KASHAMBURITA
JF-Expert Member
- Mar 27, 2021
- 204
- 655
- Thread starter
- #141
MALIPO KITANDANI 01 HADI 02
MWANZO WA STORY
KISOLO CHA 01
Ilikuwa ni miaka ni shamra shamra zilizofanyika katika kanisa la Anglican Tegeta ambapo kulikuwa na sherehe madhubuti ya harusi iliyofanyika kati ya Erick Jackson Makoti Temu pamoja na binti Janeth Williamson Massawe ambao walifunga ndoa yao takatifu katika kanisa hilo takatifu zaidi
Viapo vya kutokuachana hadi kifo kiwatenganishe zilitaradadi, machozi yakamtoka binti wakati anavishwa pete na mwenzake huyo Erick kwani walikuwa wametoka mbali sana mpaka kuamua kuoana.
Sherehe kubwa ilienda kufanyika katika maeneo ya Mlimani City, Mwenge Jijini hapo hapo Dar es Salaam na hata ilipomalizika walikuwa na furaha tele.
Ndoa hii ilikuwa ni furaha kwa watu wengi, kwani Erick alikuwa na pesa nyingi sana huku akijihusisha na biashara ya kuuza mchele kutoka Mbeya na kusambaza jijini Dar es Salaam na mikoa mingine ya pwani. Huku Aneth akiwa na biashara ya miamala ya simu na benki, zote alifunguliwa na Erick mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya Shahada ya Kwanza katika chuo kikuu cha Dar es Salaam miaka mitatu iliyokuwa imepita.
Familia zao zilifurahi watoto hao kuungana na kuwa mwili mmoja, waliwapa zawadi nyingi sana ziwasaidie katika maisha yao.
Hata hivyo licha ya furaha kuwepo upande wa Aneth na familia yake, na upande wa Erick na familia yake, kuna upande wa tatu ,wa kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Amidu, alikuwa katika mawazo na stress zisizopingika.
Amidu alikuwa ni mmoja kati ya vijana ambao walikuwa wamehudhuria sherehe zile tena kwa mwaliko rasmi, kwani alikuwa karibu sana na watu hao wawili ambao walimsapoti katika vitu vingi sana licha ya kutokuwa na elimu kubwa lakini walimpenda maana alijituma na alifanya kazi za Erick kwa zaidi ya miaka saba.
Amidu aliondoka pale kwenye sherehe ya harusi, Mlimani City akavua koti lake lake na kubaki na shati jeupe lililolowa jasho, akalegeza tai shingoni kisha akatoka akiwa na mawazo tele tele kwani alionekana kuna jambo lililokuwa likimsibu kijana yule
Marafiki ambao pia walikuwa karibu na Amidu walimuona akitoka kwenye sherehe wakati sherehe bado haijaisha, tena alikuwa speed, macho yalikuwa mekundu sana.
“Oya wapi mzee?” Aliuliza kijana mmoja aliyekuwa akiitwa Elisha Michael lakini Erick alipita bila kujibu lolote na kutoka kupitia mlango mdogo mpaka nje
Huku ndani aliacha mawazo upande wa marafiki zake wale walibaki wakiulizana vipi, au amepata tatizo gani mbona anaondoka hata sherehe haijaisha, hakuna chakula chochote kilicholiwa, walijua labda kapatwa na tatizo
Elisha alihisi vibaya, akaondoka eneo lile, akaenda chooni na kutoa simu mfukoni akampigia ili angalau amuulize kama kuna tatizo lolote lakini Amidu alipoiona simu aliikatilia mbali halafu akazima simu hakutaka mawasiliano kabisa.
Kwa miguu Amidu alitembea mpaka akafika mawasiliano, alipofika aliingia katika mtaa moja pembeni kidogo mwa stendi, kuna kamto fulani, aliketi kando ya ule mto akaanza kulia huku akilaumu
“Nimekukosea nini??? Mimi nimekosea nini mpaka ninyanyasike hivi?? Alisema huku machozi yakimtiririka kwani alionekana kuna jambo zito sana lililokuwa limemkumba kijana yule
Licha ya watu wa ulinzi kumfuata pale kando ya mto na kumuambia aondoke lakini Amidu alikesha paleplae Mtoni, mbu wakimuuma baridi ikimtafuna, bila kuogopa vibaka waliokuja na kumpora simu yake alikuwa analia sana kijana Amidu.
Upande wa kwenye sherehe Bwana harusi, Erick alikuwa na wanafamilia, na marafiki ndipo akamuita Elisha na kumuuliza “Amidu yuko wapi??”
