Kama tittle inavyojieleza Mwanaume kufanya yafuatayo haipendezi:-
1) Kuwa mbeya au kushiriki umbea kwa namna yoyote aidha kwa kukusudia au kwa kutokusudia.
2) Kutumia maneno haya:-
Shosti/Shostito, My, Mie, Mwaya, Nimekumisije, Msyuuuu...,My Maa, Ptuuuuu...., Utantaka,haalooo, jamaani n.k
3) Kutumia hela na Mwanamke yeyote au Mpenzi wako au Kumhonga kisha kulalamika mbele ya Wanaume wenzio. Sasa si ulienjoy naye,sisi tukusaidiaje? (Hapo Unajichoresha)
4) Kutamka neno "Nimeshindwa" au "Siwezi" mbele ya mwanamke...ni bora useme "Nitalishuhulikia" haijalishi unaweza au huwezi hilo suala.
5) Kulalamika kupita kiasi au kuweka kitu rohoni muda mrefu, (haipendezi pia kwa dume). Kama umekerwa Tunasemaga tu kavukavu.
6) Kuomba ushauri wa kitoto toto. Mfano,kitu kidogo unachoweza kushuhulikia ukiomba ushauri ni kujishusha na kujidharau.
7) Kuwa Mnafiki, mfano unajua kabisa chama flan kina unyonyaji na maovu na unashabikia kisa una maslahi bila kusimamia ukweli.
Ongeza nyingine...