FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
- #221
Shukrani sana mkuu asante kwa kupitia uzi huuKati ya stori zinazovutia watu wengi. Kongole mkuuu
Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shukrani sana mkuu asante kwa kupitia uzi huuKati ya stori zinazovutia watu wengi. Kongole mkuuu
Wewe ni tomasosafi Sana. wameumizana tu bila kuuana.
sikutaka wauane kabisa.
kuanzia leo Mimi ni Baruan.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa shilingi 500 tu njoo umalizie kurasa za moto sana tano za mwisho[emoji3578]
chief Mimi niliacha kuweka Hela kwemye simu.Kwa shilingi 500 tu njoo umalizie kurasa za moto sana tano za mwisho[emoji3578]
Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Sawa sawa japo sio lazima iwe kwenye cm ndo itumwe[emoji2768]
Duuh hatari kitu kinazidi kunogaHADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA 71
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA................
Sekunde mbili tu Calvin alikuwa amepotea hapo, wote walisimama kwanza kwa wasiwasi wasiamini kinachotokea kwamba inawezekanaje mtu huyo kupotea hiyo sehemu hata Baruan alishtuka hakuwahi kuuona uwezo wa huyo bwana mdogo hivyo kupotea hapo kichwani taa nyekundu iliwaka kwamba aliepo hapo sio mwanadamu wa kawaida kama alivyokuwa anamchukulia yeye.
ENDELEA..................................
Zilipita sekunde ishirini tu pekee alionekana Calvin akiwa amesimama upande wa pili, wanaume wanne Kati ya hao nane waliokuwa wamesimama hapo ukiachana na yule aliyekuwa akiugulia maumivu kwa kupigwa na Baruan walikuwa hawana shingo zao, Calvin alikuwa ameushika upanga wake vizuri mkononi ukiwa umetapakaa damu kwenye makali yake wala hakuujali sana wale wanne kwa walicho kiona hapo walianza kukimbia kwa spidi kuelekea getini alikokuwa Luciana, hawakujua kama huyo mwanamke mbele yao ni komando. Zilirushwa star mbili kwa nguvu upande wa nyuma na kuzama kwenye vichwa vya wanaume wawili, wawili walikuwa wamelikaribia geti la kutokea kilifanyika kitendo cha kutisha sana, Luciana alijibetua kwa sarakasi moja kali ya nyuma akiwa hewani alichomoa bastola mbili kiunoni mwake na kuwatandika nazo zaidi ya risasi kumi wanaume hao waliokuwa wanakuja upande wake, aliwaua vibaya sana kwa kutoboa toboa vichwa vyao, aliyekuwa yupo chini Baruan aliivunja shingo yake kwa nguvu kwa kuutumia mguu wake hapo ilikuwa ni vita ya wanaume hakutakiwa mtu mlaini kuwa maeneo hayo. Tomaso alikuwa akitetemeka sana asijue ni kipi cha kukifanya alitaka kukimbia Calvin alimkonyeza Luciana ambaye alijirusha hewani na kufyatua risasi mbili zilizo mpata Tomaso vyema kwenye mguu wake hakuwa na sehemu ya kukimbilia tena alipaswa amsubirie Calvin amalizane naye kwa usahihi kabisa.
"Unaweza ukanipa sababu ya msingi ni kwanini mnayatenda haya kwa watu wanyonge wasiokuwa na hatia yoyote?, mzee wangu Jackson Aron na mkewe Alice Jackson waliwakosea nini mpaka muweze kuwafanyia ukatili wa namna ile? shida ilikuwa ni pesa tu au kulikuwa na mengine nyuma yake?...niambie haraka" sauti nzito na kali kutoka kwa Calvin aliitamka mbele ya Baruan akihitaji majibu na sababu ya msingi mpaka wawauwe wazazi wake ambao walikuwa kila kitu kwake, wakati huo alikuwa amesogea sana mahali alipokuwa Baruan akiliweka panga lake mgongoni. Baruan alizikunja ngumi zake kwa usahihi lakini Calvin aliskitika tu akitikisa kichwa . Tomaso alikuwa akipiga makelele alipigwa teke moja la mbavu na Luciana akimsihi aache makelele yake kwa sababu ameyataka yeye mwenyewe ikambidi asikilizie maumivu hayo chini chini, sababu ya Luciana kumpiga Tomaso teke hilo zito alikuwa anahitaji kuushuhudia mpambano huo wa hao wanaume wa shoka kwa utulivu mkubwa hakutaka usumbufu ni watu ambao sifa zao zilikuwa zinatisha sana hasa pale unapopata bahati ya kukutana nao.
"Tumeumbwa kwenye dunia moja tena na MUNGU mmoja ila wanadamu sisi ni tofauti kabisa na ndio maana hata imani ya misingi ya dini ni tofauti kabisa, nimezaliwa nikiwa mwanadamu mwema sana ila ulimwengu ulinifanya nikawa mtu wa kutisha sana, nimewaua watu wengi mno kwa sababu ya maisha ambayo kuna baadhi ya vijana huwa wanayaota kuyaishi. Hii dunia kuna vitu viwili ni mhimu sana kwenye kuishi kwako chakwanza ni labda uwe na pesa sana ndipo utakapo yaishi maisha vizuri na kwa amani au uwe maarufu sana na pesa zitakufuata zenyewe. Ni hatari kubwa sana unapotaka kushindana na mtu ambaye ana hivyo vitu vyote kwa sababu anakuwa na nguvu kubwa sana, mimi ningekuwa wewe ningechagua kuhama nchi nikayaishi maisha yangu mbali sana na nchi hii kuliko kutafutana na watu ambao nchi wanaiendesha watakavyo wao. Angalia saivi kila sehemu unatafutwa kuliko hata maskini wanavyo itafuta pesa ya Kodi ya nyumba unadhani utakimbilia wapi? ni kweli mimi ndiye niliyewaleta wale vijana kutoka Afghanistan na niliwafuata mimi mwenyewe Ahmed Abdulrazack na kaka yake Abdul Abdulrazack Kwa lengo la kuwadhoofisha wanasiasa wenye nguvu kubwa ili waziri mkuu apewe nchi, na ndio tukio lililompeleka bwana mdogo Ahmed gerezani baada ya kulipua kanisa kule Kawe na kuua watu miatano. Kufa kwa baba yako haikuwa kwenye mpango yeye alitakiwa kufilisiwa tu basi aachwe hai lakini kutokana na ukaidi wake ndio sababu ikampelekea kuuliwa" Baruan alijibu huku akiwa anamzunguka Calvin, mwanaume alikuwa ameyafumba macho akiisikilizia hadithi hiyo fupi kwa machungu makubwa.
"una familia?" ndilo swali pekee ambalo Calvin alimuuliza Baruan.
"Mimi ninaweza kukusaidia bwana mdogo kwa sababu hawa watu wamenisaliti tayari sipo upande wao" Baruan aliongeza kwa kujiamini akijua mambo ni mepesi sana.
"Nijibu nilicho kuuliza" aliongea kwa ukali Calvin.
