Hadithi ya Wafungwa kwenye Pango (Fumbo la Maisha)

Apollo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2011
Posts
4,920
Reaction score
3,240
Hii ni hadithi ambayo ilikuwa ni fumbo ambalo mpaka leo hii Plato hatasahauliwa kwa kuweza kutumia ufahamu wake kuelezea uhalisia wa maisha na ufahamu wa mwanadamu ulivyo kwa ujumla. Ni mfano ambao kila mtu ameachiwa tafsiri yake ni kila mtu atauelewa kutokana na mwanga alioweza kuuona maishani wake.

Miaka za zamani kulikwepo na mwanafalsafa mmoja aliyekuwa anaitwa Plato katika tamaduni za wagiriki. Naamini wengi wanamfahamu Plato kama mojawapo kati ya wanafalsafa wakubwa walioweza kufundisha mengi Ugiriki na maisha yake kuheshimiwa kutokana na utambuzi wake juu ya falsafa na maisha kwa ujumla.

Plato

Plato Aliwahi kuhadithia hadithi moja. Hadithi hiyo aliielezea kwa kufafanua maisha kwa ujumla yapoje na mwanadamu na ulimwengu.

"Fikiria pango ambalo ndani yake kuna watu wamefungwa tangu walipozaliwa na maisha yao wamefungwa ndani ya pango hilo.

Wafungwa walio ndani ya pango na hawawezi kutoka wala kugeuka nyuma

Na katika kufungwa kwao wamelazimishwa kutazama ukuta uliokuwa mbele yao. Watu hao wamefungwa shingoni na nyuma na wala hawawezi kugeuka nyuma kutazama kilichopo nyuma lakini maisha yao wamekuwa wakitazama mbele tu na wameshazoea na hawafahamu tena kama kuna kugeuka nyuma.

Wafungwa waliofungwa na kuutazama ukuta maisha yao yote wakiishi kuutazama ukuta, mwanga hafifu wa moto uliopo nyuma yao, na wakisikia sauti za wapita njia bila wao kuwatambua wala kutambuliwa.

Nyuma yao kuna moto unawaka. Na katikati ya moto ule unaowaka muda wote na pango wafungwa walipo kuna barabara inayopita kwa juu. Na fikiria kila siku kuna watu mbalimbali wanaopita kwani barabara ile ilikuwa inakwenda sokoni. Wanapita watu wa aina mbalimbali, mizigo na wanyama au mifugo. Vivuli vyao vinaonekana kwenye ukuta ambao wale wafungwa wanautazama muda wote na kutengeneza aina mbalimbali za vivuli vinavyopita na vinaonekana ni vikubwa na wao hawafahamu chochote kuhusu kilichopo nyuma yao na moto ule una mwanga hafifu unaotengeneza vivuli vya vitu na watu wanaopita kwenye barabara iliyopo katikati ya mwanga wa moto na kuelekea kwenye pango la wafungwa.

Barabara ya kwenda sokoni iliyopo nyuma yao ambayo wapita njia wanapita bila kujua kuwa kuna wafungwa chini. Wapita njia hao vivuli vyao na vya wanyama na mizigo yao huonekana kwenye ukuta mbele ya wafungwa na sauti zao na zikisisika na wafungwa bila kufahamu zimetoka wapi.

Fikiria maisha yao yote wao wanaona hicho ni kitu cha kawaida na hiyo ndio dunia yao. Maisha yao yote wanazaliwa wapo kwenye pango na mpaka wanakufa wao wanatazama projection ile tu na hawajui lolote mpaka wanamaliza maisha yao Vizazi na vizazi zinapita na kuona hiyo ni kawaida. Vivuli, sauti za wapita njia, sauti ya moto unawaka lakini hawajui vinapotoka bali hujua vile vivuli ndio chanzo.

Sasa fikiria endapo mfungwa mmoja akatolewa kwenye pango, anapowekwa nje ambapo kuna mwanga wa jua na yeye hajazoea ni lazima ataumia sana na itamchukua muda kuuzoea kwani maisha yake yote na vizazi vyake hakuwahi kuhimili mwanga kama huo. Na akiweza kuona atashangaa sana. Atagundua kuwa alikuwa hafahamu chochote na hakutegemea kufahamu hayo.

Mfungwa aliyeishi maisha yake yote kufungwa kwenye pango na kutazama ukuta tu akifanikiwa kuuona ulimwengu na maisha mengine ambayo hakuwahi kuyaona maishani mwake.

