blackstarline
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 3,278
- 7,966
- Thread starter
- #301
Pamoja sana mkuu, karibu kwenye kitu chao kingine Hadithi ya umslopagaas - JamiiForums
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pamoja sana mkuu, karibu kwenye kitu chao kingine Hadithi ya umslopagaas - JamiiForums
Aiseee" finally "nimeimaliza"... bonge si la TheorySiku ile usiku Bwana George alitusimulia habari za safari yake. Kwa uchache ilikuwa hivi: miaka miwili nyuma alitoka mji wa Sitanda kujaribu kufika milima ya Sulemani.
Ile barua niliyompa Jim hakuipata, wala hakupata habari zake mpaka leo hivi. Lakini alisikia habari kwa wenyeji wengine.
Hakujaribu kufika kwenye maziwa ya Sheba bali alifuata njia ile nyingine tuliyorudia sisi, yaani njia iliyo bora kuliko ile iliyoandikwa katika ramani ya mzee Silvestra.
Yeye na Jim walipata taabu nyingi katika jangwa lile, lakini kwa bahati walifika hapa pahali penye majani na maji, ndipo Bwana George alipopatikana na ajali. Siku moja alikuwa kakaa kando ya mto na Jim alipanda juu kujaribu kutafuta asali.
Alipokuwa akifanya hivi, jiwe kubwa lililegea likaporomoka likamwangukia likamvunja mguu vibaya sana.
Basi tokea siku ile hakuweza kwenda vizuri, ikawa hawezi kwenda mbele wala kurudi nyuma, akaazimia kukaa pale pale.
Waliweza kupata chakula cha kutosha, maana walikuwa na risasi nyingi na wanyama huja penye majani na maji yale usiku usiku kila siku. Basi huwapiga wanyama, nakula nyama, na ngozi walizitengeneza ziwe nguo zao.
Basi Bwana George akamaliza kusimulia hadhithi yake, akasema, ‘Basi hapa tumekaa kwa muda wa karibu miaka miwili tukitumai kuwa labda wenyeji watapita na kutusaidia, lakini hawakuja.
Hivi jana usiku tulifanya shauri kuwa Jim aniache hapa naye ajaribu kufika mji wa Sitanda na kupata watu watusaidie. Tulikata shauri kuwa aondoke kesho, lakini hakika sikutumai kuwa ataweza kurudi tena.
Na sasa wewe, ambaye katika watu wote duniani sijakutumainia kabisa, wewe niliyekufikiri kuwa umenisahau na kukaa Uingereza kwa raha, umekuja bila ya kukutarajia.
Ni jambo la ajabu, tena bahati sana.’
Basi alipokwisha kusema, Bwana Henry akaanza kusimulia habari za mambo muhimu katika safari yetu, tukakaa sana usiku ule tukizungumza.
Nikamwonyesha almasi zile nilizopata, akasema, ‘Lo! Kweli mmepata kitu katika taabu zenu, si kama mimi nisiyestahili hata kuhesabiwa sasa.’
Bwana Henry akacheka, akasema, ‘Almasi hizi ni mali ya Quatermain na Good. Hivyo ndivyo tulivyopatana, ya kuwa watagawana mali yoyote tutakayo ipata.’
Basi, maneno yale yalinitia katika fikra, na nilipokwisha kumshauri Bwana Good, nilimwambia Bwana Henry kuwa sisi sote wawili tunataka hata na yeye ashirikiane nasi katika kugawanyana zile almasi, na kama yeye hakubali, basi sehemu yake tutampa ndugu yake aliyevumilia taabu nyingi kuliko sisi katika kujaribu kuzipata.
Mwisho akakubali namna tulivyopatana, lakini Bwana George hakupata habari mpaka baada ya siku nyingi. Basi, hapo nadhani nitamaliza hadithi yangu.
Safari yetu ya kuvuka jangwa mpaka mji wa Sitanda ilikuwa safari ya taabu nyingi, hasa kwa sababu ilitupasa kumsaidi sana Bwana George ambaye mguu wake wa kulia ulikuwa dhaifu sana, na ukamfanyia matata.
Lakini tulivuka, na kusimulia habari zake ingekuwa kukariri hadithi ile niliyokwisha isimulia.
Tulifika Sitanda, tukaona bunduki na vyombo vyetu vingine vipo salama, lakini nadhani Yule mzee aliyekuwa akivitunza hakupenda kutuona tena.
Baada ya miezi sita tulifika kwangu, katika mji wa Durban, na ndipo ninapokaa sasa na kuandika habari hizi. Na sasa nakupeni Kwaherini nyote mliosafiri pamoja nami katika safari hiyo ndefu na ya ajabu kuliko zote nilizosafiri.
MWISHO.
Asante mkuu.Aiseee" finally "nimeimaliza"... bonge si la Theory
Ahsante Mkuu
Asante mkuu. Avatar yako inanitisha balaa naona kama namjibu Kabila vile 😀😀
Hahahaha, usiogope Mkuu avatar tu ila namkubali sana Kabila Jr ,Mkuu shukrani sana,nimesoma yote kuanzia SAA 12 asubuhi mpk sasa, nasubiri ile nyingine sijui unatupia lini?Asante mkuu. Avatar yako inanitisha balaa naona kama namjibu Kabila vile [emoji3][emoji3]
Ila Mkuu ukifuatiliana wazungu walituzidi ujanja kitambo sanaNi simulizi nzuri ila pia inatuonesha ni kiasi ndovu walivyo dhulumiwa maisha yao maana wakati huyo walikuwa wanatembea kundi hadi ndovu thelathini lakini sasa hawazidi nusu yake
Mkuu ni kweli kabisa, na pia hii biashara ya pembe za ndovu ilianza kitambo sana wajanja walipiga hela sana.Ni simulizi nzuri ila pia inatuonesha ni kiasi ndovu walivyo dhulumiwa maisha yao maana wakati huyo walikuwa wanatembea kundi hadi ndovu thelathini lakini sasa hawazidi nusu yake
Dah! Yaani nadhani hata sasa bado tumelala bado, wazungu ni noma sana.Ila Mkuu ukifuatiliana wazungu walituzidi ujanja kitambo sana
Yaani waafrika tulikua na makosa mengi mno madogo madogo
Walituwahi Sana ,yaani makosa yetu Yale Yale ,siku zote ,nilikua nasoma hii hadithi halafu namtafakari mwandishi alivyokua anajiamini ,Asee sisi bado sanaDah! Yaani nadhani hata sasa bado tumelala bado, wazungu ni noma sana.
Kweli kabisa, siku yako ikifika mali haisaidii chochote.Kweli, mali ambayo watu wengi huitafuta maisha yao yote, mwisho wake haina thamani hata kidogo.
Ahsante kwa hii Hadithi, nimesoma jana yote mpaka mwisho, ngoja nihamie Katika Ile nyingineKweli kabisa, siku yako ikifika mali haisaidii chochote.
ngoja niende kwa Umslopagaz