Hadithi: Viumbe Hatari (Dangerous Creatures)

Hadithi: Viumbe Hatari (Dangerous Creatures)

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,781
Reaction score
6,139
Karibu kwenye mzigo huu mpya kabisa,

By CK Allan
0746 266 267

Viumbe hatari... Dangerous creatures
1
Mwaka 2030
Sauti ya televisheni ilisikika,
nilikodoa macho kwa utulivu mkubwa nikiwa nimekunja miguu kama ilivyokuwa kawaida yangu, nilibonyeza bonyeza remote yangu ya kisimbuzi na nikavutiwa na The blessed Tv ...

"Hatuwezi kumuweka CK Allan kama mtunzi wa hadithi sawa na Mzee umughaka, deepond, au analyse.. haiwezekan.. huku ni kukosea heshima uandishi"

"Hapana, wote ni waandishi sema, CK Allan hawezi kabisa kuandika kuhusu hadithi za mapenzi mwanzo mwisho...hawezi"

"Sio kwamba hawezi hataki kabisa, na mwenyewe alishasema hataki kuandika kabisa kuhusu wanawake au mapenzi " "Hahaha lini alisema hivyo? Lini?" "Ndio hebu nitajie hadithi yake yoyote ya mapenzi mwanzo mwisho!"
"Angalia Ile ya Kesi."

Nilibonyeza remote ya TV haraka na kubadilisha chaneli nyingine. Tayari nilishaanza kuchoshwa na maneno ya wale waliojiita wachambuzi ambao hakuna walichoshindwa kuchambua.

Pamoja na kuandika hadithi nyingi bado isingekuwa vyema kuanza kulinganishwa na wakongwe wengine ambao kwa namna moja au nyingine Kila mmoja alikua na mkono wake katika fasihi. Kwa hivi, niliamua kubaki na aina moja ya uandishi wa kusimulia matukio ambayo kwangu Mimi nisingeweza kuyaita hadithi.

Basi niliamua kukaa kimya kuandika mpaka miezi michache Hapo nyuma nilipoanza kusikia huo mjadala, ambao sasa nilianza kuuzoea masikioni mwangu. Ilikua Hivi, baada ya kumaliza kitabu Cha mpangaji na Mzaha wa Damu, rafiki yangu Gilly, alinitaka mara moja tuweze kupeleka kwa watu wa bongo movie waweze kununua mswada mmojawapo na angalau uweze kuwekwa katika filamu.

Kwa hivi, nilipanda mwendo Kasi mpaka upanga kwa Gily, Nikiwa na flash iliyokuwa na muswada wa vitabu,
Nilimkuta Gilly akinisubiri na Sasa tukaondoka moja kwa moja mpaka huko kwa "wadosi" Kama nilivyotarajia wadosi walitusihi kuacha flash hiyo na eti tungepewa majibu baada ya wiki tatu. Kwa hivi nikarejea yalipo makazi yangu , huko banana ambapo niliendelea kusubiri simu ya Gilly. Na kama vile vile nilivyotarajia wiki tatu ziliisha na wadosi wakapiga chini muswada wetu.

Nakumbuka Gilly alinipigia simu akiwa katika Hali ya unyonge sana baada ya kumuuliza sababu ya mswada kukataliwa "Mapenzi hamna kaka! Wamesema bongo movie Bila mapenzi ndani huuzi" na hivi ndivyo alivyonijibu, na ndivyo nilivyotarajia,

Na pole pole wadau wakaanza “kunisimanga” mitandaoni kuwa hadithi zangu ziliboa, na hakuna Cha maana nimeandika. Mtu mmoja alidiriki kunipigia simu kunitusi kwa kummalizia bando lake kwa kusoma page zaidi ya 300 za simulizi isiyokuwa na mapenzi hata kidogo!

Basi Mimi nilikua nacheka tu mara nilipopata nafasi ya kusoma comment za wadau hao na Kisha nikaendelea kuandika hadithi moja baada ya nyingine. Ni kweli sikupenda kuandika kuhusu mapenzi kwa sababu kadhaa..
Mosi, zilikuwepo Simulizi nyingi zisizo kuwa na idadi kuhusu mapenzi kwa hivi, sikuona kama nilikua na kisa kizuri kuzidi wasimuliaji wengine.

Pili, sikutaka kukosana kabisa na wanawake! Na sikupenda kuwasema vibaya wanaume wenzangu, maana hadithi yangu ingebidi kuwagusa wanaume au wanawake! Kwahiyo basi nikajikuta nakaa mbali na simulizi za wapenda nao! Nilijikuta nawaza hayo wakati simu yangu ya mkononi ilipoita, alikuwa ni Gilly, "Inabidi tuonane kaka!" Alisema Bila kuongea zaidi "Lini" niliuliza "Hata Leo jioni" alisema.