"hahahahahhah bwana mdogo mimi sio mtu wa kunitisha tisha kirahisi sana namna hiyo. Huwa sijali kuhusu kuishi kwangu hakuna mtu anaye nitegemea mimi hivyo hata nikifa sina ninacho daiwa hapa duniani zaidi ya madhambi makubwa mengi ambayo ninayo ya kunyanyasa viumbe vya MUNGU visivyo na hatia yoyote ile". Alijibu kiunyonge kidogo Baruan na kushusha machozi baada ya kutajiwa neno familia kichwani mwake ilikuwa inakuja picha ya Eunice wake.
"Sawa, ni vyema kama wapo useme mapema nahitaji unipe majina yao nikitoka hapa nikaangalie namna ya kuwasaidia kwa sababu hautaipata hiyo nafasi ya kuwaona tena kutoka sasa una dakika chache sana za kuwa hai" maneno yalikatishwa na sarakasi moja kali mno iliyokuwa imelenga kichwa cha Baruan aliiona vyema aliruka akaikwepa na kurusha ngumi yake nzito kama jiwe ilimpata vizuri Calvin kwenye paji la uso alijizungusha akatua nyuma kidogo, ngumi hiyo ilimuingia vizuri sana alikubali kwamba huyo ni mwanaume wa shoka, walianza kurushiana ngumi kali na mateke ya kutisha yaliyo fanya ziwe zinasikika sauti za mifupa tu, Baruan alikuwa mwanaume haswa Calvin alijirusha kizembe alipokea ngumi sita mfululizo zilizo mfanya atoke damu puani na mdomoni, ilimlazimu kurudi nyuma kama hatua tano akasimama vyema. Calvin alitaka kwenda kwa kasi alishangaa Baruan amemfikia baada ya kujiviringisha na sarakasi za ajabu zilizo mfanya kujizungusha mara mbili hewani kisha alitua na teke moja la kutisha kwenye kifua cha Calvin ambalo lilimnyanyua na kumrudisha Calvin hatua sita nyuma, ilikuwa adondokee kichwa ni haraka sana alijigeuza na kutua chini akiwa ameshikilia upanga wake alio uchomoa akiwa hewani, hakuna kilicho gusa ardhi isipokuwa upanga tu pekee mwili ulikuwa umebebwa na upanga wake, ilikuwa ni kama movie la kutisha sana Luciana na Baruan hata Tomaso hakuna aliye amini mwili wa mtu mzima kutua chini kwa kutumia upanga.
Calvin aliinua uso wake na kumtazama Baruan akiwa anatabasamu sana alijigeuza na kusimama vizuri.
"Nimeipenda sana aina yako ya upiganaji sijawahi kupigwa na mwanaume mmoja namna hii tena mtu kufanikiwa kumaliza dakika tano namimi una bahati sana nadhani tungepata watu kama wewe kumi wakalitumikia taifa kwa usahihi hii nchi ingekuwa mbali sana tatizo nyie ndio mnao kuja kuiharibu nchi tena hivyo siwezi kukuacha itakulazimu uende na kipaji chako au unipe sababu ya msingi ya kuyafanya haya, una dakika tatu pekee za kuyatetea maisha yako" Calvin aliongeza haya maneno baada ya Baruan kumaliza naye dakika tano tena Baruan akiwa anaongoza kwa point nyingi mno, Calvin alipiga kelele kubwa mwili wake ukianza kuvimba na alama za mishipa zikianza kujichora, aliugusa mfuko wake wa suruali kwa nguvu ilijirusha juu shilingi, ukiiona hii shilingi ujue ni hatari nzito sana ipo mbele yako, ni dakika tatu pekee zilikuwa zinahitajika Baruan kuyaokoa maisha yake, Calvin aliyainua macho yake kutazama upande wa juu ilipokuwa imerushwa shilingi hiyo alikuwa anaiangalia kwa hasira wakati inashuka chini, kabla haijagusa ardhi alikanyaga mguu mmoja chini kwa nguvu akijiandaa kuruka kwa spidi wakati huo upanga ulikuwa unazungushwa kwa spidi ya ajabu. Wakati shilingi inatua chini upanga ulikuwa umerushwa kwa kasi kali sana kuelekea alipokuwa Baruan huku nyuma Calvin akiwa anakuja kwa kasi sana kuufuata upanga wake huo. Baruan aliukwepa huo upanga ambao ulikuwa unakuja kama unazunguka kwa kuupiga teke ila hata sekunde mbili hakumaliza alikutanishwa na ngumi kali alihisi hiyo ni nyundo imempata kifuani kwake, alirushwa mbali Calvin alijizungusha juu kwa juu na kuudaka upanga wake kisha kwa spidi kabla Baruan hajatua chini aliongezwa na teke zito la kiuno na ngumi moja nzito ya kichwa iliyo mfanya kudondoka chini na kujibamiza vibaya. Calvin alikuja taratibu pale alipodondokea Baruan, mwanaume alinyanyuka Kwa nguvu akijaribu kurusha mikono yake ili kujitetea kwa huyo mtu aliye onekana wazi alikuwa hapo kwa sababu ya kuuchukua uhai wake.
Ngumi nne zilimpata Calvin ajabu alikuwa amesimama tu hakusogea popote pale, Baruan alijikusanya kwa nguvu zote ili apige ngumi nzito wakati anairusha ngumi hiyo alishangaa mkono wake ni mwepesi sana, alivyo uangalia kiganja cha mkono wake kilikuwa kipo chini upanga ulipitishwa kwa nguvu na Kasi ya ajabu mno iliyo kuwa inatisha, mwanaume huyo aling'ata meno yake kwa maumivu makali ila alijikaza kwa kuiviringisha miguu yake ili arushe mateke yake mazito, kabla hajalifikisha teke lake kwa Calvin Baruan alidondoka chini kwa kukosa balansi ya mguu mmoja ambao ulipigwa teke kali la kushtukiza na Calvin ambalo lilimvunja paja lake na mvunjiko wa mfupa ulisikika kwa nguvu na kuwafanya Tomaso na Luciana wafumbe macho pale pembeni ambapo Luciana alikuwa amemuweka chini ya ulinzi Tomaso. Baruan alikuwa ni mwanaume wa shoka hasa lakini asingeweza kuyavumilia haya maumivu alihisi mwili wote umekufa ganzi kwa sekunde kama kumi hivi kisha ilifuata sauti nzito ya kuguna kwa maumivu, kwa mara ya kwanza Leo alitoa machozi kwa kupigwa na mtu tena mwanaume mwenzake kwa kumbu kumbu zake anakumbuka aliwahi kuyatoa machozi kwa mwanamke wake Eunice tu ila leo yalikuwa yanamkuta mambo magumu sana kwenye maisha yake. Akiwa hapo chini Calvin alimpiga na teke lingine la tumbo kama anapiga mpira, teke hilo lilimfanya Baruan ajipigize ukutani na kumfanya kutoa kilio kizito usingeamini huyu ndiye aliyekuwa chuma anaye ogopwa na na kila mwanadamu aliyekuwa akikutana naye mbele yake, ilikuwa zamu yake kuyapata maumivu ambayo alikuwa akiwafanyia wenzake kwa miaka mingi sana. Mwanaume Calvin aliyafumba macho yake kisha akajirusha juu akiwa ameushika upanga wake kwa nguvu na kuruka nao kuelekea ilipokuwa shingo ya Baruan ili kumaliza kazi
"Naomba umlinde mke wangu tafadhali" sauti yenye maumivu kutoka kwenye kinywa cha Baruan ndiyo iliyofanya upanga huo upindishwe kidogo tu pembeni na kutoboa ukuta badala ya kichwa chake, neno mke lilimgusa sana Calvin alikumbuka vyema baba yake alivyokuwa anapenda kumsifia mkewe ambaye ndiye mama yake mzazi, alisita kumuua Baruan japokuwa ndizo zilizokuwa hesabu zake, hakutaka mwanaume huyo aendelee kuishi kwa yale aliyokuwa ameyafanya. Calvin aliangalia saa yake zilikuwa zimepita dakika mbili na sekunde thelathini na shilingi yake ilikuwa bado inaendelea kuzunguka, aliifuata shilingi hiyo akainama na kuichukua kisha akaanza kuandoka mahali hapo alipokuwa anapigana na Baruan akianza kuelekea alipokuwa Tomaso na Luciana.
"Maisha ya mwanadamu ni mafupi sana na ukilielewa hilo basi jua kwamba kwa namna moja au nyingine hautakiwi kuyafupisha tena maisha ya mwenzio na kuzidisha ufupi wake kuwa mkubwa, baada ya hapo huwa kinafuata kisasi ambacho ni kitu hatari sana kwenye maisha ya mwanadamu yeyote yule ambaye anakuwa anaishi kwa maumivu makali moyoni mwake na kila akikumbuka maumivu hayo huwa anajikuta ana roho mbaya sana na kuhitaji kulipa kwa wale walio mletea machungu hayo upande wake. Naelewa maumivu ya kupotelewa na watu unao wapenda sana kwenye maisha nakumbuka vyema kauli ya baba yangu aliwahi kuniambia kwamba mwanamke ni sehemu kubwa na ya mhimu zaidi Kwa mwanaume yeyote yule duniani, hakuna furaha pasipo mwanamke, mwanamke ni kiumbe pekee ambacho humfanya mwanaume aione thamani ya maisha yake na ndio maana unaona watoto wengi sana huwa wana mapenzi zaidi kwa mama zao kuliko hata baba zao. Neno mke ndilo limenifanya nikuache ukiwa hai siku ya leo najua maumivu atakayo kuwa nayo atakapo sikia kwamba umekufa na atanichukia sana bila kujua kwamba wewe ndiye uliye nifanya mimi nimekuwa katili sana namna hii, sitaki familia yako na watoto ije inichukie kwa kuwakatishia uwepo wa baba yao hapa duniani na kuwafanya kuwa watoto yatima kama mimi nilivyo hivi leo. Huna haja ya kuniambia nimlinde mkeo nenda kamlinde wewe mwenyewe" ni maneno mazito sana yenye ujumbe mkubwa ambayo Calvin aliyatamka mbele ya Baruan huku akiwa ana mrushia vichupa viwili vya dawa, hivi vingemfanya atoe maumivu yote mwilini na kumpatia nguvu za kutoka humo ndani, Baruan alilia sana kwani hayo maneno yalimchoma sana na kumfanya ajutie kukubali kutumika na watu kwa hasira zake kiasi kupelekea kuwafanya watu wengine waishi maisha ya shida sana na kusababisha idadi kubwa ya watoto yatima kwa kuwaondolea wazazi wake.
Calvin alikuwa anatembea taratibu kuelekea alipokuwa Tomaso hakuongea chochote kile zaidi ya kumbeba na kuingia naye ndani moja kwa moja, Luciana hakuwa na uwezo wa kuuliza kwa sababu mtu huyo alikuwa bado yupo kwenye hasira kali mno.
"Veronica yuko wapi" Calvin aliuliza huku macho yake yakiwa bado mekundu na mishipa imemtoka kwenye misuli yake pamoja na kwenye paji la uso.
"Yuuu...yuu....po hapa hapa ila..ila..." Tomaso alijibu huku akitetemeka sana kwa uoga.
"ila nini" Calvin aliuliza huku akiuchomoa upanga wake ulio mtisha sana Tomaso
"what??" Calvin aliuliza kwa nguvu akihofia kwamba huenda mwanamke huyo amefanyiwa kitu kibaya sana.
"ni..ni...ni mjamzito" Tomaso aliongea kwa kitetemeshi macho yake yakiwa kwenye upanga ambao alikuwa ameushika Calvin, Calvin alionekana kushtuka sana baada ya kusikia hicho kitu.
"Nani kampatia hiyo mimba" alifoka Calvin huku akiwa amemshika Tomaso kwa mkono mmoja kwa nguvu shingoni na kumnyanyua bila kujali kama bwana mdogo huyo alikuwa na risasi mbili kwenye mwili wake alizopigwa na Luciana na alikuwa akipata maumivu makali sana.
"ni..ni.yaaa....ya....yakwako" kauli ya Tomaso ilimmaliza nguvu Calvin hata upanga ulimdondoka chini na yeye mwenyewe nguvu zilimuishia akakaa kwenye sofa akiwa ameshika kichwa chake.
Unadhani nini kinaenda kutokea kwa Calvin? atampokea Veronica? na je atamueleza nini mwalimu wake Hinata Haruto Haru ambaye alimsisitiza sana kuizingatia furaha ya Jackline au Yeveda kwa zaidi ya asilimia miamoja? je Jackline ataelewa kuhusu hili? unataka kujua sababu kwanini Tomaso alimteka Veronica?........Ungana namimi ukurasa unao fuata ikiwa ndio tunaelekea kuitamatisha hadithi yetu 71 sina la ziada.
MUNGU akubariki sana
Chao[emoji2768]
Bux the story teller
#ULIMWENGUWAWATUWABAYA
Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Jero tu nakujaKwa shilingi 500 tu njoo umalizie kurasa za moto sana tano za mwisho[emoji3578]
Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
mpaka lini tenaHADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI : Bux the story teller
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA 73
SEHEMU ILIYOPITA TULIPO ISHIA................
“dada yako yupi na hukuwahi kuniambia, kauli yako ya mwisho uliniambia kwenye dunia hii haukuwahi kuwa na ndugu kwenye ukubwa wako wote ulio uishi zaidi ya rafiki tu na ndio sababu kubwa nikakufanya kuwa kama ndugu kwangu, nilikuwa tayari kukulinda kwa kila kitu na ndio sababu nilikuwamini mpaka nikakupatia Veronica uende naye Paris Ufaransa nikiahidi kuwafuata baadae, ni kipi unanificha mimi hutaki nikijue na huyo ni ndugu yupi unaye muita dada yako?” Calvin alimuuliza Tomaso kwa hasira sana akiwa amemshika kola za shati kwa nguvu akiuhitaji ukweli kutoka kwa huyo bwana mdogo. Tomaso alijifuta machozi yake yaliyo onekana kutoka kwa uchungu mkubwa sana ili amsimulie Calvin kipi kipo nyuma ya pazia mpaka yeye kufikia hatua ya kumteka Veronica kama wanavyodai wao lakini hilo hata Veronica alishtuka sijajua kama hakuwa na taarifa kwamba alikuwa mateka?
