Hainan: Kijana Mwafrika anafurahia sera ya kupunguza na kusamehe ushuru ya bandari ya biashara huria ya Hainan

Hainan: Kijana Mwafrika anafurahia sera ya kupunguza na kusamehe ushuru ya bandari ya biashara huria ya Hainan

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111375664271.jpg


VCG111375664276.jpg


Kingsford na wenzake walikuwa wakijadili mpango wa biashara katika eneo la uvumbuzi na ujasiriamali wa mtandao wa internet la Fuxing City, huko Haikou, mji mkuu wa mkoa wa Hainan.

Kijana huyu kutoka Ghana alianzisha kampuni ya biashara ya kimataifa ya Kingsford ya Hainan mjini Haikou, na kuwa afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo, huku akifungua ofisi ya pili ya kampuni hiyo nchini Ghana. Kampuni hiyo inajishughulisha zaidi na biashara ya kuagiza na kuuza nje, ikilenga zaidi bidhaa kama vile siagi ya shea na sabuni nyeusi ya Afrika. Kampuni yake inafurahia sera ya kusamehe ushuru ya bandari ya biashara huria ya Hainan, na inaagiza malighafi kutoka Afrika na maeneo mengine, na kuzichakata kuwa bidhaa huko Hainan na baadaye kuziuza China na sehemu nyingine duniani, bila kutozwa ushuru wa forodha, kodi ya ongezeko la thamani forodhani na kodi ya matumizi.

Imefahamika kuwa eneo la uvumbuzi na ujasiriamali wa mtandao wa internet la Fuxing City, huko Haikou ni mojawapo ya maeneo ya uvumbuzi mkoani Hainan, na linavutia idadi kubwa ya wavumbuzi vijana na wenye vipaji kwenye mtandao ndani na nje ya China.
 
Back
Top Bottom