FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
- #181
kwa sababu ya kumuenzi Baba yetu wa taifa tuutumie muda wetu leo kupumzisha vichwa, unapumzishaje kichwa bila kupata burudani kutoka kwa Bux the story teller?HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA 60
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA....................
"Mmmmmhhhhhh aaghr" sauti nzito ya mtu akiguna ilimshtua sana Victor ikamlazimu kugeuka haraka sana ndipo aliposhangaa sana mtu aliyekuwa akimuona nyuma yake na huenda ndiye aliyefanya Marry kuongea kwa hasira sana hapo kitandani akiwa anatia huruma na kuzidisha machozi sana.
ENDELEA.....................
"Baba" Victor alipigwa na mshangao mkubwa baada ya kugundua aliyekuwa hapo ni Kasisi Chacha hata hivyo hakupewa jibu lolote lile mzee huyu alikuwa amemkazia macho Marry au Ester pale kitandani alipokuwa amelala.
"Huyu shetani ni baba yako?" swali la ukali kutoka kwa Ester lilimfanya Victor ageuke tena kumwangalia na kumpa mgongo Kasisi Chacha
"umeshapata ukichaa?mpaka ufike sehemu unamkosea mzee wangu mpaka umuite shetani hivi una akili kweli wewe mwanamke" Victor aliuliza akiwa amebadilika macho yake kwa muda huo hakujali kama mwanamke huyo alikuwa mjamzito kitendo cha kutukaniwa mtu aliye mlea ilikuwa ni dharau kubwa sana kwake, alijiandaa ili akampige hata kofi mwanamke huyo lakini Kasisi Chacha alimdaka mkono ikabidi atulie.
"muulize mwenyewe kanifanyia nini kwenye maisha yangu" alijibu kwa ukali Ester akiwa anatoa machozi mengi sana ilimbidi Victor ageuke na kumuuliza Kasisi Chacha
"Baba kuna kitu gani kimefanyika hapa katikati mpaka akuchukie sana kiasi hiki?" Victor alitegemea jibu zuri kutoka kwa huyu mzee lakini ilikuwa tofauti kabisa na alichokuwa anakifikiria.
"nimemuweka mbali na furaha ya maisha yake ndiyo maana alivyojua juzi amenichukia sana" sauti nzito ya Kasisi Chacha iliunguruma.
"kumuweka mbali na furaha yake kivipi" swali liliulizwa na Victor.
"ndio sababu siku ile nilikwambia kwamba umekurupuka sana kuishi na huyu mwanamke, hivi ushawahi hata siku moja kukaa ukajiuliza huyu mwanamke historia yake ipoje? au ulikimbilia tu kwa kuchanganyikiwa na uzuri wake?" Maneno mazito sana yalitamkwa yaliyo mfanya kidogo Victor ajione ni mjinga sana hakuwahi hata kufuatilia maisha ya mwanamke huyo ambayo aliyaishi kabla yeye hajakutana naye.
"yule mwanaume aliyekuja kwako ukapambana naye ni mumewe halali wa ndoa kabisa ndio maana amepata mshtuko mkubwa kiasi hicho" Victor mwili ulikosa nguvu kabisa ikamlazimu kukaa chini hata hizo nguvu za kusimama hakuwa nazo kwa muda huo, hakutamani anacho kisikia uwe ni uhalisia wa mambo, alitamani mtu mmoja aje na kumwambia alikuwa anataniwa tu, alikuwa amempenda mno mwanamke huyu na aliridhia kuishi naye kwa muda ambao MUNGU atambariki kuendelea kuliona jua hakutaka kuamini eti Ester ni mke halali kabisa wa mtu tena wamefunga ndoa, baada ya kutamka maneno hayo Kasisi Chacha alitoka humo ndani haraka sana akimuacha Ester anapiga kelele pale kitandani
"unewapeleka wapi wazazi wangu shetani mkubwa wewe, niletee familia yangu kwanini unanifanyia hivi" sauti za Ester Victor hata alikuwa hazisikii akiwa amekaa chin ya kitanda hicho alichokuwa amelazwa mwanamke aliye mbebea mtoto tumboni mwake, hakuona sababu ya kuendelea kubaki ndani humo akihisi amesalitiwa pakubwa sana hakutaka hata kuijua sababu mwanaume aling'ata meno yake kwa hasira sana akanyanyuka kwa nguvu na kuhitaji kuondoka humo ndani kwa hasira ila kabla hajafanya hivyo alidakwa mkono wake alipogeuka nyuma alimuona Ester akiwa anamtazama machozi yamemjaa usoni.