Ilikuwa ni wakati wa likizo kazini kwa hivi sikuona sababu ya kuendelea kukaa nyumbani kuangalia vipindi vya masimango kuhusu uandishi wangu.ndipo niliazimu kwenda kuonana na Gilly kwa hivi basi nilienda bafuni na Kisha baada ya dakika chache nilikua nikikatisha mitaa na ilipotimia saa 10 jioni nilikua sehemu ya Ahadi kukutana na Gily, nilimkuta tayari akiwa na mtu mwingine ambaye sikuwa namfahamu. Baada ya salamu Gilly alianza utambulisho..

"Bila shaka unafahamu kinachoendelea mitandaoni kuhusu hadithi zako'
Alianza Gilly
"Yeah kwamba Sina story za mapenzi Kabisa?" Nilisema nikibugia glasi ya Maji
"Hewalaa" alijibu Gilly
"Ndio Kuna nini" niliuliza huku nikitabasamu
"Basi iyo kesi imeisha kaka!" Alisema Gilly akinywa kinywaji chake huku akitabasamu
"Sijaelewa" nilisema

"mwamba Huyu hapa, hebu msikilize" Alisema Gilly na yule jamaa akanyoosha mkono Sasa tukasalimiana.
"Yeah naitwa Jimmy nilikutana na Gilly wakati nafuatilia inshu moja pale kwa wadosi baada ya kuongea nae nikaona tuna shida sawa..." Alianza

"Iko hivi, Nina kisa Cha mapenzi ambacho kimenitokea Mimi mwenyewe mwaka Jana yaani 2029 na juzi tu hapa ndio jambo limeisha nilitamani sana kuliweka katika filamu Ili Jamii ijifunze, na nilipofika kwa jamaa wa bongo movie wakasema likae kwenye maandishi, saa kwa bahati nzuri kupitia kazi zangu nilikutana ana huyu Gilly , na sasa wakati namueleza akasema anaweza kukupata wewe kuandika hii story "
Jimmy aliongea huku uso wake ukianza kuwa na huzuni. "Subiri , kwahiyo umeshamsimulia tayar na ameona inafaa?"

Niliuliza huku Sasa mwili ukianza kusisimka
"Ndio lakini hatukuma...' Gill alimkatisha
"Story ni Kali brother ndio maana nikaona uwepo kabisa aisee"
Alisema Gilly
"Makubaliano yakoje?" Niliuliza
"Kuna option mbili, ulipwe kwa kazi ya uandishi tu au uwe na baadhi ya haki katika story nzima!" Alisema Jimmy

"Kama nilivyosema siandiki simulizi za mapenzi, kwa hivi nitaandika tu Kisha nitawakabidhi kazi yenu lakini mwandishi na mmiliki itakuwa wewe mwenyewe Jimmy! Ili athari za story uzipate wewe mwenyewe Jimmy!" Nilisema na wote tukacheka

Tulifanya makubaliano ya malipo na Kisha nikatoa simu yangu tayar kabisa kurekodi mkasa wa mapenzi wa Jimmy na tuseme hivi ndivyo Jimmy alivyoanza kutusimulia hadithi yake
 
