Hadithi: Ulimwengu wa Watu Wabaya

Hadithi: Ulimwengu wa Watu Wabaya

HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA 60
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA....................
"Mmmmmhhhhhh aaghr" sauti nzito ya mtu akiguna ilimshtua sana Victor ikamlazimu kugeuka haraka sana ndipo aliposhangaa sana mtu aliyekuwa akimuona nyuma yake na huenda ndiye aliyefanya Marry kuongea kwa hasira sana hapo kitandani akiwa anatia huruma na kuzidisha machozi sana.
ENDELEA.....................
"Baba" Victor alipigwa na mshangao mkubwa baada ya kugundua aliyekuwa hapo ni Kasisi Chacha hata hivyo hakupewa jibu lolote lile mzee huyu alikuwa amemkazia macho Marry au Ester pale kitandani alipokuwa amelala.
"Huyu shetani ni baba yako?" swali la ukali kutoka kwa Ester lilimfanya Victor ageuke tena kumwangalia na kumpa mgongo Kasisi Chacha
"umeshapata ukichaa?mpaka ufike sehemu unamkosea mzee wangu mpaka umuite shetani hivi una akili kweli wewe mwanamke" Victor aliuliza akiwa amebadilika macho yake kwa muda huo hakujali kama mwanamke huyo alikuwa mjamzito kitendo cha kutukaniwa mtu aliye mlea ilikuwa ni dharau kubwa sana kwake, alijiandaa ili akampige hata kofi mwanamke huyo lakini Kasisi Chacha alimdaka mkono ikabidi atulie.
"muulize mwenyewe kanifanyia nini kwenye maisha yangu" alijibu kwa ukali Ester akiwa anatoa machozi mengi sana ilimbidi Victor ageuke na kumuuliza Kasisi Chacha
"Baba kuna kitu gani kimefanyika hapa katikati mpaka akuchukie sana kiasi hiki?" Victor alitegemea jibu zuri kutoka kwa huyu mzee lakini ilikuwa tofauti kabisa na alichokuwa anakifikiria.
"nimemuweka mbali na furaha ya maisha yake ndiyo maana alivyojua juzi amenichukia sana" sauti nzito ya Kasisi Chacha iliunguruma.
"kumuweka mbali na furaha yake kivipi" swali liliulizwa na Victor.
"ndio sababu siku ile nilikwambia kwamba umekurupuka sana kuishi na huyu mwanamke, hivi ushawahi hata siku moja kukaa ukajiuliza huyu mwanamke historia yake ipoje? au ulikimbilia tu kwa kuchanganyikiwa na uzuri wake?" Maneno mazito sana yalitamkwa yaliyo mfanya kidogo Victor ajione ni mjinga sana hakuwahi hata kufuatilia maisha ya mwanamke huyo ambayo aliyaishi kabla yeye hajakutana naye.
"yule mwanaume aliyekuja kwako ukapambana naye ni mumewe halali wa ndoa kabisa ndio maana amepata mshtuko mkubwa kiasi hicho" Victor mwili ulikosa nguvu kabisa ikamlazimu kukaa chini hata hizo nguvu za kusimama hakuwa nazo kwa muda huo, hakutamani anacho kisikia uwe ni uhalisia wa mambo, alitamani mtu mmoja aje na kumwambia alikuwa anataniwa tu, alikuwa amempenda mno mwanamke huyu na aliridhia kuishi naye kwa muda ambao MUNGU atambariki kuendelea kuliona jua hakutaka kuamini eti Ester ni mke halali kabisa wa mtu tena wamefunga ndoa, baada ya kutamka maneno hayo Kasisi Chacha alitoka humo ndani haraka sana akimuacha Ester anapiga kelele pale kitandani
"unewapeleka wapi wazazi wangu shetani mkubwa wewe, niletee familia yangu kwanini unanifanyia hivi" sauti za Ester Victor hata alikuwa hazisikii akiwa amekaa chin ya kitanda hicho alichokuwa amelazwa mwanamke aliye mbebea mtoto tumboni mwake, hakuona sababu ya kuendelea kubaki ndani humo akihisi amesalitiwa pakubwa sana hakutaka hata kuijua sababu mwanaume aling'ata meno yake kwa hasira sana akanyanyuka kwa nguvu na kuhitaji kuondoka humo ndani kwa hasira ila kabla hajafanya hivyo alidakwa mkono wake alipogeuka nyuma alimuona Ester akiwa anamtazama machozi yamemjaa usoni.
"Hivi ni kweli yule ni baba yako?" Ester aliuliza akiwa anajikaza tu lakini alikuwa na uchungu mkubwa sana kwenye moyo wake
“kama usingekuwa mjamzito kwa huu ujinga ulio ufanya ningekuua mimi mwenyewe kwa mkono wangu”Victor alitamka kwa hasira bila kujali chochote aliutoa mkono wake kwa nguvu sana na kuanza kutoka humo ndani.

“kwhiyo wewe na baba yako ndiyo mliokuwa nyuma ya haya yote” swali la Ester lilimfanya Victor kidogo asimame.

“unapaswa ulitamke kwa heshima sana jina la huyo mzee, bila yeye ningekuwa mtoto wa mtaani mpaka leo, amenichukua nikiwa bado mdogo sana sina sehemu yoyote ya kulala, sina chakula, hakuna mtu hata mmoja aliyeweza kunijali mimi ila yeye pekeyake aliliona hilo, akanipa elimu bora sana mpaka leo nimekuwa komando mkubwa sana wa kutegemewa ndani ya idara ya usalama wa taifa pamoja na nchi kwa ujumla leo unataka kuongea nini mwanamke mshenzi wewe. Umekuja kwenye maisha yangu kwa kujifanya unanipenda sana kumbe una ajenda zako mwenyewe, kwahiyo yule hawala wako ndiye aliyekutuma uje unipeleleze maisha yangu sio hahahahahah……. Sikujua kama wewe ni miongoni mwa wanawake washenzi sana kwenye hii dunia, sikuwahi kumpenda mtu yeyote yule umenifanya nikupende nilikuwa tayari hata kukupa dunia yangu yote na kila kitu kwenye maisha yangu kumbe naishi na nyoka ndani ambaye ni mke wa mtu tena komando aliye liasi taifa, inamaanisha nawewe uko nyuma ya hili, sitaki kujua kama wewe ni gaidi kama huyo bwana ako na sitaki kujua kama mlikuwa na mpango gani kwenye maisha yangu, nitakuacha hai ila hakikisha hatuji kuonana tena kwenye maisha yetu sitakusamehe tena kama leo liweke akilini hilo” Victor aliongea kwa uchungu mkubwa kupita kiasi akiwa kwenye majonzi mazito sana hata kuongea maneno makali hayo mbele ya huyo mwanamke aliye mpenda alikuwa akijikaza tui la ilikuwa inamuuma sana, alibamiza mlango kwa nguvu kubwa na kutoka humo ndani akisahau kwamba daktari alimshauri kama mwanamke huyo anahitaji uangalizi mkubwa mno.

Kwa Ester ni kama alitoneshwa kidonda kingine kipya kwenye moyo wake licha ya kugundua kama Victor haelewi chochote juu ya hilo na sio mtoto wa Kasisi Chacha lakini ukali wa maneno ambayo Victor alimtamkia ulimfanya ajisikie kama kuna mtu kamchoma na kisu kingine kipya kwenye moyo wake, alihisi amepoteza kila kitu kwenye maisha yake mpaka siku anampata Victor aliamini huyo ndiye familia yake atakayo ishi nayo kwa furaha baada ya kuteseka na upweke wa muda mrefu sana. akiwa kwenye simanzi nzito kwenye hicho kitanda kumbu kumbu zake zilienda mbali sana tangu yupo India alivyoweza kuishi na Roland ambaye alikuwa mwema sana kwake kiasi kwamba wakaingia mpaka kwenye bahari ya huba lakini safari hiyo ilikuja kuisha baada ya kurudi nchini Tanzania baada ya Roland kupotea ghafla bila kueleweka ameenda wapi lakini kiuhalisia kazi ya Roland ilikuwa ni kuhakikisha usalama wa binti huyu tangu yupo India mpaka anarudi Tanzania baada ya kulifanya hilo kwa usahihi alipewa maelekezo na mkuu wake Kasisi Chacha kwamba haruhusiwi tena kumuona mwanamke huyo kwenye maisha yake. Maisha yake yote Ester aliishi akijua mwanaume wake huyo ameshakufa kwahiyo alishtuka mno baada ya kumuona mwanaume huyo mbele ya macho yake, ilimnyima raha pakubwa sana ni jambo ambalo hakulitegemea kabisa kumtokea muda kama huo.