"Hivi ni kweli yule ni baba yako?" Ester aliuliza akiwa anajikaza tu lakini alikuwa na uchungu mkubwa sana kwenye moyo wake
“kama usingekuwa mjamzito kwa huu ujinga ulio ufanya ningekuua mimi mwenyewe kwa mkono wangu”Victor alitamka kwa hasira bila kujali chochote aliutoa mkono wake kwa nguvu sana na kuanza kutoka humo ndani.
“kwhiyo wewe na baba yako ndiyo mliokuwa nyuma ya haya yote” swali la Ester lilimfanya Victor kidogo asimame.
“unapaswa ulitamke kwa heshima sana jina la huyo mzee, bila yeye ningekuwa mtoto wa mtaani mpaka leo, amenichukua nikiwa bado mdogo sana sina sehemu yoyote ya kulala, sina chakula, hakuna mtu hata mmoja aliyeweza kunijali mimi ila yeye pekeyake aliliona hilo, akanipa elimu bora sana mpaka leo nimekuwa komando mkubwa sana wa kutegemewa ndani ya idara ya usalama wa taifa pamoja na nchi kwa ujumla leo unataka kuongea nini mwanamke mshenzi wewe. Umekuja kwenye maisha yangu kwa kujifanya unanipenda sana kumbe una ajenda zako mwenyewe, kwahiyo yule hawala wako ndiye aliyekutuma uje unipeleleze maisha yangu sio hahahahahah……. Sikujua kama wewe ni miongoni mwa wanawake washenzi sana kwenye hii dunia, sikuwahi kumpenda mtu yeyote yule umenifanya nikupende nilikuwa tayari hata kukupa dunia yangu yote na kila kitu kwenye maisha yangu kumbe naishi na nyoka ndani ambaye ni mke wa mtu tena komando aliye liasi taifa, inamaanisha nawewe uko nyuma ya hili, sitaki kujua kama wewe ni gaidi kama huyo bwana ako na sitaki kujua kama mlikuwa na mpango gani kwenye maisha yangu, nitakuacha hai ila hakikisha hatuji kuonana tena kwenye maisha yetu sitakusamehe tena kama leo liweke akilini hilo” Victor aliongea kwa uchungu mkubwa kupita kiasi akiwa kwenye majonzi mazito sana hata kuongea maneno makali hayo mbele ya huyo mwanamke aliye mpenda alikuwa akijikaza tui la ilikuwa inamuuma sana, alibamiza mlango kwa nguvu kubwa na kutoka humo ndani akisahau kwamba daktari alimshauri kama mwanamke huyo anahitaji uangalizi mkubwa mno.
Kwa Ester ni kama alitoneshwa kidonda kingine kipya kwenye moyo wake licha ya kugundua kama Victor haelewi chochote juu ya hilo na sio mtoto wa Kasisi Chacha lakini ukali wa maneno ambayo Victor alimtamkia ulimfanya ajisikie kama kuna mtu kamchoma na kisu kingine kipya kwenye moyo wake, alihisi amepoteza kila kitu kwenye maisha yake mpaka siku anampata Victor aliamini huyo ndiye familia yake atakayo ishi nayo kwa furaha baada ya kuteseka na upweke wa muda mrefu sana. akiwa kwenye simanzi nzito kwenye hicho kitanda kumbu kumbu zake zilienda mbali sana tangu yupo India alivyoweza kuishi na Roland ambaye alikuwa mwema sana kwake kiasi kwamba wakaingia mpaka kwenye bahari ya huba lakini safari hiyo ilikuja kuisha baada ya kurudi nchini Tanzania baada ya Roland kupotea ghafla bila kueleweka ameenda wapi lakini kiuhalisia kazi ya Roland ilikuwa ni kuhakikisha usalama wa binti huyu tangu yupo India mpaka anarudi Tanzania baada ya kulifanya hilo kwa usahihi alipewa maelekezo na mkuu wake Kasisi Chacha kwamba haruhusiwi tena kumuona mwanamke huyo kwenye maisha yake. Maisha yake yote Ester aliishi akijua mwanaume wake huyo ameshakufa kwahiyo alishtuka mno baada ya kumuona mwanaume huyo mbele ya macho yake, ilimnyima raha pakubwa sana ni jambo ambalo hakulitegemea kabisa kumtokea muda kama huo.
****************************************************
Calvin baada ya kutoka Temeke hakurudi moja kwa moja Kigamboni alihisi huenda kuna watu wanaweza kumfuatilia kirahisi sana na kwa huo muda alihitaji kupumzika, mwanaume aliingia ndani ya Kawe akatafuta hoteli moja majira hayo ya usiku wa manane akafanikiwa kuipata, alilala usingizi mzito sana mpaka alipokuja kushtuka asubuhi na mapema sana, akiwa anatoka kuoga alisikia mlango unagongwa akahisi huenda kuna watu wamemtembelea mapema sana akataka kuvaa haraka sana lakini alitulia baada ya kusikia sauti moja nzuri sana ya kike basi alifungua mlango taratibu akiwa amevaa taulo tu, kama alivyokuwa ametegemea alikuwa ni mhudumu akiwa amemletea supu moja nzito sana ikiwa ni utaratibu wao wa kila siku kwa kila mteja ambaye analala ndani ya hoteli yao. Alikaa na kuanza kupata supu yake taratibu bila hata wasi wasi wowote ule, supu iligeuka kuwa chungu baada ya kuiwasha televisheni iliyokuwa humo ndani, hakuamini kitu alichokuwa anakiona mbele yake ilikuwa ni taarifa ya habari ya asubuhi kabisa na mbele ya hiyo skrini alisimama mheshimiwa waziri mkuu pembeni zikiwa zimeambatanishwa picha zake yeye mwenyewe Calvin Jackson japo kwenye hizo picha hakuwa na ndevu ikionekana ni picha za muda kidogo.
“shiiiiiiiiiiit…….” Alitamka kwa hasira akibamiza chini bakuli la supu kwa hasira akitulia ili kumsikiliza mzee huyo kwa uchache japokuwa hakujua kama ndio anaanza au anamaliza.
“Calvin Jackson Aron Mavunde ndilo jina lake huyu mtoto, kwa sasa amefikisha miaka 25 na ana mvuto mkubwa sana ukimtazama machoni, huyu ni mtoto wa tajiri mmoja mkubwa sana ambaye kwa bahati mbaya miaka mitatu iliyopita aliweza kututoka baada ya kuvamiwa na kuuawa na watu wasio julikana, huyu mtoto alipotea ghafla sana baada ya mauaji ya wazazi wake zaidi ya miaka miwili sasa huu ni watatu. Tangu wazazi wake wamekufa tumefanya uchunguzi wa kina sana tumegundua kwamba yeye ndiye mhusika mkuu wa mauaji ya wazazi wake na alifanya hivyo ili aweze kumiliki mali za wazazi wake, kwa sababu alikuwa ni mjeuri sana kwenye familia yake ndipo baba yake alipogoma kumrithisha mali zake akaamua kuwaua ili abaki na mali hivyo akaamua kuwaua ili tu azichukue. Sio hilo tu inaonekana alienda kujipanga na kuungana na makundi makubwa ya kigaidi kwani baada ya kurudi alianza kuwatafuta maaskari na wanajeshi wetu ambao wanaijua siri yake hiyo na kuwaua kikatili sana, mpaka sasa maaskari na wanajeshi alio waua ni mia moja ikiwa ni pamoja na kuwabaka wanawake saba na kuwaua wote, tulifanikiwa kumkamata kwa mara ya kwanza na raisi alitangaza hadharani lakini magaidi wenzake walivamia msafara na kumtorosha.
