Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Vipande vilivyo bakia 8 kuelekea mwishoni navitoa kwa 500 tuHADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA 68
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA................
mheshimiwa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alifoka kwa hasira sana baada ya bwana mdogo kumwambia kitu ambacho kwake wazi kisingewezekana kutokea hata iweje, hao watu wawili waziri mkuu na kasisi Chacha alikuwa akiwaamini mno kwa sababu walikuwa wanamtii sana kuliko mtu yeyote yule nchini hivyo kuambiwa ndio hao wapo nyuma ya kila kitu aligoma kabisa raisi huyu kisha akaanza kuondoka hayo maeneo akiwa na gadhabu kubwa sana moyoni huku akiwaacha Calvin na Luciana hilo eneo wakiwa wanamshangaa.
ENDELEA...............................
“haimaanishi kwamba bila wewe sitaifanya hii kazi hicho ni kitu ambacho hakiwezekani hata dunia ikigeuka leo kuwa sayari nyingine, sikuja kuomba ruhusa yako ndipo nifanye maamuzi, niliamua kukusikiliza baada ya kugundua uliwahi kuwa karibu na baba yangu vinginevyo tusingepata nafasi ya kukaa tukazungumza kwa amani sana namna hii. Ninakuruhusu kama una uhitaji wa kuwa tofauti namimi ni chaguo lako, kama utaona nacho kifanya sio sahihi pia unaruhusiwa kuchukua maamuzi yoyote kama raisi wa nchi ila nataka nikuhakikishie hakuna binadamu aliyezaliwa na mwanamke atakayeweza kunizuia kwa sasa hapa duniani kwa sababu ukiniuliza nani wa kunizuia ni watu wawili tu ndio hao nina uhakika hapa duniani wanaweza kunizuia na kuniua na kwa bahati mbaya sana ndio watu wanao niombea usiku na mchana nimalize kazi hii mapema kwani ndio wanao takiwa kunilinda na kunifanya niwe salama kwa gharama yoyote ile, sikutaka kuwatumia kwa sababu kuu mbili, yakwanza hii vita ni yakwangu mimi sio yakwao lakini sababu ya pili niliogopa kama wangeingiza mikono yao kwenye hili hii nchi ingetapakaa sana damu huenda amani ingepotea kabisa ni watu hatari sana hata ulimwengu mzima hautambui sana utambulisho wao japo kila nchi inawahitaji sana kuwapata, hawa ndio walimu wangu mimi walio nifundisha mmoja ni kama baba kwangu na mwingine ni kama kaka kwangu(alikuwa akimaanisha Hinata Haruto Haru pamoja na mtaalamu Akio jasusi wa kimarekani huyu). Hivyo usije ukahisi kwamba labda nakutegemea sana wewe hapo, hauna msaada mkubwa wowote kwangu nakuheshimu tu ila kama ikitokea ukaondoka kwa dharau leo inabidi uikumbuke hii sura vizuri usije hata siku moja ukahitaji msaada wangu tena nitakuwa na majukumu mengi sana ya kufanya, kabla hujaondoka kafungue kwenye ule mlango wa gari ile” sauti moja ya ukali kutoka kwa Calvin ilimfanya mheshimiwa asimame kidogo wakati huo alikuwa ameshaanza kupiga hatua za kuondoka eneo hilo kwa hasira, Luciana na Deus walishangaa mtoto mdogo kiasi hicho anapata wapi ujasiri wa kumjibu raisi wa nchi kiwepesi sana namna hiyo.
“umefikia hatua unamtishia amani raisi wako bwana mdogo” ilikuwa ni sauti ya raisi akiwa anageuka nyuma kumtazama Calvin kwa jicho kali sana.
“nimekuambia kwenye lile gari kuna kitu ulipaswa ukijue ila kwa sababu umekuwa jeuri sana acha tuone mwisho wako utakuwaje, kuna siku niliwahi kukwambia na leo narudia tena huwa ni hatari kubwa sana kama wewe ndiye raisi wa nchi halafu kuna viongozi wadogo ambao umewaweka wewe mwenyewe wanakuzidi akili na maarifa hicho kiti chako wanaweza kukichukua muda wowote ule wakijisikia wao kwa sababu wewe upo pale kama gazeti tu wao ndio wauzaji wakuu ambao wanaamua wanaliuza hilo gazeti kwa bei gani. Msaada wangu unaishia hapa kwenye maisha yako, nimekupa njia na kukutajia wabaya wa nchi yako na kuna viongozi wengine wengi tu wapo chini yao kwahiyo utajua namna ya kujilinda mwenyewe na unapaswa ujue kwamba wakijua kwamba unajua hautamaliza hata usiku mmoja lazima utakufa tu na nchi wataichukua kwa nguvu, raisi gani unashindwa kujiuliza kwanini watu wa ikulu wafanye mambo ya siri mpaka kupeleka wafungwa gerezani bila wewe kujua na bado unawatetea tu” Calvin aliongea kwa hasira sana huku akinyanyuka hapo na kuanza kuondoka na kuingia kwenye gari akibamiza mlango kwa hasira ikambidi Luciana ainame kutoa heshima kwa mheshimiwa raisi japokuwa alikuwa kwenye baibui haikumzuia kumpa heshima za kutosha bosi wa nchi ya Tanzania ukizingatia yeye ni komando wa nchi aliingia kwenye gari akawasha na kuushika usukani kisha akalitoa gari kwa spidi kubwa sana.
“Tunaenda wapi?” swali kutoka kwa Luciana lilimshtua Calvin walati huo alikuwa amejilaza kwenye siti ya nyuma akiwa na mawazo sana.
“nipeleke kigogo ilipokuwa kambi yenu” Luciana alishtuka baada ya kusikia hicho kitu kwa sababu alijua lile eneo litakuwa chini ya ulinzi mkali sana kwa wakati huo.
“kuna nini kule?” aliuliza tena
“nadhani kuna kitu nahitaji kukihakikisha tena ile sehemu nahitaji niwajue wale watu ni akina nani kwa sababu miezi kadhaa nyuma siku mzee Ndipo Mwalemi ameniomba nikamuokoe binti yake nilikutana na watu wakiwa na nguo za jeshi kabisa la nchi na siraha za kivita ambazo hakuna mwananchi wa kawaida anaruhusiwa kuzimiliki, nataka nijue kama ndo wale wale au kuna wengine sitaki nipige hesabu mbovu nitarudi nyuma hatua nyingi sana nina muda mchache sana wa kuendelea kuishi ndani ya nchi hii” Calvin aliongea kitu kilicho mshtua sana Luciana
“una muda mchache ukiwa unamaanisha nini?” aliuliza huku akiwa makini sana na usukani
“ni mambo mazito sana ambayo wewe huwezi kuyaelewa ila kiufupi ni kwamba kila siku zinavyozidi kwenye mbele mwili wangu unazidi kuwa hatari sana kwa sababu mwili wangu umetengenezwa na watu wengi sana kwa muda mfupi na kuna imani zao za kininja sikuzimaliza zote ila zinazidi kuniingia taratibu zenyewe kila navyokuwa na hasira hiyo inanipelekea nakuwa mtu hatari sana hususani nikiushika upanga, kuendelea kukaa sana kwenye nchi hii ipo siku nitashindwa kuzizuia hizi nguvu matokeo yake ninaweza kuwa kiumbe hatari sana kwa taifa baadae kwa maana itakuja kufika sehemu hata mwalimu wangu mwenyewe hataweza kuja kunizuia kutokana na maelezo yake hivyo sipaswi kuwa na hasira kupitilia nakuwa kiumbe kingine kabisa tofauti na hivi unavyo niona na hii sura ya kuvutia ila nikiwahi kule wana namna wanaweza kuzizuia hizi nguvu zikabaki kuwa za kawaida tu” hayo maelezo yalikuwa yakimtoa jasho Luciana alijua wazi anatembea na kifo mkononi mwake amekishika, kutembea na mtu wa aina ya Calvin ilikuwa ni hatari sana hivyo ilimpasa kuwa makini mno.
Alitaka kuuliza lakini kwa mbele akaona kuna kizuizi cha wanajeshi wengi sana alipandisha kioo kwa kasi, alivyo karibia hilo eneo alikuta kila gari linapigwa msako mkali sana njia hiyo ya kuelekea Kigogo. Alisimamishwa na gari lake akiwa anaiweka baibui yake vizuri kwani hata yeye mwenyewe kama angejulikana yupo hai lilikuwa ni tatizo kubwa alitakiwa kuuawa pamoja na wenzake siku ile. Alikuja mwanaume mmoja mwenye misuli iliyoshiba, alimsalimia mwanamke huyo kwa heshima kulingana na mavazi ya stara aliyokuwa ameyavaa akionekana macho tu pekee, mwanaume huyo aliye onekana kuwa mtu aliye iva kwenye dini yake alimuuliza mwanamke huyo kistaarabu huku akiitoa picha ya Calvin na kumuonyesha Luciana alitikisa kichwa kuonyesha wazi hakuwahi kumjua mwanaume huyo kwenye maisha yake, alimruhusu apite kwa sababu aliona ni mwanamke safi sana anaye ijua dini yake hivyo humo ndani asingekuwa na mtu huyo ila hesabu zake zilienda vibaya sana hilo ndilo gari alilokuwa amepanda Calvin, mwanajeshi yule alilitazama sana lile gari mpaka linaishia sababu ilikuwa ni moja licha ya mwanamke yule kuwa na mavazi yale bado alikuwa na mashaka naye sana kwa aina ya macho aliyokuwa nayo, huwa wanakuwa nayo watu ambao ni hatari sana kwenye mapigano hususani makomando au magaidi wakubwa yapo tofauti sana na macho ya kawaida ila aliamua kupotezea tu.