****************************************************
Calvin baada ya kutoka Temeke hakurudi moja kwa moja Kigamboni alihisi huenda kuna watu wanaweza kumfuatilia kirahisi sana na kwa huo muda alihitaji kupumzika, mwanaume aliingia ndani ya Kawe akatafuta hoteli moja majira hayo ya usiku wa manane akafanikiwa kuipata, alilala usingizi mzito sana mpaka alipokuja kushtuka asubuhi na mapema sana, akiwa anatoka kuoga alisikia mlango unagongwa akahisi huenda kuna watu wamemtembelea mapema sana akataka kuvaa haraka sana lakini alitulia baada ya kusikia sauti moja nzuri sana ya kike basi alifungua mlango taratibu akiwa amevaa taulo tu, kama alivyokuwa ametegemea alikuwa ni mhudumu akiwa amemletea supu moja nzito sana ikiwa ni utaratibu wao wa kila siku kwa kila mteja ambaye analala ndani ya hoteli yao. Alikaa na kuanza kupata supu yake taratibu bila hata wasi wasi wowote ule, supu iligeuka kuwa chungu baada ya kuiwasha televisheni iliyokuwa humo ndani, hakuamini kitu alichokuwa anakiona mbele yake ilikuwa ni taarifa ya habari ya asubuhi kabisa na mbele ya hiyo skrini alisimama mheshimiwa waziri mkuu pembeni zikiwa zimeambatanishwa picha zake yeye mwenyewe Calvin Jackson japo kwenye hizo picha hakuwa na ndevu ikionekana ni picha za muda kidogo.

“shiiiiiiiiiiit…….” Alitamka kwa hasira akibamiza chini bakuli la supu kwa hasira akitulia ili kumsikiliza mzee huyo kwa uchache japokuwa hakujua kama ndio anaanza au anamaliza.

“Calvin Jackson Aron Mavunde ndilo jina lake huyu mtoto, kwa sasa amefikisha miaka 25 na ana mvuto mkubwa sana ukimtazama machoni, huyu ni mtoto wa tajiri mmoja mkubwa sana ambaye kwa bahati mbaya miaka mitatu iliyopita aliweza kututoka baada ya kuvamiwa na kuuawa na watu wasio julikana, huyu mtoto alipotea ghafla sana baada ya mauaji ya wazazi wake zaidi ya miaka miwili sasa huu ni watatu. Tangu wazazi wake wamekufa tumefanya uchunguzi wa kina sana tumegundua kwamba yeye ndiye mhusika mkuu wa mauaji ya wazazi wake na alifanya hivyo ili aweze kumiliki mali za wazazi wake, kwa sababu alikuwa ni mjeuri sana kwenye familia yake ndipo baba yake alipogoma kumrithisha mali zake akaamua kuwaua ili abaki na mali hivyo akaamua kuwaua ili tu azichukue. Sio hilo tu inaonekana alienda kujipanga na kuungana na makundi makubwa ya kigaidi kwani baada ya kurudi alianza kuwatafuta maaskari na wanajeshi wetu ambao wanaijua siri yake hiyo na kuwaua kikatili sana, mpaka sasa maaskari na wanajeshi alio waua ni mia moja ikiwa ni pamoja na kuwabaka wanawake saba na kuwaua wote, tulifanikiwa kumkamata kwa mara ya kwanza na raisi alitangaza hadharani lakini magaidi wenzake walivamia msafara na kumtorosha.

Mimi kama waziri mkuu wa hii nchi iliyo barikiwa sana amani ninalaani na kukemea haya yaliyo tokea hivyo huyu mtu nahitaji vyombo vya dola kuanzia jeshi la polisi na jeshi la nchi wamtafute popote pale alipo na aweze kuuawa kikatili sana mbele ya hadhara ili kuweza kulinda usalama wan chi yetu kwani akiachwa hai itakuwa ni hatari kwa raia na mali zao, natoa rai kwa raia wema kwa yeyote atakaye saidia kutoa taarifa juu ya upatikanaji wa mtu huyu atazawadiwa pesa za kitanzania taslimu milioni miamoja, naomba tusaidiane sana kwenye kulilinda taifa lililotengenezwa kwa jasho na damu na waasisi wetu kwa kumteketeza huyu gaidi” hotuba fupi ya waziri mkuu ilimfanya Calvin apoteze nguvu ikamlazimu akae chini akiwa na machungu makubwa sana, inauma sana mtu anayekufanya unaishi kwa shida ndiye huyo anaye kwenda kuwatangazia watu kwa jeuri kabisa kwamba wewe ndiye mtu mwenye makosa na haufai hata kidogo kwenye jamii kiufupi waziri mkuu aliona kwake hiyo ni njia rahisi sana ya kumdhibiti huyu kijana ambaye alianza kuwa hatari kwake, alitamani aweze kuingia kwenye hiyo televisheni akutane na mzee huyo aliapa angemuua kikatili kuliko binadamu yeyote yule ambaye alishawahi kumuua kwenye maisha yake. Aliuma meno kwa hasira akipiga na kupasua meza kubwa ya kioo iliyokuwa mbele yake hapo, leo alikuwa amepewa kesi nzito sana ambayo hakuwahi hata kuifikiria kwenye maisha yake, aliwaza wananchi ambao ni zaidi ya milioni 40 watamtazamaje yeye, ingekuwa ni kuua tu wanajeshi sawa vipi kuhusu kubaka wanawake na kuwaua! Ilimuumiza kichwa sana bwana mdogo, kila mtu alimchukia kwa dakika moja tu pekee alichanganyikiwa Calvin roho ilimuuma sana, wakati akiwa hapo simu yake ya mkononi ilianza kuita ghafla na kwa fujo sana.

Hasira zilikuwa zimemjaa kwa kiasi kikubwa sana na asingeweza kuongea na mtu kwa huo muda, aliona hiyo sehemu haimfai tena kwa sababu kuna mhudumu aliye mletea supu alikuwa ameshamuona tayari japo hakuwa na uhakika kama alifanikiwa kumtambua sura yake ambayo kwa sasa ilikuwa na ndevu zilizokuwa zimechongwa kwa usahihi mkubwa mno. Alivaa nguo zake ambazo zilikuwa za kazi alichukua simu yake na kila kitu chake hata hakufunga hapo ndani alitoka kwa haraka kubwa mno. Wakati anatoka wahudumu wote walimshangaa kwani nguo alizokuwa amevaa sio mavazi ya Tanzania kabisa walikuwa wanaziona kwenye picha za maninja hususani kutoka ndani ya nchi ya Japan, ni nguo za kazi na mara nyingi huwa anazivaa majira ya usiku tu leo hii asubuhi na mapema kabisa alikuwa amezitinga kwenye mwili wake na hakuna aliyeweza kumtambua kabisa kwa sababu ya kofia kubwa iliyokuwa imeficha uso wake, panga lake kama kawaida lilikuwa mgongoni na star zake za kutosha zikiwa kiunoni japo ilikuwa ni ngumu sana kuziona. Alipanda kwenye gari na kutoka ndani hapo kwa spidi kubwa kitu kilicho washtua sana baadhi ya wateja ambao walikuwa wamewahi mahali hapo kwa ajili ya kupata huduma, wakati anaanza kuitafuta bara bara ya kwenda mwenge akiwa amepandisha mpaka juu vioo vyake vya gari alipishana na gari sita za jeshi zikiwa zinaelekea sehemu ya ile hoteli alikotokea akajua lazima yule dada ameshapiga simu hivyo alijua anatakiwa kuchukua tahadhari kubwa sana kwani sura yake inaonekana inajulikana vilivyo. Ni kweli zile gari sita zilikuwa zinaelekea kwenye ile hoteli, walifika pale na kumtafuta yule dada aliyeweza kuwapigia simu akawapeleka moja kwa moja kwenye chumba alichokuwepo Calvin, wakiwa na siraha kali za vita wanajeshi wapatao hamsini walishangaa mlango huo uko wazi, waliingia haraka na kutafuta kila sehemu mpaka bafuni lakini hakukuwa na mtu. Kiongozi wa msafara alivyo angalia chini alilishika bakuli lile la supu na kuona bado la moto kabisa alitamka kwa jazba

