Haijatokea duniani, Watanzania wafaulu kufuta upinzani

Haijatokea duniani, Watanzania wafaulu kufuta upinzani

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Nacheck hapa matokeo ya uchaguzi wa Tanzania, yaani upinzani umefutwa rasmi, mpaka sasa hawana mbunge hata mmoja aliyefaulu kwenye pembe zote za nchi aliyegombea kwa tiketi ya chama cha upinzani, ni mwendo wa CCM kote kote, kijani kwa kwenda mbele.

Kwa kifupi bunge litafurika wabunge wa mlengo wa serikali, yaani mfumo wa chama kimoja ila kwa njia ya debe, hamna wa kuhoji au kupinga chochote.

Hawakuachia hata wabunge kadhaa hivi wa kuzuga ili kidogo ionekane kwa namna fulani kulikua na uchaguzi, naona wapinzani wameanzisha nyuzi humu wakituhumu uchakachuaji, kuna mmoja kaweka mfano anasema jimbo lina 125,239 (registered voters) msimamizi anatangaza wamepiga kura 437,980 Uchaguzi 2020 - Mtu timamu hawezi kushangilia matokeo haya

Yote tisa ndio, uchaguzi umeisha na hayo ndio matokeo, hamna budi ila kuyakubali na kuendelea na maisha kama yalivyoamuliwa, CCM hoyeeee!!! Hehehehehe
 
Wabongo huu ni ujinga. Demokrasia imekufa rasmi Tanzania. Tanzania is going backwards. Watalia na kusaga meno siku za usoni. Ile heshima kidogo niliyokuwa nayo kwao imeisha. Hio nchi inaelekea kubaya.

Hakuna jinsi upinzani unaweza kukosa japo kiti kimoja bungeni. Hio haiwezekani hata kidogo. Majirani zetu mnaelekea kubaya. Tunawaonya mapema tu msije mkasema hamkuambiwa.
 
Democracy ni pamoja na kukubali matokeo #niyeye amewaponza wenzake kubeza hatua za maendeleo zilizofanywa na Magufuli
 
I support Magufuli but nachukia this issues. Inamaanisha serikali yetu haitakuwa na check and balance.

Shit. Si wangekuwa fair kwenye ubunge basi urais wafanye ujinga wao.
Sisi hapa Kenya kwenye viti vya ubunge wizi sio mwingi sana. Labda kwenye urais ndio kuna wizi wa kura.
 
Wabongo huu ni ujinga. Demokrasia imekufa rasmi Tanzania. Tanzania is going backwards. Watalia na kusaga meno siku za usoni. Ile heshima kidogo niliyokuwa nayo kwao imeisha. Hio nchi inaelekea kubaya. Hakuna jinsi upinzani unaweza kukosa japo kiti kimoja bungeni. Hio haiwezekani hata kidogo. Majirani zetu mnaelekea kubaya. Tunawaonya mapema tu msije mkasema hamkuambiwa.

Tuache na nchi yetu puleeaseee, sisi ndio tunaoamua jinsi ya kuishi na hivyo ndivyo tunavyotaka nchi yetu iwe, hatutaki Upinzani unaoturudisha nyuma, isitoshe kosa la Watanzania ni nini? Tumepima Chama kipi kinatufaa tumechagua, wewe ulitake na sisi tuanzishe BBI au, ...
 
Back
Top Bottom