Hadithi: Ulimwengu wa Watu Wabaya

Hadithi: Ulimwengu wa Watu Wabaya

HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 24

SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA.............

Chamwisho anahitaji kuonana nawewe mkuu siku ya leo majira ya saa saba kasoro dakika tano za usiku pale kwenye daraja la Tanzanite na kasisitiza kwamba ana mazungumzo ya amani nawewe kwahiyo usiende pale kwa nia mbaya ana jambo la mhimu sana la kuongea nawewe na uende pekeako.” Victor alikuwa mehitimisha maelezo yake.

ENDELEA................

“mpuuzi sana huyu hivi anahisi mkuu ni mtu rahisi sana kukutana nae sio, huyu jamaa ni nani hasa mpaka ajikute anataka kutupangia vitu vya kufanya nadhani ndio nafasi yetu ya pekee ya kwenda kumkamata” Alex aliongea kwa jazba mno akionekana kuwa na hamu ya kukutana na mtu huyo ambaye alikuwa anaishia kusimuliwa tu kuhusu habari zake hapa mjini.

“nitaenda, nadhani atakuwa na mazungumzo ya muhmu sana namimi japo ni jambo la hatari mno kwani sijajua ana nia gani bado alafu ni mtu ambaye yupo kwenye uangalizi mzito wa kumkamata, alafu nikiunganisha na hayo matukio ambayo unasema watu walikuvamia hiyo inamaanisha ushaanza kujulikana, ni uzembe mkubwa sana umefanyika hata hivi unatakiwa kule uhame mapema sana naona hili jambo lina uzito mkubwa ambao mpaka sasa nashindwa kuuelewa” mzee Kasisi aliamua kukubali kukutana na mtu huyo huku akiwa na mawazo sana moyoni mwake kwani hakujua lengo hasa la mtu huyo kuhitaji kuonana na nayeye moja kwa moja ambaye ndo mkuu wa idara ya usalama wa taifa ni lipi.

“mzee sio kirahisi hivyo, wewe ni mtu mkubwa sana nchini na sio kila mtu anaweza kukuona kama watu wa kawaida isitoshe mtu mwenyewe anatumia mabavu kukuita, tunaweza kuitumia hiyo nafasi kumkamata na kama akifika kwenye mikono yetu atasema yote hawezi kuvumilia mateso ya hapa” Alex aliongeza huku akionekana kama ni mtu anae fanya maamuzi kwa kukurupuka sana na kwa kutumia mihemko mikubwa mno

“kwenye kirefu cha taasisi yetu kuna neno intelligence (akili) lina maana kubwa sana hilo neno, unapokuwa usalama wa taifa maana yake wewe ndiye mtu ambaye unatakiwa kuhakikisha nchi yako inakuwa salama pamoja na raia wake wote kwa gharama na kwa namna yoyote ile kwahiyo sio kila muda inahitajika nguvu sana, akili ndio kila kitu kwenye hizi kazi. Angekuwa na shida ya kunilazimisha kuonana nae kwa lazima kwa sababu tayari alikuwa na Victor angeweza kumtumia yeye kama ngao, lakini mpaka kaamua kuamua kuzungumza namimi kistaarabu sina haja ya kumkatalia nitaenda nione anataka nini ili kama ni mhimu kwa taifa naweza nikafanya nae makubaliano ila kama itakuwa ni kulichafua taifa langu basi ataishia pabaya sana na nitamuua mwenyewe” Mzee kasisi aliamua kumjibu Alex kwa kumpa somo kwanza kwamba sio kila muda awe anatumia nguvu tu kuna muda anahitajika kutumia akili zaidi.

“sawa mzee” Alex alijibu lakini tayari akiwa na mipango yake kichwani, hakuridhika kabisa kumwacha mkuu wake huyo aende eneo hilo peke yake kwahiyo moyoni mwake alikuwa amepanga siku hiyo awahi kabla mkuu wake hajafika ili akamuadabishe mtu huyo ikiwezekana amuweke mikononi mwao ili wakamhoji lakini hakujua kama anafanya kitu cha hatari sana ambacho kilikuwa na uwezo wa kumsababishia matatizo makubwa mno.

Miongoni mwa mitaa maarufu sana hapa ndani ya jiji la Dar es salaam, ukiacha kwa umaarufu wake wa uuzaji sana wa ndizi na kuchangamka sana kwa biashara ndogo ndogo za kuingiza mia mia,pia ni mtaa ambao unaogopwa sana inapofika majira ya usiku kwani umejaa watu wanao pendelea sana kuishi kwa kutumia baadhi ya jasho la wanyonge wasio kuwa na mabavu hasa pale wanapo kutana nao majira ya usiku, ni mitaa ya Tandika sokoni katika wilaya ya Temeke ambayo ni maarufu sana kutokana na historia yake lakini pia kwa kuwa na uwanja ambao ndilo jicho la burudani kwa watanzania wengi sana wapenda tasinia ya michezo ya mpira wa miguu, hapa nauzungumzia uwanja maarufu zaidi nchini uwanja wa taifa ufahamikao kama uwanja wa Mkapa ikiwa ni kama heshima kwa marehemu raisi wa awamu ya tatu ya nchi yetu MH Benjamin William Mkapa au LUPASO ambayo ni sehemu aliyo kuwa anatoka mheshimiwa huyu (MUNGU amlaze mahali pema mzee huyu, amin). Ndani ya mitaa hiyo majira ya saa kumi na mbili za jioni kuna gari aina ya BMW X6 kioo cha gari kinashushwa anaonekana mwanaume wa kazi Scot ambaye ni mkono wa kulia wa mzee Fabian Decco. Haikufahamika mida hii alikuwa anatafuta kitu gani hasa ndani ya mitaa hiyo ya uswahilini na gari kali sana namna hiyo ambalo kila aliye fanikiwa kuliona alikuwa analiangalia kwa matamanio makubwa sana akimuonea wivu mmiliki wa gari hilo.