“pumbavu huyu kaondoka sio muda na atakuwa hajafika mbali, ebu tuonyeshe chumba cha kamera hapa haraka sana” alikuwa anaongea kwa sauti kali ya mamlaka mwanaume huyu iliyo anza kumuogopesha mpaka huyu mhudumu aliye waita hapa. hawa walikuja na gari za jeshi lakini kiuhalisia walikuwa ni makomando kabisa wa siri waliokuwa chini ya mkuu wa majeshi, kwa aina ya mtu waliyekuwa wanamtafuta walijua kama wakienda wanajeshi basi watakufa wengi sana ikawalazimu kuweza kuwatumia makomando kabisa ikiwa ni ombi la waziri mkuu huyo kwa mkuu wa majeshi baada ya kudai anahitaji kuilinda amani ya nchi ili waweze kumaliza kazi mapema sana. waliingia kwenye chumba cha kamera na kurudisha dakika kadhaa nyuma kweli wakaona kuna mtu ana mavazi meusi anatoka humo ndani.
“tuondoke haraka sana humu ndani huyu ni yeye ametoka sio muda mrefu sana” alitamka huyo kiongozi ambaye hakuonyesha hata sura ya masiara huku akimrushia mhudumu huyo maburungutu mengi sana ya pesa kwa sababu alitoa taarifa ambazo ni sahihi kabisa na walijua wazi watampata tu na kama wakimkamata basi mwanamke huyo angetefutwa kupewa pesa yake nyingine alifurahia mno kupata pesa nyingi kiasi hicho na hakuona haja ya kuendelea kufanya hiyo kazi ya hotelini mkononi akiwa na milioni thelathini alizopewa hapa bila kujua kwamba kamsababishia matatizo makubwa sana kijana wa watu ambaye hana hatia yoyote ile, gari za jeshi zilitoka kwa spidi hapo iliwatisha baadhi ya watu wakaanza kuondoka kwenye hiyo hoteli baada ya kuamini hapakuwa na usalama wa kutosha.

Unadhani Calvin anatokaje kwenye hili? atapona vipi ikiwa kila chombo cha usalama kinamtafuta na kila mwananchi alimchukia sana kwa aina ya kesi aliyokuwa amepewa? nini hatima ya kijana huyu asiyekuwa na hatia yoyote ile?

60 inafika tamati panapo majaaliwa ungana namimi tena wakati ujao

Chao[emoji2768]
Bux the story teller

#ULIMWENGUWAWATUWABAYA

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
kwa sababu ya kumuenzi Baba yetu wa taifa tuutumie muda wetu leo kupumzisha vichwa, unapumzishaje kichwa bila kupata burudani kutoka kwa Bux the story teller?

Basi njoo na 1500 yako tu pekee uweze kuimalizia ULIMWENGU WA WATU WABAYA mpaka mwisho kabisa.

Hivyo usijisikie unyonge kukaa mwenyewe nyumbani siku ya leo wakati Bux the story teller yupo kwa ajili yako.

0621567672 (WhatsApp)
0745982347

lipia kwa hizo namba jina FEBIANI BABUYA.

Unapewa hadithi muda huo huo ili siku yako iishe vyema ukiupa ubongo burudani ya madini ya kutosha

Bux the story teller
 
Calvin atachomokaje hapa, hebu tuendeleee ndugu mwandishii
 
Baruani atakufa, Victor atamuoa Eunice, na Victor hatakuwa chini ya Kassimu chacha, Luciana hasira yake inarudi Kwa Kasimu chacha, Victor na Luciana wataungana na Calvin, tuendelee ngoma nzitoo kabisa
 
Baruani atakufa, Victor atamuoa Eunice, na Victor hatakuwa chini ya Kassimu chacha, Luciana hasira yake inarudi Kwa Kasimu chacha, Victor na Luciana wataungana na Calvin, tuendelee ngoma nzitoo kabisa
Asante sana bosi...ngoja tuone mambo ya kutisha yanayo fuata huko mbele
 
HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA 62
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA....................
Kasisi Chacha alikuwa ameingia humo ndani kwa huo muda ghafla sana akiwa na makomando wawili kutoka ndani ya idara ya usalama, wote walishangaana sana, ilikuwa inahitajika sana hawa wote kukutana ili maswali yaulizwe na kujibiwa kiusahihi mkubwa mno wote wanne wakiwepo na leo walikuwa wapo wote.

ENDELEA....................................
"unatafuta nini hapa shetani wewe" Victor aliuliza kwa ukali sana akiwa anamuangalia Baruan kwa macho makali sana wakati huo Baruan alikuwa yuko bize kumwangalia Eunice kama yeye alivyo kuwa akimjua tangu wakiwa katika shule ya Chekelei huko Tanga, ilibidi Baruan ageuke kumtazama bwana mdogo huyo kwake kwani alimzidi kila kitu kuanzia umri wa kuzaliwa mpaka ngazi za mapigano ni kama alikuwa mtoto sana kwake.
"unampenda huyu bwana mdogo" kwa mara ya kwanza Baruan aliufungua mdomo wake kumuuliza Eunice akigeuza shingo aliyokuwa anamuangalia Victor huku akiwa hajali chochote kama mtu aliye mlea na kumkuza kweye ukomando Kasisi Chacha yupo humo ndani. Alitabasamu akiwa na machungu moyoni baada ya kuona mwanamke huyo hawezi kujibu chochote.
"nilikuwa sahihi sana mahesabu yangu kwa sasa huwezi hata kunikumbuka" wakati anataka kugeuka tena ili amjibu Victor Eunice alienda na kumkumbatia kiumbe huyo wa hatari mbele ya watu wote wanne, hii ilimuuma sana Victor lakini hakuwa na nguvu za kufanya chochote kile.
"mimi waliniambia umekufa unahisi ningefanya nini mimi kwanini ulinikimbia na ulienda wapi mpaka waseme wewe umekufa?" Eunice alikuwa akilia kwa sauti kubwa aliuliza swali kwa uchungu wakati huo mzee Kasisi Chacha alikuwa amejikausha kama vile hayupo ndani humo, Baruan aliunyanyua uso wake na kumwangalia mzee Kasisi Chacha kwa umakini kisha akamgeukia tena Eunice.
"ni kwa sababu ya yule shetani pale aliamua kucheza moja ya michezo mibaya sana kufanikiwa kututenganisha mimi nawewe, alizichanga karata zake kwa usahihi sana na ni mtu mbaya sana huyu mzee ila anajificha kwenye mgongo wa kujifanya ni mtu mwema sana kwa sababu ana wadhifa mkubwa sana ndani ya serikali hii. Stori uliyopewa kwamba nimekufa hata mimi nilipewa hivyo hivyo nikaonyeshwa na mwili wako kabisa hivyo nilikuja kushtuka sana baada ya kujua kwamba upo hai na unaishi kwa mwanaume mwingine ambaye ni jasusi kama mimi( akimwangalia Victor), iliniuma sana kuona una mimba ya mtu huyo nilitamani sana kumuua kama bahati tu ulivyotokea siku ile pale niliamua kuondoka tu ila ni muda tu nimejua unaishi na huyu mtu. Sikutaka ujue kuhusu uwepo wangu kwa sababu najua kwenye maisha yako ulikuwa tayari ulishanifuta na kuipata furaha mpya, ni kama bahati mbaya tuliweza kukutana pale japo kama ungechelewa baba mtoto wako ningekuwa nishamuua mpaka sasa. Kuna vitu vingi sana ambavyo huvijui kuhusu historia ya maisha niliyo yaishi na nilikuwa wapi muda wote huo na kwanini saivi mtu ambaye nilimheshimu kama mwalimu wangu ndiye mtu ambaye nilikuwa namtafuta sana kuliko kitu chochote (akimtazama Kasisi Chacha kwa ghadhabu kubwa, walinzi wa mzee huyu walichomoa siraha zao lakini aliwazuia akiwa ameweka mikono yake nyuma anasikiliza kwa umakini).
Baada ya kujua kwamba wewe umekufa nilienda kupikwa kwenye mafunzo ya kikomando Morogoro chini ya usimamizi wa mzee huyo, ilinichukua miaka miwili, baada ya hapo nimezunguka miaka nane tofauti katika nchi zaidi ya tatu, baada ya kumaliza mafunzo hayo niliweza kurudi nchini nilifanya kazi chini yake na sikuwa mtu wa kuonekana kabisa mbele za watu kwa sababu nilitengenezwa maalumu sana kwa ajili ya taifa na nilitakiwa kuwa nguvukazi kubwa sana kuisaidia nchi linapotokea suala lolote la kiusalama na ni kweli nilifanya hivyo kwa moyo wangu wote.

