CK Allan
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 2,781
- 6,139
Karibu kwenye mzigo huu mpya kabisa,
By CK Allan
0746 266 267
Viumbe hatari... Dangerous creatures
1
Mwaka 2030
Sauti ya televisheni ilisikika,
nilikodoa macho kwa utulivu mkubwa nikiwa nimekunja miguu kama ilivyokuwa kawaida yangu, nilibonyeza bonyeza remote yangu ya kisimbuzi na nikavutiwa na The blessed Tv ...
"Hatuwezi kumuweka CK Allan kama mtunzi wa hadithi sawa na Mzee umughaka, deepond, au analyse.. haiwezekan.. huku ni kukosea heshima uandishi"
"Hapana, wote ni waandishi sema, CK Allan hawezi kabisa kuandika kuhusu hadithi za mapenzi mwanzo mwisho...hawezi"
"Sio kwamba hawezi hataki kabisa, na mwenyewe alishasema hataki kuandika kabisa kuhusu wanawake au mapenzi " "Hahaha lini alisema hivyo? Lini?" "Ndio hebu nitajie hadithi yake yoyote ya mapenzi mwanzo mwisho!"
"Angalia Ile ya Kesi."
Nilibonyeza remote ya TV haraka na kubadilisha chaneli nyingine. Tayari nilishaanza kuchoshwa na maneno ya wale waliojiita wachambuzi ambao hakuna walichoshindwa kuchambua.
Pamoja na kuandika hadithi nyingi bado isingekuwa vyema kuanza kulinganishwa na wakongwe wengine ambao kwa namna moja au nyingine Kila mmoja alikua na mkono wake katika fasihi. Kwa hivi, niliamua kubaki na aina moja ya uandishi wa kusimulia matukio ambayo kwangu Mimi nisingeweza kuyaita hadithi.
Basi niliamua kukaa kimya kuandika mpaka miezi michache Hapo nyuma nilipoanza kusikia huo mjadala, ambao sasa nilianza kuuzoea masikioni mwangu. Ilikua Hivi, baada ya kumaliza kitabu Cha mpangaji na Mzaha wa Damu, rafiki yangu Gilly, alinitaka mara moja tuweze kupeleka kwa watu wa bongo movie waweze kununua mswada mmojawapo na angalau uweze kuwekwa katika filamu.
Kwa hivi, nilipanda mwendo Kasi mpaka upanga kwa Gily, Nikiwa na flash iliyokuwa na muswada wa vitabu,
Nilimkuta Gilly akinisubiri na Sasa tukaondoka moja kwa moja mpaka huko kwa "wadosi" Kama nilivyotarajia wadosi walitusihi kuacha flash hiyo na eti tungepewa majibu baada ya wiki tatu. Kwa hivi nikarejea yalipo makazi yangu , huko banana ambapo niliendelea kusubiri simu ya Gilly. Na kama vile vile nilivyotarajia wiki tatu ziliisha na wadosi wakapiga chini muswada wetu.
Nakumbuka Gilly alinipigia simu akiwa katika Hali ya unyonge sana baada ya kumuuliza sababu ya mswada kukataliwa "Mapenzi hamna kaka! Wamesema bongo movie Bila mapenzi ndani huuzi" na hivi ndivyo alivyonijibu, na ndivyo nilivyotarajia,
Na pole pole wadau wakaanza “kunisimanga” mitandaoni kuwa hadithi zangu ziliboa, na hakuna Cha maana nimeandika. Mtu mmoja alidiriki kunipigia simu kunitusi kwa kummalizia bando lake kwa kusoma page zaidi ya 300 za simulizi isiyokuwa na mapenzi hata kidogo!
Basi Mimi nilikua nacheka tu mara nilipopata nafasi ya kusoma comment za wadau hao na Kisha nikaendelea kuandika hadithi moja baada ya nyingine. Ni kweli sikupenda kuandika kuhusu mapenzi kwa sababu kadhaa..
