Kimsingi kazi ya kukusanya na kusimamia mapato ya serikali ni ya Wizara ya fedha na taasisi zake.
Lakini kwa sasa kila waziri amejigeuza kuwa mtoza ushuru au mkusanya tozo na kuacha majukumu yao muhimu ya kusimamia ustawi wa jamii katika sekta zao.
Jana nimemsikia Waziri wa Mawasiliano na Tehama Dr Ndugulile akisema halizishwi na mchango wa Tehama kwenye pato la taifa.
Kwamba mchango wa Tehama ni 0.5% tu wakati taasisi nyingi yakiwemo mabenki yanatumia mfumo huo na kwahiyo unaweza kuchangia hadi 10% ya pato la taifa.
Tusisahau kuwa kodi na tozo zote anayekuja kulipa ni mtumiaji wa mwisho ambaye ni mwananchi wa kawaida.
Tusipokuwa makini tutamkumbuka ni yeye na kaulimbiu yake.
Maendeleo hayana vyama!