Haitawezekana Kuifuta Historia ya Uhuru wa Tanganyika kwa Kupenyeza Historia Mbadala

Haitawezekana Kuifuta Historia ya Uhuru wa Tanganyika kwa Kupenyeza Historia Mbadala

  1. Kwa maelezo ya kina ya mgogoro wa ardhi ya Wameru angalia Kirilo Japhet na Earle Seaton, The Meru Land Case, Nairobi, 1966.
  2. Angalia Iliffe, A Modern History... op.cit. uk. 502 akinukuu barua kutoka kwa Abdul Sykes kwenda kwa Sablak 8 Desemba, 1952, vilevile ya Japhet kwa Abdul Sykes 26 Septemba, 1952. Nyaraka za Japhet TNA.
  3. Stakabadhi ya hundi ya posta kwenda Usa River toka TAA, maelezo yake hayasomeki wala muandiko wa Ally Sykes. Nyaraka za Sykes.
  4. Taarifa ya Jimbo la Ziwa kwa kifupi iliyotolewa na Bwana Abbas K, Sykes. Nyaraka za Sykes. Vilevile Japhet, op.cit. uk. 62.
  5. Tanganyika, Member of Political Association, Tanganyika Government Circular No.5 (1 Agosti, 1953), Dar es Salaam, 1953
  6. K. D. Kaunda kwa A. K. Sykes, 28 Desemba, 1953, Nyaraka za Sykes.
  7. Baada ya kuunda TANU Ally Sykes alimwandikia Bargil akimjulisha habari zile. Bargil alimwandikia Ally barua na kumwambia kuwa: ‘’Tunaingia muongo wa pili wa mapambano yetu ambayo kwa hakika tutatunzwa kwa mfanikio kamili’’. Ally Sykes kwa niaba ya TANU aliandikiana na Bargil wakibadilishana mawazo na habari kuhusu harakati za kudai uhuru kwa miaka mingi.
  8. Julius K. Nyerere, Rais wa Tanganyika African Association kwa Gavana Edward Twining, 10 Agosti, 1953. Nyaraka za Sykes.
  9. Barua ya Secretariat 16 797/1/343 ya Agosti, 1953. Nyaraka za Sykes.
  10. Joseph Kimalando kwa Hon. General Secretary, 9 Septemba, 1953. Government Circular on Membership of Political Associations. Maktaba ya CCM. File 168 Folio 2.
  11. Pacha anayo muhtasari ya ule mkutano mkuu wa Julai, 1954 lakini hakuwa na rasimu ya katiba ambayo haikuweza kupatikana Maktaba ya CCM Dodoma. Bukoba ilipokea rasimu hiyo, angalia barua ya M. Lugazia kwa katibu Tawi la Bukoba DC/ HQ/ LP/ 897 Mei, 1954. Folio 16 TANU 16 lakini rasimu ya katiba iliyotajwa humo haimo ndani ya barua hiyo.
  12. Tangazo lililodurufishwa lililotolewa kwa Waafrika wote, lisilokuwa na tarehe, lisilotiwa saini na bila nembo ya TAA. Nyaraka za Sykes. Ally Sykes anasema alisambaza yale makaratasi ili kuwapasha watu habari. Nyerere alipinga mbinu hizo kwa kuhofu serikali.
  13. Angalia Listowel op. cit. uk. 233. Vilevile vilevile ëUamuzi wa Busaraí, Idara ya Habari ya Chama kwa kushirikiana na Idara ya Elimu ya Siasa, uk.2.
  14. Hati ya uthibitisho pamoja na waraka wa pongezi. Nyaraka za Sykes.
  15. Darrel Bates, A Guest of Plumes, London, 1972, uk.. 243-4.
  16. M. Lugazia kwa katibu Tawi la Bukoba DC/HQ/BK/LP/897 May, 1954 (tarehe haikutolewa) TANU folio 16 Party Archives, Dodoma. Rasimu ya katiba iliyotajwa hapo imekosekana.
  17. Pratt, op. cit.
  18. Pratt, op. cit. uk. 30.
  19. Angalia mada ya Rajabu Diwani, ''TANU ilipambana na Misukosuko Mingi,'' UHURU 3 Julai, 1974.
  20. Kabla ya Daisy Sykes kuandika habari ya babu yake, Kleist Sykes mwaka 1968, wakati akiwa mwanafunzi wa historia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, na nyaraka za Kleist Sykes kupitiwa na mwalimu wake, John Iliffe, habari za African Association zilikuwa hazifahamiki vyema. Kimalando alikuwa mwanasiasa wa siku nyingi mwenye uzoefu na kwa kauli yake alidai kuwa alikuwa mmoja wa wanachama waasisi wa African Association katika mwaka 1929 ijapokuwa kumbukumbu za Sykes za wakati huo, zinampinga. Mtu mwingine anayesemekana kuwa miongoni mwa wanachama waasisi wa African Association lakini jina lake halimo ndani ya kumbukumbu za Sykes ni Sheikh Hussein Juma aliyekuja kuwa Makamu Rais wa United Tanganyika Party (UTP).
  21. Mwaka wa 1956 Kimalando alijiunga na United Tanganyika Party (UTP) kama katibu. Rais wa UTP huko Moshi alikuwa Mohamed Badi mmoja wa watu mashuhuri sana pale mjini. Badi alijulikana sana kwa jina lake la utani ‘’Kishikio.’’
  22. Zuberi M. M. Mtemvu kwa Ally Sykes, 15 Agosti, 1954. Nyaraka za Sykes.
 
