Hadithi ya umslopagaas

Hasha, huyu kizee kichawi simkosi, Foulata pekee ndiye anayefanya moyo wangu kuwa mzito sana, umauti wake ulinitia ufa moyoni, ukaupasua katikati. [emoji29] [emoji29]
Hahaah pole sana
 
Reactions: Pep
Aisee, hii kitu ni murua sana
 
Daaah, hatari
 
Ahsante sana mkuu blackstarline
 
SURA YA TATU

Tulifunga mtumbwi wetu pamoja na mtumbwi ule mwingine kwa kipande cha kamba kilichobaki, tukakaa tukingojea mapambazuko, na kufurahi kwa vile tulivyookoka.


Baada ya kukesha sana, kukapambazuka, nami sijapata kupendezwa kuuona mwangaza kama nilivyopendezwa kuuona siku ile, ingawa uliangaza juu ya kitu cha kutisha ndani ya mtumbwi wangu.

Maana, pale chini katika mtumbwi Yule maskini askari alikuwa amelala na sime imesimama kifuani mwake, na ule mkono uliokatwa ungali umeishika sime.


Sikuweza kuvumilia kumtazama zaidi, basi, nililivuta ndani lile jiwe lililokuwa nanga yetu, nikamfungia Yule askari aliyeuawa, nikamtumbukiza majini, akazama mpaka chini.


Kisha, tulitoa mtu mmoja katika mtumbwi mwingine tukamweka katika mtumbwi wangu, tukaendelea tena katika safari yetu, wote tumeshikwa na majonzi, wala hatukuweza kuona raha kwa kufikiri juu ya mambo ya mbele yetu, ila tulitumaini kufika misioni kabla ya kuingia usiku.


Hapo mambo yalizidi kuwa mabaya, maana jioni ilipokaribia, ilianza kunyesha mvua tukalowa kabisa, tena ikawa lazima pengine kukumba maji katika mitumbwi, na kwa kuwa upepo ulitulizwa na mvua, matanga hayakufaa kitu, ikawa lazima tupige kafi kadiri tulivyoweza.


Saa tano tulishuka mahali pa wazi kando ya mto kwa upande wa kushoto, na kwa kuwa mvua ilipungua kidogo, tulivua samaki tukazibanika motoni. Hatukuthubutu kwenda kutafuta wanyama.

Saa nane tuliondoka tena, tukachukua akiba ya samaki wa kuchoma na baada ya kitambo ilianza kunyesha tena mvua nyingi kuliko kwanza.


Tena, tulianza kuona shida zaidi kwenda mbele mtoni kwa sababu ya miamba mingi, na mafungu ya mchanga, na nguvu ya mkondo wa maji ilizidi, basi, ilikuwa dhahiri ya kuwa hatutawahi kuifikia nyumba ya Bwana Mackenzie kabla usiku haujaingia na habari hizi zilizidi kutusumbua.


Ingawa tulivuta kafi kadiri tulivyoweza, lakini hata hivyo hatukuweza kwenda mbele zaidi ya maili moja kwa saa moja, na ilipofika saa kumi na moja jioni, tulikuwa tumechoka taabani, na kwa kadiri tulivyoweza kukisia, nyumba ya misioni ipo mbali mwendo wa maili kumi.


Basi, tulianza kutengeneza mambo kadiri tulivyoweza tayari kwa usiku.

Baada ya mambo yaliotokea jana, hatukuthubutu kufanya kambi nchi kavu, na hasa kwakuwa kingo za mto Tana zimefunikwa na vichaka vinene vya kutosha Wajivuni elfu tano kujificha humo wasionekane, na kwanza tulifikiri tutakuwa hatuna budi kukaa tena katika mitumbwi.

Lakini kwa bahati, tuliona kisiwa kidogo, kadiri ya upana na urefu wa yadi kumi na tano, katikati ya mto. Basi, tulipiga kafi mpaka kufikia, tukaiegesha mitumbwi yetu, tukashuka na kutengeneza mambo kadiri tulivyoweza.


Mvua ilizidi kunyesha, tukaona baridi hata ndani ya mifupa yetu, wala hatukuweza kukoka moto.

Lakini mvua ilitufariji kwa neno moja, yaani Wakazi walituambia kuwa Wajivuni hawata tushambulia wakati wa mvua kwa sababu inawasumbua sana. Tulikula kipande cha samaki kilicholowa maji, isipokuwa Umslopogaas, maana yeye kama Wazulu wote, hali samaki.