Fikiria mfungwa yule aliyefunguliwa akaamua kurudi kuwajulisha wenzie kuwa kuna dunia tofauti na hiyo, endapo akirudi kwa pale barabarani kwa juu na kuwaambia kuwa "Jamani geukeni" wenziye hawatamuelewa. Watabaki kushangaa kuwa wanasikia sauti lakini hawajui imetoka wapi kwani wanatazama mbele na pia watabakia kuona kivuli cha lijitu au kitu kikubwa kipo kwenye ukuta wanaoutazama na hawatafahamu wanaambiwa nini na nani.

Sauti yake itakuwa kama makelele, kivuli chake kitakuwa kama kinawakera muonekano wake au kitakuwa kinawachanganya kufahamu ni jitu gani hilo limetengeneza kivuli kwani hawawezi kugeuka nyuma wala hawafahamu kuna kugeuka nyuma.

Kivuli cha yule mfungwa aliyeweza kuona maisha mengine na sasa amekuja kuwaita wenziye lakini hawezi kuingia ndani bali amekaa naye kwenye barabara ya nyuma ya wafungwa na kivuli chake kuonekana mbele ya wafungwa wanaoishi kwenye pango na sauti yake kuwashangaza wenziye. Wenziye wanashindwa kufahamu mwenzao anasema nini na wanamtafsiri katika uelewa wao wa maisha yao na picha waonazo kwenye ukuta ndani ya pango

Na pia endapo akipewa nafasi hata kushuka kwenye pango chini na kuongea na watamuona kama amechanganyikiwa kwa ambayo atakuwa anawaeleza kwani wao hawakutegemea kabisa. Pia itawachukua muda na wao kuzoea mwanga wa nje kwani walizoea giza. Na inaweza kupelekea hata wakamuona yeye ni tofauti na wao na kumshangaa au kumtukuza.

MAANA.
Mpaka leo limebaki kuwa ni fumbo japokuwa wengi wamekuwa wakijaribu kutafsiri Plato alikuwa anamaanisha nini alipokuwa akielezea uhalisia wa mwanadamu. Fumbo hilo kila mmoja anaweza kulifikiria kivyake na kujitahidi kujitoa katika pango na kuweza kujitambua zaidi. Nimependa kushare hadithi hii kwani mara ya kwanza mimi kusoma hadithi hii ilinigusa sana na nikahisi inaweza ikawagusa wengine kivingine au kama nilivyoguswa nayo.

ASANTENI

VIDEO YAKE KWA WATAKAOPENDA KUONA PICHA HALISI YA HADITHI TAZAMA VIDEO HII.
 
Last edited by a moderator:
hii ina maanisha hata sie hapa dunian tumefungwa sio?

mm naona kama tumefungwa karibu kwenye kila jambo hapa ulimwenguni
ndio maana hata Sir Isaac newton alishawahi kusema
"".WHAT WE KNOW IS ONLY A DROP OF WATER AND WHAT WE DON'T IS AN OCEAN""

karibu utuelezee kwa mapana mkuu Apollo jinsi ww ulivyo itafasiri hiyo hadithi

.made in mby city.
 
Last edited by a moderator:
Hii hadithi imetiwa chumvi mno yani umeondoa maana yake kabisa .kunavipengele muhimu hujavitaja ambavyo ndo nilikuwa vinabeba ujumbe wa hadithi hii

asante mkuu gota07 kwa kuja na kuona mapungufu tajwa hapo juu
tunahitaji mchango wako hapa jukwaani wa hadithi hii
pale penye mapungufu ongezea-ongezea nyama ili twende sawa pamoja
karibu mkuu.........

Nashukuru sana.

Hii hadithi sio hadithi tu, Ni kama fumbo. Fumbo hilo limeelezea kila aina ya watu na ufahamu wao. Kila group au aina za reality zimeelezewa.

Kuna waliochained kwenye illusion (wafungwa), kuna wanaowatengenezea watu illusion za vivuli bila wao kujua (wapita njia), Kuna maana ya moto uliotengeneza vivuli, kuna maana ya Jua (Mwanga na Reality ya nje), Kuna maana ya Pango, na kuna maana ya Mfungwa anayebahatika kuuona mwanga na kujitahidi kuwaelewesha wenziye lakini hawamuelewi na wanamtafsiri kivingine. N.k, Yaani kila reality imepewa mfano wake.

Maana inabaki kwa muelewa binafsi na jinsi alivyoweza kugeuza shingo katika maisha yake na kutazama nyuma, taaratibu anaanza kutambua kuwa kumbe anachoona ni matokeo ya kunachopitapita nyuma yake, anatazama nyuma zaidi anaanza kutambua kuwa kuna mwanga nyuma yake na akitoka nje ya pango na kuona taaratibu kuweza kuhimili mwanga wa nje na kutambua kuwa vivuli vina picha halisi na picha halisi ikipigwa mwanga hutengeneza muonekano wa real object (REALITY) na kivuli cha object (ILLUSION).

ITAFUTENI KWELI, NA KWELI ITAWAWEKA HURU.

"I stood in the midst of the world, and incarnate I appeared to
them. I found them all drunk, I found none among them athirst. And my soul was grieved for the sons of men, for they are blind in their hearts and do not see that empty they have come into the world and that empty they are destined to come forth again from the world. However, now they are drunk--when they have shaken off their wine, then shall they rethink."

Jesus (The Gospel of Thomas)

Hii hadithi imetiwa chumvi mno yani umeondoa maana yake kabisa .kunavipengele muhimu hujavitaja ambavyo ndo nilikuwa vinabeba ujumbe wa hadithi hii

Nashukuru sana kwa mchango wako.

Lakini naamini hadithi hii inatofautiana katika schools na uhalisia katika kuielezea na hadithi ilivyo. Unaweza nawe ukatoa School of Thought yako kuhusu sehemu nyingine ya hadithi hii. Lakini katika source niliyoipitia kwa mara ya kwanza ilitumia uhalisia huu.
 
Ahsante kwa hadithi, sijawahi kuisoma lakini hapa nimeelewa kuwa kila mtu anakifungo chake ambacho amekizoea na anajiona yupo sawa na saa nyingine kuna mtu au watu walomfanya aingie kwenye hicho kifungo. Inaweza ikawa ni kazi anayofanya, biashara au mahusiano alokuwa nayo au pengine vitabia fulani. Sasa nadhani funzo ni kuwa tutoke nje ya boksi na tujaribu vitu vingine sehemu nyingine...tutapata mwanga zaidi.
 
Asante sana ndugu yangu. Nimejifunza kupitia mtazamo wako. Nashukuru sana.
 
fumbo lime eleweka mkuu,kazi ni kwetu kufanya uamuzi.

kama reality hatuta amua kujifunza kwa kimvuli cha kua tunajifunza ushetani,basi ila kama mtu alie ona mwanga wa nje umekamilisha kazi yako.Asante mkuu
 
Hii ni hadithi ambayo ilikuwa ni fumbo ambalo mpaka leo hii Plato hatasahauliwa kwa kuweza kutumia ufahamu wake kuelezea uhalisia wa maisha na ufahamu wa mwanadamu ulivyo kwa ujumla. Ni mfano ambao kila mtu ameachiwa tafsiri yake ni kila mtu atauelewa kutokana na mwanga alioweza kuuona maishani wake.

Miaka za zamani kulikwepo na mwanafalsafa mmoja aliyekuwa anaitwa Plato katika tamaduni za wagiriki. Naamini wengi wanamfahamu Plato kama mojawapo kati ya wanafalsafa wakubwa walioweza kufundisha mengi Ugiriki na maisha yake kuheshimiwa kutokana na utambuzi wake juu ya falsafa na maisha kwa ujumla.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Plato[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Plato Aliwahi kuhadithia hadithi moja. Hadithi hiyo aliielezea kwa kufafanua maisha kwa ujumla yapoje na mwanadamu na ulimwengu.

"Fikiria pango ambalo ndani yake kuna watu wamefungwa tangu walipozaliwa na maisha yao wamefungwa ndani ya pango hilo.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Wafungwa walio ndani ya pango na hawawezi kutoka wala kugeuka nyuma[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Na katika kufungwa kwao wamelazimishwa kutazama ukuta uliokuwa mbele yao. Watu hao wamefungwa shingoni na nyuma na wala hawawezi kugeuka nyuma kutazama kilichopo nyuma lakini maisha yao wamekuwa wakitazama mbele tu na wameshazoea na hawafahamu tena kama kuna kugeuka nyuma.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Wafungwa waliofungwa na kuutazama ukuta maisha yao yote wakiishi kuutazama ukuta, mwanga hafifu wa moto uliopo nyuma yao, na wakisikia sauti za wapita njia bila wao kuwatambua wala kutambuliwa.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Nyuma yao kuna moto unawaka. Na katikati ya moto ule unaowaka muda wote na pango wafungwa walipo kuna barabara inayopita kwa juu. Na fikiria kila siku kuna watu mbalimbali wanaopita kwani barabara ile ilikuwa inakwenda sokoni. Wanapita watu wa aina mbalimbali, mizigo na wanyama au mifugo. Vivuli vyao vinaonekana kwenye ukuta ambao wale wafungwa wanautazama muda wote na kutengeneza aina mbalimbali za vivuli vinavyopita na vinaonekana ni vikubwa na wao hawafahamu chochote kuhusu kilichopo nyuma yao na moto ule una mwanga hafifu unaotengeneza vivuli vya vitu na watu wanaopita kwenye barabara iliyopo katikati ya mwanga wa moto na kuelekea kwenye pango la wafungwa.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Barabara ya kwenda sokoni iliyopo nyuma yao ambayo wapita njia wanapita bila kujua kuwa kuna wafungwa chini. Wapita njia hao vivuli vyao na vya wanyama na mizigo yao huonekana kwenye ukuta mbele ya wafungwa na sauti zao na zikisisika na wafungwa bila kufahamu zimetoka wapi.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Fikiria maisha yao yote wao wanaona hicho ni kitu cha kawaida na hiyo ndio dunia yao. Maisha yao yote wanazaliwa wapo kwenye pango na mpaka wanakufa wao wanatazama projection ile tu na hawajui lolote mpaka wanamaliza maisha yao Vizazi na vizazi zinapita na kuona hiyo ni kawaida. Vivuli, sauti za wapita njia, sauti ya moto unawaka lakini hawajui vinapotoka bali hujua vile vivuli ndio chanzo.