2
Mimi naitwa James Maringo Mchunia ,Kabla ya mambo haya nilikuwa mwajiriwa katika shirika la kuhifadhi chakula la taifa, mpaka niliposimamishwa kazi, na naamini baada ya haya basi nitarejea kazini,
Mwaka 2027 mwezi wa Tano serikali iliamua kununua mahindi kwa wakulima wadogo wadogo kwa lengo la kuondoa ukiritimba na unyonyaji ambao ulikua ukifanyika, kwa hivi tulisambazwa karibia nchi nzima katika mikoa ambayo ilikua ikilima mahindi na ilitupasa kuhakikisha ni serikali inanunua mahindi hayo moja kwa moja kwa wakulima badala ya kutumia wafanyabiashara. Ilikuwa ni mwezi wa Saba ambapo Mimi na mwezangu isaka tulikwenda Gairo ambapo tungenunua mahindi ya Gairo, Kilindi, na baadhi kutoka kiteto kupitia Sunya,
Ni safari ambayo tuliifurahia maana mbali na kutoka nje ya ofisi tulilipwa vizuri sana na kwa miezi mitatu tuliyotakiwa kukaa huko tulitegemea kufurahia maisha kabisa!
Wakati tunafika Gairo siku ya ijumaa tulitegemea kuanza zoezi siku ya jumatatu,
Na kituo chetu tulipanga kiwe maeneo ya kiegeya
Na kwa hivi tukaona angalau weekend tuimalizie Gairo mjini, halafu jumatatu twende.
Kwahiyo baada ya kupata hoteli kesho yake jumamosi tulikua mtaani tukifaidi kwa macho uumbaji wa Mungu huko na huko, na haswa watoto wa Kikaguru.
Majira ya saa 8 mchana tulikuwa tunatoka tawi la NMB Gairo wakati Isaka aliponikazia sauti nitazame upande wa kulia kwake,
"Aiseeee!" Macho yalinitoka baada ya kuona msichana mzuri akisogelea kwenye ATM pale tulipotoka,
"Mzee nilikuambia tusiende kijijini Leo unaona sasa! Hebu mcheki mtoto yule!"
Alisema isaka akitaka kuondoa gari.
"Hapana tusiondoke kwanza!" Nilisema huku nikifungua mlango na kutoka nje
Na kumkimbilia yule dada
"Samahani dada" nilisema nikijichekesha
"Nakusikiliza" nae alijibu huku akionekana kabisa "ameshawazoea" wanaume mpaka nikaanza kuona aibu kiasi...
"Hebu katoe basi kwanza Hela halafu tuongee nakusubiri"
Nilisema huku Nikiwa naamanisha kumsubiri,
alitabasamu Kisha akaondoka zake kuelekea kwenye ATM
Na kweli baada ya dakika chache alirudi akiwa na kirisiti mkononi huku anakichana chana
"Ha kwahiyo ukanisubiri kweli!?" Alisema huku akitoa tabasamu
"Yeah, lazima nisubiri"
Nilisema
"Haya niambie unasemaje maana nawahi halafu unamchelewesha mwenzako kule!" Alisema huku akinyoosha kidole kuelekea kule alipokuwa Isaka kwenye gari na ndio nikakumbuka kumuangalia isaka ambaye alikua bize na simu yake..
"Ah sikia Mi naitwa Jimmy, naomba namba Yako Ili nikucheki baadae kama hutajali, naomba sana!" Nilisema
Na Bila kutegemea alinyoosha mkono wake na Mimi nikatoa simu nikatoa nywila nikampa akaandika namba yake
"Naitwa Angel" alisema akiondoka
"Poa yangu inaishia 267 andika Jimmy"
Nilisema huku nikirudi kwenye gari kwa furaha

"Twende zetu" nilisema nikifunga mkanda na tukarudi zetu kwenye vyumba vyetu hotelini huku mawazo yakiwa kwa angel tu. Nusu saa baadae nikiwa chumbani nikajikuta nashindwa kuvumilia nikachukua simu yangu
"Hello Angel" nilijikuta nikatuma meseji
"Hello Jimmy" alijibu
"Unafanya Nini now" nilimuuliza
"Namalizia kupika"
Aijibu
"Naomba tuonane basi jioni hii"
Nilituma Tena ujumbe huku moyo ukipiga kwa nguvu
"Poa" alijibu kwa ufupi.
Sasa kwa jinsi mapenzi yalivyonizagaa kwa haraka sikuweza kujiuliza mara mbili nilijikuta nampenda sana, hata kule kukubali haraka haraka kuonana nae sikujiuliza mara mbili niliamua kumfuata Isaka na kumuelezea kila kitu kuhusu suala zima la mimi kuingia rasmi kwenye mahusiano na Yule binti. Hata hivyo kwa wakati huu nilitaka kabisa kumuoa Angel mazima, yaani nilimpenda! Basi nilisubiri na ilipotimia saa 12 jioni nilimuuliza Angel sehemu ya kukutania na akanitajia mgahawa mmoja ambao ulikuwa karibu na aliposema anaishi. Kwa haraka nilisogea nje na kurukia boda boda
“kuna mgawaha unaitwa SISI ,nipeleke hapo”
“buku mbili broo” alisema Yule mtu wa piki piki na safari ikaanza,
Nilifika nikachagua meza iliyokuwa tulivu mwishoni kabisa kisha nikamtumia meseji mrembo Angel kuwa nimefika mitaa ile
“nakuja” alijibu.
Ni kweli baada ya dakika kadhaa nilisikia mngurumo wa piki piki nje na nilipochungulia niliona Angel akiwa anashuka kwenye piki piki na niseme wazi kuwa safari hii Angel alikuwa amependeza sana kuliko wakati ule wa mchana! Alikuwa amevaa suruali Fulani hivi ya jeans na tisheti iliyokuwa na maandishi makubwa ya herufi mbili tu “CK” kwa haraka nilitoka nje na kutoa waleti yangu ili nimlipe Yule boda boda lakini Angeli aliniwahi kwa kutoa elfu tano kwenye pochi yake na kumpa Yule jamaa wa piki piki
“ngoja nilipe” nilisema huku nikijaribu kufungua waleti yangu
“hapana usijali” alisema huku akipiga hatua kuelekea pale nilipokuwepo na kisha tukaingia ndani ya ule mgahawa, na baada ya kuketi nilinyoosha mkono na kumuita mhudumu aje kutuhudumia
 