You again. Mzee wangu kama ulishimdwa kuijenga legacy yako kwa nchi hii ujanani, huwezi tena kuijenga huku uzeeni. Tuliza akili na mwili ili Mnyaaz Mungu akujalie KIFO chema tuu
Tai...
Unadhani naandika kujijenga?
Hapana hili kwangu halijapata kuwa jambo lenye ukubwa.

Nimeona historia imeandikwa ina makosa nikaamua kusahihisha.

Kuwa hili jambo likaja kuwa kubwa ni utashi wake Allah.

Sikufanya hili kutafuta umaarufu.
 
Leo tena umeibula na Sykes!🤣🤣
Real Comrade...
John Iliffe alimwambia mwanafunzi wake Aisha "Daisy" Sykes, enzi za University of East Africa.

Ilikuwa mwaka wa 1968 John Iliffe anafanya utafiti kuandika historia ya Tanganyika.

"Daisy kila ninapopita nakuta jina la babu yako Kleist Sykes hebu andika Seminar Paper kuhusu huyu babu yako."

Mwaka wa 2008 nimepokea email kutoka Harvard kwa Prof. Emmanuel Akyampong niandike historia ya Kleist Sykes kwa ajili ya mradi wa Dictionary of African Biography (DAB) kamusi ambalo limechapwa na Oxford University Press, New York.

Sasa unafanyaje mtu?
 
Real Comrade...
John Iliffe alimwambia mwanafunzi wake Aisha "Daisy" Sykes, enzi za University of East Africa.

Ilikuwa mwaka wa 1968 John Iliffe anafanya utafiti kuandika historia ya Tanganyika.

"Daisy kila ninapopita nakuta jina la babu yako Kleist Sykes hebu andika Seminar Paper kuhusu huyu babu yako."

Mwaka wa 2008 nimepokea email kutoka Harvard kwa Prof. Emmanuel Akyampong niandike historia ya Kleist Sykes kwa ajili ya mradi wa Dictionary of African Biography (DAB) kamusi ambalo limechapwa na Oxford University Press, New York.

Sasa unafanyaje mtu?
Hongera kwa kazi yako nzuri na kupokea email toka kwa taasisi kubwa ya elimu kama Harvard.

Sincerely🙏
___________________________

Turudi hapa JF sasa.
Hapa tutakutwanga sana spana kwakua nyuma ya ukweli wa Sykes, unaviashiria vya radicalism.👌😂
 
Hongera kwa kazi yako nzuri na kupokea email toka kwa taasisi kubwa ya elimu kama Harvard.

Sincerely🙏
___________________________

Turudi hapa JF sasa.
Hapa tutakutwanga sana spana kwakua nyuma ya ukweli wa Sykes, unaviashiria vya radicalism.👌😂
RC,
Ndiyo unionavyo?
Si kitu.
 
Muda wa kuwasimulia wajukuu zako hadithi hizi, au huko misikitini wakupe madrasa ufundishe. Humu unaona kuna uelekeo wa kusikilizwa?
Bikra...
Unaniandikia kwa kejeli.
Nasikitika.

Unataja msikiti na madrasa kwa kejeli.

Hakika huu si uungwana.

Mimi naingia katika vyumba vya madarasa na kumbi za vyuo vikuu nasomesha.

Nasikilizwa.

Wewe hujafika ngazi hii lakini sithubutu kukudharau.
 
Bikra...
Unaniandikia kwa kejeli.
Nasikitika.

Unataja msikiti na madrasa kwa kejeli.

Hakika huu si uungwana.

Mimi naingia katika vyumba vya madarasa na kumbi za vyuo vikuu nasomesha.

Nasikilizwa.

Wewe hujafika ngazi hii lakini sithubutu kukudharau.

Kama unasikilizwa kweli tangu umeanza kuihubiri hiyo historia imebadilika?
 
Back
Top Bottom