Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Leo ni jumapili kabisa tulivu, wakati unaisindikiza wikiendi yako basi njoo ujisomee hadithi bora sana za kijasusi.HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 37
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA.............
chini palifunguka na kulikuwa na ngazi za kushuka chini Calvin alibaki ametoa macho kwa hali aloyo iona hapo ilimfanya amheshimu mwanamke huyu kwani hakuwa wa kawaida kama yeye alivyokuwa akimchukulia. Walifika chini kabisa na juu palijifunga, mbele yao kulikuwa na chumba kikubwa kilicho kuwa kama maabara nzuri sana lakini ndani yake kulikuwa na makomputa ya kisasa mno, Jackline alibonyeza kwenye kioo kimoja na komputa zote zikawaka ikiwemo kubwa moja ambayo ndiyo ilikuwa ikitumika kuongozea zingine.
ENDELEA............................
“mhhhhhh umewezaje kufanya haya mambo ndani ya nchi hii na vyombo vya sheria visijue?” Calvin alikuwa anauliza huku akishangaa na kuketi kwenye moja ya sofa zuri sana ndani humo ambapo kwa mbele yake kulikuwa na chumba ambako ndani yake kulikuwa na kitanda kizuri sana, friji pamoja na skrini ya kawaida ukutani na nguo za kike.
“pesa ni kitu cha hatari sana kwenye maisha baba yangu, hayo mambo yote anayafanya baba yangu ambaye huwa anatumia pesa nyingi sana kufanya nipate kila ninacho kitaka, ni vitu vichache sana ambavyo pesa haiwezi kununua kikubwa zaidi ni uhai tu pekee lakini kwa wanadamu wananunulika kiwepesi sana ukiwa na pesa ndio maana hivi vitu vinatoka nje na kuingizwa nchini kwa urahisi sana kwa sababu ya pesa tu” Jackline alilijibu swali hilo huku akiwa anaiweka frash kwenye komputa yake, Calvin alisikitika sana kuona jambo hilo kwa mwanamke ambaye yeye alikuwa akimchukulia poa sana.
“kwahiyo wewe ndiye Yevada?” aliuliza huku macho yake yote yakiwa kwenye skrini
“ndio, hilo ni jina ambalo baba alinipatia kulitumia nikiwa Tanzania” Jackline wakati huu alikuwa akiendelea kutumia code zake za siri ili kuweza kufungua mafaili ya kwenye frash hiyo ambayo yalikuwa na vizuizi vingi sana. “kweli mtoto wa nyoka ni nyoka tu haiwezi kutokea akawa kuku” Calvin alitamka chini chini bila kusikika. Dakika moja ya kuhesabau frash hiyo ilikuwa imefunguka na mbele ya skrini kubwa kulikuwa na picha ya mwanaume mmoja wa kiarabu mwenye mwili ulio shiba sana pembeni yake kulikuwa na jina Ahmed Abdulrazack, huyu ndiye mtu aliyekuwa anatakiwa akutane naye gerezani ili aweze kumpata kaka yake atakaye mpa mwelekeo wa kumpata mlengwa wake kamili baada ya kuzubaishwa kwa muda mrefu akijua Fabian Decco ndiye mhusika kumbe yeye alikuwa mtumishi tu.
Ana miaka 27 pekee kwao wamezaliwa sita lakini walio hai mpaka sasa ni wawili tu yeye na mwenzake ambaye kwenye picha kulikuwa na kivuli tu bila jina, mtu huyu muda mwingi ameishi sana kwenye kambi za kigaidi na ameua watu wengi sana kwa hivyo kwake mauaji ashayazoea na ni mtu hatari kupita kiasi unapokuwa naye karibu. Ana miaka mitatu sasa tangu afungwe na taarifa zake ni za siri mno kuzipata kwa sababu wengi wanajua amekufa tayari. Wote wawili asili yao ni Saudi Arabia na wote wapo Tanzania, kesi yake iliyo mfanya mpaka sasa yupo ndani ni kosa lililo semekana kuwa la kigaidi baada ya kuua watu miatano kwa kutumia mabomu pamoja na gesi, alikubali makosa yake yeye mwenyewe lakini hakuna alicho fanywa mtu huyu, anategemea kutoka gerezani humo baada ya miaka miwili. Ni maelezo mafupi lakini yalikuwa na ujumbe wa kujitosheleza kabisa kumuelezea mwanaume huyo wa kiarabu Ahmed Abdulrazack, kwa mbele kulikuwa na video zake mbili, moja ilikuwa ikimuonyesha namna alivyokuwa akipambana na wanajeshi kumi kutoka jeshi la kujenga taifa ambao aliwaua kikatili mno na ya pili ilikuwa ikimuonyesha akiwa ameshika kisu akichinja wanawake watano na watoto kumi mmoja mmoja mpaka wote walipoisha, ilikuwa video ya kusisimua mno ambayo ilimfanya Calvin afumbe macho kwa hasira, ilimuuma sana kuona watoto wadogo wanauawa kikatili sana namna hiyo pamoja na wanawake huku anaye fanya hivyo akionekana kukifurahia sana alichokuwa anakifanya. Jackline alikuwa anaogopa sana kwa alichokuwa anakiona mbele yake ilimbidi kuuliza kwa wasi wasi sana
“ina maana ndio hawa watu unao watafuta”
“wako wengi sana huyo mbona wa kawaida mno” mwanaume aliongea huku akitabasamu kumtoa wasi wasi bibie
“hapana Calvin usifanye hivyo hawa watu wanaonekana ni hatari sana hawana hata ubinadamu ndani yao” Jackline alikuwa akimuomba Calvin huku amepiga magoti hali aliyo iona kwa mtu huyo kwenye hizo video ilimtisha kupita kiasi. Calvin alimshika akamnyanyua baada ya kumkumbatia na kumwambia kwa utaratibu mkubwa
Instagram @iamfebian Twitter #buxmsafi Tick-tock @buxmsafi LinkedIn FEBIANI BABUYA Facebook Bux the story teller WhatsApp 0621567672
“ungekuwa umewahi kuniona japo mara moja nikiwa nimebadilika basi usingekuja hata siku moja kumuogopa mtoto mdogo kama huyo uliye muona anafanya hayo mauaji, bado ni mlaini sana mikono yake sina imani kama anweza kunigusa hata unywele wangu mmoja, anaua kikatili ila anaonekana bado ana nafsi ya uoga ndani yake inawezekana anafanya hivyo kwa sababu tu ameshazoea kufanya hivyo” mwanaume alikuwa anamtoa wasi wasi bibie kisha akampiga busu zito sana la mdomo ambalo lilimfanya mwanamke huyu mwili wake umsisimke mno, binadamu unapokuwa unagusana mwili au ukiwa hatua chache na mtu unaye mpenda sana mwili huwa unapokea mabadiliko haraka sana ndicho kilichokuwa kinawakuta watu hawa mioyo yao ilianza kuenda kasi sana wakajikuta wameangukia kwenye mapenzi mazito sana, chumba cha mtu kulala hakikuwa mbali na mahali walipokuwa hivyo walikokotana mpaka huko, mashuka yaliweza kupata shida sana usiku huo kwa kuweza kushuhudia mechi kali sana kati ya wapendanao wawili walio kuwa wamepotezana kwa muda mrefu mno. Iliwachukua masaa matano kuweza kumaliza mtanange huo ambao ulimfanya kila mmoja wao achoke sana kiasi kwamba walipitiwa na usingizi mzito mno.
Wakwanza kuamka alikuwa Calvin majira ya asubuhi, alinyanyuka na kumwangalia mwanamke aliyekuwa amelala pembeni yake, alitabasamu sana na kumpiga busu la paji la uso mwanamke huyo kwa namna alivyokuwa akimpenda kwa uzuri wake ulio kuwa haumchoshi kumtazama. Akaamua kunyanyuka ili apate hata maji ya kunywa kwenye friji lakini hakupewa nafasi hiyo alivutwa na mrembo huko kwa nguvu, alijikuta amedondokea kitandani tena hali iliyo wapelekea kucheza fainali nyingine asubuhi hiyo mpaka pale walipohisi kwamba nafsi zao zimeridhika, siku nzima walishinda pamoja humo ndani, hii ilimfanya mwanamke huyu afurahi sana kwa namna alivyokuwa anadekezwa hakutamani itokee tena akampoteza Calvin binadamu aliye mchagua miaka mingi sana iliyopita kumfanya kuwa baba wa familia yake. Mida ya jioni Calvin alikuwa anamuaga mwanamke ahuyo ambaye alikuwa analia akiwa amemshikilia shati Calvin kwani hakutaka aondoke aliogopa anaweza kupotea jumla na asirudi tena kwenye maisha yake.
“usifanye hivyo tafadhali, naomba ubaki namimi” Jackline aliendelea kulia
“natamani nikuahidi kukupa maisha ya furaha lakini kwa bahati mbaya nimechelewa sana kukufanyia hivyo, kwa sasa mimi sio binadamu ambaye ninaweza kumuahidi mwanamke furaha kwa sababu ninakatiza kwenye njia za hatari mno ambazo zinaweza zikachukua maisha yangu kwa sekunde yeyote, maisha yangu yapo kati kati ya mstari wa kifo kwa sababu kuna watu wanatamani mimi nife haraka kuliko hata wanavyo pambana na njaa na ndio hao ambao mimi nina shida nao sana, kama utaamua kunisubiri sawa weka imani kwamba ipo siku nitarudi” Calvin raundi hii aliongea kwa msisitizo akiwa anaelekea nje ya geti ambako ndiko aliliacha gari lake tangu jana alipoweza kufika mahali hapo. Jackline alikaa chini alilia sana lakini haikubadilisha uhalisia wa msimamo wa mwanaume ambaye hakuruhusu mapenzi ya mtawale sana kiasi cha kumsahaulisha kazi nzito iliyokuwa ipo mbele yake.