“mhhhh mbona unajiamini sana wewe mwanaume yani unatafutwa kama pesa hivyo na bado hata hauhangaiki kujificha umekaa huko nyuma kwa starehe tu kama kwako hapa vipi kama angeamua kuhakikisha gari zima?” Luciana aliongea huku akijichekesha
“yule kijana ndiye anayepaswa kuogopa na sio mimi, ana bahati kubwa sana kuendelea kuishi kwa sababu kama angejua mimi nipo humu alikuwa anajiponza yeye na wenzake wangekufa vibaya sana ni bora hajajua lolote” Calvin alijibu akiwa anamwangalia mtoto wa waziri aliyekuwa bado kwenye usingizi mzito kutokana na uwingi wa dawa alizokuwa amezimishwa nazo.
“raisi yupo kwenye wakati mgumu sana sijui utamsaidiaje anaonekana kuto muamini mtu yeyote yule kwa sasa nadhani atakuwa mtu mwenye mashaka makubwa sana” Luciana alionekana wazi anamsikitikia raisi huyo wa nchi yake.
“kuzungukwa na watu wa hovyo ni miongoni mwa makosa makubwa sana ambayo wanadamu wengi siku hizi huwa wanayafanya, unapaswa ukosee vitu vingi sana ila sio kukosea kupata watu sahihi wa kwenda nao safari moja kwenye maisha yako na hilo ndilo kosa linalo mtesa sana yule mzee, sijajua ni nani alimshauri kutafuta watu wa aina ile kufanya nao kazi kwa sasa wao ndio wanao mfanyisha kazi bila yeye kujua. Hana msaada wowote kwa sasa lazima atanitafuta kuniomba msamaha tu vinginevyo anaenda kufa kwa ujinga wake mwenyewe” Calvin aliongea huku akiwa anashuka kwenye gari, walikuwa wamekaribia kufika karibu kabisa na ilipokuwa hiyo ngome ya THE RED SQUARD ambayo jioni ya siku hiyo ilitoka kulipuliwa vibaya sana, hawakutaka kusogea na gari karibu sana walijua wazi lazima kutakuwa na wanajeshi ambao wameliweka chini ya ulinzi eneo hilo na hakuna mwananchi aliyekuwa anaruhusiwa kusogea karibu hapo.
*********************************
Maeneo ya Kigamboni karibu kabisa na fukwe moja ifahamikayo kama Mikadi beach majira ya saa nane kasoro za usiku unaonekana moto kwa mbali mbele ya huo moto wanaonekana wanaume wawili mmoja akiwa amekaa hana hata wasi wasi wowote mwingine alikuwa amelala hali yake ikionekana kutokuwa nzuri sana. Wanaume hao wawili alikuwa ni Baruan Mahafidhu pamoja na Thomas, Thomas hali yake haikuwa nzuri sana baada ya kupokea kipigo kizito sana kutoka kwa Baruan lakini pia ule mlipuko uliokuwa umetokea ndani ya ile meli waliyokuwepo ulikuwa ni mkali mno ulimletea madhara. Wakati wapo hapo Baruan alitabasamu huku akikumbuka tukio ambalo lilikuwa limetokea saa moja nyuma la mlipuko mkali sana, baada ya kuruka kwenye maji mwanaume huyu alikuwa na pumzi kali sana ambayo alijifua vyema akiwa nchini Cuba kwenye kumalizia mafunzo yake ya ukomando, alikuwa na uwezo wa kukaa kwa kubana pumzi kwa dakika arobaini baada ya hapo ndipo angeanza kupata taabu ya upumuaji. Wakati anajirusha zile sekunde thalathini na tano zinavyofika na meli ikalipuka alikuwa amefika mbali kidogo kwa kasi aliyokuwa nayo kwenye uogeleaji akiwa na Thomas mgongoni hivyo wakati mlipuko huo unatokea hapo uliwasaidia kufika ufukweni haraka kulingana na mawimbi makubwa yaliyokuwa yanatokea japokuwa mlipuko huo uliwaletea madhara kiasi hasa kwenye suala la upumuaji sana sana kwa kijana Thomas ambaye kwake ilikuwa ni ngumu sana kuweza kuibana pumzi kwa muda mrefu sana ila walifanikiwa kufika salama. Baruan aliamua kukoka moto hilo eneo kama kupunguza baridi kali la usiku kwenye maeneo hayo ya bahari ambapo usiku kunakuwa na upepo mkali mno wa bahari ambao husababisha baridi kuwa kubwa.