Alionekana akishuka na kuvaa kofia yake vyema akaongeza na miwani yake myeusi na kumfanya kuwa na mwonekano bomba zaidi. Mwanaume alizuga zuga kwenye duka moja akipata maji baridi huku akimuwinda mtu mmoja ambae kwake alihisi atakuwa na msaada mkubwa sana kwani alihisi mtu huyo kuna mambo atakuwa anayajua kuhusiana na kinacho endelea mjini hapa au kiasi fulani angesaidia kumwelekeza ni wapi alipokuwa Tomaso pamoja na Thomas kwani wamepotea bila taarifa yoyote.

Mtu aliyekuwa amemfuata mahali hapo alikuwa anaitwa Jarome Tenga, alifahamika kama Tenga kwa sababu alikuwa ni mtu ambae alipenda sana kuuza matenga ya kubebea ndizi na nyanya na alikuwa dalali wa vitu hivyo. Scot alimtafuta huyu jamaa mahali hapa kwa sababu huyu amesoma shule moja na Tomaso (mr makomputa) na kuna muda Scot alishawahi kumkuta wapo na Tomaso ndipo alipo tambulishwa kuhusu Jarome Tenga japo Jarome alikuwa anapotea potea mara kadhaa mjini kutokana na kutafutwa sana na jeshi la polisi kwani alikuwa ni mtu anaye jihusisha na uporaji sana pamoja na magenge ya kihalifu hapa mjini. Aliweza kutengana na Tomaso kwa sababu aliwahi kufanya mapenzi na mwanamke wa Tomaso kitu kilicho pelekea ugomvi mkubwa sana kati yao ndipo Jarome Tenga alipo amua kujiingiza kwenye mitaa ya Tandika ili aweze kuchanga upya karata za maisha yake kwa sasa kwani umri ulikuwa unazidi kwenda na alikuwa hajafanya kitu chochote kile cha maana kwenye maisha yake.

Upande wa Scot alizihitaji taarifa za muhimu kutoka kwa mtu huyo ili ziweze kumsaidia kwenye harakati zake za kumtafuta mtu ambaye amekuwa tishio sana kwao kuanzia kuwaua wale wanajeshi kimara pamoja na kuweza kumuua Brown mtu wa Kongo huyu baada ya kumvamia Victor na mtu huyo akaweza kuingilia kati, alihitaji kumjua hasa mtu gani anaeweza kuua kwa upanga kikatili sana namna hiyo lakini ilikuwa ni ngumu sana kuweza kumpata mwanadamu huyo ambaye naye kwa upande wake alikuwa na hamu kubwa sana ya kukutana na Scot ambaye ndiye muuaji halisi kabisa wa wazazi wake miaka miwili iliyo weza kupita huko nyuma.

Ilivyo fika majira ya saa mbili za usiku alikuwa ashamuona mtu wake tayari ndani ya mitaa hiyo akiwa tayari ameshafunga biashara yake na wakati huo alikuwa anajichanganya kwenye mitaa ya kucheza kamali kama ilivyo kuwa kawaida yake majira ya usiku anapokuwa ametoka kuingiza kiinua mgongo, bahati mbaya sana chote kilikuwa kinaishia kwenye kamali. Katika uchochoro mmoja wakati Jarome anakatiza alihisi kama kwa mbele kuna mtu alikuwa akija upande wake aliopo, alijaribu kuangalia mbele na nyuma na kwenye pembe zote hakufanikiwa kuona chochote zaidi ya huyo mtu mmoja ambaye alikuwa akizidi kusogea upande wake. Alitaka kukimbia kwani alijua kwa matukio aliyo kuwa anayafanya jijini hapa lazima ni watu walikuwa wakimtafuta lakini alisita baada ya kusikia bastola inakokiwa huku sauti nzito mno ikimsihi akijaribu kunyanyua hata mguu wake tu basi alikuwa anavunjwa kiuno hali iliyo mfanya ashindwe kufanya chochote zaidi ya kuamua kutulia tu.

“mbona unanikimbia?” Scot alimwuliza huku akizidi kumsogelea

“sikujui alafu ni usiku saivi unaniulizaje nakukimbia wakati mtu mwenyewe haujaja kwa wema?” Jarome alikuwa anaongea huku akizidi kumsoma mtu huyo kwani naye hakuwa mnyonge kabisa linapokuja suala la mapigano.

“umejuaje kama nimekuja kwa shali? Kwani unanijua au kuna kitu umenikosea?” Scot aliuliza kwa mara nyingine tena wakati huu akiwa amesimama

“nina mambo mengi ya kufanya ebu nambie wewe ni nani na kwangu unahitaji nini?” Jarome aliuliza akiwa hana hata tone la wasi wasi

“unaonekana unajiamini sana kijana, haina haja ya kunifahamu tunaweza tukakutana siku nyingine usinijue naishi kwenye sura nyingi hata hivi ikitokea ukanijua sitaweza kukuacha hai, ila ni kwamba kuna siku nishawahi kukukuta kwa Tomaso ni muda kidogo ndipo alipo nitambulishaga wewe hapo kama rafiki yake na mitaa yako ya Tandika sokoni hapa ambapo ndipo huwa unapenda sana kuja kujificha hasa ukisha fanya matukio yako huko, nilivutiwa na stori yako kwa namna unavyo fanya kazi zako niliona kama ni kijana unae unaweza kunifaa kwenye kazi zangu lakini nikagundua itakuwa ni hatari sana kwa sababu unafuatiliwa sana na mamlaka za serikali kwahiyo nikaamua kuachana nawewe. Leo hii nipo hapa kwa sababu Tomaso amepotea na Thomas ambaye ni mlinzi wake ghafla sana bila taarifa yoyote alafu ukizingatia hapa mjini ameibuka muuaji mpya ambaye mpaka sasa ameniulia vijana wangu wengi sana, najua unamjua vizuri Tomaso kwani ni rafiki yako wa muda mrefu sana hivyo nahitaji unipe taarifa zake sehemu ninayo weza kumpata kwani lazima atakuwa anajua chochote kwa haya yanayo endelea hapa mjini” Scot aliongeza lakini wakati huu alikuwa amesha iweka siraha yake kiunoni hali iliyo mpa ahueni Jarome.

“unapaswa uelewe kwamba mimi sio mtoa taarifa wa mkoa kwamba ukijisikia kuja kwangu unakuja kama unaenda kwa mkeo, huyo fala unaye mtaja hanihusu na wala sina muda wa kupoteza kuongea na mtu kama wewe ambaye hata sikujui, acha kushobokea watu mjini hapa utaolewa na usinitishe kwamba unaweza kuniua kirahisi hivyo kama unaenda kufuata samaki feri jiangalie sana” Jarome aliongea kwa jeuri huku akidhani anaweza kummudu mtu huyo kwa hali yoyote ile

“hayo maneno unaniambia ni mimi au kuna kitu unakumbuka kichwani ndio maana umeropoka bwana mdogo?” Scot aliuliza akiwa haamini mtoto mdogo kama huyu anapata wapi ujasiri wa kumjibu kwa dharau sana namna hiyo.

“kwahiyo unaona hapa naongea na mti, fala wewe acha kutuchanganya watu na mitaa yetu hapa ntakuzingua sasa hivi na hakuna kitu utafanya” Jarome alivyo maliza tu ,maneno yake alishtukia anapokea teke moja la kifuani lililo mpeleka mbali na mahali hapo alikuwa amemchokoza mtu mmoja hatari na katili sana bila yeye mwenyewe kuelewa. Alijaribu kurusha ngumi lakini alikuwa kama mtoto mdogo mbele ya mwanaume huyu, Scot hakuchelewa sana akatoa bastola yake na kumpiga Jarome risasi ya kichwa kwani aliona kabisa mtu huyo hana msaada wowote ule kwake. Baada ya hapo alimpigia simu bosi wake mr Decco na kumwambia hataweza kulala mpaka ahakikishe kwa muda mfupi tu anakamilisha kazi kisha akaondoka na gari yake ya kifahari ndani ya mitaa hiyo maeneo ya Tandika hapo akiwa kaacha maafa tayari.

Majira ya saa saba kasoro dakika kumi za usiku maeneo ya daraja bora sana na la kisasa ambalo ni alama nzuri sana ya nchi yetu liitwalo TANZANITE anaonekana Alex jasusi huyu kutoka usalama wa taifa akiwa emejibanza sehemu akiangaza huku na huku kama atamwona mtu yeyote, aliwahi mahali hapo kufuatia kutimiza ahadi yake ya kumkamata mtu ambaye alikuwa anahitaji kuonana na mkuu wake wa kazi kwani alihofia mtu huyo alikuwa na uwezo wa kumdhuru mtu ambaye ni muhimu sana kwa taifa hili ambaye ni mkurugenzi wa usalama wa taifa mzee Kasisi Chacha. Akiwa maeneo hayo alishtuka baada ya kusikia sauti moja nzito mno ila yenye utulivu mkubwa ikimsemesha.