Saa saba za usiku ndani ya Kigogo katika kambi ya THE RED SQUARD walikuwa wamekaa watu saba kwenye gogo nje ya nyumba hiyo iliyokuwa ndogo sana kimwonekano lakini ndani yake kulikuwa na handaki kubwa mno lililo tengenezwa kisasa wakionekana kumsubiri mtu, ni kweli dakika mbili mbele alionekana mwanaume akiwa amevaa suti moja safi sana ukimwona ungedhani pengine ni meneja wa benki moja kubwa sana, alipendeza mno kitu kilicho mpelekea madam Luciana Mwaifupa kumeza mate kwa shida. Walio kuwa hapo hao saba walikuwa ni THE RED SQUARD pamoja na makomando wengine wawili Victor na Alex, wote walikuwa wakiusubiri kwa hamu ujio wa mtu huyo ambaye hakuwa na wasi wasi wowote na mikono yake alikuwa ameiweka mfukoni bila bila shida.
“kwa namna ulivyo na mwonekano wako ungekuwa mfanya biashara ungevutia watu wengi sana kwenye biashara zako lakini bahati mbaya sana umedumbukia kwenye dunia ya ukatili usio endana kabisa na sura yako jinsi inavyo jielezea” Calvin akiwa amesimama hapo aliisikia sauti ikiunguruma nyuma yake, hakuwa na papara akigeuka taratibu na kugundua mtu aliyekuwa nyuma yake ni mkurugenzi wa usalama wa taifa ndiye aliyekuwa ameyaongea maneno hayo.
“nina mengi sana ya kuongea nawewe ila nadhani huyo binti alikupa maagizo yangu najua ndio sababu uko hapa kwahiyo kilicho nileta hapa sio kujadiliana nini napaswa kufanya, mimi bado nina mazungumzo marefu sana nawewe hatujamalizana hilo tutalimaliza siku nyingine kwa sasa nikutanishe na raisi nina muda mchache mno kwa sababu nisipokutana naye saivi inaweza kuwa hatari sana kwake” Calvin aliongea akiwa anaangalia saa yake, hii iliwashtua wote pale hata Kasisi Chacha japo hakutaka kuonyesha huo udhaifu wake mbele ya vijana wake kauli ya kusema raisi anaweza kuwa kwenye hatari alafu kauli inatoka kwa raia wa kawaida tu.
“kijana umefika hatua hadi kuyatishia maisha ya raisi? Unajua kinachoweza kukukuta? Usitulazimishe tukakuua mapema ukiwa bado mdogo sana” aliongea akiwa amekaza sura, haikuwa rahisi sana mwananchi wa kawaida mtaani unaongelea usalama wa raisi mbele ya kiongozi mkuu wa usalama nchini ni kama kijichomea tanuru la kujiulia mwenyewe ila mzee huyu alijitahidi kuificha hasira yake kwani alikuwa hataki kwenda kinyume na maagizo aliyopewa na raisi.
****************************************
“mzee wangu umeishi sana lakini bado unaonekana hii nchi hauijui vizuri hata kidogo japo wewe ndiye unaye hakikisha usalama wake, kuna mambo mengi mno yanaendelea na huelewi kwahiyo ni vyema ukawatumia hao vijana wako kuweza kushughulikia hayo mambo ya hatari kwa usalama wa nchi hii kuliko kupoteza nguvu zenu kuhangaika na watu wasio kuwa na hatia yoyote ile”. Maneno ya Calvin yalimshangaza kila mtu mahali pale lakini hakuna aliye elewa kwamba mwanaume huyo alikuwa anamaanisha nini.
“twende maana mheshimiwa anakusbiri” sauti ya mzee Kasisi ilimfanya Calvin atabasamu baada ya kujua suala lake la kukutana na raisi wan chi ya Tanzania lilikuwa limefanikiwa kwa silimia mia moja, aliiweka vyema tai ya suti yake wakati anaingia kwenye gari iliyokuwa imepakiwa pembeni mahali hapo japo alikuwa makini sana kwani hakuwahi kuwa na imani na watu hawa wa usalama hata siku moja, mzee Kasisi alikuwa akiendesha mwenyewe na alilitoa gari kwa kasi sana mahali hapo.
Upanga kwenye nyumba namba 955 ndipo gari hiyo ilipoenda kukomea, ilifunguliwa geti na wanaume wawili waliokuwa wamevalia nguo za kikomando, mwanaume alijua tu hapo kuna ulinzi mkali sana kumaanisha mheshimiwa raisi alikuwa yupo ndani mahali hapo. Gari ilipakiwa wakashuka na mzee Kasisi alimuongoza Calvin mpaka geti la pili nalo lilikuwa na walinzi japo kwenyewe walikuwa wanne, wakakutana na nyumba kubwa yenye ghorofa moja ambayo ilikuwa ya kifahari sana, walizunguka kwa nyuma walikokutana na watu sita wakiwa wamevaa suti nyeusi na vifaa vya mawasiliano masikioni ila mmoja wao alivaa nguo za jeshi na alikuwa na nyota nyingi sana kwenye mabega yake pamoja na kifuani, Calvin alielewa tu kwamba mtu huyo lazima alikuwa ni mlinzi mkuu wa mheshimiwa raisi, walikuja ili kumkagua lakini mzee Kasisi aliwazuia na kuwaambia huyo alikuwa mgeni maalumu wa raisi hawakuwa na namna zaidi ya kumpisha kwa sababu walikuwa wanamheshimu mno mzee huyo na kumwamini sana kwani muda mwingi alikuwa yupo karibu na mheshimiwa raisi. Kwa mbele kidogo kulikuwa na bustani nzuri sana ya kuvutia, ilikuwa ni usiku lakini bado uzuri wake ulikuwa ukionekana vyema sana hasa baada ya kupambwa na swimming pool nzuri sana iliyokuwa kati kati ya bustani hiyo. Pembeni yake ndipo alipokuwa amekaa mheshimiwa raisi wa nchi ya Tanzania akiwa na kanzu ndefu ya kulalia akiendelea kupata kahawa taratibu sana ikiwa ndicho kitu alichokuwa akikipenda sana majira ya usiku, mzee Kasisi baada ya kufika hapo hakuwa na imani kabisa na Calvin lakini raisi alimuomba awapishe kwani alikuwa akihitaji kuongea wakiwa wawili tu pekee.
“shikamoo mzee” ilikuwa ni salamu ya Calvin kwa raisi wake huku akiinamisha kichwa kwa heshima.
“marahaba mwanangu una miaka mingapi?”
“ishirini na nne”
“maskini bado ni mdogo sana, miaka zaidi ya 25 iliyopita muda kama huu hususani siku za wikiendi ningekuwa nipo na rafiki yangu sehemu tunainjoi, alikuwa hapendi kabisa kulala mtu yule alitamani usiku wa manane akeshe akifanya kazi lakini kwa bahati mbaya sana sitaweza kumuona tena akiwa juu ya uso wa dunia hii” raisi alitulia kisha akapiga funda la chai.
“Jackson Aron ni binadamu pekee niliye bahatika sana kuufaidi uwepo wake ulimwenguni hapa, amenipa maisha na kunifanya niheshimike duniani kote kwa akili yake na pesa zake mwenyewe” raisi aliongea kwa uchungu kidogo akijitahidi kuyazuia machozi kwa kitambaa safi sana, Calvin alishtuka inakuwaje mtu huyo amtaje baba yake mzazi halafu aanze kulia.
“mzee samahani baba yangu anahusika vipi nawewe kulia? Sijaelewa unamaanisha nini?”
“wewe bado ni mdogo sana mwanangu ni ngumu sana kuielewa hii dunia ilivyo, baba yako ni rafiki yangu wa damu tangu tukiwa kidato cha tano mpaka siku anakufa ndiye anabaki kuwa rafiki yangu bora zaidi kuwahi kuzaliwa na mwanamke” alikuwa akiongea taratibu bila hata wasi wasi mzee huyu
“hapanaa…. inakuwaje hii, baba yangu marafiki zake nawajua vyema hapo hawakuwa wengi sikuwahi kusikia hata siku moja akilitaja jina lako, leo unaniambiaje kwamba wewe ni rafiki wa baba yangu, baba na wana siasa wapi na wapi?” alihamaki sana kijana huyu ana miaka ishirini na minne saivi hajawahi hata siku moja kumsikia baba yake akimtaja mtu huyo leo anaambiwa ndiye aliyekuwa rafiki yake wa karibu zaidi hili alilipinga kabisa na alijua halikuwa na ukweli wowote.
Calvin anaazungumzo gani ya mhimu mpaka akutane na raisi? .....ukurasa wa 37 unafika mwisho ungana nami wakati ujao.
Chao[emoji2768]
Bux the story teller
#ULIMWENGUWAWATUWABAYA
Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
OoopssHADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 40
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA.............
Alishtuka baada ya kuisikia sauti nzito sana upande wa nyuma yake, ghafla taa kali ziliwaka ambazo zilimuumiza sana macho kwa sababu alikuwa amekaa muda mrefu sana bila kuweza kuuona mwanga mahali hapo akaamua kuyafumba. Aliyafumbua macho yake, ana kwa ana alionana na mtu aliyekuwa amevaa suti moja ya bei ghali sana lakini usoni kwake alikuwa amejifunika kwa kitambaa safi kilicho mfanya aonekane mdomo, pua na macho tu.
ENDELEA.....................
“wewe ni nani?” aliuliza mwanaume huyu akiwa anakaa kitandani kwani hakuwa na uwezo wa kusogea mbaali kwa aina ya minyororo aliyokuwa amefungwa kwenye kitanda chake hicho cha chuma.
“nimeshangaa sana kwanini mfungwa ubadilishe jina kutoka Ahmed Abdulrazack mpaka Mussa Mhamed sio kawaida mfungwa kuishi kwa kuuficha utambulisho wake, unaonekana wewe ni mtu wa mhimu sana kwenye umoja wenu” raisi aliongea akiwa anatabasamu huku amemkazia macho mtu huyo. Jamaa alishtuka sana baada ya kujua kwamba utambulisho wake unajulikana kwa baadhi ya watu, yeye alijua ni watu wake tu pekee ndio wanao jua kuhusu jambo hilo.
