The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,582
- 14,167
Moja kwa moja kwenye mada.
Na declare interest mapema,mimi Niko kwenye industry ya construction hususani civil works, na naishukiru Serikali walau kwa kuongeza bajeti ya Tarura kutoka Bil.272 kwa miaka 5 iliyopita hadi bil.802 mwaka huu 2022/23.
Pamoja na hayo Nimepitia bajeti za Ujenzi wa barabara za TANROADS toka 2016 hadi sasa,Nimebaini kwamba kumekuwa na ongezeko la bajeti ya Wizara ya ujenzi kwa ujumla wake lakini Cha kushangaza Serikali ilipunguza bajeti kwenye fungu la ujenzi wa barabara na kuongeza kwenye ununuzi wa ndege na ujenzi wa reli ya SGR.
Kwa Maoni yangu hii sio sawa kabisa Kwa sababu Barabara ndio mishipa ya Nchi na inachochea maendeleo ya haraka zaidi kuliko sekta zingine zote.
Ni jambo la kushangaza kwa Nchi kubwa kama Tanzania ku priotise ununuzi wa ndege na kujenga sgr ambazo zikikamilika haziwezi kuwagusa watu wengi na Wala hazitainua uchumi wa Nchi kwa haraka kama ilivyo kwa barabara.
Tabia hii ilianzishwa awamu ya Tano na Sasa bado inaendelezwa. Kwa mfano mwaka wa Fedha 2021/2022 barabara ilitengewa 1.58Til huku sekta ya Uchukuzi ikiwa 2.02 Til. na Mwaka huu wa 2022/2023 barabara imepungua hadi 1.43 Ti, huku Uchukuzi ikiongezwa hadi.2.32Ti.
Hii sio sawa ndio maana vilio vya wabunge vimekuwa vingi sana huko Bungeni na hawalilii ndege wala reli bali barabara.Huwa sielewi watu wa planning huko wizarani na wiazara ya fedha wanatumia geji gani za Kiuchumi kufanya haya maamuzi..
Saizi kilimo kimepewa pesa nyingi sasa sijui wakulima watasafirisha vipi hayo Mazao kufikia masoko ikiwa bajeti ya barabara inapunguzwa.
Mwisho hivi Kazi ya Bunge huwa ni kuweka mhuli wa kile serikali imeamua au ni ipi hasa? Badala ya kufanya marekebisho ya bajeti wao Kazi yao kupigia mhuri na kulia Lia,huu ni ujinga..
Hii sio sawa kabisa ikizingatiwa kwamba CAG amekuwa anasema ununuzi wa ndege inazidi kuleta hasara.