwanza likawafanya watizamane
kwanza. "Ana mwili wa mazoezi,
ukimtizama kwa woga unaweza
kudhani ni mcheza sinema wa
Hollywood. " yalikuwa maneno
yaliyojirudia vichwani mwa wana
usalama wale. Jina Masimba lilijengeka
ndani ya akili zao.
"Baada ya hapo ikawaje baada ya
kuondoka na huyo mtu? Lilikuwa swali
jingine. "Baada ya hapo sikumuona
tena mpaka sasa mlipokuja nyie ndio
nagundua kumbe Rose ameuawa."
Akajibu msichana yule na kuangua
kilio. Wanausalama wakaangaliana
tena. Wakiwa bado hawajaamua
kuendelea na maswali, wakamuona
msichana mwingine akisogea mbele na
kusimama.
"Mimi nilimuona wakati anaingia, na
muda mfupi baada ya kuingia alikuja
mwanaume na kumuulizia. Kwa kuwa
mara nyingi sana anafuatagwa sana,
nikamuonyesha huyo kijana chumba
chake. Baada kumuonyesha sikumuona
huyo mwanaume alipotoka na muda
huu ndio mmenishtua kuniambia Rose
amekufa." Akaeleza mwanamke yule.
"Je mtu aliyekuja mara hii anafanana
na huyo aliyetajwa na mwenzako?
Wakauluza wana usalama. "Hapana
hawafanani kabisa, huyu hakuwa yule
aliyeshuka kule hotelini. Licha ya huyu
naye kuwa na mwili wa mazoezi, pia
alikuwa mweupe na mwenye kovu
kwenye jicho la kushoto." Akajibu
mdada yule.
"Dee plus" lilikuwa jina lililopita
vichwani mwao. Sasa walikuwa
wamepata picha, aliyeshuka kule
hotelini yalikofanyika mauaji alikuwa
masimba. Aliyekuja kufanya mauaji ya
changudoa aliyenunuliwa na Masimba
alikuwa Dee plus. Hapa imekuaje? Kwa
nini mtu aingie ndani na masimba
kisha aje auawe na Dee plus? Ina
maana huyu Changudoa alikuwa na
Masimba wakati akitekeleza mauaji ya
waziri mkuu? Kwa hiyo baada
yachangudoa huyu kushuhudia kifo cha
waziri mkuu kilichofanywa na
Masimba, wakaona nao wampoteze ili
kupoteza ushahidi? Kipi kipo nyuma ya
mauaji haya? Kwa nini waziri alikuwa
akimshawishi DG wa TISS wampoteze
masimba? Yalikuwa maswali mazito
ambayo yangepaswa kujibiwa na
wahusika wenyewe. Wakati wakijiuliza
hayo ikaingia simu kutoka kwa wenzao
ambao walikuwa hoteli. Ni simu hiyo
ambayo ilizidi kuwachanganya. Camera
za usalama hazikuonyesha chochote
katika hoteli hiyo. Hata waziri mkuu
akiingia hazikuonyesha chochote.
Kubwa zaidi ni kwamba mhudumu
aliyekuwa zamu usiku hapo hotelini
ameuawa kwa kupigwa Risasi mbili
kifuani tena kwa staili kama aliyouawa
huyu changudoa. Wakaangaliana tena
na tena. Kazi ilikuwa ngumu
kupindukia.
******
Kwanza alihisi kama alikuwa ndotoni
akiota kitu ambacho kamwe
kisingeweza kutokea. Akajaribu
kujitingisha kuona kama alikuwa kweli
anaota. Hapana haikuwa hivyo,
haikuwa hivyo kwa kuwa bado alikuwa
akikisikia kilekile alichokisikia hapo
mwanzo. Ilikuwa sauti ya mtangazaji
wa Televsheni akitangaza kifo cha mtu
anayemfahamu kwa ukaribu zaidi.
Sekunde hii alikuwa akifumbua macho
yake na kushangaa akipokewa na nuru
safi yenye kuangaza mfano wa Jua la
asubuhi. Alikuwa hana nguo hata moja
mwilini huku akiwa amefunikwa kwa
shuka safi na zito. Hilo hakulitilia
mashaka, bado alitaka kuliona kwa
macho kile alichokuwa akikisikia.
Maumivu ya kisogoni bado hakutaka
kuyaulizia maswali. Alitaka kuona na
kusikia, alitaka kujua kama ni kweli kile
alichokisia. Kwa taratibu akageuza
macho yake na kutizama kule ilipo tv.
Macho yake yakapokewa na wana
Usalama wakionyesja kuhaha. Polisi
walikuwa wametanda kila sehemu
wakipekua na kuwahoji watu wote.
Maandishi yaliyopita chini ndio
yaliyompa kiwewe. Ni kweli ama
naota? Waziri ameuawa vipi? Ni nani
amemuua huyu? Yalikuwa maswali
ambayo yalimfanya akae kitako na
kushika tama. Akauona muda ule ni
wakujua alikuaje mpaka akafika pale.
Kumbukumbu yake ikaanza kurudi
taratibu, kwanza alikuwa mkuranga
kummaliza mama wa asteria. Wakarudi
mpaka katikati ya mji katika moja ya
majengo ya siri ya usalama wa taifa.
Hapo wakajaribu kumpigia masimba ili
kumjua alipo kwa kutumia mitambo
yao. Simu ya Masimba haikupokelewa..
lakini ndani ya nusu saa masimba
akapiga tena akiwa jirani na hapo.