Sasa fikiria endapo mfungwa mmoja akatolewa kwenye pango, anapowekwa nje ambapo kuna mwanga wa jua na yeye hajazoea ni lazima ataumia sana na itamchukua muda kuuzoea kwani maisha yake yote na vizazi vyake hakuwahi kuhimili mwanga kama huo. Na akiweza kuona atashangaa sana. Atagundua kuwa alikuwa hafahamu chochote na hakutegemea kufahamu hayo.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Mfungwa aliyeishi maisha yake yote kufungwa kwenye pango na kutazama ukuta tu akifanikiwa kuuona ulimwengu na maisha mengine ambayo hakuwahi kuyaona maishani mwake.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Fikiria mfungwa yule aliyefunguliwa akaamua kurudi kuwajulisha wenzie kuwa kuna dunia tofauti na hiyo, endapo akirudi kwa pale barabarani kwa juu na kuwaambia kuwa "Jamani geukeni" wenziye hawatamuelewa. Watabaki kushangaa kuwa wanasikia sauti lakini hawajui imetoka wapi kwani wanatazama mbele na pia watabakia kuona kivuli cha lijitu au kitu kikubwa kipo kwenye ukuta wanaoutazama na hawatafahamu wanaambiwa nini na nani.

Sauti yake itakuwa kama makelele, kivuli chake kitakuwa kama kinawakera muonekano wake au kitakuwa kinawachanganya kufahamu ni jitu gani hilo limetengeneza kivuli kwani hawawezi kugeuka nyuma wala hawafahamu kuna kugeuka nyuma.

[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Kivuli cha yule mfungwa aliyeweza kuona maisha mengine na sasa amekuja kuwaita wenziye lakini hawezi kuingia ndani bali amekaa naye kwenye barabara ya nyuma ya wafungwa na kivuli chake kuonekana mbele ya wafungwa wanaoishi kwenye pango na sauti yake kuwashangaza wenziye. Wenziye wanashindwa kufahamu mwenzao anasema nini na wanamtafsiri katika uelewa wao wa maisha yao na picha waonazo kwenye ukuta ndani ya pango[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Na pia endapo akipewa nafasi hata kushuka kwenye pango chini na kuongea na watamuona kama amechanganyikiwa kwa ambayo atakuwa anawaeleza kwani wao hawakutegemea kabisa. Pia itawachukua muda na wao kuzoea mwanga wa nje kwani walizoea giza. Na inaweza kupelekea hata wakamuona yeye ni tofauti na wao na kumshangaa au kumtukuza.

MAANA.
Mpaka leo limebaki kuwa ni fumbo japokuwa wengi wamekuwa wakijaribu kutafsiri Plato alikuwa anamaanisha nini alipokuwa akielezea uhalisia wa mwanadamu. Fumbo hilo kila mmoja anaweza kulifikiria kivyake na kujitahidi kujitoa katika pango na kuweza kujitambua zaidi. Nimependa kushare hadithi hii kwani mara ya kwanza mimi kusoma hadithi hii ilinigusa sana na nikahisi inaweza ikawagusa wengine kivingine au kama nilivyoguswa nayo.

ASANTENI

VIDEO YAKE KWA WATAKAOPENDA KUONA PICHA HALISI YA HADITHI TAZAMA VIDEO HII.

Myth of the cave ni philosophy tupu yenye ukweli unaenda na nyakati zote na usiochuja thanks Apollo kwa kazi nzuri
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom