Hadithi ya umslopagaas

SURA YA PILI


Baada ya muda, mambo yalipokuwa tayari, tulitoka Lamu, na baada ya kusafiri siku kumi na kukutana na mambo mengi, ambayo hapana haja kuyataja hapa tulifika mahali paitwapo Chara, kando ya mto Tana.

Katika mambo tuliyoyaona ni magofu ya miji ya zamani, nayo ni mengi katika pwani hizi. Kwa kadiri ya magofu ya misikiti na nyumba za mawe yaliyopo, miji hii ilikuwa na watu wengi sana zamani. Miji hiyo ni ya zamani sana.

Nimeambiwa ya kuwa ilikuwa maarufu hata katika wakati wa Agano la Kale, na watu waliokaa. Humo walikuwa wakifanya biashara na watu wa Uhindi na wa nchi nyinginezo.


Lakini utukufu wake umetoweka biashara ya watumwa imeumaliza na mahali pale waliposimama zamani matajiri wa kutoka nchi zilizostarabika wakati ule, wakishindania bei katika masoko yaliyojaa watu, sasa simba huja na kufanya baraza zao usiku, na badala ya mazungumzo ya watumwa na sauti za bidii za watu waliokuwa wakiwanadi, mlio wa simba hulialia katika magofu.


Huko Chara tuligombana sana na mnyapara wa wapagazi tuliowaajiri kufuatana nasi mpaka hapo, maana alitaka kututoza fedha nyingi kuliko ile tulivyopatana. Mwishowe alijaribu kututisha, ya kuwa atawapeleka Wajivuni kutushambulia.


Usiku ule yeye pamoja na wapagazi wote walitoroka pamoja na mizigo waliyoichukua. Kwa bahati hawakuziiba banduki wala risasi wala nguo zetu; si kwa sababu hawakuzitaka, ila kwa sababu zililindwa na wale askari watano wa Kikazi.


Basi, hapa tuliona dhahiri ya kuwa hatuwezi kuvumilia matata mengine ya wapagazi, na kwa kweli hatukubaki na vitu vingi vya kuchukuliwa. Lakini kama hatuna Wapagazi, tutaweza kuendelea namna gani?


Bwana Good ndiye aliyetoa shauri la kufaa. Alituonyesha mto, akasema, ‘’Hapa pana maji, na jana niliona wenyeji wengine katika mitumbwi wanawinda viboko.

Nadhani mahali anapokaa Bwana Mackenzie ni kando ya mto Tana. Je, kwa nini tusipate mitumbwi na kuiendesha mpaka kufika kwake?’’

Shauri hili zuri lilipokewa kwa furaha, na mara ile nilianza kufanya shauri la kununua mitumbwi inayofaa, kwa wenyeji wa karibu.

Baada ya kujaribu siku tatu niliweza kununua miwili mikubwa, kila mmoja uliweza kuchukua watu sita pamoja na mizigo mingine. Bei ya mitumbwi hiyo ilikuwa karibu kuimaliza bidhaa yetu yote, tena tukatoa na vitu vingine pia.

Basi, siku iliyofuata ile tuliyonunua mitumbwi, tulianza safari yetu tena. Katika mtumbwi wa kwanza mlikuwamo Bwana Good, Sir Henry na Wakazi watatu, katika ule wa pili, mimi, Umslopogaas na Wakazi wawili.

Kwa kuwa tulikuwa tukipanda mtoni, ilitupasa kuvuta kafi nne katika kila mtumbwi; ikawa kazi ngumu sana. Baada ya siku ya kwanza Bwana Good aliweza kusimamisha mlingoti katika kila mtumbwi, akatengeneza matanga, na kazi ilikuwa rahisi zaidi.


Lakini mkondo wa maji ulikuwa na nguvu, nasi hatukuweza kwenda zaidi ya maili ishirini kutwa.

Desturi yetu ilikuwa kuondoka asubuhi na mapema na kupiga kafi mpaka saa nne na nusu, ndipo jua linapokuwa kali zaidi. Basi, tulifunga mitumbwi kando ya mto tukala chakula kidogo kisha tulilala au kujizungumzisha mpaka saa tisa.

