Hadithi: Sitosahau alichonifanyia daktari wa saratani ya matiti

Hii kitu mbn kama umeruka chapter moja
Hadithi fupi!
SITOSAHAU ALICHONIFANYA DAKTARI WA SARATANI YA MATITI
SEHEMU YA KUMI NA TISA-A

Tuliishia pale Binti alipoambiwa na mama yake kwamba Doctor Hemed alishawahi kumtongoza mama huyo.

Endelea hapa
Nilishtuka sana sikuamini sana maneno yale, tangu saa ile nikawa sina imani sana na Hemed, ilikuwa ni ngumu sana kumuambia kwamba mama ameniambia vile, nilijikuta niko njia panda sijui nifanye maamuzi gani ili niweze kuachana naye.

Baadaye kidogo alinitumia ujumbe β€œNakufuata” nikakausha kimya akatuma tena β€œJiandae”

Sikujua tunaenda wapi lakini aliponifuata home niliondoka naye mpaka tukafika alipokuwa anaishi, tukaingia ndani

β€œtumekuja kufanya nini??” nilimuuliza

β€œWe twende” alisema huku akinivuta mkono tukaingia hadi sebuleni akafoka β€œJakiiiiiiiii” alikuwa anamuita Jacque ambaye aliitika akiwa tayari ametua sebuleni

β€œAbee kaka” alipofika alishtuka kuniona pale.

β€œNjoo” alisema Hemed huku akiketi kwenye sofa, mimi bado nimesimama sielewi

β€œNdio kaka….” Alisema binti, ni mrembo kwelkweli

β€œNilishakuambia naoa au sijakuambia?” alimuuliza

β€œUlishaniambia kaka”

β€œMimi nimetembea na wewe??” aliniuliza

β€œHapana hujawahi”

β€œSasa kwanini unatangaza kwamba niko kwenye mahusiano mimi na wewe??”

β€œMimi???” Jacque aliuliza kwa mshangao

β€œNdio wewe…..nilipokuja na huyu dada hapa nilikuambia ni nani??” alisema Hemed huku akininyooshea kidole

β€œUliniambia ni mchumba wako” alisema

β€œNilikuambia nataka kumfanyaje??”

β€œKumuoa”

β€œSasa kama nilikuambia ni mchumba wangu mbona unataka kuniharibia?”

β€œKaka mimi sijasem….”

β€œPumbavu wewe….nimeshajua ndo tabia zako kuniharibia, hata kwa mama yake Nasra ni wewe ulikuwa unafanya hivyo

Jacque alikaa kimya kabisa hakujibu chochote, nikabaki namuona mnafiki mkubwa anataka kuninyima bahati yangu, Hemed akasema β€œKuanzia leo sikutaki ndani kwangu natafuta mfanyakazi mwingine” alisema

β€œBoss…..Kaka…..Naomba unisamehe” binti alianza kulengwa na machozi mpaka akapiga magoti chini β€œNaomba kaka unisamehe” alisema β€œSitorudia tena” alisema huku akilia sana

β€œToka!!! Mimi ninahitaji mke, halafu wewe kazi kuniharibia tu??” aliuliza

β€œHapana boss…naomba unisamehe, sifanyi hivyo makusudi ila nafanya hivyo kwa sababu nakupenda” alifunguka mtoto Jacque nikashangaa….nilimuona Hemed mwenyewe ameduwaa anamtazama na kumuuliza

β€œUnanipenda mimi??” aliuliza Hemed huku akiwa anajishika kifuani mwake kwa ajili ya kuonyesha nafsi Jacque akiwa analia alitikisa kichwa kumaanisha ni kweli alikuwa anampenda….19 B NDIO HIYO NLIYOPOST
 
Daktari ana balaa huyu!!
 
Huu uzi ni moto wa kuota ukiwa na le mubebez pembeni vinginevyo nyeto hii hapa [emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…