Hadithi ya Wafungwa kwenye Pango (Fumbo la Maisha)

Hadithi ya Wafungwa kwenye Pango (Fumbo la Maisha)

Safi sana mleta mada,this is "ALLEGORY OF THE CAVE". Mkuu hili ni fumbo zuri sana mkuu,naweza nikasema fumbo hili limebeba uhalisia wa maisha ya binadamu.
 
Kifungo
FB_IMG_1532498225442.jpeg
 
Mwanadamu mimi haiwezekani kujua kila kitu.. kuna mengi siyajui.,, hivyo yafaa kujifunza kila siku..
 
Najaribu kulifikiria hili fumbo mara mbili mbili naona limekaa kiimani zaidi,lakini bado najiuliza hao jamaa walikuwa wanakula au hawali manake wamefungwa minyororo.
 
Hili si fumbo per se.

Ni analogy, ni falsafa.
Falsafa ya ufaham, falsafa ya mtazamo (relativistic perspective).
Kikubwa zaidi ana-demonstrate kwa jinsi gani pamoja na ujuzi wote tunaodhani tunao kuhusu 'reality' ni kwa namna gani tunaweza kuwa wrong kabisa au yaani tunajua kidogo mno.

Ni falsafa fikirishi ya kujiuliza "Tunajua Kweli Tunachojua?" Na " Tutajuaje zaidi kama hatujui zaidi?"

Point ya muhimu zaidi ni pale ambapo anakuja mtu aliyeona ambacho hujawahi ona wala kufikiria.
Hii ndo ilipelekea akina Gallileo kuuawa. Wao walikuwa ni mfano wa huyo mtu mmoja aliyekuwa pangoni akatolewa, akaona, halaf akarudi kuwaambia na wengine. Lakini wa pangoni walikuwa comfortable sana na vivuli vya pangoni kiasi kwamba walichukizwa na dhana ya tofauti kabisa ya ukweli.
Plato aliona mbali mno.
Na kitu kinachofurahisha sana ni kwamba hali hii ni sugu katika historia ya binadam mpaka sasa. Na mifano ni mingi mpaka leo.
 
Hii imekaa sana kiimani ni sawa sasa aje mtu akwambie imani yako ya dini fulani sio kweli na mungu hayupo, ukweli ni huu nnaokwambia mimi,hautamuelewa kabisa.
Wengi tunaishi katika dini za kukalilishwa tangia tukiwa wadogo mwislamu anajiona dini yake ndo halali na mkristo anajiona hivyohivyo wote wamefungwa minyororo wanaangalia mbele tu hawaruhusiw kuangalia nyuma ndomana humu yanapokuja mabandiko kama ya kufanya meditation wanakuja wafia dini kukataza watu wasijaribu utaskia ooh hayo mafundisho ya shetan kwa nini usione hiyo dini yako ndo ushetani unaona meditation ndo ushetani?
mi naona tusikae sehemu moja tujaribu kutoka na sehemu nyingine kuchungulia tuone pakoje kama pazuri au pabaya kuliko kuhukum tu bila ya ushahidi.
 
Hili si fumbo per say.

Ni analogy, ni falsafa.
Falsafa ya ufaham, falsafa ya mtazamo (relativistic perspective).
Kikubwa zaidi ana-demonstrate kwa jinsi gani pamoja na ujuzi wote tunaodhani tunao kuhusu 'reality' ni kwa namna gani tunaweza kuwa wrong kabisa au yaani tunajua kidogo mno.

Ni falsafa fikirishi ya kujiuliza "Tunajua Kweli Tunachojua?" Na " Tutajuaje zaidi kama hatujui zaidi?"

Point ya muhimu zaidi ni pale ambapo anakuja mtu aliyeona ambacho hujawahi ona wala kufikiria.
Hii ndo ilipelekea akina Gallileo kuuawa. Wao walikuwa ni mfano wa huyo mtu mmoja aliyekuwa pangoni akatolewa, akaona, halaf akarudi kuwaambia na wengine. Lakini wa pangoni walikuwa comfortable sana na vivuli vya pangoni kiasi kwamba walichukizwa na dhana ya tofauti kabisa ya ukweli.
Plato aliona mbali mno.
Na kitu kinachofurahisha sana ni kwamba hali hii ni sugu katika historia ya binadam mpaka sasa. Na mifano ni mingi mpaka leo.
Uchambuzi uliotukuka.... Asante sana[emoji112][emoji112][emoji106][emoji115][emoji123][emoji123][emoji123][emoji123]
 
Ahsante kwa hadithi, sijawahi kuisoma lakini hapa nimeelewa kuwa kila mtu anakifungo chake ambacho amekizoea na anajiona yupo sawa na saa nyingine kuna mtu au watu walomfanya aingie kwenye hicho kifungo. Inaweza ikawa ni kazi anayofanya, biashara au mahusiano alokuwa nayo au pengine vitabia fulani. Sasa nadhani funzo ni kuwa tutoke nje ya boksi na tujaribu vitu vingine sehemu nyingine...tutapata mwanga zaidi.
Asante haya maelezo yame nibariki
 
Ukweli kabsa, Kuna watu wanakesha mchana na usiku wanafanya juu chini kila wawezavyo kutengeneza fake reality.

Kila tunachokiona hakina uhalisia na maana kamili kama kinavyoonekana. Wengi tumeishia kusema ni Mpango wa Mungu yaani ni kana kwamba Tunasema hatuwezi kubadili chochote maana ni mpango wa Mungu.
Wengine huishia kusema Kazi za shetani bila kuchukua hatua na kufikiri nje ya box.

Tumepewa akili na ufahamu, tuna nafasi kubwa ya kureason why this? Sisi sio robot.

Kifungo cha fikra na mtazamo tulichofungwa kinafungulika ikiwa tutakubali kusikia na kuchagua kipi tuamini na kipi tusiamini, uhuru wa fikra tunao nini tufikiri na kuamini na nini tusikfikirie.

Dunia ipo mbali tunapaswa kufungua akili na kuwaza mbali zaidi na kuona uhalia wa kila kinachoonekana.

Tunapaswa kuishi miaka kumi mbele ya umri wetu kifikra.

Shule,hospital,religious,mashirika ya misaads, nk kuna haja ya kuvitazama kwa jicho la tatu.
Daah " umeongea fact tupu " asante sana
 
Back
Top Bottom