Akakumbuka walipoondoka mpaka
kinondoni akiwa sambamba na
mwamvita. Punde tukio zima
likajirudia. Hasa kuwekewa bunduki
kisha kupigwa kwa kitako cha bastola
kisogoni. Machozi taritibu ya kaanza
kushuka. Alijitolea kwa kila kitu kwa
sababu ya kikundi chao. Akamsaliti
masimba kwa sababu yao. Alifanya kila
kitu kwa sababu ya faida yao, lakini leo
walikuwa wakimsaliti na kutaka
kumuua. Hilo likamuuma sana. Bado
macho yake hayakubanduka kwenye
Tv. "Nani amemuua waziri na kuniokoa
mimi? Ina maana masimba ndio
amefanya hay..... Kabla hajamaliza
kujiuliza maswali mlango wa chumba
alichopo ukafunguliwa. Akageuka na
kutizama huko. Macho yake
yakakutana na macho ya masimba
aliyekuwa akiingia. Teddy hakuuficha
mshangao machoni mwake sambamba
na hofu usoni mwake. Macho yake
yakashindwa kumiangalia kwa muda
mrefu. Maswali na aibu ya usaliti
vikauvaa uso wake. Ni masimba huyu
huyu aliyemuokoa mara ya kwanza
katika mazingira ya kifo. Ni masimba
huyu tena amemuokoa kwa mara ya
pili tena kwa kumuua mtu ambaye
yeye alimuogopa sana. Hakuwa na
shaka kwamba masimba ndiye
aliyemuua waziri mkuu. Lakini swali
alimuuaje mtu ambaye alikuwa na VIP
PROTECTION kwa kila anapotembea na
kuwa mahala popote? Je baada ya
kuzimia kutokana na kupigwa
alipelekwa wapi? Na kwa nini
walimgeuka wakati alishaamua kurudi
kwao? Hapo ndipo alipoukaza uso
wake na kumuangalia masimba usoni,
akitegemea kukutana na mikunjo ya
hasira. Haikuwa hivyo, tabasamu
lilitanda usoni kwa masimba. Macho
yake yalikuwa yakimuangalia Teddy
katika utulivu. Teddy akashindwa
kuvumilia, sekunde hii alikuwa
amesimama akipiga hatua kumfuata
Masimba. Alikuwa akitembea kwa
kuyumba. Bado tabasamu lilitanda
usoni kwa masimba. Tabasamu ambalo
lilitoweka ghafla baada ya teddy
kusimama mbele yake. Tukio la
kulipuka nyumba ya mama wa asteria
na kusababisha kifo chake na mjukuu
lilijirudia. Bastola ilikuwa mkononi
mdomo wake ukimtizama teddy.
Hapakuwepo utani kabisa machoni
kwa masimba. Teddy akashtuka kisha
baridi ikauvaa mwili wake. Kidole cha
masimba kikashuka mpaka kwenye
trigger. Sasa alikuwa akikivuta kitufe
tayari kwa kumlipua teddy. NIWAKATI
HUO HUO MLIPUKO MDOGO UKASIKIKA
HUMO NDANI.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 
Nitakupata tu
Sehemu ya 030.
Chumba kizima kilikuwa kimya, kila
mmoja akiwa amejiinamia chini
akiwaza na kuwazua.hakuna aliyeamini
taarifa kwamba waziri amekufa. Tena
amekufa kwa kupigwa risasi. Ameuawa
vipi? Na nani? Teddy? Ama ni nani?
Yalikuwa maswali tata, yalikuwa
maswali ambayo yalikosa majibu. Wao
ndio walikuwa na waziri, wao ndio
waliokwenda na waziri kule
magomeni. Wakamuacha na teddy
pale hotelini kwa pendekezo lake.
Alitaka kumuonja teddy autambue
utamu wake, alipanga
atakapofanikisha hilo basi atamuua
Teddy kwa mikono yake. Lakini
kinyume chake waziri ameuawa yeye
huku akiachwa peke yake. Hakuna
mlinzi aliyemshuhudia teddy au muuaji
akitoka chumbani kwa waziri. Hicho
kilikuwa kitendawili, kitendawili
ambacho hakikupata mtenguaji.
Hakuna ambaye haujui ulinzi wa
viongozi wa nchi. Hakuna asiyejua
wanausalama wanavyokuwa makini
katika kazi yao. Lakini Usiku wa Jana
walinzi hao hawakutenda
kilichozoeleka. Hapo wakauona
mwisho wao, mwisho wa maovu yote
waliokuea wakitenda. Waliishi kifahari
na kufanya kila kitu wakilindwa na mtu
ambaye Leo hii alikuwa hayati.
Wakiliwaza hilo punde wakauona
mlango ukisukumwa kisha sura ya
mwanadada akijipenyeza hapo ndani.
Alikuwa mwamvita akitembea
akionyesha kuchoka. Hata yeye sasa
alikuwa akiona muda unakwenda
ndivyo sivyo. Yalikuwa mmoja kati ya
watu waliotumwa kwenda kunusa
kilichopo nyumba ya kifo cha mfadhili
wao. Mkononi alikuwa amekamatia
kitu mfano wa karatasi. Baada ya
kusogea mpaka karibu na watu wale
akabwaga kitu alichokishika mkononi.
Watu wale wakasogea kila mmoja
akielekeza Hicho lake pale mezani.
Macho yao yakajikuta yakiangalia picha
mbaya. Wasichana wawili tofauti
walikuwa wameuawa katika staili mbili
tofauti. Wakati mmoja akionyesha
kulala katikati ya dimbwi la damu,
huyu wa pili alionekana amewekwa
ndani ya pila, lakini kitu
kilichowasisimua zaidi, ni pale
kugundua kila marehemu alikuwa na
matundu ya risasi upande wa kushoto
wa kifua. Hilo likawafanya kwanza
wawe kimya wakimtizama Mwamvita
Usoni. Bado hawakuijua sababu ya
kuwaletea zile picha. Lakini baada ya
kuangaliana kwa mda huku macho ya
mwamvita yakiongea, wakarudisha
macho pale chini. Jimmy akaziangalia
sura za marehemu wale kwa sekunde
tano tu, akawakumbuka.