ENDELEA.........................
“sisi tulizaliwa wawili na sio peke yangu kama watu wote wanavyojua, tupo mapacha mimi na dada yangu ambaye ndiye mkubwa kwangu. Baada ya kuanza kufanya kazi na hawa watu nilikuwa nayajua madhara yake ndiyo sababu sikuwahi kumwambia mtu yeyote yule kwamba sisi tupo wawili kwa sababu niliogopa kumuingiza dada yangu matatizoni. Siku ile ambayo tulitakiwa kwenda Ufaransa wakati tumefika Buguruni nilipigiwa simu na namba ngeni, ni waliokuwa wanaonekana kunijua vizuri sana kwa sababu inaonekana ni muda mrefu mno waliweza kunifuatilia na kuweza kugundua uwepo wa dada yangu. Kwanza sikuweza kuamini kitu kama hicho kwa sababu ilikuwa ni siri nzito sana mpaka pale nilipokuja kuisikia sauti yake akihitaji msaada. Niliwaomba sana wasimfanye chochote kile waseme wanacho kihitaji kwangu, niliogopa sana kitu walichokuwa wameniambia, kwani walisema wanakuhitaji sana wewe pamoja na pesa zako zote.
Niliwaeleza kwamba ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa bora waseme kingine lakini hawakunisikiliza walisema kama nahitaji kumuokoa dada yangu basi ni lazima nihakikishe nakupata wewe, niliwaza sana kwamba hili suala linawezekana vipi kufanyika ndipo nilipopata akili ya kumtumia Veronica nilijua wazi hauwezi ukakubali akaingia kwenye matatizo wakati wewe upo. Nilicho kifanya niliwaeleza kwamba wewe ndiye uliyepiga simu na umehitaji tughairi kufanya safari, hawakuweza kunipinga kwa lolote kwa sababu walijua moja kwa moja ni wewe ndiye uliye sema, niliona mahali pa kuja kuifanyia hiyo kazi ni hapa kwangu na hii ni nyumba yangu ya muda mrefu sana ambapo ndipo alipokuwa akiishi dada yangu kabla hajachukuliwa na hawa watu. Kwa mara ya kwanza niliwaza sana kwamba atakuwa ni nani huyu maana Fabian Decco alishakufa sikupata jibu kamili kwa vile walikuwa wapo wengi sana wenye kukuhitaji. Niliwaomba wanipe muda ni kazi ngumu sana wamenipa waliniambia miezi mitatu isizidi kila kitu kiwe kimeisha.
Thomas nilimuita pembeni nikampatia milioni themanini na kumhitaji asirudi tena maisha yake yote kwa sababu alionekana kushtuka sana tangu siku ya kwanza kufika hapa ni baada ya kuwaona walinzi wengi ambao hata mimi mwenyewe sikuwa nawafahamu kabisa ila nilijua tu ni watu ambao ndio walikuwa wamemteka ndugu yangu na walikuwa hapa kuhakikisha natekeleza majukumu yao wakiwa wameizunguka hii nyumba alianza kuwa na wasi wasi sana na niliona angeniharibia kila kitu mwisho nimkose dada yangu hivyo nikamtoa mapema sana. Kuhusu Veronica mpaka leo hajui chochote kwani baada ya kufika naye hapa nilimdanganya kwamba huko nje anatafutwa kila sehemu na anatakiwa kujificha ndani ya hicho chumba ambacho nilikuwa nikimpatia kila kitu mpaka siku utakapokuja kumchukua mwenyewe. Nimehangaika sana kukupata kwenye simu yako kwa sababu kwenye mitandao yote ya siri namba yako ilikuwa haionekani mpaka jana ndipo ilionekana kuwa hewani na ndio muda ambao nilikupigia simu kukuelekeza kwamba uje kariakoo na bilioni 50 ili umsaidie Veronica kwa vile nilijua huwezi ukagoma kuja kwahiyo wanaume hao uliowaua nje ndio waliotakiwa kuja kukuchukua kule na kukupeleka kwa kiongozi wao. Inawezekana hautanisamehe lakini naomba umsaidie dada yangu sina mtu mwingine wa kunifanyia hivi ndio sababu nilikuwa tayari hata kufanya kitu chochote kile kwa ajili yake, hawa watu ni wabaya sana mitandao yao ni hatari mno huwa wanawateka mabinti wanaenda kuwauza kwenye makasino nje ya nchi wanawatelekeza huko kwa kuwaathiri na madawa ya kulevya inapelekea wanakuwa hawana uwezo wa kukimbia kwa vile wanakuwa na uhitaji sana na madawa, kama ukichelewa sana wanaweza kumuua muda wowote ule au kumtorosha nchini kwani kila kinacho endelea hapa kwangu kule wanaona naomba tafadhali” simulizi fupi ya bwana mdogo ilimfanya Calvin atoe machozi na kunyanyuka pale alipokuwepo akamfuata na kumkumbatia Tomaso alikuwa ameonyesha ushujaa mkubwa sana kuweza kujitoa kwa namna yoyote ile ili tu ahakikishe ndugu yake anakuwa salama kutoka kwa hao watu, ni ndugu wachache sana kwenye hii dunia ambao wana roho nzuri ya namna hii, Calvin hakuweza kumchukia baada ya kuujua ukweli ila alimuona ni kijana shujaa sana ambaye hakuwa tayari kumsaliti ndugu yake wa damu. Wote waliokuwa humo ndani walitokwa na machozi mpaka kwa kiumbe hatari huyu Baruan alitiririkwa na machozi mengi sana ni siku moja tu tena ndani ya muda mfupi alipata masomo mawili kutoka kwa watu wawili tofauti, somo la kwanza lilikuwa ni maneno ya Calvin ambayo yalimfanya ajione yeye ni mnyama sana lakini aliachwa hai wakati kwa aliyo yafanya alistahili kufa, somo la pili alilipata kwa bwana mdogo Tomaso hapa baada ya kuonyesha ujasiri wa kumsaidia ndugu yake bila kujali chochote ndio sababu alikuwa tayari kumsaliti hata Calvin, neno familia na uzito wa damu alio uonyesha Tomaso ilimfanya Baruan ajisikie kama ni mtu mwenye hatia kubwa sana kwenye maisha yake kwa kusababisha vilio kwenye familia nyingi sana ndani na nje ya nchi alikuwa na uchungu mkubwa sana na mheshimiwa waziri mkuu pamoja na mkubwa wake wa kazi ambaye ndiye amemfundisha kila kitu kwenye maisha yake Kasisi Chacha.
“dada yako anarudi hapa muda sio mrefu ulipaswa kuniambia hili suala mapema sana” Calvin alimjibu Tomaso ambaye kwake alikuwa kama mdogo wake akiwa anang’ata meno yake kwa hasira akiwa anazitazama kamera hapo mbele yake kwa hasira kisha akatabasamu alitamka neno moja tu mbele ya hiyo kamera i’m coming(nakuja) akiwa na uhakika kwamba wahusika wanamuona vizuri kulingana na maelekezo ya Tomaso.
“hapana usiondoke tena naogopa kubaki peke yangu usiniache” Veronica alikuwa amemshikilia Calvin akiwa hataki aondoke tena hapo kwa sababu alijua wazi kama akiondoka inaweza kumchukua muda mrefu sana kuweza kurudi au huenda asirudi tena watu aliokuwa anaenda kuwafuata walikuwa wanatisha mno kwa mambo waliyokuwa wanayafanya halafu ubaya walikuwa ndio wakubwa wa nchi ilikuwa inamtisha mno mwanmke huyu, Calvin alimgusa mashavu yake akiwa mwingi wa tabasamu usoni alimkonyeza Luciana ambaye alipitisha kidole chake kwenye shingo ya Veronica akapoteza fahamu, ilifanyika hivyo ili kuokoa muda hawakutakiwa kukaa sana hiyo sehemu ilikuwa ni hatari pia walitakiwa kumuwahi mheshimiwa waziri mkuu. Baada ya Veronica kupoteza fahamu Calvin alitoa star ndogo mbili kiunoni, wote walishtuka wakidhani huenda kuna mtu anauliwa hapo maana kiumbe huyo alikuwa hatabiriki na alikuwa anazidi kuwa na uwezo wa ajabu sana kila siku ya MUNGU kunavyokucha, aliinamia sehemu aliyokuwa yupo Tomaso alimshika vizuri na kuzizamisha star hizo sehemu zilizokuwa na risasi na kuzitoa risasi hizo akiwa amezishika zote mbili mkononi. Hakuna ganzi iliyotumika hapo Tomaso alipiga makelele mpaka akazimia kwa maumivu makali, Calvin alitoa kichupa kidogo ambacho kilioonekana kuwa na unga unga ndani yake alivimiminia kwenye hivyo vidonda na ghafla vidonda vikaanza kukauka hapo hapo.
“hivi haya mambo umeyajulia wapi mbona kama unajua kila kitu?” Baruan aliuliza kutoka kule mlangoni alipokuwa ameugemea mlango wake mguu mmoja ukiwa hauwezi kabisa kufanya kazi yoyote ile, Calvin aliinua macho yake kwa usahihi akimwangakia jasusi huyo ambaye alikuwa ameiasi nchi yake.
“ni mambo machache sana ambayo siyajui kwa sababu tu mwanadamu hawezi kuwa na uelewa na kila kitu anaweza kukufuru ila muda sio mrefu sana unaenda kunijua kiundani pamoja na kwamba haya yote nimeyajuaje” alilijibu kiufupi swali la Baruan baada ya kuonekana kushangazwa na uwezo wa Calvin kuanzia kwenye mapigano, akili, matumizi makali sana ya mitandao hata uwezo wa kutibu watu akionekana kutumia dawa za ajabu ambazo hazikuwahi kuonekana ndani ya nchi ya Tanzania kabisa.
“huyu mtu anapatikana wapi”Calvin aliuliza akiwa anahitaji kujua kama waziri mkuu alikuwa anapatikana sehemu gani ndani ya nchi hii ya Tanzania.
“tutaenda wote nitakupeleka, huyu mimi ndiye ninaye mjua kwa usahihi sana, ana nyumba yake moja maeneo ya mbezi ambako ndiko alikokuwa anaishi kwa sasa(wakati huo Baruan alirushia mezani ramani ndogo ambayo ilikuwa inaonyesha namba ya nyumba hiyo iliyokuwa inapatikana maeneo ya Mbezi beach) lakini ana kambi yake ndogo maeneo ya kibiti, mambo yakimzidia ndio huwa anakimbilia kule kwa sababu kuna ulinzi mkali sana na ana watu wanne hatari mno wanao mlinda kule hivyo najua lazima atakimbilia kule tu inatupasa tumfuate huko” Baruan alijibu kwa ujasiri mkubwa, kutokana na hali yake Calvin alitaka kuongea neno lakini akaona huyo ni komando mkubwa sana asingeweza kukubali kuiachia vita njiani.
“sawa, Luciana utawalinda Tomaso na Veronica kama kuna tatizo lolote litatokea, halafu hakikisha nyumba ya huyo mzee huko mbezi unaiteketeza ila kabla ya kufanya hivyo hakikisha kama ndani kuna watu tusije kuua watu wasiokuwa na hatia yoyote ile, mimi naenda kibiti saivi nikirudi Kasisi Chacha hataweza kuiona asubuhi ya siku itakayokuwa inafuata” mwanaume alitamka hayo maneno kimsisitizo sana huku akiwa amekamilika kwa kila kitu, kiunoni alikuwa na star(nyota) za kutosha na siraha yake ambayo ndiyo ilikuwa mbaya zaidi namaanisha upanga wa kale ambao ni mali ya thamani sana ndani ya nchi ya Japan ulikuwa upo mgongoni kwake ukiwa umepachikwa kwa usahihi sana kwenye ala yake. Alikuwa anaelekea mlangoni ambapo ndipo alisimama Baruan Mahafidhu, kilifanyika kitendo cha ghafla sana ambacho kila mtu alishtuka. Calvin alirusha teke la nguvu kuelekea kwenye mguu ambao alikuwa amemvunja Baruan, jamaa alikuwa mwepesi sana kuukwepesha mguu huo ambao ulikuwa mbovu lakini hata hivi ulidakwa na Calvin kwa kasi ya ajabu aliuzungusha kwa nguvu kisha akaupiga ngumi kali ambayo ilimfanya Baruan agugumie kwa maumivu.
Hawakuamini tukio hilo kwa sababu kila mtu alijua Baruan alikuwa amesamehewa kwa moyo wote hata Baruan mwenyewe alishtuka sana lakini alishangaa wakati mguu huo unafika chini haukuwa na maumivu yoyote yale na uliweza kusimama wenyewe, Baruan alivyo mtazama Calvin mwanaume alikuwa akicheka tu na ndiyo siku ambayo wote walishuhudia meno thelathini na mawili ya kijana tajiri huyu tangu wamfahamu kwa sababu alikuwa anatabasamu kidogo tu muda mwingi huwa ameikunja sura yake, alikuwa ni kijana mwenye mvuto sana Calvin.
“hii imewezekanaje huu mguu si ulikuwa umevunjika?” Baruan alikuwa bado haamini akiwa anaupigiza mguu huo chini kuhakikisha kama upo salama kweli au ni ndoto zake za mchana, ilikuwa ni kweli kabisa mguu wake ulikuwa salama.
“aina ya hilo pigo hii dunia tunayo watu watatu tu ni mimi na walimu wangu wawili, hilo paja halikuvunjwa ila niliitenganisha mifupa kutoka kwenye goti mpaka kiunoni hivyo mifupa ndiyo iliyo pishana na sio kuvunjika, ni binadamu wachache sana wanaweza kulitambua hilo” Calvin aliongea huku akimpa mkono Baruan huku nyuma Luciana alirusha kikaratasi kidogo sana kilicho enda kunasa mgongoni mwa Calvin na hakuonyesha mshtuko wowote ule Luciana alitabasamu tu. Wanaume walienda kwenye gari ambayo wamekuja nayo Calvin na Luciana. Baruan alishangaa humo ndani kuna mwanamke ambaye hakumtambua kabisa akiwa amefungwa ila alikuwa ameyafumbua macho yake kwa usahihi akijaribu kujifungua Calvin hakuongea chochote kile alilitoa gari hayo maeneo kwa kasi kubwa mno akiwa anaianza safari ya Kibiti.
Asubuhi hiyo wakati Calvin anaelekea kwa Tomaso ndio muda ambao mheshimiwa waziri mkuu alikuwa amesimama mbele ya maiki akiwa live nchi nzima baada ya kusema kwamba ana mkutano mkubwa sana na waandishi wa habari.
“ndugu zangu watanzania ni furaha kubwa sana kwangu kuwa nanyi tena siku ya leo ikiwa tumepewa upendeleo wa pekee kuweza kuishi tena basi utukukufu uende kwake MUNGU, siku mbili zilizopita ni mimi ndiye niliyekuwa nimesimama mbele yenu kuelezea kesi ya kijana mmoja ambaye alituhumiwa kwa kesi ya mauaji ya kukusudia pamoja na kuwabaka wanawake na kuwaua afahamikae kama Calvin jackson. Ulifanyika uchunguzi wa kina sana na tumeendelea kufanya bila kulala mpaka leo asubuhi tumejirishisha kwa asilimia miamoja kwamba mtu huyu alikuwa hahusiki kabisa na haya matukio yote mawili(akiwa ameishikilia picha kubwa ya Calvin) ni kosa la kikazi lilifanyika kwa sababu alikuwa yupo karibu sana na maeneo ambayo tukio la ubakaji lilifanyika pamoja na mauaji hivyo ilikuwa ni lazima ahisiwe na kuchukuliwa hatua kali kwa kuyalaani sana haya mambo mabaya yanayo endelea hapa nchini hususani ya unyanyasaji wa kijinsia ila kwa bahati nzuri watuhumiwa husika wamekamatwa na wote wameweza kuuawa kwa kukatwa vichwa bila kupelekwa mahakamani ikiwa ni kama onyo na fundisho kubwa sana kwa yeyote anaye jihusisha na haya mambo maovu.
Sisi kama serikali tumeongea na kijana wetu ambaye ametuelewa kwa sababu naye anaungana pamoja na sisi katika kulilinda taifa lake husika tunapenda kumshukuru kwa moyo wake wa kukubali kushirikiana nasisi kwa muda wote ambao alikuwa ameshikiliwa na jeshi la polisi hivyo kuanzia sasa yupo huru na hakuna chombo cha usalama chochote kitakacho msumbua na popote pale wasikiapo taarifa hii waondoke mtaani haraka sana na wasiendelee kumsumbua raia yeyote yule, tunaombeni radhi kwa aina ya usumbufu ulio tokea yote ni kuhakikisha tunailinda amani ya pekee tuliyo barikiwa kwenye nchi hii MUNGU ibariki Tanzania” alikuwa anaonekana mtu safi sana Christopher Hamza akiwa mbele ya kamera lakini huo haukuwa uhalisia wake mtu huyo alitoa hotuba fupi ambayo ilionekana kuwagusa watu wengi sana kwa sababu ndiyo ilikuwa taarifa ya kwanza kabisa ya asubuhi hiyo.
Baada ya kutoka hapo alikuwa anatoka jasho sana wakati anarudi kwenye chumba chake televisheni ilikuwa imewaka alishangaa kuona taarifa nyingine baada ya aliyokuwa anaitangaza mwenyewe kuisha, ilikuwa ni meli lake la kifahari ambalo liliteketea lote kwa moto mkali, alishtuka mpaka alikaa chini hakuelewa imetokeaje mpaka meli hiyo ambayo amewekeza pesa nyingi sana iweze kutekete kirahisi sana namna hiyo, alihisi kama roho inamtoka aliichukua simu yake na kupiga namba mahali lakini haikupatikana kabisa alimuita mlinzi wake haraka akimuomba aandae msafara alikuwa anahitaji kuondoka hiyo sehemu haraka mno. Taarifa zilianza kusambaa chini chini lakini hatimae zikaanza kukua kila kwenye chombo cha habari zikiihusisha meli hiyo na uvamizi wa kigaidi ambapo ilionekana meli ilikuwa ya mheshimiwa waziri mkuu. Alitoka humo ndani haraka sana wakati anafika nje waandishi wa habari walikuwa bado hawajaondoka walihitaji kupata taarifa kutoka kwa mheshimiwa kulingana na taarifa ambazo zilikuwa zimesambazwa muda mfupi sana mitandaoni kuhusu meli hiyo kuwa yake na kuhusishwa na matukio ya kigaidi, hakujibu chochote walinzi wake walifanya kazi kubwa sana mpaka akafanikiwa kuingia kwenye gari lake, msafara wake ulitoka hapo kwa kasi sana yeye akionekana kuchanganyikiwa kabisa.
Ikiwa tunaelekea kutamatisha hadithi hii yenye kurasa 75 leo sina la ziada tena MUNGU akubariki.
Chao
Bux the story teller
#ULIMWENGUWAWATUWABAYA
Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
Kwa sasa itasomwa kila siku mpaka iishe, usiwe na hofumpaka lini tena
okay nitaqKwa sasa itasomwa kila siku mpaka iishe, usiwe na hofu
Sent from my TA-1053 using JamiiForums mobile app
[emoji41]HADITHI: ULIMWENGU WA WATU WABAYA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
MTUNZI: Bux the story teller
WHATSAP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA SABA
SEHEMU ILIYOPITA TULIPOSISHIA............
Tunarudi ndani ya Japan katika jiji la Osaka kwenye nyumba ya mzee Haruto, asubuhi na mapema sana calvin aliamshwa na Akio ili kuanza rasmi mazoezi yatakayo chukua takribani miaka miwili na zaidi, lengo ni kumuweka kijana sawa ili aweze kuikabili hatari kubwa sana iliyopo mbele yake, adhima kubwa ikiwa ni kulipa kisasi kwa wale wote ambao walikatisha maisha ya wazazi wake, aliapa kutomwacha hata mmja.
