Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MKABATA UJENZI WA BARABARA MTILI - IFWAGI (KM 14) WASAINIWA - JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI
Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mhe. Exaud Silaoneka Kigahe tarehe 20 Juni, 2023 ameshuhudia utiaji saini Mikataba ya Ujenzi wa Barabara Mtili - Ifwagi yenye urefu wa kilometa 14 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki ambaye amesema mradi wa uboreshaji wa barabara za vijijini kwa ushirikishaji na ufunguaji wa fursa za kijamii na kiuchumi (RISE) unaotekelezwa chini ya TARURA na utajenga barabara Km 535 katika mikoa 4 nchini.
Hafla ya utiaji saini Mikataba ya Ujenzi wa barabara za Mtili - Ifwagi (Km 14) na Wenda - Mgama (Km 19) mkoani Iringa kwa kiwango cha Lami imefanyika kwenye Manispaa ya Iringa tarehe 20. 06. 2023
Mradi wa RISE utajenga jumla ya Km 535 za barabara ya Lami kwenye Wilaya za Iringa, Mufindi, Kilolo, Handeni, Mbongwe na Ruangwa.
Mradi wa RISE umeanza Nov. 2021 na utakamilika June, 2027 ambapo utahusisha ujenzi wa barabara za Mikoa Km 135 zilizoko chini ya TANROAD, ujenzi wa barabara za Wilaya Km 400 za TARURA, Matengenezo ya Maeneo korofi km 4,500 -TARURA, Matengenezo ya kawaida ya Barabara kwa kutumia vikundi km 23,000- TARURA pia kupitia mradi huu ajira 35,000 zinatarajiwa kupatikana.
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Angellah J. Kairuki na Naibu Waziri Mhe. Exaud Kigahe wakishuhudia utiaji saini wa Mikataba ya ujenzi wa barabara za Mtili - Ifwagi KM 19 na Wenda - Mgama KM 14 mkoani Iringa chini ya mradi wa Uboreshaji wa Barabara za Vijijini kwa Ushirikishaji na ufunguaji wa Fursa za kijamii na kiuchumi (RISE) tarehe 20/06/2023 mkoani Iringa.
Picha na Matukio mbalimbali yakionyesha Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara akishuhudia na kuzungumza wakati wa utiaji saini Mikataba ya Ujenzi wa Barabara Mtili - Ifwagi yenye urefu wa kilometa 14 ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami.