Hadithi: Ulimwengu wa Watu Wabaya

Hadithi: Ulimwengu wa Watu Wabaya

HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 49
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA.........
"hahahahahahaha....hivi unajua yule mtu uliye muua alikuwa ni nani kwangu? Leo nakutoa mfupa mmoja mmoja mpaka unakufa kikatili sana kama ndugu yangu alivyo kufa, kama utabahatika kuishi leo basi hakikisha unaniua mimi kwanza ndipo utaweza kutoka mzima hapa" mwanaume aliongea na kucheka kwa uchungu mkubwa na hasira sana akitokwa na mchozi kwani mtu aliye kuwa mbele yake kwake alikuwa zaidi ya shetani na aliahidi atamalizane naye yeye mwenyewe.

ENDELEA...........................
"kwenye maisha ya mwanadamu moyo pekee ndicho kitu ambacho huwa kinaumia zaidi pale yanapo fanyika mambo nyuma na matarajio, kwenye maisha yako umenifanyia kitu ambacho ni ngumu sana kwa mwanaume mwenye moyo ambao ni dhaifu sana kuweza kuvumilia, umeniibia furaha ya maisha yangu na bado unalalamika kuhusu mimi kumuua ndugu yako huyo" Baruan aliongea akisogea mahali alipokuwa amesimama Victor lakini maneno haya yalimfanya Victor amshangae mno mtu huyu na kumfanya asielewe chochote kile.
"mhhhhh unajua nini kuhusu furaha ya binadamu mtu katili kama wewe?"wakati huu Victor aliongea akiwa anaikunja ngumi yake vizuri kwani alijua sio muda mahali hapo panaenda kutokea balaa zito na ndiyo sehemu aliyo kuwa akiipenda zaidi kwenye maisha yake, alipenda mno mchezo wa mapigano mtu, huyu kwake ilikuwa kama burudani tofauti na watu wengine walivyo kuwa wakiiogopa tasnia hiyo ya mchezo wa ngumi
"bado una akili ya kitoto huwezi kuelewa chochote ila mtakufa kikatili sana viumbe dhaifu kama nyie na huyo anaye watuma nataka ayashuhudie haya maumivu halafu baadae nitamalizana naye yeye mwenyewe" neno dhaifu lilimuuma sana Victor hakuweza kusubiri kuendelea kupokea dhihaka kutoka kwa huyu mtu, mwanaume alichomoka kama umeme kumfuata mwanaume huyo aliye kuwa amevaa zake suti safi, alimfikia pale alipo Victor alijizungusha sarakasi ya mbele kwa nguvu wakati anatua chini alimchota Baruan mtama mkali kabla hajatua alirusha teke moja zito sana lililompata Baruan kifuani alirushwa mbali kidogo lakini kiumbe huyu alijizungusha akiwa juu hajatua chini na kutua chini kama vile hakuna kilicho mtokea huku akitoa kitambaa na kujifuta mahali alipokuwa amechafuliwa na teke la Victor.
"ni zaidi ya miaka kumi(10) sasa hakuna binadamu amewahi kunipiga ngumi nikasikia maumivu wewe ndiye wa kwanza, upo tofauti sana na wenzako na huenda ningefanya kosa kubwa mno kama ningekuchukulia kwa udogo nilio kuwa naufikiria mwanzo" Baruan aliongea kwa msisitizo huku akiukunja mkono wake kwa hasira wakati huo Victor alikuwa ameshafika na kuanza kushambulia kwa nguvu kubwa mno hiyo haikumfanya huyu kiumbe arudi nyuma hata hatua moja alikuwa mwepesi kupita maelezo hakuna ngumi hata moja ya Victor iliyo fanikiwa kumgusa hata nguo yake tu, Victor alishtukia akipigwa ngumi moja kali maeneo ya taya iliyo mfanya arudi nyuma Kwanza na kuuweka mdomo wake sawa, Baruan alikuwa amebadilika sana kiasi cha kuwa mtu wa kutisha alikuwa anakuja kwa mapigo ya ajabu kiasi kwamba Victor hakuwa na uwezo wa kuzuia hata moja, zilirushwa ngumi mbili ambapo moja Victor alifanikiwa kuizuia lakini alipata maumivu makali sana kwenye mkono alio utumia kuzuia ngumi hiyo kutokana na ukomavu wa mtu huyu, ngumi ya pili ilipenya mpaka kifuani ilimfanya ateme funda la damu kwa maumivu makubwa lakini mtu huyo hata hakumpa nafasi ya kupumua Victor alinyanyuliwa kwa kasi na kupigwa kiganja kichwani kabla hajakaa sawa lilizungushwa teke la nguvu na kumpeleka chini alidondoka vibaya sana, wakati yupo pale chini Baruan alikuwa anaenda kumaliza kazi kwa kuruka juu kisha akawa anashuka kwa goti kali la shingo bahati nzuri Victor aliliona vyema hivyo alijizungusha haraka na goti likatua chini, Victor aliogopa sana kwani sehemu ambayo goti hilo lilishukia palibonyea kiasi japo palikuwa na zege, alijua huyo aliye kuwa mbele yake hakuwa levo yake kwenye mapigano kabisa na sio mwanadamu wa kawaida. Baruan alinyanyuka kwa nguvu kisha alajifuta suti yake mahali hapo kwenye goti baada ya kuchafuka kwa vumbi kidogo kwenye ile zege, akaitoa bastola yake na alitamka maneno ya dharau sana wakati huo Victor alikuwa akitema mafunda ya damu kwa maumivu makali mno kifuani na alihisi kama kifua kinawaka moto kwa ngumi kali chache tu alizopigwa.
"unanipotezea muda tu wewe bado ni binadamu dhaifu sana mifupa yako milaini mno, una zaidi ya miaka kumi ya kufanya mazoezi ili uweze kusimama namimi ulingoni, kukupiga Kwa mkono naona ni kunichafua tu kwa sababu naona kama napigana na mwanamke, ikariri hii sura ili hata siku ukiniona huko kuzimu uikimbie" Baruan aliikoki vyema bastola yake ili asipoteze muda wake lakini kabla hajafyatua risasi ilisikika sauti ya Marry mlangoni ikimuita Victor baada ya kuona amechukua muda mrefu bila kurudi wakati umeme ulikuwa umesharudi kama kawaida, sauti hiyo ilimshtua sana Baruan na kumfanya aghairi kwanza kufyatua risasi hiyo aligeuka nyuma kitu kilicho mfanya Marry ashtuke kwa uoga baada ya kuiona hiyo sura ambayo hakuitegemea kabisa kuiona mbele yake, hata Baruan aliishiwa na nguvu hata mkono wenye silaha alio kuwa amemnyooshea Victor aliushusha chini akiwa ametoa macho sana, mwanaume aliangalia tumboni na kumuona mwanamke huyu akiwa na ujauzito aliikunja sura yake kwa hasira na kutoka hapo ndani bila kuongea chochote kile. Victor alishangaa sana kuhusu kilicho kuwa kikiendelea hapo na alishindwa kuelewa hao watu wanajuana? au kuna nini kati yao mbona wote wameshtuka sana kuweza kuonana? hata hivyo hakuchukua muda mrefu alidondoka chini na kuzimia kwa mapigo ya hatari aliyo kuwa ameyapokea kwa huyo mtu.

Ndani ya ofisi ya mkurugenzi wa usalama wa taifa Kasisi Chacha alikuwa amesimama mbele akiwatazama makomando wanne walio kuwa mbele yake wameinamisha vichwa huku wawili wakiwa wamefungwa bandeji vichwani.
"haya mtu wangu yuko wapi maana naona mmekuwa mabubu kama hamuelewi nilicho watuma" aliongea kwa sauti kali kidogo akiwa anawaangalia watu hao mbele yake
"Mzee sio rahisi sana kama tulivyo kuwa tumefikiria" kauli ya komando huyu ilifanya apigwe jicho kali mno ikambidi akae kimya.
"Mzee utusamehe sana kwa kilicho tokea, huyo mtu tulifanikiwa kumuweka kwenye tageti na tulikuwa tumefanikiwa kumzimisha kwa sababu wakati tunaenda pale alionekana akiwa kwenye maumivu makali sana lakini wakati tunataka tumchukue kuna mtu mwingine ameingilia hili jambo na sio mwanadamu wa kawaida hata kidogo wenzangu wote walipigwa vibaya sana mimi pekee ndiye nilibaki na nguvu na kuwabeba, alifika pale na kuondoka na huyo mtu" yalikuwa ni maelezo ya yule mmoja ambaye Akio aliweza kumuacha salama kabisa wakati anamchukua Calvin, kidogo ilimfanya mzee huyu kutulia kisha akauliza kwa sauti yenye mamlaka
"unasema kuna mtu ameingilia hili suala? kivipi na ni nani huyo mpaka awashinde wote wanne?" alikuwa amemkazia komando huyu macho ili aweze kumpatia jibu kuhusiana na huyo mtu anaye sema alifika na kuondoka na Calvin
"ilikuwa ni usiku lakini alikuwa akionekana vyema kabisa, kwa asili anaonekana kabisa ni Mmarekani na anamjua vyema yule mtu kama sio ndugu yake basi kuna uhusiano wowote kati yao, tumejaribu kupambana naye lakini sio mtu wa kawaida hata kidogo huyu ni hatari hata kuliko huyu uliye tuagiza tukamchukue na anaonekana ni mtu mwenye mafunzo makubwa kupita kiasi kwa sababu kwa aina ya upambanaji wake anaonekana ni mtu ambaye mifupa yake haina maji kabisa, ni migumu sana sina imani hata kama kisu cha kawaida kinaweza kuzama kwenye ile ngozi yake japokuwa naye ana mwonekana wa kilaini sana kama Calvin sema wametofautiana uraia tu kwamba yule ni Mmarekani ila vitu vingi wanaendana sana hata aina ya uongeaji wao" alitoa maelezo marefu kidogo yaliyo weza kumwacha mzee huyu kwenye mshangao mkubwa kwani hakuelewa huyu mtu anatokea wapi na lengo lake hasa ni nini na Kwa wakati huo alikuwa amefeli kumpata Calvin.
"nendeni nitawaita" aliongea huku akiipiga meza kwa hasira sana hayo maelezo yalimchanganya mno mzee huyu akiwa ameachwa njia panda, alilaani kitendo hicho cha kuweza kusumbuliwa akili na mtoto mdogo ikiwa amedumu kwenye kazi hiyo kwa miaka mingi mno na hakuwahi kukutana na ugumu mkubwa wa kesi yoyote ile kama ilivyo kuwa hii kesi ya Calvin basi hakukaa hapo akawa amepanda gari kwa kasi ya ajabu kuelekea fukwe ya Coco kuangalia sehemu ambayo mauaji ya Abdul na wenzake yalifanyika ili aone kama anaweza kupata kitu chochote kwenye kesi hiyo. Alifanikiwa kufika mahali hapo mkononi mwake alikuwa amebeba laptop pekee, alikuwa mtaalamu sana mzee huyu aliifungua video ambayo kamera za usalama zilifanikiwa kuinasa japokuwa kwenye video hiyo kulingana na nguo alizo kuwa amevaa muuaji huyo hazikumruhuusu kuonekana sura yake hata muda ambao alikuwa anavua kofia yake kumuonyesha Abdul yeye ni nani alikuwa ameipa kamera hiyo mgongo hivyo hawakumuona. Mzee huyo aliitazama video hiyo kwa namna watu walivyo kuwa wakiuliwa kikatili alifumba macho akifananisha na uhalisia ambao ulikuwa ukitokea aliifunga laptop yake kwa hasira mno
"hahahahahahahahaah.....nikikukamata wewe mtoto nitakuua kwa mikono yangu mwenyewe" aliitamka kauli hii pamoja na kucheka kwa uchungu sana, alikuwa alishamjua muuaji wa hao binadamu zaidi ya kumi na mbili walio kuwa wameuliwa kikatili sana, kwake ilikuwa ni dharau kubwa mno kuzubaishwa na mtoto ambaye alikuwa na uwezo hata wa kumzaa, aliliondoa gari kwa kasi sana hayo maeneo akiwa na mawazo sana na ndio muda ambao alikumbuka kwamba ni zaidi ya siku kadhaa akiwa hajaenda kwa Victor basi ilimbidi kugeuza gari na kuelekea Mikocheni kwa Victor akiwa haelewi kama mtoto wake huyo alikuwa yupo kwenye matatizo mazito sana kwa wakati huo na haikufahamika kama anaweza kuamka tena.