Mimi kama waziri mkuu wa hii nchi iliyo barikiwa sana amani ninalaani na kukemea haya yaliyo tokea hivyo huyu mtu nahitaji vyombo vya dola kuanzia jeshi la polisi na jeshi la nchi wamtafute popote pale alipo na aweze kuuawa kikatili sana mbele ya hadhara ili kuweza kulinda usalama wan chi yetu kwani akiachwa hai itakuwa ni hatari kwa raia na mali zao, natoa rai kwa raia wema kwa yeyote atakaye saidia kutoa taarifa juu ya upatikanaji wa mtu huyu atazawadiwa pesa za kitanzania taslimu milioni miamoja, naomba tusaidiane sana kwenye kulilinda taifa lililotengenezwa kwa jasho na damu na waasisi wetu kwa kumteketeza huyu gaidi” hotuba fupi ya waziri mkuu ilimfanya Calvin apoteze nguvu ikamlazimu akae chini akiwa na machungu makubwa sana, inauma sana mtu anayekufanya unaishi kwa shida ndiye huyo anaye kwenda kuwatangazia watu kwa jeuri kabisa kwamba wewe ndiye mtu mwenye makosa na haufai hata kidogo kwenye jamii kiufupi waziri mkuu aliona kwake hiyo ni njia rahisi sana ya kumdhibiti huyu kijana ambaye alianza kuwa hatari kwake, alitamani aweze kuingia kwenye hiyo televisheni akutane na mzee huyo aliapa angemuua kikatili kuliko binadamu yeyote yule ambaye alishawahi kumuua kwenye maisha yake. Aliuma meno kwa hasira akipiga na kupasua meza kubwa ya kioo iliyokuwa mbele yake hapo, leo alikuwa amepewa kesi nzito sana ambayo hakuwahi hata kuifikiria kwenye maisha yake, aliwaza wananchi ambao ni zaidi ya milioni 40 watamtazamaje yeye, ingekuwa ni kuua tu wanajeshi sawa vipi kuhusu kubaka wanawake na kuwaua! Ilimuumiza kichwa sana bwana mdogo, kila mtu alimchukia kwa dakika moja tu pekee alichanganyikiwa Calvin roho ilimuuma sana, wakati akiwa hapo simu yake ya mkononi ilianza kuita ghafla na kwa fujo sana.
Hasira zilikuwa zimemjaa kwa kiasi kikubwa sana na asingeweza kuongea na mtu kwa huo muda, aliona hiyo sehemu haimfai tena kwa sababu kuna mhudumu aliye mletea supu alikuwa ameshamuona tayari japo hakuwa na uhakika kama alifanikiwa kumtambua sura yake ambayo kwa sasa ilikuwa na ndevu zilizokuwa zimechongwa kwa usahihi mkubwa mno. Alivaa nguo zake ambazo zilikuwa za kazi alichukua simu yake na kila kitu chake hata hakufunga hapo ndani alitoka kwa haraka kubwa mno. Wakati anatoka wahudumu wote walimshangaa kwani nguo alizokuwa amevaa sio mavazi ya Tanzania kabisa walikuwa wanaziona kwenye picha za maninja hususani kutoka ndani ya nchi ya Japan, ni nguo za kazi na mara nyingi huwa anazivaa majira ya usiku tu leo hii asubuhi na mapema kabisa alikuwa amezitinga kwenye mwili wake na hakuna aliyeweza kumtambua kabisa kwa sababu ya kofia kubwa iliyokuwa imeficha uso wake, panga lake kama kawaida lilikuwa mgongoni na star zake za kutosha zikiwa kiunoni japo ilikuwa ni ngumu sana kuziona. Alipanda kwenye gari na kutoka ndani hapo kwa spidi kubwa kitu kilicho washtua sana baadhi ya wateja ambao walikuwa wamewahi mahali hapo kwa ajili ya kupata huduma, wakati anaanza kuitafuta bara bara ya kwenda mwenge akiwa amepandisha mpaka juu vioo vyake vya gari alipishana na