Akio alimchukua na kumpeleka kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa kikubwa sana ajabu kilikuwa kitupu yaani hakikuwa na kitu chochote ndani yake “here we go, iweke akili yako sawa na usahau kila kitu ulicho kiacha, hapa inahitajika akili yako kwa asilimia miamoja kila sekunde kwani unaenda kufundishwa vitu vikubwa sana ambavyo kisheria mtu kama wewe hutakiwi kabisa kuvijua na ni kosa kubwa sana ikijulikana, sijajua ni kitu gani baba yako alimpa master mpaka akakubali kukufundisha kirahisi namna hii, haijawahi kutokea kabla, nina imani utakuwa ni kijana mwenye bahati sana”. Ni maneno aliyo yazungumza Akio akiwa siriasi sana tofauti na mwanzo alivyokuwa anatabasamu tangu amekutana na Calvin, hali hii hata Calvin ilimtisha sana akajua huko mbele wanakoelekea hakuna masiara hata kidogo.
ENDELEA..................
“sawa nimekuelewa” alijibu kifupi Calvin.
“leo hautafanya zoezi lolote lile la kutumia nguvu ila nina ihitaji akili yako sana kama nilivyo kwambia mwanzo, leo ndio siku ya muhimu zaidi yawewe kukaa hapa kwani miaka yote miwili utakayo kuwa hapa itategemea kama utakielewa na kukizingatia hiki unacho enda kukiona na kujifunza leo, narudia tena kila neno ulielewe vema na ulihifadhi vema kwenye akili yako” yalikuwa maneno ya Akio, aliyaongeza kwa msisitizo sana huku amemkazia Calvin sura isiyokuwa na dalili yoyote ile ya mzaha.
ACHA COMMENT YAKO NA LIKE KURASA YANGU KISHA UNGANA NAMIMI MPKA MWISHO WA KIGONGO HIKI
“Mafunzo yako yatahusisha miaka miwili hapa, lakini ndani ya hiyo miaka miwili utafundishwa na watu watano tofauti, siwajui ni akina nani hao wengine zaidi ya master ambaye najua atakuwa wa mwisho kukufundisha ukishakomaa vya kutosha na usiniulize kwanini utafundishwa na watu wengi hivyo hata mimi sijui kwahiyo sitaki maswali, kama utakuwa na swali lolote la kumhusu master subiri mwaka uishe ndipo utakapo pata bahati ya kumwona tena utamuuliza” aliongea Akio
“haaaaaaaaaa unasema mwaka? Kivipi? Sijakuelewa, yani mtu nimetoka kukutana nae jana na anaishi hapa unasema nimuone mwaka?” alishangaa sana Calvin hivyo aliuliza maswali mengi sana kwa mkupuo.
“mhhhhhhh bwana mdogo kuna mambo mengi sana ambayo huyajui bado, **** una kumbu kumbu vizuri nimekwambia wewe una bahati sana, yule sio mtu wa kuoneka hovyo hovyo na ni binadamu wachache sana wanao mfahamu yule, hatufiki hata watano tunao mjua vizuri, yule ni urithi mkubwa wa hii dunia ambayo nchi nyingi kubwa duniani zinatamani zimpate ili ziutumie uwezo wake kwa maendeleo yao na nikuonye tu siku ukikutana nae chunga sana kinywa chako kwa sababu ukiongea vibaya hata neno moja tu kwake litakugharimu maisha yako yote, yule ni mtu hatari sana na hao wote unao waona wanafanya mazoezi ya hatari sana kule nje hakuna hata mmja ambae ashawahi kumwona wala kumjua, sitaki tena maswali” Akio alimalizia kumwelezea
“Au ndio sababu sikuelewa kilicho tokea kwenye gari, nikajikuta nimelala mpaka nakuja kushtuka tushafika, ina maana hii ni sehemu ya siri sana ambayo hatakiwi mtu yeyote kuweza kuifahamu. Calvin alitabasamu baada ya kulielewa hilo, akajua basi yupo sehemu salama sana japo pia ni ya hatari sana”
Akio aligusa ukutani likaja box la kioo lililo hitaji nywila{password} ili liweze kufunguka, kuna namba aliziingiza mara gafla pale katikati ya kile chumba kitupu ulitokea mlango mkubwa sana wenye kioo kigumu sana, Akio aliuendea akaweka mkono wake wa kushoto kama fingerprint kisha kuna maneno akayatamka kwa lugha ya kigiriki ambayo ilikuwa ngeni kabisa kwa Calvin aliyekuwa kwenye mshangao mkubwa sana kwa kile alicho kiona mbele yake na hakuelewa chochote hata ile lugha pia. Baada ya mlango kufunguka mbele yao zilitokea screen kubwa sana ambazo ziliwaka baada ya Akio kuongea maneno yake.
Mbele ya zile screen zote tano liliandikwa neno ESPIONAGE kwa lugha ya Kiswahili likiwa na maana ya UJASUSI Calvin alikuwa msomi kwahiyo haikumpa shida kuelewa,
“hili ndilo somo letu la leo, kabla hujaanza chochote kwanza unatakiwa uelewe ujasusi ni nini?”.
“Espionage au ujasusi asili yake ni ufaransa ambapo neno hili limetoka kwenye neno lifahamikalo kama espionner likimaanisha kupeleleza na mpelelezi alikuwa akiitwa espion. Ujasusi ni upelelezi ambao unahusisha upatikanaji wa taarifa za siri sana na za ndani sana kutoka kwenye vyanzo visivyo patikana kirahisi au ambavyo havina taarifa za moja kwa moja za wazi, lakini ukusanyaji wa hizo taarifa unakuwa hauna ruhusa yoyote ile kuweza kuufanya kutoka kwa mmiliki wa hizo taarifa. Kiufupi ni njia isiyo ya uhalali ya ukusanywaji wa taarifa za ndani na za siri, yaweza kuwa ni ndani ya nchi au nje ya nchi. Taarifa hizo zinalenga kuleta faida chanya zinazo onekana kwa maslahi mapana ya taifa, na mtu anae husika na hiyo kazi ya kijasusi anaitwa jasusi au Espionage agent. Hawa ni watu ambao huwa ni wa siri sana kutoka kwenye nyanja au taasisi nyeti sana hapa namaanisha idara za usalama wa taifa.
*************************************
Hawa ni watu wa siri zaidi ndani ya nchi na ndio wanao hakikisha nchi inakuwa salama kwa gharama yoyote ile ikiwabidi hata kukatisha maisha yao na ndio maana nchi nyingi sana zinatumia pesa nyingi kuweza kuwatengeneza hawa watu kwani ndio watu muhimu zaidi kwenye nchi ukimtoa Raisi wa nchi husika, mara nyingi hawa watu huwa wanatambulika tu kwa viongozi wao ambao ni wakurugenzi wa usalama wa taifa na wanaishi kwa code maalumu na sio majina yao, ni mara chache sana huwa wanajulikana kwa watu wengine au viongozi wengine ndani ya nchi labda ikitokea kuna dharura ya mhimu sana.