Na Flash niliyorekodi simulizi ya jimmy ikapatwa na virus ikalika🥱🥱🥱
 
3
Angel aliagiza kinywaji laini tu na mimi nikagiza malt ya kahawa , huku tukiendelea kupiga hadithi za hapa na pale,
Kwa haraka tulionekana kama mtu na mpenzi wake kabisa,
Angel hakuwa muongeaji sana alitaka tu kujua nilichomuitia pale jioni ile
“angel ujue inaweza kuwa ajabu lakini kiukweli mimi nimekupenda kabisa!” nilianza kufunguka
Basi Angel alicheka sana mpaka nikashangaa
“aisee kwanini unanicheka hivi mpaka najisikia vibaya” nilimuuliza nikitabasamu
“unajua Jimmy nimefurahi sana.. yaani nilijua tu utasema umenipenda, umevutiwa na mimi na blah blah za wanaume.. ila sikutegemea ungesema eti umenipenda “kabisa” !!
Alisema Angel
“kwahiyo neno KABISA ndio likuchekeshe hivi Angel” nilimuuliza huku na mimi nikianza kucheka na hatimaye wote tukacheka!
“yaani you are so funny... honest sijawahi kukutana na mwanaume akasema amenipenda kabisa!
“basi na mimi sijawahi kukutana na mwanamke mzuri kama wewe ndio maana nimekupenda kabisa” nilisema huku tukizidi kucheka tena.
Tulipiga story mpaka majira ya saa mbili kasoro ambapo Angel aliomba kuondoka akidai kuna dada yake ambaye amekuja kumhudumia
Maelezo ya Angel yalikuwa hivi, yeye ni mzaliwa wa Arusha Monduli, alikokulia na kumalizia masomo yake , kwa sasa ni mhitimu wa chuo na anasubiri “mahafali” mwezi wa 11 kuhitimu shahada yake na dada yake ameolewa pale Gairo na amejifungua kwa opareshini wiki moja iliyopita na hivi amekuja kumsaidia kwakuwa hana mfanyakazi, na yeye ameamua kubadilisha kidogo mazingira ya nje ya Arusha.
Basi nilimsindikiza hadi nje ambapo nilitafuta boda boda akapanda huku tukiahidi kuwasiliana baadae! Nami nilirudi hotelini haraka na kumsimulia Isaka kila kitu kilichotokea baina yangu na Angel.
“mwanangu huyu demu akiingia , nachukua mazima!” nilimwambia Isaka
“dah kweli umezama mzee, siku ya kwanza tu?” aliuliza Isaka huku akicheka
Ni kweli usiku ule nakumbuka tulichati hadi saa 6 usiku mimi na Angel na kisha tulikubaliana kuonana kesho yake jumapili kuagana maana jumapili hiyo hiyo jioni tulitakiwa kuondoka Kwenda Kilindi tayari kuanza zoezi la ununuzi wa mahindi siku ya jumatatu.
 
4
Jimmy aliendelea kutusimulia hadithi yake na wakati mwingine mimi na Gilly tulitazamana na kucheka au kusikitika mara kadhaa,
“aisee naona kwa leo tuishie hapa, mimi nimuwahi wife kwanza, then kesho asubuhi mapema tutaendelea ili tumalize kabisa” nilitoa maoni yangu baada ya kutazama saa yangu ,
Na wenzangu wote wakakubaliana na hoja yangu na wote tukaingia kwenye gari ya Gilly na kuondoka.
“kwahiyo kwasasa Isaka yuko wapi?” nilimuuliza Jimmy wakati tukiwa ndani ya gari
“utajua mengi zaidi kuhusu yeye kesho, lakini kwa ufupi sana ni kwamba, aliuwawa!” alisema Jimmy kwa huzuni
“whaaat?” na mimi nilihamaki
“brother.. nisingeweza kukutafuta kwa kazi mbovu.. relax brother safari hii tuna stori bab kubwa” alisema Gilly..
Kwa maneno hayo ya Gilly akili yangu iliniambia hii ni zaidi ya hadithi ya mapenzi tu bila shaka huko mbele tutaona mengi zaidi niliwaza.
Nilirudi nyumbani na baada ya kumsimulia mke wangu Habari za Jimmy, alitamani na kumsikiliza kwahiyo, nikaunganisha simu yangu na kiredio kidogo pale chumbani na kurudia tena kusikiliza ile simulizi ya Jimmy.
“naona kama Jimmy, ana hofu bado!” mke wangu aliongea
“kwanini?” niliuliza
“sikia ni kama anatamani kumaliza hadithi yake kwa haraka sana as if haamini kama hadithi yake itatoka” mke wangu alichangia
“ushaanza ujasusi wako” nilimtania huku nikizima ile simu na kupanda kitandani.
Usiku ule nilitafakari sana kuhusu kisa cha Jimmy, zaidi sana ni baada ya kuambiwa kuwa Isaka alikuwa amefariki au tuseme ameuwawa kama alivyosema Jimmy,
Ni kama kuna sauti iliniambia hii ni zaidi ya hadithi ya mapenzi tu,
“tutajua kesho” nilijisemea huku nikijaribu kutafuta usingizi.
**********************************************************
Kesho yake mapema Gilly alinipigia twende tukamalizie simulizi ya Jimmy,
Kwakuwa ilibidi niipate mapema nami nianze jukumu langu la kuiweka ile simulizi katika maandishi kama tulivyokuwa tumekubaliana mwanzo, kwa hivi nikajiandaa haraka kuelekea sehemu ya kukutania.
Nilikuta tayari waamewasili na kwakuwa ilikuwa mapema Gilly alishauri tuanze na supu kwanza kisha tupate sehemu tulivu tuendelee na mazungumzo yetu.
“ haya tuendelee sasa Jimmy, nadhani ulituacha pale mlipanga kuonana kesho yake kuagana na Angel, alianza Gilly
“yeah kumbuka usiku mzima tulikuwa tunachati tu kwahiyo kesho yake angel aliniambia ataenda misa ya kwanza kisha akitoka majira ya saa 4 tunaweza kuonana,
Ni kweli asubuhi yake alikuja akisema anatokea kanisani, tulipata kifungua kinywa kwa Pamoja na tukapiga hadithi kadhaa na Angel alikubali rasmi kuwa mpenzi wangu na kuahidi tutakuwa tunawasiliana nikiwa huko kijijini.
Kwahiyo jioni ile tuliondoka kuelekea Kilindi na mara kwa mara nilikuwa nikiwasiliana kwa video call na angel kila sehemu tuliyokuwa tunaenda,
Hakika mapenzi yalikuwa moto moto sana na kwa ufupi ni kuwa mtoto Angel aliniteka kabisa!
Jimmy aliendelea kuongea huku mara kadhaa akiwa kama anayekumbuka baadhi ya matukio huku akitingisha kichwa!
 
5
Tulifika salama kabisa kule kijijini na tuliendelea na kazi vizuri kwakuwa tayari wananchi walipewa taarifa zetu kwahiyo hatukupata shida yoyote katika kukusanya mazao, na tulishirikiana vizuri kabisa na uongozi wa Kijiji.
Kila wakati nilikuwa nikiwasiliana na Angel, hususani pale kazi zilipokuwa zimepungua, na usiku ndio ilikuwa balaa!
Naweza kusema hakuna siku ilipita mimi na Angel hatukuwasiliana.
Baada ya wiki moja alinipa taarifa kuwa anataka kurudi arusha, wazazi wake wamepata safari ya nje ya nchi na kwa hiyo hakukuwa na mtu wa kubaki nyumbani kwahiyo akanisihi nikimaliza shughuli hiyo nipitie Arusha kabla sijaenda Dar! Basi nilikubaliana nae na kumruhusu kiroho safi arudi Arusha,
“vipi kuhusu mambo ya pesa, hajawahi kukuomba pesa yoyote?” hatimaye Gilly aliuliza
“huwezi kuamini, hata kuna siku nyingine ni yeye ndie alikuwa akinitumia pesa ya vocha! Na hata nilipojaribu kumwambia nimtumie nauli hiyo ya Kwenda Arusha, alikataa kabisa akisema tayari alishatumiwa pesa na baba yake na pia dada yake alishampa pesa ya kutosha! Ilifika hatua mpaka Isaka mwenyewe alimkubali kuwa huyu ndie wife material!” jimmy aliendelea na hadithi yake.
Hata hivyo mara baada ya kufika Arusha kuna mambo yalianza kunipa wasi wasi
Kwanza mara nyini usiku alikuwa hapatikani, au tuseme wakati mwingine simu haikupokelewa! Na mara nyingi angekuwa wa kwanza kunitafuta kesho yake kuwa alipitiwa na usingizi, ama simu ilikuwa silent na hakujua alipoiweka, na kunihakikishia kabisa kuwa hakuna tatizo lolote kabisa! Na kwakuwa nilikuwa nimezama, sikujaribu kuchunguza zaidi!
Kwa maelezo yake, walikuwa wanaishi Monduli lakini walihamia Arusha mjini baada ya baba yake kuhamishiwa kikazi huko, kwa maelezo yake alisema kuwa baba yake alikuwa mwajiriwa katika mojawapo ya taasisi za kiserikali ila hakuniambia ni taasisi gani! Kwa hiyo basi baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya ukusanyaji wa mazao na kuwasajili wakulima wote waliouza mazao yao kwenye mfumo maalum, mimi na Isaka tuliamua Kwenda kumalizia siku kadhaa sehemu nyingine..
Isaka yeye alikuwa na dada yake Korogwe Tanga kwahiyo tukaona ni vyema tumpitie pale, nimuache kisha mimi niende Arusha kumuona Angel, then nirudi nimpitie Isaka turudi zetu Dar, kulingana na maongezi yetu na Angel alisema hakuna shida kwasasa yeye muda wote yuko free maana wazazi wake hawakuwepo nyumbani , kwa hivi nikaona bora nimfanyie surprise nisimwambie kama naenda Arusha.
Kwahiyo mara baada ya kufika Korogwe moja kwa moja niliunganisha kwa basi kuelekea Arusha! Njiani nilikuwa nawasiliana na Angel akasema yupo nyumbani kwao ametulia tu! Kwa hivi niliona kana kwamba dereva wa basi hachangamki jinsi inavyotakiwa!
Kila wakati nilitazama nje kuona kama tunakaribia Arusha! Na hatimaye saa 5 na nusu usiku tuliingia stend kuu ya mabasi Arusha, nilishuka haraka na kuvaa begi langu dogo mgongoni na kisha nikatoka nje ya stendi na nilitoa simu yangu haraka na kurequest usafiri uliokuwa Jirani ambapo niliona ni ndani ya dakika 10 na nilipokuwepo,
Nilijaribu kumpigia Angel lakini simu yake ilikuwa inaita tu! Hata hivyo sikuwa na mpango wa kumuona usiku ule nilisubiri usafiri ili nipate sehemu ya kupumzika kesho yake nionane nae!
 
6
Nilipata hoteli nzuri usiku ule nikajipumzisha na kupitiwa na usingizi, asubuhi niliamka haraka na kujiandaa kisha nikatoka mtaani na kununua zawadi kadhaa kwa ajili ya Angel, baada ya kumaliza kupata kifungua kinywa sasa nilikuwa tayari kuonana na Angel,
Nilitoa simu yangu na kumpigia, simu iliita tu bila kupokelewa,
Kisha baada ya dakika chache akapiga yeye,
“hello dear, Samahan sana nilikuwa nafanya usafi hapa nikasema nikimaliza nitakucheki” alianza mwenyewe kujitetea
“ok, nina surprise yakoo…” nilianza
“whaaat” aliuliza
“sikia nakupigia video call” nilimwambia
“okay”
Hata hivyo ilichukua dakika kadhaa hata hivyo alikua kama kwenye mazingira ambayo sikuweza kuyaelewa kwa haraka hivi kwa siku ile, alikuwa kwenye bustani nzuri sana ya maua na amekaa kwenye bembea
“hapa ni wapiiiiii?” nilimwambia baada ya kupokea,
“haaaaaa, don’t tell me you are in….” aliongea huku akishika mdomo
“yeah, nimekuja kwa ajili yako dear!” nilisema huku nikitabasamu
“JIMMY NO!” alisema huku uso wake ukibadilika, na ile furaha ikakata kabisa
“what honey? Nipo arusha kwa ajili yako!” nilisema tena
Na kwa mshangao mkubwa simu ikakatwa na akanipigia kawaida
“hello Angel, mbona umekata, whatswrong?” nilimuuliza nikiwa nimehamaki
“sikia , ni vigumu mimi kutoka hapa nilipo, naomba nielewe tu kwa leo JIMMY! TRUST ME hatuwezi kuonana!” alisema Angel na sasa nilishindwa kuvumilia ni kama kuna kitu kilikuwa kinanikaba kooni hivi nikakata simu..
Sikuelewa kama tayari nilikuwa nimekaa chini mpaka niliposikia vicheko vya wapita njia pembeni yangu ndipo nikaundua kwamba Tayari kumeanza kuchangamka!
Nilijikuta nashindwa kuelewa kama nilie au nicheke, nilisimama na kuita boda, nikarudi hotelini,
“kaka sitapitia tena Korogwe mi narudi Dar leo leo napanda ndege tu sina jinsi!” nilimwambia Isaka kisha nikakata simu nikazima maana sikutaka maswali mengi zaidi
Angel why?
Nilijiambia mwenyewe bila kupata majibu
**********************************************
NILIFANYA booking ya ndege ya saa 9 jioni na muda uliobaki niliamua kuosha macho sehemu kadhaa za jijini Arusha, sikutaka kabisa kuwasha simu yangu,
Kwa haraka nilijikuta nawaza sana kuhusu Angel
“dah Watoto wa elf 2 ni balaa sana” nilijisemea huku nikiwaza
“lakini huyu mtoto pengine ni uoga tu wa mapenzi na wanaume, mbona ananipenda kabisa yule mtoto!” nilijikuta najiuliza maswali mengi bila majibu
sikuona cha kufanya pale Arusha kwani nilihisi kila mtu ananizomea,
niliamua Kwenda zangu uwanja wa ndege tayari kabisa kurudi Dar..
 
6
Nilipata hoteli nzuri usiku ule nikajipumzisha na kupitiwa na usingizi, asubuhi niliamka haraka na kujiandaa kisha nikatoka mtaani na kununua zawadi kadhaa kwa ajili ya Angel, baada ya kumaliza kupata kifungua kinywa sasa nilikuwa tayari kuonana na Angel,
Nilitoa simu yangu na kumpigia, simu iliita tu bila kupokelewa,
Kisha baada ya dakika chache akapiga yeye,
“hello dear, Samahan sana nilikuwa nafanya usafi hapa nikasema nikimaliza nitakucheki” alianza mwenyewe kujitetea
“ok, nina surprise yakoo…” nilianza
“whaaat” aliuliza
“sikia nakupigia video call” nilimwambia
“okay”
Hata hivyo ilichukua dakika kadhaa hata hivyo alikua kama kwenye mazingira ambayo sikuweza kuyaelewa kwa haraka hivi kwa siku ile, alikuwa kwenye bustani nzuri sana ya maua na amekaa kwenye bembea
“hapa ni wapiiiiii?” nilimwambia baada ya kupokea,
“haaaaaa, don’t tell me you are in….” aliongea huku akishika mdomo
“yeah, nimekuja kwa ajili yako dear!” nilisema huku nikitabasamu
“JIMMY NO!” alisema huku uso wake ukibadilika, na ile furaha ikakata kabisa
“what honey? Nipo arusha kwa ajili yako!” nilisema tena
Na kwa mshangao mkubwa simu ikakatwa na akanipigia kawaida
“hello Angel, mbona umekata, whatswrong?” nilimuuliza nikiwa nimehamaki
“sikia , ni vigumu mimi kutoka hapa nilipo, naomba nielewe tu kwa leo JIMMY! TRUST ME hatuwezi kuonana!” alisema Angel na sasa nilishindwa kuvumilia ni kama kuna kitu kilikuwa kinanikaba kooni hivi nikakata simu..
Sikuelewa kama tayari nilikuwa nimekaa chini mpaka niliposikia vicheko vya wapita njia pembeni yangu ndipo nikaundua kwamba Tayari kumeanza kuchangamka!
Nilijikuta nashindwa kuelewa kama nilie au nicheke, nilisimama na kuita boda, nikarudi hotelini,
“kaka sitapitia tena Korogwe mi narudi Dar leo leo napanda ndege tu sina jinsi!” nilimwambia Isaka kisha nikakata simu nikazima maana sikutaka maswali mengi zaidi
Angel why?
Nilijiambia mwenyewe bila kupata majibu
**********************************************
NILIFANYA booking ya ndege ya saa 9 jioni na muda uliobaki niliamua kuosha macho sehemu kadhaa za jijini Arusha, sikutaka kabisa kuwasha simu yangu,
Kwa haraka nilijikuta nawaza sana kuhusu Angel
“dah Watoto wa elf 2 ni balaa sana” nilijisemea huku nikiwaza
“lakini huyu mtoto pengine ni uoga tu wa mapenzi na wanaume, mbona ananipenda kabisa yule mtoto!” nilijikuta najiuliza maswali mengi bila majibu
sikuona cha kufanya pale Arusha kwani nilihisi kila mtu ananizomea,
niliamua Kwenda zangu uwanja wa ndege tayari kabisa kurudi Dar..