Saa tisa tulianza tena kuvuta kafi mpaka saa kumi na moja hivi, ndipo tulishuka kando ya mto kufanya kambi, na Bwana Good alianza kujenga boma la miiba na kukoka moto kwa msaada wa askari wetu.


Mimi pamoja na Sir Henry na Umslopogaas tulikwenda kuwinda tupate nyama kwa kitoweo chetu.

Kwa desturi hatukuona shida kupata mnyama, maana wanyama wa kila namna wapo kando ya mto Tana. Siku moja jioni Sir Henry alipiga twiga mchanga wa kike, na ubongo na mifupa yake ulikuwa mtamu sana.


Siku nyingine nilipiga kuro wawili, mmoja upande wa kushoto, na mmoja upande wa kuume, na siku moja Umslopogaas, ambaye kama Wazulu wote walivyo, hana shabaha, aliwahi kupiga pofu mnono kwa bunduki niliyomwazima.


Pengine tulibadili namna ya chakula chetu kwa kupiga kanga au ndege wengine waliokuwa wengi, kwa risasi, au kwa kuvua namna ya samaki wazuri waliokuwamo tele katika mto Tana.

Siku tatu baada ya kuondoka, jambo baya lilitokea.

Tulikuwa tunakaribia kando ya mto ili kufunga mitumbwi yetu na kupanga kambi tayari kwa usiku, tukaona mtu amesimama juu ya kilima kidogo mwendo wa yadi arobaini toka hapo tulipokuwapo, naye alikuwa anatuangalia sana. Kumtazama tu, mara nilitambua ya kuwa ni askari wa Kijivuni.


Na hata kama ningalikuwa na shaka kulitambua kabila lake ningalijuwa mara ile, maana Wakazi walinong’ona kwa hofu, ‘’Mjivuni!’’
 
Jinsi alivyotisha alipokuwa amesimama hivyo, amevaa mavazi yake ya vita! Nimezoea sana watu wa makabila mengi maisha yangu yote, lakini nadhani sijaona mmoja aliyekuwa wa kutisha zaidi ya huyo.


Kwanza alikuwa mrefu sana, nakisia alikuwa mrefu kama Umslopogaas, tena umbo lake zuri mno ila labda jembamba kidogo.

Lakini uso wake ulikuwa mwovu sana. Alikuwa ameshika mkuki mrefu kadiri ya futi tano na nusu katika mkono wake wa kuume, na bamba lake lilikuwa na urefu wa futi mbili na nusu, na uoana wake inchi tatu, na mwisho wa kipini chake ulikuwa na ncha ya chuma urefu wa futi moja au zaidi.


Kwa mkono wake wa kushoto alikuwa ameshika ngao ya ngozi ya nyati iliyotiwa alama alama.

Alikuwa amevaa vazi la manyoya ya mwewe begani, na kuzunguka shingo yake alivaa kipande kirefu cha kitambaa kadiri ya futi kumi na saba, na upana wake ulikuwa futi moja na nusu; kina mstari wa rangi katikati yake kwa marefu.


Ngozi ya mbuzi iliyokuwa mavazi yake ya siku za amani ilifungwa kiunoni kwa mkanda, na katika mkanda amechomeka sime upande wa kuume na rungu upande wa kushoto lakini labda vazi lililonivuta macho zaidi lilikuwa manyoya ya mbuni yaliyo fungwa kuuzunguka uso wake.

Duara hii ya manyoya ilifungwa chini ya kidevu chake, ikapita kichwani ikawa kama duara inayouzunguka uso wake mwovu.

Katika visigino vya miguu alikuwa amevaa manyoya meusi, na kwa juu ya machavu ya miguu amevaa vishungi vya manyoya ya mbega.

Basi, hayo ndiyo mavazi ya Yule Mjivuni, aliyesimama akituangalia tulipokuwa tukikaribia katika mitumbwi yetu, lakini kueleza tu hakufai, lazima mtu amwone ndio atambue namna alivyokuwa.