Hii huwa inahusisha sana mambo ya kijeshi au kisiasa ndiko sana ambako ujasusi umewekezwa sana kwa maana ndizo sehemu za muhimu zaidi kwenye nchi yeyote ile hapa duniani, ni kazi za hatari sana kwa sababu unampeleleza mtu au nchi bila ruhusa yake, kwahiyo ikitokea umekamatwa jua utateswa sana na utatakiwa utoe siri zote kitu ambacho umeapa kukilinda kwa maisha yako yote, ni bora ufe wewe mmja lakini sio kutoa taarifa za kuhatarisha taarifa za kuleta maafa na majonzi kwa maelfu ya watu.
Hivyo sheria ya kwanza ya ujasusi ni siri hata iwe nini awe nani ambae anatakiwa afe unatakiwa umuache afe lakini sio kutoa siri ya nchi ila kichwani mwako unapaswa uelewe kwamba ukikamatwa na kwa sasa nchi nyingi sana zinapiga vita sana hiki kitu kwa sababu kinahatarisha usalama wan nchi kwahyo adhabu yake ni mateso yasiyo vumilika, kufungwa jela au kuuawa. Haya ya leo yatunze sana kichwani mwako na usisahau hata kimoja kwa sababu ndiyo maisha ambayo unaenda kuyaishi mpaka unakufa” yalikuwa ni maelezo marefu sana kutoka kwa Akio akiwa anamfundisha bwanamdogo Calvin maana halisi ya ujasusi na mambo yaliyomo ndani yake.
“Daaaaah", aliongea baada kuhema kwa nguvu sana, aliogopa na kutetemeka huku anajifuta jasho kwa nguvu ingali mle ndani mlikuwa na kiyoyozi kikali, Calvin huku akijiwazia alijisemea “ina maana haya mambo ni magumu sana kiasi hiki, kumbe nchi zina mambo makubwa ya hatari kuhakikisha taifa linakuwa salama yaani ni bora hata uhai wa mtu utoke ili nchi iwe salama, hii ni hatari sana, hii ilimtisha mno”.
Hii hali Akio aliweza kuiona akaamua kutabasamu kwa mbali na kumwambia
“ kwa leo tumeishia hapa, kajiandae kesho rasmi ndo unaanza kuyafanyia kazi yale niliyotoka kukuelezea hapa nafikiri utakuwa umenisikiliza kwa makini sana na bila shaka umenielewa pia sana waweza kwenda” Alimaliza akio, jasusi huyu ambae amepewa amsimamie Calvin kwa miezi takribani nane kabla hajaja mtu mwingine kumfundisha mpaka watimie watu watano kwa takribani miaka miwili na zaidi ndipo atakapo ruhusiwa kuondoka.
Calvin aliondoka akiwa na mawazo sana kwa maana aliambiwa mambo ambayo kwake yalikuwa magumu na sasa akaelewa kwanii mzee Hiruto alimwambia hawezi kumruhusu mapema kwani anajua hatari iliyopo mbele yake, hiyo ikamuongezea nguvu ya kuweza kufanya mazoezi kwa nguvu zake zote na akili zake zote ili aweze kuwakabili watu walio leta maafa na majonzi kwenye familia yake.
Kijana Calvin rasmi sasa alianza kupata mafunzo ya hatari sana ya mapigano kwa ajili ya kuuimarisha vema mwili wake kuanzia kwenye mifupa mpaka utimamu wa akili. Alijifunza kwa spidi kali sana mpaka ilipo timia miezi mitano mbele, siku moja usiku Akio alimwita sehemu yenye uwazi kidogo ili waweze kuongea, Calvin alivyofika pale taa zote zilizimika ghafla, hii ilimtisha sana lakini mbele yake alimuona Akio akiwa amevaa nguo nyeusi za kininja na alimpa ishara amfate, lilikuwa ni giza kubwa sana hakuelewa wanapita wapi ila alikuja kushangaa wakiwa nje kabisa pembezoni mwa mto mmja mkubwa kukiwa kuna baadhi ya miti miti mirefu sana.
“Yamato ndilo jina la mto huu, ni mto wenye historia kubwa sana ndani ya nchi hii kutokana na kwamba ni jina la mlolongo wa sheria za urithishwaji wa madaraka katika nyumba za kiutawala za kifalme ndani ya Japan, ni mto wenye urefu wa takribani kilomita za mraba sitini na nane.
Nina historia kubwa sana na huu mto pamoja na huyo mzee Haruto, huu ndio mto ulio nifanya mimi nikakutana nae na nina sababu ya msingi ya kukuleta hapa, kwanza nataka unifahamu mimi ni nani kisha tutafanya hicho cha pili kilicho nifanya nikulete huku, je Akio ni nani? nini kilimkuta? ilikuaje? Na kwanini iwe ni kwenye huu mto?
UNGANA NAMI MPAKA MWISHO WA KIGONGO HIKI
Miaka kadhaa nyuma kama kumi na mitano iliyopita nilikuwa kijana mwenye umri wa miaka kumi na mitano, nimezaliwa katika miongoni mwa majimbo maarufu sana nchini marekani lijulikanalo kwa jina la Minessota.
Kwa bahati mbaya sana sikubahatika kuishi na baba yangu ambae kwake kamali ndiyo ilikuwa kila kitu, hakuwa na neno familia kwenye kichwa chake na kwa taarifa nilizo pewaga ni kwamba alishawahi kumiliki mali nyingi sana lakini kamali ikamfanya kuwa hohe hahe na bado aliendelea kuishi kwenye ndoa yake ya kamali, aliondoka nikiwa na miaka sita pekee na mpaka leo sijui kama yupo hai au alishakufa.
Nimeishi maisha yangu yote na mama yangu mzazi pekee, alikuwa anafanya shughuli za hatari na aibu sana ili mradi tu aweze kunisomesha, nilikuwa namheshimu sana yule mwanamke kuliko kitu chochote kile, basi siku moja aliniaga majira ya jioni kwamba anatoka mara moja na asingechelewa kurudi, lakini haikuwa kama vile alivyo niahidi ilipita siku nzima bila kurejea nyumbani mpaka kesho yake ambapo alikutwa akiwa amefanyiwa kitendo cha kinyama sana na kuuawa pembezoni mwa club moja pale jimboni, nililia sana kwa sababu yeye pekeake ndiye familia niliyokuwa nimebakiwa nayo na nilimpenda mno kiasi kwamba siwezi kuelezea. kwahiyo mpaka hapo nikawa sina familia tena na ilinibidi niishi kwa nguvu na akili zangu mimi mwenyewe kwenye hii dunia iliyo jaa dhuluma, hapo ndipo nilipokuja kubadilika hadi roho yangu na kuwa mtu nisiye na huruma hata kidogo kwa hawa wanao wanyanyasa watu bila hatia yoyote eti kwa sababu tu wao wana pesa na nguvu, tokea hapo nilikuja kuwa mtu mkatili sana.
Nini kilitokea kwenye maisha ya Akio? kutoka Marekani alikuja kuhusiana vipi na mto Yamato uliopo Japan?............... ukurasa wa Saba unafika tamati, tukutane katika kurasa zijazo. Hii ni ULIMWENGU WA WATU WABAYA na mimi ni Bux the story teller.... Chao[emoji996]View attachment 2264040