gari sita za jeshi zikiwa zinaelekea sehemu ya ile hoteli alikotokea akajua lazima yule dada ameshapiga simu hivyo alijua anatakiwa kuchukua tahadhari kubwa sana kwani sura yake inaonekana inajulikana vilivyo. Ni kweli zile gari sita zilikuwa zinaelekea kwenye ile hoteli, walifika pale na kumtafuta yule dada aliyeweza kuwapigia simu akawapeleka moja kwa moja kwenye chumba alichokuwepo Calvin, wakiwa na siraha kali za vita wanajeshi wapatao hamsini walishangaa mlango huo uko wazi, waliingia haraka na kutafuta kila sehemu mpaka bafuni lakini hakukuwa na mtu. Kiongozi wa msafara alivyo angalia chini alilishika bakuli lile la supu na kuona bado la moto kabisa alitamka kwa jazba
“pumbavu huyu kaondoka sio muda na atakuwa hajafika mbali, ebu tuonyeshe chumba cha kamera hapa haraka sana” alikuwa anaongea kwa sauti kali ya mamlaka mwanaume huyu iliyo anza kumuogopesha mpaka huyu mhudumu aliye waita hapa. hawa walikuja na gari za jeshi lakini kiuhalisia walikuwa ni makomando kabisa wa siri waliokuwa chini ya mkuu wa majeshi, kwa aina ya mtu waliyekuwa wanamtafuta walijua kama wakienda wanajeshi basi watakufa wengi sana ikawalazimu kuweza kuwatumia makomando kabisa ikiwa ni ombi la waziri mkuu huyo kwa mkuu wa majeshi baada ya kudai anahitaji kuilinda amani ya nchi ili waweze kumaliza kazi mapema sana. waliingia kwenye chumba cha kamera na kurudisha dakika kadhaa nyuma kweli wakaona kuna mtu ana mavazi meusi anatoka humo ndani.
“tuondoke haraka sana humu ndani huyu ni yeye ametoka sio muda mrefu sana” alitamka huyo kiongozi ambaye hakuonyesha hata sura ya masiara huku akimrushia mhudumu huyo maburungutu mengi sana ya pesa kwa sababu alitoa taarifa ambazo ni sahihi kabisa na walijua wazi watampata tu na kama wakimkamata basi mwanamke huyo angetefutwa kupewa pesa yake nyingine alifurahia mno kupata pesa nyingi kiasi hicho na hakuona haja ya kuendelea kufanya hiyo kazi ya hotelini mkononi akiwa na milioni thelathini alizopewa hapa bila kujua kwamba kamsababishia matatizo makubwa sana kijana wa watu ambaye hana hatia yoyote ile, gari za jeshi zilitoka kwa spidi hapo iliwatisha baadhi ya watu wakaanza kuondoka kwenye hiyo hoteli baada ya kuamini hapakuwa na usalama wa kutosha.
Unadhani Calvin anatokaje kwenye hili? atapona vipi ikiwa kila chombo cha usalama kinamtafuta na kila mwananchi alimchukia sana kwa aina ya kesi aliyokuwa amepewa? nini hatima ya kijana huyu asiyekuwa na hatia yoyote ile?
60 inafika tamati panapo majaaliwa ungana namimi tena wakati ujao
Chao[emoji2768]
Bux the story teller
#ULIMWENGUWAWATUWABAYA
Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Basi njoo na 1500 yako tu pekee uweze kuimalizia ULIMWENGU WA WATU WABAYA mpaka mwisho kabisa.
Hivyo usijisikie unyonge kukaa mwenyewe nyumbani siku ya leo wakati Bux the story teller yupo kwa ajili yako.
0621567672 (WhatsApp)
0745982347
lipia kwa hizo namba jina FEBIANI BABUYA.
Unapewa hadithi muda huo huo ili siku yako iishe vyema ukiupa ubongo burudani ya madini ya kutosha
Bux the story teller