Haijawaji kutokea mgao wa umeme mwaka mzima, awamu hii ni kiboko

Haijawaji kutokea mgao wa umeme mwaka mzima, awamu hii ni kiboko

Jamani jamani hamuogopi?
Mwisho wa siku huyo mtu ni taasisi yenye rasimali watu na fedha za kutosha kumfuatilia yeyote na kumtia adabu.

Ukweli ni kwamba Mh.Samia amekwama hapa kwenye suala la umeme na uwajibikaji watumishi ktk taasisi za umma.

Amefeli pakubwa mno kiasi kwamba 2025 Kama kura zitaheshimiwa anaweza asirudi kukalia kiti chake Ikulu.

Tume nzima ya uchaguzi ameteua yeye sasa kwanini asirudi ikulu?
 
Upigaji ni matokeo ya ujinga.

Yani unapiga wewe leo, hujui mjukuu wako ataishi kwenye nchi ya aina gani

Upigaji = Ubinafsi = Ujinga.

Watoto na wajukuu zao ndio hao wamewajaza kwenye uvccm na uchupukizi ili baadae na wao waendelee kula keki ya taifa
 
Hii nchi Sasa inapoelekea ni pabaya, Toka Awamu ya Mkapa, haijawaji kutokea Mgao mkali wa Umeme kama huu Awamu hii inayoitwa ya sita, Mgao ambao umedumu zaidi ya Mwaka Mmoja.

Hii Serikali Sasa ikibidi tu iwashe mitambo ya kifisadi ya IPTL Kwa maana mtu unawezaje kuvumilia Mgao wa zaidi ya Mwaka Mzima, mvua zinyeshe zisinyeshe Mgao upo pale pale.

Serikali itafute Namna hata kuleta Umeme waafuta watakaoweza wanunue watakaoshindwa wakae Giza.

Awamu hii ya SITA Mimi naiita Awamu ya Giza Totoro, Bodi imevunjwa mara tatu, wakurugenzi wamebadilishwa mara mbili, lakini Mgao ni ule ule
Tunaowapa Ruzuku ili watupiganie wao Wanajenga magorofa tu ya Mwenyekiti wao!!

Hakika awamu hii ya Sita Serikali imeshindwa na Upinzani umeshindwa Zaidi
 
Back
Top Bottom