Aliwakumbuka wote kwa pamoja.
Mmoja alikuwa mhudumu wa hoteli
yalikofanyika mauaji, na mwingine
alikuwa ni changudoa, Naye alikuwa
akifanyia biashara pale pale travertine
magomeni. Hapo akaunganisha picha
na kupata jibu kwa nini picha zilikuwa
pale.
"Wamesafirishwa kama kufumbwa
midomo. Hawa ndio wangetupa majibu
juu ya kilichotokea. Ni wakati wa
kufanyakazi bila kumtegemea mtu.
Tukae tukijua kuwa hata sisi
tutachunguzwa. Tutaanza kufuatiliwa
na tutanuswa kila tutakapo pita. Jimmy
nadhani wewe utahojiwa, nadhani
utafuatiliwa kuliko sisi. Unatakiwa
makini zaidi. Kama teddy yupo salama
mpaka mud huu ni lazima atataka
kulipiza kwa kilichotokea. Naadhani
mapambano yameanza sasa." Aliongea
mwamvita huku akiendelea kutizama
zile picha. Wrote mle ndani wakaafiki.
Ilikuwa lazima wamsake Teddy.
****
Ofisi za idara ya usalama wa taifa
zilikuwa katika hekaheka kubwa.
Vijana walikuwa mtaani wakinusa na
kutafuta chochote. Shinikizo kutoka
kwa rais ndio kitu kilichokuwa
kikiivuruga akili ya mkurugenzi wa
usalama wa Taifa Mr Godliving Kimaro.
Muda wote alikuwa akipakipigiwa
simuakiulizwa hili na lile. Hasa
akiulizwa wapi amefikia katika suala
hili. Kichwa chake kilikuwa
kimevurugika, hakuwa akijua wapi pa
kuanzia na hata kumalizia. Taarifa za
kwamba mhudumu wa Zamu katika
hoteli alimouawa WazirWaziri naye
ameuawa katika aina ya kuufumba
mdomo asiongee chochote.
Changudoa aliyesemekana kwamba
ameonekana akiwa na mwanaume
anayetuhumiwa kufanya unyama huo
naye ameuawa. Tena wote wakiuawa
katika staili moja kwakupigwa risasi
kifuani. "Alikuwa kijana aliyejengeka
kimazoezi mwenye muonekano kama
mcheza sinema. Begani alimbeba
msichana aliyeonekana kupoteza
fahamu" alikuwa akiirudia taarifa
aliyotumiwa na vijana wake. Taarifa
ambayo bado haikumfumbua na
kumtoa gizani katika sakati hili.
Kilikuwa ni lazima ajue na atambue
nani alionekana na waziri kabla ya kifo
chake. Hakuchelewa katika hilo, muda
mfupi baadae simu yake ilikuwa sikioni
akiipiga namba Fulani.
[4/12, 16:11] ibrahim: Simu ilikuwa
sikioni akiongea na namba Fulani.
Alikuwa akitoa maelekezo ya nini
kifanyike katika muda ule. Wana
usalama hawakuwa wametulia, kila
sehemu walijaa. Mpaka inafika jioni
bado hapakuwa na chochote cha
maana kilichofanyika. Kila mmoja
alikuwa akihisi na kuongea hiki. Ni
katika hao mmoja peke take ndiye
alikaribia kufahamu ukweli. Suala
kwamba aliyeua alikuwa Masimba hilo
hakuwa na shaka nalo, lakini
angemuaminisha vipi mkurugenzi?
Akaona huu ulikuwa wakati
wakuliondoa suala hili katika
kutuhumiwa kina jimmy na
kulihamishia mikononi kwa Masimba.
Alitambua kama likiachwa kisha
lijekugundulika kwamba waziri alikuwa
nyuma ya biashara haramu hata wao
wasingepona. Akainuka na kuuendea
mlango wa chumba chake. Akaufungua
mlango na kutoka nje. Alihitaji kwenda
kumuona mkurugenzi wa usalama.
Huyu alikuwa mmoja kati ya wale
waliompa kazi masimba
[4/12, 17:48] +255 717 808 444:
Alikuwa ni yule aliyempa masimba kazi
ya kufuatilia mzigo wao. Kazi ambayo
ndio iliyomfanya masimba kuingia
katika matatizo haya , matatizo
yakuweka rehani maisha yake kwa
kunusurika kulipuliwa pale
alipotegewa Bomu kwenye gari. Lakini
Leo alikuwa ameamua kuukandamiza
msumali wa moto katika kidonda
kibichi. Gari yake ya kifahari ikatembea
kwa mwendo wa taratibu katika
barabara za hili jiji. Mawazo ilikuwa ni
kujivua katika hili ambalo kama
lingefanikiwa basi wangekuwa sehemu
nyingine. Lakini kwa kuwa
halikufanikiwa basi aliamua kulitenda
hili taratibu na akiwa peke yake.
Hakupenda kuwaambia wala
kuwashilikisha wenzake. Gari ikaenda
kuegeshwa kwenye maegesho ya
magari katikati ya jiji la dar es salaam.
Akatembea kwa miguu akielekea
katikati ya jengo moja ambalo
hutumiwa sana na Idara ya usalama wa
Taifa. Muda wote aliokuwa akitembea
hakuacha kuangalia nyuma, alikuwa
akihofu kuwa alikuwa akifuatiliwa.
Hata alipogeuka hakumuona yeyote,
wala kuona macho yanayomtazama
kwa hila. Akaufikia mlango wa jengo
hilo , vijana waliokuwa pembeni
wakamuangalia sekunde kadhaa kisha
wakaonyesha kumuacha aendelee na
safari yake. Hawakumuacha tu kwa
kumuacha Bali ilikuwa amri kutoka
ndani. Akaufungua mlango kisha
kuuruhusu mwili wake uingie.. Miguu
ikitembea kuelekea ndani kabisa.
Macho machache yalimtizama na
mengine mengi kumpuuza. Aliamua
kufanya hivyo, aliamua kuusema
ukweli ili ijulikane nani amehusika
kuisafirisha roho ya Waziri.
*****
Mdomo wa bastola ulikuwa
ukimtizame Teddy. Sura ya mtu asiye
na masihara ilikuwa mbele yake.
Alimjua masimba kwa mda mrefu,
lakini hakuwahi kumuona akiwa katika
hali hii. Hasira, chuki, na neno kifo ndio
kitu pekee kilichosomeka kwenye USO
wa mtu huyu. Macho yake
yakashuhudia vidole vikishuka taratibu
katika kitufe cha kufyatulia risasi.
Teddy akatamani kuongea kitu.
Mdomo haukufumbuka na wala
maneno hayakutoka. Akabaki
kumuangalia masimba katika sina ya
upole na kutia huruma. Alikuwa ni
mwenye majuto. Hakuweza kuvuta
hata sekunde alishuhudia Risasi Ikipita
pembeni kidogo ya kichwa chake na
kwenda kuchimba ukutani. Teddy
Hakuamini Macho yake, Akaporomoka
chinu akiuomba msamaha, lakini
Masimba hakuwepo pale. Alishaondoka
mbele yake.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 031
alihitaji kuongea chochote na
masimba, alihitaji kuuomba
msamaha katika matendo yote
aliyoyatenda. lakini masimba
hakuwepo, hakumuona mbele ya
macho yake. kwa mara nyingine
akajaribu kuirudisha kumbukumbu,
kumbukumbu ambayo hakuwa
nayo. amefikaje mikononi kwa
masimba? wakati alikuwa
sambamba na mwamvita na
wanausalama wengine? nini
kilinitokea? hapo akauruhusu
mkono wake kushika nyuma ya
kisogo. jeraha dogo ndio kitu
kilichoirudisha kumbukumbu. naam
alikumbuka kile kilichofanywa juu
yake pale waliposimama pale
kinondoni. hapo tukio zima
likajirudia. akasimama na kuyaendea
mavazi yake ambayo yalikuwa
pembeni kidogo mwa kitanda.
akayavaa. akafunua mtoto wa
kitanda, macho yake yakatua
kwenye bastola yake sambamba na
vitu vyake vingine. akavichukua na
kuvisunda mifukoni. dakika
zilizofuata alikuwa akishuka ngazi
akiicha nyumba ile huku kichwa
kikiwa kizito. hakujua kile
kilichosababisha wenzake
wamgeuke. aliua na kumsaliti
masimba lakini bado hakuonekana
kufanya lolote kwa wenzake. kwa
wakati huu hakuwa muoga tena.
aliamua kupambana nakundi lake.
kama mzigo wa madawa alikuwa na
uhakika kuwa anao masimba, sasa
kipi ambacho kina mfanya
asisaidiane na masimba? .alimaliza
kushuka ngazi na kuufikia mlango
wa kutokea nje, akaufungua
taratibu na kutupia macho yake kwa
nje, alishangaa kukutana na vichaka,
vichaka ambavyo viliizunguka
nyumba nzima. katikati kulikuwa na
kijinjia chembamba ambacho
kilitumika kama njia kwa watu
wanaoishi hapo. Hilo likamshangaza
kwanza. hakuwa anapajua pale,
hakuwa anaijua sehemu ile. akajipa
moyo na kutoka katika nyumba ile
akikifuata kile kinjia chembamba.
alitembea katikati huku macho yake
yakizunguka huku na huko,
mazingira hayakuwa rafiki sana ki
usalama kwake. sehemu ile
haikuonyesha kuwa makazi ya watu
na hapakuwa dalili ya uwepo wa
watu. alitembea kwa muda wa
dakika kumi bila kukutana na mtu.
hilo likaendelea kumtisha na kumtia
hofu. lakini ni ndani ya muda ule
akausikia ngurumo wa pikipiki.
[4/14, 14:01] ibrahim: Ni katika muda
ule ule akausikia mngurumo wa
pikipiki katika maeneo ya jirani na
pale alipokuwa akiendelea
kutembea. Mngurumo ule
ukaendelea kusogea, sasa alikuwa
akiusikia ukisogea karibu kabisa na
yeye. Muda mfupi teddy alikuwa
amehama pale njiani na kujitupa
pembezoni mwa barabara. Sasa
alikuwa nyuma ya kichaka akitizama
kule barabarani. Haikupita hata
dakika akaiona pikipiki aina ya
Honda ikitokea. Juu yake alikaa MTU
ambaye alimfahamu. Juu yake alikaa
mwana usalama dee plus. Alikuwa
akiiendesha pikipiki kanakwanba
hapa kuwa na hatari kwake. Teddy
akamuangalia sana dee plus mpaka
alipopotea machoni. Masimba, kisha
dee plus! Kuna nini hapa? Ina
maaana Dee yupo na Masimba katika
suala hili? Yalikuwa maswali ambayo
hayakuwa na majibu.
*****
Walichoka vichwa vyao, hawakuwa
wameupata usingizi tokea
walipopata taarifa ya kifo cha waziri
mkuu. Walikuwa wakikesha
wakinusa hiki na kile. Mkanganyiko
uliojitokeza katika kifo cha waziri
mkuu. Kitendo cha watu ambao
wangeweza kuwapa mwanga
katika mkasa huu kuuawa kulizidi
kuwapa ugumu katika kumjua
muuaji kwa kuwa mpaka sasa
walikuwa wakimhisi Masimba
kutokana na wajihi wa muuaji
waliopewa na dereva tax. Simu
zilikuwa zikimiminika kutoka kwa
wana usalama mbalimbali
[4/14, 18:39] ibrahim: Wana usalama
walikua wakiripoti kutoka kila
sehemu. Licha ya hivyo hakuna
ripoti yoyote ambayo iliwasaidia
kumpata muuaji ama kusaidia japo
kupatikana kwa mwanga katika hili.