"majira ya saa nne za asubuhi ndio muda ambao Calvin alikuwa anafika kwenye nyumba yake maeneo ya Kigamboni, lakini akiwa anasogea maeneo hayo alishtukia nje ya nyumba yake kuna magari yaliyo onekana kuwa ya Ikulu japo kwa mtu asiye yajua ilikuwa ni ngumu sana kuweza kuyatambua magari hayo. Ilikuwa ni kitu cha ajabu sana kwani hakuwahi kumtajia mtu sehemu aliyo kuwa anaishi lakini alipiga usukani kwa hasira baada ya kukumbuka kwamba wakati wote alikuwa akiishi na kifaa cha mawasiliano ndani ya mwili wake kwahiyo ni muda mrefu Raisi alikuwa akijua mahali alipokuwa akiishi.
"umenifanya nimekaa sana mahali hapa mwanangu shida nini mpaka jana umedharau wito wangu" Ilikuwa sauti nzito ya mheshimiwa raisi akiwa anashuka kwenye gari lililo kuwa karibu na mlango wa geti wakati huo raisi alikuwa akitengeneza kola la shati lake lililo ndani ya suti ya bei ghali sana.
"Shikamoo mzee" Calvin alisalimia kama alivyo kuwa amezoeshwa na wazazi wake pale anapo kutana na watu wakubwa walio mzidi umri.
"Mhhhhh marahaba ebu twende ndani tukaongee kidogo kwani nina mazungumzo marefu kidogo leo nawewe" Raisi aliongea huku akisogelea geti ambalo Calvin alikuwa amelifungua, wakati wanaingia mahali hapo mheshimiwa raisi alishangaa sana kuiona familia ya jaji mstaafu halikadhalika familia ya jaji walishangaa mno kumuona raisi mahali hapo na hawakujua alikuwa akitafuta nini iliwabidi wamsalimie kwa heshima kiasi kikubwa. Walipandisha mpaka chumba cha juu kabisa ambako kulikuwa na upepo mzuri sana wa bahari.
"nimeshangaa sana unavyo niambia kwanini usiku wa jana sikuweza kufika ndani ya kisiwa cha Mbudya ambako ulitaka tukutane kwa sababu wale watu nilijua wewe ndiye uliye weza kuwatuma kwangu" Calvin aliongea maneno ambayo yalimshitua sana mheshimiwa raisi ikambdi aulize kwa mshangao
"Watu gani hao?"
"ni watu wa usalama wa taifa" kauli hii ilimfanya mheshimiwa raisi ang'ate meno kwa hasira sana kwani moja kwa moja alijua ni Kasisi Chacha ndiye aliyeweza kuwatuma hao watu kumkamata Calvin
"Walikuwa wangapi na kilitokea nini juu ya hao watu?" Raisi aliuliza kwa wasi wasi huku akiukagua mwili wa Calvin ili aweze kuona kama upo sawa.
"Nadhani ulisikia kuhusu mauaji yaliyo weza kufanyika ndani ya fukwe ya Coco?" Calvin hakujibu alicho ulizwa bali aliuliza swali lingine
"Ndio, kwamba ni wewe ndiye uliye husika na yale mauaji ya kikatili namna ile?" Raisi naye aliuliza swali lingine
"ndiyo"
" wale watu ni akina nani na kwanini uwaue kikatili namna ile wana uhusiano wowote na hili?"
"wakati nipo gerezani kule Pemba ndani ya siku tatu tu nilikuwa nimempata mtu wangu na niliondoka naye, kuhusu hilo sikutaka kukuweka wazi mapema kwa sababu nilitaka niujue ukweli kwanza ndipo niweze kukutana nawewe, nilisindikizwa na helikopita mpaka maeneo ya Bagamoyo ambako kuna nyumba yangu nyingine. Baada ya kumbana vizuri Ahmed aliweza kufanya mawasiliano na kaka yake ambaye nilihitaji kuonana naye ili niweze kumkabidhi mdogo wake akiwa yupo hai kabisa baada ya kugundua huyu Abdul ndiye mtu aliye toa kauli ya mwisho ya wazazi wangu kuuliwa kwnye simu usiku ule ambao kamwe siwezi kuusahau kwenye maisha yangu nilikuwa natamani mno kuweza kumpata huyu kiumbe. Tulikubaliana tukutane pale ndani ya fukwe ya Coco pale, sikuona haja ya kumwacha hai Ahmed kwa aina ya uhalifu aliokuwa ameufanya hivyo nilimuua kule kule Bagamoyo. kwa mara ya kwanza niliweza kukutana na huyo mtu niliye kuwa na uchungu naye sana, hakuamini nilivyo muonyesha video ya mdogo wake akifa kikatili ndani ya mashine ya kusagia vyuma hivyo naye kiasi fulani alipitia uchungu kiasi chake kabla hajapoteza maisha na hicho ndicho nilikuwa nakihitaji lakini mimi sikumuua yule mtu" maelezo mafupi ya Calvin yalimfanya mheshimiwa raisi afumbe macho kwa ukatili ambao mwanaume aliweza kuufanya kwa Ahmed.
"hujamuua wewe kivipi tena na umekubali wakati nakuuliza?" Raisi ilimlazimu kushangaa baada ya Calvin kusema hakumuua yeye mtu huyo.
Ukurasa wa 49 sina la ziada tena tukutane wakati ujao
Chao[emoji2768]
Bux the story teller

#ULIMWENGUWAWATUWABAYA
Hadithi hii ya ULIMWENGU WA WATU WABAYA tumebakisha episodes 27 mpaka kufika tamati Kabisa na kutandika daruga ....Kwa shilingi 2500 tu pekee njoo uiamalizie yote Kwa siku moja tu uburudike na moja ya hadithi bora sana.

Namba za malipo ni

0621567672 (WhatsApp)
0745982347

Zote jina ni FEBIANI BABUYA.

Njoo uburudike na kalamu ya Bux the story teller
 
Binafsi najulisha kumaliza kuisoma story yote tuendelee na kawaida.
 
HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA 57
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA.....................
Aliyatoa macho Calvin baada ya kujua kwamba waziri mkuu naye ana mtu ambaye ndiye chanzo cha haya yote na ndiye master wa mchezo mzima, alijipiga kibao kichwani kwa kufanya maamuzi ya hasira kwa kumuua mapema Abdul ambaye inawezekana angemsaidia sana kujua siri ambazo aliona bado zipo mbele yake, alichukia mno mwanaume aliona sasa ni muda sahihi wa kumfuata Anuary Jaden huenda anajua mambo mengi sana, alizibeba nguo zake akizivaa kwa haraka mno kisha akaubeba upanga wake na frash na kutoka ndani humo kwa spidi sana.
ENDELEA........................................
JNIA (Julius Nyerere International Airport)
Gari aina ya Range Rover iliingia kwa spidi kali na kwenda kupaki haraka huku akishuka mtu ndani akiwa hajatulia kabisa, alikuwa ana hamu sana ya kufika mwisho wa safari yake, mtu huyo alikuwa ni Kasisi Chacha alikuwa amefika hapo baada ya kupewa taarifa kwamba vijana wake wa usalama wa taifa wameweza kuuawa kikatili sana huku wakilikuta koti moja ikionyesha kwamba mmoja amefanikiwa kutoroka humo ndani. Alifika sehemu ambayo walikuwa wamefia makomando hao wa idara ya kijasusi ya usalama wa taifa, haikuhitaji kuwaangalia hata mara mbili kwa jinsi walivyokuwa wanatisha kutokana na aina ya vifo walivyokuwa wamekufa, aliikunja sura yake kwa hasira kwa jinsi alivyokuwa anawaamini sana hao viumbe hakudhania kwamba kuna mtu anaweza kuwaua kirahisi hivyo.
"kuna kamera yoyote mahali hapa" alimuuliza moja ya maaskari aliokuwa amewakuta pale na bahati mbaya sana walikuwa hawamjui kabisa kwa sababu alikuwa ni mtu wa kuishi kwa siri kubwa.
"alafu wewe mzee uondoke haraka hapa usituletee ukichaa wako hapa huoni tupo bize na kazi Kwanza hairuhusiwi mtu wa kawaida kuingia humu, Harun ebu mchukueni huyu akatueleze vizuri kituoni" askari huyo aliongea kwa dharau akidhani Kasisi Chacha ameingia pale bahati mbaya, alipigwa jicho moja kali sana hata hivyo walitoa siraha na wakafanikiwa kumkamata, hakuleta ubishi kwa sababu alijua wana siraha na alikuwa amechelewa kufanya maamuzi sahihi, walienda naye mpaka kituo kikubwa cha polisi cha Osterbay, wakati wanamshusha kwenye gari alitamka kauli moja ya utata mkubwa ambayo askari wote walishangaa sana wakilikagua vizuri gari lililokuwa limebeba miili ya makomando hao waliofia airport.
"bwana mdogo kama utafanikiwa kuliona tena jua la kesho basi utakuwa umependelewa kuishi maisha marefu sana hapa duniani umefanya kosa moja kubwa sana kwenye maisha yako" alimjibu askari huyo bila kumtazama wakati wanamshusha kwenye gari hilo kwa kumsukuma sukuma.
"Mkuu" ilikuwa ni sauti ya mkuu wa kituo cha polisi cha Osterbay akitoa heshima kwa Kasisi Chacha huku akipiga saluti kwa heshima, ni muda ambao alikuwa anatoka ndani ya kituo ili aelekee kwake, alishangaa sana kuona mzee huyo amefungwa pingu hata hivyo Kasisi Chacha hakumjibu kitu ikambidi mkuu wa kituo akamfungulie mwenyewe kwa uoga kwani alikuwa akimjua vizuri sana huyo binadamu aliyekuwa mbele yake.
"hivi ndivyo ulivyo wafunza vijana wako kutokuwa na nidhamu na kazi zao?" Kasisi Chacha aliuliza Kwa sauti yake nzito yenye mkwaruzo huku akiinyoosha mikono yake baada ya kufungwa kwa muda kidogo na kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake. Wale maaskari pamoja na yule aliye amuru mzee huyo akamatwe walikuwa wanashangaa kwa namna walivyo weza kuona mambo yanaenda waligundua kabisa kwamba huyo alikuwa ni kiongozi mkubwa sana kwenye nchi hii waliogopa mno.
"paaaaa" ulikuwa mlio wa risasi ambayo ilipigwa na Kasisi Chacha kuelekea kwa yule askari aliye amuru yeye akamatwe, kilikuwa ni kitendo cha ghafla kilicho mshangaza kila mtu, mtu anawezaje kufanyia mauaji kituo cha polisi, hata hivyo hakuwajali aliitupa bastola hiyo ambayo alikuwa ameichomoa kwenye kiuno cha mkuu wa kituo, akachukua gari moja wapo ya waliyo kuja nayo askari wale kutoka airport.
"baada ya saa moja nahitaji hiyo miili niikute hospitalini pamoja na gari langu" baada ya kutamka maneno hayo alilitoa gari ghafla sana hapo akielekea mahali ambapo simu yake ilikuwa ikimuongoza kulingana na ujumbe alio kuwa ametumiwa.
"mmefanya kitu cha kipumbavu sana wajinga nyinyi ona huyu mpuuzi mpaka kauawa, mnapata wapi ujasiri wa kumkamata mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa na ni komando mstaafu hivi mna akili nyie, jiandaeni huenda wote mtakufa" kauli ile ya mkuu wa kituo akiwafokea askari wake iliwafanya waanze kutetemeka walijua wazi mtu huyo lazima angerudi na hakuna ambaye angepona katika hilo ndipo mmoja alikumbuka kauli za mzee huyo wakati anashushwa kwenye gari alivyo mwambia yule askari kwamba kama akiliona jua atakuwa na bahati sana kauli yake ilitimia baada ya kumuua pale pale, hawakuwa na imani kama wataendelea kuwa hai tena hivyo waliubeba mwili wa mwenzao aliye pigwa risasi muda huo kiunyonge sana huku mkuu wa kituo akipanda kwenye gari lake kwa hasira na kuondoka.
Gari aliyo ipanda Kasisi Chacha ambayo aliiendesha kwa spidi ya kutisha ilienda kusimama kwenye geti moja kubwa sana maeneo ya Sinza, hapo palikuwa ni nyumbani kwa Roland Michael moja Kati ya vijana wake wa muda mrefu sana, aliingiza gari lake, akashuka kwenda kuungalia mwili wa mtu huyo, aliyafumba macho kwa hisia kali alicho kiona mbele yake kilikuwa kinatisha sana, kichwa na mwili vilikuwa vilitenganishwa na mwili huo ulikuwa umewekwa kwenye mfuko wa naironi na maafisa usalama waliokuwa wamefika hapo kabla yake. Hakukaa sana hapo nje mzee huyu akapitiliza mpaka ndani kilipokuwepo chumba cha siri sana cha kuongozea kamera, alikuwa mwenyeji mno kwenye nyumba hiyo aliugusa ukuta mmoja kwa vidole vyake ukatokea mlango mkubwa wa kioo, aliweka tarakimu nane za siri mlango huo ukafunguka ndipo mahali palipokuwa na skrini nyingi sana kubwa, aliziwasha zote vizuri kisha akaanza kurudisha matukio nyuma kujua kilicho tokea. Alijua itakuwa ni Calvin amefanya haya yote baada ya kuligundua hilo kule uwanja wa ndege, mbele yake ilikuwa inaonekana sura ya Baruan Mahafidhu kijana aliye mtengeneza kwa mikono yake mwenyewe.
Aliitazama kwa umakini mkubwa hiyo video ambayo ilimtoa machozi kwani kijana aliyekuwa akichinjwa kama kuku mbele yake alikuwa ndiye msiri wake mkubwa na alimtii sana, alikuwa na siri nyingi mno za mtu huyu, alimtumia jinsi anavyotaka yeye kauli ya mwisho ya Baruan Mahafidhu ya kusema atamfuata mwenyewe amuue kwa mkono wake ilimfanya akacheka kwa hasira huku akipigiza mkono kwenye meza kwa hasira na kutoka humo ndani bila kumsemesha mtu yeyote yule kati ya wale maafisa usalama waliokuwa wamekuja kuuchukua mwili wa Roland pamoja na kufanya uchunguzi. Matukio hayo ya muda mfupi kati ya makomando watatu wa usalama wa taifa pamoja na kijana wake Roland yalimpa mawazo mno, ilimpelekea kuendesha gari kwa hasira zisizo weza kuelezeka akiwa haelewi aende wapi kupunguza machungu hayo, njia sahihi aliona ni kwenda ndani ya kasino lake kubwa lililofahamika kama SEVEN WORLD CASINO lilikuwa na club ndani yake na lilipatikana maeneo ya Posta Dar es salaam, alifika na kupaki gari yake ambayo hakukumbuka hata kuizima, aliingia ndani huku akitoa simu yake mfukoni na kupiga sehemu simu hiyo.
"I want him dead now(nahitaji huyo mtu afe sasa)" alitamka kwa hasira huku akituma picha sehemu ambayo haikujulikana ni wapi, alienda sehemu yenye wanawake na kuwaita wanawake sita waliokuwa wametokea mataifa mbali mbali, walikuwa ni wanawake warembo sana kiasi kwamba ungehisi wanafaa kuwa wanawake wa kuoa na kuishi nao ndani ya nyumba lakini pesa ni kitu kinacho badilisha aina ya maisha ambayo binadamu wengi sana wanayapanga usije ukadhulumu mali ya mtu wala kuitoa roho ya mtu kwa sababu ya pesa japo unatakiwa kila ukilala na kuamka ujue kwamba pesa ni kitu cha mhimu sana kwenye maisha ya binadamu hasa pale ambapo hautaki kudhalilika sana na kujielezea sana kwa hawa walimwengu wenye roho mbaya sana, ndivyo ulivyokuwa kwa hawa wadada licha ya kuwa wazuri sana lakini walikuwa wametengwa kabisa na kitu kinacho itwa pesa hivyo iliwalazimu kujirahisisha sana kwa watu wenye ukwasi wao ili waweze kuyafanya maisha yawe kama walivyokuwa wameota kuyaishi.
Waliingia chumbani wote sita wakiwa uchi wa mnyama hata Kasisi Chacha alikuwa ameshavua nguo zake zote akibugia pombe zilizo jazwa meza nzima, baada ya wale wanawake kuingia wala hakuuliza zaidi ya kuwavamia, ni muda mrefu kidogo alikuwa hajakutana na mwanamke hivyo alikuwa na hamu kubwa kupitiliza, kwa muda huo hakuwaza hata kwamba hapa duniani huwa kuna magonjwa yanayo sababishwa na hivyo vitu, alikuwa mwanaume hasa badala wale wanawake wamuelemee wao ndio walioanza kuelemewa na mzee huyu aliyekuwa komando mkubwa na mkurugenzi wa usalama wa taifa ila kwa siri kubwa sana, wale wanawake walikiri kwamba kweli huyo alikuwa mwanaume wa shoka sana na wengine wakatamani kama angeweza kuwaoa basi ndoa zao zingekuwa za bahati sana, masaa mawili waliyatumia ipasavyo watu hao saba humo ndani chumba kilikuwa hovyo maana vitu vilitupwa kila upande wakati wa shughuli nzito ya mzee huyo kwa hao mabinti sita hatimaye walichoka sana na wote saba walipitiwa na usingizi huku wakiwa wamelewa sana.

***********************************
TEMEKE DAR ES SALAAM
Maeneo ya Sokota majira ya saa saba usiku kulikuwa kumetulia sana, ni muda ambao watu wengi huwa wanajifungia ndani na familia zao, wengine na wapenzi wao na isingekuwa rahisi sana muda huo ukamkuta mtu anazurura hovyo kwa uasili wa aina ya matukio ya kutisha yaliyokuwa yanatokea kwenye wilaya hiyo, Temeke ni miongoni mwa maeneo yanye historia za kutisha sana kwenye upande wa usalama wa maisha ya watu ikidaiwa kuwa na watu wengi ambao walipenda sana kuishi kwa kutumia migongo ya wenzao, kwao kazi ilikuwa ni sumu kufanya walitegemea kukaba masaa ya usiku ili wapate chochote kitu cha kuwafanya waendelee kuwa sawa kwa upande wa mfuko kwenye hili jiji lenye kila aina ya changamoto.
Maeneo ya Sokota ndipo mahali ambapo Calvin alisimamisha gari hilo akiwa makini sana, alishuka haraka baada ya kuzima kabisa gari na kuanza kuifuata njia ya kuelekea Gongo la Mboto, hatua kumi za kutembea aliweza kusimama baada ya kuhisi kuna watu wanamfuata kwa nyuma, kuna mtu alipita kwa kasi mbele yake akapotelea uchochoroni mwanaume akatabasamu na kuyafumba macho yake kwa usahihi mkubwa, masikio ndiyo ilikuwa silaha yake kubwa linapokuja suala la kutumia hisia, kwa mjongeo wa ardhi kutokana na vishindo vya hao watu waliweza kugundua kwamba walikuwa wapo wanne tu. Ghafla sana alipotea hayo maeneo kwa spidi za hatari sekunde ya kumi wale watu walikuwa wamefika pale alipokuwepo Calvin wakiwa na mapanga mkononi huku sura zao zikiwa zimekomaa sana kuonyesha maisha magumu na bangi ndiyo ilikuwa sehemu ya kuishi kwao hapa duniani, yule aliyekuwa amepotelea kichochoroni baada ya kumpita Calvin kama kumtisha ili asiendelee kwenda mbele alijitokeza na kuanza kuwashangaa wenzake baada ya kukuta wapo wenyewe bila mtu ambaye alidhania wangekuwa wameshamuweka kwenye mikono yao.
Wakati huo Calvin alikuwa amejibanza kwenye mti mmoja mdogo uliokuwa upo maeneo ya kuoshea magari, aliwasikiliza watu hao kwa usahihi na kugundua walikuwa wakibishana kuhusu kupotea kwake.
"Mhhhhh...aagh mnataka nini?" mwanaume aliguna kidogo kisha akajitokeza mbele yao na kuwauliza walikuwa wanahitaji nini kwake
"vua nguo zako zote na kila ulicho nacho kiache halafu kimbia usigeuke nyuma mpaka unafika kwako" aliongea mmoja wao kwa majivuno huku akilishika shika panga lake lililokuwa linang'aa vyema kwa namna lilivyokuwa limenolewa na wataalamu.
"hahahahahah" Calvin alicheka sana baada ya kugundua waliokuwa mbele yake ni vibaka wa kawaida tu na sio watu aliokuwa anawadhania tangu mwanzo.
"Mpuuzi wewe unakuja kwenye mitaa ya watu halafu tunakwambia vitu unaleta jeuri sasa hauondoki tena mahali hapa lazima ufe huwezi kuonyesha dharau mbele ya wanaume wenye mji wao" Calvin hakuyajali kabisa maneno ya huyo jamaa aliyempiga mkwala zaidi aliingiza mkono mfukoni mwake akatoa bunda la pesa na kuwarushia akijua ni njaa tu inawasumbua kisha akageuza ili aanze kuondoka.
"we mrembo kakuruhusu nani uondoke, toa kila kitu kwenye mfuko wa......." sentensi yake iliishia njiani alilishika tumbo lake akiomba msaada wenzake waweze kumsaidia, neno mrembo lilikuwa ni dharau sana kwa Calvin wakati anaitamka sentensi yake mwanaume aligeuka haraka na kuirusha star yake kwa hasira kubwa, ilimchana chana yule kibaka alikuwa na dakika chache sana za kuweza kuwa hai, wenzake wawili walimfuata Calvin kwa nguvu kuweza kulipa kisasi cha mwenzao aliona wanampotezea muda kufika kwa mtu wake, alijibetua sarakasi moja ya haraka iliyo enda kuishia kwenye vichwa vya watu hao mmoja alipita na mkono wake kwa kuuzungusha upanga wake kwa hasira , kibaka huyo alijuta kuwepo hayo maeneo siku hiyo alipiga kelele sana mkono wake ulikuwa umekatika kabisa na kwa wakati huo alikuwa ni kilema mpya mjini.
"tokeni hapa au mnataka niwafanye kama wenzenu" aliwaambia wale vibaka wawili waliokuwa wameanza kutetemeka huku mwenzao mmoja akwa amekufa na mwingine mkono umekatwa, aliwaongeza mabunda mawili ya pesa pale chini na kuondoka kwa haraka huku nyuma walimbeba mwenzao aliyekatwa mkono kwa aliyekufa hawakuwa na muda naye tena, walitoka hapo haraka kwa uoga mkubwa wakiamini mtu huyo anaweza kurudi tena ikawa hatari kwao.
Kwenye nyumba nzuri ambayo kibao kilikuwa kinasoma namba 111 ndimo mahali alimokuwa anaishi Anuary Jaden, huyu ni mtu aliyekuwa amempata kwenye ile frash aliyo ichukua kwa Abdul, alionekana kuwa ndiye mtu aliyekuwa anatengeneza taarifa za uongo za hawa watu ili kuficha uhalisia wao. Nyumba ilikuwa kimya sana cha ajabu mlango ulikuwa uko wazi kabisa alijua wazi kwa wakati huo hakukuwa na usalama wa kutosha hapo alianza kuingia ndani kwa tahadhari kubwa mno, nyumba hii ilijengwa kama nyumba ya kupangisha ilikuwa na vyumba vingi sana kama vya kupangisha, chumba cha mwisho kabisa aliweza kuona kuna mwanga mdogo uliokuwa unaonekana kwenye sehemu ndogo yenye uwazi chini ya mlango, alisogea hapo na kuupiga mlango kwa nguvu akaingia ndani kwa sarakasi akiwa ameshika star zake mkononi kwa tahadhari kubwa lakini hakuona chochote, alipo geuza macho upande wake wa kushoto aliona kuna mwili wa mtu ukiwa umetapakaa damu kila sehemu ilimbidi asogee kuweza kushuhudia kitu hicho, alipigwa na butwaa baada ya kuona damu ni mbichi kabisa ikionyesha wazi tukio hilo limetokea hata dakika haijaisha, mwanaume aligeuka haraka lakini hakuona kitu, alivyo angalia mbele yake dirisha lilikuwa wazi huku likitingishika kuonyesha kuna mtu katoka hapo muda mfupi ulio pita alichungulia na kumuona mtu mmoja akiishia kwenye kona ya nyumba ya jirani yake.
Huyu muuaji ni nani na kwanini amuue wakati huu Anuary, kwamba alijua Calvin atafika hapa na kama alijua hilo unadhani Calvin atatoka salama hapa?.

57 inafika mwisho tukutane tena wakati ujao.
Bux the story teller
#ULIMWENGUWAWATUWABAYA

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Imalizie hadithi hii kwa shilingi 1500 tu mpaka ukurasa wa 76

Namba za malipo
0621567672 (WhatsApp)
0745982347
Jina FEBIANI BABUYA

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA 58
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA.....................
Mwanaume aligeuka haraka lakini hakuona kitu, alivyo angalia mbele yake dirisha lilikuwa wazi huku likitingishika kuonyesha kuna mtu katoka hapo muda mfupi ulio pita alichungulia na kumuona mtu mmoja akiishia kwenye kona ya nyumba ya jirani yake.
ENDELEA..........................
Calvin aliwaza haraka na kusonya baada ya kugundua kwamba watu hao lazima walikuwa wanajua kwamba angefika hapo kwa huo muda, hii ni ishara kwamba kwake wanapajua vilivyo mpaka muda anatoka walikuwa wamelitambua hilo mapema sana alisonya huku akigeuka nyuma yake kuangalia kitandani alimwona kijana huyo ambaye alikuwa bado mdogo sana kwa mwonekano akionekana kuwa na kati ya miaka 19 au 20. Alitoka haraka kupitia mlangoni ili kama kuna mtego wowote uliwekwa kumtamanisha apitie dirishani aweze kuukwepa vyema, alielewa kwamba kama watu hao wamefanikiwa kujua ujio wake basi ni lazima hawapo mbali na hayo maeneo. Alitoka taratibu kwa tahadhari kubwa akisikiliza kwa makini kama kuna hatua zozote za kuashiria uwepo wa mtu kwenye hayo maeneo lakini kulikuwa kimya sana. Kuna sauti ya mvumo wa kitu alihisi inakuja kwake ikamlazimu kuinama haraka kilipita kisu kwa kasi kubwa ila alipogeuka nyuma hakuweza kuona mtu yeyote aliye onyesha kukirusha hicho kisu, alisimama pale pale bila kufanya mjongeo wowote ule, kutembea ilikuwa ni ishara ya kujichanganya mwenyewe kwa sababu milango yake ya hisia isingefanya kazi vyema. kwa mbali sana alihisi kama kuna alama za uwepo wa watu na watu hao walionekana kuwa wataalamu sana kwa sababu hawakuonekana kuwa mbali lakini kwa namna wanavyo tembea alijua wazi amezungukwa na watu wasiokuwa wa kawaida hata kidogo.

"mnavizia vizia nini? mnashida namimi halafu mnajificha ficha jitokezeni haraka mnanipotezea muda" Calvin aliongea kwa sauti kubwa akiamini watu hao wanamsikia vyema baada ya kuona wanamchanganya kwani alikuwa haelewi wanatokea upande upi licha ya kuyafumba macho yake kwa usahihi. Walitokea wanaume wawili mbele yake ila bado alijua sio hao tu mwingine akatokea kulia kwake akiwa anaiwasha sigara yake, mwingine alitokea kushoto kisha akamalizia watano kutokea nyuma ambaye alikuwa anapiga makofi akionekana wazi anaufurahia uwepo wa mtu huyo hapo.
"kwa umri wako huo ulitakiwa uwe unashinda ofisini ukishika kalamu kuandika mahesabu ya pesa za makampuni ya baba yako kwa mali ambazo ungebakiziwa lakini ulivyo na akili ya kijinga unahangaika kufuatilia maisha ya watu ambao hata vyombo vya sheria havina uwezo wa kuwafuatilia" ilikuwa sauti nzito ya mwanaume huyo aliyekuwa anapiga makofi wakati anafika hapo. Calvin alifumbua macho yake na hata hakuhangaika kuwahesabu tena alikuwa ashajua mahali hapo walikuwa wamesimama watu wa kazi sana watano.