“hahahhahhah mimi naitwa Mussa mhame……….” Aliamua kujikaza na kutoonyesha wasi wasi wake wowote lakini raisi alimkatisha `
“najua wewe ni gaidi mkubwa sana ndio maana waliamua kudanganya kwamba umekufa kwa upuuzi uliokuwa umeufanya kumbe umekuja kuhifadhiwa huku, sasa hao ndugu zako wote kuanzia kaka yako ambaye anajifanya anaishi kwa kujificha sana wanaenda kufa vifo kibaya sana halafu nitakuja kumalizana nawewe hapa hahahahahaahahha…. Mnajifanya wajanja sana kwenye nchi za watu hahahahahahaa”. Mheshimiwa raisi aliongea akiwa ananyanyuka huku akiwa anacheka sana kwa furaha. Ahmed ambaye anatumia jina lake la uongo kama Mussa aliogopa sana japo alikuwa ni gaidi mkubwa, suala la yeye kujulikana uwepo wake na ndugu yake ambaye walikuwa na mipango mkubwa sana lilimfanya aanze kutoa jasho kwani alihisi ndugu yake huko uraiani anaweza kuwa kwenye hatari kubwa sana na akiwa hapo hakuwa na namna yoyote ile ya kumsaidia kwa sababu hakukuwa na namna ya mtu kuja kukutembelea gerezani hapo kiurahisi ili imsaidie kufikisha ujumbe kwa watu wake.
“wewe ni nani mpumbavu mkubwa wewe nitakuua endapo ukijaribu kunigusia ndugu yangu” aliongea kwa jaziba mno mwanaume huyu akijaribu kuivuta minyororo hiyo kama anaweza kuikata amuue mtu huyo aliyekuwa mbele yake lakini hakuwa na uwezo wa kufanya hivyo
“kuna mtu atakuja sio muda sana ndani ya siku hizi atakupa maelekezo nini cha kufanya, huyo mtu sio binadamu wa kawaida utatakiwa kuwa makini sana unapokuwa unazungumza naye kwani mnaweza kumaliza mazungumzo ukiwa tayari hauna kiungo hata kimoja kwenye mwili wako, na kunijua mimi ni nani, siku utakayo nijua basi ujue kwamba ndiyo siku ambayo itakuwa ni mara ya mwisho wewe kuendelea kuitwa jina la mwanadamu uliye hai” raisi aliongea huku akiwa anatoka ndani humo akimalizia na kicheko “hahahahahahahahahh”.
“yule niliyekuja naye ni kijana wangu, kuna kazi amekuja kuifanya humu ndani, utaenda kwenye chumba utakacho mhifadhi keshokutwa saa za usiku atakuelekeza anacho kihitaji humu ndani, kumbuka hilo” raisi alikuwa anampa maagizo mkuu wa gereza hilo baada ya kumsubiri kwa muda kidogo kutoka huko alikokuwa kukutana na Ahmed Abdulrazack kwani hakutaka mazungumzo yake mtu yeyote ayasikie, wakati huo mkuu huyo wa gereza alikuwa anamsindikiza kutoka nje ya eneo hilo baada ya kumaliza kilichokuwa kimemleta humo ndani.
Calvin alikuwa bado hajatolewa minyororo yake wakati anapelekwa kwenye selo yake ambayo ilikuwa juu kabisa ya selo zingine na ilikuwa na huduma zote za mhimu ndani kasoro televisheni tu kwa maana watu hao hawakutakiwa kabisa kujua vitu vinavyo endelea uraiani, ulikuwa ukifungwa huko ni kama upo gizani na huwezi ukaona nuru yoyote wala kuona uzuri na ubaya wa kitu chochote kile. Wakati anapelekwa kuelekea kwenye hiyo selo yake, selo za pembeni walikuwa wanasikika wanaume walio jaa miili sana
“tumeletewa mke, mtoto mzuri huyo walah namuoa mimi hahahahhhahah” ni moja ya wababe wa kuogopeka sana ndani ya gereza hilo alikuwa akijigamba kwa sauti kubwa. Mwanaume ile kauli ilimuuma sana aligeuka tu na kumwangalia yule mtu sura, jamaa akamuonyeshea Calvin kidole cha matusi lakini hakuwa na cha kufanya kwa muda ule.
“siku mbili zikiisha ndipo utatolewa hiyo minyororo yako na hakikisha hauleti usumbufu wowote ule utaishi vizuri sana humu ndani” kauli kutoka kwa askari magereza Calvin aliweza kuielewa vyema akaingia chumbani kwake na kulala.
IKULU DAR ES SALAAM
Ndani ya ukumbi wa mikutano ikulu wanaonekana watu saba wakiwa wameizunguka meza ambayo mara nyingi ndiyo hutumika kufanyia mikutano mikubwa, mbele anaonekana mheshimiwa raisi akiwa anawatazama kwa umakini makamu wa raisi, jaji mkuu, waziri mkuu, spika wa bunge la Tanzania, mkuu wa majeshi na mkuu wa jeshi la polisi nchini. Aliwatazama kwa umakini na kuwakazia macho kwa zaidi ya dakika tano mpaka wao wenyewe walianza kujishtukia.
“viongozi wa mihimili mikubwa yote ya nchi mko mbele yangu na ni muda kidogo hatujaonana mnaweza kunikumbusha majukumu yenu mmoja mmoja?” raisi aliongea akiwa anaendelea kuwakazia macho, alikuwa hawaamini hata kidogo watu hawa tangu apate tahadhali kutoka kwa Calvin na alijua msaliti wake lazima yupo miongoni mwa hawa, isingewezekana mtu mwenye nyazifa ndogo kuweza kujaribu kumpindua kwa chini chini.
“lakini mkuu kazi zetu ziko wazi sana nadhani tungeandaa tu ripoti halafu tukakuletea ukazipitia ingekuwa vyema zaidi, ila kusema wote hapa kila mtu aanze kutaja majukumu yetu itakuwa kama hujatutendea haki ukiangalia na nafasi tulizo nazo nchini” yalikuwa ni maneno ya jaji mkuu ambaye alikuwa anaijua sheria kuliko hata anavyo lijua jina lake.
“wakati namalizia masomo yangu ya chuo kikuu niliwahi kuambiwa hakuna kitu mwanasheria atashindwa kukifanya akiamua, anaweza kuubadilisha ukweli ukawa uongo na uongo ukawa ukweli, anaweza kumpa kesi mtu asiye husika na aliye husika akaendelea kuishi maisha bora sana huku wanyonge wakiozea jela na maskini, kwa wakati ule hii ndio sababu iliyo nifanya nikaichukia sana sheria kwa sababu nilihisi inakandamiza watu ila mimi leo ndiye ninaye pitisha sheria zote nchini, aisee haya maisha yanaenda kwa kasi sana. mheshimiwa jaji mkuu nimekuelewa vizuri sana, vipi mwingine nani anaungana na mheshimiwa jaji mkuu?”. Mafumbo yasiyo julikana lengo lake ni nini yalizidi kuwaumiza watu hawa humu ndani kwa sababu raisi hakuwa wa kawaida kama walivyo kuwa wamemzoea ila leo alikuwa anaongea maneno tata sana.
“mheshimiwa nini kinaendelea? Kama kuna tatizo waweza kutuambia tukaangalia namna ya kulitatua”. Makamu wa raisi mr Alex Kweleka alizungumza baada ya kusimama.
“wakati nikiwa mdogo mama yangu aliwahi kuniambia mwanangu kwenye maisha yako unatakiwa uelewe kwamba haujawahi kushindwa ila muda wako wa kushinda ndio bado” raisi alizungumza kwa tabasamu huku akiwaangalia mkuu wa majeshi na waziri mkuu kwa zamu. Wote walibaki wanaangaliana kwa mshangao tu wasielewe nini kinaendelea lakini mheshimiwa huyu kuna kitu alikuwa anajaribu kujiridhisha ili aone kama kipo sawa kwa hawa watu au kama atapata chochote. Siku zote “simba Mwenda pole ndiye mla nyama” aljisemea mwenyewe kisha akawaangalia tena mkuu wa majeshi, waziri mkuu na spika wa bunge kwa umakini halafu akasema.
“mnaweza kwenda mwishoni mwa wiki hii nahitaji ripoti zenu za mwaka mzima” aliondoka bila kuaga kiasi cha kuwatia wasi wasi viongozi hawa wakubwa wa nchi walijua kwamba hali haikuwa nzuri hata kidogo. Mheshimiwa raisi baada ya kutoka hapo alienda kumuita mkuu wa kitengo cha ulinzi wa kielektroniki ndani ya ikulu na kumtaka amuunganishie kamera zote za ikulu haraka mno ili awe anajua kila kinacho endelea na alimtaka iwe siri kubwa sana.
Siku ya kwanza ndani ya gereza la ALL DEAD kulikuwa kumekucha salama kabisa, Calvin alikuwa kafunguliwa chumba chake muda wa kwenda kunywa chai akiwa bado na minyororo yake mwilini, alikuwa na sura ya mvuto sana kiasi kwamba wafungwa wote walikuwa wakimtazama yeye tu, ndani ya gereza hili kulikuwa na wafungwa miamoja na hamsini yeye akawa wa mia moja na hamsini na moja. Wakati anatembea kuna jamaa yule wa jana aliyekuwa amesema atamuoa humo ndani alimnong’oneza sikioni wakati anapita hapo “wewe ni wangu humu ndani”, mwanaume macho yalibadilika rangi ila hakusema chochote minyororo mingi aliyokuwa amefungwa ilimzuia kufanya kitu chochote. Hakuwa na namna alienda sehemu aka kaa ili kupata kifungua kinywa, kilikuwa ni chakula kibaya sana alivyoweka mdomoni tu akatema chote, haikuchukua hata dakika mbili kuna mabwana jela wawili walikuja na kumpiga virungu vingi sana lakini mwanaume hakuweza hata kushtuka alikuwa amekaa hivyo hivyo huku akiwa amefumba macho. Wafungwa waliokuwa karibu nae neo hilo walimshangaa sana inakuwaje mwanaume mlaini kama huyu anaweza kuvumilia kipigo cha hayo maumivu? Hawakuwa na jibu lolote lile.