Elisha alimtazama kisha akasema “Aliondoka kwa hasira hapa hatujui kapatwa na nini”
Aneth kusikia maneno yale alishtuka na kumtazama Elisha kisha akamuuliza “Kaondoka akiwa na hasira?”
“Ndio, alikuwa na hasira sana.....alionekana mwenye stress, nilimuongelesha wala hakunijibu chochote, alionekana kukwazwa na kitu fulani kizito sana”
“Duuh itakuwa tatizo nini?” Erick aliuliza
“Hatujui sasa” alijibu Elisha
*
Saa kumi na moja alfajiri, Amidu aliinuka pale mtoni alipokuwa akatembea mpaka barabara kuu, akalipia pikipiki na kupelekwa nyumbani kwake alipokuwa amepanga maeneo ya Shekilango, ndipo akavua nguo na kuingia ndani ya bafu akajifungia na kufungulia maji ya bomba la mvua yakammiminikia mwilini halafu akaketi chini sakafuni huku akizidi kutokwa na machozi ambayo yalibebwa na maji na kutiririshwa moja kwa moja mpaka kwenye chemba ya serikali
JE KIPI KILICHOMSIBU KIJANA AMIDU MPAKA ANAPATA TABU SANA? USIKOSE KISOLO CHA PILI
KISOLO CHA PILI
Siku saba zilipita bila Amidu kuonekana mtaani, simu ilikuwa haipatikani kabisa, na hata walipoenda nyumbani kwao hawakumkuta kabisa kijana yule, walipata mawazo teletele.
Kizaazaa kilianza pale Zanzibar, kwenye fungate lililokuwa likifanyika na wanandoa wawili wapya, Erick na mkewe Aneth Massawe. Hii ni baada ya Aneth kujaribu kuwasiliana na Elisha na kumuuliza kama wamefanikiwa kumuona Amidu ambaye alikuwa mtu mwenye ukaribu mkubwa sana na watu hao hasa kibiashara, alikuwa na nyota ya biashara hasa.
“Shem huyu Amidu hajapatikana, hayupo kule nyumbani kwake, vile vile hayupo kwao mkoani morogoro, kamwe hawakujua kaelekea wapi” ilikuwa ni sauti ya Elisha ikisikika katika tundu la sikio la kushoto la Aneth masawe ambaye alikuwa nje ya hoteli ya kifahari mjini Zanzibar akiwa ameegemea baraza ya hoteli hiyo waliyokuwa wamekodisha vyumba kadhaa kwa ajili ya fungate lao.
Erick akiwa amejifunga taulo kiunoni alitoka, barazani, akamkuta mkewe amesimama anaangalia mbali, huku akiwa na mawazo tele, akamkumbatia kwa nyuma kitendo kilichomshtua binti hadi akadondosha simu
“Ah wewe” aliongea kwa mshtuko mwanamke yule kwa mshtuko “Umenishtua”
“Oh I am sorry baby....kwani vipi mbona umeniacha ndani peke yangu?” aliuliza Erick huku akiokota simu ilikuwa imepata kreki kwenye kioo kilindi (protector)
“Imepasuka???” Binti badala ajibu swali, naye alipachika swali juu juu
“Usijali hii ni protector tu...anyway tutaweka nyingine kesho usijali”
“Sawa”
Erick alimpatia simu mkewe kisha akamshika “embu twende ndani bwana”
Waliingia ndani lakini Aneth hakuwa na furaha hata chembe. Waliketi kwenye sofa kisha binti akasema “Hivi unajua Amidu hajapatikana?”
“Usijali atapatikana tu, ndo uwe na mawazo hivi mke wangu?” aliuliza Erick
Aneth alitabasamu kwa kujilazimisha kisha akasema “Sio hivyo, nilijua atakuwa kule nyumbani atusaidie biashara zetu kipindi tuko huku honeymoon”
“Ah tunarudi siku si nyingi, usijali kuhusu hili atakuwa sawa tu”
“Kweli unasema hivi? Ni mambo mangapi ameshawahi kutusaidia katika maisha? Ni kwanini aondoke tena siku ya harusi yetu? Au ulimkwaza Erick? Nambie nina wasiwasi, yule nimeshamfanya kama mdogo wangu eti”
“Usijali kuhusu hilo tutafuatilia, acha niongee na Elisha halafu atalimaliza hili, sawa??” aliuliza kijana Erick
“Sawa mume wangu”
Erick kwa haraka hakuelewa, alijua ni undugu uliojengeka kati ya familia yao pamoja na kijana Amidu pamoja na marafiki wengine kama kina Elisha na kadhalika.