Walihangaika zaidi ya kuhangaika.
Walipekuwa kila sehemu lakini bado
hawakupata chochote cha
kuwasaidia. Sasa kila mmoja alikuwa
amechoka na kuchoka, kila mmoja
alitamani kusema ameshindwa, kila
mmoja alitamani japo kupata dakika
tatu za usingizi. Lakini haikuwa
hivyo. Simu za chief zilikuwa
zikiwasumbua sana. Kila wakati
alihitaji kujua walipoishia katika hili.
Ni wakati kila mmoja ameinama chini
akifikiria hilo, simu ya mmoja kati
yao ikaupata uhai. Simu ilikuwa
ikiita. Mwana usalama yule
akaichukua simu kisha kuitizama.
Aliikuta namba mpya, aliikuta namba
ambayo haikuwa imehifadhiwa.
Kabla hajaipokea akatoa ishara ya
kuiunganisha simu ile. Baada ya
hapo akaipokea.. " Magomeni Makuti
nyumba namba 089 kuna MTU
atawafaa katika tukio hili." Baada ya
kauli hiyo simu ikakatwa na simu
kuzimwa kabisa. Wote
wakatizamana... Hawakutaka
kuchelewa, simu zikapigwa sehemu
mbalimbali, wapelelezi waliokaribu
na sehemu lilipotokea tukio
wakaanza kusogea sehemu
walioambiwa. Hata wale waliokuwa
katika ofisi za muda nao walitoka
wakielekea huko. Kila mmoja
alikuwa akiifikiria ile simu. Simu
iliyopigwa na MTU asiefahamika.
Dakika kumi na tano baadae
walikuwa karibu kabisa na nyumba
husika. Macho yao yakiwanusa
askari kanzu kibao waliosimama
kama wahuni ama watu wenye
mambo yao. Makachero wale
wakashuka kisha wawili
wakaongoza kuelekea kwenye ile
nyumba. Wakati wanaukaribia
mlango mkubwa wa kuingilia ndani
ya nyumba ile, wakawaona
wasichana wawili wamesimama
wakionyesha kuongea kitu. Maafisa
wale wakasogea mpaka karibu yao.
Kabla hawajatoa salamu,
wakamsikia msichana mmoja kati ya
wale waliosimama akimuaga
mwenzake. Hawakujishuhulisha
naye, macho yao yote yalikuwa
katika mazingira yanayoizunguka
nyumba ile. Kila sehemu ilijaa watu
wao.. Wakamfikia mwana Dada yule
kisha kumsabahi. Baada ya salamu
wakamueleza kile ambacho
walikifuata pale. Kubwa likiwa ni
kuwa wanamgeni wao katika
nyumba ile.
Binti akakitigisha kichwa chake huku
akiwatizama vijana waliosimama
mbele yake. " Nyie ndio wageni wa
Khadija? hatimaye akauliza binti .
"Ndiyo, sisi ndiye haswa wageni."
Baada ya kuangaliana kwa nukta
hatimaye wakajibu. Binti hakuongea
tena, aliwakaribisha na kuwaongoza
kuelekea chumba cha huyo Khadija.
Wana usalama walikuwa makini kwa
kila hatua. Mazingira ya jumba lile ,
yalikuwa yakitia mashaka. Kufika
mbele kidogo binti akaonyesha
kidole akiwaonyesha makachero
wale chumba cha huyo Khadija.
Wana usalama wakamtaka
wangozane ili awe mgongaji. Binti
hakubisha, hatua tano mbele wote
walikuwa wamesimama mlangoni
mwa chumba cha Khadija. Binti
waliyemkuta akaanza kuugonga
mlango, licha ya kuugonga kwa
muda mrefu, lakini hapakuwa na
uitikiaji kutoka ndani. Kengele za
hatari zikagonga vichwani mwa
makachero wale. Mikono ikashuka
na kuingia mifukoni mwao,
wakampa ishara binti. Ishara ya
kujaribu kuufungua mlango.. Binti
akashika kitasa na kukinyonga.
Mlango ukafunguka, wakati huo huo
macho ya wana usalama yakatua
ndani "Damu" ni neno lililogonga
vichwa vyao.. Hatua iliyofuata wote
walikuwa wamesimama mbele ya
maiti ya mwanamke, Kisu kikubwa
kikionekana kuzama tumboni..
WAKATIZAMANA
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 032
Kisu kilizamishwa katikati ya tumbo la
mwanadada yule. Wana usalama
wakatizamana na kutizamana. Mtu wa
tatu mwenyekufahamu juu ya
kilichotokea alikuwa ameuawa
kinyama. Nani amelifanya na hili? Nani
amemjua huyu mwanamke? Walikuwa
kwenye bumbuwazi la takribani
sekunde kumi. Kila mmoja alikuwa
amesafiri kimawazo, kila mmoja
alikuwa akiwaza kile walich0kutana
nach0. Maiti ya msichana huyu ilikuwa
imetulia kitandani. Binti
aliyewasindikiza hapo naye alikuwa
katika fadhaha. Hakuwa akiamini kile
alichokuwa akikitizama mbele ya
macho yake. Ni dakika tano zimepita
tokea alipokuja yule mwanamke,
mwanamke mwenye shangwe na
bashasha, mwanamke
aliyemchangamkia kana kwamba
wanafahamiana. Ni mwanamke huyu
aliyemuulizia marehemu, ni
mwanamke huyu aliyeingia chunbani
kwa marehemu na kutoka. Kutoka
katika muda ule ule, hakukawia tokea
kuingia na hata kutoka. "Ni yeye, ni
yeye aliyemuua!! Hii ilikuwa sauti
iliyotamkwa na kupenya katika ngoma
za masikio ya makachero waliokuwa
wamepigwa butwaa. Macho
yakamuangalia dada huyu kisha swali
likafuatia. Swali ambalo liliulizwa na
makachero wote. "Nani?...