Majira ya jioni ilikuwa ni kawaida sana ndani ya gereza hilo siku za wikiendi kukuta kuna mpambano kati ya wafungwa wenyewe kwa wenyewe, basi mwanaume alijisogeza hapo na kukaa kwenye sakafu, macho yake hayakuweza kutulia alikuwa akiangalia huku na huku kama ataweza kumuona mtu wake lakini haikuwa hivyo hakuweza kumuona, ilimshtua sana kwa sababu tangu jana yake hakuweza kumuona mpaka sasa. Ulingoni walikuwa wamesimama wanaume wawili mmoja alikuwa ni yule aliye ahidi kumuoa
gerezani hapo, sekunde thelathini pekee mtu yule aliweza kumvunja mwenzake mkono na mguu ikawalazimu kusimamisha mpambano, kwa maringo jamaa yule alimfuata Calvin alipokaa na minyororo yake na kumpiga piga usoni kisha akaondoka kibabe lakini wakati jamaa yule mwenye mbavu za kutosha akiwa anaishia kwenye kona moja humo ndani alisikia vizuri sana sauti ya Calvin ikisema
“kama ungefanikiwa kunifahamu hata kwa uchache sana usingetamani hata kuniona kwenye macho yako wala kuombea niwe karibu yako” mwanaume hakuweza kukaa sana akaamua kuondoka pale na askari mmoja akampeleka mpaka chumbani kwake na minyororo yake mwilini.
siku ya pili kulikucha vyema sana, Calvin akiwa ameketi baada ya kuamka alishangaa kumuona mkuu wa gereza akifungua mlango huo ili kuingia ndani, alitulia tu kumuangalia mzee huyo anafanya nini, mzee huyo hakuongea sana alimfungulia minyororo yake yote halafu akakaa pembeni yake.
***************************
“una bahati sana kijana wangu, ni mara chache sana huwa namuona raisi huyu akimpa mtu ofa kama yakwako, haijawahi kutokea mtu akafungwa ndani ya gereza hili na raisi akahitaji tumsikilize anacho kihitaji nadhani utakuwa silaha yake kubwa sana kwenye mambo yake” mkuu wa gereza alikuwa akiongea huku akiwa anamuangalia Calvin vizuri, mwanaume alitabasamu tu kisha akatamka sentensi fupi sana
“wanadamu tumeumbwa na ubinafsi wa kujipendelea sana na huwa wasahaulifu mno” Calvin aliongea akiwa anaendelea kujinyoosha baada ya kukaa ndani ya minyororo kwa siku mbili nzima
“unaweza ukaenda moja kwa moja kwenye pointi yako unamaanisha nini?” mkuu wa gereza hili haluelewa hivyo akauliza ili afafanuliwe vizuri.
“una kichwa kigumu mno tutapoteza muda mwingi sana nikianza kukuelewesha kila neno, leo usiku nahitaji nikutane na huyo mtu ambaye raisi alikuja kumuona” mwanaume hakuwa hata na tone la wasi wasi
“una uhakika gani kama raisi alimuona na ulijuaje kama raisi ataenda kumuona huyo mtu baada ya kufika hapa?”
“sina imani kama utakuwa na familia maana utakuwa baba wa hovyo sana, umeikosa elimu ya duniani kwa kukariri elimu ya darasani ndio maana vitu vidogo unaanza kuhangaika, unashindwa kujiongeza kwamba kwanini raisi alisema unisikilize au unadhani npo kwa bahati mbaya hapa, nishachoka kuongea naomba uondoke humu nina mambo mengi ya kuwaza” Calvin aliikunja sura yake mkuu wa gereza hakuwa na namna zaidi ya kuondoka japo hizi kauli kutoka kwa mtoto ambaye alikuwa hata na uwezo wa kumzaa ndiye aliye kuwa anamtamkia kwa ujasiri zilimkera sana ila hakuwa na namna alijua akifanya lolote mheshimiwa raisi hataweza kumwacha salama.
Ilifika mchana majira ya kwenda kupata chakula ndio muda ambao Calvin alitoka chumbani kwake tangu aamke asubuhi, alikuwa akitembea taratibu mno akiwa anaangalia baadhi ya mazingira humo ndani, alifika sehemu yake ya kulia chakula, lakini kabla hata hajaanza kula yule mwanaume anaye msumbua kila siku alitabasamu sana kitu kilicho washangaza wafungwa wengi sana mle ndani kwani huyo jamaa alikuwa akiogopeka sana. wakati mwanaume huyu anaingia wafungwa wengi walikuwa wakiinama kama ishara ya kutoa heshima lakini mwamba alikuwa amekaa akiendelea kula chakula bila papara yoyote.
“we mrembo wangu kwahiyo haujajua bado namna ya kuishi humu ndani kama wenzako sio?” Calvin alishtushwa na sauti ya mwanaume iliyo kuwa ikiunguruma kutoka nyuma, alikuwa anaikumbuka vyema kwahiyo hakuhangaika kugeuka nyuma akaendelea kupata chakula chake.
Mwanaume huyo aliona kama dharau alisogea hapo haraka ili amuadabishe kijana mdogo huyu aliirusha ngumi yake kwa hasira mno lakini kilicho tokea hapo kilimshangaza kila mmoja humo ndani, kwa kasi ya hali ya juu Calvin alijizungusha hapo alipokuwa amekaa na kugeuka kwa kasi sana aliudaka huo mkono uliokuwa umelenga kumpiga kisha akauzungusha kwa nguvu na kuachia ngumi kali sana kwa huyo mtu aliyo pelekea mkono kupinda kabisa na kuvunjika, jamaa aliguna kwa maumivu lakini hakuamini kama mtoto wa aina hiyo anaweza kumpiga, alijikusanya kwa mkono mmoja ulio baki na kuurusha kwa nguvu aliambulia kupigwa teke la mbavu lililo mfanya akainama chini bila kupenda wakati bado haja nyanyuka alikutana na viganja viwili vya mikono kichwani na kumfanya apoteze uwezo wa kusikia kichwa kilikuwa kinamuua mno alihisi kimepasuka. Wakati hali hiyo inaendelea walifika vijana wake watatu kwa hasira walimfuata Calvin ambaye alikuwa tayari amesha rudi kukaa na kuendelea kula chakula chake. Huwa hapendi kupotezea muda mwanaume huyu hivyo alinyanyuka akiwa na hasira alicho wafanya hawa vijana watatu ni kuwavunja miguu yao yote na mikono kisha akaondoka zake kurudi kwenye chumba alicho kuwa amepangiwa. Mkuu wa gereza alifika eneo hilo na kuwabeba hao wafungwa wanne ili wakatibiwe wala hakuongea chochote, ila ile hali iliwafanya wafungwa wengine wamuogope sana Calvin baada ya kufanya mambo ya kutisha sana kwa dakika zisizo zidi hata tano.
Ukurasa wa 40 unafika mwisho ungana nami tena wakati ujao. Langu jina naitwa Bux the story teller.
Chao[emoji2768]
#ULIMWENGUWAWATUWABAYA
Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
SafI tuko pamojaHADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA

Leo wikiend jipatie hadithi ya ULIMWENGU WA WATU WABAYA na kuimalizia mpaka mwisho kwa shilingi 3000 tu pekee mpaka ukurasa wa 76.HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 41
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA.............
Huwa hapendi kupotezewa muda mwanaume huyu hivyo alinyanyuka akiwa na hasira alicho wafanya hawa vijana watatu ni kuwavunja miguu yao yote na mikono kisha akaondoka zake kurudi kwenye chumba alicho kuwa amepangiwa. Mkuu wa gereza alifika eneo hilo na kuwabeba hao wafungwa wanne ili wakatibiwe wala hakuongea chochote, ila ile hali iliwafanya wafungwa wengine wamuogope sana Calvin baada ya kufanya mambo ya kutisha sana kwa dakika zisizo zidi hata tano.
ENDELEA.......................
“kaeni mbali na yule mtu mtakufa wote wapuuzi nyinyi” mkuu wa gereza alifoka kwa hasira wakati anaondoka mahali hapo kwenda kuwapatia matibabu wanaume hao wanne walio jeruhiwa vibaya na Calvin, aliwatahadhalisha wafungwa hao kwa sababu hata yeye alipewa onyo mapema sana na mheshimiwa raisi kuchunga mdomo wake anapokuwa mbele ya kijana huyo ni mtu hatari sana licha ya kuwa na sura nzuri inayoweza kukudanganya kwa tabasamu lake zuri.
Ndani ya miongoni mwa hoteli bora mno katika jiji la Dar es salaam inayopatikana ndani ya Mikocheni iitwayo The Amariah Boutique Hotel, ni hoteli nzuri sana yenye kila urembo wa kuvutia, ndani ya ukumbi wa mikutano wanaonekana baadhi ya watu wakiwa wameizunguka meza iliyokuwa mbele yao wakionekana wanamsubiri mtu. Dakika mbili baadae kuna mwanaume aliyekuwa anaonekana kuwa mtu mzima kidogo akiwa amevalia suti nyeusi nzuri mno iliyokuwa imeshonwa kwa ustadi mkubwa kupita kiasi lakini sura yake ilikuwa imefunikwa na barakoa huko kichwani akiwa amevaa kofia kubwa kiasi kwamba usingeweza kumtambua hata kidogo kwamba alikuwa ni nani mtu huyo na humo ndani kulikuwa na nini hasa. Wakati anaingia watu wote walisimama na kutoa heshima kwa kuinama naye akawajibu kisha akaenda kukaa sehemu yake ambayo ilikuwa imeandaliwa maalumu kwa ajili yake.