Kweli sikuweza kuona sehemu zote za mavazi yake kwa mara ile, ila nilipata nafasi nyingi baadaye kuziona.

Tulipokuwa tukisita na kufikiri shauri la kufanya, Yule Mjivuni alijinyosha wima kwa madaha, akautisa mkuki wake kutuelekea, kisha, aligeuka akateremka upande wa pili wa kilima.

Sir Henry aliita kutoka mtumbini mwake, akasema, ‘’Ati! Yule mnyapara amelishikilia neno lake na kutuletea Wajivuni.

Je, waonaje, itakuwa salama kuteremka kando ya mto?’’

Mimi sikufikiri ya kuwa itakuwa salama, lakini hata hivyo hatukuweza kupika katika mitumbwi yetu, wala hatukuwa na chakula kilichoweza kuliwa bila kupikwa, kwa hivi ilikuwa vigumu kujua shauri la kufanya.

Mwishowe, Umslopogaas alitoa shauri, yaani yeye aende kupeleleza, akatambaa katika kichaka kama nyoka, nasi tulikaa katikati ya mto tukingoja, Baada ya kupita nusu saa alirudi, akatuambia kuwa hakuona hata Mjivuni mmoja karibu.

Lakini aliona mahali walipokuwa wamefanya kambi karibuni, naye alifikiri ya kuwa waliondoka kadiri ya saa moja tu na Yule mtu tuliyemwona hakosi alipelekwa kupeleleza habari zetu.


Basi, hapo tulishuka, tukaweka mtu wa kushika zamu, tukaendelea kupika chakula na kukila. Kisha, tulifanyashauri juu ya hali yetu.

Kwetu yakini, iliwezekana kuwa Yule Mjivuni hana shughuli na sisi, ila labda ni mmoja wa kikosi cha Wajivuni waliokuwa wakienda kuwashambulia watu wa kabila jingine.

Rafiki yetu Yule Bwana Balozi wa Lamu alituambia kuwa vikosi vya namna hiyo vinatembea tembea.

Lakini tulipojikumbusha maneno ya Yule mnyapara, na kufikiri namna Yule Mjivuni alivyotutikisia mkuki wake, tuliona ya kuwa jambo hilo halikuendelea bali lilielekea ya kuwa wanatufuata wakingojea wakati unaofaa kutushambulia.

Basi, kama ni hivi, yapo mashauri mawili yanayowezekana, la kwanza tuendelee mbele, na la pili turudi nyuma.

Lile la pili lilikataliwa mara ile, maana ilikuwa dhahiri kwamba tukirudi tutapambana na hatari zilezile tutakazo pambana nazo kama tukiendelea, tena tulikuwa tumekaza nia kwenda mbele kwa vyovyote.

Lakini tuliona kuwa si salama kupiga kambi na kulala usingizi nchi kavu, kwa hivi tuliingia katika mitumbwi yetu, tukaipeleka katikati ya mto, ambayo haukuwa mpana sana, tukatia nanga, yaani mawe makubwa yaliyofungiwa kamba ya mnazi.

Hapa tulikuwa karibu kabisa kuliwa na mbu, na jambo hili pamoja na fikra za hali yetu ilinizuia nisilale usingizi kama wenzangu, ingawa wanashambuliwa na mbu.
 
Basi nilikaa nikivuta tumbako na kuwaza juu ya mambo mengi na hatari ipo ya kupatwa na homa kwa kulala mahali kama hapa, tena mguu wangu wa kuume umekufa ganzi kwa kukaa hali umekunjwa katika mtumbwi, lakini nilianza kuufurahia uzuri wa usiku.

Miali ya mbalamwezi ilichezacheza juu ya uso wa maji yanayopita kasi kuendea baharini, kama maisha ya wanadamu yapitavyo kuendea kaburini, mpaka yakang’aa kama utando mpana wa fedha, yaani mahali pa wazi pasipo fikiwa na vivuli vya miti.

Lakini karibu na kando ya mto palikuwa giza sana na upepo ulivuma katika matete, ukafanya sauti ya kuhuzunisha.


Upande wa kushoto, ng’ambo ya mto, palikuwapo namna ya ghuba ndogo yenye mchanga pasipo na miti, na hapo niliweza kuona vivuli vya wanyama wengi waliokuja kunywa maji, mpaka kwa ghafla nilisikia ngurumo ya kutisha sana, na mara ile wote wakatimka.

Baadaye kidogo, niliona umbo kubwa la simba akija kunywa maji baada ya kula kwake.

Halafu aliondoka, ndipo niliposikia kishindo katika matete kadiri ya yadi hamsini kutoka hapo tulipokuwapo, na baada ya dakika chache kitu kikubwa cheusi kiliibuka katika maji.

Kumbe, ni kichwa cha kiboko. Kikazama tena bila kufanya sauti, kikaibuka tena karibu, yaani kadiri ya yadi tano tu kutoka mahali tulipo.

Hapo niliona ya kuwa yupo karibu sana, na kwa hivi sikuona raha, na hasa kwa kuwa alionekana kama atakaye kujua mitumbwi yetu ni kitu gani.

Alikifunua kinywa chake kipana, labda apige miayo tu, nikayaona meno yake, nikafikiri jinsi anavyoweza kuusagilia mbali mtumbwi wetu mdogo kwa dhoruba moja.

Nilianza kufikiri labda itafaa nimpige risasi, lakini nilipofikiri zaidi, niliazimu kumwacha kama asipojaribu kuushambulia mtumbwi. Halafu alizama tena bila kufanya sauti hata kidogo, wala sikumwona tena.

Papo hapo nilitupa macho ng’ambo ya kuume, nikawa kama ninaweza kuona kitu cheusi kinapita katika mashina ya miti.

Macho yangu ni makali sana, nami nadhani niliona kitu kwa hakika, lakini kama ni ndege, au mnyama, au mtu sikuwa na hakika.

Lakini papo hapo wingu jeusi lilipita mbele ya mwezi, kwa hiyo sikukiona kilekitu tena. Tena, papo hapo nilisikia mlio kama wa bundi akilia mfulilizo, baadaye kukawa kimya kabisa isipokuwa sauti za kuchakacha katika miti na matete, wakati upepo ulipoyatikisa.

Lakini kwa jinsi isiyoelekezeka, sasa nilianza kushuku hatari za kuona hofu,hapakuwapo wala sababu ya dhahiri ya kunitia hofu hivyo zaidi ya zile zinazomzunguka msafiri yeyote katika nchi ya Afrika, lakini hata hivyo, bila shaka niliona hofu.

Lakini nilikaza nia nisishindwe na hofu, ingawa jasho baridi lilinitoka pajini mwa uso. Wala sikukubali kuwaamsha wenzangu.

Hali yangu ilizidi kuwa mbaya, na moyo wangu ulinipigapiga kama moyo wa mtu anayekaribia kufa. Na mishipa yangu ilinichezacheza kana kwamba kitisho kiovu kiko karibu. Watu waliopata kuota jinamizi, watafahamunamna hali yangu ilivyokuwa.
 
Lakini hata hivyo nilijikaza nikakaa kimya, nikageuza uso wangu tu kumtazama Umslopogaas na Wakazi wale wawili waliokuwa wamelala kando yake.

Nilisikia kishindo kidogo cha kiboko mbali, na Yule bundi alilia tena, na upepo ulianza kuvuma katika miti na kufanya sauti ya kuhuzunisha iliyopoozesha moyo. Baadaye nilipata kujua kuwa Wajivuni huitana kwa kuiga sauti ya bundi.

Juu niliona wingu jeusi, na chini maji meusi yalikuwa yakipita kasi, nikaona kama kwamba mimi na mauti tupo katika yake. Niliona ukiwa kabisa.


Mara damu yangu ilikuwa kama imevia katika mishipa yangu, na moyo wangu kusimama kimya. Je, ni ndoto tu ama ndio mwendo?

Niliyageuza macho yangu kuutazama mtumbwi wa pili uliokuwa ukielea kando yetu, nisiuone, ila badala yake niliona mkono mweusi mwembamba umeinuliwa juu ya ubavu mwa mtumbwi.

Hakika ni jinamizi! Lakini mara ile uso mwovu ulitokea juu kama kwamba umetoka majini, ndipo mtumbwi ulipoinama, kisu kikang’aa ghafla, na Mkazi mmoja aliyekuwa amelala kando yangu akapiga ukelele na kitu cha moto kilichuzurika usoni pangu.

Mara ile kuduwaa kwangu kukakoma, nikatambua kwamba si jinamizi, ila tumeshambuliwa na Wajivuni wanaogelea majini.

Nikashika silaha ya kwanza niliyoweza kuipata ikatokea kuwa ni shoka la vita la Umslopogaas, nikapiga kwa nguvu zangu zote pale nilipokuwa nimekiona kisu kinang’aa .
Pigo liliangukia juu ya mkono wa mtu likaugandamiza juu ya ubavu mnene wa mtumbwi, na kuukata kisiginoni.

Yule mtu asifanye sauti hata kidogo akatoweka kama kivuli, alikuja kama kivuli na akaondoka kama kivuli. Ameacha nyuma yake ule mkono wake wenye damu ungali umeshika sime ile iliyokuwa imechomwa katika moyo wa mtumishi wetu msikini.


Mara kulikuwa ghasia na fujo, nikadhani, sijui ni kweli au je, nikaona vichwa vyeusi vingine vikielea majini kuendea ng’ambo ya kuume, ambako mtumbwi wetu uliendea kasi kwa sababu kamba ile iliyokuwa na nanga ya jiwe imekatwa kwa kisu.


Mara nilipotambua hivyo, nilifahamu pia ya kuwa shauri lao ni kuikata kamba ili mtumbwi uchukuliwe na maji ili kuiendea ile ng’ambo ya kuume; na huko bila shaka Wajivuni wanangojea kutuchoma kwa mikuki yao.

Basi, nilishika kafi moja mwenyewe, nikamwambia Umslopogaas aishike nyingine, maana wale Wakazi walikuwa wameduwaa kwa hofu hata kushindwa kuhema, tukapiga kafi kwa nguvu kurejea tena katikati ya mto.

Wala hatukufanya hivyo kwa haraka zaidi kuliko ilivyopasa, maana katika dakika nyingine tungali kwamba na bila shaka ingalikuwa ndiyo mwisho wetu.

Mara tulipofika katikati ya mto tena, tulianza kupiga kafi kupaendea pale ulipokuwapo ule mtumbwi mwingine umetiwa nanga nayo ilikuwa kazi ngumu na hatari pia, kwa sababu hakuna la kutuongoza ila sauti ya Good, maana alipiga kelele mara kwa mara.

Mwishowe tuliufikia mtumbwi, tukashukuru tulipoona ya kuwa hawakushambuliwa.

Haikosi ule mkono ulioikata kamba ya mtumbwi wetu ungaliikata yao, na Yule mtu asingalivutwa na tamaa ya kuua na jambo hilo, ingawa lilitupotezea maisha ya mtu mmoja na Yule Mjivuni mkono wake, lakini pia lilituokoa sote wengine tusiangamizwe.

Kukosa kukiona kile kitisho kiovu kikitokea juu ya ubavu wa mtumbwi, kitisho ambacho sitakisahau mpaka siku ya kufa kwangu. Mtumbwi wetu ungalichukuliwa kando ya mto kabla sijatambua umepatwa na nini, na habari hizi hazingaliandikwa nami.
 
Wacha nianze kuirarua taratibu

Shukran mkuu blackstarline
 
Aisee, kumbe ma legend wote wapo ndani [emoji39] [emoji39]

Team imetimia
 
Mbona na hii inaonekana ni kali sana? Safi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…