Ndipo ulipoanza usiku wa taabu kupita zote ninazozikumbuka, isipokuwa taabu ya usiku ule ambao sisi watu weupe watatu tulivumilia pamoja tulipokuwa karibu kuangamia kwa baridi na theluji juu ya Ziwa la Sheba katika safari yetu ya kuiendea nchi ya Wakukuana.

Usiku ulikuwa kama hauna mwisho, na mara mbili tatu nilifikiri labda askari wetu wawili watakufa kwa maji na baridi na taabu. Bila shaka wangalikufa kama tusingaliwapa divai mara kwa mara.


Niliweza kuona ya kuwa hata Yule mzee shupavu Umslopogaas naye pia anaona maumivu, ingawa alikaa kimya tu, wala si kama wale Wakazi waliolalamikia hali zao bila kunyamaza. Mambo yalizidi kuwa mabaya kwenye saa saba ya usiku tuliposikia tena mlio wa bundi.

Basi, tukajifanya tayari kujitetea kama tukishambuliwa, lakini nadhani tungalishambuliwa wakati huo, tungalishindwa upesi.

Lakini labda mlio ulikuwa wa bundi hasa, au labda Wajivuni nao waliona taabu hata hawana moyo kutushambulia. Kwa vyo vyote hatukuwaona kabisa.

Hatimaye kulipapazuka na ukungu ukatambaa juu ya uso wa maji, na kulipokuwa kweupe, kukatakata, na mvua iliacha kunyesha, ndipo jua tukufu lilipochomoza, tukajivuta miguu, tukaenda tukasimama katika joto la jua, tukashukuru.
 
Naweza kufahamu kwa nini watu wengine wasiostarabika huliabudu jua, na hasa kama hali ya maisha yao huwalazimisha pengine kuvumilia mvua na baridi kali.


Baada ya kupita nusu saa, tulikuwa tukiendelea tena vizuri kwa msaada wa upepo mzuri. Mioyo yetu ilichangamka kwa kuuona tena mwanga wa jua, tukawa tayari kuzicheka shida na hatari zilizotuelemea jana.


Basi, hivyo tuliendelea kwa furaha mpaka kadiri ya saa tano, na hapo tulipoanza kufikiri kushuka kama ilivyokuwa desturi yetu ili tujaribu kuwinda wanyama tupate kula, mara mto ulipinda, tukaona nyumba imara ya Kizungu iliyozungukwa na baraza imesimama vizuri juu ya mwinuko.

Nyumba ilikuwa imezungukwa na boma la mawe, na handaki nje ya boma.
Karibu na nyumba palikuwa na mti mrefu sana, namna ya msunobari.

Mimi nilikuwa wa kwanza kuiona ile nyumba, nami sikuweza kujizuia nisipige ukelele wa furaha, na wenzangu nao na watumishi wetu pia wakapiga ukelele kadhalika.


Sasa hatukuwa na nia ya kusimama tena. Tukasukuma mbele kwa nguvu, lakini ingawa nyumba ilionekana kama I karibu, ilikuwa mbali kwa kuufuata mwendo wa mto, wala hatukuifikia mpaka saa saba.

Ndipo tulipojiona chini ya mwinuko iliposimama ile nyumba.

Tuliisogeza mitumbwi, yetu mpaka kando ya mto, tukashuka, tukawa katika kuikweza nchi kavu ndipo tulipoona watu watatu waliovaa mavazi ya Kizungu wanatujia kwa haraka wakipita katikati ya miti.

Bwana Good aliwachungulia kwa rodi yake, akasema, ‘’Bwana mmoja, na Bibi mmoja na mtoto mwanamke mmoja, wanakuja kistaarabu karibu na bustani ya kistaarabu kutulaki katika mahali kama hapa kweli hili ni jambo la ajabu kupita yote!’’


Basi, walitukaribia. Yule Bwana Mckenzie alikuwa mtu mwembamba, mwenye mvi, na uso wake ulikuwa wa kupendeza, akasema, ‘’Mhali gani mabwana, natumaini hamjambo?

Watu wangu waliniambia tangu saa moja ya kuwa waliona mitumbwi miwili inakuja mtoni, basi, tumekuja kuwalaki.’’ Na Yule bibi, akasema, ‘’Tumefurahi sana kuonana tena na watu weupe.’’

Tukavua kofia zetu kuwaamkia, tukawajulisha tu nani. Kisha, Bwana Mackenzie akasema, tumefurahi sana kuwaona. Mwaka mzima umepita tangu alipofika hapa mtu mweupe wa mwisho aliyetujia.’’


Huku nyuma tulikuwa tukiupanda ule mwinuko ambao sehemu ya chini yake ni mashamba ya mahindi na maboga na viazi, na vyakula vinginevyo.

Wenyeji wengine, watu wa misioni walikuwa wamejenga nyumba zao katika mashamba hayo.

Katikati ya mashamba palikuwa na barabara, na kando yake ilikuwapo michungwa mingi iliyojaa machungwa.

Tokea hapo nimependa sana bustani, na nilipoiona ile ya Bwana Mackenzie nilifurahi sana, nikasema, ‘’Lo, bwana, tazama jinsi ilivyo nzuri bustani yako’’.

Akajibu, ‘’Kweli, ni bustani nzuri sana, wala si ajabu kwa sababu nimefanya kazi nyingi humo, lakini pamoja na hivyo tabia ya nchi hii ni nzuri, na miti huota vizuri sana.’’

Basi, tukaendelea, tukafika kwenye ile handaki ambayo upana wake ulikuwa futi kumi, imejaa maji, na ng’ambo yake palikuwa na boma la mawe urefu wa kwenda juu futi nane, lina vitundu huko na huko vya kupitishia bunduki.

Na juu yake pametapakaa mawe makali na vigae vilivyosakafiwa katika mgongo wa ukuta.

Bwana Mackenzieakalielekezea kidole chake, akasema, ‘’Hii ndiyo kazi yangu iliyo kubwa, au tuseme hii pamoja na kanisa lililojegwa nyuma ya nyumba.

Ilichukua mimi na wenyeji ishirini muda wa miaka miwili kuichimbua ile handaki, na kulijenga boma, lakini kabisa sikuweza kuona ni salama, mpaka kazi zilipokwisha.

Sasa ninaweza kujitetea juu ya watu wakali wote wa katika nchi ya Afrika, maana chemchem inayojaza handaki maji imo ndani ya boma juu ya mwinuko, nayo hububujika siku zote, nami kila mara ninayo akiba ya chakula nyumbani cha kutosha miezi minne.’’
 
Basi, tulivuka daraja dogo, tukapita katika mlango mwembamba katika ukuta wa boma tukaingia katika bustani nzuri sana.

Katikati ya kiwanja mbele ya nyumba, tuliuona ule mti mrefu, na Bwana Mackenzie alituambia kuwa ni mnara wake wa kuangalia nchi yote, kisha, akasema, ‘’Lakini hamkosi mnaona njaa, basi haya twendeni.’’

Tulipokwisha kula, tuliviwasha viko vyetu vya tumbako, na Sir Henry akasimulia habari za safari yetu, na mkarimu wetu alisikiliza kwa fadhaa.

Akasema, ‘’Ni dhahiri ya kuwa wale Wajivuni waovu wanawafuata, nami nashukuru sana kuwa mmefika nyumbani kwangu salama.

Nadhani hawatadhubutu kuwashambuli hapa. Lakini ni bahati mbaya, maana karibu watu wangu wote wamekwenda pwani kupeleka pembe za ndovu na vitu vingine.

Wako watu mia mbili katika msafara huo, na kwa hivi wamebaki watu ishirini tu wanaoweza kulilinda boma letu ikiwa watatushambulia.

Lakini hata hivyo, nitatoa amri kadha wa kadha ili tusije tukatokewa ghafla.’’ Akamwita mtu mmoja aliyekuwa amesimama nje katika bustani, akamwambia maneno kwa Kiswahili. Yule mtu alisikiliza, kisha, alipiga saluti akaondoka.

Bwana Mackenzie alipokaa tena, nilimwambia, ‘’Natumaini sana ya kuwa hatutawaletea misiba, basi ni afadhali twende mbele na kubahatisha ajali yetu, kuliko kuwaletea wale watu waovu hapa.’’

Akajibu, ‘’Hapana kabisa, hamwendi sasa. Wajivuni wakija, basi watakuja, lakini nadhani nitaweza kuwapokea kwa namna itakayofaa. Mimi siwezi kumwondoa mgeni aende zake hata kama Wajivuni wote wa duniani wakija.’’


Nikasema, ‘’Sasa nakumbuka, Bwana Balozi wa Lamu alituambia kuwa alipata barua kutoka kwako, ambayo kwayo ulimpa habari ya kwamba mtu mmoja alifika toka mbali akasema ameona watu weupe mbali sana ndani ya nchi. Je, unasadiki habari alizokuambia?


Nauliza kwa sababu mara mbili tatu katika, maisha yangu nimesikia tetesi ya habari hizo kwa wenyeji waliotoka kaskazini mbali sana, ya kuwa taifa la watu hao lipo.’’

Bwana Mackenzie asijibu kwanza, ila alitoka chumbani, kisha alirudi tena amechukua upanga wa namna.

Ulikuwa mrefu, na bamba lake ambalo lilikuwa nene na zito lilikuwa limetiwa temsi lote hata kufika karibu na makali yake, na kazi yake ilipambwa kwa dhahabu. Akasema, ‘’Je, umepata kuuona upanga kama huu?’’

Sote tuliutazama sana, tukavitikisa vichwa vyetu.
Akaendelea akasema, ‘’Nimeuleta kuwaonyesha kwa sababu Yule mtu aliyesema ameona watu weupe ndiye aliyeuleta pamoja naye tena, kwa sababu unafanya habari alizozisema kuwa kama kwamba ni kweli.

Kama asingaliuleta nisingalimsadiki. Tazameni; nitawaambieni habari zote kadiri ninavyozijua, lakini si nyingi.

Siku moja jioni nilikuwa nimekaa barazani, na maskini mtu aliyedhoofu sana alikuja akichechemea, akaketi mbele yangu.

Nikamuuliza ana habari gani, akaanza kuniarifu habari kama yeye ni mtu wa kabila linalokaa mbali sana kaskazini.

Na jinsi kabila lake lilivyoangamizwa na watu wa kabila jingine, na yeye pamoja na watu wengine wachache waliosalia, walifukuziwa kaskazini zaidi kupita ziwa liitwalo Laga.

Kutoka huko, alikwenda mpaka ziwa jingine lililoko juu ya mlima, akaliita ‘ziwa lisilo na mwisho kwa kwenda chini.’

Na huko mkewe na ndugu yake wakafa kwa ugonjwa wa kuambukiza labda ndui na kwa hivi watu wa huko walimfukuzia jangwani atoke katika miji yao.

Akatangatanga kupita juu ya milima muda wa siku kumi, kisha, akaingia katika gongo la mwitu wa miti yenye miiba.

Na siku moja akaonekana huko na watu weupe wengine waliokuwa wakiwinda, wakamchukua mahali ambapo watu wote ni weupe, wakaao katika nyumba za mawe.


Alikaa hapo muda wa juma moja amefungiwa katika nyumba, mpaka siku moja mtu mwenye ndevu nyeupe, aliyemtambua kuwa ni mganga, akaja kumtazama, kisha akaongozwa kupita katika mwitu wa miti yenye miiba mpaka jangwani, akapewa chakula na upanga huu, ndivyo alivyosema, akaachwa huru.’’

Sir Henry alikuwa akisikiliza sana habari hizi, akasema, ‘’Ndiyo, halafu alifanya nini?’’
Bwana Mackenzie akasema, ‘’Kadiri alivyosema, alipatikana na taabu na maumivu yasiyo na idadi, akaishi siku nyingi anakula mizizi na matunda ya porini, na vinyama alivyoweza kuvikamata na kuviua.

Mradi aliweza kuishi, na kwa mwendo wa Pole pole alisafiri akijia kusini mpaka akafika hapa.

Sikupata simulizi ya mambo yote ya safari yake, nilimwambia arudi kesho yake, nikamwamuru mmojawapo wa wanyapara amtunze usiku ule.

Yule mnyapara alimchukua, lakini Yule maskini alikuwa na upele mwingi hata mke wake mnyapara asikubali aingie ndani asije naye akapata upele pia. Basi alipewa blanketi akaambiwa alale nje.

Ikatokea ya kuwa wakati huo, simba mmoja alizoea kutembeatembea karibu, na kwa bahati mbaya alisikia harufu ya Yule msafiri maskini, akamrukia, akamuuma kichwa hata karibu kutoka kabisa.

Wale waliokuwamo nyumbani hawakuwa na habari, na huu ulikuwa ndio mwisho wake na wa hadithi yake juu ya watu wale weupe na **** habari hizo ni kweli ama si kweli, siwezi kuwaambia.

Je, wewe Bwana Quatermain waonaje?’’

Nilitikisa kichwa changu, nikajibu, ‘’Mimi sijui.

Yapo mambo mengi ya ajabu yaliyofichika katikati ya kochi hii kubwa, nami sipendi kusema kuwa ni kweli, Ama si kweli.

Lakini liwalo lolote na liwe, tumekaza nia kujaribu kuvumbua habari,. Tumenuia kusafiri mpaka Lekakisera, na kutoka huko tutaenda kule kwenye Ziwa Lagana kama wako watu weupe wanaokaa kupita hapo, basi tutajaribu tuwezavyo kuwagundua.’’

Bwana Mackenzie akasema, ‘’Ninyi watu ni jasiri sana.’’ Akacheka kidogo, tukaziacha habari zile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…