“ulikuwa una shida namimi?” alikuwa ni tajiri Calvin Jackson akiuliza bila papara yoyote

“kumbe ndo wewe aisee, sijaamini nilijua ni bonge la jitu la kutisha” alex aliuliza kwa furaha mno akidhani ashampata mtu huyo tayari

“ulikuwa unanitafuta sana?” Calvin alimuuliza huku akitabasamu

“nimekutafuta sana na nilishangaa ni mtu gani huyu mwenye ujasiri wa kufanya ukatili wa namna hii bila kuogopa uwepo wa sheria”

“sijaja hapa kwa ajili yako usitake kunipotezea muda, najua wewe ni mtu wa usalama na uko hapa kuhakikisha ulinzi wa mkubwa wako wa kazi kwa hilo nakupongeza sana kwani unaonekana ni mtu unaye ijua vyema kazi yako ila kuna muda unaonekana ni mtu mkurupukaji sana na hii inaweza kuja kukufanya ukaishia sehemu mbaya sana kwahiyo nakuhitaji uondoke hapa kwani kama nilikuwa na ubaya na kiongozi wako nisinge hitaji kuongea nae kwa amani ningemtafuta mwenyewe, nadhani mkuu wako atakuwa hapa muda wowote kuanzia sasa kwahiyo ondoka haraka kama hakuna kilicho tokea” Calvin awamu hii aliongea akiwa yupo serious kidogo

“unadhani unaweza kunishawishi kwa maneno yako ya kipuuzi kama hayo mhalifu mkubwa kama wewe ambaye nilikuwa nakutafuta kwa hamu kubwa mno”. Alex aliongea wakati huo alikuwa anamfuata Calvin kwa kasi sana na kurusha ngumi mbili ambazo zilimpata Calvin tumboni na kifuani lakini alikuwa amesimama vile vile bila kutikisika, Alex akaamua kuongeza teke moja sana ambalo alijibetu na kumkita nalo Calvin maeneo ya shingo kiasi kwamba angekuwa mwenzangu namimi hiyo shingo alikuwa inavunjwa lakini mwanaume alikuwa amesimama tu akimtazama Alex wakati huo Alex alikuwa anahisi amepiga mti.

“kama una familia inayo kutegemea ni vyema ukautumia muda wako kukaa nao vyema kwa kipindi hiki ambacho umebarikiwa kuwa hai na viungo vyako vyote mwilini vinafanya kazi kwa usahihi na kama huna ni bora utafute mke ili siku ukipotea kwenye uso wa dunia uache hata alama ya kwamba uliwahi kuishi kwa kuacha watoto kuliko kupoteza muda wako kutaka mashindano na watu ambao hata huwajui kabisa itakuletea matatizo makubwa sana. Aina ya hizo ngumi pamoja na mateke uliyo nipiga ningesema nikupige mimi mpaka sasa navyo zungumza jina lako lingekuwa limeshabadilika na kuwa marehemu kwahiyo jiangalie sana na siitaki sura yako tena mbele yangu”. Calvin aliongea kistaarabu sana kama kawaida yake huku akiangalia saa yake ilikuwa imebaki dakika moja tui li muda ufike ambao alimtaka mzee huyo aweze kufika mahali hapo. Lakini Alex alikuwa mbishi mno aliamua kuja kwa mara nyingine tena kujaribu bahati yake lakini kabla hajafika Calvin alikuwa amefika alimpiga ngumi moja tumboni iliyo mfanya Alex atapike damu mara tatu mfululizo akiwa ameegemea moja ya chuma pembezoni mwa daraja hilo.

“nimeomba mazungumzo ya amani na bosi wako ndiyo sababu ntakuacha hai ili asije akanifikiria vibaya lakini vinginevyo nilitakiwa kukuua huwa spendi watu ambao sio waelewa kama wewe, ikitokea tukakutana siku nyingine ulimi wako utakuwahisha huko unako taka kwenda” wakati huu Calvin aliongea akiwa tayari macho yake yamekuwa mekundu. Alivyo maliza tu kuongea aliona kwa mbali taa za gari zikiwa zinakuja upande wake ilimlazimu kusimama kati kati ili mtu huyo aweze kumuona vizuri na ni kweli alikuwa ni mzee Kasisi Chacha, alishangaa sana kumuona Alex maeneo hayo ambapo alimpiga jicho kali sana kitu kilicho mpelekea Alex kuondoka haraka sana huku akiwa bado anatoka damu mdomoni.
Kuna nini Calvin anahitaji kuongea na mzee huyu? Ndo kwamba amekubali yaishe aiachie sheria ifanye kazi yake? nini hatima ya maisha yake ya kisasi?.....ndo kwanza ukurasa wa 24 unafika mwisho MUNGU akubariki tukutane wakati mwingine tena

Chao

Bux the story teller

#ULIMWENGUWAWATUWABAYAView attachment 2320943
Asante sana mkuu
 
Kusoma hadithi ya ULIMWENGU WA WATU WABAYA kwa sasa ni shilingi 4000 mpaka mwisho kabisa mwisho ni 76

Nicheki WhatsApp 0621567672

Kawaida 0745982347

kwa ambaye atahitaji PDF ambayo ina mwanzo mpaka mwisho ni shilingi 5000 za kitanzania.

Namba za malipo

0621567672
0745982347
Jina FEBIANI BABUYA zote mbili.....hakiki jina kabla ya kutuma, ukituma tu njoo moja kwa moja muda huo huo nakupatia unaenjoy

Karibuni sana[emoji3578][emoji1666]
JamiiForums1035128080.jpg
 
Kama uliwahi kuangalia move ya Ninja Assassin basi yule star wa move ni Calvin.mimi nimesoma yote hii hadithi ni Kali mnooooo,,mcheki mtunzi akutumie
 
Haina shukrani kwangu,,Mimi nabidi nikushukuru wewe kwa kuniuzia seleas nzuri kwa bei nyepes na Kali yote humu tangu nijiunge jamii mwaka 2011,,iliyofatia ya paniela,,komando zed wimba na jasus honda
I appreciate this buddy.......kuna mizigo mikali sana inakuja [emoji3578][emoji109]

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 26

SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA.............

Aliamua kuagiza kinywaji huku akiendelea kuangaza huku na huko kama anaweza kumuona mtu wake lakini hakuweza kumwona, ilipita nusu saa nzima bila kuona chochote akiwa anakaribia kuachana na hilo jambo akaona mtu yule akiwa anatoka na wanaume wenye miili mikubwa sana ya mazoezi kama sita hivi, akainama ili asijulikane kama ni yeye, aliwaangalia kwa umakini sana na kuwaona kuna picha mtu yule akiwa anawaonyesha wale wanaume huku akionekana kuwasisitiza sana juu ya picha hiyo mpaka pale walipoweza kutoka nje ya club hiyo.

ENDELEA...................

Aliamua kumuulizia mhudumu kuhusu wale watu, alijibiwa ni watu ambao muda mwingi huwa wanakuwa pale na ni watu hatari sana wanao ogopeka mno kwenye mji huo wa mbinga, Calvin akatabasamu baada ya kujua atawapata muda wowote, aliondoka mahali hapo mpaka ilivyo fika majira ya saa mbili za usiku ndipo alipo rudi tena na kwa sasa alikuwa amerudi kufanya kazi mwanaume. Alichagua meza moja ambayo ilikuwa ipo maeneo yenye giza giza kidogo kwa wakati huo lakini alishtuka anaguswa bega lake, akatabasamu baada ya kuona kuna mrembo anajipitisha pitisha mbele yake, haikumpa tabu kuelewa kwamba mwanamke huyo ni utafutaji ndo unamfanya kuwa hivyo, alikuwa anawaheshimu wanawake kupita kiasi kijana huyu aliamua kutoa kibunda cha pesa na kumpa mwanamke huyo huku akimsihi akazitumie kufanya biashara na aachane na hicho anacho kifanya kwani kinampotezea sifa ya kuwa mwanamke bora, mwanamke huyo alishukuru huku akilia kwani hakutegemea kama kuna watu wenye roho nzuri kiasi hicho wanao endelea kuishi juu ya uso wa dunia, vijana wengi ukiwa na uhitaji wa pesa kama ni mwanamke hasa maeneo ya mjini lazima wangetaka kubadilishana na mapenzi kwa mwanamke kwani ilishageuzwa kuwa biashara lakini ilikuwa tofauti, bibie aliondoka kwa kukimbia huku akiwa na furaha sana.

calvin alikuwa anaendelea kuangaza macho huku na huko kwenye meza ya ng’ambo yake aliweza kumuona mtu wake akiwa amezungukwa na wanawake watatu wakimpa burudani, alimsubiri atoke mahali pale ili akazungumze naye kinaga ubaga, hazikupita hata dakika tano yule jamaa alitoa simu mfukoni ikionyesha kuwa inaita kisha akatoka nayo nje haraka sana wakati huo Calvin alikuwa akimfuatilia taratibu, safari ya mtu huyo iliishia nje kwenye parking ya magari, aliongea na simu mtu yule kisha akawa anaondoka mahali hapo kuelekea pembezoni kidogo mwa mji, Calvin alikuwa akiendelea kumfatilia taratibu ila wakati wanakatiza kwenye kona moja alichukuliwa mtama bila kujua huyo aliye mvamia katokea wapi kwani alikuwa ameiweka akili yake kwa yule mtu wa mbele yake ili asiweze kumpoteza.

“nimekuona tangu unaingia pale club, nashukuru umejileta wewe wenyewe kwani tangu asubuhi nilivyo kuona tu nilikuwa nakutafuta sana bahati mbaya nikawa nimekukosa” yule kijana ambaye Calvin alikuwa akimfuatilia alikuwa amesimama akimuelezea vyema kwamba ujio wake pale ulikuwa umejulikana mapema sana, Calvin alicheka sana baada ya kugundua aliingia mahali pale kizembe mno kiasi cha kujulikana haraka, aliwachukulia watu hao ni wazembe mno kumbe yeye ndiye aliye kuwa mzembe kwa siku hiyo.

“nilijiuliza sana mpaka ukawa unaniangalia kwa wasi wasi kiasi kile lazima utakuwa unanijua, mimi mwenyewe nilikuwa nina hamu kubwa sana ya kuongea nawewe, unaweza kuwaambia hawa watu wako watupishe ili tufanye mazungumzo unieleze kwanini ulikuwa ukinikimbia asubuhi yote ile na kwanini uwe na wasi wasi sana baada ya kuniona mimi” Calvin alikuwa anaongea wakati huo akiwa analikunja shati lake.