Kafupiiiii
 
7
Nilirudi Dar,
Na moja kwa moja nikaenda nyumbani kwangu kimara, nilioga kisha nikalala,
Saa mbili usiku nilistuka baada ya kuhisi njaa sana, sikuwa na jinsi zaidi ya kwenda jikoni kurekebisha chakula , baada ya kula na kuoga sasa ndio nikakumbuka simu,
Nilikuta meseji nyingi za isaka na moja ilitaka nimpigie nikirudi hewani
"Tutaongea ukija Dar kaka" nilimwambia Isaka hivyo tu
"Najua una hasira na mimi lakini naomba nielewe mpenzi"
Ilikua meseji ya Angel.
Sikumjibu chochote baadae nikaona huu ni ujinga kupelekeshwa kizembe na kitoto cha elfu 2! Kwahiyo niliamua kufuta na namba yake na kuamua kumtoa kichwani!
Hatimaye wiki moja ikipita na nilimsimulia Isaka kila kitu kilichotokea baina yangu na Angel
"Kwani yule dogo alishawahi kula hata mia yako?"
Hapana
"Ulishafanya nae mapenzi?"
Hapana
"Ulishamtambulisha kwenu?"
Hapana
"Sasa kwanini uone kama kakufanyia kitu cha ajabu sana,
Relax mzee hivi vitoto vya elfu 2 vinataka taiming sana,
Hapa ningekuona mjanja ukitafute hiki ukibinyee usiku mzima kutoa hasira,
Halafu ndio ukiteme"
Yalikuwa maneno ya Isaka,
Ambaye alidhani kwa akili zake hapo ananitia moyo eti!
Basi siku zilienda siku hiyo ilikuwa siku ya Ijumaa jioni wakati natoka kazini simu yangu iliita ,
Alikuwa ni dogo mmoja tunakaa nae jirani
"Hello kaka Jimmy ,mimi Oscar hapa"
"Yes , vipi!"
"Kuna manzi yupo hapa anakuulizia "
"Hapo kwangu?"
"Ndio hapa nyumbani kwako ,
Nimemuuliza jina kakataa kutaja"
Alisema Oscar
Kuhusu Oscar.
Ni kijana wa nyumba ya jirani ambapo wakati mwingine nilipokuwa nje ya Dar , nilimuachia ufunguo wangu kwa ajili ya kuwasha taa, na dharula nyinginezo,
Oscar alikuwa amemaliza kidato cha sita tulikuwa tunaishi wote kwenye hizi nyumba za national housing upande wa chini, na jinsi ilivyo
Ilikuwa mgeni yoyote akiingia lazima aonekane na pande zote mbili kwakuwa tulitumia geti moja
"Alikuja na usafiri gani?"
Nilimuuliza Oscar
"Tax kaka"
"Yupoje ukimcheki"
"Ni mweupe hivi mrefu na ana shape hivi "
Alisema Oscar
"Hebu angalia kuna picha nakutumia uone kama ni yeye ni jibu kwa masej"

Nilisema huku nikitafuta picha ya Angel na kumtumia Oscar
"Ni yeye"
Alijibu
"Shiiiit"
Huyu dogo kakuaje nyumbani kwangu? Sasa niliwaza huku nikiwa sijui kama nikumbalie au nimfukuze!
Nilijaribu kumuuliza Isaka kama ni yeye alimuelekeza kwangu lakini alikataa kabisa,
"Itafahamika"
Nilijisemea huku nikirudi barabarani na kuendelea na safari kuwahi nyumbani...
Ni kweli nilifika na mara tu nilipoingiza gari ndani
Angel alinikimbilia haraka na kunikumbatia kwa nguvu! Nilishindwa kumtoa na ghafla nilijikuta tu hasira zote zinayeyuka kama barafu kwenye moto..
Nilitoa mizigo michache kwenye gari na Oscar akanisaidia kuingiza ndani kisha yeye akaondoka na kutuacha!
Nilimuacha Angel sebuleni nikaingia chumbani kubadilisha nguo nikarudi sebuleni na sasa nilikuwa tayari kwa mahojiano
Kwakuwa nilikuwa na maswali mengi.. hata hivyo ni kama yeye mwenyewe alijua ninayo mengi kwahiyo akaanza yeye mwenyewe kufunguka
 
Back
Top Bottom