"mdomo upo kwa ajili ya kuongea lakini sio kila unacho kiongea kinapaswa kutoka mdomoni, najua mnaitaka sana roho yangu kuliko hata mnavyo itafuta pesa hapa duniani bahati mbaya hamjayajua madhara ya kuifuatilia roho hii inaweza kuwapotezea kila kitu kwenye huu ulimwengu" alikuwa anaongea Calvin huku akichezesha vidole vyake kwa usahihi, alikuwa akizipiga hesabu zake vyema alielewa kutoka hapo ilikuwa ni shughuli nzito.
"hahahahhaahahahaha alafu walivyokuwa wanamsifia nilijua ni mwanaume wa shoka ndo kuhangaika na usiku wote huu kumfuata mtoto mlaini namna hii hizi ni dharau kubwa sana" aliongea mwingine mmoja ya wale wanaume akionekaa kusikitika sana kukatisha usingizi wake kumfuata mtu dhaifu kama huyo. Alivyo maliza kuongea tu aliona kitu kina kuja upande wake ilikuwa ni star moja yenye makali sana, alifanikiwa kuidaka huku akicheka, kicheko chake hakikudumu hata sekunde tano shingo yake ilitobolewa vibaya sana, wakati ameidaka ile star ya kwanza alifurahi akijua amemaliza kazi bila kuweza kujua kama zilirushwa mbili moja ilienda kumaliza kazi, mtu wa kazi hasa alikuwa amekufa kizembe kupita kiasi. Walikuwa wamebaki wanne walichukia sana mwenzao kufa kupumbavu namna ile mbele ya macho yao. Yule aliyeonekana kuwa kiongozi wao alikimbia kwa spidi kumfuata Calvin, zilirushwa ngumi sita ambazo nne Calvin alizipangua vyema lakini mbili zilizama kifuani kwake na kumpa maumivu makali mno, mtu huyo alikuwa anakuja kwa kasi kama jini dakika moja mbele Calvin alikuwa chini kwa mashambulizi makali aliyo yapata kwa mtu huyo, alisimama na kujinyoosha vizuri huku akijifuta futa vumbi kwa maumivu.
"tusifike hatua mbaya namna hii ya kupotezeana maisha huyo aliyekufa anatosha, mnaweza kunambia ni nani amewatuma halafu nyie mkakaa pembeni kabisa ya haya mambo kwa sababu naua watu ambao hata hawahusiki kabisa na hii kesi yangu" Calvin alikuwa anaongea akiwa anajinyoosha mwili wake walau kupunguza maumivu ya ngumi nzito alizopewa na huyo mtu aliyekuwa anapigana nae muda mchache ulio pita.
"kama tukikuacha hai sisi tunaenda kufa kwahiyo hakuna namna ya wewe kuishi kama huwa una namna ya kukimbia hakikisha unainusuru roho yako mapema sana" yule mwanaume aliyekuwa anavuta sigara aliongea lakini wakati huo alikuwa amemfikia Calvin, zilipigwa ngumi za kiume na Calvin moyoni alikiri wazi watu hao walikuwa wamekomaa vilivyo, yule komando wakati anakuja kwa kasi kumpiga teke kwa sarakasi Calvin mwanaume alipiga mguu chini akuurusha mchanga kwa nguvu ulio enda kumuingia machoni yule komando alilia kwa kushikilia macho yake, Calvin alijua ndio muda sahihi wa kumaliza kazi alijiviringisha kwa teke kali alilolenga kuivunja shingo ya yule komando kabla hajamfikia alishtukia anapigwa na kitu kama nyundo kifuani na kurushwa mbali sana, kwanza hakujua mtu huyo katumia nini kumpiga alikuwa chini akitoa damu mdomoni. Wakati anaenda kumaliza kazi kwa yule komando mwenzake mmoja aliliona hilo hivyo alimuwahi Calvin kwa pigo kali la ngumi ya kifua.
Calvin aliona kabisa ameelemewa na akifanya masihara hao wanaume lazima wamuue, alijitupa juu kama mzimu na kutua vyema akiwa amesimama, macho yake yalikuwa yamebadilika na kuwa mekundu sana kwa huo muda hakuwa na akili ya kibinadamu kabisa. Mwili ulikazwa kiasi kwamba unaweza ukadhani hakuna damu inayo pita hapo, aliifuta damu iliyokuwa kwenye mdomo wake na kuuchomoa upanga wake mgongoni, aliyafumba macho yake kwa hisia kali akijua wazi unyama unao enda kufanyika hapo haikuhitajika roho ya ubinadamu kuushuhudia.
Yule komando aliye mpiga ngumi nzito ya kifua alikuwa anakuja kwa mbwembwe sana akijua Calvin ni dhaifu mno lakini alishangaa mtu amepotea ghafla na haonekani aliko, hii iliwatisha makomando watatu ikiwa mmoja wao alikuwa anaendelea kujitoa vumbi la mchanga kwenye macho yake.
"Watch out he's a monster (angalieni ni shetani huyo)" mmoja alitamka kuwatahadharisha wenzake, alivyo maliza sentensi yake tu alikuwa hana mguu mmoja ulikuwa chini alilia kwa sauti kali ya maumivu hata hivyo haikudumu sana kichwa kilitengenishwa na kiwili wili kwa nguvu damu zikiwa zinatiririka kama maji kwenye sehemu ya shingo iliyo tenganishwa ya mtu huyo halafu akaonekana mbele yao akiwa amesimama na upanga wake unavuja damu macho yamekuwa mekundu kama yanatoa mwanga wa kutisha, wale makomando watatu ambao walikuwa wapo salama mpaka muda huo walishtuka na kuogopa walidhani huenda huo ulikuwa mzimu na sio mwanadamu wa kawaida haiwezekani binadamu wa kawaida kuweza kupotea namna hiyo, hii aina ya mapigano Calvin alifundishwa siku ya mwisho kabisa kuishi Japan wakati amepewa mtihani wa mwisho na Hinata Haruto Haru ili aweze kumruhusu kuja Tanzania, alipewa dakika tatu za kuweza kumpiga mzee huyo ngumi moja tu, alipata tabu sana kwa sababu mzee huyo alikuwa anatumia hisia kupotea kwenye macho ya mwanadamu wa kawaida, ilikuwa inahitajika mtu mwenye mafunzo makali mno pamoja na spidi kubwa ya macho kuweza kumuona mtu huyo, hakuna uchawi unao tumika ila ni imani ya mapigano kwa watu walio bobea sana kwenye hiyo sanaa wanakuwa na kasi kubwa sana kama macho yako yamezoea kuangalia tu televisheni na mpira huwezi kuwaona wanapo amua kutumia nguvu zao zote. Huu ndio uwezo ambao Calvin alikuwa anautumia kwa makomando hawa.
Mwingine alijaribu bahati yake kuja kwa mwendo wa zigzaga alibonyea kidogo chini akionekana kulenga eneo ya tumbo alichanganya mapigo yake wakati ngumi inakaribia kumfikia Calvin mwanaume alipotea, yule komando aligeuka haraka baada ya kuhisi kama mtu kampitia pembeni yake, ilikuwa ni kweli wakati anageuka alikutana na teke la shingo alipiga kelele baada ya kuteguliwa shingo yake upanga ulizamishwa ndani ya mdomo wake alitobolewa vibaya sana, Komando mmoja baada ya kuona wenzake wanauliwa na mtu ambaye anaonekana na kupotea aliamua kujihami kwa kuanza kukimbia, hatua ya tano kupiga alidondoka chini mguu ulikuwa umekatwa vibaya na ulitisha kuutazama zilikuwa zimepitishwa star mbili kwenye mguu mmoja ulibakia kidogo sana kuweza kunyofoka wote mwanaume alikuwa akisogea taratibu wakati komando huyo anaomba msamaha hakuwa na maelezo mengi aliuzamisha kifuani upanga wake na kuushindilia kwa mguu mpaka ukatokezea upande wa pili kisha akauchomoa na kuuvuta kwa nguvu huku macho yake yakiwa kwa komando mmoja aliyekuwa amebakia na ndiye aliye onekana kuwa kiongozi wao, macho yalimtoka lakini hakuogopa sana kama wenzake alijiamini sana.
"nijibu maswali yangu tuachane hapa kwa amani ujue kuna muda roho ya kibinadamu inanijia na najuta sana kuwa mtu mkatili sana namna hii, nimetoa roho za watu wengi sana wasio husika na hili jambo kwa sababu tu ya tamaa na viburi vyao sitaki kufanya haya mambo tena naweza nikakosa cha kujitetea kwa MUNGU siku akinichukua japo wanadamu mmenikosea pakubwa sana" Calvin aliunguruma wakati ananyanyuka pale chini kuchomoa panga lake kifuani mwa yule komando aliye muua kikatili huku akisogea alipokuwa amesimama komando ambaye ndiye pekee alikuwa amesalia mahali hapo.
"sina imani sana kama kuna mtu anaweza kukusamehe kwa aina ya mauaji unayo yafanya, hapa kuna mawili ni labda wewe ufe au mimi nife ili mmoja wetu aweze kuishi ama tufe wote lakini hakuna mtu wa kukuruhusu wewe kuondoka hapa ukiwa mzima wa afya namna hiyo" sauti nzito ya bezi kali kutoka Kwa huyo komando iliunguruma kuonyesha hakuogopa chochote ambacho Calvin alikuwa amekifanya hiyo sehemu.
"sawa, ila maswali yangu mepesi tu huyu bwana mdogo mliye muua ni nani? kwanini mumuue?, mlijuaje kama nakuja hapa? na aliye watuma ni nani maana naona kuna mtu ameongezeka katika hili suala sasa mnanichanganya" Calvin alionekana kabisa kudharau na kuuliza maswali yake kama kawaida.
"kama ukiweza kunipiga ndani ya dakika tatu nitakujibu maswali yako ukishindwa ndani ya hizo dakika tatu mimi ndiye nitakaye kuua" Maneno yake yalimfanya Calvin atabasamu kwa mara ya kwanza tangu abadilike, yule komando alikuwa anakuja kwa spidi ya ajabu wakati huo Calvin aliidondosha chini shilingi yake ambayo alikuwa anaitumiaga tu kwa watu walio iva sana na ilikuwa inazunguka kwa dakika tatu, zikiisha dakika tatu ikiwa bado hajakudondosha chini huwa anatoa nafasi nyingine ya mtu kuishi ila ukishindwa kuzimaliza hizo dakika tatu mpaka inadondoka chini maana yake adhabu yako ni kifo, hakutaka kuutumia upanga wake aliuchomeka kwenye ala yake mgongoni na kuukaza mwili wake vyema kwa nguvu akiyafumba macho, ngumi iliyo lengwa kumfikia usoni aliidaka vyema akiwa macho kayafumba kabisa akitaka kuuvunja mkono huo alipigwa na ngumi nzito ya mbavu ila hakuhisi chochote japo Yule komando alifanikiwa kuponyoka kwenye mkono huo wa mauaji ila alirusha kiganja cha nguvu kilicho mpata yule komando shingoni alirudi nyuma kidogo akidhani huenda ni kisu kimepita hapo alipata moyo baada ya kujua hajakatwa yupo salama, Calvin alikuwa anakuja yeye kwa spidi na nguvu kubwa ilifika sehemu yule komando akawa na kazi ya kupangua tu, alipigwa staili ambayo hakuwahi kuiona hata kwenye mapigano yoyote duniani, Calvin aliruka sarakasi ya mbele kumpiga mtu huyo kifuani wakati anakwepa mwanaume alijirudi sarakari ya nyuma akiwa hajaigusa ardhi bado alikunjuka teke moja zito lilimpata yule komando kwenye mbavu alienda kujipigiza vibaya kichwa ukutani kwenye nyumba iliyokuwa pembeni yao akaanza kuvuja damu sana. Alifuatwa hapo chini kama na mtu kama mzimu kwani spidi aliyokuwa anakuja nayo Calvin alikuwa hata hamuoni vizuri alipigwa teke la tumbo lililo mpeleka mpaka ukutani tena mgongo ulijibamiza vibaya akawa anahema kwa shida mno, lilifuata teke zito la kifua alitapika damu nyingi hata hivyo hakuwa na mtu wa kumuonea huruma, Calvin alijirusha juu sana wakati anatua chini ilisikika mifupa ikivunjika kwa sauti kubwa, komando huyo alikuwa amekaribishwa kwenye ulimwengu wa walemavu kwa kuvunjwa magoti yake yote mawili alilia sana wala usingejua ni komando mkubwa sana ndiye alikuwa akitoa hiyo milio ya kutia huruma kubwa, hizo sauti zilisikika vyema kwa wenyeji wa hayo maeneo hakuna aliye jihangaisha kutoka kila mtu aliufunga mlango wake vizuri kwani walikuwa wamesha zoea matukio ya kutisha kila siku kwenye hiyo mitaa.
"Kuna muda wanaume huwa inatakiwa kuongea kistaarabu tu bila kupotezeana nguvu za kufanya kazi kwa sababu jamii itakufanya sehemu ya kukupatia masimango kama mwanaume hautakuwa na uwezo wa kufanya kazi na ukajipatia kipato kizuri, dunia imebadilika sana siku hizi sio kila sehemu inahitajika kutumia nguvu kubwa kueleweshana jambo, nimekuuliza kistaarabu sana ukajifanya wewe unayajua sana haya mambo ila nikwambie kitu kwenye hii dunia ya watu wenye nguvu kubwa unatakiwa uelewe kwamba kuna watu wamekuzidi kila kitu lakini bado hawajionyeshi sasa unapokuwa unawalazimisha watu wa aina hiyo wakuonyeshe vitu vyao kwa nguvu huwa ni hatari mno kwani huwa hawakumbuki kama kuna neno huruma kwenye haya maisha" Calvin alikuwa akimpa somo huyo komando ambaye alikuwa akihema kwa nguvu huku anatoa machozi ya uchungu, alikuwa na maumivu makali ya kichwa na mgongo lakini pia alikuwa amepoteza miguu yake yote miwili.
"naomba niue ndugu yangu ni aibu kubwa mno kuishi nikiwa kwenye hali kama hii nitamtazama nani atakaye niheshimu tena na sikuishi na watu vizuri kwenye maisha yangu" alikuwa akiomba msaada wa kuuawa mtu huyu kwa namna alivyo fanywa hakuona kama kuna nafasi nyingine ya kuishi bila manyanyaso hapa duniani.
"ikitokea ukaja kupewa nafasi ya kuyaishi maisha mengine kwa wakati ujao basi usimsahau MUNGU wako hata kama umefanikiwa kiasi gani pia hakikisha unayaishi maisha kwa usahihi siku zetu zinahesabika kila masaa ishirini na manne yanavyo katika ndivyo tunavyozidi kuwa na nafasi ndogo sana ya kuendelea kuwa hai, sasa nijibu maswali yangu tusimalizane vibaya unaweza ukatenda wema wa mwisho ukapata cha kujitetea mbele ya MUNGU wako kwa kuwaanika hawa mafisadi na kulisaidia taifa nikawasafisha mapema kabla hawaja ziharibu familia nyingi zaidi nchini" Calvin alimuelezea mtu huyu kistaarabu sana kiasi kwamba mwanaume huyo maneno yalimuingia vizuri sana na kujihisi ni mkosefu mbele za MUNGU ni bora hata atumie nafasi hii kutenda wema wa mara ya mwisho, alihema kwa nguvu kujipa nafasi ya kupumua kutuliza kidogo maumivu, akakohoa kidogo kuliweka koo lake safi aweze kumpa Calvin ukweli wa mambo.
58 inafika tamati tukutane tena wakati ujao
Chao[emoji2768]
Bux the story teller
#ULIMWENGUWAWATUWABAYA

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Huyu mzee kasisi chacha nahisi ndio kiongozi wa majambazi na ndie aliyemuweka madarakani waziri mkuu.mtazamo wangu tu.
 
HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA 59
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA.....................
unaweza ukatenda wema wa mwisho ukapata cha kujitetea mbele ya MUNGU wako kwa kuwaanika hawa mafisadi na kulisaidia taifa nikawasafisha mapema kabla hawajaziharibu familia nyingi zaidi nchini" Calvin alimuelezea mtu huyu kistaarabu sana kiasi kwamba mwanaume huyo maneno yalimuingia vizuri sana na kujihisi ni mkosefu mbele za MUNGU ni bora hata atumie nafasi hii kutenda wema wa mara ya mwisho, alihema kwa nguvu kujipa nafasi ya kupumua kutuliza kidogo maumivu, akakohoa kidogo kuliweka koo lake safi aweze kumpa Calvin ukweli wa mambo.

ENDELEA....................

“Hawa watu unao tafutana nao ni hatari sana na ni watu wenye mamlaka makubwa mno serikalini, sisi tunafanya kazi chini ya waziri mkuu wa nchi hii japokuwa jambo hili tumeweza kuligundua hapo juzi tu kwani tulikuwa tukisimamiwa na mwanaume mmoja ambaye ni hatari sana hautakiwi hata kuomba kukutana naye kwenye maisha yako anaitwa Baruan Mahafidhu. Tumekaa kambini kwa muda wa miaka miwili, huwa tunatoka nje ikiwa kuna kazi maalumu ya kwenda kuifanya, tulikuwa jumla ishirini na tano pamoja na Baruan lakini wenzetu kumi tuliambiwa wamekufa na hatukujua wamekufa vipi taarifa zao zilikuwa ni chache mno (Calvin alitabasamu kwani watu hao aliwaua yeye mwenyewe kwa mkono wake). Huyo bwana mdogo ambaye wewe umekuja kumuona hapa ndiye mtu pekee ambaye alikuwa ana siri zote za watu hao kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa anaongoza mifumo yao yote ya kimtandao pamoja na kutengeneza taarifa za uongo za hao watu ambazo zimefanya imekuwa ngumu sana kuweza kuwapata. Ana miaka ishirini tu pekee tumepewa taarifa zake leo asubuhi baada ya kuona mauaji yamezidi sana na muda wowote anaweza kutafutwa akatoa siri za wakubwa. Tulipewa kazi ya kuja kumchukua tumpeleke sehemu iliyo salama tumeamua kumuua baada ya kukuona ukiwa unaingia na gari maeno haya muda ule unapambana na wale vibaka tulikuwa tupo hapa hivyo njia rahisi ya kuendelea kutunza siri ilikuwa ni kumpoteza kabisa duniani” alikuwa akiyatamka maneno yake kwa maumivu makubwa sana huyu komando wakati huo Calvin alikuwa amekaa tu anamsikiliza, akakohoa damu kwa nguvu akatema kisha akaendelea.

“saivi wewe ndiye mtu unaye tafutwa mno kupita kiasi na unatakiwa uuawe kwa gharama yoyote ile, wazo lakwanza ilikuwa ni kuzipata mali zako ndipo uuawe au uachwe ukiwa huna kitu chochote kile lakini kwa namna ulivyokuwa mtu hatari sana unatakiwa uuawe moja kwa moja ndipo mali zako ziweze kubebwa, baada ya kutoka Kongo saivi makazi yetu yapo katikati ya bahari ila bahati mbaya sana sikufanikiwa kujua ni upande upi wa bahari kwa sababu tunavyo pelekwa tunafungwa macho na tunavyotoka tunafungwa macho” alitulia baada ya kutoa maelezo yake mafupi komando huyu ambaye bado alikuwa yupo kwenye maumivu makali sana.

“kwahiyo huko baharini naweza kufika vipi ili niwapate hao watu)? Calvin aliuliza kwa upole kwa sababu aliyekuwa mbele yake alikuwa tayari kumsaidia, komando huyo aliingiza mkono mfukoni kwake akatoa kifaa kidogo ambacho kipo kama limoti

“hiki ni kifaa cha mawasiliano, ukibonyeza hiyo alama nyekundu tu basi wote kumi walio baki ndani ya meli watakuja ilipo hiyo alama, hiyo ndiyo njia tunayo itumia kuwasiliana kwa sisi wote ili kama inahitajika msaada wenzetu wanakuja haraka sana japo hiyo anapewa kiongozi wa msafara tu hivyo hapa mimi ndiye pekee niliye kuwa nacho hiki kifaa” alitoa maelezo sahihi sana mtu huyu huku akimpatia Calvin kifaa hicho.
“na kuhusu kwangu mmewezaje kupajua?” swali la Calvin lilimfanya komando huyu ateme damu chini kisha akajibu
“inasemekana wakati mauaji ya jaji mkuu yanatokea wewe uliweza kuondoka na ile familia mahali pale lakini kuna kosa moja kubwa sana ambalo uliweza kulifanya, simu zote za ile familia zilikuwa zimewekwa kwenye mfumo tayari hivyo iliweza kujulikana kirahisi sana kwamba mpo kigamboni bahati mbaya sana siku tunafika pale kwako hatukukuta mtu inaonekana ile familia ulikuwa ushaitoa kwahiyo tuliondoka tukijua pengine umeshtuka mapema ndio maana hatukurudi mpaka leo tukiendelea kukufuatilia kwa makini sana, ile sehemu unatakiwa kuhama haraka sana kwa sababu muda wowote watakujia pale na huenda mpaka muda huu kuna watu wapo tayari ile sehemu” Calvin alifurahi sana baada ya kujua hata hao watu pia walikuwa wakimsakama sana kwahiyo isingekuwa kazi ngumu sana kukutana nao.

“kuna mtu mwingine ambaye unamjua yupo nyuma ya waziri mkuu?” aliuliza akimkazia macho komando huyo kwa nguvu.
“hapana japo huwa tunahisi hilo jambo ila kwa sababu Anuary umemkosa hapa mtafute mtu mmoja anaitwa Baruan Mahafidhu huyu ndio mkono wa kulia wa waziri mkuu na ndiye anaye jua kila kitu cha yule mzee japo kwa sasa ni siku tatu hajaonekana kabisa na simu hapokei kitu kilicho onekana kumchanganya sana mheshimiwa, zaidi ya hapo hakuna nacho kijua” alimaliza maelezo yake yote ambayo Calvin aliyahitaji akiwa yupo kwenye hali mbaya.
“umelisaidia sana taifa lako lazima utakuwa na thawabu yako siku ya mwisho, unaweza ukanambia unataka nikupe msaada gani? Kwa sababu umenisaidia kunipa maelekezo ambaye huenda nisingeyajua yangehatarisha usalama wangu na raia wengine wengi sana” maneno ya Calvin yalimtoa machozi huyu mwanaume
“wewe ni mdogo kwangu kiumri lakini leo nitakuita kaka, nimekuja kugundua kwamba wewe ni mtu mwema sana tofauti na nilivyokuwa nimetegemea mara ya kwanza, upo tofauti kabisa na wanavyo kusema huko nje. Kwa ukarimu wako ndugu yangu kuna vitu viwili nilivisahau nataka nikwambie kimoja ni mhimu sana na kitakusaidia sana kwenye safari yako. Cha kwanza kwa kesi yako ambayo ilisemekana wewe kupelekwa gerezani kesho waziri mkuu anaenda kukuchafua upya kwa sababu siku ile unapelekwa picha zako zilifichwa uso hivyo unaenda kutangazwa rasmi kama gaidi namba moja nchini na vyombo vyote vya sheria vinaenda kukutafuta zaidi hata ya pesa kwahiyo unatakiwa uanze kuishi kwa kujificha sana na kuchukua tahadhari maana unaenda kuwa mbaya kwa serikali pamoja na wananchi kwa ujumla” haya maneno yalimshtua sana Calvin, alichukulia kimasihara sana hili jambo lakini hakujua kama madhara yake yanaweza kumshinda baadae, aliivuta pumzi kwa nguvu akiwa mwenye mawazo kidogo

“na hicho cha pili ambacho umesema ni kizuri ni kipi” Calvin alikuwa ana shauku kubwa sana ya kutaka kulijua hilo huenda lingemsaidia sana kuweza kutatua tatizo lake jipya ambalo kesho linaenda kumtokea
“kesho jioni majira ya saa mbili mtoto wa kike wa mheshimiwa waziri mkuu anaingia nchini baada ya kukaa nje kwa miaka zaidi ya saba alikokuwa anasoma na inasemekana mama wa mtoto huyo alikuwa ni mwanamke anaye jiuza na haijulikani wapi alipo mpaka hivyo waziri mkuu hakutaka hiyo skendo chafu impate ndiyo sababu alilifanya hili jambo kuwa siri kubwa mno na wanao jua hili ni watu wachache sana, ukimpata huyo mwanamke utakuwa umepata karata aina ya JOKEY ambayo itakuwezesha kuziongoza karata zote alizokuwa nazo waziri mkuu kwani anampenda sana mtoto huyo kuliko kitu chochote kile, usiende kichwa kichwa huyo binti analindwa na makomando wakubwa mno, MUNGU akusaidie katika hilo jitahidi sana kukiokoa hiki kizazi nimekuja kugundua tulipandikizwa roho za kishetani sana ndio maana hatukuwa na utu kabisa ndani mwetu ila nina ombi moja tu la mwisho kutoka kwako” yalikuwa maelezo ya kusisimua sana ambayo kiasi fulani yaliweza kulirejesha tabasamu la Calvin.
“ok nambie nitafanya kama unavyotaka nambie” aliongea kwa furaha sana Calvin
‘naomba uniue kwani ukiniacha kwenye hali hii nitaishi maisha magumu sana kwa niliyo yafanya inatosha na nastahili kufa, sina cha kupoteza kwani hata familia sijawahi kuwa nayo nimekuwa nikiishi kama mnyama ila nashukuru sana kukufahamu vizuri mtu kama wewe kabla sijapotea kwenye uso wa dunia utanikuta huko mbele ndugu yangu” Calvin alishtuka sana mtu anaomba kuuawa huku akitoa machozi kumaanisha yupo siriasi sana na anacho kisema. Mwanaume alifumba macho hakutaka kupoteza muda kwa sababu alijua komando kama huyo hataweza kubadilisha msimamo wake pale anapohitaji kufanya jambo lake, sekunde thelathini mbele alikuwa ameushika upanga wake mkononi ukiwa umejaa damu alishapita na shingo ya huyo komando japo ilimuuma sana kumpoteza huyo mtu ambaye amekuwa mhimu sana dakika za mwisho, hakuwa na cha kusubiri mahali hapo aliiokota shilingi yake na kulifuata gari lake kisha akaondoka kwa spidi kali sana.
Siku ya nne tangu aweze kulazwa hospitali akiwa kwenye hali mbaya sana Victor ndio muda ambao alikuwa anakurupuka kwenye usingizi huo wa kifo baada ya kufumbua macho kwa mara ya kwanza tangu akutane na kipigo kikali mno kutoka kwa Baruan Mahafidhu, kichwa kilikuwa kinamuuma sana kila akijaribu kuinuka hapo kitandani basi aliamua kujilaza kwanza aone hatima yake maana mpaka muda huo alikuwa hakumbuki chochote kile kilichokuwa kinaendelea. Baada ya dakika tano kumbu kumbu zake zilianza kurejea vyema kabisa akakumbuka lile tukio la siku ya mwisho alijikuta akikurupuka sana kutoka hapo kitandani akihitaji kwenda nyumbani akamuone mwanamke wake kwani alikuwa na maswali mengi sana kuhusu tukio la siku ile, hata hivyo hakuwa na nguvu zozote zile za kuweza kusimama peke yake aliishia kutoa machozi tu hali aliyokuwa nayo ilikuwa ni aibu kubwa sana mbele ya komando kama yeye. Daktari aliyekuwa na umri ulio onyesha wazi ni mtu mzima sana aliingia kwenye hicho chumba kwa hali aliyokuwa nayo Victor alimsikitikia kwa kiasi kikubwa mno kijana huyu
“unahitaji kumuona mwanamke wako” swali la daktari lilimtoa kwenye taharuki
“kwani nayeye yupo hapa?” aliuliza kwa mshangao sana Victor kwani siku ile wakati anazimia Marry alikuwa yupo sawa tu japo alionyesha mshtuko mkubwa baada ya kumuona Baruan. Daktari alimchukua taratibu akiwa anamsaidia kutembea kwa kumshikilia akampeleka kwenye chumba ambacho hakikuwa mbali na hayo maeneo, humo ndani ndicho chumba ambacho alikuwa amelazwa Marry kwa siku nne mpaka leo.
“ana muda gani tangu yupo hapa? na vipi usalama wake pamoja na mtoto tumboni? Victor alimuuliza huyu daktari macho yake yakiwa bize kumwangalia Marry ambaye muda wote macho yake yalikuwa yamejaa machozi yakishuka taratibu.
“ana siku nne hapa” daktari alimjibu bila kupepesa macho
“unataka kuniambia mimi nimelala siku nne nikiwa sijitambui” Victor alipigwa na butwaa kwa yale maelezo ya daktari.
“wewe ni miongoni mwa binadamu wenye bahati sana kuwahi kuishi hapa duniani, kwa namna ulivyokuwa umevunjika hatukuwa na imani kama unaweza kusimama tena, huyo mtu aliyekufanyia hivyo hautakiwi kukutana naye tena kwenye maisha yako kwa sababu kama atakupiga tena zaidi ya ngumi nne una hatari kubwa ya kupata mtindio wa ubongo unao weza kukupelekea kupoteza kumbu kumbu zako zote, ukichaa au kufa. Mkeo ana mimba ya miezi sita sasa ila bahati mbaya imeonekana alikiona kitu ambacho kilimshtua sana kwenye maisha yake huenda ana historia nacho kubwa sana na hakutegemea kukiona wakati ule ile sehemu hivyo presha yake inapanda na kushuka sana kwa sasa anatakiwa kupata mtu ambaye atakuwa karibu naye muda wote ili awe sawa” Victor hakujali sana kuhusu hali yake alikuwa na wasiwasi sana kuhusu mwanamke yule ambaye alikuwa yupo mbele yake, alitoka kwenye kioo hicho kilichopo nje alipokuwa anatazama ndani na kuchechemea mpaka ndani ya chumba hicho, hali ilikuwa imekuwa tofauti sana na alivyokuwa amefikiria yeye mwanamke aliyekuwa mbele yake alikuwa kwenye hali ya huzuni kubwa wakati yeye alitegemea mwanamke huyo akimuona atafrahi sana,ni kitu kilicho muuma mno jasusi huyu.
"Shetani mkubwa wewe umefuata nini hapa na unataka nini kwenye maisha yangu, wewe ni nani na kwanini unifanyie haya nimekosa nini mimi kwenye hii dunia?" Sauti ya ukali ya Marry ya ghafla sana ilimshtua sana Victor akashindwa kuelewa amefanya kosa gani mpaka mwanamke huyu aliye mpenda sana awe mkali sana mbele yake wakati yeye ndiye aliyekuwa na maswali mengi sana ya kumuuliza mwanamke huyo.
"Mmmmmhhhhhh aaghr" sauti nzito ya mtu akiguna ilimshtua sana Victor ikamlazimu kugeuka haraka sana ndipo aliposhangaa sana mtu aliyekuwa akimuona nyuma yake na huenda ndiye aliyefanya Marry kuongea kwa hasira sana hapo kitandani akiwa anatia huruma na kuzidisha machozi sana.
Unahisi huyu mtu aliyefika hii sehemu ni nani hasa?

