Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Utoaji wa Tuzo ya Mwalimu Julius Nyerere ya Uandishi Bunifu 2024-2025 kwa nyanja ya Ushairi, Hadithi za Watoto, Riwaya, Tamthiliya zinatolewa leo, Aprili 13, 2025 kwenye Ukumbi wa Super Dom Masaki Dar rs Salaam na hii ni Kuelekea miaka 50 ya Taasisi ya Elimu Tanzania ( TET).
Mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, amemtuma Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega kumuwakilisha.
Ikumbukwe Aprili 7, 2025 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akizungumzia tuzo hizo, alisema:
"Tuzo ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu ni miongoni mwa njia bora za kuenzi fikra, falsafa na maono ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye aliweka msingi wa matumizi na ukuzaji wa lugha ya Kiswahili kama nyenzo ya elimu, umoja na maendeleo ya jamii ya Watanzania.
“Tuzo hii ni heshima kwa Mwalimu Nyerere lakini pia ni jukwaa mahsusi kwa waandishi chipukizi na wakongwe kuonyesha umahiri wao katika nyanja mbalimbali za uandishi kama vile riwaya, ushairi, hadithi za watoto na tamthiliya.”
========================
Orodha teule ya miswada 10 bora katika kila nyanja inayowania tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu itayofanyika Aprili 13,2025 Jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho kimefanyika Aprili 13, 2025 katika ukumbi wa The Super Dome uliopo Masaki Jijini Dar es Salaam, huku lengo likiwa ni kubadilishana uzoefu baina yao ili kuendelea kukuza sanaa ya uandishi wa vitabu kwa lugha ya kiswahili.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Charles Mahela amewasili katika ukumbi wa The Super Dome tayari kwa kushiriki katika tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu ambayo inafanyika leo Aprili 13, 2025.
Wageni mbalimbali katika hafla ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo limeandaliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania kwa kushirikiana na kamati ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya uandishi Bunifu chini ya uangalizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Mhadhiri, Mwandishi wa vitabu na Mchoraji Maarufu wa Chuo Kikuu cha Sultan Quaboos cha nchini Oman, Prof. Ibrahim Noor anasema “Nimerudi nyumbani kushuhudia matunda ya Watanzania kupitia kazi bunifu ya fasihi, lakini pia nawapongeza Watanzania wote na Wanafamilia wa baba wa Taifa kwa kutimiza kumbukizi ya miaka 102 kuzaliwa Mwalimu Julius Nyerere.”
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Tanzania, Dkt Anneth Komba akieleza maendeleo, mafanikio na mchango wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu ambayo hafla yake inafanyika ukumbi wa The Superdome.
UJUMBE WA MGENI RASMI
Baadhi ya nukuu za Waziri Ulega wakati akisoma hotuba kwa niaba ya Dkt. Phillip Mpango, amesema:
Kiswahili ni miongoni mwa Lugha Kuu 10 Duniani, Kiswahili kinafundishwa katika Vyuo vikuu vingi Duniani, kinatumika pia katika vyombo vya Habari mbalimbali vya kimataifa ikiwemo BBC, DW…
Hiyo ni dalili kuwa kizuri chajiuza, hivyo utoaji wa Tuzo za Kiswahili ni ishara ya kukuza na kuendeleza lugha hiyo.
Natoa wito kwa Watanzania kujitokeza kushiriki kwenye Tuzo hizi za Mwalimu Nyerere, nawapongeza Washindi wa Mwaka huu (2025) na wengine wote waliowasilisha miswada, wale ambao hawakupata nafasi ya kuwa miongoni mwa washindi wasikate tamaa.
Serikali yetu itaendelea kutoa fedha ili kuziwezesha Tuzo hizi kuendelea, natoa wito kwa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kuendeleza Tuzo hizi.
Washindi mbalimbali wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu 2025 kupitia vipengele vya Ushairi, Riwaya, Tamthilia na Vitabu vya Watoto wakipokea mfano wa hundi toka kwa mgeni rasmi wa hafla ya utoaji wa tuzo iliyofanyika katika ukumbi wa The Superdome, Masaki.
Pia soma ~ Waziri wa Elimu amtangaza Dkt. Mpango kuwa Mgeni Rasmi Tuzo za Taifa za Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu