Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
fumbo lime eleweka mkuu,kazi ni kwetu kufanya uamuzi.
kama reality hatuta amua kujifunza kwa kimvuli cha kua tunajifunza ushetani,basi ila kama mtu alie ona mwanga wa nje umekamilisha kazi yako.Asante mkuu
Asante sana ndugu yangu.
Kuna watu hawawezi kutoka nje ya wanachofahamu (BOX). Ni watumwa na wamefungwa shingo hawawezi kugeuka NA hawatambui hilo kama kuna kugeuka kwani nao wanawafuata wenzao ambao ni wafungwa kama wao, bila kuuliza nao wanaona ni NORMAL.
Mungu hayupo kabisa kama watu wengi wanavyodhani. MUNGU NI ZAIDI YA WANAVYODHANI. Lakini wao wanampa personality ya kama naye ni mwanadamu kuwa ana HASIRA, WIVU, ADHABU, au personality ya uanadamu. NO.
Tutoke nje ya pango na kuuona MWANGA wa kweli. Badala ya kuzoea mwanga wa moto uliopo kwenye pango unaowatengenezea vivuli vya wapita njia waliopo nyuma yao watoke waone MWANGA wa nje mkuu na unaong'aa zaidi ya moto. Nao ni zaidi ya moto.
Hapo kuna level mbili
Level ya kawaida ni illusion ya kawaida ambayo hata kina Plato Na Aristotle waliweza kupita
Level ya pili ni kubwa sana
Kufikia formlessness ambapo utakuwa umeenda mbali kabisa
Utakuwa una uwezo wa kutoka Na kurudi nje ya pango Na kuamua ukae wapi Ingawa ukikaa pangoni itakuwa inakukera utatamani ukae nje milele
Hapo total illusion itakuwa imeisha
Hii level ya pili ni kitu kikubwa na kigumu kuweza kukifanya, level ya kwanza inaweza kuelezeka na kutafsirika kwa uhahisi zaidi
Hii level ya pili ni kitu kikubwa na kigumu kuweza kukifanya, level ya kwanza inaweza kuelezeka na kutafsirika kwa uhahisi zaidi
Kumbe walimu wapo wengi?
Ndugu mshana tugawie kidogo ulichonacho kichwani.
Hii hadithi imetiwa chumvi mno yani umeondoa maana yake kabisa .kunavipengele muhimu hujavitaja ambavyo ndo nilikuwa vinabeba ujumbe wa hadithi hii
Nataka nisitoke nje ya mstari wa mada husika kuhusu myth of the cave ya Plato kama ilivyoletwa na Apollo
Level ya kwanza ni level ya kawaida kabisa level ya kwenda shule kusoma na kuelimika kwamba ulikuwa hujui na sasa unajua na hicho unachokijua unakitumia kwa manufaa yako na ya Jamii nzima, ulikuwa kizani sasa umetoka uko nuruni! Ukisoma na ukashindwa kuelimika au ukashindwa kutumia elimu yako kwa manufaa ya wote, basi wewe bado ni mfungwa kwenye kifungo kilekile cha nira za ujinga kule shimoni cha kuona kivuli chako kama ni mtu halisi
Level ya pili ambayo naweza kuuita advanced level ni level ya juu zaidi na ngumu
Unapotoka kwenye shimo na kuja nje na kujua uhalisia wake (kusoma na kuelimika) unakuwa kwanza umejikomboa kutoka kifungo cha nira za ujinga, Unajitambua na unafanya yale yote mazuri kwa ajili ya ustawi wa Jamii
Sasa level hii ya pili ni kuondoa sasa makandokando yatokanayo na kupata elimu bila kuelimika au kupata maarifa/elimu isiyokusaidia kwa lolote, yaani umeshatoka shimoni uko nje mwanga umeuona lakini huna tofauti na wale waliobaki shimoni uko nje lakini fikra zako ni sawa na wale waliobaki shimoni ambao hawajawahi kutoka nje na kuona mwanga(kusoma bila kuelimika)
Hapa sasa mafundisho ya meditation na masomo ya utambuzi yanapokuja na hii ndio level ya pili............
Ni kweli mkuu,wewe usha fanya kazi yako kama mjumbe.kazi kwetu kwa wanao amini na
kutoka nje ni sawa ila ambao hawataki kutoka nje usha nawa kwao.Mimi ni mwanafunzi wako mzuri na kwa mada hizi nadhani very soon nitakua msaidizi wenu kupeleka hili gurudumu la elimu iliofichwa kwa wengi zaidi.
Narudia tena.ubarikiwe mkuu Appolo,na wengine wote wenye moyo kama wako wa kutoa elimu hiii.Asante
Napenda kushukuru sana ndugu yangu, nami nitajitahidi kushare kile ambacho ninakifahamu katika kuhakikisha wengi wanaamka.
Ubarikiwe sana.