"Mwanamke!!. Akajibu huku
akiendelea kufuta machozi.
"Mwanamke gani? Wakauliza tena
wanausalama. "Mliyenikuta naye hapo
nje. Ni yeye aliyemuulizia marehemu
na ni yeye aliyetoka humu chumbani.
Harafu pia hata marehemu
aliyoonyesha kutokumfahamu huyu
mwanamke." Alijibu mwanamke yule.
Wanausalama wakamuangalia
wakimkazia macho. Bado walikuwa
katika kiza kizito. Sekunde mbili
baadae simu zikasambaa kila kona.
Mwanamke mwembamba mrefu
afuatiliwe na kukamatwa. Kwa kuwa
nyumba ile ilikuwa imezungukwa na
wana usalama, haikuwa vigumu
kumkunbuka mwanamama huyu.
Kwani wakati akitoka kwenye ile
nyumba walimuona. Licha ya kumuona
lakini walikuwa wameshachelewa,
kwani wakati taarifa inakuja tayari
mwanamke yule alikuwa amekwisha
tokomea. Licha ya wana usalama
kuhangaika na kuwasiliana kwa muda
ule, hapakupatikana taarifa yoyote ya
kuwasaidia. Wote wakarudisha macho
yao tena kwa binti yule. Walihitaji
kupata mawili matatu kutoka kwa
mwanadada yule juu ya mwanamke
aliyemhisi kufanya mauaji hayo.
"Sisi ni maafisa wa polisi, tuko hapa
kumfuatilia marehemu baada ya
kuambiwa ana habari fulani."
Vitambulisho vyao vilikuwa mbele
kumuaminisha mwanamke yule. Baada
ya kuviangalia kwa muda, mwanamke
yule akawarudishia huku akionekana
akitetemeka kwa mbali. "Tunahitaji
kujua kuhusu marehemu. Alikuwa
nani? Alifanya kazi wapi? Na kipi
kingine unafahamu ambacho kinaweza
kuwa ndio chanzo cha kifo chake.
Yalikuwa maswali ambayo yalimfanya
mwanadada yule kuangalia juu kama
ni mwenye kufikiria kitu, kisha kwa
sauti ya kukata tamaa akanena.
"Binti alikuwa ni changudoa, hiyo ndio
kazi ambayo ilimuweka hapa mjini.
Akajibu binti huku macho yake
yakiusgangaa mshangao kutoka
kwenye sura za makachero hawa.
"Enhe ukiacha uchangudoa kipi kingine
ambacho alikifanya? Lilikuwa swali la
pili.
"Hakuwa na kazi nyingine zaidi ya
hiyo." Akajibu.
"Biashara hiyo alikuwa akiifanyia wapi?
"Travertine hapo usalama." Akajibu.
Kwa mara nyingine wana usalama
wakatizamana. Wakaki wakitizamana
makachero wale, yule mwanamke
akaongeza. "Kingine ambacho nahisi
kimesababisha huyu binti kuuawa ni
kushuhudia watu wa mwisho kuingia
na waziri pale hotelini sambamba na
rafiki yake kushudia mauaji ya Waziri
mkuu. Wote walikubaliana leo hii
wakaongee na vyombo vya usalama.
"Wana usalama wakaangaliana tena.
Watu wawili waliomuhimu na msaada
mkubwa walikuwa wamesafirishwa
kuzimu. Wamesafirishwa ili kuzibwa
midomo. Hawakutakiwa kufumbua
mdomo kuliongea hili popote na hilo
lilikuwa limefanikiwa.
******
Alihitaji kujiondoa katika hili ambalo
limetokea. Kucharuka kwa wana
usalama kulizua hofu na mashaka
miongoni mwao. Waliiona njia ya
kujitoa katika hili ni kumchoma
masimba kwenye vyombo vya
usalama. Walitaka kushindilia msumari
wakiamini Masimba bado alikuwa
akitafutwa na vyombo vya usalama.
Walilijua hilo kwa kuwa hata wao
walikuwa washirika wa waziri mkuu.
Hata wao walikuwa wakilijua shinikizo
ambalo alikuwa akipewa mkurugenzi
wa Idara ya ujasusi kuhusu kutafutwa
kwa masimba. Wakata kulitumia hilo
kump0teza masimba. Hawakujali kuwa
wao ndi0 walikuwa chanzo, chanzo cha
kile kinachoendelea. Leo hii walikuwa
wamepanga kwenda kuonana na
mkurugenzi wa idara ya ujasusi
nyumbani kwake. Wali0na hii ni kama
njia bora na sahihi kwao katika
kujisafisha na hilo. Muda wao wa
kukutana ilipangwa kufanyika usiku wa
siku hiyo, ilikuwa ni lazima wamuone
kwa njia yoyote.
Ilikuwa usiku wa saa tano, ukimya
ulikuwa umetawala katika viunga
vy0te vya oysterbey. Hapaku0nekana
mtu y0y0te zaidi ya gari moja moja
ambazo zilikuwa zikipita kuelekea
sehemu mbalimbali huku nyingi zikiwa
ni za wakazi wa eneo hilo. Pembeni
kidogo mwa barabara ile alisimama
mtu mmoja macho yake yakitizama
nyumba fulani ambayo ilikuwa mbele
yake. Mtu huyu alikuwa hapo baada ya
kupenyezewa taarifa kuwa wapo watu
ambao walipanga kwenda kulitangazia
taifa kwamba yeye alikuwa ndiye
muuaji aliyeitoa Roho ya waziri.
