Hahaha, eti Yamoto Band wanaimba matusi, Hivi mnamjua huyu?

Hahaha, eti Yamoto Band wanaimba matusi, Hivi mnamjua huyu?

kende

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2013
Posts
3,527
Reaction score
1,668
Atleast wao wanaimba kwa mafumbo sana kiasi kwamba watoto na vichwa maji kama mimi hatuwezi kuelewa kinachoongelewa, ila huyu brother wao Mh Temba alikuwaga noma tena naona sikuhizi kapunguza. Leo nilikuwa nimekaa sebuleni na mzee wangu, kwenye tv zikawa zinapigwa old schools, si kikagongwa kitu cha Temba ft Ray C kinaitwa 'Nipe mimi', ebwana nilivumilia weee but uzalendo ukanishinda, ilipoisha verse ya kwanza ikabidi nijifanye naenda msalani. Haya ni baadhi ya maneno ya kwenye wimbo huo;-

Nasikia utamu nasikia utamu mpaka kumoyo| Mdadi ushanipanda mi kachaa.....then Ray C anaitikia kwa mahaba (Ngojaaaaaaa), then Temba anaendelea;

Ngojangoja yaumiza matumbo, niipe niweeke ongeeza makeeeke nkishamaliza nicheeke
........,
Unaisikia inavyokuingia unafagilia unachukia unafagilia unachukiaaa?.....Ray C anajibu kwa mahaba ( ahkhaaaaah....)


#Dah , kungekuwa na tuzo za waimba mitusi Temba angekuwa anachukua kila mwaka


 
Last edited by a moderator:
mi sio msanii

Ukiitishwa mkutano au semina ya JF members halafu ukapewa nafasi ujitambulishe kwa jina Lako la JF utasimama na kusema unaitwa "KENDE". Hata kama unakataa kuwa wewe sio msanii hilo jina lako la JF linaashiria kuwa wewe ni msanii sanii fulani hivi.
 
Kuna jamaa anaitwa MSAGA SuMu
Ndoo kaanzisha kile kibwagizo cha MaMA aMiNaaaaaaa
Ndo kiboko yao kwa mitusi tena ile mizima mizima
 
Kuna jamaa anaitwa MSAGA SuMu
Ndoo kaanzisha kile kibwagizo cha MaMA aMiNaaaaaaa
Ndo kiboko yao kwa mitusi tena ile mizima mizima

Afadhali yeye ambaye nyimbo zake zinapigwa kitaa tu haziendi hewani
 
Nyingine ya temba anaimba "nazama natoa,nazama natoa,najua kabla sijamvua mwenyewe atachojoa"
temba kwa kuimba matusi,sio kiboko tena ila ni tembo.
Yamoto wakajifunze kwa temba,
 
Nyingine ya temba anaimba "nazama natoa,nazama natoa,najua kabla sijamvua mwenyewe atachojoa"
temba kwa kuimba matusi,sio kiboko tena ila ni tembo.
Yamoto wakajifunze kwa temba,

supu ya pweza na konyaaagi hiyo mechi yake.....
 
Temba asipotaja Pilipili au kachumbali kwenye wimbo basi huyo sio temba au inspector asipotaja misosi.
 
Back
Top Bottom