Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nani tena anayeharibu mipango huyoAah kasisi mbona anataka kutibua mipango yetu bwana aaahaaa[emoji57][emoji57][emoji57]
Leo mtasoma viwiliFebian baba weekend hii jana tumelala njaa
Hayo ndio mambo sasa ubarikiweLeo mtasoma viwili
kasisi chachaNani tena anayeharibu mipango huyo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mbona baba tenaFebian baba weekend hii jana tumelala njaa
Mmh nimesoma huku nakodoa macho na koo imenikauka kama vile ndo naangalia mapiganoHADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 30
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA.............
Hii hali iliwashangaza hawa wawili wakiwa wanashindwa kumtathimini mwanaume huyo kwa maana alikuwa haeleweki hata maneno yake anayaongea kwa mafumbo mno, walichanganyikiwa kwanza walishangaa anasemaje kesho atakuja wakati wao wanaishi kwa siri sana sasa kajuaje mahali wanapokaa na angeweza vipi kuja mahali hapo hawakupata majibu, baada ya muda kidogo Sebastian aliamua kumbeba mwenzake ambaye kwa wakati huo alikuwa hawezi hata kutembea, Sebastian alijikongoja mpaka sehemu ya mbali kidogo walipokuwa wamepaki gari lao na kumpandisha mwenzake huyo kwa shida huku nae akiwa anasikia maumivu kila sehemu ya mwili wake kisha akaondoka kwa mwendo wa taratibu.
ENDELEA.............
Ndani ya kambi ndogo ya siri sana ya THE RED SQUAD wakiwa ndani kabisa ya chumba kilichopo chini ya ardhi ndani ya mitaa ya Kigogo, ni mitaa iliyokuwa inasifika sana kwa mambo ya kutisha hasa baada ya kuwa na idadi kubwa mno ya wahalifu waliokuwa wanafanya mambo ya kutisha kupitiliza, kupitia CCTV camera waliweza kuliona gari ambalo walikuwa wameondoka nalo makomando hao wawili Sebastian na Deogratius likija kwa kasi mno, walishtuka kwanini imekuwa hivyo kitu kilicho wapelekea kufungua mlango wa siri na kuweza kutoka mpaka nje, walikuta gari likiwa limesimama tu na hakuna aliyekuwa anatoka wala hakukusikika kelele yoyote ile, walienda kwa tahadhari mno ndani ya gari hilo wlishangaa kumuona Sebastian Mgeni amelalia usukani huku Deogratius akiwa hajitambui kwa chochote. Waliwatoa nje lakini walishangaa kuona Deogratius mguu wake umegeuka na kuna mfupa ulikuwa eneo ambalo sio sahihi basi Luciana aliushika kwa nguvu na kuugeuza ili kuurudisha kwenye hali yake ya kawaida, muda huo Deogratius alikuwa hana hata uwezo wa kutoa sauti alikuwa akitoa machozi kwa mbali, Felix alikuwa amechukia sana kumuona ndugu yake Sebastian akiwa kwenye hiyo hali ngumu ya maumivu lakini kwa wakati huu hakuwa na kitu chochote cha kufanya ilibidi wawatibu kwanza na kuwaacha wapumzike ili waeleze kilicho tokea.
Baada ya saa moja kupita Sebastian ndiye alikuwa wakwanza kurudi kwenye hali yake
“nini kimetokea mpaka mkawa kwenye hali ya kudhalilisha makomando wakubwa kama nyinyi?” Luciana aliuliza kwa hasira sana kwani aliona ni dharau kubwa sana kwa makomando wakubwa sana kama hawa kuwa kwenye hali mbaya namna hii
“yule sio binadamu kama tulivyo kuwa tumeambiwa he’s completely a monster (akimaanisha kwamba Calvin sio mwanadamu bali lilikuwa ni jini), ana sura nzuri sana ukimwangalia na anaongea kistaarabu sana ila akibadilika kinakuwa sio kiumbe cha kawaida, kwa wakati ule alikuwa anaweza hata kutuua sema katuacha kwa kudai kwamba sisi ni walinda amani wa nchi hivyo hawezi kutuua na kaamua kumvunja mguu Deogratius kama kumfunza heshima kwa kauli zake mbovu, kama ningekuwa natoa ushauri kwenye uumbaji ningeshauri asije kuzaliwa mwanadamu wa vile kwa maana sitatamani kukutana nae tena ni hatari mno” Sebastian alikuwa anaeleza kwa uchungu kwani hakuwahi kupigwa tangu apate mafunzo ya upiganaji ila leo aliweza kupigwa kama mtoto na kijana mdogo sana ambaye kwa miaka ni mdogo kwake
“shiiiiiiiit haiwezekani wanaume wa kazi kama nyie mpigwe na mtoto mdogo namna hiyo ni uzembe mkubwa mno” aliongea kwa hasira Luciana kiongozi huyu wa THE RED SQUARD huku akipiga ngumi kwa nguvu ukutani hali iliyopelekea ukuta kubonyea kwa uzito wa ngumi hiyo.