Ilikuwa ni usiku uliojaa kiza kinene, walikuwa wanafanya mambo yao kitandani, binti alikuwa hajaridhika lakini hakutaka kuendelea, ghafla tu moto ulimkata na kujikuta anamuomba mumewe aahirishe tendo lile walilokuwa wakilifanya
“Why? Kwanini tuache kufanya?”
“Erick, nimechoka, unajua kabisa tumefanya mara nyingi sana tangu tuje hapa, leo hata hamu sina, naomba nipumzike tu” alisema binti
“Okay sawa” Erick hakujali sana, maana alikuwa amefanya mara nyingi na binti yule na vile vile alikuwa sio mgeni kwake.
Saa nane na nusu, simu ya Erick iliita na alipoitazama alikuwa ni Elisha anampigia, ndipo akamtazama mkewe ambaye alikuwa amelala kando kisha akapokea na kuongea kwa sauti ndogo kabisa ambayo anajua haitamsumbua mkewe aliyekuwa fofofo
“Hallo”
Elisha naye akasema “Hallo kaka, najua nakusumbua katika muda wako huu wa kupumzika” aliongea Elisha kwa masham sham halafu akakohoa na kuonyesha ana huzuni kubwa
“hamna tatizo, uko powa wewe?”
“Siko powa kaka”
“Tatizo nini Elisha?”
“Kaka, mwili wa Amidu umekutwa baharini alishakufa”
“Alishakufa???? Kivipi???” Erick aliuliza kwa mshangao mkubwa sana huku akiketi kitandani bila kutarajia.
“Ndio kaka”
“We embu acha masihara bwana” alisema huku akiinuka na kutembea kuelekea mlangoni akafungua mlango taratibu mpaka nje akasimama barazani”
Elisha alilia sana, machozi yalimtiririka kule alipokuwa ndipo akasema “Ndio kaka, ninaumia sana”
“Aliuawa au imekuwaje?”
“Daaah” Elisha alizidi kuongea kwa uchungu, “Inavyosemekana alijirusha mwenye baharini, lakini polisi wanaendelea na uchunguzi” Elisha aliongea akizidi kulia, machozi yalimshinda akashindwa kuongea kabisa
Ulikuwa ni uchungu wa hali ya juu, hakukuwa na namna kabisa, hata hivyo alijikuta anakata simu na kumuacha njiapanda Erick
Erick alibaki na mawazo tele, ndoa imeanza na visirani, ile furaha iliyokuwa imemjaa baada ya kuoa, ilitoweka na kugeuka kuwa huzuni kubwa. Erick aliwasha data, akaingia katika mtandao wa Instagram, ilikuwa hata haijapita dakika nyingi, alikuwa amepost Millard Ayo akiandika kichwa cha habari
“MWILI WAKUTWA BAHARINI, YASEMEKANA ALIJIUA KWA MSONGO WA MAWAZO, huku ikifuatiwa na maelezo
Kijana mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Amidu Hassani, miaka 24 amepatikana mwili wake baharini maeneo ya Mbezi beach akiwa amekufa, inasemekana alijirusha baharini kwa lengo la kujiua kwa sababu alikuwa na msongo wa mawazo, polisi kanda maalum ya Dar es Salaam wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo”
Hii habari ilimdhirishia Erick kwamba kweli Amidu amefariki, alijiuliza maswali kedekede, kwamba ‘Kwanni ajiue? Kwani alikuwa na stress gani mpaka ashindwe kuniambia? Kwani aliona siwezi kumsaidia? Au alipima akakutwa na ngoma nini?”
Yote haya yalikuwa ni maswali kichwani mwa Erick, ndipo akapita mtandao wa WhatsApp na kuchungulia status, aliona marafiki zake wengi wakiwa wamechapisha hadhi zao huku wakiandika R.I.P MWANANGU HASSAN, ILA UMEONDOKA MAPEMA SANA na maneno mengine kama hayo.
Erick taratibu aliingia katika kitanda chake, akajilaza na kumkumbatia mkewe ambaye alikuwa hajapata taarifa maana alikuwa usingizini....JE ANETH AKIAMKA NA KUKUTANA NA TAARIFA ZILE ATAFANYEJE? NA KWANINI Amidu AJIUE? USIKOSE KISOLO CHA 03
like halafu comment
Usisahau kunifollow kashamburita ili uburudike