Hai: Aliyekuwa Diwani wa CHADEMA aachiwa huru kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi baada ya DNA kuonesha Mtoto aliyezaliwa sio wake

Hizi chuki na visasi vya kisiasa vinaondoa utu na ubinaadamu wetu kama watanzania, hapo lazima mwanaccm alikua injinia wa huo mchezo
 
Mungu ameamua kuliponya taifa kwa udhalimu huu yaani siasa hizihizi zinatesa watu hivi, tuome sana toba ukatili na kuoneana ni kitu kibaya sana , nakumbuka wale wanaume waliolawitiwa kwa nguvu huku wamelekezewa mitutu ya bunduki Zanzibar hizi zooote ni laana tombe sana toba
 
Inamaana mwanafunzi aliyebakwa hatapata haki yake?

Si mwanafunzi kabakwa?

Japo hajabakwa na mtajwa hapo awali ila yupo aliyembaka,atafutwa basi.

Kwa maelezo ya mbakwaji ni kuwa hajawahi shiriki ngono na mtu mwingine zaidi ya mtuhumiwa, sasa hapo unataka asakwe mtu hewa?!
 
Baada ya kufanya unyama huu MATAGA wakamwita shujaa wa Africa
 
Kuna mstari mwembamba Sana wa kumtofautisha idi amini dada na Magufuli.
 
Kwa maelezo ya huyo binti kwa mujibu wa taarifa hii ni kuwa aliieleza mahakama hajawahi shiriki ngono na mtu mwingine tofauti na mshitakiwa maishani mwake, kwa maelezo hayo logically ni kuwa kama DNA results zinakataa kuwa huyo si baba wa mtoto basi na kosa la ubakaji automatically linakufa.
 
Alibaka au alifanya tu kwa makubaliano ila ndio ikawa hivyo

Kubaka mtu yeyote au kufanya kwa makubaliano na underage, mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari ni kosa kwa mujibu wa sheria mkuu,
Hii ishu inafikirisha Sana inanikumbusha ishu ya akina babu seya inawezekana na wao walibambikiwa ile kesi yao ushahidi ukatengenezwa kutumia wale watoto Ila nayo ni ngumu Sana kuukubali kwa umriwa wale watoto.
Suala la kubambikiwa mimba /watoto kitaa lipo Sana.
Ila hizi roho za kuamua kuwasingizia watu kesi za uongo ni hatari tuombeane Mungu tu haya maisha sikuhizi yamekuwa hatarishi lolote linaweza kukutokea katika maisha ukabaki unashangaa.
 
Yes... Adai fidia itakayotoa fundisho kwa Mataga! Mwendazake angekua hai Mwamba Angeozea Kisongo!
Sasaiv haki zitapatikana, maana waliyekuwa wanamuogopa kama Mungu mpaka wananyima watu haki zao ili wamfurahishe yupo futi 6 chini kimyaaa
 
Unaweza ukambaka mtu na usimpe ujauzito mkuu.
Ila kwenye hii kesi inaonyesha mahakama waliamua kuweka burden of proof kwenye mimba./mtoto ( kupima dna akizaliwa) na sio kwenye kitendo Cha ubakaji kutokana na masuala ya muda
Inawezekana labda ni kweli huyo diwani alikuwa anatembea na huyo binti pamoja na watu wengine na huyo binti akapewa ujauzito na mtu mwingine sio diwani.
Maelezo ya binti kwamba hakuwahi kutembea na mtu mwingine zaidi ya diwani ninayatilia Shaka.
Mkemia mkuu wa serikali alihojiwaga akasema uhakika wa vipimo vya dna vya ofisi yake majibu yake ni sahihi kwa asilimia 99 na matokeo yao hayajawahi kutofautiana hata wakirudia.
 
Upinzani umepitia magumu sana kwenye utawala huu, hivi wale waliokua wanajiona miungu watu baada ya kufariki mtukufu wao watakua kwenye khali gani sasa🤔🤔
 
Katika ushahidi wa shahidi muhimu wa kesi hiyo ambaye ni mwanafunzi, alidai mahakamani hapo wakati akitoa ushahidi wake kwamba, hakuwahi kufanya ngono na mtu mwingine yoyote maishani mwake, tofauti na mshtakiwa huyo.
Kwahiyo walikuwa wakifanya ngono na si kubakana
 
Tanzania ilipita katika kipindi kibovu kuliko wakati wowote.
 
Kwa ushauri wangu, tuungane tuishauri serikali kuangalia upya sheria zetu za jinai ili watuhumiwa wanaobambikiwa makosa kwa sababu binafsi ikithibitika mahakamani bila mashaka yoyote kuwa mtuhumiwa kabambikiwa kosa x na y, basi sheria iseme kosa hilo linaenda (kama lilivyo) kwa mtu aliyebambikia (y) na ndiye atakayetumikia adhabu ya kosa hilo. Kwa maoni yangu, kufanya hivi kutaleta haki zaidi katika utoaji haki.
 
hiyo mimba ilitoka wapi sasa na wakati hajawahi kufanya mapenzi na mtu yoyote?
Je wewe unaamimi au una ushahidi wowote wa uhakika kuwa kweli huyo binti hajawahi kufanya mapenzi na mtu mwingine yeyote zaidi ya huyo mshtakiwa??!!
 
Sidhani kama Mwendazake atakaribia hata geti la mbinguni. Wale wote aliokuwa akiwatumia kutesa wapinzani kina Ole Sabaya na Gumbo wamebaki hawajui kesho yao maana ngao waliyoitegemea haipo tena.
 
Alibaka au alifanya tu kwa makubaliano ila ndio ikawa hivyo
Kasomi au Kajinga? Vile kabisa tuseme hujui maana ya kubaka inapohusu watoto? Mtu chini ya miaka 18 ni mtoto. Anawaza, kunena na kutenda kitoto. Hata kama amekutongoza yeye umebaka!
Kwa dhana hiyo miaka 30 inakuhusu. Yule jamaa aliyesema majaji wetu wanakopi na kupeisti naye alikuwa mbumbumbu wa hiyo dhana. Isipokuwa kiaina. Fataki wale miaka jela. Mabinti wasirudi shule. Hasomeshi wazazi bure. Fataki alibaka kwa dhana ya mtoto. Mzazi wa mimba za utotoni alitaka mwenyewe kwa ujinga wa Kasomi! Hapo chacha(sio mura!).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…