Akiwa amekaa hapo anamsubiria Thomas aamke ili aweze kuongea nae kinaga ubaga aweze kumjibu maswali yake alihisi kama kuna mtu amepita ghafla hilo eneo ikamlazimu kusikiliza kwa umakini mkubwa sana, mara ya pili alisikia kama kuna nyayo za watu mara ya kwanza alihisi atakuwa ni mmoja lakini baadae anakuja kugundua ni nyayo za zaidi ya watu wawili alicheka kwa sauti kubwa sana Baruan ikiwa haifahamiki kama ni uoga au kuwacheka hao watu waliokuwa wamefika kwenye hiyo sehemu majira hayo ya usiku wa manane. Mbele yake walisimama wanaume nane walio shiba mno lakini hata hivi hakuwa na wasi wasi kabisa alikuwa bado amekaa pale pale chini akiendelea kuota moto wake.
“maisha yanaenda kwa kasi kubwa sana yaani hadi mimi pia leo nawindwa hahahahahaahha aisee kweli wanadamu inatupasa mara moja moja tumkumbuke sana MUNGU wetu huenda ni kweli tuna maisha mafupi mno tofauti na nilivyokuwa nafikria mimi” alikuwa anayatamka haya maneno akiwa na furaha kubwa sana tofauti na watu waliokuja hapo walivyokuwa wanafikiria walijua huenda angeogopa sana kuwaona hiyo sehemu, aliendelea kuchochea vikuni vichache vilivyokuwa kwenye hilo eneo huku Thomas akiwa amelala usingizi mzito mno na hali yake mbaya kwa misuko suko aliyokuwa ameipitia siku hiyo asielewe nini kinatokea kwa muda huo hiyo sehemu.
“kwahiyo umeona unaogopa kukaa mjini ukaona uje ujifiche sehemu kama hii mwanaume wa shoka kama wewe ukidhani hatutakupata? Sikuwahi kufikiria kama nawewe inafika sehemu ni muoga sana kiasi hiki” huyu aliyekuwa anaongea hapo mbele alikuwa ni mtu ambaye anajuana vizuri sana na Baruan waliishi wote kwa zaidi ya miaka miwili ndani ya kambi ya kikomando ya Morogoro ambako Baruan alipata mafunzo yake chini ya Kasisi Chacha, mtu huyu aliyekuwa anafahamika kwa jina la Derick Ndago alikuwa ameiweka mikono yake nyuma akiwa anaangaza huku na huku akionekana kusikitika sana komando kama Baruan kuwa eneo kama hilo kulingana na maisha yake aliyokuwa akiyaishi.
“mmmmmmhhhh unazeeka vibaya sana Derick ungali bado mdogo sana, ni miaka mingi kidogo imepita tangu tuonane na sikutarajia kukuona tena leo kwenye sehemu kama hii ila huenda ni vyema tumeonana ili tupate kutakiana safari njema ya maisha mapya ambayo mmoja wetu anaenda kuyaanza(kifo) muda sio mrefu japo unayo nafasi ya kuyazuia hayo. Baada ya kugundua kwamba natumikishwa kufanya mambo ya hovyo sana kuna muda inaniuma sana kuwa mtu mkatili kupitiliza japo sikujaaliwa kuwa hivi ni walimwengu walinifanya niwe hivi ila nakusihi tu kuna mambo mengi sana ambayo huyajui kuhusu mimi hivyo kaa mbali na haya mambo kabisa kwa hiki ulicho kifanya leo nitakusamehe na kuhesabia kwamba ni bahati mbaya tu imetokea” Baruan alikuwa bado amekaa chini hata presha hana licha ya kuona wanaume waliokuwa hapo walikuwa siriasi sana mikono yao ikiwa na mapanga mazito yaliyokuwa yana waka waka licha kigiza totoro kilichokuwa kimetanda hayo maeneo kikipunguzwa kidogo na mwanga wa moto aliokuwa ameukoleza hapo pamoja na bastolola za kutosha viunoni.
Delick tumwambie ukweli kuhusu huyu kiumbe au tumuache aokolee moto kiganjani?....Calvin na Baruan wanakutana kinatokea nini Kati yao????
Naitupa kalamu yangu muda unanidai 68 naweka nukta tukutane wakati ujao
Chao[emoji2768]
Bux the story teller
#ULIMWENGUWAWATUWABAYA
Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Respect sana kwako, loading........Aisee popcorn zilizoisha ni nyingi sana
Nadhani uliisubiri kwa hamu sana ndio maana imekuwa fupi70 umeifanya fupi sana