KijanaHai
Member
- Aug 7, 2022
- 7
- 6
Hadithi ya kuhuzunisha
Changamoto Za Vijana
Tatizo la ajira kwa vijana ni kilio kilichokosa mfariji wa kudumu. Japo kwa Afrika kilio cha ajira machozi yake ni damu Tanzania Vijana wanaongezeka na tatizo linaendela kukua uku wazazi wengi ambao walifurahia ujio wa watotot wao kwa kuwapa majina mazuri na kila hitaji na kutumia mpaka zile raslimali walizofukia udongoni ilimradi kijana wao waliyemkuza awe na mustakabali mzuri wa maisha yake licha ya kusoma katika shule zilizokosa madawati na umbali mrefu wa kutembea kufuata matumaini ya kesho (Elimu) bado ata wale walio tafuta kesho za watoto wao kwa kuwalipia ada kubwa na usafiri toka nyumbani mpaka shuleni na wao nyumba zao ziko na misiba ya vjana wao walio amua kuchagua silaha za kujiulia kama utumiaji wa madawa ya kulevya, kujiuza, wizi, ujambazi, ulevi wa kupindukia.
Vilio hivi vinatokana na kukosa mifumo rafiki toshelevu ya kumuandaa, kumlinda, kuwezesha, kumuongoza na kumjenda ambayo ni sera rafiki, mipango rafiki, kodi rafiki kwa vijana wajasiriamali, mikopo rafiki isiyo na urasimu, Elimu yenye ubora na kukidhi ushindani wa kidunia, Ukosefu wa majukwaa tetezi sauti za vijana, na kunyimwa fursa ya uwakilishi katia vyombo vya kimaamuzi ili kutetea ajenda zao muhimu.
Nyumba nyingi za chini ya ardhi zimefukia ndoto za vijana wengi waliokuwa wanasubiri mifumo rafiki ipatikane kufufua matumaini yao ya kuishi kama vijana walio hai na wengine wamezikwa kwa kupigwa na vipigo vya wnanchi wenye hasira kali baada ya kuibiwa mali zao wengine kwa kunywa sumu au kunjinyonga kwa kutia kitanzi shingoni mwao, wengine maradhi ya ukimwi na mengine hayawezi kutamkika yaliwaondoa kwani walilamika hawakusikika kilio chao mwisho walikata taamaa ya maisha yao, sio kwamba wote hao hawakupenda kuishi kama wenzao waliopo hai leo na wengine wakiendelea kupotea kwenye macho yetu kufuata wenzao katika dunia nyingine isiyojukilana kuna neema na changamoto zipi .
Licha ya yote kitanzi kikubwa kwa vijana wnaoendelea kupambana kinachowanyonga pindi wanapoamua kujitutumua kutafuta ajira wanakutana nacho ofisi mbalimblai kinaitwa uzoefu na mtaji. Ivyo vijana wengi wanajaribu kila namna wanayoona inafaa na sasa kamali ndiyo imeonekana mkombozi kwa vijana wengi na inakuwa kwa kasi pasipo vijana kujali hasara zake za kiakili na upotevu wa kifedha bado ndio mdomo pekee wa mamba wanaoona afadhali kwao wanaweza kutoa samaki mamba aliye mmeza pasipo kujali watangatwa mara ngapi.
Kwa mwenendo huu utuwezi kutengeneza Tanzania yenye maendeleo endelevu yanayotokana na nguvu kazi ya vijana kama tunavyojinadi zaidi ya kutengeneza vijana WALALAMIKAJI NA WANAOSUBIRI KUJILIPA SIKU WAKIPATA FURSA KATIKA TASISI BINAFSI NA UMMA KUFIDIA MACHUNGU. Kuna namna mbili zinazoweza kuanza kutusaidia kutoka kwenye janga hili lililobeba volcano inayosubiri mda wowote kulipuka.
Hadithi ya Kufurahisha
NANI NAWAJIBIKA?