“ni vizuri sana leo mmefika wote kwahiyo mnisikilize kwa umakini, mipango yetu ilikuwa inaenda vizuri sana kabla ya huyu mtoto kujitokeza, baada ya ujio wake ndipo matatizo yameanza, shida yangu nilitaka arudi ili tuweze kufanikiwa kumpata ili tuchukue mali zake zote alizo achiwa na mzee wake kabla ya uchaguzi kufika lakini umefanyika uzembe mkubwa mno na wa kipumbavu kushindwa kulikamilisha hilo ndani ya miaka miwili iliyoweza kupita nyuma, kwa sasa inatakiwa auawe haraka sana na hizo mali nitazichukua kwa ulazima kwani zitakosa msimamizi. Sasa amekuwa ni mtu wa hatari sana upande wetu, nilishangazwa sana amewezaje kuwaua makomando wote wale peke yake lakini nimekuja kugundua kwa sasa sio kiumbe wa kawaida hata wa kuombea kukutana naye na nadhani kuna ishu anaifanya na mheshimiwa raisi ambaye ghafla sana amebadilika bila kuweka wazi sababu ni nini, inaonekana kuna mambo alishaweza kuyahisi kwahiyo umakini mkubwa sana unahitajika juu ya hili jambo vinginevyo tutafanya vitu vya hovyo sana sitaki uzembe ulio jitokeza ujirudie tena” mtu huyo alikuwa akiwaelezea watu wake ambao walikuwa mbele yake baada ya kushindwa kukitekeleza kile alichokuwa amepanga kukifanya
“mzee nimekuelewa vizuri sana lakini nilitaka kujua kwanini uliamua kumuua Fabian Decco ingali ulijua yeye ndiye msaada wa pekee?” aliuliza swali mwanaume mmoja aliyekuwa mdogo kuliko wote humo ndani.
“imetumika zaidi ya mwaka mzima kumshawishi kwa nguvu ili akubali kuifanya kazi yangu lakini hakuonyesha ushirikiano wowote wa kueleweka zaidi ya kuweka ahadi za uongo tu, nilijua anaweza kuja kuwa hatari kwetu sisi wenyewe kama angefanikiwa kukutana na huyo mtoto na akaweza kumpa baadhi ya siri zetu japokuwa mimi hanifahamu lakini sikuwa na uhitaji naye sana” alijibu kwa sauti kavu mzee huyu huku akiwasha sigara yake ya bei ghali mafunda mawili bila kujali hali ya wengine kama wataipenda au hawataipenda.
“sasa tutakuaminije mzee mwisho wa siku ukimhisi tu mtu unamuua si utatumaliza wote humu ndani” kijana huyo aliyekuwa ameuliza swali la kwanza aliongea kwa ghadhabu huku akiwa amesimama bila hata kuruhusiwa kitu kilicho pelekea mzee yule kumwangalia kwa jicho la hasira sana, haizikuisha hata sekunde thelathini waliingia wanaume wawili wenye suti nyeusi walimfuata yule bwana mdogo mmoja akiwa na mfuko wa plastiki na kisu, alichinjwa kama kuku na damu yake akikingwa kwenye mfuko huo ili asichafue hali ya humo ndani. Aliuawa kikatili mno mbele ya watu wengine kwenye mkutano huo ukiwa unaendelea, iliwatisha sana hiyo hali hivyo iliwalazimu kufunga midomo yako yasije yakawakuta kama yaliyo mkuta mwenzao.
“nilisha waonya, kunisimamia bila ruhusa kama umenioa na kuuliza swali mara mbili mbili ni kosa na dharau kubwa mno kwangu, mtoto mdogo kama huyo anapata wapi ujasiri wa kunipigia kelele hahahahahahahahhahahhahah………., nawapeni siku mbili kabla sijaingia mimi mwenyewe kazini mniletee ripoti kwamba bwana mdogo yuko wapi mkishindwa yatawakuta yaliyo mkuta mwenzanu” alitoka kwa ghadhabu sana mzee huyu baada ya kumaliza kuongea, siku yake ilikuwa tayari ilisha haribika. Alivyo fika nje alipiga simu moja sehemu.
“makomando wote kumi na tano walio hifadhiwa msituni huko nawahitaji kesho wawe wamefika hapa haraka sana huko kambi ivunjwe wahamishiwe Dar es salaam na utasimamia kila kitu, sitaki uzembe ufanywe hata kidogo juu ya hili jambo” kisha akakata simu na kuondoka mahali hapo.
ALL DEAD PRISON
Majira ya saa saba za usiku ndani ya gereza hili alionekana mkuu wa gereza akielekea katika chummba cha Calvin, alifika na kufungua mlango hawakuongea chochote zaidi ya Calvin kuanza kumfuata nyuma mzee huyu, walifika sehemu na kuanza kushuka ngazi za chini kwenye moja ya selo zilizokuwa huko chini. Walifika sehemu mkuu huyu wa magereza akaonyesha mkono kwenye selo iliyokuwa mbele yake kwamba ndipo mahali alipokuwa anahitajika mtu huyo kwenda.
“washa taa za huko chini baada ya dakika mbili zijazo na uniandalie safari ndani ya masaa mawili yajayo ninatakiwa kuwa nje ya hapa haraka sana na uandae safari ya watu wawili kabla wafungwa wengine kuamka” alikuwa anamwambia maneno hayo mkuu wa gereza lakini aliondoka haraka baada ya kusikia kelele za mwanaume mmoja akiomba msaada huko chini. Mlango ulikuwa wazi hivyo aliingia na kutoa mguno kitu kilicho mshtua mno Ahmed Abdulrazack kwani hakuna mfungwa hata mmoja aliye kuwa anaruhusiwa kuingia kwenye selo ya mtu huyo kutokana na uhatari wake.
“nani wewe?” aliuliza swali huku akiwa anaacha alichokuwa anataka kukifanya kwa mwanaume mwenzake humo ndani, hakujibiwa chochote, ilimbidi kuuliza tena kwa hasira na sauti kali “nani wewe mpu…..” lakini alikatishwa na mwanga wa taa kali ulio muumiza macho, alivyo yafumbua mbele yake alikutana na sura ya kijana mdogo tu akiwa ameyafumba macho yake, ghafla Calvin aliyafumbua macho yake kwa mara ya kwanza alifanikiwa kuiona sura hiyo ambayo aliweza kuiona vyema sana kwenye frash aliyokuwa amepewa na Mr Fabian Decco alitabasamu baada ya kuona mtu huyo amefunguliwa minyororo yake kama alivyo taka kumkuta akiwa yupo huru kabisa ili waongee kiutu uzima, kwa pembeni alikaa mfungwa mmoja ambaye alikuwa akitia huruma kwa kitendo alicho kuwa anataka kufanyiwa na mwanaume huyo, ilimuuma sana Calvin alichukia sana kuona mwanaume mwenzake anafanyiwa kitendo kama hicho hivyo akamuonyesha mfungwa yule ishara ya kuondoka mle ndani naye hakufanya ajizi alikimbia sana jamaa yule akiwa haamini kama kapona hakujihangaisha hata kutazama nyuma tena kujua usalama wa mtu aliye msaidia.
“hahahahahahhaha, bwana mdogo huo ujasiri wa kunitolea mtu wangu unautolea wapi? lakini hata wewe ni mrembo sana unanifaa hahahahahahahahah……” alicheka mno Ahmed akiwa anafurahia sana kumwona huyo kijana mbele yake.
“haya unayo yatenda ndivyo ulivyo funzwa kwenu na mama yako?” mwanaume aliufungua mdomo wake akiwa ndani ya selo hiyo kubwa kiasi yenye kitanda tu pekee kwa mara ya kwanza
“dogo una bahati mbaya sana kuingia kwenye hili gereza kwa umri wako huo ulipaswa umalize kunyonya kwanza mambo ya humu huyawezi wewe ni mlaini mno, leo nataka uyafahamu maisha ya gerezani ili siku nyingine ukisikia neno gereza uwe unakimbia kijiokoa, huku hawaishi binadamu ni kama tuna miili ya wanadamu lakini nafsi zetu ni za kishetani, naenda kukufanyia mambo mabaya sana ambayo yatakufanya kila ukilala uwe unaota kwa kuogopa kila unapo iona sura yangu au kuisikia sauti yangu popote pale hahahahhahahah..” Ahmed Abdulrazack aliongea kwa kujigamba mno.
“nadhani siku mbili zilizo pita kuna mtu ambaye nina uhakika hukumjua hata kidogo alikuja hapa akaongea nawewe na alikutahadhalisha namna ya kuutumia mdomo wako unapokuwa una ongea namimi” Calvin aliongea akiwa bado ameuweka mkono wake nyuma bila wasi wasi wowote ule , Ahmed alishangaa sana na kucheka kwa dharau yaani mtoto mdogo sana kwake mwenye sura ya mvuto ndo aliambiwa auchunge sana mdomo wake mbele yake, alicheka mno mtu huyu kumdharau Calvin kwani hakufanania kabisa na maneno aliyokuwa anayazungumzia.
“juzi umeongea na mheshimiwa raisi kistaarabu na kubembelezwa leo upo namimi kuna maswali kadhaa ambyo ujibuji wako ndio utakao fanya nifanye maamuzi ya kumuua kaka yako au nimuache hai pamoja nawewe mwenyewe” Calvin alikuwa akiongea huku akisogea alipokuwa mtu huyo. Ahmed alishtuka na kuogopa sana baada ya kusikia alikuwa anaongea na mheshimiwa raisi, jasho lilianza kumtoka mno kwa sababu mipango yao ilikuwa ni kumpindua bila yeye mwenyewe kujua chochote wakati wa uchaguzi ikiwezekana hata kumuua kama ikishindikana kumtoa madarakani lakini kuambiwa aliongea na raisi ilimaanisha anajua kila mpango wao na ni kitu cha hatari mno mtu huyu kuwahi kukisikia kwenye maisha yake, alijitahidi kujikaza ili asionekane kama yupo kwenye hiyo hali lakini ilishindikana alikuwa akitokwa na jasho jingi mno,
“kaka yako yuko wapi na bosi wenu ni nani?” mwanaume aliuliza kwa sauti ya mgandamizo baada ya kuona mtu huyo hamjibu chochote kile.
“kwa sababu unaonekana ushaanza kuyajua mambo yetu baadhi inabidi nikuue humu humu ndani bila mtu yeyote kujua” aliongea mwanaume huyu kwa hasira huku akiwa anakuja kwa kasi sana kitu kilichi mfanya Calvin atabasamu mno. Ahmed alirusha ngumi mbili za nguvu zilizo mpata vizuri Calvin tumboni na wala hakuhangaika kuzikwepa alikuwa anahitaji kuupima uwezo na uzito wa ngumi za huyu mtu, zilimrudisha nyuma hatua kadhaa kisha alishtukia teke kali kwenye paja lake, lilimfanya akauma meno kwa nguvu kwani sehemu hiyo alikumbuka alipigwa kisu na Scot na palikuwa hapajapona vizuri bado.