“hahahhaha unataka uongee na nani?, naskia wewe ndiye uliye bahatika kuendelea kuishi baada ya familia yako kupotezwa huko jijini Dar es salaam, sina taarifa zako nyingi sana lakini picha yako ninayo na ilishasambazwa sana, kuna watu walikuwa wanakusubiri ujitokeze ili wakugombanie kama pesa kwani inadaiwa kuendelea kuishi kwako unakwamisha mambo mengi ya wakubwa, utofauti wa kwenye picha na ulivyo ni ndevu tu basi, picha niliyo nayo hauna ndevu na ilichukuliwa mtandaoni, asubuhi nilikuwa nakuangalia vyema ili niweze kujua kama nakufananisha au ndiye mwenyewe lakini nilijipa uhakika kwamba ni wewe baada ya kukutazama vyema na ni lazima ufe haraka sana ili tulipwe pesa zetu vizuri” aliongeza yule kijana

“kwahiyo mkilipwa pesa mpo tayari kupoteza maisha ya watu ambao hata hawajawakosea chochote?” Calvin aliuliza akiwa amechukia sana kwanini vijana wadogo kama hawa wenye nguvu za kutosha kabisa wasitafute pesa kwa njia za halali mpaka wanaamua kujiingiza kwenye shughuli za mauaji ya watu wasio na hatia na kuishia kupewa pesa za pombe tu kutoka kwa watu wanao jali maslahi yao tu na kuyachukulia kiwepesi sana maisha ya watu wengine.

“ndugu yangu pesa imebadilisha taswira halisi ya ulimwengu, pesa imekuwa hazina kubwa ya ulimwengu, pesa inaweza kukifanya chochote kile ndiyo sababu unasikia vita haviishi kila siku duniani huko, watu wanapigania uchumi wao, watu wanalinda maslahi yao, bila pesa anakujali nani ndugu yangu, umaskini unazalilisha sana, inapotokea nafasi ya kupoteza nafsi za watu ili kuingiza pesa basi sisi wengine huwa hatujishauri mara mbili hata watu mia moja tunawaua tu ili tupate pesa ndiyo sababu ukienda sehemu za mijini dada zetu wanajirahisisha sana yote kwa sababu ya pesa, pesa ni haramu sana siku hizi huku aliye igundua akiwa zake kaburini hata haimsumbui” yule kijana alijibu kwa kijiamini sana huku akiwasha sigara yake kana kwamba alichokuwa anakifanya kilikuwa ni sahihi sana.

“leo nataka nikufunze ili ujue pesa haina umuhimu kuzidi maisha ya watu, pesa ni mhimu sana lakini hautakiwi kuipata kwa kuyatoa maisha ya mtu mwingine hiyo ni hatari mno pale inapo kurudia upande wako, maisha ya mtu yana thamani kubwa sana na hili binadamu wengi huwa wanalielewa pale wanapokuwa wanaivuta pumzi ya mwisho wakiwa hawana namna ya kuishi tena zaidi ya kuzipigania pumzi zao za mwisho, ndio muda ambao utaelewa kwamba uhai una thamani kuliko hata hizo pesa unazo zinadi kwa kuzipa sifa nyingi mno na hili unaenda kulithibitisha hapa leo, najua unanifahamu ndio maana una picha zangu na unahitaji kuyatoa maisha yangu, naomba unipe maelekezo Samson Nelson yuko wapi hapa mbinga?” Saa hii mwanaume alikuwa amebadilika kidogo

“mawazo yangu yalikuwa sahihi kukufananisha asubuhi mtu sahihi kabisa, sijajua umejuaje kama huyo mtu yupo huku ila umefanya kosa kubwa sana kwani huyo mtu usidhani unaweza kumpata na hapa mjini huwezi kutoka ukiwa hai nakuua mimi mwenyewe” alijigamba mno yule kijana kwa sababu alikuwa na wanaume sita walio mzunguka mahali pale. Alirudi nyuma hatua kadhaa kuwapisha vijana wake waweze kuifanya kazi mara moja. Wakwanza alikuja kwa pupa sana alipigwa ngumi moja maeneo ya kwenye moyo alibaki ameganda kama sanamu kwani moyo wake uliacha kufanya kazi kwa muda baada ya kupigwa na ngumi yenye uzito wake unao jitosheleza, Calvin aliskitika sana alijua ni watu wa mapigano kumbe alikuwa ameletewa watu wa gym ambao wengi wao mjini saivi chipsi ndicho chakula chao kikuu,hakutaka kuua viumbe dhaifu sana kama hao

“ondokeni hapa haraka sana kabla sijabadilisha maamuzi siwezi kupigana na viumbe dhaifu sana namna hii, aliongea hivi kwa sababu alijua wale vijana sita hawakuwa na hatia yeye alikuwa na shida na huyu mmoja anaye mjua vizuri lakini wale wanaume waliona kama dharau kubwa sana waliamua kumfuata wote, kilicho fanyika hapo Calvin aliamua kuanza kuwatengua kila mmoja ili wasifanye chochote kwani aliona atawaua bure, dakika mbili wale watu walikuwa hawajiwezi kwa chochote, aliona hiyo isingewafanya kuacha waliyokuwa wanayafanya, aliamua kukata mkono wa kila mmoja kati yao ili ziwe alama za maisha yao wanavyokuwa wanataka kufanya ukatili kwa watu wengine wawe wanajiwazia wao kwanza, alikata mkono ,mmoja mmoja kwa kila mwanaume kati ya wale sita kisha yule aliyekuwa amempiga kwenye moyo alimuongeza ngumi nyingine na kuwaambia huyo atashtuka baada ya masaa 24 lakini hakuweza kuuacha mkono wa kulia wa mtu huyo alipita nao kwa upanga wake akiacha vilio kwa wale wanaume walio kuwa wanalia kama Watoto wadogo.

“samson yuko wapi?” aliamua kumuuliza tena kijana yule ambaye ujeuri wote ulikuwa umeisha kwani wakati huo nguvu zilikuwa zimemuishia alikuwa amedondoka chini akitetemeka kwa uoga, hakuwahi kufikiria kwamba hii dunia ina aina ya watu makatili wa hivyo, lakini bado hakusema ni wapi anakopatikana mtu huyo.

“nitakufanyia ukatili wenye hujawahi kuuona hapa duniani, najua nyumba ya huyo mtu japo sina uhakika sana kwani hawa watu wana tabia ya kubadili badili mazingira ya kuishi sasa nataka unitajie nyumba anayo patikana nijue kama ndo yenyewe sitaki kupoteza muda” kijana yule aliendelea kukaa kimya, mwanaume alipita na sikio moja la yule kijana kitu kilicho pelekea kilio kikubwa sana katika mitaa hiyo

“shiiiiiiiiiii, unanipigia kelele, nambie mtu huyo yuko wapi” aliona kimya kwa sababu kijana huyo alikuwa anaendelea kulia, kijana wa watu aliongeza kilio huku akigala gala chini baada ya kushuhudia kiganja chake cha mkono kikienda chini , aliomba sana mtu huyo aweze kumwacha hai asimuue

“huwa sipendi watu wenye dharau za kipuuzi namna hii nakuuliza hunijibu, jifunze kutumia viungo vyako vizuri, kuna muda unapaswa kuutumia mdomo na kuna muda unapaswa uyatumie masikio yako vizuri mno kusikiliza unacho ambiwa kisha ubongo wako ufanye maamuzi yaliyo sahihi , nadhani kwa maumivu unayo yapata kwa sasa na kuomba nisikuue utakuwa umeanza kuelewa thamani ya uhai wa mtu, huwa ni ngumu sana kuelewa mpaka pale inapofika hatua hauna namna nyingine ndo unaelewa thamani ya hiyo pumzi unayo idharau sana na kuichukulia kirahisi pindi unapokuwa bado upo hai, kifo ni siri moja nzito sana kwani hata wenye mabavu sana wanakuwaga na wasi wasi mno linapokuja suala la kifo, mimi mwenyewe naua wale walio nifanyia ubaya lakini kuhusu kufa ninaogopa mno kwani naijua sana thamani ya huu uhai tulio barikiwa tangu siku niliyo mshuhudia mzee wangu akikata roho kwenye mikono yangu mwenyewe, kama tutabahatika kuja kukutana katika maisha mengine basi usiitangulize kauli ya pesa mbele ya uhai wa mtu bwana mdogo”, Calvin aliongea wakati huo akiwa amemwinamia kijana huyo alipokuwa amelala, alimwonyesha namba ya nyumba na kijana huyo alionekana kukubali kwamba hapo ndipo mahali alipokuwa mtu huyo afahamikae kama Samson Nelson kutoka Morogoro.

Ilikuwa ni pembezoni mwa mji sehemu yenye miti mingi sana, ikiwa ni nusu saa tu tangu atoke mahali alipokuwa amefanya ukatili mkubwa sana kwa wale vijana saba, alifanikiwa kuliona jumba moja kubwa sana mahali hapo ambalo lilikuwa linawaka vizuri sana taa zake na ni kweli alisadiki maneno ya kwamba mwenye pesa hata aende sehemu mbaya vipi ila yeye bado ataishi maisha mazuri tu. Akiwa amejibanza kwenye moja ya mti maeneo hayo aliweza kuona kuna walinzi wanapita pita getini kwa nje kitu ambacho hakukitegemea kabisa, aliivaa vyema kofia yake akajifunga na kitambaa usoni akafumba macho kwa hisia kali mno akatamka “MUNGU naomba unisamehe kwa hiki ninacho enda kukifanya sina namna nyingine tena”, aliitoa simu yake na kuingia kwenye mitandao yake ya siri ya kijasusi, haikuisha hata dakika moja lile jumba lote umeme ulikuwa umezima, walinzi walianza kuzunguka huku na huku kuona kama wanaweza kuirudisha hiyo hali ya umeme kuwaka kwani ilikuwa ni ghafla sana na hawakuelewa tatizo lilikuwa ni nini mpaka umeme uweze kuzimika ghafla sana kiasi hicho.

Wale wawili wa nje mmoja alishangaa mwenzake anadondoka chini huku akiwa ameshika shingo yake, alitaka kuikoki silaha yake lakini alikuwa amechelewa alishtukia panga lipo shingoni likiwa linawaka sana mida hiyo ya usiku wa saa nne.

“bosi wako yuko wapi” sauti nzito sana iliuliza kwa nyuma iliyo muamuru mtu huyo aeleze ni wapi alipo huyo anaye kaa hapo

“sijui aliko” alijibu kwa jeuri yule mlinzi kitu kilicho pelekea upanga kuzamishwa kidogo shingoni na kumpelekea kutoa sauti ya maumivu makali alishtukia akipewa teke kali na kumuamuru akae kimya lasivyo ataipoteza shingo yake.

“yuko wapi?” Calvin aliuliza huku akiwa anaendelea kuuzamisha upanga maeneo ya shingoni mwa mtu huyo

“yupo floor ya chini kabisa ya ardhi saivi ana mwanamke ameingia naye” alijibu huku akigugumia kwa maumivu makali sana mlinzi huyu

“mpo wangapi humu ndani na huko chini nafikaje?”

“humu tupo kumi, kufika huko chini kuna password maalumu huwa zinafungua mlango wa siri kila baada ya dakika tano, ukikosea mara moja mlango unajilock jumla mpaka aje afungue mwenyewe kwa kutumia jicho lake au miongoni mwetu walinzi ndo tunaweza kufungua” baada ya kutoa majibu upanga ulizungushwa mbele ya shingo na kumfanya kufa vibaya sana. Mwanaume aliruka mpaka ndani kwa umakini mkubwa sana kwani alikuwa na kazi ya kumalizana na walinzi wengine nane, aliona watatu wakiwa wamekaa pamoja wakiongea taratibu, aliwaibukia mbele yao, kulikuwa na kiza walijua ni mwenzao lakini aina ya utembeaji walikuja kushtuka kwamba wamevamiwa. Ulipigwa mkono kwa dakika tatu wawili walikuwa wamevunjwa shingo zao, huyu mmoja alianza kukimbia ili kunusuru maisha yake lakini upanga ulirushwa kwa ufundi mkubwa mno upande wa nyuma, ulizama mpaka ukatokezea mbele kabisa ya tumbo kisha ukachomolewa kwa kasi sana na kurudishwa mahali pake. Alienda kwenye mlango wa kuingilia ndani lakini mlango ulikuwa umefungwa, alilisogelea dirisha ili aweze kuvunja kioo lakini alitulia baada ya kusikia vishindo vya mtu kwa ndani vikielekea upande wake alio kuwa yeye, haukupita muda mlango ukafunguliwa ikionyesha mtu huyo alikuwa anataka kujua usalama wa nje,wakati anatoka kichwa tu alirudishwa ndani na ngumi nzito mno kutoka kwa mtu ambaye alikuwa hata hamuoni, wakati anahangaika kuweza kujua aliye mpiga yuko wapo wakati huo umeme uliwaka ghafla sana.

“shiiiiiiit” alitamka Calvin wakati anamfuata mtu huyo mahali alipokuwa amedondokea

“wenzako wako wapi?” aliuliza Calvin

“wewe ni nani?” alijibu yule mtu akiugulia maumivu makali kwa ngumi aliyoweza kupigwa nayo. Calvin kabla hajaongeza neno lolote alihisi kama kuna nyayo za mtu zinazo kuja maeneo hayo ya sebuleni, alirusha ngumi moja kwenye eneo la shingo la mtu huyo na kuivunja vibaya sana kwani alihisi atampigia kelele na kumharibia. Mwenzake alivyofika alishtuka baada ya kuona mwezake yupo chini alafu haoni mtu mwingine yeyote ndani hapo, aliitoa bastola yake huku akimfuata mwenzake pale chini kwa uoga mkubwa mno, wakati anainama kumkagua mwenzake, aligusana na upanga kwenye shingo yake ulio kuwa unachuruzika damu mbichi kabisa na sauti kali isiyo na masiara ikimuamuru atupe silaha yake, alitii na kuanza kufuata maelekezo kutoka kwa huyo mtu
Calvin atafanikiwa kumpata huyu mtu na nini hatima ya haya yote? Ukurasa wa 26 unafika tamati tukutane tena wakati ujao.
Chao.....

Bux the story teller

#ULIMWENGUWAWATUWABAYAView attachment 2323429
Nomaaa imefika patamu
 
Kwa wapenzi wa hadithi zangu, nunua sasa hadithi ya ULIMWENGU WA WATU WABAYA Kwa shilingi 4000 tu nakupatia mpaka mwisho unaisoma yote[emoji3578]

Lipia kwa namba 0621567672 Kwa haloteli jina FEBIANI BABUYA au M-pesa kwa namba 0745982347 jina FEBIANI BABUYA, ukituma unaipata muda huo huo pia kuna hadithi nyingine kali Sana ya kijasusi inaitwa I WANT TO DIE JUDGE ( NATAKA KUFA HAKIMU) ukinunua nakupa na ofa ya LOVE STORY moja bure kabisa wahi mapema ufurahie na kuujaza ubongo madini ya kutosha.

Lakini pia kwa wale ambao wanahitaji kujiunga na group letu la WhatsApp tayari lipo ambalo ni shilingi 3000 tu kwa mwezi unasoma mwezi mzima kila siku ya MUNGU[emoji3578] namba za malipo ni zile zile 0621567672 na 0745982347 zote jina ni FEBIANI BABUYA, ukituma tu nichek kwa namba ya WhatsApp 0621567672 au kawaida kwa 0745982347

Karibuni sana kwenye hadithi kali za Bux the story teller [emoji3590]
JamiiForums1035128080.jpg
 
Aah kasisi mbona anataka kutibua mipango yetu bwana aaahaaa[emoji57][emoji57][emoji57]
 
Back
Top Bottom