Ilikuwa taarifa alioipuuza baada ya
kuipata, lakini baada ya kuchunguza
kwa makini majibu alioyapata yalikuwa
ni yale yale. "Unataka upewe hii kesi.
Unachotakiwa ni kuwawahi watu hao"
ulisomeka ujumbe ambao alitumiwa na
wake usiku wa siku ile. Hapo ndipo
alipoamua kutos tiketi kwa watu hawa,
watu ambao wao ndi0 chanzo cha haya
yanayoendelea kufanyika.
Macho yake bad0 yalitizama nyumbani
pale, hapakuonekana uwepo wa watu,
hapaku0nyesha kama kuna mtu ndani
yake. Wakati akiliwaza hilo akaziona
taa za magari zikimulika mbele ya
nyumba ile. Punde akaisikia honi ya
gari. Moyoni akafurahi kwa kuamini
mwenyeji wake alikuwa amerejea na
ulikuwa muda wa kuipeleka tiketi
yake. Akauvuta muda akisubiri geti
lifunguliwe mtu wake aingie ndani.
Muda wote mkono wake ulikuwa juu
ya bast0la yake. Hazikupita dakika
mbili gari ilikuwa imeshaegeshwa
ndani. Mwanaume akaondoka pale
pembezoni mwa barabara na kuanza
kusogea taratibu kuelekea ndani ya
nyumba ile. Giza la usiku lilimfanya
ahisi ni mwanga katika macho yake.
Alilipenda giza kama alivyokuwa
akiipenda bastola yake, haikuwa
bastola tu bali hata mwandani wake.
Mwandani ambaye alimfanya ajihisi yu
peponi kamasio paradise. Akaifikia
nyumba ile kwa karibu san. Ilikuwa
nyumba iliyozungushiwa ukuta mrefu
sana mithili ya jumba la ikulu. Juu ya
ukuta ule kulipitishwa nysta za umeme
na kuufanya uzio ku0nekana ni hatari.
Akaangalia kwa dakika kama mbili,
baada ya hapo akaamua kuingilia
kwenye lango la mbele kule ambapo
alikuwepo mlinzi. Akatembea kama
mpita njia mpaka alipotokea lango la
mbele. Macho yake yapaka yalikuwa
yakiangalia huku na huko.. muda
kidogo akamuona mlinzi akizunguka
zunguka.. Hapo akaamua naye
kujitokeza na kuanza kutembea
akielekea pale.
 
NITAKUPATA TU
SEHEMU YA 033
Muda mfupi baadae alikuwa
akitizamana na mlinzi wa jumba lile.
Masimba akas0gea kama mpita njia
mwenye kutaka kuuliza kitu. Mlinzi
naye hakushtuka katika hilo, akasogea
kumsikiliza zaidi mtu huyu ambaye
alimjia kama mhitaji. Hatua ya kwanza
na yapili zilikwenda bila kutokea
chochote, hatua mbili kabla hajamfikia
mtu yule kikatokea kitu cha
kustaajabisha kwake na hata kwa
masimba, taa zote za jumba lile
zilikuwa zimezimwa katika namna ya
kushangaza. Hilo likamvuta masimba,
likamvuta likimtoa pale alipokuwa na
kumsogeza upande tofauti. Ni muda
huo huo alipoisikia sauti ya mlinzi yule
ikilalama katika aina ya maumivu.
Lilikuwa lalamiko ambalo halikudumu
hata kwa theruthi ya sekunde. Ukimya
ukarudi tena katika utawala wake.
Ukimya wa kutisha na kuogopesha.
Masimba bado akaivuta dakika
nyingine ya pili ili kuangalia kile
kinachotokea. Kelele ya mlinzi
ilimaanisha kuwa alipigwa shaba. Hilo
halikubishwa katika kichwa na akili ya
masimba. Hakujua huyu alikuwa nani
katika wakati huu, wakati ambao
alijipanga mwenyewe na hakuwa
amemwambia mtu yoyote kuja kwake
hapa. Haukuwa muda sahihi wa
kujiuliza maswali, ulikuwa muda wa
kukijua kile kilichotokea. Hilo
likamfanya masimba airuhusu miguu
yake kutembea, mkononi aliikamatia
bastola yake, sasa akaamua kwenda
ueleke0 tofauti, aliamua kurudi kule
alipotoka. Akaufikia ukuta wa jumba
lile, akautizama kwa makini safari hii
akitaka kufanya kitu. Hakujua kile
kilichotokea ndani na hata kile
kilichompata mlinzi. Muda huu alikuwa
juu ya mti mmoja kati ya mingi
iliozungushiwa kwenye jumba lile.
Aliupanda na alipofika usawa wa uzio
ule akajitoa pale juu ya mti na kutua
chini bila kutoa kishindo. Baada ya
kutua, akachepuka na kubana
pembeni. Bado ukimya wa kuogofya
ulichukua sehemu kubwa. Akajitoa
pale alipokuwa amebana na kusogea
kuelekea mlango wa nyuma. Kila hatua
yake moja ilikuwa ikienda sambamba
na macho yake. Akaufikia mlango na
kutulia hapo. Bado hakusikia chochote
kutoka ndani. Hamu ya kujua
kilichotokea ikaongezeka, hamu
haikumithilika. Hilo likamfanya
akinyonge kitasa ku0na kama mlango
ungefunguka. Ni kweli mlango ulikuwa
wazi, ni kweli mlango haukuleta kizuizi
"ameingilia hapa" lilikuwa neno
lililogonga kichwani kwake.
Akausukuma mlango taratibu na
kuruhusu macho yake kutangulia
kutizama ndani. Lakini hakufanikiwa
kukiona kitu kutokana na giza.
Akaufungua zaidi kisha kuingia kabisa.