Mwaka mmoja tangu nitue Tanzania nilifanikiwa kuanza kumjua mzee huyu kwa undani sana, ni mtu hatari sana kuliko kitu chochote hapa nchini na bahati mbaya sana hata mheshimiwa Raisi halitambui hili mpaka leo. Baada ya uchunguzi wangu wa kina niligundua amewaua wazazi wako na familia yako yote(Eunice alitaka kudondoka kwa presha hiyo kubwa lakini alidakwa na mwanaume Baruan waweza kumwita Rashid Bakari na kukalishwa kitandani kwa usahihi kabisa), nilivyo lijua hilo na baadhi ya siri zake nyingi za mambo yake mengi aliyokuwa anayafanya kwa siri hususani ndani ya Casino lake kubwa la SEVEN WORLD CASINO ambalo lina ushetani mkubwa sana ndani yake ndio muda ambao alinitengenezea kesi ya kuonekana nimeliasi taifa langu huku akijaribu kuniua, nilijitahidi kulielewesha jeshi na kuwaambia kwamba mimi sikuhusika kwa lolote lile bahati mbaya sana hakukuwa na mtu yeyote yule wa kunisikiliza upande wao jeshi zima lilinisaliti vibaya sana iliniuma mno nikaapa nitamtafuta kila aliye nisaliti, nilifanikiwa kuwaua makomando ishirini ambao walitumwa kunitafuta na ugomvi na serikali ulianzia hapo. Baada ya hapo nilikuja kuwa mtu hatari sana ambaye hakuna binadamu alitamani kukutane naye. Huyu mzee ndiye yupo nyum.........." Kabla hajaitamka hiyo sentensi yake kilirushwa kisu kikali maeneo ya shingoni ambacho kilikuwa kama maji tu kwa kiumbe huyo alijibetua kwa nguvu akakidaka kisu hicho kisha akatua chini kama hakuna kilicho tokea humo ndani akakitupa chini, Victor alikuwa bado haelewi kinacho endelea, walikuwa wameingia wanaume wengine sita, walikuwa ni makomando hawa wa idara ya kijasusi ya usalama wa taifa, walikuwa hapo kuhakikisha mwanaume huyo hatoki humo ndani na kiongozi wao anakuwa salama kwa asilimia miamoja kwani miongoni mwa kazi walizo kula kiapo ni kumlinda mtu huyo kwa gharama yoyote ile.

Walikuwa wametimia makomando nane ambao walikuwa hapo kumlinda mzee huyo.

"unaogopa sana watu kukujua kiundani eeh hahahahahahaha, kama nikikuacha leo mzee utakuwa na bahati kubwa sana haijalishi uko na nani" Baruan alivyo maliza kauli yake tu kuna komando alikuwa anakuja kwa kasi sana akiwa anarusha visu vyake viwili ila alishangaa mtu huyo anavidaka visu hivyo kwenye makali na kuvivunja kwa nguvu kisha akarusha ngumi kali sana kwa komando huyo iliyo mpata kwenye mbavu zilizo vunjika kwa nguvu sana kisha akashika shingo ya komando huyo na kuivunja vibaya habari yake ikawa imeishia hapo, Baruan alikuwa ni mtu hatari sana, Eunice alikuwa haamini kama anaye muona mbele yake ndiye huyu Rashid aliyeweza kufunga naye ndoa akiwa kijana mpole Sana, Victor alisogea taratibu mguu wake ukiwa bado haujapona akamkumbatia mwanamke huyo ili asione kinacho enda kutokea kwani alielewa unyama unao enda kutokea kwenye chumba hicho kidogo ulikuwa ni wa kutisha na mwanamke huyo hakupaswa kuuona hata kidogo. Licha ya huo ukatili uliofanyika hapo Kasisi Chacha hakuonyesha wasi wasi wowote ule hata kushtuka kabisa akauliza swali kwa Baruan na kuufungua mdomo wake kwa mara ya kwanza tangu aingie humo ndani.

"Badala unipigie magoti uniombe msamaha nione kama naweza kukusamehe Kwa sababu ni moja ya vijana ambao mnafanya kazi chini yangu mpaka leo, unaendelea kufanya ujinga mwingine wa kuwaua vijana hawa, Roland ulimuua kikatili vile kwa sababu gani?" Mzee huyu alikuwa akiuliza kwa ukali akiwa amemkazia macho Baruan ambaye naye hakuwa hata na chembe ya wasi wasi kabisa.

"Huenda ningemsamehe alitamka kauli ambayo nilitakiwa kumgawa vipande vipande anaongeaje kwa dharau kwamba alilala na mke wangu(Marry alishtuka sana baada ya kusikia yule mtu alikuwa amekufa) hivyo baada ya yeye ni zamu yako wewe hapo" sauti nzito ya Baruan ilisikika akiwa anatoa visu vyake viwili vyenye makali sana kiunoni hakuhitaji kutumia silaha alinja itapiga kelele na kuwashtua wengi humo ndani ilitakiwa wayamalize kiume.

"hahahahahahaha mtoto mdogo sana nimekulea mwenyewe unataka kujifanya unajua sana, sasa nakufanyia kitu ambacho hata ungepata nafasi ya kusalia hai usingeweza kukisahau kamwe kwenye maisha yako" Kasisi Chacha alitamka kwa sauti kubwa yenye mamlaka makubwa akiitoa simu kubwa kwenye mfuko wake, Baruan alishtuka baada ya kuiona simu ya aina hiyo alikuwa akiijua vyema kazi yake ghafla sana alijizungusha kwa nguvu umeme ukakatika humo ndani na kuwashtua watu wote.

******************************************
Saa kumi na mbili za jioni Calvin alikuwa ameamka tayari ndani ya kambi ya THE RED SQUARD, alijiandaa haraka sana kwani alikuwa na kazi nzito sana ya kuifanya saa mbili za usiku.

"zingatieni sana nilicho waambia ilitakiwa mpaka sasa muwe mmetoka humu ndani kuna hatari kubwa inaweza kutokea leo, Mimi naondoka ila msijisaha ......" kabla hajamalizia sentensi yake Kwa Luciana aliyekuwa mbele yake amevalia kanguo kepesi tu kumtamanisha mwanaume huyo simu yake iliita kwa nguvu sana ilibidi kuipokea kwani hiyo namba walikuwa nayo watu wachache sana isingekuwa rahisi sana kwa mtu ambaye hamjui kumpigia.

"Hello tajiri" ilikuwa sauti moja ndogo sana ya kiume kutoka upande wa pili ilimshangaza kidogo

"Wewe nani na unataka nini" aliuliza kwa sauti yake nzito sana

"hahahaahaha kuwa mpole uharaka wako unaweza kuponza maisha ya mtu" sauti hiyo ndogo ilimjibu kwa jeuri kubwa mno.

"Tomaso sio" hakuwa na papara sana licha ya kungundua huyu alikuwa ni Tomaso bwana mdogo ambaye alijitoa kumsaidia na alimuokoa kuingia kwenye mikono ya jasusi mwenye roho ngumu kweli kweli Victor, alijua bwana mdogo hakuwa upande wake mpaka muda huo licha ya mara ya mwisho kuweza kuwaagiza waende Paris Ufaransa ambako aliamini watakuwa salama kabisa na alimsisitiza sana bwana mdogo huyo pamoja na mlinzi wake Thomasi kuhakikisha usalama wa Veronica kwa gharama yoyote ile vinginevyo asinge muelewa mtu, mwanamke huyu kwa sasa alikuwa kama familia kwake baada ya kuachiwa usia na mzee Ndipo Mwalemi au Mgaya siku ile anakufa maeneo ya Kimara kumlinda binti yake huyo kama roho yake .

"Vipi una wasi wasi nitakuwa nimemfanya vibaya huyu kimwali ambaye anaonekana anakupenda sana hahahahahahaha" haikuwa kawaida kabisa kwa bwana mdogo huyo kuwa na jeuri sana mbele ya huyo mwanaume kwa sababu alikuwa akimwogopa sana Calvin hivyo Calvin alishangaa sana kipi kinampa jeuri huyo bwana mdogo mpaka afikie hatua ya kumjibu Kwa jeuri kiasi hicho.

"Hakuna binadamu amewahi kunisaliti halafu akaendelea kuishi tena, sina muda wa kuitoa roho dhaifu namna hiyo, sitaki kujua ni nani amekutuma au ulitumwa kwangu ila nakupa masaa 24 uniletee huyo mwanamke kwenye mikono yangu akiwa yupo salama bila hata alama ya kibao kama nilivyo kukabidhi" aliongea kistaarabu sana Calvin unaweza ukahisi hakukuwa na tatizo lolote lile lililokuwa limetokea hapo.

"Sio kirahisi sana hivyo Kaka mkubwa, unajua nyakati zinaenda sana na maisha yanabadilika kwa kiasi kikubwa sana, kwa sasa nimekuja kugundua kwamba hii dunia pesa ndo kila kitu kwangu, nahitaji kuwa mtu mkubwa sana mambo ya kuogopana ilikuwa zamani mno na hivi sasa huwezi kupata hata nafasi ya kunisogelea nalindwa sana na hautaweza kunipata kamwe bila kufanya kama navyotaka mimi kwahiyo unapaswa unisikilize kwa umakini mkubwa bwana mkubwa" Tomaso alikuwa akijiamini mno na wala usingekaa ukaamini kwamba ndo Yule Tomaso mwoga wa Goba rafiki wa zamani wa Jarome aliye uawa na Scot maeneo ya Tandika alikojulikana kama Tenga.