Mosi, zilikuwepo Simulizi nyingi zisizo kuwa na idadi kuhusu mapenzi kwa hivi, sikuona kama nilikua na kisa kizuri kuzidi wasimuliaji wengine.
Pili, sikutaka kukosana kabisa na wanawake! Na sikupenda kuwasema vibaya wanaume wenzangu, maana hadithi yangu ingebidi kuwagusa wanaume au wanawake! Kwahiyo basi nikajikuta nakaa mbali na simulizi za wapenda nao! Nilijikuta nawaza hayo wakati simu yangu ya mkononi ilipoita, alikuwa ni Gilly, "Inabidi tuonane kaka!" Alisema Bila kuongea zaidi "Lini" niliuliza "Hata Leo jioni" alisema.
Ilikuwa ni wakati wa likizo kazini kwa hivi sikuona sababu ya kuendelea kukaa nyumbani kuangalia vipindi vya masimango kuhusu uandishi wangu.ndipo niliazimu kwenda kuonana na Gilly kwa hivi basi nilienda bafuni na Kisha baada ya dakika chache nilikua nikikatisha mitaa na ilipotimia saa 10 jioni nilikua sehemu ya Ahadi kukutana na Gily, nilimkuta tayari akiwa na mtu mwingine ambaye sikuwa namfahamu. Baada ya salamu Gilly alianza utambulisho..
"Bila shaka unafahamu kinachoendelea mitandaoni kuhusu hadithi zako'
Alianza Gilly
"Yeah kwamba Sina story za mapenzi Kabisa?" Nilisema nikibugia glasi ya Maji
"Hewalaa" alijibu Gilly
"Ndio Kuna nini" niliuliza huku nikitabasamu
"Basi iyo kesi imeisha kaka!" Alisema Gilly akinywa kinywaji chake huku akitabasamu
"Sijaelewa" nilisema
"mwamba Huyu hapa, hebu msikilize" Alisema Gilly na yule jamaa akanyoosha mkono Sasa tukasalimiana.
"Yeah naitwa Jimmy nilikutana na Gilly wakati nafuatilia inshu moja pale kwa wadosi baada ya kuongea nae nikaona tuna shida sawa..." Alianza
"Iko hivi, Nina kisa Cha mapenzi ambacho kimenitokea Mimi mwenyewe mwaka Jana yaani 2029 na juzi tu hapa ndio jambo limeisha nilitamani sana kuliweka katika filamu Ili Jamii ijifunze, na nilipofika kwa jamaa wa bongo movie wakasema likae kwenye maandishi, saa kwa bahati nzuri kupitia kazi zangu nilikutana ana huyu Gilly , na sasa wakati namueleza akasema anaweza kukupata wewe kuandika hii story "
Jimmy aliongea huku uso wake ukianza kuwa na huzuni. "Subiri , kwahiyo umeshamsimulia tayar na ameona inafaa?"
Niliuliza huku Sasa mwili ukianza kusisimka
"Ndio lakini hatukuma...' Gill alimkatisha
"Story ni Kali brother ndio maana nikaona uwepo kabisa aisee"
Alisema Gilly
"Makubaliano yakoje?" Niliuliza
"Kuna option mbili, ulipwe kwa kazi ya uandishi tu au uwe na baadhi ya haki katika story nzima!" Alisema Jimmy
"Kama nilivyosema siandiki simulizi za mapenzi, kwa hivi nitaandika tu Kisha nitawakabidhi kazi yenu lakini mwandishi na mmiliki itakuwa wewe mwenyewe Jimmy! Ili athari za story uzipate wewe mwenyewe Jimmy!" Nilisema na wote tukacheka
Tulifanya makubaliano ya malipo na Kisha nikatoa simu yangu tayar kabisa kurekodi mkasa wa mapenzi wa Jimmy na tuseme hivi ndivyo Jimmy alivyoanza kutusimulia hadithi yake