59 sina la ziada tena tukutane wakati ujao

Chao[emoji2768]

Bux the story teller

#ULIMWENGUWAWATUWABAYA

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Kwa shilingi 1500 tu isome hadithi hii mpaka mwisho.

Namba za malipo ni

0621567672 (WhatsApp)
0745982347

Jina FEBIANI BABUYA

unatumiwa muda huo huo[emoji3578]

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA 60
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA....................
"Mmmmmhhhhhh aaghr" sauti nzito ya mtu akiguna ilimshtua sana Victor ikamlazimu kugeuka haraka sana ndipo aliposhangaa sana mtu aliyekuwa akimuona nyuma yake na huenda ndiye aliyefanya Marry kuongea kwa hasira sana hapo kitandani akiwa anatia huruma na kuzidisha machozi sana.
ENDELEA.....................
"Baba" Victor alipigwa na mshangao mkubwa baada ya kugundua aliyekuwa hapo ni Kasisi Chacha hata hivyo hakupewa jibu lolote lile mzee huyu alikuwa amemkazia macho Marry au Ester pale kitandani alipokuwa amelala.
"Huyu shetani ni baba yako?" swali la ukali kutoka kwa Ester lilimfanya Victor ageuke tena kumwangalia na kumpa mgongo Kasisi Chacha
"umeshapata ukichaa?mpaka ufike sehemu unamkosea mzee wangu mpaka umuite shetani hivi una akili kweli wewe mwanamke" Victor aliuliza akiwa amebadilika macho yake kwa muda huo hakujali kama mwanamke huyo alikuwa mjamzito kitendo cha kutukaniwa mtu aliye mlea ilikuwa ni dharau kubwa sana kwake, alijiandaa ili akampige hata kofi mwanamke huyo lakini Kasisi Chacha alimdaka mkono ikabidi atulie.
"muulize mwenyewe kanifanyia nini kwenye maisha yangu" alijibu kwa ukali Ester akiwa anatoa machozi mengi sana ilimbidi Victor ageuke na kumuuliza Kasisi Chacha
"Baba kuna kitu gani kimefanyika hapa katikati mpaka akuchukie sana kiasi hiki?" Victor alitegemea jibu zuri kutoka kwa huyu mzee lakini ilikuwa tofauti kabisa na alichokuwa anakifikiria.
"nimemuweka mbali na furaha ya maisha yake ndiyo maana alivyojua juzi amenichukia sana" sauti nzito ya Kasisi Chacha iliunguruma.
"kumuweka mbali na furaha yake kivipi" swali liliulizwa na Victor.
"ndio sababu siku ile nilikwambia kwamba umekurupuka sana kuishi na huyu mwanamke, hivi ushawahi hata siku moja kukaa ukajiuliza huyu mwanamke historia yake ipoje? au ulikimbilia tu kwa kuchanganyikiwa na uzuri wake?" Maneno mazito sana yalitamkwa yaliyo mfanya kidogo Victor ajione ni mjinga sana hakuwahi hata kufuatilia maisha ya mwanamke huyo ambayo aliyaishi kabla yeye hajakutana naye.
"yule mwanaume aliyekuja kwako ukapambana naye ni mumewe halali wa ndoa kabisa ndio maana amepata mshtuko mkubwa kiasi hicho" Victor mwili ulikosa nguvu kabisa ikamlazimu kukaa chini hata hizo nguvu za kusimama hakuwa nazo kwa muda huo, hakutamani anacho kisikia uwe ni uhalisia wa mambo, alitamani mtu mmoja aje na kumwambia alikuwa anataniwa tu, alikuwa amempenda mno mwanamke huyu na aliridhia kuishi naye kwa muda ambao MUNGU atambariki kuendelea kuliona jua hakutaka kuamini eti Ester ni mke halali kabisa wa mtu tena wamefunga ndoa, baada ya kutamka maneno hayo Kasisi Chacha alitoka humo ndani haraka sana akimuacha Ester anapiga kelele pale kitandani
"unewapeleka wapi wazazi wangu shetani mkubwa wewe, niletee familia yangu kwanini unanifanyia hivi" sauti za Ester Victor hata alikuwa hazisikii akiwa amekaa chin ya kitanda hicho alichokuwa amelazwa mwanamke aliye mbebea mtoto tumboni mwake, hakuona sababu ya kuendelea kubaki ndani humo akihisi amesalitiwa pakubwa sana hakutaka hata kuijua sababu mwanaume aling'ata meno yake kwa hasira sana akanyanyuka kwa nguvu na kuhitaji kuondoka humo ndani kwa hasira ila kabla hajafanya hivyo alidakwa mkono wake alipogeuka nyuma alimuona Ester akiwa anamtazama machozi yamemjaa usoni.
"Hivi ni kweli yule ni baba yako?" Ester aliuliza akiwa anajikaza tu lakini alikuwa na uchungu mkubwa sana kwenye moyo wake
“kama usingekuwa mjamzito kwa huu ujinga ulio ufanya ningekuua mimi mwenyewe kwa mkono wangu”Victor alitamka kwa hasira bila kujali chochote aliutoa mkono wake kwa nguvu sana na kuanza kutoka humo ndani.

“kwhiyo wewe na baba yako ndiyo mliokuwa nyuma ya haya yote” swali la Ester lilimfanya Victor kidogo asimame.

“unapaswa ulitamke kwa heshima sana jina la huyo mzee, bila yeye ningekuwa mtoto wa mtaani mpaka leo, amenichukua nikiwa bado mdogo sana sina sehemu yoyote ya kulala, sina chakula, hakuna mtu hata mmoja aliyeweza kunijali mimi ila yeye pekeyake aliliona hilo, akanipa elimu bora sana mpaka leo nimekuwa komando mkubwa sana wa kutegemewa ndani ya idara ya usalama wa taifa pamoja na nchi kwa ujumla leo unataka kuongea nini mwanamke mshenzi wewe. Umekuja kwenye maisha yangu kwa kujifanya unanipenda sana kumbe una ajenda zako mwenyewe, kwahiyo yule hawala wako ndiye aliyekutuma uje unipeleleze maisha yangu sio hahahahahah……. Sikujua kama wewe ni miongoni mwa wanawake washenzi sana kwenye hii dunia, sikuwahi kumpenda mtu yeyote yule umenifanya nikupende nilikuwa tayari hata kukupa dunia yangu yote na kila kitu kwenye maisha yangu kumbe naishi na nyoka ndani ambaye ni mke wa mtu tena komando aliye liasi taifa, inamaanisha nawewe uko nyuma ya hili, sitaki kujua kama wewe ni gaidi kama huyo bwana ako na sitaki kujua kama mlikuwa na mpango gani kwenye maisha yangu, nitakuacha hai ila hakikisha hatuji kuonana tena kwenye maisha yetu sitakusamehe tena kama leo liweke akilini hilo” Victor aliongea kwa uchungu mkubwa kupita kiasi akiwa kwenye majonzi mazito sana hata kuongea maneno makali hayo mbele ya huyo mwanamke aliye mpenda alikuwa akijikaza tui la ilikuwa inamuuma sana, alibamiza mlango kwa nguvu kubwa na kutoka humo ndani akisahau kwamba daktari alimshauri kama mwanamke huyo anahitaji uangalizi mkubwa mno.

Kwa Ester ni kama alitoneshwa kidonda kingine kipya kwenye moyo wake licha ya kugundua kama Victor haelewi chochote juu ya hilo na sio mtoto wa Kasisi Chacha lakini ukali wa maneno ambayo Victor alimtamkia ulimfanya ajisikie kama kuna mtu kamchoma na kisu kingine kipya kwenye moyo wake, alihisi amepoteza kila kitu kwenye maisha yake mpaka siku anampata Victor aliamini huyo ndiye familia yake atakayo ishi nayo kwa furaha baada ya kuteseka na upweke wa muda mrefu sana. akiwa kwenye simanzi nzito kwenye hicho kitanda kumbu kumbu zake zilienda mbali sana tangu yupo India alivyoweza kuishi na Roland ambaye alikuwa mwema sana kwake kiasi kwamba wakaingia mpaka kwenye bahari ya huba lakini safari hiyo ilikuja kuisha baada ya kurudi nchini Tanzania baada ya Roland kupotea ghafla bila kueleweka ameenda wapi lakini kiuhalisia kazi ya Roland ilikuwa ni kuhakikisha usalama wa binti huyu tangu yupo India mpaka anarudi Tanzania baada ya kulifanya hilo kwa usahihi alipewa maelekezo na mkuu wake Kasisi Chacha kwamba haruhusiwi tena kumuona mwanamke huyo kwenye maisha yake. Maisha yake yote Ester aliishi akijua mwanaume wake huyo ameshakufa kwahiyo alishtuka mno baada ya kumuona mwanaume huyo mbele ya macho yake, ilimnyima raha pakubwa sana ni jambo ambalo hakulitegemea kabisa kumtokea muda kama huo.


****************************************************
Calvin baada ya kutoka Temeke hakurudi moja kwa moja Kigamboni alihisi huenda kuna watu wanaweza kumfuatilia kirahisi sana na kwa huo muda alihitaji kupumzika, mwanaume aliingia ndani ya Kawe akatafuta hoteli moja majira hayo ya usiku wa manane akafanikiwa kuipata, alilala usingizi mzito sana mpaka alipokuja kushtuka asubuhi na mapema sana, akiwa anatoka kuoga alisikia mlango unagongwa akahisi huenda kuna watu wamemtembelea mapema sana akataka kuvaa haraka sana lakini alitulia baada ya kusikia sauti moja nzuri sana ya kike basi alifungua mlango taratibu akiwa amevaa taulo tu, kama alivyokuwa ametegemea alikuwa ni mhudumu akiwa amemletea supu moja nzito sana ikiwa ni utaratibu wao wa kila siku kwa kila mteja ambaye analala ndani ya hoteli yao. Alikaa na kuanza kupata supu yake taratibu bila hata wasi wasi wowote ule, supu iligeuka kuwa chungu baada ya kuiwasha televisheni iliyokuwa humo ndani, hakuamini kitu alichokuwa anakiona mbele yake ilikuwa ni taarifa ya habari ya asubuhi kabisa na mbele ya hiyo skrini alisimama mheshimiwa waziri mkuu pembeni zikiwa zimeambatanishwa picha zake yeye mwenyewe Calvin Jackson japo kwenye hizo picha hakuwa na ndevu ikionekana ni picha za muda kidogo.

“shiiiiiiiiiiit…….” Alitamka kwa hasira akibamiza chini bakuli la supu kwa hasira akitulia ili kumsikiliza mzee huyo kwa uchache japokuwa hakujua kama ndio anaanza au anamaliza.

“Calvin Jackson Aron Mavunde ndilo jina lake huyu mtoto, kwa sasa amefikisha miaka 25 na ana mvuto mkubwa sana ukimtazama machoni, huyu ni mtoto wa tajiri mmoja mkubwa sana ambaye kwa bahati mbaya miaka mitatu iliyopita aliweza kututoka baada ya kuvamiwa na kuuawa na watu wasio julikana, huyu mtoto alipotea ghafla sana baada ya mauaji ya wazazi wake zaidi ya miaka miwili sasa huu ni watatu. Tangu wazazi wake wamekufa tumefanya uchunguzi wa kina sana tumegundua kwamba yeye ndiye mhusika mkuu wa mauaji ya wazazi wake na alifanya hivyo ili aweze kumiliki mali za wazazi wake, kwa sababu alikuwa ni mjeuri sana kwenye familia yake ndipo baba yake alipogoma kumrithisha mali zake akaamua kuwaua ili abaki na mali hivyo akaamua kuwaua ili tu azichukue. Sio hilo tu inaonekana alienda kujipanga na kuungana na makundi makubwa ya kigaidi kwani baada ya kurudi alianza kuwatafuta maaskari na wanajeshi wetu ambao wanaijua siri yake hiyo na kuwaua kikatili sana, mpaka sasa maaskari na wanajeshi alio waua ni mia moja ikiwa ni pamoja na kuwabaka wanawake saba na kuwaua wote, tulifanikiwa kumkamata kwa mara ya kwanza na raisi alitangaza hadharani lakini magaidi wenzake walivamia msafara na kumtorosha.

Mimi kama waziri mkuu wa hii nchi iliyo barikiwa sana amani ninalaani na kukemea haya yaliyo tokea hivyo huyu mtu nahitaji vyombo vya dola kuanzia jeshi la polisi na jeshi la nchi wamtafute popote pale alipo na aweze kuuawa kikatili sana mbele ya hadhara ili kuweza kulinda usalama wan chi yetu kwani akiachwa hai itakuwa ni hatari kwa raia na mali zao, natoa rai kwa raia wema kwa yeyote atakaye saidia kutoa taarifa juu ya upatikanaji wa mtu huyu atazawadiwa pesa za kitanzania taslimu milioni miamoja, naomba tusaidiane sana kwenye kulilinda taifa lililotengenezwa kwa jasho na damu na waasisi wetu kwa kumteketeza huyu gaidi” hotuba fupi ya waziri mkuu ilimfanya Calvin apoteze nguvu ikamlazimu akae chini akiwa na machungu makubwa sana, inauma sana mtu anayekufanya unaishi kwa shida ndiye huyo anaye kwenda kuwatangazia watu kwa jeuri kabisa kwamba wewe ndiye mtu mwenye makosa na haufai hata kidogo kwenye jamii kiufupi waziri mkuu aliona kwake hiyo ni njia rahisi sana ya kumdhibiti huyu kijana ambaye alianza kuwa hatari kwake, alitamani aweze kuingia kwenye hiyo televisheni akutane na mzee huyo aliapa angemuua kikatili kuliko binadamu yeyote yule ambaye alishawahi kumuua kwenye maisha yake. Aliuma meno kwa hasira akipiga na kupasua meza kubwa ya kioo iliyokuwa mbele yake hapo, leo alikuwa amepewa kesi nzito sana ambayo hakuwahi hata kuifikiria kwenye maisha yake, aliwaza wananchi ambao ni zaidi ya milioni 40 watamtazamaje yeye, ingekuwa ni kuua tu wanajeshi sawa vipi kuhusu kubaka wanawake na kuwaua! Ilimuumiza kichwa sana bwana mdogo, kila mtu alimchukia kwa dakika moja tu pekee alichanganyikiwa Calvin roho ilimuuma sana, wakati akiwa hapo simu yake ya mkononi ilianza kuita ghafla na kwa fujo sana.

Hasira zilikuwa zimemjaa kwa kiasi kikubwa sana na asingeweza kuongea na mtu kwa huo muda, aliona hiyo sehemu haimfai tena kwa sababu kuna mhudumu aliye mletea supu alikuwa ameshamuona tayari japo hakuwa na uhakika kama alifanikiwa kumtambua sura yake ambayo kwa sasa ilikuwa na ndevu zilizokuwa zimechongwa kwa usahihi mkubwa mno. Alivaa nguo zake ambazo zilikuwa za kazi alichukua simu yake na kila kitu chake hata hakufunga hapo ndani alitoka kwa haraka kubwa mno. Wakati anatoka wahudumu wote walimshangaa kwani nguo alizokuwa amevaa sio mavazi ya Tanzania kabisa walikuwa wanaziona kwenye picha za maninja hususani kutoka ndani ya nchi ya Japan, ni nguo za kazi na mara nyingi huwa anazivaa majira ya usiku tu leo hii asubuhi na mapema kabisa alikuwa amezitinga kwenye mwili wake na hakuna aliyeweza kumtambua kabisa kwa sababu ya kofia kubwa iliyokuwa imeficha uso wake, panga lake kama kawaida lilikuwa mgongoni na star zake za kutosha zikiwa kiunoni japo ilikuwa ni ngumu sana kuziona. Alipanda kwenye gari na kutoka ndani hapo kwa spidi kubwa kitu kilicho washtua sana baadhi ya wateja ambao walikuwa wamewahi mahali hapo kwa ajili ya kupata huduma, wakati anaanza kuitafuta bara bara ya kwenda mwenge akiwa amepandisha mpaka juu vioo vyake vya gari alipishana na gari sita za jeshi zikiwa zinaelekea sehemu ya ile hoteli alikotokea akajua lazima yule dada ameshapiga simu hivyo alijua anatakiwa kuchukua tahadhari kubwa sana kwani sura yake inaonekana inajulikana vilivyo. Ni kweli zile gari sita zilikuwa zinaelekea kwenye ile hoteli, walifika pale na kumtafuta yule dada aliyeweza kuwapigia simu akawapeleka moja kwa moja kwenye chumba alichokuwepo Calvin, wakiwa na siraha kali za vita wanajeshi wapatao hamsini walishangaa mlango huo uko wazi, waliingia haraka na kutafuta kila sehemu mpaka bafuni lakini hakukuwa na mtu. Kiongozi wa msafara alivyo angalia chini alilishika bakuli lile la supu na kuona bado la moto kabisa alitamka kwa jazba

“pumbavu huyu kaondoka sio muda na atakuwa hajafika mbali, ebu tuonyeshe chumba cha kamera hapa haraka sana” alikuwa anaongea kwa sauti kali ya mamlaka mwanaume huyu iliyo anza kumuogopesha mpaka huyu mhudumu aliye waita hapa. hawa walikuja na gari za jeshi lakini kiuhalisia walikuwa ni makomando kabisa wa siri waliokuwa chini ya mkuu wa majeshi, kwa aina ya mtu waliyekuwa wanamtafuta walijua kama wakienda wanajeshi basi watakufa wengi sana ikawalazimu kuweza kuwatumia makomando kabisa ikiwa ni ombi la waziri mkuu huyo kwa mkuu wa majeshi baada ya kudai anahitaji kuilinda amani ya nchi ili waweze kumaliza kazi mapema sana. waliingia kwenye chumba cha kamera na kurudisha dakika kadhaa nyuma kweli wakaona kuna mtu ana mavazi meusi anatoka humo ndani.
“tuondoke haraka sana humu ndani huyu ni yeye ametoka sio muda mrefu sana” alitamka huyo kiongozi ambaye hakuonyesha hata sura ya masiara huku akimrushia mhudumu huyo maburungutu mengi sana ya pesa kwa sababu alitoa taarifa ambazo ni sahihi kabisa na walijua wazi watampata tu na kama wakimkamata basi mwanamke huyo angetefutwa kupewa pesa yake nyingine alifurahia mno kupata pesa nyingi kiasi hicho na hakuona haja ya kuendelea kufanya hiyo kazi ya hotelini mkononi akiwa na milioni thelathini alizopewa hapa bila kujua kwamba kamsababishia matatizo makubwa sana kijana wa watu ambaye hana hatia yoyote ile, gari za jeshi zilitoka kwa spidi hapo iliwatisha baadhi ya watu wakaanza kuondoka kwenye hiyo hoteli baada ya kuamini hapakuwa na usalama wa kutosha.

Unadhani Calvin anatokaje kwenye hili? atapona vipi ikiwa kila chombo cha usalama kinamtafuta na kila mwananchi alimchukia sana kwa aina ya kesi aliyokuwa amepewa? nini hatima ya kijana huyu asiyekuwa na hatia yoyote ile?

60 inafika tamati panapo majaaliwa ungana namimi tena wakati ujao

Chao[emoji2768]
Bux the story teller

#ULIMWENGUWAWATUWABAYA

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Kwa shilingi 1500 tu isome hadithi hii mpaka mwisho.

Namba za malipo ni

0621567672 (WhatsApp)
0745982347

Jina FEBIANI BABUYA

unatumiwa muda huo huo

Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom