Hai: Aliyekuwa Diwani wa CHADEMA aachiwa huru kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi baada ya DNA kuonesha Mtoto aliyezaliwa sio wake

Hai: Aliyekuwa Diwani wa CHADEMA aachiwa huru kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi baada ya DNA kuonesha Mtoto aliyezaliwa sio wake

Mahakama ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, imemwachia huru diwani wa zamani wa Masama Mashariki (CHADEMA), John Munisi, ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Marire...
Hii wapeni kina zittokabwe waende wawaonyeshe WB na matajiri wao EU. Msichana kapata mimba jatangatanga kambambikizia mtu anafungwa maisha. Akushafungwa binti karudi Ndanda Girks kumalizia masomo yake baadaye ambambikizie mtu mwingine.
 
Haya yote ilikuwa ni kazi ya ile empire ya kishamba.
... Mwenyezi Mungu amlaani huko aliko; imeniuma sana hii kitu. Yaani nimeji-feel kama ni mimi; nimetetemeka kwa hasira basi tu. Dah; na huyo "mwanafunzi" abanwe aseme huo uchafu aliutoa wapi na mhusika alipwe fidia ya kutosha.
 
Mtoto angekufa je? Jamaa si angeozea uko? Au dna inapimwa hata kama mtu kaenda-zake?
 
Mahakama ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, imemwachia huru diwani wa zamani wa Masama Mashariki (CHADEMA), John Munisi, ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Marire.

Akisoma hukumu hiyo Leo, Hakimu Mkazi wa Wilaya hiyo, Jasmin Abdul amesema mahakama hiyo haijamtia hatiani mshtakiwa huyo katika makosa mawili yanayomkabili, kwa kuwa vipimo vya sampuli za vinasaba (DNA), kuonyesha mtoto aliyezaliwa, hakuwa mtoto wa mshtakiwa.

Aidha, hakimu huyo amesema kwa kuwa mtoto aliyezaliwa si wa mshtakiwa, mahakama hiyo haioni sababu ya kuamini kwamba mshtakiwa alimbaka mwanafunzi huyo, hivyo inamwachia huru.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Lebulu Mbise, kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti.

Anadaiwa alitenda kosa la kwanza katika Kijiji cha Ngira, Wilaya ya Hai, kwa kumbaka mwanafunzi huyo Aprili 4, mwaka 2019, kosa alilotenda akijua ni kinyume cha sheria.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo, kinyume na kifungu 130 (1) (2) na kifungu 131 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura 16 ya Sheria iliyofanyiwa Marejeo Mwaka 2000.

Aidha, ilidaiwa pia mahakamani hapo kwamba, mshtakiwa alitenda kosa la pili katika kijiji hicho hicho, kwa kumpa ujauzito mwanafunzi huyo Aprili, kinyume na Sheria ya Elimu, kifungu cha 60 (A) (2) na (3) iliyofanyiwa Marejeo Mwaka 2002.

Katika ushahidi wa shahidi muhimu wa kesi hiyo ambaye ni mwanafunzi, alidai mahakamani hapo wakati akitoa ushahidi wake kwamba, hakuwahi kufanya ngono na mtu mwingine yoyote maishani mwake, tofauti na mshtakiwa huyo.

Wakati mshtakiwa Munisi, akitoa utetezi wake akiongozwa na Wakili Elia Kiwia, alidai hakuwahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na mwanafunzi huyo, wala hakuwahi kufanya ngono naye.

Mshtakiwa huyo alijitetea kwamba alibambikiziwa kesi hiyo, baada ya kiongozi mmoja, kumlazimisha ajiunge na Chama Cha Mapinduzi (CCM) alipokataa, ndipo akambambikizia kesi hiyo namba 127 ya mwaka 2019.

Chanzo: IPP MEDIA
nani anahusika kumtesa mtu kwa makusudi? Mwanafunzi hana hatia kwakuidanganya mahakama? Ifike wakati wanaobambikia kesi watu wapate adhabu ile ile ambayo angepata mtuhumiwa.
 
Binti ana kesi ya kujibu. Baba tarajiwa imesthibika si yeye! Kaidanganya mahakama
Sio baba wa mtoto, lakini inawezekana ni kweli alibaka. Huo utetezi uliotumika kumtetea mtuhumiwa unaacha maswali mengi sana
 
Back
Top Bottom