"Bwana mdogo tamaa za muda mfupi zisikufanye ukaiona hii dunia ni kubwa sana kama akili yako inavyo kutuma, bado mikono inaifanya dunia kuwa kijiji kidogo sana kwa kasi ya ukuaji wa teknolojia, nakupa nafasi ya mwisho achana na huo ujinga unao uwaza kwa sababu hakuna sehemu utaenda nikashindwa kukupata, ninaweza kukupata kwa masaa kumi tu haitajalisha upo upande gani wa ulimwengu, hizo kompyuta zako zisikusahaulishe mimi ni nani na wewe bado ni kiumbe dhaifu sana, nina kazi nyingi za kufanya hayo masaa ishirini na manne yatumie vyema kuniletea huyo bibie" aliongea kauli hii Calvin akiwa siriasi sana na kwa msisitizo kupita kiasi.

"Tuache kutishana mapema hivi ujue huyu mwanamke nipo naye kwenye mikono yangu ukijifanya kiburi namuua na sina hasara yoyote ile vipi kwako wewe lazima utajihisi binadamu mwenye hatia sana kumpoteza kwa uzembe wako mwanamke ambaye umeombwa umlinde kwa gharama yoyote na umpe maisha mazuri" Tomaso leo alikuwa amempatia Calvin vilivyo, mwanaume alikamatika basi ikambidi awe mpole kwa namna bwana mdogo huyu alivyokuwa anajiamini ilimtia shaka alihisi huenda kuna watu nyuma yake wanao mpa kiburi sana namna hiyo, alikuwa dhaifu sana aliamini asingejiamini mwenyewe kufanya hivyo.

"Sawa, unataka nini?" Calvin aliuliza kistaarabu
"nataka bilioni 50 mpaka asubuhi uwe ushazituma" Tomaso aliongea kwa kujiamini utadhani hizo pesa yalikuwa ni magazeti tu.

"Mhhhhhhh hiyo pesa ni kubwa Sana siwezi kukupa, usiichukulie kiwepesi sana namna hiyo pesa ambayo haujahusika hata kidogo kuichuma" Calvin alishangaa kwanini bwana mdogo huyo atake pesa yote hiyo kirahisi sana namna hiyo hivyo aligoma kuitoa.

"ok haina shida nitakuelekeza sehemu ya kwenda kuipata maiti ya Veronica ikifika asubuhi" Tomaso alijibu kwa jeuri kitu kilicho mshtua sana Calvin.

"Sawa, nitakupa ila hakikisha huyo mwanamke anakuwa salama kwa sababu kama kikitokea chochote nadhani unanijua vizuri nitakufanyia kitu kibaya sana, asubuhi nakutumia hiyo pesa yako" mwnaume alijibu kwa hasira huku akiikata simu na kutaka kuondoka kawa hasira lakini Luciana alimdaka mkono.

"Kinaendelea nini mbona ghafla sana? nani katekwa? naweza kukusaidia" Luciana aliongea akiwa anamaanisha lakini Calvin alimwangalia tu bila kumjibu na kuskitika kwa sababu alijua mwanamke huyo alitamka tu pasipo kuelewa huyo mtu aliyekuwa anamtaja anaijua komputa kuliko hata chakula, kumpata kwake ilikuwa ni kazi ngumu mno kwani alikuwa anaweza kubadilisha location zaidi ya miambili kwa dakika zikasoma nchi mbali mbali duniani. Mwanaume hakuona haja ya kujibu akatoka hapo ndani akiwa na dhana zake za kazi, Luciana hakumwelewa Calvin anaenda wapi ikabidi amfuate kwa spidi akatoka naye mpaka nje ya kambi hiyo akiendelea kumsihi amwambie tatizo nini aone anamsaidiaje, lakini mwanaume hakuweza kumjibu chochote kile, walitembea kwa umbali kidogo wakati huo kiza kilikuwa kimeanza kuingia, Luciana akiwa anang'ang'ania Calvin amwambie ukweli waliskia mlio mkubwa sana ambao ulifanya ardhi itetemeke sana, waligeuka kwa haraka kubwa maskini hawakuamini kile walichokuwa wanakiona, kambi ya siri ya THE RED SQUARD iliyokuwa chini ya ardhi ilikuwa imelipuka vibaya sana na mle ndani walikuwepo makomando wanne wa THE RED SQUARD. Luciana hakuweza hata kuhema vizuri alidondoka chini akiwa ameshikilia moyo wake akitoa machozi mazito mno, waliokuwa mle ndani walikuwa ndo familia ya pekee kwake.
Unataka kujua kwanini Baruan aliogopa sana baada ya kuona Kasisi Chacha ametoa simu yake ikapelekea umeme kuzima humo ndani?, unataka kujua kipi kimempata Tomaso mpaka ajiamini mbele ya Calvin namna hii?, unataka kujua hatima ya makomando hawa wa THE RED SQUARD?

62 naachia kalamu inafika tamati tukutane tena wakati ujao
Chao[emoji2768]
Bux the story teller

#ULIMWENGUWAWATUWABAYA
Kwa sasa hadithi hii unaweza kuisoma Kwa shilingi 1000 tu pekee za kitanzania.

Tuma pesa Kwa namba

0621567672 (WhatsApp)

0745982347

Zote jina ni FEBIANI BABUYA

Njoo uimalizie mapema tuanze na kigongo kingine.....ukituma tu pesa yako nakupatia muda huo huo
 
HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA 64
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA................
kitanda kilimsaidia kupunguza kasi ya hizo risasi, kitanda kikiwa kimesimamishwa mwanaume huyo aliyekuwa amekidaka hicho kisu alisogea hapo baada ya kupiga risasi nyingi sana lakini alishangaa hakukuwa na mtu, alivyo yainua macho yake dirisha lilikuwa wazi kuonyesha mtu huyo alitokea hapo alisikitika sana akizirudisha silaha zake kiunoni.

ENDELEA.........................
“umefanya kosa kubwa sana kumuacha huyo mtoto aendelee kuishi tena anaweza kunisumbua baadae ebu hakikisha mnampata haraka sana, ndiye pekee anaye yajua mambo yangu mengi sana kiundani” Kasisi Chacha alitamka kwa sauti yake nzito sana akiwa anaongea na komando huyo aliyekidaka kisu wakati Baruan anakirusha kwake. Kasisi Chacha alikuwa anajiamini sana humo ndani alijua Baruan hawezi kufanya lolote lile kwa sababu kupitia kamera za siri za usalama zilizokuwa zimetegwa ndani ya hospitali hiyo aliweza kupata taarifa za ujio wa huyo kiumbe hapo ambaye alikuwa chini ya waziri mkuu kwa miaka mingi sana hivyo alifanikiwa kuja na makomando wa kutosha pamoja na komputa yake ya mkononi iliyokuwa na uwezo wa kumsambaratisha Baruan atakapokuwa karibu na mzee huyu ili mtu huyo asiweze kutoroka lakini hesabu zake zilienda vibaya sana baada ya mwanaume huyo kupotea kwenye mazingira ambayo hakuna mtu angetegemea hivyo ilimhitaji kuingia upya kwenye mifumo yake ya kijasusi kuzipata upya taarifa za kijana wake wa zamani huyo kisha aitumie nafasi nyingine kama wakikutana siku nyingine wakiwa karibu anaweza kuiwasha kwa usahihi chip ndogo iliyopo kwenye kichwa cha Baruan na kumuua kikatili mno kwa kumpasua mishipa yote ya kichwa.

“nisamehe mkuu huyu anapatikana haraka sana sehemu yoyote ile ndani ya jiji la hili la Dar tunampata hawezi kwenda mbali nina vijana wangu nimewasambaza kila kona waweze kumpata haraka sana” komando Jabiri kama alivyo julikana kwa jina lake, hakuwa mtanzania bali alikuwa ni mhamiaji kutoka nchi ya Somalia, alikuja kupewa uraia baada ya kuonyesha uimara wake kwenye mapigano ya mtaani akachukuliwa na kuwa miongoni mwa wanajeshi walio pata bahati ya kupelekwa nje ya nchi kupata mafunzi zaidi.

“haujui lolote kuhusu huyo mtu hakuna hata mmoja kati yenu mwenye uwezo wa kusimama naye hata dakika tatu, nahitaji umpigie simu Chris nataka nikutane naye haraka halafu mpotee hii sehemu sitaki ijulikane kuna uvamizi wowote umefanywa hapa, linaweza likafika kwa raisi mambo yangu yakafeli ikiwa bado ni mapema sana” Kasisi Chacha aliongea huku akiwa anaondoka, aliupiga mlango wa hapo ndani kwa hasira baada ya kuipoteza kizembe sana simu ambayo ingemuwezesha kumpata huyo mwanaume kiwepesi.

“mzee kwani wewe ni nani hasa?” Kasisi Chacha alishtukia sauti ya bezi kali ikimuuliza swali, alivyo angalia pembeni aligundua huyo mtu ni Victor

“haya mambo hayakuhusu kabisa kaa nayo mbali sana ikiwezekana nenda mbali na huyo mwanamke kuna mambo hupaswi kuyajua ni lazima utakufa” alitamka kwa ukali huyu mzee bila kupepesa macho yake.

“kuhusika na mauaji ya familia za watu, mara umewatenganisha mke na mume, mbona sikuelewi wewe mzee na nilikuamini sana? hivi huna huruma angalia binti wa watu yupo kitandani saivi ni mjamzito amezimia kwahiyo hicho ndicho unacho kihitaji kwenye maisha yako? nambie ukweli huenda nikakusaidia katika hili huenda unayatengeneza mambo ambayo kwa baadae hautaweza kuyabeba, nasema hivi kwa sababu wewe kwangu ni zaidi ya baba itaniuma sana kama kitu nacho kifikiria kichwani kwangu kikawa kweli unaweza ukaishia pabaya sana, wewe ni na….” Victor alikuwa anaongea kwa hasira sana na kwa sauti kubwa lakini alizuiliwa kwa sauti zaidi sita za risasi zilizopita karibu yake, alifumba macho kwani alijua risasi hizo zimeshampata ila bahati nzuri zilipigwa pembeni, wakati anafumbua mambo alishangaa mkubwa wake wa kazi Kasisi Chacha alikuwa akiishia kwenye moja ya kona hapo hospitali na mkononi mwake akiwa na bastola kumaanisha yeye ndiye aliyeweza kupiga risasi hizo, Victor alilia kwa uchungu alihisi ni miongoni mwa watu ambao dunia ilisha wasaliti, aligeuka nyuma kuangalia kwenye chumba kilichokuwa karibu yake kumwangalia Marry aliyekuwa amezimia kitandani akiwa na ujauzito mkubwa sana.

Majira hayo ya usiku kwenye moja ya mitaa ya Ubungo maeneo ya mawasiliano kuna mwanaume mmoja alikuwa anakimbizwa kwa kasi sana, alikuwa anakimbia ikionekana wazi alikuwa anayasaidia maisha yake kutoka kwa moja ya mwanaume aliyekuwa akimuandama vibaya sana majira hayo ya usiku, haikuwa usiku sana hivyo watu walikuwa bado wengi sana mtaani, walishangaa kwanini mtu huyo ayawinde maisha ya mwenzake kiasi hicho kwa sababu kama mtu huyo angekuwa amemuibia alipaswa kupiga kelele kuomba msaada lakini alipita akiwa kimya sana huku akiwa amevaa koti kubwa sana lililo mfika mpaka maeneo ya miguuni. Kijana huyo aliyekuwa anakimbia aliingia kwenye kichochoro kimoja ambacho huwa kinatumika sana na watembea kwa miguu wanao toka kwenye stendi ya mawasiliano kuja kwenye stendi kuu ya magari ya Ubungo, maeneo hayo kuna kimto kidogo kinacho pitisha maji machafu kukiwa kumepambwa na kimsitu kidogo chenye mianzi mingi kuliko miti mingine, ndipo alipokuwa amefika huyo kijana, alisimama akihema kwa nguvu akasimama na kuangalia pande zote lakini hakuweza kuona mtu yeyote yule kidogo sura yake ilipata nuru akaanza kutembea taratibu, hakupiga hata hatua tatu alipigwa na teke lenye uzito wake likamrudisha kule kule alikokuwa ametoka alijibamiza kwenye moja ya mti uliokuwa karibu na hayo maeneo. Alijikongoja kusimama kwa sarakasi moja maridadi sana kisha akajinyoosha akiwa na wasi wasi mkubwa sana.

“kwahiyo kwa akili zenu fupi mlijua mtaweza kunikimbia hahahahahah, sasa leo nataka nikuonyeshe namna unavyo takiwa kuishi na wakubwa zako” sauti nzito iliyoshiba ya Baruan Mahafidhu ndiyo iliyokuwa ikisikika kwa huo muda maeneo ya Ubungo hapo. Huyu ndiye aliye onekana kumsakama kijana wa watu aliyekuwa anayaokoa maisha yake. Kijana huyu alikuwa ni Thomas ambaye ni mlinzi wa Tomaso, ilikuwa ni ajabu sana kumuona saivi kwenye mitaa hii ya Ubungo wakati mara ya mwisho walienda Paris Ufaransa yeye, Veronica pamoja na Tomaso mweneyewe.

Calvin na Luciana baada ya kufanikiwa kumteka yule mwanamke maeneo ya uwanja wa ndege walichukua tax mpaka gongo la mboto wakidai kwamba yule mwanamke ni ndugu yao amepatwa na tatizo baada ya dereva huyo kuhoji kwa jinsi wanamke huyo alivyokuwa amebebwa ukijumlisha na mavazi ya Calvin yalikuwa yamemtisha kidogo, dereva hakuwa na tatizo kwa sababu yeye alijali zaidi mlo wake. walishuka kisha wakaanza kuifuata njia ya pugu, wakakunja kushoto kwao, hatua kumi tu walikuwa wamesimama mbele ya jumba moja kubwa sana la kifahari, Luciana aliligusa geti hilo kisha akatamka maneno sita kwa kilugha chake mlango mzito uliotengenezwa kwa madini ya shaba uliweza kujifungua wenyewe wakaingia humo ndani.

“mhhhhhh mtoto wa kike umewezaje kumiliki nyumba ya gharama na ya siri sana kwenye mazingira kama haya?” Calvin aliunguruma wakati anamtua mwanamke aliyekuwa amemuweka begani kwake kwa zaidi ya saa moja sasa.

“tunalipwa pesa nyingi sana lakini usipo angalia unaweza ukazimalizia kwenye starehe tu kwa sababu unajua pesa zingine zinakuja muda wowote ule ila bahati mbaya sana mimi sio mtu wa starehe hivyo huwa najenga majumba tu ndio furaha yangu, nina nyumba nane hapa Dar es salaam tano nimepangisha japo hawamjui mmiliki huwa wanaishia kutuma pesa tu hatuonani na tatu nimezitenga kwa ajili ya kazi zangu. Hapa tulipo ni salama sana hakuna mwanadamu yeyote anajua kuhusu hizi nyumba zangu wewe ndo wakwanza” Luciana alijibu wakati huo alikuwa akitabasamu.

“unatakiwa ujue kwamba ipo siku MUNGU atakuchukua hivyo ni vyema ukatafuta familia nzuri tu ukaishi maisha ya kawaida upate hata watu wakurithi mali zako hizi haipendezi kwa mtoto wa kike mzuri sana mpaka umri kama huo unahangaika kutafutana na roho za watu usiku mtaani” Calvin alijibu wakati huo anajitupa kwenye sofa zuri lililokuwa humo ndani.

“mbona wewe ni tajiri mkubwa sana hapa nchini na inasemekana kwamba huenda baba yako ndiye alikuwa mtu tajiri zaidi nchini hivyo nawewe bila shaka ndo utakuwa tajiri mkubwa zaidi kwa sasa Tanzania na haujaoa kwa nini uniseme mimi?” Maneno yale yalimgusa Calvin aliyejifanya kutoa darasa kwa mwenzake wakati hata yeye mwenyewe alikuwa hana hata mtoto wa kumwachia mali zake zote hizo, alipotezea kama sio yeye aliyekuwa akiongea mara ya kwanza na kujifanya yupo bize kuwasha televisheni basi Lucy alicheka sana akimimina juice yake ya matunda iliyokuwa imewekwa kwenye friji hapo ndani.

“nataka huyo mrithi wa mali zangu unipatie wewe” Luciana aliongea bila kupepesa macho akiwa amemkazia macho Calvin mpaka akajishtukia ikabidi anyanyuke na kuulizia bafu lilipo kwani aliona kabisa huyo mwanamke alikokuwa anaelekea sio kwenyewe hata kidogo, Luciana alijiamini sana hata yeye mwenyewe alijishangaa huo ujasiri mbele ya huyo mtu kautolea wapi kuongea hayo maneno hata hivi aliridhia kutoka moyoni kwamba alimpenda mwanaume huyo japokuwa alimzidi umri kwa miaka zaidi ya nane.

“hello mheshimiwa” ilikuwa sauti ya Calvin baada ya upande wa pili kupokea simu.

“nani wewe” sauti kali ilitokea upande wa pili mwa hiyo simu

“unavyo piga hayo makelele unaniumiza masikio yangu ebu kuwa mstaarabu kwenye uongeaji wako” Calvin alijibu kibabe na kwa jeuri iliyo mshangaza mtu wa upande wa pili

“bwana mdogo huenda haujui unaongea na nani hiyo jeuri ya kunijibu kama mimi mjomba wako wa damu inaweza ikaleta madhara mpaka kwa familia yako yote” upande wa pili sauti ilijinadi kuonyesha kwamba aliyekuwa anaongea alikuwa ni mtu mzito sana.

“ni majira ya usiku sana saivi simu haiwezi kukosewa kizembe sana namna hiyo mzee wangu, nadhani naongea na Chris dalali wa zamani maeneo ya Manzese” Calvin alijibu kwa kujiamini sana akiwa anaendelea kupata juice yake taratibu ya embe. Hilo huyo mtu wa pili lilimshtua na kumtisha kupita kiasi kwa sababu hakutaka sana mambo yake yawe yanazungumziwa kwenye midomo ya watu wengi sana, aliua watu wengi sana waliokuwa wanamjua kiundani mtu huyo.

Ukurasa wa 64 sina la ziada tena

Chao[emoji2768]

Bux the story teller

#ULIMWENGUWAWATUWABAYA
Kwa sasa hadithi hii unaweza kuisoma Kwa shilingi 1000 tu pekee za kitanzania.

Tuma pesa Kwa namba

0621567672 (WhatsApp)

0745982347

Zote jina ni FEBIANI BABUYA

Njoo uimalizie mapema tuanze na kigongo kingine.....ukituma tu pesa yako nakupatia muda huo huo
 
HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA 65
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA................

“ni majira ya usiku sana saivi simu haiwezi kukosewa kizembe sana namna hiyo mzee wangu, nadhani naongea na Chris dalali wa zamani maeneo ya Manzese” Calvin alijibu kwa kujiamini sana akiwa anaendelea kupata juice yake taratibu ya embe. Hilo huyo mtu wa pili lilimshtua na kumtisha kupita kiasi kwa sababu hakutaka sana mambo yake yawe yanazungumziwa kwenye midomo ya watu wengi sana, aliua watu wengi sana waliokuwa wanamjua kiundani mtu huyo.

ENDELEA......................

“nani wewe” sauti ya upande wa pili ilijibu kwa wasi wasi kubwa

“Monica Denis nafkiri unamkumbuka na kumjua kwa usahihi sana” Calvin aliuliza tena kwa msisitizo kuonyesha hakubahatisha kumpigia simu mtu huyo.

“unataka nini kwangu” huyo mwanaume aliamua kujiongeza kwa maelezo ya Calvin alionekana wazi kwamba alikuwa akimjua vizuri huyo mtu hivyo alitambua kuna kitu anahitaji kwake.

“mzee wangu siasa na uongozi ziliwekwa ili kuweza kusaidia jamii na wananchi wa sehemu husika waishi kwenye misingi bora hususani hii nchi yetu ambayo tumebarikiwa amani sana, bahati mbaya sana watu kama nyie mmeigeuza siasa kuwa michezo michafu huku mkiwahadaa wananchi kwa sera zenu za uongo midomoni ajabu mkigeuza migongo tu mnawarushia vumbi kwa jeuri na dhihaka kwa sababu mnajua nyie hamuwezi kuteseka kwa lolote kama walala hoi wachache ambao wameamua kuikubali hali yao na kuamini MUNGU pekee ndiye msaada wao wa mwisho. Mnaua watu wewe na wenzako na hakuna kitu sheria inawafanya kwa sababu hata hao walio ishika sheria ndio kama wewe tu, huwa hawakumbuki hata kidogo ni wapi walitoka kabla ya kuingia kwenye hivyo viti ila nataka nikuthibitishie tu kwamba kwenye nchi hii kama nipo hai hakuna mwananchi ataendelea kuteseka tena waambie na wenzako (akaguna kidogo). Ulikuwa na maisha magumu sana pale Manzese ukiwa huna hata mia mfukoni unategemea upate wateja wa nyumba ili mdomo uende kinywani, wakati huo ulikuwa kijana bora sana ukapendwa na kila mtu ila bahati mbaya sana wanadamu wengi mna roho nyepesi sana linapokuja suala ya pesa, pesa imebadilisha uhalisia wa maisha na kuwafanya wenye nayo ndio pekee waonekane wana haki ya umiliki wa dunia hii na asiye kuwa nayo hana thamani yoyote wala hawezi kusikilizwa, sasa unapaswa uelewe kwamba pesa sio kila kitu kwenye maisha japo unatakiwa uwe nayo.

Monica Denis ni mwanamke uliye zaa naye kwa siri sana kwa sababu hukutaka ijulikane kwa watu kwa vile ulijua ni mwanamke anaye jiuza, maskini mdada wa watu licha ya kukuzalia na kuamua kuitunza siri hiyo moyoni mwake bado ukamuua bila kujali maisha ya mtoto ya baadae atakapo kuuliza wapi alipo mama?, ulivyo mbinafsi ukaamua uangalie upande wako tu sasa unatakiwa uandae maswali ya kumjibu mtoto wako siku atakayo ujua ukweli bwana Christopher Hamza, nadhani kwa sasa umeanza kupata picha kwamba unaongea na mtu wa namna gani hivyo uwe na heshima sana unapo ongea namimi nikiamua hata kesho hicho kiti chako hauwezi kukaa tena nina video zako na picha zako za utupu wako kibao ukiwa unawadhalilisha watoto wakike wadogo kabisa, sijakupigia simu tuanze kubishana nahitaji unisikilize kwa umakini mkubwa sana” Calvin alitoa simulizi fupi kuonyesha kwamba anamjua huyo mtu kuliko hata yeye mwenyewe alivyokuwa anafikiria.

Upande wa pili mtu huyo aliyekuwa anasikiliza maelezo hayo ya Calvin alianza kutoka jasho mapigo yake ya moyo yakiongezeka, hakuweza kutulia sehemu moja, alikuwa mtu mwenye wasi wasi sana alijibu kwa uoga ulio pitiliza.

“sawa kijana wangu unataka nini?” sauti ya unyenyekevu ilimtoka huyo mtu, upande wa pili alikuwa anaongea waziri mkuu wa nchi ya Tanzania Christopher Hamza. Monica ndiye mwanamke aliyeweza kuzaa naye mtoto wa kike wa pekee baada ya kupata nafasi ya kuwa waziri mkuu wa nchi ya Tanzania akiwekwa na mtu asiyejulikana aliamua kumuua huyu mwanamke ili hizo skendo chafu za waziri mkuu kuzaa na mwanamke anaye jiuza zisije zikavuja kwa wananchi pamoja na kwa raisi hivyo aliamua kumuua kwa siri kubwa sana bila mtu yeyote kujua ili kuweza kuilinda nafasi yake na ndio muda alioweza kumtoa mtoto wake nchini na kumpeleka kwenye nchi za watu kupata masomo yake.

“una mtoto wa kike mzuri sana ila namsikitikia sana aliweza vipi kuwa mtoto wa binadamu kama wewe, kila nikimtazama namuonea huruma sana akijua ukweli wako nadhani anaweza akalaani kuwa na baba wa aina yako” Calvin aliongea akionekana wazi alikuwa akisikitika juu ya hilo jambo.

“wewe mpuuzi unasemaje? mwanangu anaingiaje katika hili, mshenzi wewe usije ukathubutu kumuongelea mwanangu tena nitakuua wewe na kizazi chako chote nadhani haujanijua vyema kwamba mimi ni nani sio?” aliongea kwa jazba waziri mkuu akionekana wazi hakupenda mtoto wake atajwe hovyo kwani alimpenda sana huyo binti yake huyo wa pekee.

“huyo mtoto unayepiga makelele unajua yuko wapi kwa sasa?” Calvin aliuliza akiwa ameibadilisha sauti yake kuwa kwenye hali ya usiriasi sana, waziri mkuu alitoa simu yake ndogo mfukoni akawapigia watu wake waliokuwa wameenda kumchukua binti yake na kumpeleka kwenye makazi yake ya siri yaliyopo Tegeta lakini jibu alilopewa ni kwamba hawapatikani akaangalia namba zingine akawapigia wale wanaume waliokuwa wakimlinda binti yake tangu yupo nje ya nchi jibu lilikuwa ni hilo hilo kwamba hawapatikani kama wa mwanzo aliogopa sana.

“usihangaike na vitu ambavyo haviwezekani kamwe nahitaji unisikilize kwa umakini mkubwa mno,binti yako ninaye mimi hapa, ni mzuri sana hivyo kuendelea kunipigia makelele ya ukali utanifanya niwaze mengine ya kumfanyia huyu mwanamke ukizingatia mimi ni mwanaume rijali. Una mambo mawili makubwa ambayo unatakiwa unayafanye ili umpate huyu mtoto wako vinginevyo nitamfanyia ukatili ambao hata wewe haujawahi kuufanya kwenye maisha yako, jambo la kwanza kesho navyo amka asubuhi nahitaji nione taarifa mpya ya habari ikitangaza kutengua kauli zako za za jana ambazo zimefanya kila mwananchi anione mimi kijana wa hovyo na wa ajabu mno kuwahi kuzaliwa kwenye nchi hii kwa kunisingizia kesi ya mauaji na ubakaji wakati kiuhalisia hizi ndizo kesi ambazo wewe ndiye unayetakiwa kuzibebea msalaba hivyo nataka kwa kinywa chako mwenyewe ukalisahihishe hilo na uwaambie watu wako wote ikiwemo hao makomando wa jeshi la nchi pamoja na jeshi la polisi waache kunitafuta mara moja mimi sio wa kuwindwa namna hiyo mtaani kama pesa bila kuhusika kwa chochote baada ya hapo nitakwambia nini cha kufanya hilo likiisha. Jambo la pili nahitaji unipatie jibu ni nani yuko nyuma yako, hilo jibu nalihitaji haraka sana kwa muda huu hapa kabla sijabadili maamuzi yangu” waziri mkuu alishika moyo wake kwa presha ya mambo aliyokuwa ameambiwa hapo ilimbidi anywe maji kwanza ili kidogo apate nguvu, kwanza alishangaa sana imewezekanaje mtu huyo akajua mtoto wake anafika leo nchini? hii ilimtisha na kuhisi huenda mtu huyo anamjua sana kuliko anavyo mfikiria, suala la kwenda kwa waandishi wa habari halikuwa tatizo kubwa sana kwake lilikuwa ndani ya uwezo wake ila jambo zito lilikuwa ni kumtaja mtu aliyekuwa nyuma yake kwa sababu kama angeitoa hiyo siri ilikuwa lazima auawe, dakika nzima iliisha akiwa kimya hajaongea chochote waziri mkuu alikuwa kama amechanganyikiwa.

“unanipotezea muda nina kitu cha msingi sana napaswa kukifanya muda huu hapa kama huyo mtu ni mhimu sana kuliko familia yako basi haina tatizo nitamalizana na mwanao mwenyewe” sauti ya Calvin ndiyo iliyo mshtua kutoka kwenye dimbwi hilo zito la mawazo.

“hapana hapana tafadhali sana naomba usimfanye chochote huyo mtoto nitakwambia nitakwambia tafadhali lakini nataka nikujue kwanza wewe ni nani?” waziri mkuu alionekana wazi kumpenda sana huyo mtoto wake hakuwa tayari kuona mtoto wake akifa wakati alikuwa na uwezo wa kumsaidia.

“Calvin Jackson Aron Mavunde” sauti hiyo nzito ilimfanya waziri mkuu atoe macho makubwa sana akiwa haamini muda wote alikuwa anaongea na mtu ambaye anamtafuta sana ili amuue na ndiye huyo aliye mbebea mtoto wake hakuwa na imani tena kama kutakuwa na usalama wowote ule.

“nipo nyuma ya mkurugenzi wa usalama wa taifa mr Kasisi Chacha” sauti ya kinyonge ya waziri mkuu iliweza kumshtua sana Luciana, alisikia vizuri sana wakati jina la mkubwa wake wa kazi likitajwa kwa usahihi kwani simu ilikuwa imewekwa laud speaker ila kwa Calvin hata hakushtuka kabisa, aliijua vizuri hulka ya wanadamu kuishi kwenye Ngozi ya kondoo ikiwa ni chui, usaliti upo kila sehemu hivyo hakuwahi kumwamini binadamu yeyote yule tangu siku wazazi wake wanapoteza maisha na kauli ya mzee wake ya kuto amini watu alikuwa akiiishi kwa usahihi sana.

“una uhakika na unacho kisema” aliuliza tena kwa msisitizo

“ndiyo ila tafadhali naomba usimfanye choch……” waziri mkuu kabla hajamaliza kuongea simu ilikuwa imekatwa, haraka sana aliwapigia watu wake waweze kuitafuta hiyo namba ya Calvin ilipo, alishangazwa na jibu alilopewa baada ya kuambiwa kwamba hiyo namba ilikuwa haipo kabisa na hakuna mtu alishawahi kuitumia hapa duniani, alichoka mzee huyu akiishia kutukana tu matusi.

Kwa Luciana ilikuwa ni ngumu sana kuamini kitu alichokuwa anakisikia hapo, alicheka kwa nguvu lakini kwa uchungu sana akitoa machozi.

“hili linawezekana vipi hapana hapanaaaaaa huyu mjinga kakudanganya ili tu mtoto wake awe salama” Luciana alipiga kelele nyingi sana asiamini kile kilichokuwa anakisikia.

“binadamu wengi huwa wanajifunza kupitia makosa yao lakini ukiona mtu anafanya kosa na bado anaendelea kulilinda kosa lake au kuendelea kulifanya ikiwa anajua ni kosa hiyo ni hatua kubwa sana ya ujinga kwenye maisha yake, wewe ni mwanamke ambaye kwa sasa ulitakiwa uwe kwako unalea familia yako kwa furaha lakini umeyaharibu maisha yako kwa kuwalinda watu wa aina kama hii wakiwa wanatenda maovu kila siku halafu leo unataka kuwakingia kifua tena kusema hawahusiki, unaishi kila siku na hawa watu mpaka uwakatalie? Wewe ni nani anajua kwamba una nyumba hizi hapa mjini? hata wenzako uliokuwa umeishi nao kwa zaidi ya miaka mitano hakuna hata mmoja anaye lijua hili. Siri ni kitu ambacho kimebeba uhalisia mkubwa sana wa maisha ya watu, kusingekuwa na siri kuna wanadamu hawakupaswa kabisa kuchangamana na hili kundi la viumbe dhaifu wa MUNGU wasio kuwa na hatia yoyote lakini wanauawa kila siku na hawa wauaji ndo umekuwa ukiwalinda kwa zaidi ya hiyo miaka yako mitano sasa hiyo jeuri ya kumtetea mtu aliye zaliwa na mama yake peke yake ambaye hata mama yake kuna mambo mengi tu hayajui kuhusu wewe mtu wa mbali ambaye mmejuana tu kwenye kazi hicho kiburi cha kusema hapana unakitolea wapi?, punguza ujinga kwa kuipata elimu ya bure ya mtaani ndio maana mipango yenu mingi huwa inafeli kwa kukurupuka kufanya maamuzi ya kipuuzi na kuwaamini amini watu hovyo, leo tu jioni umetoka kuwapoteza wenzako wanne bado unakazana tu hawa watu hawahusiki ebu nitokee hapa nisije nikakufanyia kitu kibaya bure” Calvin aliongea kwa sauti ya ukali akionekana wazi kuchukizwa na jibu la Luciana hata macho yake yalikuwa yamebadilika rangi alikuwa akichukia sana akitokea mtu kuwalinda hao watu ambao ndo wahusika wakuu wa mauaji ya familia yake na sasa hatimae alikuwa amemjua mtu ambaye alikuwa anatamani sana amfahamu kwa muda mrefu, Luciana ilimlazimu awe mpole japo kichwani alikuwa na mawazo mengi sana.

Mwanaume akaichukua simu yake na kutuma code mahali kisha akamwambia Luciana.

“jiandae tunatoka ndani ya dakika kumi, nadhani lazima utakuwa na gari hapa tunahitajika kulitumia Luciana alivaa zake ushungi na kuyaacha tu macho Calvin akiwa na nguo zake za kazi alimbeba mrembo huyo aliyekuwa bado yupo kwenye usingizi mzito, wakaelekea mpaka nje kuna sehemu palikuwa na tanki la maji Luciana akalisogeza pembeni na kubonyeza namba za siri mbele yao palipokuwa kama ukuta wa kawaida pakajifungua na huko ndani kulikuwa na gari nyingi sana walichangua Land Rover kitu kilicho mfanya Calvin atabasamu na kuona kweli huyo alikuwa mwanamke wa kazi sana, dereva alikuwa Luciana mwenyewe aliliondoa gari kwa kasi ya ajabu majira hayo ya saa tisa za usiku wakionekana wazi wanawahi mahali.

65 sina la ziada MUNGU akubariki sana

Chao[emoji2768]

Bux the story teller

#ULIMWENGUWAWATUWABAYA
Stay put sio muda sana nitakileta kipande cha 66 japo leo kama Simba angeshinda mngesoma viwili.....kimoja kinakuja

Wako

Bux the story teller
 
Back
Top Bottom