Hatua tatu mbele alihisi kukanyaga kitu
mfano wa maji. Hilo likamfanya kutaka
kuinama kuangalia. Pua zake zikainasa
harufu ya damu. Damu mbichi iliokuwa
ikichuruzika kutoka mahala fulani
katika mwili wa binadamu. Damu
ikamsisimka. Akahisi kuwahiwa na mtu
katika hili. Lakini alikuwa nani?
Lilikuwa swali ambalo halikupata
majibu. Na hakutaka kupata jibu kwa
wakati ule. Akahama pale na
kuendelea kusogea mbele, hakupiga
hata hatua tatu akajikuta akijikwaa
kwenye kitu mfano wa mwili wa
binadamu. Akaongeza umakini na
kuugusa mwili ule. Akajikuta
akionyesha mshangao baada ya
kugundua mwili uliolala chini ulikuwa
mwili wa mtoto mdogo ukiwa hauna
uhai. Alitegemea kuona mengi lakini
hilo hakulitegemea. Mtoto kuuawa
kwa risasi!!!ni nani huyu? Lilikuwa
swali lisilo na majibu. Ina maana mzigo
uliyopotea ndio chanzo cha hays
yansyotokea? Bado alikuumiza kichwa
chake kwa maswali.
Wakati anapewa kazi ya kufuatilia
mzigo uliopotea hakujua kama kazi
ingemfikisha huku. Hakujua kama
yangetokea haya. Hamu yake ya
kuwajua wauaji wa Asteria ndiyo
sababu ya leo hii Masimba kutafutwa.
Akaucha pale chini mwili wa yule
mtoto asie na hatia. Akasogea zaidi na
zaidi, kutokea tu sebuleni akashtuka
baada ya taa zote kuwashwa.
Hazikuwashwa patupu bali zikafuatiwa
na mngurumo wa gari kutoka nje.
"Wamekimbia" alinong'ona masimba
huku sasa akishuhudia kile
kilichotendeka. Watu watano
walikuwa chini wamelaliana juu ya
dimbwi la damu huku risasi
zikionekana kuiharibu miili yao. Hilo
likamshangaza Masimba, sio
kushangazwa na nauaji yale bali watu
waliouawa. Kwa mara ya kwanza
akauhusudu uwezo wa mtu huyu,
uwezo wa muuaji huyu. Watatu kati ya
watu watano waliouwa pale walikuwa
ni watu wake, watu ambao alitaka
kuwapa tiketi zao. Lakini alishangaa
kuwakuta wote wakiwa
wamesafirishwa tayari tena na mtu
ambaye hakuwa akimjua. Hili likampa
shaka na hata wasiwasi kwamba
inawezekana kuna watu au mtu
anatembea naye katika hili.
********
Vifo vya wasichana watatu ambao ndio
pekee waliokuwa wakiwajua wauaji
kiliitikisa sana idara ya ujasusi. Sasa
wapelelezi walikuwa wakikesha katika
vyumba vya watu hudika wakizani
kwamba wanaweza kupata chochote
cha kuwasaidia. Licha ya kujaribu
kupekuwa katika makazi yote ya
marehemu hawakufanikiwa kupata
chochote cha kuwasaidia. Mtu pekee
aliyekuwa amebaki katika hilo alikuwa
ni yule dereva tax. Huyu alikuwa
amefichwa katika jengo moja
linalomilikiwa na wana usalama. Leo
waliamua kurudi tena baada ya
mambo kuendelea kuwa magumu.
Licha ya kuhojiana naye sana lakini
waliamini kwamba wanaweza kupata
chochote kwa mara nyingine.
Hawakutaka kupuuza hilo. Muda mfupi
baadae walikuwa ndani ya chumba
wakihojiana na mtu huyu. Wana
usalama wakaendelea hili na lile.
Wakimtaka akumbuke zaidi kile
ambacho alikiona kabla ya kukodiwa
na watu hao ambao bado walikuwa
wakisakwa na wana usalama mpaka
muda ule
. Dereva wa tax akakaa kimya kwa
muda akiwaza hili na kuwazua. Kwa
mara ya kwanza alianza kukijutia
kitendo cha kutoa siri ambayo akuwa
nayo. Usumbufu wa maswali na hata
vitisho ilikuwa kawaida kwa
wanausalama wengi duniani hasa pale
wanapohitaji kitu. Vitisho ilikuwa
sehemu moja na mbinu ya mwisho
kuitumia pale wanapokutana na
ugumu katika mbinu zao nyingine.
Dereva bado alikuwa kimya akijaribu
kukumbuka kilichotokea kabla ya
kuwapata watu wale watatu usiku ule.
Haikupita dakika hata tatu tayari
alikuwa ameshakumbuka kitu. Gari ya
kifahari ikiingia, kisha walinzi watano
wakashuka kabla ya mtu fulani
kushuka. Mtu yule hakuwa ameshuka
peke yake bali alikuwa sambamba na
watu wengine watatu. Wawili
walikuwa watu weusi na mmoja
alikuwa raia mwenye asili ya Asia. Yeah
walikuwa watu hao. Baada ya
kukumbuka hilo akainua macho na
kuwatizama tena wana usalama, kisha
kwa sauti ya chini akasema. "Yeah
nimekumbuka. Wakati mheshimiwa
akishuka, alishuka sambsmba na watu
wengine watatu. Wawili walikuwa
weusi na mmoja alikuwa na Asili ya
Kiasia. Hao walikuwa tofauti na walinzi
ambao walishuka kabla." Wana
usalama wakaangaliana kisha mmoja
akanena..
"SURESH SIGH na JIMMY LAMBERT
LAZIMA WATAFUTWE KUANZIA SASA.
HAWA NI WATU AMBAO WATA...... kabla
hajamaliza kauli yake, simu yake ya
mkononi ikaiiita.. Kutupa macho juu ya
kioo cha simu akakutana na Jina Chief.
Hakupokea kwa muda ule.
Inaweza kuwa picha ya Mtu 1

 
Back
Top Bottom