Haiwezakani siye tusiwe na korona wakati Kenya wana visa zaidi ya 1600, jihadhari

Haiwezakani siye tusiwe na korona wakati Kenya wana visa zaidi ya 1600, jihadhari

Kwani Kenya ni Tanzania au Tanzania ni Kenya? Mbona Dar kuna Corona lakini kuna mikoa ya humu humu nchini haijapata maambukizi? Wewe vipi kwanini ulinganishe na Kenya? Mkiitwa wachawi mnakataa kama Kenya ni wajomba zako nenda kawasaidie kuuguza wagonjwa
 
Acha wapambane kivyao na sie tunapambana kivyetu, kwani serikali imesema Corona hakuna? Watu wengine jamani, watu hatufanani kila mtu Mungu kampangia fungu lake
 
Akajikoronize hukohuko!!
Kujiriwadha[emoji777]
Kujiliwaza[emoji818]
Mkuu mbona kama unawaonea wivu Kenya kwa idadi hiyo ya wagonjwa walio nayo?

Kwani nani kasema imeisha? Kama unaona Kenya wanafaidi corona hamia huko nawe ukaburudike.
 
Hivi wewe unawaamini kina Bashite na Stone? Jikinge wewe na familia yako korona ipo na inatafuna watu wewe ukitaka kujua kwamba ipo pitia page ya rais wa twita aka GOGOKI.
Hvi huyu Jamaa GOGOKI Yupo nchi gani mpaka anajiamini kiasi kile kinachonishangaza ni kwamba anaposti vitu vingi ambavyo hutegemei kuvipata kokote kule.
 
Kenya inaendelea kupima na kupambana na korona wakati siye tunajidanganya imekwisha.

Leo hii wamegundua visa 147, hii inaonyesha Korona bado ipo na inaongezeka badala ya kupungua.

Najua wanaopenda kusikia habari nzuri wakati wa majanga kujiriwadha, na kama wenye akili ya kutuliza wajinga kwa uongo wanavyotaka, watapinga hili vikali.

Wapya 147 wakutwa na corona Kenya akiwemo mtoto wa mwaka mmoja.
Kila mtu atabeba furushi lake. Tusipende kumdharau Mwenyezi Mungu na kufikiri science ina kila majibu kwenye hii dunia
 
sisi ni tanzania na wao ni kenya.sisi tunatumia maombi,nyungu,NIMR na dawa zingine za asili.
wakati kenya wanasubiri mzungu apate dawa mwakani
 
Tz Nina imani wengi tunayo tunatembea nayo ni vile hatupimwi...
Uzuri ama hii zaidi inaua wazee Na wagonjwa ..
 
Mbona we hujafa na mitaani hatuoni vifo wala ndugu,rafiki pia. Kufa wewe kwanza ndo tuamini kua ugonjwa upo na unawaweza wabongo
Una ndugu au rafiki Tanzania nzima? Sioni haja ya kuleta ubishi wa vijiwe vya kahawa. Wewe chukua tahadhali na sio lazima kila siku upewe idadi ya wagonjwa itakusaidia nini?
 
Kenya inaendelea kupima na kupambana na korona wakati siye tunajidanganya imekwisha.

Leo hii wamegundua visa 147, hii inaonyesha Korona bado ipo na inaongezeka badala ya kupungua.

Najua wanaopenda kusikia habari nzuri wakati wa majanga kujiriwadha, na kama wenye akili ya kutuliza wajinga kwa uongo wanavyotaka, watapinga hili vikali.

Wapya 147 wakutwa na corona Kenya akiwemo mtoto wa mwaka mmoja.
Kwa hiyo we unatakaje? Usifosi tufanane kenya ,kenya. Bongo, bongo. Au kama una wasi wasi na bongo hamia kenya. Tusitishane hapa! Corona tumeiga rasmi jumapili ya idi mosi. Utaki andamana.
 
Kila mtu ashinde mechi zake, tukutane kwenye hesabu, Jiwe amesema koona imekaribiaa kuisha na inarudi wuhani
 
Kenya inaendelea kupima na kupambana na korona wakati siye tunajidanganya imekwisha.

Leo hii wamegundua visa 147, hii inaonyesha Korona bado ipo na inaongezeka badala ya kupungua.

Najua wanaopenda kusikia habari nzuri wakati wa majanga kujiriwadha, na kama wenye akili ya kutuliza wajinga kwa uongo wanavyotaka, watapinga hili vikali.

Wapya 147 wakutwa na corona Kenya akiwemo mtoto wa mwaka mmoja.

Scientific Research gami imewahi Kufanyika na Kusema kwamba Ugonjwa ukitokea Kenya au Uganda basi ni lazima na Tanzania nao waupate?
 
Mbona Kenya wanaposhinda marathon na sisi hatushindi haushangai iweje ushangae hili mkuu.
 
Leo nimesikiliza mahojiano kati ya mtangazaji wa bbc na Mwenyekiti wa Madaktari Tanzania,
Mtangazaji anauliza umetumia kigezo gani kusema idadi ya wagonjwa imepungua?! Daktari badala ya kujibu kitaalam amebaki anambwelambwela tu.
Nikajua hii ni siasa tu. Ugonjwa upo na unaua jamani.
Chukueni tahadhari!! Kubanwa mbavu, kifua na kushindwa kupumua sio experience nzuri kabisa.
Inatesa sana
 
Kwa hiyo we unatakaje? Usifosi tufanane kenya ,kenya. Bongo, bongo. Au kama una wasi wasi na bongo hamia kenya. Tusitishane hapa! Corona tumeiga rasmi jumapili ya idi mosi. Utaki andamana.
Jina lako linasema yote lol.
 
Back
Top Bottom