Excellent point. Nchi nyingi zilizoharibikiwa na kuwa failed states zilianza hivi hivi. Huku makundi ya machawa, kwa uzuzu wao, yakishabikia na kufurahia mwenendo huo yakifikiri ni suala la upande "wao" wenye nguvu za dola dhidi ya kundi fulani "adui" la upinzani wasio na uwezo wowote. Matokeo yalikuwa ni kuimarisha magenge ya watawala wanaotegemea ukatili na mauaji, magenge ambayo baadaye katika kugombania madaraka yakageukana na kuanza harakati za kuangamizana na kuangamiza taifa kwa ujumla.
No one has monopoly of violence, cruelty and killing. Tuendelee kutengeneza taifa la makatili na wauaji miongoni mwa ndugu, majirani na marafiki katika jamii yenye tamaa ya madaraka huku tukiendelea kuimba nyimbo mfu za kuombea amani na utulivu nchini. It's just a matter of time before this house of cards blows up into shards of real, apocalyptic misery.