“ongea tu kiongozi ila huyu mtu usikutane naye ni kiumbe hatari mno kuliko hata unavyoweza kuitaja hatari yenyewe nina uhakika yule angeamua kuichukua hata ikulu ana huo uwezo nadhani, ana mapigo ya ajabu na kuna muda anakuwa kama anapotea kwani ana kasi kubwa kama upepo na hata ngumi yake akikupiga nayo unaweza ukahisi umepigwa na chuma kizito mno, yule sio mtu wa kuomba kukutana naye mara nyingi kwenye haya maisha itakupelekea kuwa mtu usiyekuwa na bahati hata kidogo” ilisikika sauti ya Deogratius ambaye kwa wakati huu fahamu zilikuwa zimemrejea akiwa kitandani mguu wake umefungwa na plasta na kwa wakati huo hakuwa hata na uwezo wa kusimama
“pumbavu sana anapatikana wapi huyo mtu?” Luciana aliuliza kwa hasira mno ili aweze kukutana na mtu huyo kwani alikuwa na hamu ya kukutana naye mwenyewe baada ya kuona anasifiwa kupita kiasi, ilikuwa hivyo hata kwa Felix alimtamani sana mtu huyo baada ya kumpigia ndugu yake hakuelewa alikuwa na uwezo gani mpaka wamsifie sana namna hiyo
“mhhhhhhh hata msihangaike sana kumtafuta amesema kesho atakuja mwenyewe majira ya saa saba kasoro za usiku” Sebastian aliongea, kwake akiona ni kawaida tu lakini ilikuwa ni kauli ya kushangaza mno, inawezekana vipi akawafuata watu wanao ishi kwa siri sana namna hiyo kwani hata wenyeji wa maeneo ya kigogo walikuwa hawatambui uwepo wa majasusi hao katika hayo maeneo. Luciana aliangalia kwenye shati aliyokuwa amevaa Sebastian alitabasamu baada ya kuona juu ya kifungo cha shati kulikuwa na kitu kidogo kama kidoti cheusi, alikiangalia kwa ufasaha na kugundua kwamba hiyo ilikuwa ni tracking device, alikuwa amejua kwamba mtu huyo alikiweka mahali hapo bila Sebastian kuelewa ndio maana alikuwa na ujasiri wa kusema wasihangaike kumtafuta atakuja yeye mwenyewe kwani alikuwa amejua mahali wanapo patikana kupitia hiyo device(kifaa).
“anaonekana ni mtu makini sana anapoyafanya mambo yake, hiki ni kifaa cha kunasa mawimbi ya sauti pamoja na camera ambayo inaonyesha kupitia kitone kidogo cha maji kilichowekwa katikati ya kifaa hicho, hiki ni kifaa cha kijapani na niliwahi kukiona mara moja tu nilipokuwa Thailand kukamilisha mafunzo ya mapigano ya miaka miwili, nilikuwa na rafiki yangu mmoja kutoka Japan ndiye alikuwa nazo na aliniambia huwa zinamilikiwa na jasusi mmoja hatari sana nchini humo na anatafutwa sana ila hakuna ajuaye mahali anapo patikana, kwahiyo kuona mtanzania anazo inamaanisha atakuwa anajuana na mtu huyo hivyo atakuwa ni mtu hatari sana, amefanya vizuri kuweza kutambua mahali tulipo hiyo kesho siendi popote namsubiri kwa hamu sana aweze kufika mahali hapa alafu mimi nitamalizana naye mwenyewe” ni maelezo alikuwa Anaya elezea Luciana kumhusu mtu wao huyo ambaye alikuwa na hamu naye isiyo elezeka, maelezo hayo yalimuacha Sebastian mdomo wazi kwani hakuelewa hicho kifaa aliwekwa muda gani, aliskitika sana.
NIFOLLOW Instagram @iamfebian Twitter #buxmsafi Tick-tock @buxmsafi LinkedIn FEBIANI BABUYA Facebook Bux the story teller WhatsApp 0621567672
Wasakana waonana, saa sita na dakika zake hamsini na tano gari aina ya V8 linaingia maeneo ya Jangwani bila wasi wasi wowote ule, Calvin alikuwa amefika mahali hapo kuonana na mtu wake ambaye ndiye amemfanya ahangaike mpaka kwenda mbinga ili ampate, alishuka kwenye gari na kwa mbele yake kidogo aliona wanaume wanne wakiwa wamesimama hawana hata wasi wasi wowote, alitabasamu sana baada ya kumuona mtu wake kwa mbali akiwa anasogea na hao vijana wake watatu ambao ndio alikuwa anawatumia kama mkono wake wa kulia kufanya shughuli zake baada ya mmoja wao ambaye ni Brown Kasongo kupotea kwa kuingia kwenye mikono ya Calvin.
“mdogo wangu yuko wapi?” Scot ambaye sasa tunamjua kwa jina la Isack Nelson aliuliza kwa pupa mno kwani hakuwa na uhakika kama mdogo wake anaweza kuwa salama mpaka muda huo. Wakati huo huo kabla hajajibiwa walisikia sauti ya buti la ghari likigonga gonga kumaanisha mtu huyo aliyekuwepo ndani alikuwa amerejewa na fahamu. Calvin hakujibu chochote wala kugeuka bado alikuwa anamtathimini kwa undani mwanaume huyo mwenye mbavu za kutosha ambaye ndiye mhusika mkuu wa mauaji ya wazazi wake. Scot alikimbilia kuke kwenye buti la gari na kufungua haraka sana, alimuona mdogo wake akiwa hana mkono mmoja lakini alikuwa amesafishwa vizuri mwili wake na hakuwa na shida yoyote hata kidonda chake hakuwa analalamika kama kinamuuma ni baada ya kuweza kutibiwa pindi alipokuwa amepoteza fahamu zake, alimkumbatia kwa hisia sana pacha wake ambaye alikuwa ndiye kila kitu kwake na alimshukuru MUNGU ndugu yake huyo hakuweza kuuawa. Wakati wote huo mwanaume alikuwa hajaongea chochote na alikuwa anamwangalia mtu huyo alivyokuwa anamhngaikia ndugu yake huyo, Scot alimkalisha ndugu yake huyo kisha akamfuata Calvin pale alipokuwa akiwa na hasira nae sana
“nimekutafuta kwa miaka yote miwili na ulifanikiwa kunikimbia, umerudi kimya kimya alafu unaenda kumfanyia unyama wa namna hii mdogo wangu, leo nakuzika ukiwa uko mzima kabisa” Scot alikuwa anaongea kwa hasira sana kwani alihisi huyu mtu asingekuwa na uwezo wa kumfanya lolote
“ningekuwa mimi ndiye wewe nisingetamani kabisa kukutana na mtu ambaye niliingamiza familia yake unajua kinacho tokea? umenihangaisha kwa kujificha kwako sura lakini hatimae nimekupata kwa msaada mkubwa sana wa Tomaso ambaye kwa sasa unamtafuta sana ili akuwekee sura nyingine uendelee kuongeza idadi ya watoto yatima kwenye nchi hii kwa kuwaua wazazi wao. Leo nataka nizitumie robo tatu ya nguvu zangu na upanga wangu kwa ufasaha sana kwani haitakiwi kubaki hata kucha ya mwili wako ikiwa hai, adhabu yako ni zaidi ya kifo unapaswa uyapitie mateso ambayo walipitia wazazi wangu kabla hawajakata kauli kisha nitaenda kumalizana na huyo bosi wako ambaye naenda kuchukua mali zote ambazo anatamba nazo mjini kutesea watu ikiwa ni pamoja na kukulisha wewe hapo bahati mbaya sana hajui bado zile mali zipo chini ya hati miliki ya jina langu, najisikia vibaya sana naenda kuingia kwenye historia ya kuwa muuaji katili sana kuwahi kutokea kwenye nchi hii lakini sina namna nyingine ya kufanya acha iwe tu” Calvin alielezea kwa hisia sana kwani mtu aliye waondoa wazazi wake katika ulimwengu huu alikuwa yupo mbele yake baada ya muda mrefu sana kupita.
“hahahhahhahahahahha hakuna binadamu wa kuzaliwa kuweza kupigana namimi kwenye hii nch…….” Scot hakumalizia vizuri sentensi yake wakati huo upanga ulirushwa kwa nguvu na kutoboa kichwa cha mmoja kati ya wale vijana wake watatu alio kuja nao pale, wakati upanga unafika mwanaume alikuwa anakuja kwa spidi ya ajabu alijibiringisha na kutumia moja ya ngumi kali sana ya mkono wa kulia ambayo aliishindilia kwenye eneo la moyo la kijana wa pili kati ya wale watatu na kupelekea kifua kubonyea kabisa ndani,kijana yule alimwaga damu huku moyo wake ukishindwa kabisa kusukuma damu na kumfanya kufa kifo cha kikatili sana akiwa amesimama pale pale, alikuwa amebaki mmoja huyu alitaka kukimbia baada ya kushuhudia unyama huo kwa watu wawili ndani ya sekunde thelathini tu pekee katika eneo hilo. Star alirushwa kwa ustadi mkubwa na kukata mshipa wa damu wa mguu wa mtu huyo, Calvin alikuwa ameushika upanga kwa nguvu sana mkononi mwake aliushusha kwenye shingo ya mtu huyo kwa hasira na kukitengenisha kichwa na kiwili wili. Scot alikuwa bado anashangaa maana ilitumika dakika moja tu pekee bila kuzidisha hata sekunde moja kuweza kuwaua kikatili mno makomando hawa ambao walikuwa ni watu wa jeshi lakini waliasi na kwenda kutafuta utajiri kwa njia isiyokuwa ya halali.
************************************
“mdogo wako nitamuacha hai sitamuua ila nataka ajifunze kupitia wewe na kwa namna unavyo enda kufa kikatili ili kwa maisha atakayo yaishi aweze kuthamini uhai wa watu wengine, nitamkabidhi kwenye mikono ya serikali ili akasaidie kuweza kutoa taarifa ya baadhi ya magenge ya kihalifu ambayo yanazidi kuharibu mwenendo wa nchi yangu, kwa wewe ukifika kuzimu hakikisha unawaomba msamaha wazazi wangu kwa sasa wataanza kupumzika kwa amani huko waliko, kama tukija kubahatika kuonana kwenye maisha mengine tena unapaswa uwe umebedilika kwa kila kitu kwani nitahakikisha nakutafuta upya bado kufa kwako sitaridhika sana kwa kosa lako kubwa la kuidhulumu furaha yangu ya kuniulia wazazi wangu” Calvin baada ya kumaliza kuongea alikuwa anakuja kwa spidi huku ameukaza mno mkono aliokuwa ameshika upanga wake mpka mishipa mikubwa ya damu ilikuwa inaonekana kwenye mkono huo, Scot alitoa visu vyake viwili kwani kwa kasi ya mtu huyo aliona bastola haikuwa na umuhimu sana mahali hapo, wanaume alirusha teke likampata vizuri sana Scot kifuani lakini alikuwa imara akarudi nyuma kidogo tu kisha akakaa vyema lakini Calvin alikuwa amefika na alikuwa anarusha ngumi za hatari mno pamoja na panga, Scot alijikuta anaelemewa na kukatwa mkono wa kulia ulio anza kutoa damu kwa Kasi, Calvin alisimama na kufumba macho yake alikimbia kwa spidi kama anapotea Scot alirusha visu vyote viwili ambapo kimoja kilimpata Calvin kwenye paja na kuzama lakini hakuhisi chochote kwani alikuwa ameshabadilika alizamisha upanga tumboni kwa Scot na kuutoa kwa nguvu kisha alijibetua na round kick iliyo mpelekea Scot kuruka mbali, mwanaume alimfuata kule kule juu akamrudisha na goti mpaka chini wakati huo Scot alikuwa anakohoa damu na hali yake ilikuwa imebadilika na kuwa mbaya.
Wakati anamsogolea Scot alishikwa mguu na Samson akimuomba sana amuache hai ndugu yake huyo lakini haikusaidia mwanaume macho yake yalikuwa mekundu na kwa huo muda hakuwa na nafasi ya kumsikiliza bindamu yeyoye yule, alimsukuma samson kwa nguvu ambaye alikuwa analia mno kisha akamsogelea Scot, akimwangalia kwa uchungu sana pale chini akaitoa simu ya Scot kwenye mfuko, akamshikisha kidole chake ambapo ilifunguka, moja kwa moja alitafuta moja ya namba ambayo ilionekana kuwasiliana sana na mtu huyo iliyo andikwa bosi akaenda moja kwa moja kwenye video call na kuipiga, ndani ya dakika ilipokelewa na hakuwa mwingine bali Mr Fabian Decco, mzee huyo alishtuka sana na kuogopa mno baada ya kuiona sura ya Calvin kwenye simu ya Scot, Calvin hakuongea kitu aliisogeza vyema kwa Scot na wakati huo alikuwa ameushika upanga kwa nguvu sana, alikata shingo ya Scot kikatili mno na kuifanya kutengana kabisa na kichwa chake, hali hii ilimpelekea mr Fabian Decco kufumba macho kwa hisia hilo jambo lilikuwa linatisha kupita kiasi na hakuwahi kushuhudia kwenye maisha yake, Calvin alitamka neno moja tu
“nakuja mzee tutaongea vizuri siku tukikutana”, baada ya kushuhudia mauaji ya kaka yake kipenzi na wa pekee Samson alipata ukichaa pale pale, ni baada ya kuona unyama wa kutisha mno kwa mtu ambaye ndiye pekee aliyekuwa kama familia kwake, hakika alikuwa amelipwa ubaya wao waliokuwa wanaufanya kwa miaka mingi sana. Calvin aliunguruma kwa sauti kubwa sana na kupiga kelele kwa uchungu mno kama simba mwenye njaa kali sana, aliichukua simu yake mfukono na kumpigia mkuu wa idara ya usalama wa taifa.
Nini hatima ya kisasi cha Calvin, ataweza kuwakwepa usalama wa Taifa? akimpata Mr Fabian Decco unadhani atakuwa amemaliza kisasi chake? Huyu mtu wa tatu anaye onekana kumsaidia Mr Decco ni nani na kwanini amsaidie?......ukurasa wa 30 unafika mwisho....kalamu yangu imegoma kuendelea kuandika tena till the next time.
Chao[emoji2768]
Bux the story teller
#ULIMWENGUWAWATUWABAYAView attachment 2329775
Enjoy it[emoji3590][emoji3578]Mmh nimesoma huku nakodoa macho na koo imenikauka kama vile ndo naangalia mapigano
Huyo kasimu anachokitafuta atakipatakasisi chacha
Kwa haya mambo mazuri, Febian baba tuendelee Leo ni siku nyingine baba[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mbona baba tena
Ongea na Febian Kwa mara ya mwisho kama ameshindwa kuelewa unajua Nini Cha kufanya kama nilivyokupa mafunzo japani usiniangusheMimi kama Calvin naposema kitu naomba nielewke jamani siongei mara x 2
Huyu namla nyama Fabian kwa sabb nataka nirudishe mali zote za mzeeOngea na Febian Kwa mara ya mwisho kama ameshindwa kuelewa unajua Nini Cha kufanya kama nilivyokupa mafunzo japani usiniangushe
[emoji3578]Febian tuwezeshe Leo tuhesabiwe Kwa Amani, umetulaza njaa siku mbili etii