Wazazi wa vijana wa Kitanzania jukumu lao ni kuleta watoto duniani na mwenye jukumu la kumlea uyu mtoto mpaka awe kijana mwenye kutimiza malengo na ndoto zake na kulisaidia taifa ni serikali. Serilaki kama mlezi wa vijana anajukumu la kuhakikisha vijana wanaandaliwa mifumo rafiki ya kisera, sheria, Elimu na Mazingira. Mwenye Jukumu la pili la kufikia ndoto za kijana na kulisaidia taifa lake ni kijana mwenyewe. Leo sitatoa lawana na kueleza changamoto bali nitajikita kuwashauri Serikali kama mlezi na Kijana kama Mlelewa jukumu lake ili kutengeneza hadithi nzuri.
A. Serikali ifanye nini Kumuwezesha kijana Kuwa Mtafutaji badala ya mlalamikaji.
Bada ya kufanya mabadiliko hayo na mengine baada ya miaka 20 Tutakuwa na Tanzanaia tuitakayo inayojengwa na vijana wenye uwezo wa kutafuta na si kulalamika.
#Vijana
Asanteni kwa kusoma hadithi hii ndefu ✍️🙏

- Kuwapata nafasi za uongozi vijana kuwaandaa kuwa viongozi bora wenye uzoefu kwa;
- kubadili sifa za kugombea na kuteuliwa nafasi mbali kwa kufanya marekebisho katika Katiba ya Tanzania mwaka 1997 Sura ya pili sehemu ya pili 67 sheria ya 1994 Na 34 ib.11, sheria ya 2000 Na 3 iba. 9 kifungu (4) Umri wa kuwa makamu pili uwe kuanzia miaka 35.
- Kurekebisha sura ya tatu sehemu ya pili (67) sifa za mtu kuwa mbunge sheria ya 1984 Na.15 ib.13, sheria ya 1992 Na 4 ib.19,sheria ya 1995 Na12 ib.10, sheria ya 2000 na 3 ib. 12 Kifungu 1 (b),kuondoa kigezo cha ulazima mgombea atokane na chama pekee bali kuwe na mgombea binafsi.
- Kuhuisha mchakato wa upatikanaji wa balaza la vijana
- Kutengeneza mifumo rafiki kwa vijana wajasirimali kwa kutoa kipindi cha ukuaji wa miaka miwili, kuwe na lesini ya biashaya A kwa vijana wanaoanza biashara na B wazoefu baada ya miaka miwili kuanza kuingia kwenye mifumo ya kodi.
- Kuboresha mifumo ya kuwasaidia vijana ikiwemo (4-4-2) na ofisi ya waziri mkuu si kutoa mikopo tu bali elimu ya uendeshaji biashara na usimamzi wa fedha.
- Kutengeneza sera mpya kwani sera ya 2007 haiendani na wakati uliopo.
- Maboresho ya sera shindani ya elimu itakayo muandaa kijana katika maswala ya teknolojia na fani zingine za kitaaluma.
- Kutengeneza Inovation Hub and Talents Academy kila mkoa na taifa.
- Kujitolea sehemu mbalimbali ili kukuza uzoefu ambao ni kigezo kikubwa cha kupata ajira rasmi.
- Matumizi sahihi ya simu janja kujiingizia kipato mfano kupiga picha na kuuza kwenye wavuti mbalimbali.
- Matmizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa kutumia fursa za wafuasi kutangaza biashara za watu, kujifunza na kufuata majukwaa yanayotoa fursa mbalimbali.
- Kutumia vipaji walivyonavyo vizuri.
- Kuomba/kushiriki fursa mbalimbali za ndani za kusafiri katika majukwaa mbalimbali zinazolipiwa au kutolewa bure ili kujitangaza na kutenegeza mtandao wa watu wapya kuwasilisha mawazo yako.
- Kutumia fursa za rasilimali za asili Mito, bahari, maziwa, misitu, mbuga, sehemu za kihistoria.
- Kujifunza elimu ya usimazi wa fedha na kuweka akiba.
- Kuwekeza sehemu mbalimbali mfano Benki, UTT, Kununua Hisa.
- Kutumia fursa za mazingira yanayokuzunguka tafuta tatizo linalosumbua jamii yako ligeuze fursa kwa kuleta suluhu.
- Anza biashara mali kauli kwa watu wanaotoa vitu unaenda kuuza kisha mnagawana faida.
- Jifunze lugha kuu za mawasiliano duniani.
- Kuwa mwalimu wa kiswahili kwa wageni fungua accounti yuotube na mitandao ya kijamii.

Upvote
1