Bux the story teller, KOMENTI NA KULIKE KWENYE PAGE YANGU
“ndugu yangu unataka kuniua siriasi kumbe kwahiyo tutaongea kwa amani au mpaka tuvunjane kwanza mifupa?” aliuliza macho yake yakiwa yamebadilika na kuwa mekundu, Ahmed hakumjibu alikuja tena lakini alikutana na ngumi nzito mno kwenye mkono wake iliyo mfanya aunyooshe mkono wake ulio kuwa umeanza kumuuma sana kabla hajamaliza Calvin alikuwa amefika alipeleka teke zito lililo mpata Ahmed kwenye kichwa chake na kujibamiza ukutani karibu na kitanda chake, baada ya kuona anaanza kuelemewa aliichomoa mnyororo mmoja uliokuwa umeunganishwa na kitanda chake cha kulalalia hicho. Aliurusha kwa haraka sana lakini ulidakwa na mwanaume alikuwa anauzunguka mnyororo huo kwa kujiviringisha haraka sana alimfikia mtu huyo na na kumpiga ngumi moja mbaya sana maeneo ya shingoni, Ahmed aliuachia mnyororo huo na kulegea kabisa alikuwa amezimishwa, Calvin aliitoa sindano ndogo sana akamchoma Ahmed shingoni halafu kuna dawa akamnusisha puani.
“masaa ishirini na nne utakayo amka yatakukutia sehemu ambayo utanieleza kila kitu” aliongea hivyo huku akimbeba mwanaume huyo, kwa aina ya sindano aliyo mchoma kama asingemnusisha hiyo dawa basi asingeweza kumaliza hata dakika kumi alikuwa anakufa moja kwa moja.
Mwanaume alinyoosha kuelekea mlangoni ambapo alimkuta mkuu wa gereza akiwa anamsubiri na mzee huyu hakuuliza chochote kwa sababu alijua mtu huyo alikuwa mahali hapo kwa niaba ya raisi maana yake kama angemsumbua ilikuwa inakula kwake kama mtu huyo angefikisha taarifa yake kwa mheshimiwa raisi. Walitoka mpka nje kabisa ya gereza hilo, waliikuta helikopita ya dharura ikiwasubiri mahali hapo, mwanaume aliomba simu moja akapewa kisha akamshukuru mkuu wa gereza kwa kutamka.
“mzee sitausahau kamwe msaada wako huenda siku moja tutakutana tena”, mwanaume akatoa saluti na kupanda helikopita baada ya kumpandisha mtu wake kisha wakaondoka mahali hapo na rubani wa gereza hilo.
BAGAMOYO, TANZANIA
Ni mji ambao unadaiwa kugunduliwa mwishoni mwa karne ya 18 japo unasemekana kuwa ni mji ulio panuliwa kutoka kwenye mji wa zamani sana wa makazi ya waswahili ulio julikana kama Kaole mnamo karne ya 8, ni mji ulio kuwa umechaguliwa kuwa makao makuu wa ya wajerumani Afrika Mashariki wakati wa utawala wa kikoloni wa wajerumani. Bagamoyo ni eneo linalo patikana katika pwani ya bahari ya hindi ndipo mahali ambapo helikopita iliyokuwa imembeba Calvin iliweza kutua kutokana na maelekezo ya Calvin mwenyewe, mwanaume alishuka na mtu wake huku akimpa ishara ya heshima rubani huyo aliye weza kuwaleta mahali hapo kisha helikopita hiyo ikaondoka kwa kasi kurudi ndani ya visiwa vya pemba mida hiyo ya saa kumi za usiku. Mwanaume alitembea akiwa amembeba mtu huyu kwa nusu kilomita aliweza kufika kwenye nyumba moja kubwa sana ambayo ilikuwa ipo ufukweni kabisa mwa bahari, aliweka kidole chake getini na geti likafunguka, kwenye mlango wa kuingilia ndani alikutana na mlango mgumu sana ulio tengenezwa kwa madini ya shaba, mwanaume aliweza kusogeza jicho lake kwenye hicho kitasa na mlango ukafunguka kwa wepesi mno, alitabasamu baada ya kuona picha ukutani akiwa yeye mama yake pamoja na baba yake.
Ilimkumbusha historia ya miaka mingi sana katika eneo hilo, hiyo ni nyumba ambayo baba yake aliweza kumnunulia akiwa anamalizia masomo yake ya sekondari, ni siku moja walipokuja kupumzika wikiendi kwenye nyumba hiyo alijikwaa na kuanguka hakuumia ila alijifanya kama amezimia kuona wazazi wake watafanya nini, mama yake alichanganyikiwa sana huku akiwa anatoa machozi akimkumbatia mtoto wake, baba yake alikuwa akihangaika kumpigia simu daktari wake aweze kufika haraka mno maeneo hayo, dakika moja tu aliamka akiwa anatabasamu basi wazazi wake walimfinya mashavu wakimtaka aache kuwatisha huku wakifurahi sana.
mwanaume kumbu kumbu hizo zilikuwa zinamuumiza sana kwani watu hao hakuwa na uwezo wa kuwaona tena kwenye upeo wa macho yake, aliikunja ngumi yake kwa hasira na kukipasua kiti kidogo kilicho kuwa karibu na sofa mahali hapo, alimuangalia mtu wake kwa hasira akaamua kwenda kumfungia kweny stoo akimsubiri kwa hamu sana aweze kuamka aongee naye vizuri.
41 natundika daruga till next time
Bux the story teller
Chao[emoji2768]
LIKE NA KUKOMENT KWENYE PAGE YANGU
#ULIMWENGUWAWATUWABAYA
Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Hiki ndicho kitabu changu bora zaidi cha kijasusi kuwahi kukiandika mpaka muda huu.......idea generation, mpangilio wa matukio, uwingi wa nchi na wahusika..Dope..... Tanzania X Japan [emoji119]......it's a movie not a tale ULIMWENGU WA WATU WABAYA [emoji2768]Leo wikiend jipatie hadithi ya ULIMWENGU WA WATU WABAYA na kuimalizia mpaka mwisho kwa shilingi 3000 tu pekee mpaka ukurasa wa 76.
Namba za malipo ni
0621567672 (WhatsApp)
0745982347
Jina FEBIANI BABUYA
Ukilipa tu nicheki unatumiwa hapo hapo[emoji3578]
Ndiyo mkuuTuendelee tuendelee Leo weekend
Ndiyo mkuu
Leo nipo home tu kwahiyo mtakula madini ya kutosha mtasoma kurasa mbili [emoji2768]Ndiyo mkuu
Hapo Sawa ngoja niagize popcorn kabisa maana hii sirizi haitaji usumbufuLeo nipo home tu kwahiyo mtakula madini ya kutosha mtasoma kurasa mbili [emoji2768]
Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Goodbye mpaka wakati mwingine tena[emoji112]HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 46
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA...........
"Hahahahahahaha kama umenishindwa mimi hivi unaweza ukasimama na Baruan Mahafidhu hata dakika moja kweli wewe, lazima ufe kwa upumbavu ulio ufanya wa kumuua mdogo wangu" alitamka kwa uchungu sana Abdul Ahmed kwa maumivu makali ya mkono aliyo kuwa akiyasikia mahali hapo, aliinama chini na kuibeba bastola yake ili ammalize Calvin.
ENDELEA.......................
Kilifanyika kitendo cha kushtukiza mno, wakati Abdul anainyanyua bastola ghafla aliitupa kwa maumivu makali sana ya mguu, star ilikuwa imeukata mguu vibaya, sekunde za kuhesabu upanga ulikuwa umeutengenisha mguu wake, alilia sana mwanaume huyu hakuamini kama mguu wake hakuwa nao tena mguuni aligeuka nyuma kuangalia alikutana na Calvin akiwa ameushika upanga wake vyema kabisa, alitaka kukimbia kwa namna mtu huyo alivyo kuwa anafanya mambo ya kikatili lakini haikuwezekana kabisa kufanya hicho kitu kwa sababu hakuwa na mguu tena wakati wote alikuwa amekaa chini akitoa machozi ya uchungu. Calvin hakuwa na huruma na watu hawa hata kidogo na alikuwa ashaahidi kubadilika kuwa kama walivyo kuwa wametaka, aliunyanyua upanga wake tena na kuukata mguu ulio kuwa umebaki hivyo mpaka wakati huu Abdul hakuwa na mguu wowote jina lake lilikuwa limebadilika na kuwa kilema huku akiwa ameachwa na mkono mmoja tu pekee. Calvin aliinama bila kuongea, akaingiza mkono kwenye mfuko wa Abdul kisha akatoka na ile frash ambayo ilikuwa na siri zote za Abdul tangu siku ya kwanza kuingia Tanzania, wakati ananyanyuka hapo ilimuwekea star moja mbele yake mwanaume huyo katili kutoka Afghanstan. Kuna kosa moja kubwa sana alilifanya Abdul wakati wa kuinama chini hilo ndilo lililogharimu maisha yake yote .
“itumie hiyo ili uepukane na aibu inayo enda kukukumba hata mbele ya mabosi zako pamoja na wananchi ulio waonea sana kama wakifanikiwa kukuona kwenye hiyo hali” Calvin alitamka kwa msisitizo kisha akalizungusha panga kutoka kwenye sikio la upande wa kulia mpaka sikio la upande wa kusho la Abdul, alikuwa ameyakata macho kikatili sana na haikufaa hata kutazama hilo tukio, Abdul alijuta kuwa mwanadamu aliye zaliwa zama moja na huyo kiumbe aliyekuwa mbele yake kwani mpaka muda huo alikuwa ni kilema wa miguu yote na mkono mmoja haikutosha akapofuliwa kwa kukatwa macho yake ambayo ndiyo yalimuwezesha kuona kila kitu cha dunia alilia sana usingeweza kudhani huyu ndiye aliye kuwa katili wa kuchukua roho za watu kila alipokuwa anataka yeye, yeye na mdogo wake waliishia pabaya na walikufa vifo vibaya sana. mwanaume baada ya kufanya hicho kitu hakuweza kusimama alikuwa anaondoka taratibu kwani hali yake ilikuwa mbaya sana baada ya kupigwa risasi sehemu ya kifuani na ilikuwa imekaa muda mrefu hivyo ilimpelekea kupata maumivu makali mno lakini hakuwa na namna ya kubaki hapo ilikuwa ni lazima aondoke. Huku nyuma Abdul alibaki kama mwanadamu mnyonge zaidi kuwahi kuishi duniani aliwaza sana anaenda vipi kuishi maisha akiwa kwenye hali hiyo, aliwaza namna wanadamu walivyo kuwa na dhihaka kwa watu wenye mapungufu au ukilema bila kujua ni mipango ya MUNGU japo kwa yeye alikuwa amejitakia mwenyewe, hakuona sababu ya kuendelea alipapasa mbele yake kwa shida akafanikiwa kuipata star ambayo Calvin alimuachia hapo ili imsaidie kupunguza maumivu ya kuendelea kuishi akiwa hivyo basi mwanaume alijikata shingo yake haikuchukua hata dakika moja mwamba huyu wa kutisha akawa ameyafumba macho yake ambayo asinge weza kuyafumbua tena mpaka siku ya hukumu kwa MUNGU, maneno ya Calvin ya kumtaka mwanaume huyu ajiue mwenyewe yalikuwa yametimia.
“nooooooooooo, hapanaaaa haiwezekani haiwezekani” ilikuwa ni sauti ya uchungu ulio pitiliza kutoka kwa Victor baada ya kupatiwa taarifa na Luciana kwamba rafiki yake Alex hawakuwa naye tena katika uso wa dunia baada ya kuuliwa kikatili san ana moja ya watu walio kuwa wanahitaji kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria kwa matukio waliyo kuwa wanadhaniwa kwenda kuyafanya. Wakati huo walikuwa ndani ya ofisi ya mheshimiwa mkurugenzi wa usalama wa taifa na ndiko mwili wa Alex ulikuwa umehifadhiwa, hawakutaka mwili huo uende kwenye mikono ya polisi kwa sababu walikuwa wameshajua kilicho sababisha kifo chake hivyo hawakuhitaji mambo yawe mengi kuhangaika na polisi. Watu wote humo ndani ikiwemo mkurugenzi wa usalama wa taifa na viongozi wengine wa juu sana pamoja na THE RED SQUARD walikuwa wakimuonea huruma sana mwanaume huyo kwa namna alivyo kuwa akitoa machozi mbele ya rafiki yake.
Bux the story teller nicheki kwenye page yangu kisha ukomenti na KULIKE
“kwenye maisha ukiona mwanaume analia sana na kutoa machozi namna hiyo unapaswa kumuonea huruma sana jua hilo ni jambo ambalo limemgusa mno na huenda maumivu yake ni makubwa kiasi kwamba kama ni mtoto wa kike asinge weza kuyavumilia” Luciana alikuwa akiongea haya maneno na Sebastian ambaye alikuwa karibu yake, akaenda kumshika bega Victor na kumuomba amfuate, alimpeleka kwenye moja ya chumba kimoja kikubwa ambacho kilikuwa na baridi sana humo ndani, ulitolewa mwili ndani ya jokofu na rasmi sasa Victor alia mini kwamba rafiki yake hakuwa naye tena kwenye haya maisha. Ikabidi Luciana amuache amalize uchungu wake humo ndani, mwanaume hakuweza kuyazuia machozi yake alilia sana kwani aliye kuwa amelala mbele yake alikuwa ni mtu mhimu sana kwenye maisha yake tangu wakiwa wadogo mpaka jeshini, hakubahatika kuwa na ndugu hivyo huyu kwake alimchukulia kama kaka, alikumbuka namna walivyo kuwa wanacheka na kufurahi pamoja, utani mwingi wa Alex akimkumbusha kuoa ulimtoa machozi sana. baada ya saa moja kupita aliweza kutoka ndani huko baada ya kulia kwa muda mrefu na machungu yake kuisha alirudi kwenye ukumbi wa mikutano alifanikiwa kumkuta Luciana akiwa anamsubiri pale wengine walikuwa wametoka nje.
“hivi mmefanikiwa kumjua aliye weza kufanya hiki kitu kwa ndugu yangu? Kwa maana nilisikia anapewa maagizo aje kuwasaidia airport ajabu nyie wote mpo salama kabisa shida nini?” Victor aliuliza akiwa anapokea kinywaji baridi kutoka kwa Luciana.
“tangu tumefika hapa Deogratius umemuona?” ilikuwa sauti ya Luciana akiuliza
“mhhhhhh imenishangaza kidogo yeye kuto kuwepo hapa nikajua huenda kuna kazi amepewa kufuatilia” Victor alijibu huku akipiga funda la kinywaji hicho lililo kuwa linamsaidia kupunguza hasira kifuani kwake
“siku ya pili leo bado hajaamka, asubuhi amechezesha mikono yake mpaka jioni nadhani atakuwa kwenye hali yake ya kawaida” Luciana alikuwa akielezea huku akisikitika.
“huyo mwanaume ni nani?” Victor alikuwa ameelewa kwanini Alex alikuwa amekufa baada ya maelezo mafupi kutoka kwa Luciana.
“sina taarifa zake nyingi sana ila ndiye kiongozi wa hawa makomando 15 ambao mpaka sasa wote wamefanikiwa kuingia nchini na inasemekana ni mtu hatari mno akikufikia, tulitakiwa kuwazuia mapema, walikuwa watatu pekee kwa siku ya jana pale uwanjani na nilifanikiwa kuwaona kwa macho yangu mwenyewe lakini dakika moja tu kamera zilipoteza uwezo wa kufanya kazi wakati zinarudi kwenye hali yake walikuwa wameshapotea, getini kulikuwa na wenzangu na Deogratius alikuwa pale mapokezi na mimi nilikuwa na Sebastian kwenye chumba cha kamera. Nadhani nilivyo toa taarifa kwa vile hawakupitia mlango wa mbele wa kutokea Deogratius alitambua kwamba ni lazima wangetumia mlango wa dharura na ndiyo sababu akaenda kule japo hatukuelewa kilitokea nini tulimkuta amezimishwa tu hiyo ilitupa maswali mengi sana kwanini aliachwa hai na yule mtu nadhani hilo atalijibu akiamka, katika kufuatilia ile njia ya dharura ndipo mbele nilikutana na damu nyingi sana nilivyo angalia pembeni nilifanikiwa kuuona mwili wa Alex ukiwa umetapakaa damu sana, nilishangaa mno kwa sababu Alex sikujua kama atahusishwa kwenye kazi hii”. Luciana alikuwa akielezea huku akijaribu kuvuta hisia za tukio la jana kwa umakini mkubwa.
“hii ni hatari kubwa sana kwa taifa, sijajua ni kwa nini ila sio kawaida makomando zaidi ya kumi na tano wanaamuaje kuiasi nchi yao bila sababu ya msingi?” sasa hao si hata ikulu wanaweza kuichukua kabisa, watu kumi na tano wenye mafunzo kama yetu wanapo ungana pamoja ni jambo la hatari kubwa kupita kiasi, mimi huyo jamaa nitamtafuta mwenyewe lakini tunahitaji msaada wa yule bwana mdogo kwa hapa tulipo fikia ni pabaya sana tunaweza kuishia pabaya kama kilicho mkuta rafiki yangu” Victor wakati huo alikirusha kikopo kwenye sehemu ya kuhifadhia taka akiwa anajinyoosha
“mhhhhhh… sio kirahisi namna hiyo yule bado ni muasi na anatafutwa sana na usalama ni suala gumu sana kuungana na mtu ambaye anajichukulia sheria mkononi hata wakuu hawawezi kulikubali hili” Luciana aliona hicho ni kitu kisicho wezekana.
“niliwahi kuambiwa kauli moja na rafiki yangu kwamba kama hauwezi kushindana naye basi ungana naye tu, yule pale uwezo wake ni mkubwa sana kuliko sisi hapa kama akitukubalia kushirikiana nasisi tunaweza kulimaliza suala hili kiurahisi sana ila bila hivyo tunaenda kuwapoteza watu wengi sana, fikiria kwa umakini sana ili tujue nini tunaenda kukifanya” Victor alikuwa akiongea wakati huo alikuwa anatoka mahali hapo na kumuacha Luciana akiwa mwenye maswali mengi sana.
Ndani ya bahari ya hindi kati Kati kabisa linaonekana meli kubwa la kifahari na humo ndani ndiyo iliyo kuwa kambi ya hawa makomando 15 wakiongozwa na Baruan Mahafidhu, Kwa mbali ilionekana boti moja ya kifahari ikiwa inakuja kwa mbali ilivyo karibia Baruan alienda kumpokea mwanaume aliye kuwa anashuka humo ndani, alipiga saluti kwa heshima kubwa lakini hakuitikia, walinzi wake wanne ambao alikuwa nao kwenye boti hiyo walitaka kumfuata lakini aliwapa ishara ya kubaki humo. Baruan alishtuka kuwaona watu hao mahali hapo kwani alishawahi kuziona picha zao wakiwa wana tafutwa na umoja wa mataifa na aliwajua vyema ni watu wa kutisha sana wanapo pita popote pale alitamani kuuliza kitu Kwa waziri mkuu lakini akasita. Baruan ndiye alikuwa mkono wa kulia wa mheshimiwa waziri mkuu, ni kijana wake aliye mtumikia Kwa muda mrefu na Kwa heshima sana hivyo alimuamini sana kuliko kitu chochote kile kwenye maisha yake.
"Tangu nikupigie simu siku ile nina imani utakuwa umesha waandaa vijana tayari?" aliuliza mheshimiwa akiendelea kuiweka suti yake vizuri.
"Ndio bosi wako Sawa kabisa wanasubiri amri yako tu" Baruan alijibu akiwa amesimama kikakamavu mbele ya mtu aliye kuwa anamfanya ale mjini.
"Safi, kaandae kikao chini kabisa ya meli kwenye chumba cha kazi nakuja baada ya dakika tano" maelezo yaliji tosheleza kabisa kumfanya Baruan kuondoka haraka mahali hapo. Dakika 10 mbele kwa mara ya Kwanza makomando hawa 15 waliweza kumuona bosi wao ambaye alikuwa anafanya kazi kama kivuli kwao Kwa zaidi ya miaka miwili. Wengi walishangaa sana baada ya kujua haya yote yapo nyuma ya mheshimiwa waziri mkuu lakini hawakuwa na cha kufanya Kwa sababu mtu huyo alikuwa akiwalipa pesa nyingi sana na waliogopa mno kuuawa hivyo iliwabidi kuwa wapole
****************************************
"ni muda mrefu kidogo nadhani mlitamani sana kunifahamu leo imetokea hiyo nafasi kwenu, kufanikiwa kunifahamu inamaanisha maisha yenu Kwa sasa yapo rehani sana kama tu midomo yenu itakuwa myepesi mno kwenye utoaji wa maneno". Mheshimiwa aliguna kidogo kisha akaendelea "hiki kinacho fanyika hakija anza Leo wala jana ni kitu cha muda mrefu sana ndio maana kumekuwa na uwekezaji mkubwa mno wa pesa, ni lazima nikae ikulu iwe ni kwa kushinda kwenye kura au kumwaga damu za watu, hapa mna kazi kubwa mbili za kuzifanya, yakwanza ni kumtafuta bwana mdogo afahamikaye Kwa jina la Calvin Jackson huyu nina kazi kubwa na Mali zake nilizo zihangaikia kwa zaidi ya miaka mitatu sasa lakini nimechelewa kuzipata kutokana na kumwamini mpuuzi mmoja aitwaye Fabian Decco hivyo uzembe wa aina ile utawapelekea pabaya sana, suala la pili kama haya yasipo enda vizuri nitahitaji mheshimiwa raisi auawe" maelezo yake yaliwashtua kiasi kikubwa makomando wote walio kuwa humo ndani isipokuwa Baruan peke yake, waliogopa mno kwani sio rahisi sana kwa mwanajeshi hata uiasi nchi yako vipi kufikia hatua ya kuwaza kumuua raisi wa nchi yako, lililuwa ni jambo la hatari kubwa sana ikijulikana na walijua wazi kumuua raisi sio japo jepesi kama Mzee huyo alivvyo kuwa akilielezea, hakuna aliye thubutu kuongea lolote juu ya hilo kulingana na ugumu wake.
"Nadhani mtakuwa mmenielewa vizuri wiki moja ijayo hili jambo liwe limeis........." kabla hajamalizia hata maneno yake kuna ujumbe uliingia kwenye simu yake ikambidi aufungue kwa haraka mno baada ya kuona ilikuwa ni video iliyo tumwa Kwa njia ya WhatsApp, aliifungua haraka ile video iliyo kuwa imetoka moja Kwa moja Kwa watu wake waliopo ndani ya idara ya usalama wa taifa. Ilikuwa ikionyesha mauaji ya kikatili ambayo Calvin aliyafanya kikatili kwa vijana wake wakiongozwa na Abdul Abdulrazack, alikuwa ni mtu mwenye roho ngumu na ya kinyama mno lakini ile video ilimtisha sana hakuamini kama huyo mtu alikuwa mkatili namna hiyo Kwa sababu hakuwahi kumshuhudia zaidi ya kusimuliwa. Ilikuwa ni video iliyo patikana kwenye kamera za usalama wa taifa zinazo wekwa kwa siri sana maeneo mengi ambayo huwa yanapatikana watu wengi ni kwa ajili ya usalama wa raia pamoja na nchi kwa ujumla.
"Pumbavu namhitaji huyu mtoto haraka sana nitamuua kwa mkono wangu Mimi mwenyewe" alipiga meza Kwa hasira na kutoka ndani humo bila hata kuaga akapanda kwenye boti yake ya kifahari na kuondoka kwa hasira kubwa.
Calvin alifanikiwa kufika nyumbani akiwa kwenye hali mbaya sana, ilikuwa ni majira ya usiku wa manane hakutaka kumsumbua mtu ikambidi kwenda kwenye chumba chake ili apate matibabu, alitumia zaidi ya saa moja akiwa anajitoa risasi na kujipatia matibabu ili apumzike. Baada ya kumaliza alikuwa akijisikia vibaya sana hivyo aliona ni muda sahihi wa kupata nafasi ya kwenda kulala lakini akiwa anaelekea kulala simu yake iliita kwa fujo mno, alishtuka kwani hakikuwa kitu cha kawaida kwake kutokea hali kama hiyo, ikambidi aipokee ili amsikilize mtu huyo ni nani na anataka nini.
"Hello" ilikuwa ni sauti nzito ya mwanaume kutoka upande wa pili lakini Calvin hakujibu kitu
"Kwanini umeenda nje na makubaliano yetu bwana mdogo huoni kama unanikosea heshima" Calvin alitabasamu baada ya kugundua hiyo ilikuwa sauti ya raisi
"Mzee umeipata vipi hii namba yangu, ni wanadamu wachache sana wanao ijua hii namba" Calvin alijibu huku akiwa anasikilizia maumivu makali ya kifua
"Mhhhhhhhh kichwani mwako unatakiwa uelewe kwamba mimi ndiye raisi wa nchi hii, hakuna kitu kinaweza kuendelea kwenye nchi yangu nisikijue, angalia kwenye mgongo wako karibu kabisa na bega lako hapo" maneno ya raisi yalimshitua sana, ikambidi atazame haraka kwenye kioo kilicho kuwa mbele yake, alishangaa baada ya kuona kuna alama nyekundu iliyo kuwa ikionekana Kwa mbali Sana, aligundua kwamba ni kifaa cha mawasiliano, alichukia sana kuona hiyo hali ilimaanisha kwamba raisi alikuwa anamuona kila mahali alipo wakati yeye aliua ametoka gerezani kwa siri kubwa.
"Mzee usije ukanishawishi nikabadili maamuzi mpaka kwako kwanini umenifanyia hivi?" aliuliza kwa hasira Calvin
"Huwa simwamini kirahisi mtu moja Kwa moja ili kuthibitisha hilo unaweza ukanijibu kwamba ni kwanini umetoka gerezani bila mimi kujua? " Raisi aliuliza kitu kilicho mfanya Calvin akae kimya tu alihisi huenda mtu huyo kuna mchezo anamchezea.
"ndani ya saa moja uwe umefika kisiwa cha Mbudya haraka mno utanikuta hapo uje unijibu maswali yangu" kisha simu ikakatwa. mwanaume hali yake haikuwa nzuri lakini hakuwa na namna zaidi ya kufanya hivyo alivyo ambiwa. Alichukua gari yake haraka na kutoka ndani hapo kwa kasi sana lakini akiwa kigamboni maeneo ya darajani alihisi kama kuna gari mbili zinamfuata ila hakuzitilia sana maanani, alienda nazo mpaka mwenge hapo ndipo alijihakikishia kwamba ni yeye alikuwa anafuatiliwa bila shaka, mwanaume aliongeza kasi ya gari na kupitiliza mpaka Tegeta ili awapoteze watu hao, alifika sehemu alizima gari na kushuka kisha akajibanza sehemu kuona kama kuna mtu atatokea mahali hapo.
" Unadhani utakimbia mpaka lini bwana mdogo" ni sautu moja ya msisitizo kavu sana ilitokea nyuma na mahali alipokuwa amejibanza, hakuona sababu ya kuendelea kujificha alishangaa anawaona wanaume wawili mbele yake na wawili nyuma yake, hilo halikumshtua sana
"Hauwezi kuukimbia mkono wa sheria ebu usitake tukupatie ukilema ukiwa bado mdogo namna hiyo, vaa pingu hizo tuondoke" sauti ya yule mtu wa kwanza ilimuamuru tena huku mwanaume huyo akimrushia Pingu Calvin ambazo aliziacha zidondoke tu
" Aliya watuma ni raisi au nani? Calvin aliuliza kwa jazba akidhani ni mheshimiwa raisi ndiye aliye watuma watu hao. Hakupewa nafasi ya kupatiwa jibu kuna mwanaume alikuja akijikunja kwa mateke makali yalimpata Calvin alizuia lakini yalimuingia vizuri mno kwa sababu hali yake ilikuwa mbaya sana baada ya kutoka kujitoa risasi ya kifua iliyo kuwa imepigwa karibu kabisa na moyo muda sio mrefu. Walikuja wawili kwa kasi ya ajabu mwanaume alijirusha juu kwa kutumia nguvu kubwa kitu kilicho mfanya atoe damu puani kwa nguvu alizokuwa ametumia alishuka Kwa ngumi kali mbili zilizo wapata wale watu shingoni na wote wakarudi nyuma haraka sana wakisikilizia maumivu makali mno huku wakishikilia shingo zao. Calvin alidondoka chini ghafla baada ya kupigwa sindano ya sumu na moja ya wanaume wawili walio kuwa wapo nyuma yake, baada ya kuona uhatari wake waliamua kutumia nafasi hiyo vizuri mwanaume alitaka kujikaza lakini ilishindikana alikuwa kwenye hali mbaya na maumivu makali mno.
Hawakuwa na imani naye tena na hawakuwa na uhakika kama kweli amelala hapo chini mmoja aliruka kwa nguvu na kushuka kwa teke kali kwenye shingo ya Calvin lakini kabla hajafanya hivyo alipigwa ngumi kali sana iliyo mpelekea kurudi nyuma zaidi ya hatua kumi huku akisikilizia maumivu makali kupita kiasi ya mbavu, wote wanne walishangaa mbele yao alisimama mwanaume mmoja mtanashati mno na mwenye tabasamu hafifu usoni mwake, walidhani ni Calvin amenyanyuka ila mwanaume mwili wake ulikuwa upo chini ukiwa haufahamiki kama kafa au bado yupo hai.........
Huyu mwanaume mpya ni nani? Kaja kufanya nini hapa? Kwanini aje wakati huu? Ana uhusiano gani na Calvin na hawa watu walio mvamia Calvin ni akina nani? ....
Ukurasa wa 46 sina la ziada tena tukutane mpaka wakati ujao tupate majibu ya maswali yetu....
Langu jina naitwa Bux the story teller
Chao[emoji2768]
#ULIMWENGUWAWATUWABAYA
Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app